Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Halima Mdee Awapa Makavu Wanaosema Chadema Imeishiwa Sera

$
0
0
Halima Mdee Awapa Makavu Wanaosema Chadema Imeishiwa Sera
Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima James Mdee (CHADEMA) amesema hoja inayoenezwa kwamba upinzani wameishiwa sera hivyo kufanya tukio la Mbunge mwenzao (Tundu Lissu) kama agenda kuu ni hoja nyepesi sana kwa suala zito kwani wao kama chama hawawezi

kunyamaza kimya kwa tukio ambalo lingemtoa uhai kiongozi huyo.
Mh. Mdee ametoa jibu hilo wakati akifanya mahojiano na EATV website na kusema kwamba kama Chama ambacho Mbunge wao amepata matatizo katika eneo ambalo linaaminika liko salama kamwe hawawezi kukaa kimya na kuongeza kwamba hoja ya wao kutembelea kiki hiyo iishe, na vyombo vya usalama wanapaswa kuhakikisha wanawakamata waliofanya shambulio hilo 
"Hatuwezi kukaa kimya kwa matukio yanayotokea, huu siyo utamaduni wenu. Siyo utamaduni wetu watu kupotea bila jeshi la polisi kutoa taarifa inayoeleweka, viongozi kutolewa silaha hadharani na watu ambao wanaaminika wanajulikana lakini hatujaona wakichukuliwa hatua. Mbunge kupigwa risasi maeneo yenye CCTV kamera na waliofanya tukio hilo kutokamatwa, Wananchi kuchanga fedha kwa ajili ya maafa na kisha kutumiwa kwa kazi nyingine na serikali au ni kiki ipi ambayo tunaitumia au kiki ni nini wakati tunakemea mambo yanayohatarisha ulinzi na Usalama? " Mh. Mdee.
Mbunge Mdee amesema kwamba kama ni sera chama chao bado kina sera nyingi ambazo wanaendelea kuzitekeleza kuanzia zile ambazo waliziahidi wakati wa uchaguzi na kwamba kama chama hawawezi kushindwa kuwa na sera lakini ni lazima wakemee mambo ambayo awali hayakuwahi kuzoeleka kuonekana nchini.
Akigusia suala la Mbunge wa Singida Mashariki kupigwa risasi Mdee amesema "Lissu alikuwa ni mtu wa Kufa ila kwa kudra za Mungu ameushinda mauti ndiyo maana tunapaza sauti kwa tukio lililotokea kwani hatufahamu tukikaa kimya nani mwingine atafuata hivyo niwashauri watu wasitoe majibu mepesi kwenye hoja nzito".




“Naishi Mjini kwa Kudanga" Gigy Money

$
0
0
“Naishi Mjini kwa Kudanga" Gigy Money
MUUZA nyago asiyeishiwa vituko Gigy Money amefunguka kuwa jina lake limekaa kipesapesa ingawa yeye mwenyewe maisha yake kutwa kucha ni kuwatumia wanaume (udangaji) ndiko kunamweka zaidi mjini.

Akipiga stori na Showbiz- Xtra, Gigy amesema, moja ya vitu ambavyo vinavutia watu wengi ni uzuri wa jina lake na ambalo limekaa kipesapesa ingawa yeye maisha yake kwa sasa hayafanani na maana ya jina hilo.

“Jina langu tamu sana, maana yake hata namna linavyo-sound ni jina moja zuri ambalo lipo kipesapesa, ajabu pamoja na uzuri wa jina hilo maisha yangu mimi hayafanani na jina hilo, naishi kwa kudanga na maadili ya hapa na pale,” alisema Gigy Money.

Nandi Awajia Juu Wanaomfananisha na Rubi Asema 'Kunifananisha Naye ni Kuukosea Heshima Muziki Wangu'

$
0
0
Nandi Awajia Juu Wanaomfananisha na Rubi Asema 'Kunifananisha Naye ni Kuukosea Heshima Muziki Wangu'
MREMBO aliyelikamata anga la Bongo Fleva, Nandy amewataka watu wanaomfananisha na mwanamuziki mwenzake Ruby kuacha mara moja kwa kuwa kila mtu ana ladha yake.

Akipiga stori na Showbiz Xtra, Nandy amesema, kwa muda mrefu mashabiki wake wamekuwa wakifananisha muziki wake na wa Ruby kitu ambacho haoni kama kina mashiko kwa kuwa kila mtu ana ladha yake ya kipekee ambayo mwenzake kakosa.

“Namheshimu Ruby ni mwimbaji mzuri, lakini kunifananisha naye ni kuukosea heshima muziki wangu, ladha ya muziki wangu ni tofauti kabisa na Ruby kama unaujua vizuri muziki utabaini muziki wetu ni tofauti kabisa,” alisema Nandy bila kufafanua kwa undani zaidi.


Rais Mugabe Ametaka Kurudishwa kwa Hukumu wa Kifo

$
0
0
Rais Mugabe Ametaka Kurudishwa kwa Hukumu wa Kifo
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ametaka kurudishwa kwa hukumu ya kifo nchini mwake kwani watu wanacheza na maisha ya watu kwa kuua wenzao.

Rais Mugabe ametoa taarifa hiyo alipokuwa kwenye mazishi ya mwanasiasa mwenzake mjini Harare, na kusema kuwa sheria ya kunyongwa irudishwe kwani watu wanacheza na kifo kwa kuua wenzao.
“Acha turudishe hukumu ya kifo, watu wanacheza na kifo kwa kuua wenzao, hivi hii ndio sababu ya kuikomboa nchi? Tunataka nchi hii iwe ya amani na furaha, sio nchi ambayo watu wanauana”, amenukuliwa Rais Mugabe.

Taarifa zimeendelea kueleza kwamba kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa ya Waziri wa Sheria kusema kuwa zaidi ya watu 50 wameomba nafasi ya kazi ya kunyonga watu mwezi uliopita.
Tukio la mwisho la kunyongwa mtu hadi kufa nchini humo lilikuwa mwaka 2005 baada ya mtu aliyekuwa akifanya kazi ya kunyonga kustaafu, ambapo mpaka sasa zaidi ya wafungwa 90 wapo wanasubiri hukumu ya kifo.


Mamba Mkubwa wa Urefu wa Mita 3 Aleta Tahaluki India Akutwa Nje ya Nyumba ya Mwanaume Mmoja

$
0
0
Mamba Mkubwa wa Urefu wa Mita 3 Aleta Tahaluki India Akutwa Nje ya Nyumba ya Mwanaume Mmoja
Mwanamume mmoja katika kijiji kilicho jimbo la mashariki mwa India la Orissa, alipigwa na mshangao baada ya kumpata mgeni ambaye hakumtarajia nje ya nyumba yake - mamba wa urefui wa mita 3
Dasharath Madkami alimpata mamba huyo baada ya kuamshwa na sauti zisizo za kawaida usiku.
Jiwe kubwa linalocheza nchini Tanzania
Alipiga kamsa na wanavijiji wakafika ambao walimfunga mamba huyo kwa mti.
Mamlaka za wanyamapori kisha zikafika kumuokoa mnyama huyo.

Hata hivyo kulikuwa na mzozo kuhusu ni wapi mambaohuyo angepelekwa.
Mamba mkubwa Big Daddy kufanyishwa ndoa Mombasa
Maafisa wa misitu walitaka kumuachilia myama huyo kwenda kwa bwagwa lililoku karibu ambapo alitoka, lakini wanavijiji wakakataa wakohofia kuwa angerudi tena.
Mamba huyo hata hivyo aliachiliwa kwenda mto Balimela ulio umbali wa kilomita 60.

Lazaro Nyarandu Atoa Maneno Haya Baada ya Kumtembelea Tundu Lissu kwa Mara ya Pili

$
0
0
Lazaro Nyarandu Atoa Maneno Haya Baada ya Kumtembelea Tundu Lissu kwa Mara ya Pili
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini ambaye amejiuzulu nafasi yake hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu amemtembelea tena Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jijini Nairobi Kenya ambapo anapatiwa matibabu na kumuombea.

Lazaro Nyalandu alipotangaza kujiuzulu nyazifa zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua ya kujiuzulu Ubunge wake kwa Spika wa Bunge Job Ndugai alifunga safari na kwenda nchini Kenya, ambapo huko alipata nafasi ya kumtembelea Mbunge Tundu Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.
"Mungu akuangazie nuru za uso wake na kukupa amani kaka yetu mpendwa Tundu Lissu. Akakuponye majeraha na maumivu yako na kukufanya Taifa kubwa. Kwa wote wanakuombea na kukupenda, ikawe heri kwao, na kwako iwe amani, uponyaji na mafanikio. Utukufu ujao uwe Mkuu kuliko ule wa awali" alisema Lazaro Nyalandu
Mbunge Tundu Lissu bado yupo nchini Kenya jijini Nairobi akipatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Dodoma.

"Mastaa Walevi Ndiyo Wanakiona cha Moto na Kulalamika Vyuma Vimekaza ” Amanda

$
0
0
"Mastaa Walevi Ndiyo Wanakiona cha Moto Maana Vyuma Vimekaza ” Amanda
STAA wa filamu za Kibongo, Amanda Poshi ameibuka na kueleza kuwa kutokana na watu wengi kulia ugumu wa maisha kwamba vyuma vimekaza, wanaokoma na kukiona cha moto zaidi ni wale mastaa walevi.

Akipiga stori na Amani, Amanda alisema wapo mastaa waliokuwa wamezoea kunywa pombe na kulewa kila siku lakini kwa kipindi hiki wanakoma kwa kuwa hawana fedha za kunywa kama zamani hivyo anajipongeza kwa kuwa katika maisha yake yote starehe yake kubwa ni soda tu.

“Sina hata tatizo na mtu maana naenda zangu sehemu nzuri nakaa nakunywa soda huku nikitafakari mipango yangu yaani najiachia kwa raha zangu maana ndiyo starehe yangu kubwa, mastaa waliozoea kulewa ndiyo wanakoma maana vyuma vimekaza kweli,” alisema Amanda bila kuwataj

Kimenuka Acacia Viongozi Wawili wa Juu Wajiudhulu Nyadhifa Zao

$
0
0
Kimenuka Acacia Viongozi Wawili wa Juu Wajiudhulu Nyadhifa Zao
Mkurugenzi Mkuu wa Acacia nchini Tanzania Brad Gordon na Mkurugenzi Mkuu wa fedha Andrew Wray, wamejiuzulu nyadhifa zao ingawa bado watakuwa chini ya kampuni mpaka mwisho wa mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na kampuni hiyo na kusema kwamba Mkurugenzi Mkuu Brad Gordon anarejea nyumbani kwake Australia na Andrew Wray anatafuta fursa mahali kwengine.
Tayari Bodi ya Acacia imewataja watu ambao watachukua nyadhifa za wawili hao, ambao ni Peter Geleta ambaye atakuwa Mkurugenzi Mkuu na Jaco Maritz atakachukua nafasi ya Andrew Wray aliyekuwa Mkurugenzi wa fedha.
Peter ambaye ametajwa kuwa na uzoefu kwenye uchimbaji madini kwa muda wa miaka 35 ameshawahi kufanya kazi na mgodi wa Anglo Gold Ashanti kwa miaka 25 na kampuni ya Barrick, na alijiunga na Acacia mwaka 2012 na alishawahi kuwa Meneja Mkuu kwenye mgodi wa Bulyanhulu.
Acacia imewashukuru viongozi waliojiuzulu Brad Gordon na Andrew Wray kwa muda wao wote waliokuwa hapo huku wakisema walifanya nao kazi vizuri, na kuwatakia heri huko waendako, huku wakiamini waliochukua nafasi yao watafanya kazi kama ambavyo inastahili.

Inasikitisha Boss Amhamuru Mfanyakazi Wake Kutembea Uchi Ofisini

$
0
0
Inasikitisha Boss Amhamuru Mfanyakazi Wake Kutembea Uchi Ofisini
Yaani unaambiwa dunia ina mambo kweli kweli kwani tumesikia mengi na tutaendelea kushuhudia mengi zaidi. Boss mmoja mjini Warsaw, nchini Poland ameamuru mfanyakazi wake mmoja wa kike kutembea uchi ndani ya Ofisi kubwa ya mauzo ya jumla ili kuongeza molali na ufanisi kazini kwa wanaume ambao alidai kuwa wamekosa ari kwenye utendaji.

Mwanamke huyo ambaye naye hakuwa na namna alivua nguo zake zote huku akiziba kifua kwa sidiria na kutumia mawani ya jua na kuanza kutembea ofisini mbele ya Wanaume waliokuwa wamesimama msururu kwa amri kutoka kwa Boss.

Taarifa kutoka kwa vyombo vya habari nchini Poland, vimeeleza kuwa mwanamke huyo alilipwa pesa mara tatu ya mshahara wake ili kufanya tukio hilo kwa lengo la kuwachangamsha wanaume ili kurudisha ari ya utendaji kazi.

Hata hivyo tukio hilo lilifanyika kwa muda wa dakika 20 tu na baadae mwanamke huyo akavaa nguo na kukaa kwenye meza yake na kuendelea na majukumu yake kazini hapo kama kawaida.Tazama video hapa chini (Video by Daily Mail)

Video hiyo inayoonekana imerekodiwa kwa kutumia simu ilianza kusambaa mtandaoni nchini humo wiki iliyopita huku watu wengi wakipinga vitendo kama hivyo mitandaoni na kumkosoa Boss wa Kampuni hiyo ya mauzo.

Serikali Yawafukuza Watumishi 71 Huku Saba Wachunguzwa

$
0
0
Serikali Yawafukuza Watumishi 71 Huku Saba Wachunguzwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewafukuza kazi watumishi 71 na wengine 7 wakichunguzwa kwa tuhuma za rushwa huku watu wengine watatu ripoti zao zikiwa TAKUKURU na wawili wengine wao wameshafikishwa mahakamani tayari.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale akiwa mkoani Kigoma amethibitisha hilo na kusema kuwa watumishi hao ni wale waliokuwa wakihudumu katika mizani mbalimbali ya nchini na kudai kuwa wamekuwa wakikiuka taratibu mbalimbali.
"Wafanyakazi 71 tumewafukuza kazi lakini uchunguzi unaendelea kwa watu wengine saba ambao wao tunauhakika wanajiusisha na rushwa lakini kam tunavyojua uchuzi ni lazima pia wapo watu watatu ripoti zao tayari zipo TAKUKURU huku watu wengine wawili wao tayari wameshafikisha mahakamani" alisema Mfugale
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale amesema idadi ya wafanyakazi hao 71 waliofukuzwa ni toka mwezi Januari 2017 mpaka Oktoba mwaka huu.

Kigogo wa ESCROW Ameachiwa Huru na Mahakama

$
0
0
Kigogo wa ESCROW Ameachiwa Huru na Mahakama
 Mahakama  Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma ambae alikua anakabiliwa na kosa la kupokea rushwa ya Sh. milioni 323 kutoka kwa Mfanyabiashara James Rugemalira.

Taarifa inaeleza zaidi kwamba fedha hizo zilikua ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW ambapo kigogo huyo ameachiwa na hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa TAKUKURU, Leonard Swai kuomba kesi hiyo iondolewe Mahakamani chini ya kifungu cha 98 (a) cha  sheria ya Makosa ya Jinai (CPA).

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alisema Mshtakiwa huyo amefutiwa kesi na kwa sasa yupo huru ambapo kama utakumbuka, Rugonzibwa alifikishwa Mahakamani kwa Mara ya kwanza January 14, 2015 na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU).

Inadaiwa alipokea rushwa hiyo ya milioni 323 kutoka kwa Rugemalira ambae alikuwa ni mshauri huru wa kitaalamu, Mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo.

Babu Tale Jela Yamuita Baada ya Kushindwa Kulipa Milioni 250

$
0
0
Babu Tale Jela Yamuita Baada ya Kushindwa Kulipa Milioni 250
Meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), Abdul Nassib maarufu Diamond Platnum, Hamis Taletale na nduguye Idd Taletale sasa wanachungulia kifungo jela kwa kushindwa kulipa fidia ya Sh250 milioni, ambazo kampuni yao ya Tiptop Connection Limited inadaiwa.

Februari 18 mwaka jana, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliiamuru kampuni hiyo kumlipa fidia ya Sh250 milioni, Mhadhiri wa Dini ya Kiislam, Sheikh Mbonde kwa kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake, kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hata hivyo meneja huyo wa Diamond, maarufu kama Babu Tale na nduguye wakiwa wakurugenzi na wanahisa pekee wa kampuni hawakuweza kulipa fidia hiyo wala kuweka wazi mali za kampuni hiyo, hivo Mbonde akalazimika kufungua maombi ya utekelezaji wa hukumu hiyo.

Mahakama hiyo katika uamuzi uliotolewa na Naibu Msajili Wilbard Mashauri Juni 9 mwaka huu iliwaamuru wakurugenzi hao wa kampuni hiyo kuweka wazi mali za zinazomilikiwa na kampuni yao hiyo.

Alisema kuwa iwapo watashindwa kutaja mali za kampuni hiyo basi wao wenyewe watalazimika kulipa kiasi hicho cha fedha au mali zao binafsi kukamatwa na kuuzwa na kwamba iwapo hawatakuwa na mali za kulipa fidia hiyo

“Kama hawana mali, basi watakamatwa na kufungwa gerezani kama wafungwa wa madai kwa mujibu wa masharti ya Amri ya 21 Kanuni ya 38(1) ya CPC (Kanuni za Mashauri ya Madai) Sura ya 33 marejeo ya mwaka 2002.”alisisitiza Naibu Msajili Mashauri.

Katika kutekeleza agizo la Mahakama kwa wakurugenzi hao, kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd imewapa siku 14 Babu Tale na nduguye kutekeleza uamuzi na agizo hilo la Mahakama.

Taairifa hiyo ya Yono imekabidhiwa leo Alhamisi na Meneja Masoko wa Yono, Kene Mwankenja kwa mjumbe ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani, Kata ya Kwembe, wilayani Ubungo, Wilson John ili kuwafikishia kina Babu Tale

Iwapo hawataweka wazi mali za kampuni hiyo ili zipigwe mnada au walipe fidia hiyo ambayo kampuni yao inadaiwa ama kama hawatakuwa na mali zao binafsi ambazo zinaweza kupigwa mnada, basi wao wenyewe itabidi watupwe jela, kama Mahakama ilivyaomuru.

“Tumewapa notice (taarifa) hiyo ili kuwapa nafasi ya kumaliza suala hilo ndani ya muda huo. Wakilimaliza sawa, lakini wakipuuza basi wajibu wetu ni kutekeleza tulichoelekezwa.” amesema Mwankenja.

Katika hati ya madai ya kesi hiyo namba 185 ya mwaka 2013 na wakati wa usikilizwaji, Juni 6, 2013 Sheik Mbonde aliingia makubaliano na kampuni hiyo, kutumia kazi zake za mawaidha, kwa kuzalisha, kurekodi na kuzisambaza.

Pamoja na mambo mengine, walikubaliana kampuni kulipia gharama za kurekodi masomo na mafundisho ya mihadhara yake, kumnunulia gari, kumjengea nyumba na kugawana faida ya mauzo.

Hata hivyo, baada ya kukamilisha kurekodi masomo saba, maofisa wa kampuni hiyo walimkatia mawasiliano hadi alipobahatika kukutana na mmoja wao, Adam Waziri ambaye alimweleza kuwa wamesitisha mpango wa kuendelea na kazi hiyo.

Hata hivyo, Agosti 9, 2013, wakati mdai akiendesha mhadhara Bahi Dodoma, alibaini kuwa DVD za masomo yake zilikuwa zikiuzwa sokoni Dodoma na katika  mikoa mbalimbali kama vile Mbeya, Tanga na Dar es Salaam, bila ridhaa yake wala makubalino.

DVD hizo kwa mujibu wa hati hiyo zilikuwa ni za masomo mbalimbali aliyokuwa ameyatoa na kwamba makava ya DVD hizo yalikuwa na nembo na namba za simu za maofisa wa mdaiwa.

 

Shamsa Ford Awapa Makavu Wanaomponda Kuuza Duka Badala ya Kumuajili Binti

$
0
0
Shamsa Ford Awapa Makavu Wanaomponda Kuuza Duka Badala ya Kumuajili Binti
MREMBO wa Bongo Movies, Shamsa Ford ametoa povu la aina yake kwa mashabiki wanaomponda kwa kitendo cha yeye kuuza duka mwenyewe badala ya kumuweka binti amuuzie.

Akizungumza na Amani, Shamsa ambaye anamiliki duka la nguo na mumewe Chid Mapenzi lililopo Kinondoni jijini Dar, alisema haoni aibu yoyote kuuza mwenyewe dukani hapo kwa sababu ustaa bila kipato chochote ni sawa na mzigo tu hivyo wanaomponda kwenye mitandao ya kijamii wanajisumbua.

“Unajua kuna watu nawashangaa sana wananiambia si nitafute mtu akae dukani halafu mimi nifanye nini? Mastaa wengi wamezoea kulala tu sasa mimi siwezi unapopata fursa ni lazima uitumie ipasavyo,” alisema Shamsa.

MCT Yafunguka Kuhusu Wanaokiuka Uhuru wa Waandishi wa Habari

$
0
0
MCT Yafunguka Kuhusu Wanaokiuka Uhuru wa Waandishi wa Habari
Baraza la Habari Tanzania (MCT) kupitia Katibu Mtendaji wake, Kajubi Mukajanga limesema kuwa mkiukaji mkuu wa uhuru wa waandishi wa habari ni serikali kupitia jeshi la polisi.

Akizungumza na waansihi wa habari leo jijini Dar es salaam, Kajubi amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita hofu kwa waandishi wa habari na tasnia nzima imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hali ambayo imesababisha waandishi kutofanya kai kwa uhuru na weledi.

Kajubi ameeleza kuwa katika kipindi cha miezi sita magazeti matano yamefungiwa mpaka sasa huku akisema mbali na hilo waandishi mbalimbali wa habari wamepata misuko suko hali ambayo haijawahi kuonekana katika historia ya Tanzania huku akieleza kuwa ni mambo ambayo yanalishushia hadhi taifa letu mbele ya Jumuiya ya Kimataifa.


Wakili Ameanzisha Kesi ya Kutaka Mahari Kufutiliwa

$
0
0
Wakili  Ameanzisha Kesi ya Kutaka  Mahari Kufutiliwa
Wakili mmoja wa kike nchini Zimbabwe ameanzisha kesi ya kufutilia mbali lobola au mahari akisema kuwa ni mila iliopitwa na wakati ambayo inawafanya wanawake kuonekana kama mali kulingana na gazeti la serikali la Herald.

Priccilar Vengesai anaamini kwamba iwapo utamaduni huo utaendelea ,familia zote za mume na mke zinafaa kulipa mahari kwa maslahi ya usawa wa kijinsia, gazeti hilo limeongezea.
Amewasilisha malalamishi yake katika mahakama juu, mahakama ya kikatiba akitaka kusikilizwa kwa kesi yake kwamba utamaduni huo unakiuka haki za raia.
Gazeti hilo limemnukuu bi vengesai akisema kwamba anataka kuolewa na hataki kupitia aliyopitia alipokuwa katika ndoa.

Sikushiriki katika kuuliza gharama ya mahari. Sikupewa fursa ya kuuliza kwa nini mharai ilitolewa.
Hali yote hiyo ilinifanya mimi kuonekana kama ''mali'' ambapo kiwango cha thamani yangu kilipendekezwa na wajomba zangu na mume wangu akalipa.

Hatua hii ilinivunja moyo na hali hiyo kuniweka chini ya udhibiti wa mume wangu kwa kuwa najihisi kwamba nilinunuliwa.
Mimi natoka katika kabila la Shona na ningependelea kuingia katika ndoa mara tu kesi hii itapokamilika na uamuzi kutolewa.
Chini ya utamaduni wa kabila la shona, Lobola ama mahari lazima alipiwe mwanamke kabla ya ndoa kukubalika katika familia na jamii.
Katika hali ambapo Lobola haijalipwa, wazazi na jamaa wa familia ya mwanamke hawataruhusu ndoa hiyo kuhalalishwa chini ya sheria ya ndoa.

Kuachana na Nay Kumenipa Akili ya Kujibidiisha Katika Biashara- Siwema

$
0
0
Kuachana na Nay Kumenipa Akili ya Kujibidiisha Katika Biashara- Siwema
MZAZI mwenziye na mwanamuziki Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema Edson amefunguka kuwa kama asingepitia misukosuko ya kimapenzi na mzazi mwenziye huyo mpaka kuachana basi asingepata akili ya kujibidiisha kibiashara.

Siwema mwenye makazi yake jijini Mwanza, alisema baada ya kupata misukosuko alitafakari na kuamua kupiga moyo konde na kusimama kama mwanamke ili afanye kitu ambacho kitamsimamisha na kuendelea na maisha yake.

“Unajua ukikumbwa na misukosuko hasa ya kimapenzi akili inatanuka, nilijiongeza haraka na leo hii nina duka langu kubwa la nguo hapa Mwanza na maisha yanaendelea, ningekaa kulilia mapenzi ningechemka,” alisema Siwema

Wakati Najiuzulu Nilifanya kwa Nia Yangu Sikuwa Nimepata Barua ya Kufukuzwa CCM- Nyarandu

$
0
0
Wakati Najiuzulu Nilifanya kwa Nia Yangu Sikuwa Nimepata Barua ya Kufukuzwa CCM- Nyarandu
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa hajawahi kupata barua yoyote kutoka CCM inayomfukuza unanacha kama inavyodai.

Mh. Nyalandu ameiambia Bongo5 kuwa ndani ya chama hicho huwa kuna utaratibu na hawamfukuzi mtu kwa barua bali kuna kuwa na vikao vinavyohusiana na maadili hivyo basi amesema tangu awe ndani ya chama hicho hakuna kikao kilichowahi muita kuhusiana na masuala ya maadili.

“Wakati najiuzulu tarehe 30 mwezi Oktoba, nilifanya hivyo kwa nia yangu mwenyewe na kwa uamuzi wangu mwenyewe, sikuwa nimepata barua yoyote kutoka CCM inayonifukuza, kwahiyo dhana ya kwamba kulikuwa na barua yakunifukuza uanachama sio kweli lakini vilevile ikumbukwe kwamba mimi sikuwa mwananchama wa kawaida mimi nilikuwa ni mbunge ana jimbo pili nilikuwa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na utaratibu wa chama chetu haufukuzwi tu kwa barua huwa kuna vikao vinavyohusiana na maadili huwa vinakaa,” amesema Nyalandu.

“Hakuna kikao chochote tangu niwe mwananchama ambacho kiliwashawahi kuniita kuhusiana na masuala yanayohusiana na maadili, kwahiyo mimi naona tungejikita tu kufanya muktabari wa nchi yetu tufanye siasa za ushindani na turuhusu watu wawe huru na tusisababishe malumbano ambayo hayana sababu yoyote,”ameongeza.

Nyalandu Jumatatu hii ya tarehe 30 Oktoba mwaka huu aliamua kukihama chama cha Mapinduzi (CCM) na kujivua ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini.

Mchungaji Msigwa Akomalia Kumng'oa Spika 'Hoja Yangu Ipo Pale Pale Naamini Wabunge Wenye Akili Wataniunga Mkono'

$
0
0
Mchungaji Msigwa  Akomalia Kumng'oa Spika 'Hoja Yangu Ipo Pale Pale Naamini Wabunge Wenye Akili Wataniunga Mkono'
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha nia yake ya kutaka kumuondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai iko pale pale.

Mchungaji Msigwa mwezi Oktoba 2017 alionyesha nia ya kupeleka hoja Bungeni ili kumuondoa Spika Job Ndugai katika nafasi yake hiyo na kusema atatumia kanuni za Bunge na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya hivyo kwa kile anachoamini kuwa Spika wa Bunge ameshindwa kusimama vyema katika nafasi hiyo jambo ambalo limepelekea Bunge hilo sasa kuonekana halina nguvu na kushindwa kuisimamia serikali.
Msigwa amesema kuwa anaamini kuwa wabunge mbalimbali ambao wana akili wataungana na hoja yake hiyo ya kutaka kumuondoa Spika Job Ndugai katika kiti hicho kwa kutumia kanuni za Bunge na Katiba ya nchi.
"Hoja ya kumung’oa spika iko pale pale! Naamini wabunge Wenye akili wataiunga mkono" aliandika Mbunge Msigwa kupitia mtandao wake wa Instagram
Wabunge mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakitoa lawama kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi sasa linashindwa kuisimamia serikali ipasavyo na wengine wamekuwa wakidai kuwa Bunge hilo linaendeshwa na serikali, jambo ambalo limemfanya Mbunge Msigwa kutaka kupeleka hoja ya kumuondoa kiongozi wa Bunge hilo Spika Job Ndugai.


Kakunda: Viondozi wa Dini Wataadhalishwa Kufungisha Ndoa Asema 'Binti Hatoolewa Bila Leaving Certifikate'

$
0
0
Kakunda Viondozi wa Dini Wataadhalishwa Kufungisha Ndoa Asema 'Binti Hatoolewa Bila Leaving Certifikate'
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Joseph Kakunda amewatahadharisha Viongozi wa dini nchini kujihadhari na kuwaozesha wasichana ambao hawajamaliza elimu ya kidato cha nne ili kuwakamata wazazi wote wanaoshiriki kuwaozesha watoto wao kwasababu

Amesema kuwa watoto wa kike wanashindwa kumaliza masomo kwasababu ya mimba ama kuozeshwa jambo ambalo limeendelea kuisumbua serikali katika juhudi zake za kuokoa maisha ya watoto wa kike ili waendelee na masomo na kuongeza kuwa Wilaya ya Nkasi kuna tatizo sugu la mimba kwa kuwa na mimba 152 kati ya 325 kwa Mkoa mzima.
Amefafanua kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini sana maisha ya watoto wa kike na inaendelea kuweka mikakati ya kila namna ili kuhakikisha kuwa wasichana hao wanapata elimu stahiki, kwa kuanza na elimu bure na kuendelea na mikakati ya marekebisho ya sheria kadhaa ili watoto wa kike waendelee na masomo.

“Haiwezekani mtu anatakatisha fedha hapati dhamana, halafu mtu anampa mimba mwanafunzi na kisha anapata dhamana, tunakoelekea ili uolewe lazima uwe na “leaving Certificate” ama tujue kuwa hukusoma kabisa ili tuwahoji wazazi, mwananfunzi ambae ataolewa kwa kukatishwa masomo kamata wote na funga miaka 30, wazazi wa pande mbili, aliyeoa, aliyeolewa, wanaoshangilia, aliyefungisha ndoa wote miaka 30 jela,” alifafanua.
Aidha, amewashauri wanaharakati kuungana pamoja katika kuwaelimisha watoto wa kike na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha mimba zinapungua na kuwa vitendo hivyo haviendelei, ili kuwainua watoto wa kike kielimu.

Nimejipanga Kuhakikisha Timu Yangu Inavunja Rekodi ya Yanga- Omog

$
0
0
Nimejipanga Kuhakikisha Timu Yangu Inavunja Rekodi ya Yanga- Omog
Timu ya Simba haijawahi kushinda mechi mbili mfululizo kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, lakini safari hii kocha Joseph Omog ametamba kuvunja rekodi hiyo .

Kocha Omog ameandaa mpango mkakati maalumu ambao utakiwezesha kikosi chake kuibuka na pointi sita kwenye mechi mbili wanazokwenda kucheza Nyanda za Juu Kusini.
Akifafanua zaidi Omog amesema kuwa  amepania kuhakikisha timu yake inavunja rekodi ya Yanga kwa kushinda mechi hizo mbili ingawa amekiri kuwa siyo jambo dogo.
“Msimu uliopita tulijitahidi kufanya hivyo lakini ilishindikana msimu huu tunaanza tena kucheza ugenini mechi zote mbili kwa ubora wa kikosi tulichokuwa nacho naamini tunaweza kuvunja rekodi ya Yanga”. 
Omog amesema anaziheshimu timu za Mbeya City na Tanzania Prisons, lakini msimu huu ataomba wawasamehe kwani wamejipanga kuhakikisha wanarudisha heshima na hadhi ya Simba.




Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images