Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Ajibu Atoa Shukrani Yanga Awagawa Milioni Moja kwa Wachezaji Wenzake

$
0
0
Ajibu Atoa Shukrani Yanga Awagawa Milioni Moja kwa  Wachezaji Wenzake
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ibrahim Ajibu ambaye ni tegemeo hivi sasa jana aliwagawia wachezaji wenzake shilingi 400, 000 kama sehemu ya shukrani kwao baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mbili za Ligi Kuu Bara na kuzawadiwa shilingi milioni moja.
Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu akabidhiwe shilingi milioni moja na Kundi la la Whatsap la Yanga For Life linaoundwa na baadhi ya wasanii ya filamu nchini.
Ajibu alipewa shilingi milioni moja baada ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Bara ambazo amezicheza.
Mechi hizo, alizozicheza ni dhidi ya Kagera Sugar ambayo alifunga na kumtengenezea bao moja Mzambia, Obrey Chirwa mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera.
Ajibu aligawa fedha hizo, jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo kumalizika yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kabla ya leo saa 11:30 alfajili kuelekea Mkoani Singida kuvaana na Singida Unite mchezo utakaopigwa keshokutwa Jumamosi Uwanja wa Namfua.
Na Mwandishi Wetu


T-Pain Amepanga Amempeleka Lil Wayne Kortini.

$
0
0
T-Pain Amepanga Amempeleka Lil Wayne Kortini.
 Kampuni ya muimbaji huyo, Nappy Boy Productions inaishtaki Young Money kwa huduma iliyoifanya kwenye album ya Tha Carter III.

Kampuni hiyo imedai kuwa T-Pain alitayarisja wimbo “Got Money,” ambao aliimba pia. Pia mmoja wa wasanii wake, Young Fyre, alitayarisha wimbo “How to Hate” uliomo kwenye album hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mahakamani, Young Money ilitakiwa kumlipa T-Pain mrabaha toka kwenye mradi huo. Na sasa kampuni inataka ilipwe $500,000.

Tanzania Yapata Neema ya Bilioni 129 Kutoka Umoja wa Ulaya

$
0
0
Tanzania Yapata Neema ya Bilioni 129 Kutoka Umoja wa Ulaya
Umoja wa ulaya umeipatia Tanzania jumla ya Euro Million 50 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 129 za kitanzania katika kufadhili Mpango wa Taifa wa umeme vijijini ambapo jumla ya vijiji elfu 12 vitapatiwa umeme

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutia saini juu ya ufadhili huo wenye masharti nafuu ambapo Tanzania haitatakiwa kurejesha Fedha hizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bwana Dotto James amesema kuwa umoja waulaya unalenga kuona mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka 5 unafikiwa kikamilifu hususani katika sekta ya nishati katika uzalishaji na usambazaji ili kurahisisha shuguli za kimaendeleo nakuondoa umasikini vijijini
Kwa upande wa Kamishna wa Umoja wa Ulaya Duniani Mr. Neven Mimica anasema, kufikiwa kwa mpango wa tatu wa umeme vijini REA unaomalizika 2020 kunategemea upatikanaji umeme wa uhakika suala ambalo litachochea kwakiasi kikubwa kufikiwa kwa mpango wa maendeleo endelevu ya dunia ya mwaka 2025
Ufadhili wa maendeleo ya umoja wa ulaya kwa Tanzania kwa sasa unafikia jumla ya Trillion I .07

Erasto Nyoni Atangazwa Mchezaji Bora Mwezi Oktoba

$
0
0
Erasto Nyoni Atangazwa Mchezaji Bora Mwezi Oktoba
MCHEZAJI kiraka wa Simba, Erasto Nyoni ametangazwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo wa wa mwezi Oktoba.
Hiyo ni baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi nne za Ligi Kuu Bara ambacho amezicheza huku akisaidia timu yake kupata matokeo mazuri.
Kiraka huyo, alijiunga na Simba kwenye msimu huu wa ligi kuu akitokea Azam FC mara baada ya mkataba wake kumalizika.
Nyoni akicheza nafasi ya beki wa pembeni namba mbili hadi sasa tayari ameitengenezea mabao matano katika mechi za ligi ambazo amezicheza.

Erasto ambaye anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani amekuwa chachu ya matokeo mazuri kwa timu ya Simba tangu asajiliwe akitokea Azam FC.
Mechi ambazo zimempa uchezaji bora katika mwezi huu hadi kupelekea kutwaa tuzo hiyo ya uchezaji bora ni dhidi ya Njombe Mji, Stand United, Mtibwa Sugar na Yanga kati ya hizo walishinda mbili na kutoa sare mbili.
mwisho.

Nandy "Kunifananisha na Ruby ni Kuukosea Heshima Mziki Wangu"

$
0
0

MREMBO aliyelikamata anga la Bongo Fleva, Nandy amewataka watu wanaomfananisha na mwanamuziki mwenzake Ruby kuacha mara moja kwa kuwa kila mtu ana ladha yake.
Akipiga stori na Showbiz Xtra, Nandy amesema, kwa muda mrefu mashabiki wake wamekuwa wakifananisha muziki wake na wa Ruby kitu ambacho haoni kama kina mashiko kwa kuwa kila mtu ana ladha yake ya kipekee ambayo mwenzake kakosa. “Namheshimu Ruby ni mwimbaji mzuri, lakini kunifananisha naye ni kuukosea heshima muziki wangu, ladha ya muziki wangu ni tofauti kabisa na Ruby kama unaujua vizuri muziki utabaini muziki wetu ni tofauti kabisa,” alisema Nandy bila kufafanua kwa undani zaidi.

Harmorapa "Bado Mimi Nipo Natrend Instagram...Watu Wananipost Kila Siku"

$
0
0

Msanii ambaye hakauki vituko mitandaoni Harmorapa, amewajibu watu wanaomsema kuwa amepotea pamoja na kiki zake zote, na kusema kwamba hajapotea isipokuwa yuko busy na biashara. 

Harmorapa ameyasema hayo leo kwenye eNewz ya East Africa Television, na kusema kwamba watu wanatakiwa wajue licha ya muziki Harmorapa ana maisha yake mengine ambapo pia ni mfanyabiashara, na sasa hivi yuko busy na kazi za biashara ikiwemo kusafiri, lakini mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu atawapa kazi mpya. 

"Watu waelewe sipo kimya, sasa hivi nipo busy na biashara nasafiri sana, ile kuonanana tu ni bahati,  project zangu za muziki zinaendelea kama kawaida wiki ijayo naachia dude jipya, watu wajue tu mimi nipo, wamemzoea Harmorapa leo kafanya hiki mara hiki, sasa hivi niko busy na muziki wangu bado upo, kama kutrend kila siku natrend, naingia Instagram nakuta tu mtu amenipost bado machoni mwa watu naonekana, bado mimi nipo na nitakuwepo na vitu vitaendelea", amesema Harmorapa. 

Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba msanii huyo ameshapotea kwenye game, kwani hawezi kufanya muziki na anachotegemea yeye ni kiki ambazo anazifanya na kuchekesha watu.

Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya Haitafika Mbali- Madee

$
0
0
Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uoya Haitafika Mbali- Madee
Msanii Madee Seneda ambaye ni baba mlezi wa Dogo Janja, amewataka maharusi wake Irene Uwoya na Dogo Janja kutosikiliza watu kwani wakifanya hivyo hata mwaka hawatamaliza.

Madee ameyasema hayo alipokuwa akipiga stori na Queen Fifi na JR kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba amefurahi kuona Dogo Janja kaoa ingawa alishtushwa na taarifa hizo, lakini kikubwa ni kuwaombea ili wasisikilize maneno ya watu.
Madee ameendelea kusema kwamba wawili hawa wote ni watu maarufu hivyo kutakuwa na maneno mengi kutoka kwa watu, na iwapo wakisikiliza basi ndoa yao haitafika mbali.


Daxo Chali Ni Mtoto Mdogo Siwezi Kubishana Naye- Nay wa Mitego

$
0
0
Daxo Chali Ni Mtoto Mdogo Siwezi Kubishana Naye- Nay wa Mitego
Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kusema hawezi kubishana wala kuongea chochote juu ya tuhuma ambazo Daxo Chali amekuwa akizitoa kwake na kusema yeye si mtu wa kubishana au kuongea na watoto wadogo.

Nay Wa Mitego amesema hayo alipohojiwa na eNewz na kusema mtayarishaji huyo wa muziki bado ni mtoto hata kazi yake bado hajaijua vizuri na kudai kutokana na hayo ndiyo maana anataka kuitia doa 'label' ya Mj Records kwa kupeleka mambo hayo kwenye vyombo vya habari.
Mtazame hapa Nay wa Mitego akifunguka zaidi.




Rosa Ree Awapa Makavu Wasanii Wanaonunua Idadi ya Views You Tube

$
0
0
Rosa Ree Awapa Makavu Wasanii Wanaonunua Idadi ya Views You Tube
Rapper Rosa Ree amefunguka mambo kadhaa kuhusu idadi ya views katika mtandao wa YouTube kutumika kama kigezo cha muziki kukubalika.

“Kuna watu wanaosikiliza muziki na kuupenda na kuukubali lakini hawana access ya YouTube, so many wanaweza kusikiliza hata wabibi kijijini wanasikiliza huo wimbo lakini hawana uwezo wa kuingia YouTube, so huwezi ukasema views za YouTube ndio uzuri wa wimbo au ndio ukubwa na kukubalika” amesema Rosa Ree.

Alipoulizwa iwapo anaamini kuwa kuna tabia ya wasanii kununua views kama inavyokuwa ikidaiwa, alijibu; “sijui kama inawezekana kwa hiyo hicho kitu siwezi kukiongelea kitu ambacho sikijui, mimi personal sijawahi kununua views”.

Kwa sasa Rosa Ree anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Dow ‘ baada ya kukimbiza na ngoma kama Up In The Air na One Time.


Kijana Aliyevamia Shule na Kubaka Walimu na Wanafunzi Akamatwa

$
0
0
Kijana Aliyevamia Shule na Kubaka Walimu na Wanafunzi Akamatwa
Polisi imemdaka kijana alievamia shule na kujaribu kubaka Walimu na Wanafunzi kwa mkupuo Arusha.

Ndio utajiuliza aliwazaje au kuanzaanza vipi kufikiria kwamba anaweza kuvamia shule na kuwabaka kwa mara moja Walimu pamoja na Wanafunzi.

Hata hivyo kijana huyo aitwae Musa Shakifu hakufanikiwa kwenye jaribu hilo la kuvamia shule ya Msingi Oltroto iliyopo Arumeru na tayari Jeshi la Polisi limemdaka ambapo Kamanda wa Polisi Charles Mkumbo amesema wanaendelea kumuhoji.



Mwalimu wa zamu kwenye shule hiyo amekiri kuvamiwa na kijana Musa ambae alionekana kutumia nguvu za kupitiliza kutaka kuwabaka kwa mkupuo Waalimu pamoja na Wanafunzi.

Sijaalikwa Kwenye Ndoa ya Dogo Janja Kwakuwa ni Kiki Ingekuwa Kweli Ningealikwa- Nandy

$
0
0
Sijaalikwa Kwenye Ndoa ya Dogo Janja Kwakuwa ni Kiki Ingekuwa Kweli Ningealikwa- Nandy
STAA wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amefunguka kuwa, kama msanii mwenzake, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’ angemuoa msanii wa Bongo Muvi, Irene Uwoya ni lazima angealikwa kutokana na ukaribu waliokuwa nao.

Akipiga stori na Star Mix, Nandy alisema kipindi hiyo ishu inatokea alikuwa kwenye ziara ya kimuziki lakini licha ya hivyo ni wazi angejulishwa.

“Kwa kuwa ishu imebainika ni kiki sioni haja ya kuwalaumu wawili hao kwa kuwa naamini hawakukurupuka kufanya hivyo. Lakini kama ingekuwa kweli ningealikwa tu,”alisema.

Ujumbe wa Nape Nnauye Baada ya Nyarandu Kujiuzulu' Chama Cha Siasa Ni Itikadi'

$
0
0
Ujumbe wa Nape Nnauye Baada ya Nyarandu Kujiuzulu' Chama Cha Siasa Ni Itikadi'
Baada ya Mbunge wa Singida Kaskazini kujivua ubunge na kujiondoa katika chama cha Mapinduzi(CCM), Lazaro Nyalandu hatimae Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa Chama cha siasa ni Itikadi.

Nape kupitia ukurasa wake wa twitter ameweka picha inayomuonyesha mbunge huyo na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ndg Kinana wakiwa wameweka kwa pamoja alama ya kidole gumba.

Chama cha siasa ni ITIKADI, itikadi ni IMANI.Siamini SANA katika kubadili Imani KIENYEJI.Nitashughulikia MAPUNGUFU nikiwa ndani sio NJE!

Nyalandu alikihama chama cha Mapinduzi Oktoba 30 mwaka huu ambapo alieleza kuwa amechoshwa na mwenendo wa siasa wa sasa.


Steve Nyerere Afunguka Anavyokoshwa na Aunt Ezekiel 'Bongo Muvi Ninamuheshimu Aunt Pekee'

$
0
0
MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Steve Nyerere amefunguka kuwa mwanamke anayemheshimu Bongo Muvi kwa sasa ni Aunt Ezekiel pekee.

Akizungumza na Star Mix Steve alisema kuwa, anamheshimu kwa sababu ni mwanamke ambaye hajabweteka na amejitahidi sana kukusanya hela anazopata kufanya mambo ya maana kama alivyojenga nyumba maeneo ya Kigamboni tofauti na mastaa wengine.

“Yaani kwa kweli Bongo Muvi kwa wanawake nampa heshima kubwa Aunt,ni mdada ametulia na mzazi mwenziye amepata watoto lakini pia ameweza kujituma mpaka kujenga nyumba tofauti na wengine,”alisema Steve   

Akaunti ya Twitter ya Rais Trump 'Yapotea kwa Muda''

$
0
0
Akaunti ya Twitter ya Rais Trump 'Yapotea kwa Muda''
Akaunti ya mtandao wa Twitter ya rais Donald Trump ilipotea kwa muda siku ya Alhamisi lakini, ikarudishwa baadaye , kampuni hiyo imesema.
Twitter imesema kuwa akaunti hiyo kwa jina @realdonaldtrump iliondolewa na mfanyikazi mmoja na baadaye kuelezea kuwa ilikuwa siku yake ya mwisho kazi.
Akaunti hiyo iliondolewa kwa muda wa dakika 11 na sasa kampuni ya Twitter inachunguza.
Bwana Trump ambaye ni mtumizi wa mtandao wa Twitter wa mara kwa mara akiwa na wafuasi milioni 41.7 hajatoa tamko lolote kuhusu swala hilo.
Siku ya Alhamisi jioni, wale waliotembelea akaunti ya rais Trump waliona ujumbe uliosema ''pole ukurasa huu hauko kwa sasa!''
Baada ya akaunti kurejeshwa , ujumbe wa kwanza wa bwana Trump ulikuwa kuhusu ule mpango wa Republican wa kupunguza kodi.
Hatahivyo@POTUS ambayo ndio akaunti rasmi ya rais Trump haukuathiriwa.

Twitter imesema kuwa inachunguza tatizo hilo na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa kisa kama hicho hakitokei tena.
Kampuni hiyo ilisema katika ujumbe wake kwamba wamebaini katika uchunguzi wao kwamba kisa hicho kilifanywa na mfanyikazi anayewahudumia wateja ambaye alifanya hivyo katika siku yake ya mwisho ya kazi.
Tunatathmini kisa chote kikamilifu.
Bwana trump alijiunga na mtandao wa twitter mnamo mwezi Machi 2009.
Amekuwa mtumiaji mkubwa wa mtandao huo kwa kukuza sera zake mbali na kuwashambulia wapinzani wake wakati wa kampeni za urais 2016 na hata baada ya kuchukua mamlaka mnamo mwezi Januari.

Kutana na Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed Kutoka Bagamoyo...Ana Dawa za Kurudisha Mapenzi na Zingine Nyingi

$
0
0
MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

USHAURI: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.

Shilawadu Mnaelekea Kaburini Kuna la Kujifunza Toka Kikundi cha ze Comedy ya Masanja

$
0
0
Miaka ya zamani kidogo Kikundi cha ZE COMEDY cha kina Masanja -mkandamizaji na wenzake kilikuwa na umaarufu na hata kupita baadhi wasanii wa muziki wa dansi, bongo fleva na hata bongo movies. Walikuwa wakipata mialiko mikubwa ya pesa ndefu kwenye sherehe, mikutano na majeshini kwenda kutumbuiza watu.

Kuna Kipindi Masanja alikuwa maarufu mpaka alikuwa hawezi kutembea mitaani hovyo bila ya walinzi na alijaribu hata kugombea ubunge katika jimbo moja huko nyanda za juu.Umaarufu wa ZE COMEDY ulianza kupungua baada ya kuanza kufanya vichekesho vya upande mmoja, kufurahisha wakubwa, kulewa sifa na kujiingiza kwenye siasa au kukubali kutumiwa na wanasiasa.

KIPINDI CHAO CHA SAA MOJA USIKU ENZI HIZO KILIKUWA MAARUFU KULIKO HATA TAARIFA YA HABARI.

Kipindi cha SHILAWADU ingawa nao walianza kwa kasi lakini naona wanaanza kuelekea kaburini.Kama SHILAWADU ni kuhusu umbea ni kwanini umbea mwingine wanaogopa kusema ,kwaninini siku hizi kila umbea wanaosema wa msanii unafuatana na kutambulisha wimbo mpya wa msanii, ina maana sio umbeya tena ni vitu mnapanga kabla, matangazo yamekuwa mengi na mmebakiwa na vitu viwili tu ni HAMISA MOBETO na DIAMOND.

Hata leo najua MAPOVU NI HAYO TU na mtakuwa mnaandaa msanii wa kutambulisha ngoma mpya baada ya kutunga skendo, hivi ile ya zamaradi na Ruge mbona ahtukusikia mapovu!!!

KUWENI MAKINI mnaelekea kubaya

By Kasulamkombe

Full Video: Harusi ya Dongo Janja na Irene Uwoya

$
0
0
Wakati mjadala ukiendelea kuhusu taarifa zinazodai Dogo Janja na Irene Uwoya kufunga ndoa, hatimaye Dogo Janja ametuletea video hii inayoonyesha tukio zima la sherehe yake. VIDEO:

Msimamo wa Nape Nnauye Kuhusu Kuhama CCM

$
0
0
Mbunge wa Mtama kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kwamba haamini katika masuala ya kuhama chama cha siasa kwa sababu kila chama kina itikadi yake na kwamba, itikadi ni sawa na imani ambayo mtu hawezi kuhama kienyeji kama inavyodhaniwa.

Nape ambaye amewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alisema endapo kwenye chama chake kutakuwa na mapungufu, atayashughulikia akiwa ndani, na sio kuhama chama.

“Chama cha siasa ni itikadi, itikadi ni imani. Siamini sana katika kubadili imani kienyeji. Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani sio nje!,”  aliandika Nnauye.

Katika maneno, Nape aliambatanisha na picha yake akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye alitangaza kukihama chama hicho kutokana na kile alichodai kuwa kimepoteza mwelekeo na kwamba hakiwezi tena kuisimamia serikali kama ilivyokuwapo awali.

Nyalandu ambaye amekitumikia Chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa alisema kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna moja au nyigine, CCM nayo imekuwa chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Oktoba 30 Nyalandu alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kusema kuwa angependelea kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa kidemokrasia na uhuru wa mawazo.

Tangu alipotenguliwa Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekuwa akihusishwa na tetesi za kukihama chama hicho, jambo ambalo amekuwa akikanusha mara kwa mara akiamini kwamba hahitaji kuto

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.

Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Kajala Amwagia Manoti Kassim Mganga

$
0
0
Kajala Amwagia Manoti Kassim Mganga
HUKU watu mbalimbali wakiwemo maarufu nchini wakilia kuwa, hali ya uchumi siyo nzuri ‘vyuma vimekaza’, mwanadada anayefanya vizuri kwenye ulimwengu wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ hivi karibuni ameibua gumzo baada ya kumfanyia kufuru Kassim Mganga ambaye ni staa wa muziki wa Bongo Fleva.

Kufuru aliyoifanya Kajala ni ya kummwagia minoti Kassimu alipokuwa akitumbuiza kwenye shoo katika Ukumbi wa Next Door uliopo Masaki jiji Dar, kiasi cha kuibua gumzo kutoka kwa wahudhuriaji waliofika ukumbini hapo.

“Mh! Jamani kweli kwa watu wengine vyuma vimeachia, yaani kwenye hali kama hii mtu anaweza kumwaga minoti hivi? Kweli ukisema huna pesa, si kila mtu hana pia,” alisikika mwanadada mmoja aliyekuwa kwenye shoo hiyo.
Naye njemba mwingine ambaye alikuwa karibu na paparazi wetu alisikika akimwambia mtu aliyekuwa amekaa naye karibu kwamba: “Matukio ya watu kufanya kufuru kwa kumwaga noti siku hizi yamepungua

Na hata kwa ambao bado wanamwaga minoti, wengi ni wanawake tofauti na wanaume walivyokuwa wanafanya, labda kwa sababu wengi wao wanahongwa.” Hata hivyo, kwa Kajala maneno hayo ambayo watu mbalimbali walikuwa wakizungumza kutokana na tukio alilokuwa analifanya ni kama yalikuwa yanamhamasisha kuendelea kumfanyia kufuru Kassim kwani aliendelea kumdondoshea monoti huku mwanamuziki huyo akilitaja jina lake (Kajala).


Baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alimtafuta Kajala ili aweze
kulizungumzia tukio hilo ambapo alifunguka; “Kiukweli Kassimu mimi alinikosha. Wimbo wake aliokuwa anauimba wa Somo ninaupenda sana na ndiyo maana sikuona shida kummwagia minoti. “Sifikirii kama ni kitu kibaya mtu kuonesha furaha yake, hasa sehemu za burudani kama hizo ambazo tunakwenda kwa ajili ya kuzifurahisha nafsi zetu.”

Kajala alipoulizwa alimmwagia mkali huyo wa Bongo Fleva kiasi gani cha fedha alisema kuwa, hakumbukuki maana hakuwa anahesabu na kuongeza kuwa kwake hilo ni suala la kawaida kabisa hasa akiwa amefurahishwa kwa kupewa kile ambacho moyo wake unapenda. “Pesa kama hivyo siwezi kuona shida kutoa pale ninapokuwa kwenye furaha zangu, ninatafuta kwa ajili ya kutumia na matumizi yenyewe ndiyo kama hayo,” alimaliza Kajala.
Chanzo Global Publishers
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images