Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104744 articles
Browse latest View live

‘Mpemba wa Magufuli’ Kupelekwa Mahakama ya Mafisadi

$
0
0
‘Mpemba wa Magufuli’ kupelekwa Mahakama ya Mafisadi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo November 1, 2017 imeelezwa kuwa jalada la kesi ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo ya Tsh. Milioni 785 inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ linaandaliwa kupelekwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwenye ‘Mahakama ya Mafisadi’

Haya yameelezwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulishakamilika na kinachofanyika sasa ni jalada la kesi hiyo kuandaliwa ili liende Mahakama ya Mafisadi.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi November 15, 2017 ambapo katika kesi hiyo mbali ya Mpemba, Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh 785.6 milioni.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na October, 2015 wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh 392.8 milioni bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

October 26, 2015 Washtakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo 10 vyenye uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya dola za Marekani 30,000 sawa na Sh 65.4milioni.

Wanadaiwa kuwa October 27, 2015 wakiwa Tabata Kisukuru pia walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya dola za Marekani 15,000 sawa na Sh  32.7 milioni.

Feza Kessy Afurahishwa na Mafanikio ya Ngoma Yake ya 'Kaa Kijanja'

$
0
0
Feza Kessy Afurahishwa na Mafanikio ya Ngoma Yake ya 'Kaa Kijanja'
Msanii wa muziki Bongo, Feza Kessy amefunguka anachojivunia kwa sasa ni mafanikio yaliyofikiwa na ngoma yake ‘Kaa Kijanja’ ambayo amemshirikisha Nikki wa Pili.

Muimbaji huyo amesema ngoma hiyo imeweza kumpeleka katika hatua nyingine kabisa ukilinganisha na hapo awali.

“Nafikiri imeniweka katika position nzuri kama female artist wa Tanzania, so I thanks my supporter, am very happy, am very great full kwa sababu imenitoa from one level to another, sasa hivi nipo kwenye  level nzuri naweza kusema kwa sababu ya Kakaa Kijanja” amesema Feza.

Feza kwa sasa ametajwa kuwania tuzo za Afrima katika kipengele cha Best Female Artiste in Eastern Africa, tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa November 10 hadi 12 mwaka huu Lagos nchini Nigeria.



Mapya Yaibuka Sakata la Kujiudhuru Nyarandu Ofisi ya Bunge Yatoboa Siri

$
0
0
Mapya Yaibuka Sakata la Kujiudhuru Nyarandu Ofisi ya Bunge Yatoboa Siri
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi, CCM, Lazaro Nyalandu  ya kumtaarifu Spika kuhusu uamuzi wake wa kujiuzulu Ubunge.

Taarifa ya ofisi hiyo hata hivyo imesema, Spika amepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu, Bw, Nyalandu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.
Imeongeza kuwa, CCM kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mh. Spika kuwa, Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.
Taarifa hiyo imefafanua kwamba, kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1) (f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.
“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo, Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.” Imesema taarifa ya Spika
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu aliutangazia umma hivi karibuni kuwa anakihama chama hicho na kuonyesha nia ya kuhamia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa madai ya kuwa chama cha CCM kimepoteza muelekeo.


Mbwa asimamisha mechi Bolivia Akimbia na Mpira Katikati ya Mechi

$
0
0
Mbwa asimamisha mechi Bolivia Akimbia na Mpira Katikati ya Mechi
Mbwa wa polisi amezua taharuki wakati alipoingia uwanjani na kukimbia na mpira wa mchezo wa kati ya  Blooming dhidi ya Nacional de Potosi waLigi Kuu Bolivia.

Mbwa huyo wa polisi alifanikiwa kutoka mikononi mwa askari aliyekuwa amemshika na kuingia uwanjani wakati mechi ikiendelea kabla ya kuung’ata mpira na kukimbia.

Kitendo hicho cha mbwa kukimbia na mpira ukiwa mdomoni mwake kilisababisha mechi kusimama kwa sekunde 40.

Askali walianza kumkimbiza mbwa huyo uwanjani jambo lililofanya mashabiki wa watazamaji kupata burudani ya aina yake.

Mwisho mchezaji Alejandro Quintana anayechezea Blooming alifanikiwa kumkata mbwa huyo na mechi kuendelea.

Mwisho wa mechi hiyo Blooming ilifanikiwa kushinda kwa mabao 4-2, lakini mbwa huyo wa polisi ndiye aliyeshika vichwa vya habari.

Mahakama ya Juu Yasitisha Uchaguzi wa Rais Liberia

$
0
0
Mahakama ya Juu Yasitisha Uchaguzi wa Rais Liberia
Mahakama ya juu zaidi nchini Liberia imeamrisha maandalizi ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kusitishwa kufuatia madai ya udanganyifu kutoka kwa mgombea aliyeondolewa kutoka kinyanganyiro hicho.
Mcheza soka wa zamani George Weah na makamu wa Rais Joseph Boakai wanatarajiwa kukutana katika duru hiyo ya pili ya tarehe 7 Novemba.
Lakini mgombea wa chama cha Liberty Charles Brumskine, ambaye alichukua nafasi ya tatu amepinga matokeo hayo.
Uchaguzi Liberia: Weah na Boakai kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa rais
Aliyekuwa mke wa Charles Taylor kujibu mashtaka Uingereza
Uchaguzi wa mwezi uliopita ndio wa kwanza huru kufanyika tangu kukamilika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003.
Mahakama imeamrisha chama cha Liberty na tume ya uchaguzi nchini humo kupeleka kesi zao ifikapo Alhamisi.
Lakini msemaji wa tume ya uchaguzi Henry Flomo aliambia BBC kuwa hajajulishwa rasmi kuhusu amri hiyo ya mahakama.
Waangalizi wa kimataifa wakiwemo wale kutoka muungano wa Ulaya hahawajaelezea hitilafu yoyote wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi

Kwa Nini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo?

$
0
0
 KWA NINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE  MADOGO?

Matatizo haya yame kuwa yakiwaathiri watu wengi sana kisaikolijia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wenzao kwa kawaida mwanaume ana takiwa awe na uume kuanzia inch(6_8)  vinginevyo mtu huyo atakuwa na matatizo.

Zipo sababu nyingi zinazo sababisha tatizo hilo  baadhi ni upungufu wa  vichocheo (Hormones za Getrogen) Ambazo  mwanaume akisha balehe vichocheo hivi huchochea  ukuaji wa  uume, chango husababisha NEVA ambayo huathiri misuri ya uume.

Ngiri ambayo Huleta maumivu ya tumbo kuunguruma  na kujaa guess, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri , miguu kufa ganzi, maumivu ya kiuno,upigaji wa punyeto sababu hizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembaba na mara kwa mara hipelekea kupunguka kwa nguvu za kiume na ham ya tendo la ndoa hukosekana na kuisha kabisa

NSUMBU:__Ni dawa dawa inayo zalisha hormones za Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.

NZAGI :--Ni dawa bora ya kurudisha  nguvu za kiume na kukupa hamu ya kurudia tendo la ndoa mara dufu utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4)bila hamu kuisha (kuchoka) dawa hii ni tiba kamili kwa matatizo hayo. Dawa hii pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk(15_30)kwa tendo moja la ndoa dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji kuanzia miaka(18_90)wana ruhusiwa kuzitumia

Pia tunatibu KISUKARI, PRESHA, PUMU, MALARIA SUGU, MIMBA KUHARIBIKA(Chango)

POWER :__Ni dawa ya mitishamba inaongeza hips, (makalio), miguu, ina punguza maziwa (chuchu). Ina toa harufu mbaya sehem  za siri Nk. Pia anazo dawa za  mvuto wa mapenzi,biashara, kurudishwa kazini, kumuita aliye mbali kwa mda mfupi tu OSTADH JUMA ANAPATIKANA MALARIA ZAKHIEM SIMU:_0769-597778 au 0784-002216 au 0627457957 Wote mnakaribishwa

Watetezi Haki za Wanyama Walaani Vifaranga Kuteketezwa

$
0
0
Watetezi wa haki za wanyama wamelaani kuteketezwa vifaranga vya kuku 6,400 vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria.

Vifaranga hivyo mali ya Mary Matia (23), vyenye thamani ya Sh12.5 milioni vilikamatwa mpakani Namanga vikitokea nchini Kenya.

Kuteketezwa kwa vifaranga hivyo jana Jumanne Oktoba 31,2017 kumeibua mjadala ikielezwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria.

Kazi ya kuviteketeza eneo la Namanga wilayani Longido ilifanyika ikishuhudiwa na maofisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Wizara ya Mifugo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Akizungumza wakati wa kuviteketeza vifaranga hivyo, ofisa mfawidhi wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasebwa amesema kazi hiyo imefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Magonjwa ya Wanyama namba 17 ya mwaka 2003. Pia, amesema Serikali mwaka 2007 ilitoa tangazo kupiga marufuku kuingizwa nchini vifaranga vya kuku na mayai.

Hata hivyo, watu mbalimbali wamehoji ulazima wa kuviteketeza vifaranga hivyo badala ya kuvirudisha vilikotoka kama alivyoomba mmiliki wake Matia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ustawi wa Wanyama (Taweso), Dk Thomas Kahema akizungumza na Mwananchi leo Novemba Mosi 2017 amesema anatambua dhamira ya Serikali ya kuzuia magonjwa ya kuambukizwa kutoka nchi jirani lakini kulikuwa na njia mbadala ya kufanikisha suala hilo.

Dk Kahema amesema mamlaka za Serikali zilitakiwa kuvirudisha vifaranga hivyo vilikotoka ili visieneze magonjwa kama inavyohofiwa.

Amesema kuviteketeza ni ukatili ambao hauungi mkono na kwamba, wanalaani kitendo hicho ambacho kinatoa taswira mbaya kwa Taifa linaloonekana halijali haki za wanyama.

“Zipo njia nyingi ambazo wangeweza kutumia mbali na kuchoma, mbona wakikamata ng’ombe hawawachomi moto?” amehoji Dk Kahema.

Amesema Sheria ya Ustawi wa Wanyama ya mwaka 2008 inasisitiza kutambuliwa kwa haki za wanyama, kwa hiyo kuteketezwa vifaranga hivyo kunaonyesha jinsi utekelezaji wa sheria unavyoibua utata.

Dk Kahema amesema vifaranga hivyo vingepimwa kubaini kama vina maambukizi na ingebainika havina vingetaifishwa au kugawiwa wajasiriamali, magereza au vituo vya watoto yatima.

Amesema hana uhakika kama sheria iliyotumika kuteketeza vifaranga hivyo inaeleza wazi kwamba viteketezwe.

Mkurugenzi mtendaji huyo amesema mamlaka hazikuweka wazi kama vifaranga hivyo vilikuwa na  maambukizi.

Amesema vifaranga havina hatia bali aliyevileta ndiye anayetakiwa kuchukuliwa hatua.

Baadhi ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii wameonyesha kutoridhishwa na hatua iliyochukuliwa na mamlaka za Serikali wakieleza ni ukatili dhidi ya wanyama.

Abbas King ameandika kwenye ukurasa wa Facebook wa Mwananchi kuwa, “Hivyo vifaranga vina roho au vinaendeshwa kwa umeme? Kwa nini msivigawe kwa watoto yatima wakafuge vikue wafanye kitoweo, kama vina madhara virejeshwe kwao walioleta wapigwe faini.”

Tumaini Kyama ameandika katika ukurasa huo kuwa, “Swali langu ni kuwa kama alikuwa kachukua mkopo wa biashara huyo mmiliki wa hivyo vifaranga mkopo ataurudisha na nn sitaki kujua hayo mengine nimewaza kwa sauti tu. Tunapambana na umasikini au tunafurahia umasikini wa baadhi ya watu.”

“Ukiukwaji wa sheria ya wanyama na pia wamerudisha maendeleo nyuma. Vilevile hawajavipima vifaranga na kutufahamisha vina magonjwa gani na hata hivyo si wangevirudisha vilikotoka ili aliyevinunua arejeshewe fedha yake na kama ni faini apigwe ili iwe funzo kwa wafanyabiashara,” ameandika Lightdod Shayo.

  By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

Papa Francis Akiri Kushikwa na Usingizi Wakati Anapofanya Maombi

$
0
0
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amekiri kwamba mara nyengine yeye hushikwa na usingizi wakati anapoomba.

''Wakati ninapoomba , mara nyengine mimi hushikwa na usingizi'', alisema katika kipindi kimoja cha kanisa hilo cha TV2000 kilichochapishwa katika mtandao wa You tube.

''Mtakatifu Theresa pia alikuwa akilala'', alisema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 kuhusu mtakatifu huyo wa karne ya 19.
Lakini akasema kuwa kushikwa na usingizi wakati wa maombi huwa ''kunamfurahisha mungu na kwamba Wakristo walitakiwa kuhisi kama watoto wanaolalia mkono wa baba yao''.
Ripoti zinasema kuwa papa Francis hulala mwendo wa saa tatu na kuamka saa kumi alfajiri kila asubuhi.

Raia huyo wa Argentina amekuwa kiongozi wa kanisa katoliki tangu 2013 na amekuwa na ratiba ilio na mambo mengi ya ziara za kigeni na mikutano ya kuonekana hadharani.

Amekuwa maarufu kwa baadhi ya mabadiliko na uwazi katika uongozi wake hususan katika utumizi wa lugha ya moja kwa moja inayoeleweka.

Dr. Mashinji Aamua Kufunguka....

$
0
0
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Vicent Mashinji‏ ametupa jiwe gizani na kudai kwamba kitendo cha dola kumkamata mtu kwa tuhuma za uchochezi ni udhaifu wa serikali katika kujibu hoja.

Dr. Mashinji amesema kwamba siasa zenye msamiati wa  uchochezi huwa hazipo hivyo kwani wadhaifu huwa ndiyo wanaotumia mabavu na siyo hoja.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dkt Mashinji ameandika "Najenga hoja, unasema mi mchochezi. Kweli umekosa ushawishi jitafakari upya, siasa za sasa msamiati wa uchochezi haupo. Ni hoja kwa hoja!"

Hivi karibuni viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakikamatwa na jeshi la polisi mara kwa mara kwa tuhuma za uchochezi

Rosa Ree Aeleza Sababu za Kutokuwepo Tena Lebo ya The Industry

$
0
0

Tazama VIDEO  Hapa Chini Rosa Ree Akihojiwa na Mtangazi wa Times Radio Lily Ommy Kuhusu Kutoka Lebo ya The Industry:

Babu Aliyemfanyia Tohara Dogo Janja Afunguka, Asema Irene Uwoya ni Size yake

$
0
0
Babu mmoja Arusha amewatoa hofu mashabiki waliodai dogo janja huenda akawa anachapiwa mzigo na vijana wabemba nondo mjini,amedai kwa jinsi anavyomfahamu dogo janja alivyo lazima Uwoya atulie kabisa,pia ameongeza hata kama wangekuwa Wolper,Uwoya ,Wema na Aunt Ezekiel pamoja lazima wote wangetulia tu.

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Kutana na Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed Kutoka Bagamoyo...Ana Dawa za Kurudisha Mapenzi na Zingine Nyingi

$
0
0
MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

USHAURI: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.

Mwamuzi Elly Sassi Amjibu Manara 'Manara Amekosa Kuwaeleza Wanasimba'

$
0
0
Baada ya msemaji wa Simba Haji Manara jana kusema mwamuzi Elly Sassi aliwaonea kwenye mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga Novemba 28 mwamuzi huyo amejitokeza na kusema Haji Manara amekosa cha kuwaeleza Wanasimba.

Elly Sassi amesema Haji Manara anatakiwa kujua sheria za soka kwanza ndio aongee vinginevyo aende TFF akapate mafunzo ya kuwa mwamuzi sio kuangalia tukio moja kisha kulitafsiri kiushabiki.
“Nafikiri Haji Manara amekosa cha kuwaambia Wanasimba lakini matukio na maamuzi ya uwanjani siku ya mchezo hayana utata wowote kwa watu wanaojua sheria za soka ndio mana baada ya mchezo wakufunzi mbalimbali wa CAF walinipongeza”, amesema Elly Sassi.
Mwamuzi huyo ambaye amejizolea sifa miaka ya hivi karibuni kutokana na uchezeshaji wake ameenda mbali zaidi na kutafsiri kisheria matukio ambayo Manara anahisi yalipaswa kuwa penalti.
“Tukio la Yondani kisheria ni kweli alishika, lakini dhamira na namna ya tukio lilivyokuwa mkono haukuwa na mawasiliano na mpira na alikuwa ameruka juu katika harakati za kuokoa mpira ukafata mkono wala hakutumia mkono kuokoa mpira huo sawa na tukio la Tshishimbi”, amesema Saasi.

Mama Mzazi wa Dogo Janja Ampa Baraka Zote Mwanaye Kwenye Ndoa Yake Asema 'Nimelidhika Hata Mtume Mohamad Alioa Mwanamke Mkubwa'

$
0
0
Mama Mzazi wa Dogo Janja Ampa Baraka Zote Mwanaye Kwenye Ndoa Yake Asema 'Nimelidhika Hata Mtume Mohamad Alioa Mwanamke Mkubwa'
Mama mzazi wa msanii Dogo Janja Bi. Zaituni Omari, amesema habari za mtoto wake kuoa ni za kweli na yeye kama mzazi alimpa baraka zote, vinginevyo asingeweza kuoa.

Mama yake Dogo Janja ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari na kusema kwamba yeye kama mzazi ameridhika kwani pia ametimiza matakwa ya dini.
“Alishawahi kuniambia kuwa anataka kuoa na mimi nikampa baraka zote, alivyokuwa tayari alinijulisha akaniambia kama kuna uwezekano niende isipokuwa kuna mambo yakaingilia kati, ila kwa vile Madee ni kama baba yake na ninamuamini sana nikawaruhusu waendelee, kila anachofanya hafanyi yeye kama yeye lazima kiko nyuma yangu, sio stori za kiki ni kweli kaoa na hawezi kuoa bila kuwasiliana na familia yake”, amesema mama yake Dogo Janja.
Kuhusu suala la tofauti ya umri kati yake na Irene Uwoya, mama yake Dogo Janja amesema kwamba suala la umri halijalishi sana isipokuwa kikubwa ni maelewano.
“Nimeridhika kwa sababu hata dini yetu ya Kiislam Mtume Mohamad alioa mwanamke mkubwa, kwa hiyo umri haujalishi, kikubwa na maelewano”, amesema Mama yake Dogo Janja.
Ijumaa ya wiki iliyopita kulianza kuonekana kwa picha mtandaoni zinazoonyesha Irene Uwoya na Dogo Janja

Mbwana Samatta Atajwa Kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2017

$
0
0
 Mbwana Samatta Atajwa Kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2017
Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF imetaja orodha ya wachezaji 30, watakao wania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2017 huku jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk likiwemo katika  listi hiyo.

Baadhi ya wachezaji waliyopo katika orodha ni pamoja na mshindi wa mwaka 2015, Pierre-Emerick Aubameyang, mshindi wa tatu mwaka 2016, Sadio Mane huku jina la mshindi wa mwaka jana, Riyad Mahrez raia wa Algeria likikosekana.

Mbwana Samata (Tanzania & Genk), Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto), Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord), Christian Atsu (Ghana & Newcastle), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund), Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester United), Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal), Keita Balde (Senegal & Monaco), Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye), Yves Bissouma (Mali & Lille), Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor), Yacine Brahimi (Algeria & Porto), Essam El Hadary (Egypt & Al Taawoun), Junior Kabananga (DR Congo & Astana), Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco), Naby Keita (Guinea & RB Leipzig), Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly), Sadio Mane (Senegal & Liverpool), Moussa Marega (Mali & Porto), Victor Moses (Nigeria & Chelsea), Youssef Msakni (Tunisia & Al Duhail), Michael Olunga (Kenya & Girona), Fabrice Ondoa (Cameroon & Sevilla), Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), Thomas Partey (Ghana & Atletico Madrid), Mohamed Salah (Egypt & Liverpool), Jean Michel Seri (Cote d’Ivoire & Nice), Percy Tau (South Africa & Mamelodi Sundowns), Bertrand Traore (Burkina Faso & Lyon), William Troost-Ekong (Nigeria & Bursaspor)

Mchezaji Bora wa Mwaka anaechezea ndani ya Afrika

Nasr Eldin Ahmed (Sudan & Hilal Obeid), Junior Ajayi (Nigeria & Al Ahly), Karim Aouadhi (Tunisia & CS Sfaxien), Aristide Bance (Burkina Faso & Al Masry), Alkhaly Bangoura (Guinea & Etoile du Sahel), Achraf Bencharki (Morocco & Wydad Athletic Club), Jeremy Brockie (New Zealand & Supersport), Fawzi Chaouchi (Algeria & MC Alger), Oussama Darfalou (Algeria & USM Alger), Muaid Ellafi (Libya & Ahly Tripoli), Tady Etekiama (DR Congo & AS Vita), Ahmed Fathi (Egypt & Al Ahly), Dean Furman (South Africa & Supersport United), Sylvain Gbohouo (Cote d’Ivoire & TP Mazembe), Tarek Hamed (Egypt & Zamalek), Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco), Saber Khalifa (Tunisia & Club Africain), Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance), Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly), Ayman Majid (Morocco & FUS Rabat), Ben Malango (DR Congo & TP Mazembe), Aymen Mathlouthi (Tunisia & Etoile du Sahel), Mohamed Meftah (Algeria & USM Alger), Sabelo Ndzinisa (Swaziland & Mbabane Swallows), Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns), Mohamed Ounnajem (Morocco & Wydad Athletic Club), Elsamani Saadeldin (Sudan & Al Merreikh), Saladin Said (Ethiopia & Saint George), Geoffrey Serunkuma (Uganda & KCCA), Percy Tau (South Africa & Mamelodi Sundowns).

Kura za kupata washindi wa tuzo hizo zitapigwa na makocha wa timu za taifa, benchi la ufundi la timu za taifa, Kamati za Maendeleo na jopo la wataalamu wa vyombo vya habari.

Wakati washindi wa tuzo hizo wakitarajiwa kutangazwa katika Jiji la Accra nchini Ghana   Januari 4 mwaka 2018.

Nyarandu Akanusha Taarifa Zinazosambazwa Kwenye Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Nyarandu Akanusha Taarifa Zinazosambazwa Kwenye Mitandao ya Kijamii
WAKATI Bunge likimtema rasmi aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Lazaro Nyalandu, mwenyewe amejitokeza na kuponda habari zinazosambazwa kueleza ubaya akisema ni uzushi.

Jana Nyalandu alisema taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo WhatsApp na Facebook kuelezea kasoro za kiutendaji akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ni uzushi ambao Watanzania wanapaswa kuupuuza.

Nyalandu alitangaza kujivua gamba CCM, kuandika barua ya kuachia kiti cha ubunge na kueleza nia yake ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jumatatu iliyopita.

Chadema, kupitia Katibu Mkuu wake, Dk. Vicent Mashinji, kilitangaza kumpokea awe mwanachama na kwamba alichelewa kutoa uamuzi huo.

Lakini jana taarifa ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, ilieleza kuwa hajapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu nafasi yake.

Aidha, Ndugai alisema alichopokea ni barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM ya Oktoba 30, kimsingi, ikimtaarifu kuwa Nyalandu amepoteza sifa ya kuwa mwanachama wa chama hicho na ubunge kwa mujibu wa ibara ya 13 ya katiba yao.

Katika ujumbe alioandika katika akaunti yake ya mtandao wa Tweeter jana, Nyalandu alisema ni uzushi, uongo wa kupuuzwa na aibu kubwa.

"Fake news alert! (Tahadhari habari za uzushi!) Habari hii ni ya kutungwa na kufikirika. Kibaya zaidi ni ya uongo. Siasa za aina hii ni za kizamani. Aibu tupu!" Aliandika Nyalandu katika akaunti yake hiyo.

Katika ukurasa huo, Nyalandu ambaye amekuwa Mbunge wa CCM tangu mwaka 2000, aliambatanisha na majadiliano ya watu wanne kwenye kundi la WhatsApp liitwalo 'Chadema Taifa' yakionyesha washirikia wake ni Mchungaji Peter Msigwa, Nyalandu na muundaji wa kundi.

Katika kundi hilo, ilidaiwa Nyalandu ameandika kuwa yuko katika wakati mgumu kwa kuwa serikali inataka kumshtaki kwa kuhusika kuuza vitalu na wanyama, na kwamba anaomba ushauri.

Katika majadiliano hayo, muundaji wa kundi, anayedaiwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anaonekana kumpa pole Nyalandu na kumshauri kuhama chama hicho.

Mbali na chapisho hilo la Nyalandu, maandiko mbalimbali yamesambaa kwenye mitandao ya kijamii tangu tamko la Nyalandu la Jumatatu, yakieleza jinsi alivyogawa vitalu vya uwindaji na wanyamapori.

Mwaka 2012, aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye, alitangaza operesheni ya kuvua magamba, akiwataka wanachama wa CCM wote ambao hawatakiwi, kukihama chama hicho haraka kabla ya kuvuliwa magamba.

Kutokana na operesheni hiyo ya CCM, Chadema kiliibuka na operesheni 'Vua Gamba Vaa Gwanda', ikiwa na lengo la kuvuna wanachama wengi waliokataliwa CCM na kuwataka kuvaa sare za chama hicho na kuungana nao.

Katika taarifa yake ya kujitoa CCM Nyalandu aliyochapisha katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Nyalandu aliomba kutua Chadema ili aungane nao kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini.

"Nitaomba kama itawapendeza wanachama wa Chadema, basi waniruhusu kuingia malangoni mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na Chadema na Watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa kidemokrasia na uhuru wa mawazo."

Nyalandu (45) alisema amejiuzulu ubunge kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inawafaa kwa majira na changamoto lukuki.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida na Mjumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, alisema: "Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, sote kama taifa tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu."

Aliandika zaidi: "Ni maombi yangu kwa Mungu kuwa haki itamalaki Tanzania, upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za kisiasa na makabila yote nchini uimarike. Tushindane kisera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu na taifa lililo imara na nchi yenye adili."

Nyalandu alitangaza nia kuwania urais Desemba 28, 2014 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Ilongero jimboni kwake, wakati akihutubia mamia ya wananchi.

Katika mkutano huo, Nyalandu alisisitiza "sasa ni zamu ya vijana kuongoza nchi" huku akiwaambia wananchi kuwa safari yake ya ubunge kwa miaka 15 inaanzisha safari nyingine bila kuwaeleza ikiwa bado ana nia na ubunge au la. Siku hiyo, aliambatana na mkewe, watoto na wazazi wake.

Ingawa alikuwa mmoja kati ya wanaCCM 38 waliojitokeza kuwania urais mwaka 2015, jina lake lilikatwa pamoja na kina Lowassa na Sumaye na kuteuliwa Rais Magufuli kupeperusha bendera ya chama hicho.


Zifahamu Faida Mbalimbali za Tangawizi Katika Mwili Wako

$
0
0
Zifahamu Faida Mbalimbali za Tangawizi Katika Mwili Wako
Hicho ni kiungo kinachotokana na mzizi wa mmea unaoitwa Tangawizi. Ni mmea unaofanana sana na binzari, ikiwa bado haijamenywa maganda yake.

Pia, ni bidhaa inayopatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi, anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au hata kilo akipenda.

Hivi karibuni akiwa mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, ambaye sasa ni mbunge wa Viti Maalum (CCM), aliendesha kampeni kubwa ya uzalishaji wa tangaweizi wilayani humo, ikiwa sehemu ya zao la biashara.

Mmea huo unaweza kuonekana kama wa kawaida na watu kuutumia tu katika mtindo wa mazoea, lakini ni kiungo kinachotumiwa kama dawa.

Pia, kiungo hicho kinaweza kutumika kikiwa ama kibichi au kimekaushwa na kutengenezwa katika mfumo wa unga.

Faida zake

Tangawizi ni kati ya mimea mingi yenye maajabu. Unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa zaidi ya 72 mwilini mwa mwanadamu.

Ina faida zaidi hasa kwa wagonjwa walioathirika na maambukizi ya Ukimwi. Hivyo, kwa wale wenye matatizo ya aina hiyo, wanaweza kufaidika zaidi na maaajabu ya mmea huo - tangawizi.

Namna ya kutumia katika nafasi yake ya dawa, ikiwa imesagwa au mbichi imepondwa, inaweza kutumika kama kinywaji na imezoeleka kwa watu wengi.

Namna rahisi ya kuitumia tangawizi ni katika chai. Inakuwa mbadala wako wa majani ambayo yenyewe huwa na vimelea vya kafeini, ambavyo vinachangia magonjwa mengi mwilini.

Pia, inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mboga zingine, kuongezwa katika ‘juisi freshi’ na kuleta ladha nzuri ambayo ni dawa.

Kuna mambo yafuatayo yanatokana na matumizi ya tangawizi:

-Kuongeza hamu ya kula.
-Kupunguza kichefuchefu.
-Kutapika na kuharisha.
-Inatibu kisukari.
-Shinikizo la damu.
-Kuongeza msukumo wa damu.
-Kutoa sumu mwilini.
-Maumivu ya tumbo.
-Gesi tumboni.

Pia,tangawizi inasaidia kuyeyusha chakula tumboni mwa binadamu. Vilevile, ina nafasi ya kusaidia matatizo ya mafua na magonjwa mengineyo.


Yanga Kuwakosa Ngoma, Tambwe, Kamusoko na Juma Abduli Katika Mechi Dhidi ya Singida United

$
0
0
Yanga Kuwakosa Ngoma, Tambwe, Kamusoko na Juma Abduli Katika Mechi Dhidi ya Singida United
Kikosi cha Yanga kitaondoka kesho mapema kwa basi lake kwenda Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Singida United Jumamosi Uwanja wa Namfua.

Lakini wachezaji wanne tegemeo hawatakuwepo kwenye msafara huo ambao ni beki Juma Abdul, kiungo Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe.
Abdul hatakuwemo kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano, wakati Kamusoko, Ngoma na Tambwe wote ni majeruhi wa muda mrefu.
Yanga inaendelea na mazoezi asubuhi ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kabla ya safari ya kesho kwenda kupambana na timu inayofundishwa na kocha wao wa zamani, Mholanzi, Hans van der Pluijm.
Yanga inakwenda kwenye mchezo huo, ikitoka kutoa sare na wapinzani wa jadi, Simba kwa kufungana 1-1 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Uhuru. Sare hiyo imefanya timu hizo ziendelee kufungana kwa pointi 16 kileleni mwa Ligi Kuu.
Ligi Kuu itaendelea Ijumaa, Maji Maji FC wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati Jumamosi Singida watakuwa wenyeji wa Yanga Uwanja wa Namfua, Singida na Ndanda FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mechi nyingine za Jumamosi, Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wataikaribisha Mbao FC Uwanja wa Saba Saba na Azam FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Jumapili kutakuwa na mechi mbili ambapo Mbeya City watakipiga na Simba, Lipuli FC nao wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Mobetto Alijitabilia Kutelekezwa na Diamond Kabla Haya Hayajatokea- Seth

$
0
0
Mobetto Alijitabilia Kutelekezwa na Diamond Kabla Haya Hayajatokea- Seth
MSANII wa filamu, Seth Bosco amefunguka kuwa sakata la kuzalishwa na kutelekezwa na msanii wa Bongo Fleva, mwanamitindo Hamisa Mobeto alijitabiria kabla hayo hayajatokea.

Akistorisha na gazeti hili, Seth alisema Mobeto kwa mara ya kwanza alishiriki katika filamu waliyocheza pamoja kama wahusika wakuu inayokwenda kwa jina la Poor Player ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ambako ndani yake alicheza kila kitu ambacho kimekuja kumtokea.

“Yaani Mobeto ni kama alijitabiria mapema maana kabla hajazaa alicheza filamu kama amezaa na mwanaume mwenye mwanamke mwingine kisha akamtelekeza na mtoto kitu ambacho kimemtokea kweli baada ya kuzaa na Mbongo Fleva na kumtelekeza kwa kutotoa matumizi ya mtoto,” alisema Seth.

Viewing all 104744 articles
Browse latest View live




Latest Images