Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Ni Kweli Kimeeleweka -Navy Kenzo

$
0
0
Ni Kweli Kimeeleweka -Navy Kenzo
NAVY Kenzo kruu ya watoto wa kishua katika Afrika Mashariki, inaundwa Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ na Aika Mareale. Mbali na kufanya Bongo Fleva katika level za juu, pia wanamiliki lebo ya The Industry iliyowahi kuwasainisha wanamuziki kadhaa wakiwemo Rosa Ree na Wildad.

Baada ya mwaka jana kutikisa na Albamu ya AIM (Above In A Minute) wakiwa na ngoma kadhaa ikiwemo Kamatia Chini, mwaka huu wameonekana kupunguza makeke. K
utokana na ukimya huo, Over Ze Weekend ilimsaka mmoja wa memba, Aika ambaye juzikati zilisambaa habari kuwa ni mjamzito ili aweze kufungukia sababu za ukimya wao, lakini pia ishu ya ujauzito, tetesi za kufulia na kuondokewa na wanamuziki wote ndani ya lebo.

Huyu hapa; Over Ze Weekend: Hongera kwa ujauzito Aika.
Aika: Asante, ni kweli kimeelewekaaa…hahahaa…
Over Ze Weekend: Unatarajia kujifungua lini?
Aika: Desemba 2, mwaka huu. Over Ze Weekend: Waoh! Mungu awe upande wako na bila shaka, mmekwishachungulia na kujua jinsi ya mtoto?
Aika: Ndiyo, ni mtoto wa kiume na jina lake ataitwa Gold.
Over Ze Weekend: Je, inawezekana suala lako la ujauzito ndilo limefanya Navy Kenzo kupotea kwenye gemu?
Aika: Siyo kweli. Hatujapotea, tupo tu kimya na tuliamua kuwa hivyo kutokana na hali yangu ya ujauzito.

Over Ze Weekend: Lakini hamuoni kukaa kimya kunawafanya kuwa mbali na ‘fansi’ wenu? Kwa nini usingekuwa kimya wewe mwenye ujauzito na Nahreel akafanya kazi kama kawaida.
Aika: Tunafanya kazi kama kundi na tumekuwa kimya labda kwa kutoa tu wimbo, lakini mbali na mimi kuwa kwenye hali hii, tunafanya shoo nyingi tu.
Over Ze Weekend: Unakwenda kuwa mama, je, nini
Over Ze Weekend: Je, kuna kitu special ambacho unaweza kuwaeleza mashabiki wenu, utajifungulia wapi na mmeandaa nini baada ya mtoto kuzaliwa?
Aika: Haaa… haaa,
surprise ni surprise tu. Watu wasubiri vitu vizuri havihitaji haraka.
Over Ze Weekend: Ni siri gani mnayo kwa kudumu kama kundi ilhali ni wapenzi?
Aika: Kuheshimiana, tunapokuwa kazini, mimi ninasimama kama Aika na Nahreel anasimama kama Nahreel na ndiyo maana tunaenda.
Over Ze Weekend: Mngependa mtoto wenu aje kurithi kipaji chenu?

Aika: Unajua hatuwezi kumchagulia ila akiwa mkubwa atachagua mwenyewe
kitabadilika kwenye kazi yako ya muziki? Aika: Hakuna kitakachobadilika. Aika ni yuleyule, suala la kuwa mama ni baraka nyingine kwenye maisha yangu.
Over Ze Weekend: Navutiwa kuendelea kuuliza, je, ni kweli kuwa ndiyo sababu pia ya wanamuziki wa lebo yenu kuwakimbia?
Aika: Si kweli, baadhi ya wanamuziki wetu tumewaondoa na wengine wameondoka wenyewe.
Over Ze Weekend: Kwa nini mmewaondoa?
Aika: Sitapenda kuzungumzia sana maana hilo limekwishapita.

Over Ze Weekend: Je, mmewaondoa au wameondoka wote?
Aika: Ndiyo! Navy
Kenzo ni Aika na Nahreel tu kwa sasa.
Over Ze Weekend: Vipi kuhusu kufulia? Je, ni kweli mmeshindwa kuendeleza ujenzi wa mjengo wenu wa ghorofa mliouanza kwa mbwembwe nyingi, kumudu kuendesha lebo na kuwahudumia wanamuziki walioondoka? Aika: Hili nalo ninalisikia kwako kwa mara ya kwanza.
Sisi hatujafulia, tunaendelea na biashara zetu na mambo yetu yanakwenda vizuri tu. Nikuambie tu kwa mwaka huu, Navy Kenzo wamefanya vitu vikubwa kuliko miaka mingine

Simba Yatimiza Ahadi Yake, Yarejea Kieleni

$
0
0
Simba Yatimiza Ahadi Yake, Yarejea Kieleni
Klabu ya soka ya Simba imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Mbeya City jioni ya leo.

Simba ilifanikiwa kupata bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 7 akipokea pasi safi ya Jonas Mkude ambaye leo ameanza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza msimu huu.
Bao la Kichuya lilifanikiwa kudumu kwa dakika 45 za kwanza pamoja na kuwepo kwa mashambulizi ya hapa na pale kwa timu zote mbili, lakini umakini wa walinda milango Aishi Manula wa Simba na Fikirini Bakari wa Mbeya City uliwanyima nafasi ya kufunga washambuliaji wa timu hizo.
Simba sasa imefikisha alama 19 na kupaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiishusha hadi nafasi ya pili timu ya Azam FC yenye alama 19 pia zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Baada ya mchezo wa leo raundi ya 9 imekamilika ambapo ligi itasimama kidogo kupisha kalenda ya shirikisho la kimataifa la soka FIFA, ambapo timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars itasafiri kucheza na Benin.

Watu 26 Wauawa kwa Kupigwa Risasi Kanisani Texas, Marekani

$
0
0
Watu 26 Wauawa kwa Kupigwa Risasi Kanisani Texas, Marekani
Watu 26 wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu mwenye silaha aliyewafyatulia risasi waumini katika kanisa moja jimbo la Texas wakati wa ibada, maafisa wanasema.
Shambulio hilo lilitekelezwa katika kanisa la First Baptist Church katika mji wa Sutherland Springs, mji mdogo katika wilaya ya Wilson, Texas.
Mshambuliaji, ambaye anadaiwa kuuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo, aliingia kanisani na kuanza kuwafyatulia risasi watu mwendo wa saa tano unusu asubuhi (17:30 GMT).
Gavana Greg Abbott amethibitisha idadi ya waliofariki na kusema ndicho kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutekelezwa kwa kutumia bunduki katika historia ya texas.
"Kutakuwa na majonzi na masikitiko mengi kwa wale walioathiriwa," aliambia wanahabari.
Mkuu wa idara ya usalama wa Texas Freeman Martin amesema waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 72.
Kwa nini raia hawawezi kupokonywa bunduki Marekani
Maafisa wamesema watu zaidi ya 20 pia walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.
Bw Martin amesema mshukiwa ni mwanamume mzungu wa umri wa miaka 20 ambaye alikuwa amevalia mavazi meusi na fulana ya kujikinga dhidi ya risasi pamoja na kuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa.
Alianza kufyatua risasi nje ya kanisa kabla ya kuingia ndani na kuendelea kufyatulia watu risasi.
A woman and her children take part in a vigil for victims of a mass shooting in Sutherland Springs, Texas, US., November 5, 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Mwanamke na watoto wake wakishiriki ibada ya mkesha kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio la Sutherland Spring, Texas
Wakazi walihudhuria mkesha wa kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio hilo la Sutherland SpringsHaki miliki ya pichaAFP
Image caption
Wakazi walihudhuria mkesha wa kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio hilo la Sutherland Springs
Mwenyeji "alitwaa bunduki yake na kuanza kumfyatulia " risasi mshukiwa kabla ya mshukiwa huyo kutoroka akitumia gari.
Raia huyo alimwandama mshukiwa huyo ambaye aliendesha gari lake na kisha kuliangusha katika barabara wilaya ya Guadalupe.
Polisi waelimpata mshukiwa akiwa amefariki ndani ya gari lake.
Haijabainika iwapo alifariki kutokana na majeraha ya risasi aliyojisababishia mwenyewe au kutokana na mejaraha kutoka kwa raia huyo, Martin ameongeza.
FBI officials arrive at the site of a mass shooting in Sutherland Springs, TexasHaki miliki ya pichaKSAT 12 / REUTERS
Image caption
FBI wamefika kufanya uchunguzi
Mshukiwa ametajwa kuwa Devin P Kelley, 26, kwa mujibu wa vyombo vya jhabari Marekani.
Polisi bado hawajathibitisha jina lake.
Mhubiri wa kanisa hilo la First Baptist Frank Pomeroy, ameambia ABC News kwamba binti yake wa miaka 14 kwa jina Annabelle ni miongoni mwa waliouawa.
Sutherland Springs ni mtaa mdogo wenye wakazi wasiozidi elfu moja ambao hupatikana kilomita 50 hivi kusini mashariki mwa mji wa San Antonio mjini Texas.
Maafisa wa FBI kutoka San Antonio wametumwa kufanya uchunguzi lakini kufikia sasa lengo la mshambuliaji halijabainika.

Rais Donald Trump, ambaye yumo ziarani Asia, ameshutumu kisa hicho na kusema ni "kitendo cha uovu" na kusema kwamba Wamarekani watajikwamua na kusalia na umoja.
"Na kupitia kwa machozi na kupitia huzuni hii, tunasalia imara, imara zaidi," ameongeza.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump
 Donald J. Trump ✔@realDonaldTrump
May God be w/ the people of Sutherland Springs, Texas. The FBI & law enforcement are on the scene. I am monitoring the situation from Japan.
11:06 PM - Nov 5, 2017
 39,398 39,398 Replies   34,356 34,356 Retweets   146,067 146,067 likes
Twitter Ads info and privacy
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump
Mauaji hayo yametokea mwezi mmoja tu baada ya mshambuliaji mwingine kufyatulia risasi watu waliokuwa wakihudhuria tamasha ya muziki Las Vegas na kuwaua watu 58 pamoja na kujeruhi mamia wengine, katika kisa kibaya zaidi cha mauaji ya kutumia bunduki katika historia ya Marekani nyakati za karibuni.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Afariki Katika Ajali ya Ndege

$
0
0
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Afariki Katika Ajali ya Ndege
Mwanamfalme mmoja nchini Saudi Arabia amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na yemen, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, naibu gavana wa mkoa wa Asir, alikuwa akisafiri pamoja na maafisa kadha wa serikali helikopta hiyo ilipoanguka, runinga ya Al-Ikhbariya imesema.
Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.
Saudi Arabia ilisema ilitungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi.

Pia, wikendi, watu wengi wakiwemo wana wafalme 11 na mawaziri wanne walikamatwa katika kampeni ya kukabiliana na rushwa ambayo inatazamwa kama njama ya kuimarisha mamlaka ya mrithi mtarajiwa wa ufalme.
Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi Mohammed bin Salman.
Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, aliyefariki, ni mwana wa mwanamfalme aliyekuwa wa kwanza katika urithi awali.
Babake, Muqrin bin Abdul Aziz, alitengwa na ndugu wa kambo wa Mfalme Salman miezi kadha baada yake kurithi ufalme mwaka 2015.
Shirika la habari la Okaz limesema taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema hakukuwa na manusura kwenye ajali hiyo ya ndege.

Majambazi Wameuawa kwa Kupigwa Risasi na Polisi

$
0
0
Majambazi Wameuawa kwa Kupigwa Risasi na Polisi
Watu watano wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi waliokuwa doria.

Taarifa ya polisi imesema watu hao waliuawa walipojaribu kuwavamia wafanyabiashara wa madini katika machimbo ya Mwime nje kidogo ya Mji wa Kahama.

Watuhumiwa pia wanadaiwa kuhusika na mauaji ya viongozi wa Serikali ya Mtaa, polisi na wanasiasa mkoani Pwani katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alisema jana kwamba watu hao walijeruhiwa usiku wa kuamkia jana katika eneo la Mwanva katika Halmashauri ya Mji wa Kahama walipokabiliana ana kwa ana na polisi waliofika eneo hilo.

Kamanda Haule alisema baada ya polisi kufika kwenye eneo la tukio, watu hao walijificha kwenye mashimo yanayotumiwa kuchimba mchanga na kuanza kurushiana risasi na askari.

Alisema katika mapambano hayo, watuhumiwa walizidiwa nguvu na kujeruhiwa na walifariki dunia walipokuwa njiani kupelekwa hospitali.

Alisema katika eneo la tukio, polisi walikuta bunduki moja aina ya SMG na risasi 25 zilizokuwa kwenye magazini. Pia walikuta mabomu mawili ya kutupa kwa mkono.

Katika uchunguzi wa awali, Kamanda Haule alidai kwamba watu hao ni miongoni mwa waliokuwa wakifanya uhalifu mkoani Pwani ambao walikimbia huko baada ya kudhibitiwa.

Kamanda Haule aliwataka wananchi kufika katika Hospitali ya Mji wa Kahama kuwatambua marehemu kauli ambayo pia ilitolewa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kahama, Dk David Lucas.

Shuhuda wa tukio hilo, Justina Elias alisema walisikia milio ya risasi saa tatu usiku wa kuamkia juzi na baada ya muda walitoka kwenda kuangalia na kukuta watu wakiwa wameuawa.

ACT Wazalendo Watoa Msimamo Wake Kujiunga Ukawa

$
0
0
ACT Wazalendo Watoa Msimamo Wake Kujiunga Ukawa
Chama cha ACT Wazalendo kimeweka wazi msimamo wake kuhusu suala la kujiunga na UKAWA ambapo kimesema suala hilo ni pana na lazima lizingatie maslahi ya chama.

Akiongea leo kwenye kipindi cha East Afrika Breakfast cha East Afrika Radio, Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho Ado Shaibu, amesema suala la kujiunga au kutojiunga UKAWA litaamuliwa na wanachama na viongozi.
“Ni kweli kila mtu anazungumza yake kuhusu msimamo wa chama chetu lakini ukweli ni kwamba kwa hali ya kisiasa ilivyo nchini kuna mambo yanalazimu vyama vya upinzani vishirikiane, lakini ikija suala la kujiunga UKAWA lazima ujue maslahi ya chama ndani ya umoja huo”, amesema Ado Shaibu.
Ado ameongeza kuwa ikifikia wakati kuna ulazima wa ACT Wazalendo kujiunga na UKAWA basi suala hilo litaamuliwa na viongozi pamoja na wanachama.

Kwa upande mwingine Shaibu amewataka wanachama wa ACT Wazalendo kuendelea kukiunga mkono chama hicho wakati huu ambao sera zake zimejikita zaidi kwenye kuutafuta uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara kwani ndio njia pekee ya kuongea na wananchi moja kwa moja.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..


JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.

Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Wanachadema 12 Wakamatwa kwa Kumshambulia Diwani Arusha

$
0
0
Wanachadema 12 Wakamatwa kwa Kumshambulia Diwani Arusha
Siku kadhaa baada ya wanachama 12 kutoka Chadema kukamatwa kwa kosa la kumshambulia mgombea wa udiwani wa kata ya Muriet wilayani Arusha, Francis Mbise wanatarajiwa kupandishwa kizimbani leo.

Wafuasi hao akiwemo Kaimu Katibu wa Chadema wilayani Arusha, Innocent Kisanyage walishikiliwa  na polisi eneo la FFU kwa Morombo wakidaiwa kumshambulia mgombea huyo wa CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Novemba 5 Kamanda  wa Polisi jijini Arusha (RPC), Charles Mkumbo alisema kwamba wafuasi hao wote 12 watafikishwa mahakamani leo Jumatatu.

Madee Akerwaa na Wanasema Ndoa ya Dogo Janja na Iren Uwoya ni Kiki

$
0
0
Madee Akerwaa na Wanasema Ndoa ya Dogo  Janja na Iren Uwoya ni Kiki
Msanii Madee ameonyesha kukerwa na baadhi ya watu hata wasanii ambao wanadai ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ni kiki.

Madee ambaye ni kama Baba Mleze wa Dogo Janja ameiambia FNL ya EATV kuwa kitu hicho ni kibaya sana kwani kuna uwezekano msanii akawa anahitaji msaada wa haraka na watu wakachukulia hilo kama kiki.

“Kitu ambacho nimekigundua na ni kibaya na kinaendelea kutokea ni watu kuamini katika kiki, hata leo ikitokea nimegongwa na gari nakuumia watu bado wataamini ni kiki na kushindwa kunisaidia,” amesema Madee.

“So kama hili suala lingekuwa la kumsaidia Janja ili aokoke kwenye jambo labda ni baya basi tungekuwa tumeshamuumiza kwa sababu watu wote wanaamini kwenye kiki, hadi sasa watu wengi hawaamini kama Dogo Janja, hivi vitu vingine vya kusema kiki tuviache” ameongeza Madee.

Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa yao October, 28 mwaka huu kwa mujibu taarifa za mitandao ya kijamii lakini September 4 ndipo Dogo Janja aliweka wazi hilo kuwa wamefunga ndoa.

ACT Wazalendo Watoaa Msimamo Wake Kuhusu Kujiunga na UKAWA

$
0
0
ACT Wazalendo Watoaa Msimamo Wake Kuhusu Kujiunga na UKAWA
Chama cha ACT Wazalendo kimeweka wazi msimamo wake kuhusu suala la kujiunga na UKAWA ambapo kimesema suala hilo ni pana na lazima lizingatie maslahi ya chama.

Akiongea leo kwenye kipindi cha East Afrika Breakfast cha East Afrika Radio, Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho Ado Shaibu, amesema suala la kujiunga au kutojiunga UKAWA litaamuliwa na wanachama na viongozi.
“Ni kweli kila mtu anazungumza yake kuhusu msimamo wa chama chetu lakini ukweli ni kwamba kwa hali ya kisiasa ilivyo nchini kuna mambo yanalazimu vyama vya upinzani vishirikiane, lakini ikija suala la kujiunga UKAWA lazima ujue maslahi ya chama ndani ya umoja huo”, amesema Ado Shaibu.
Ado ameongeza kuwa ikifikia wakati kuna ulazima wa ACT Wazalendo kujiunga na UKAWA basi suala hilo litaamuliwa na viongozi pamoja na wanachama.

Kwa upande mwingine Shaibu amewataka wanachama wa ACT Wazalendo kuendelea kukiunga mkono chama hicho wakati huu ambao sera zake zimejikita zaidi kwenye kuutafuta uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara kwani ndio njia pekee ya kuongea na wananchi moja kwa moja.

Kalapina Afunguka Kuhusu Harmorapa

$
0
0
Msanii wa muziki wa rap Bongo, Kalapina amefichua kilichompoteza Harmorapa katika game baada ya kung’aa kwa kipindi kifupi.

Rapper huyo ambaye pia mtangazaji wa tv, amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm kuwa kupotea kwa Harmorapa kunatokana na kuwa kiki nyingi kuliko kazi.

“Kuna dogo mmoja alikuwa ana kiki alioneka hata wakati Mhe. Nape anatolewa kwaju katika mambo ya watu wasiojulikana yanaanza kurise akatoka baruti anaitwa nani yule mtoto? (Hamorapa), yeah!!, zilikuwa ni kiki kazi ndogo mcheki sasa yupo wapi” amesema Kalapina.

Amendelea kwa kusema kuwa kiki ni vitu vya uongo uongo na havina maana katika maisha ya kimuziki ya msanii badala yake wasanii wafanye kazi nzuri, waandike mistari ambayo inawashika watu mpaka mtu ajiulize huyo alifikiria nini kuandika hii ngoma

Msanii Patoranking Apata Shavu Kwenye Jarida la Guardian

$
0
0
Msanii Patoranking Apata Shavu Kwenye Jarida la Guardian
Kila mwenye mafanikio ana stori juu ya kuyapata mafanikio hayo na ndiyo maana jarida la Guardian kupitia kipengere cha Life, kutoka Nigeria limempa shavu mkali wa muziki Patoranking kuelezea mambo kadhaa yanayohusu maisha yake kabla ya kuingia katika game.

Patoranking, ambaye jina lake halisi ni Patrick Nnaemeka Okorie, msanii wa muziki na muandishi wa mashairi anayefanya muziki wa reggae na dancehall uliochanganywa na twist ya Nigeria amezungumzia mambo kadhaa yanayomuhusu yeye kupitia jarida hilo liliotoka hapo jana.

Patoranking pia amezungumzia maisha aliyokulia Ebute Metta pamoja na jina lake aliloliamini kabla ya mafanikio

Zitto Kabwe, Hana Mpango wa Kurudi CHADEMA- Addo Shaibu

$
0
0
Zitto Kabwe, Hana Mpango wa Kurudi CHADEMA- Addo Shaibu
Msemaji wa chama cha ACT Wazalendo, Addo Shaibu, amesema kiongozi wa chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe, hana mpango kabisa wa kurudi CHADEMA, licha ya kuwa na harakati kama zao na kuomba ushirikiano wao.

Addo Shaibu ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba licha sasa hivi ACT Wazalendo kimeamua kuendeshwa kiharakati kama ilivyo CHADEMA, na licha ya kutaka kuunganisha nguvu katika baadhi ya mambo ambayo yataupa ushindi upinzani, lakini ifahamike kuwa hana mpango wa kurudi huko.
“Tunajua kwa nini Zitto aliondoka, alikuwa na mgogoro na CHADEMA, na ndio sababu ya kuanzisha ACT, wakitazama lugha yake kwamba wapinzane tushirikiane wanaona kama lugha yake na CHADEMA imekuwa haina tofauti, mazingira ya kisiasa ndio yanalazimika hivyo, mambo wanayoyapitia CHADEMA na sisi tunayapitia, inalazimisha lugha iwe ya pamoja, hatuwezi kuunganisha vyama, na nakuhakikishia Zitto hana mpango kwa sasa wa kurudi ndani ya CHADEMA”, amesema Addo Shaibu.
Hivi karibuni Zitto Kabwe alisikika akiomba ushirikiano kutoka kwa vyama vya upinzani hususan CHADEMA ili kuweza ksuhinda kwenye chaguzi ndogo ndogo za udiwani zinazokuja, na kuibua hisia kuwa huenda chama hicho sasa kinataka kujiunga na CHADEMA kuwa pamoja.

Zitto Kabwe Aitikia Wito wa Polisi

$
0
0
Zitto Kabwe Aitikia Wito wa Polisi
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Doroth Semu amefika katika kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha kilichopo Kamata, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Semu amefuatana na Katibu wa Kamati ya Ulinzi ya chama hicho, Mohamed Babu.

Viongozi hao pamoja na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Yeremia Maganja wanatakiwa kufika katika kitengo hicho wakiwakilisha wajumbe wote wa Kamati Kuu ambao walitakiwa kuripoti leo.

Wakati viongozi hao wakiwasili hapo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe ameripoti Kituo cha Polisi Chang'ombe jijini Dar es Salaam ambako anatuhumiwa kwa uchochezi.

Baada ya kuripoti kituoni hapo, Zitto ametakiwa kurejea tena Ijumaa Novemba 17,2017.

“Nimeambiwa nirudi wiki ijao siku ya Ijumaa Novemba 17," amesema Zitto.

Kiongozi huyo ameelekea Kamata ambako anatakiwa kuripoti katika kitengo cha uhalifu wa makosa ya kifedha.



Godbless Lema Amefungua Mkakati Uliopangwa na Jeshi la Polisi Kumkamata

$
0
0
Godbless Lema Amefungua Mkakati Uliopangwa na Jeshi la Polisi Kumkamata
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa kuna  mkakati umepangwa na jeshi la polisi ili akamatwe.

Mh. Lema kupitia ukurasa wake wa twitter amesema kuwa wanaishi maisha magumu na hawana budi kuvumilia maisha hayo.

Mkakati umepangwa,nikamatwe na na Jeshi la Polisi leo,maelekezo yamekwishatolewa .Tunaishi maisha magumu sana,hatuna budi kuvumilia.

Lema ni Mbunge ambaye amezoeleka mara nyingi kutumia ukurasa wake wa twitter kueleza mambo mbalimbali yanayoihusu jamii na yeye pia.

Mwigulu Nchemba Awataadhalisha Wananchi

$
0
0
Mwigulu Nchemba Awataadhalisha Wananchi
Waziri wa Mambo ya Ndani na Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM  amewataka wananchi ambao wanafanya uchaguzi mdogo wa udiwani nchini wasitumie hasira kwenye upigaji kura bali wachague wagombea wa CCM ili kutimiza nguzo

tatu za uongozi.
Mh. Nchemba ameyasema hayo wakati akimnadi Mgombea udiwani wa kata ya Nangwa wilaya ya Hanang  ambapo amewaambia wananchi watambue kwamba serikali iliyopo madarakani inaongozwa na CCM hivyo kuwachagua wwagombea hao 
Aidha Mh. Nchemba ameongeza kwamba uchaguzi mdogo ni uchaguzi rahisi sana kama watu wataamua kutafakari kwasababu ilani inayotekelezwa ni ya CCM na la pili ni huu ni uchaguzi wakujaza nafasi
"Kwasasa ilani inayofanya kazi ni ya CCM hivyo msifanye hasira katika kuchagua kwani huwezi kuwasha tochi kwa kuweka mabetri mawili ya CCM alafu la tatu liwe bunzi, Tochi haiwezi kuwaka," Mh. Nchemba
Pamoja na hayo Nchema amewataka wananchi hao waweze kumpitisha mgombea huyo mwanamke kwa kudai kwamba anafaa kuongeza na kwamba wa kina mama ni waaminifu zaidi kwani Diwani aliyepita alikuwa mwanaume lakini alihukumiwa mahakamani kwa kosa la ubadhilifu wa mali za umma

Majambazi Watano Waliohusika Katika Mauaji Kibiti na Mkuranga Wauwawa na Polisi

$
0
0
Majambazi Watano Waliohusika Katika Mauaji  Kibiti na Mkuranga Wauwawa

mkoani Pwani, wameuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga

Majambazi hao waliokuwa wakituhumiwa kwa mauaji ya Kibiti wameuawa walipokuwa wakitaka kufanya jaribio la kuwapora wafanyabiashara wa dhahabu mjini Shinyanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amesema mauaji hayo yametokea baada ya jeshi hilo Kitengo cha Intelejensia kupata taarifa ya kuwa kuna majambazi ambao walikuwa wamejipanga kufanya uhalifu.
“Baada ya Polisi kupata taarifa hizo, askari walienda katika eneo hilo ambalo lilikuwa na vichaka pamoja na mapango ambayo yalisababishwa na uchimbaji holela wa mchanga”. Amesema Kamanda Haule
Kamanda Haule amefafanua zaidi kuwa  walipofika walianza kurushiana risasi kabla ya kuwazidi na kuwakamata majambazi hao wakiwa wamejeruhiwa vibaya,  na wakati wakipelekwa hospitali wote watano walipoteza maisha.
Ameongeza baada ya kuuawa na kupekuliwa, walikutwa na bunduki moja aina ya Short Machine Gun (SMG) yenye risasi 25 pamoja na mabomu mawili ya kurushwa kwa mkono.

Ikitokea Nimetimukliwa Simba Wala Sitoshtuka.- Omog

$
0
0
Ikitokea  Nimetimukliwa Simba  Wala Sitoshangaa- Omog
LICHA ya kuwepo kwa tetesi nyingi zikimhusisha Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, kutaka kutimuliwa kikosini hapo, mwenyewe ameibuka na kusema kuwa, ikitokea hivyo wala hatashtuka.

Hivi karibuni, kumekuwa na taarifa nyingi za chinichini zikimhusisha kocha huyo kutaka kutimuliwa kutokana na kile kilichoelezwa kushindwa kupanga kikosi cha ushindi kwenye baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara licha ya kuwa na wachezaji wengi mahiri.

Katika usajili wa dirisha kubwa uliofungwa Agosti 6, mwaka huu, Simba ilisajili wachezaji 14, hali ambayo inaifanya timu hiyo kuwa na nyota wengi wazuri akiwemo Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi. Licha ya kujaza nyota wengi kama hao, lakini Simba katika baadhi ya mechi imekuwa haipati matokeo ya kufurahisha jambo ambalo limetafsiriwa moja kwa moja kuwa Omog ameshindwa kukiongoza kikosi hicho.

Wakati tetesi hizo zikizidi kuenea, Simba ilimleta nchini kocha Masoud Djuma raia wa Burundi ili awe msaidizi wa Omog baada ya kuondoka kwa Mganda, Jackson Mayanja, lakini imeelezwa kuwa, pindi Omog akiondoka, Mrundi huyo atachukua mikoba hiyo kwani alipokuwa akiinoa Rayon Sports kabla ya kutua Simba, alikuwa kocha mkuu.

Akizungumzia mustakabali wake ndani ya Simba, Omog amesema: “Kwa sasa naona naifanya kazi yangu kwa ufasaha kwani ukiangalia msimamo tupo vizuri tu na wala si sehemu mbaya. “Makocha wengi wamekuwa wakitimuliwa kwenye timu zao, hivyo wala sihofi i ikitokea jambo hilo kwa sababu naamini hakuna nilichoshindwa kukifanya, kama ushindi tunapata.”

Trump: Japan Itayatungua Makombora ya Korea Kaskazini

$
0
0
Trump: Japan Itayatungua Makombora ya Korea Kaskazini
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Japan itatungua makombora ya Korea Kaskazini, kwa kutumia mitambo ya kijeshi iliyonunuliwa kutoka Marekani.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kwamba, taifa lake litatungua makombora hayo kabla ya kutua ardhini, "ikiwa hilo litahitajika".
Viongozi hao wawili, walisema hayo walipozungumza na waandishi habari wakati wa kumalizika rasmi kwa ziara ya kwanza ya kitaifa ya Bwana Trump nchini Japan.
Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili hatari juu ya mipaka ya Japan.

Trump aapa kukabiliana na Korea Kaskazini kwenye ziara yake ya Bara Asia.
Alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari leo Jumatatu, Bw Trump alisema kwamba, Bwana Abe atanunua "kiasi kikubwa cha zana za kivita" kutoka Marekani.
Akigusia zana hatari za kinuklea za Korea Kaskazini, Trump alisema kuwa Bw Abe "atazishambulia zikiwa bado angani" mara tu atakapokuwa amemaliza kununua silaha hizo za kijeshi, anazosema kuwa itatoa ajira ya kazi kwa Wamarekani na pia "kutoa usalama kwa Japan".
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images