Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Habari Mbaya...Jinamizi la Majeruhi Lamkumba Mchezaji Mbwana Samatta...Hata Cheza Mpira Miezi Sita

$
0
0
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Ally  Samatta atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita baada ya kupata majeraha wakati akiitumikia klabu yake.

Samatta aliumia Jumamosi wakati KRC Genk alipokuwa ikiikabili Lokeren katika mchezo wa ligi kuu ambao ulimalizika kwa timu zote kutoka suluhu.

Katika mchezo huo, Samatta alidumu uwanjani kwa muda wa dakika 40 kabla yakutolewa nje kwa kujeruhiwa mguu.

Samatta ambaye pia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hatakuwa katika kikosi cha Stars kitakachocheza dhidi ya Benin kwenye mchezo wa kirafiki utakaopigwa Novemba 12 mwaka huu nchini Benin.

Licha ya Samatta kuwa majeruhi, wachezaji wengine wa Stars pamoja na kocha Salum Mayanga wameahidi kupata ushindi kwenye mchezo huo kitu ambacho wanaamini kitakuwa faraja kwa nahodha wao.

Rais Magufuli Aipongeza TANROADS Kuokoa Bilioni 4.5 za Mradi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 07 Novemba, 2017 amefungua barabara ya lami ya Kyaka – Bugene Mkoani Kagera yenye urefu wa kilometa 59.1 iliyogharimu Shilingi Bilioni 81.597 fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo yenye urefu wa kilometa 183.1 ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda na Burundi.

Kabla ya kufungua barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli amesafiri kwa barabara hiyo kutoka Kyaka hadi Karagwe zilipofanyika sherehe za ufunguzi na amempongeza mkandarasi, kampuni ya CHICO ya China, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na timu ya wataalamu wa TANROADS kwa kuusimamia mradi huo wao wenyewe kwa gharama ya shilingi Milioni 519.2 badala ya kuajiri msimamizi ambaye angelipwa zaidi Shilingi Bilioni 4.5.

“Napenda kuwapongeza sana TANROADS kwa kusimamia mradi huu nyinyi wenyewe, zaidi ya Shilingi Bilioni 4 mlizookoa kwa kuwatumia wataalamu wetu kuusimamia mradi huu ni fedha nyingi sana, nataka kitengo hiki cha usimamizi wa miradi tukiimarishe, hivi sasa tunao wahandisi 15,000 wanaoweza kufanya kazi hizi, tuwatumie” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli pia amezungumza na waandishi wa habari waliokuwa wakirekodi na kurusha matangazo ya sherehe hizo ambapo amewashukuru kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao, na ipo tayari kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kuwezesha mafunzo ya kuwaongezea ujuzi.

Sherehe za ufunguzi wa barabara ya Kyaka – Bugene zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Prof. Norman Sigalla King, Wabunge wa Mkoa wa Kagera na viongozi wa Dini na Siasa.

Akiwa njiani kuelekea Karagwe Mhe. Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa Kyaka na kusikiliza kero zao ambapo amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Kagera kutowabughudhi wananchi wanaojihusisha na shughuli za kilimo, na badala yake wawasaidie kuondoa migogoro ya ardhi, kusajili mifugo yao na kuinua uzalishaji wa mazao ili Mkoa wa Kagera uwe na malighafi za kutosha kuanzisha viwanda.

“Pale Mtukula tumejenga kituo cha pamoja cha huduma mpakani (One Stop Border Post) kati yetu na Uganda, lengo letu ni kurahisisha biashara kati ya Tanzania na Uganda, kwa hiyo nataka kuona wananchi wa Kagera mnachangamkia fursa hii, anzisheni viwanda kama vya nyama na mazao mengine ya kilimo, fugeni mifugo kisasa ili mnufaike” amebainisha Mhe. Rais Magufuli.

Akiwa Bukoba Mjini kundi kubwa la wananchi wa mji huo limeusimamisha msafara wake ambapo baada ya kupokea kero mbalimbali, Mhe. Rais Magufuli ameahidi kutekeleza ahadi yake ya kutatua tatizo la uhaba wa maji katika mji huo na ametoa wito kwa viongozi wa Manispaa ya Bukoba kuwasilisha Serikalini andiko la kuomba kujengewa kituo cha mabasi kama wananchi walivyomuomba.

“Ndugu zangu mimi nipo pamoja na nyinyi, kero zenu nazijua na tutazishughulikia, ninachowaomba punguzeni kubishana, mnapoteza muda mwingi kubishana badala ya maendeleo, mnajichelewesha, Mji huu hautakiwi uwe hivi ulivyo” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli kesho tarehe 08 Novemba, 2017 ataendelea na ziara yake Mkoani Kagera ambapo atatembelea shamba la miwa na kiwanda cha sukari cha Kagera kilichopo Misenyi na kujionea uwekezaji mkubwa na wa kisasa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Bukoba

Siri ya Kikao Cha Myalandu na Lowassa..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Novemba 8

$
0
0

Siri ya Kikao Cha Myalandu na Lowassa..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Novemba 8

Polisi Wafanya Upekuzi Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Waondoka na Nyaraka, Vifaa vya Kielektoniki

$
0
0
Polisi Wafanya Upekuzi Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Waondoka na Nyaraka, Vifaa vya Kielektoniki
Jeshi la Polisi limefanya upekuzi Makao Makuu ya Chama cha ACT- Wazalendo na kuchukua nyaraka, vifaa vya kiilektonikia vilivyotumika kuandaa taarifa ya kusinyaa kwa uchumi wa nchi.

Upekuzi huo umefanyika leo mchana muda mfupi baada ya Zitto kwenda kuripoti Kitengo cha Uhalifu wa Makosa ya Kifedha Kamata jijini Dar es salaam na kutakiwa kurejea tena Novemba 21.
Taarifa iliyotolewa jioni hii na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema polisi walifika ofisini hapo saa 6 mchana na wameondoka mida ya saa 10 na wamechukua flash, laptop (kompyuta mpakato) na nyaraka ambazo ni taarifa kwa umma iliyotolewa kupitia wanahabari.
Ado amesema kwamba “Wamesema watakwenda kufanyia kazi vifaa hivyo na watavirejesha haraka ila hawajasema hasa ni lini," ameongeza
Mapema leo Jeshi hilo la polisi lilishikilia simu ya mkononi ya Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe kwa upelelezi huku yeye akisema mawasiliano aliyokuwa akiyafanya yamezingatia uhuru ulipo katika Katiba.


Nilimwacha Rose Muhando Kwakuwa Alikua Akiwatapeli Watu Sasa Amebadirika Ntamrudisha Hivi Karibuni- Msama

$
0
0
Nilimwacha Rose Muhando Kwakuwa Akiwatapeli Watu Sasa Amebadirika Ntamrudisha Hivi Karibuni- Msama
BAADA ya mwimbaji wa muziki wa Injili, Rose Muhando kupotea kwa muda mrefu kwenye ulimwengu huo, aliyekuwa meneja wake, Alex Msama amefunguka kumrudisha kwenye chati kama zamani kwani hivi sasa amebadilika.

Akizungumza na Za Motomoto News, Msama alisema alimuacha Rose kwa kuwa alikuwa akiwatapeli watumishi wa Mungu fedha alizokuwa akipewa kwa ajili ya shoo na kesi kibao kujaa polisi, lakini kwa asilimia kubwa hivi sasa ame-‘change’ hivyo atamrudisha soon.

“Rose alizidisha sana mambo yake ya utapeli ndiyo maana nikaacha kufanya naye kazi na tangu hapo amepotea kabisa kwenye ulimwengu wa Injili, ninamrudisha hivi karibuni tu, mashabiki wake wakae tu mkao wa kula maana ni mwimbaji mzuri sana anayejua kuimba,” alisema Msama.

Snura Afata Nyayo za AY, FA Aiburuza Kampuni Mahakamani

$
0
0
Snura Afata Nyayo za AY, FA Aiburuza Kampuni Mahakamani
WAKATI marapa marafiki Ambwene Yesaya ‘AY’ na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ wakiwa wamekaa mkao wa kula kusubiri mamilioni ya shilingi walizoshinda mahakamani kama fidia kwa kampuni moja kutumia wimbo wao bila idhini, Snura Mushi ambaye ni mkali wa Bongo Fleva, naye anatarajia kuiburuza mahakamani kampuni moja ya unga kwa kutumia wimbo wake wa Majanga kwenye matangazo yao bila makubaliano.

Akibonga na Za Motomoto News, Snura alisema tayari mwanasheria wake amewapelekea ‘notice’ ya siku saba akiwataka kumlipa fidia ya shilingi bilioni 2.1 kwa kutumia wimbo wake bila idhini yake hivyo kama hawatajibu chochote kesi hiyo itapelekwa mahakamani.

“Kiukweli nimesumbuka kwa muda mrefu sana tangu mwaka 2015, nimewahi kuwatafuta wanasheria watatu ikashindikana, nikaenda COSOTA nako hakuna kilichoeleweka lakini kwa sasa nimepata mwanasheria mwingine ambaye naamini atafanikisha na nitapata haki yangu maana ushahidi na kila kitu kipo,” alisema Snura.

Vanessa Mdee Ampa Jux Masharti Haya Ili Warudiane

$
0
0
Vanessa Mdee Ampa Jux Mashariti Haya Ili Warudiane
Good news ni kuwa Jux anaweza kupokelewa tena moyoni mwa Vanessa Mdee, bad news ni kuwa masharti ni magumu. Wawili hao walipokea shangwe za kutosha wikiendi kwenye show ya Fiesta mjini Morogoro baada ya Jux kutumia zaidi ya dakika 3 kumuimbia Vanessa wimbo ili warudiane.

Baada ya Jux kuimba kwa hisia hadi kupiga magoti, Vee ambaye alioneshwa kutoridhika, alimueleza masharti yake. “Huyu brother msimu wote wa Fiesta amekuwa akiniimbia sijui anauawa, sijui analia sielewi mimi,” alisema Vanessa huku uwanja ukilipuka kwa shangwe.

“Sasa sikilizeni,” aliendelea. “Nyie wote hapa ni mashahidi. Bado siamini kama anataka kurudiana na mimi. Nampa dakika 15 tu tukikutana Fiesta Dar es Salaam nyie ni mashahidi, akiweza fresh kama vipi aendelee kuuawa au sio?”

Jux alisema atazifanyia kazi dakika 15 hizo ili ampate tena mrembo huyo aliyeachana naye miezi michache iliyopita.


Kitendo cha Ray C Kunishambulia Mtandaoni Kilimdhalilisha Sana -Nandy

$
0
0
 Kitendo cha Ray C Kumshambulia Mtandaoni Kilimdhalilisha Sana -Nandy
Nandy amesema kitendo cha Ray C kumshambulia mtandaoni kwa kuimba wimbo wake, kilimdhalilisha. Amesema Ray C ni muimbaji aliyekuwa akimuangalia tangu akiwa mdogo na hivyo kumshambulia mtandaoni ni kitu kilichomuumiza.

Wiki kadhaa zilizopita, Ray C alimshambulia Nandy kwa kuimba wimbo alioshirikishwa na Mez B, Kama Vipi kwenye Fiesta. Ameiambia Dizzim Online kuwa ukaribu wa Ray C na THT ambao wanamsimamia Nandy pia ulimfanya ashangazwe na mrejesho wa msanii huyo mkongwe.

Amedai kuwa licha ya kuandika kwenye Instagram kumwelesha Ray C kwanini aliimba wimbo wake na kumweleza anavyomheshimu, alimtumia ujumbe binafsi wa simu lakini hakujibiwa. “Sio kitu kizuri ni kama amenidhalilisha bila kosa,” amesema Nandy.

Donald Trump Amuonya Kim Jong-Un Moja kwa Moja

$
0
0
Donald Trump Amuonya Kim Jong-Un Moja kwa Moja
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.
''Usitudharau, Usitujaribu," alisema, huku akishutumu hali ilivyo nchini Korea Kaskazini.
Bwana Trump alimzungumzia moja kwa moja rais Kim akisema kuwa ''silaha unazojilimbikia hazikufanyi wewe kuwa salama lakini zinakuweka katika hali hatari''.
Kiongozi huyo wa Marekani yuko katika ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya bara Asia.
Kwengineko katika hotuba yake amesema kuwa huku Korea Kaskazini ikiona uvumilivu kuwa udhaifu sasa kuna utawala mpya nchini Marekani

Bwana Trump pia ameutaka ulimwengu hususan China na Urusi kuiwekea shinikizo kali Pyongyang kusitisha utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia.
Dunia haiwezi kuvumilia hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao unaitishia na silaha za kinyuklia.
Mataifa yote yaliowajibika yanafaa kuungana kuangamiza utawala wa kikatili wa Korea Kaskazini kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeuunga mkono, kupata usaidizi wowote ama hata kukubalika, alisema.

Jibu la Manara kwa Yanga “Simba Ishavuka Kwenye Makaratasi Dunia ya Sasa Ipo Kiganjani"

$
0
0
Jibu la Manara kwa Yanga “Simba Ishavuka Kwenye Makaratasi Dunia ya Sasa Ipo Kiganjani"
Club ya Dar es Salaam Young Africans hivi karibuni ilifanikiwa kupiga hatua na kuingia katika utaratibu mpya wa kuanza kutoa magazine ya club itakayokuwa inatolewa mara nne kwa mwaka.

Yanga wametangaza kuwa watakuwa wanatoa magazine inayohusiana na mambo mbalimbali kuhusu club yao, historia za wachezaji wao na mambo mbalimbali ya club hiyo.

Yanga magazine itakuwa inatolewa mara nne kwa mwaka yaani kila baada ya miezi mitatu, baada ya habari hizo kutoka na magazine hiyo kuanza kusambaa mtaani, mashabiki wanaoaminika kuwa wa Yanga walianza kucomment na kumwambia afisa habari wa Simba Haji Manara afanye utaratibu kama huo kwani Yanga ni mfano wa kuigwa.

Baada ya Haji Manara kuona comment hiyo akajibu hivi “Simba ishavuka huko kwenye makaratasi dunia ya sasa ipo kiganjani sisi tunatoa magazine kila mwezi kwenye app ya club”

“Kijarida cha kufungia maandazi? Nenda kwenye app yetu kaone monthly magazine zetu halafu ndio uniletee hicho kijarida chenu”

Takukuru Yajitosa Uchunguzi Bodi ya Mikopo

$
0
0
Takukuru Yajitosa Uchunguzi Bodi ya Mikopo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inafanya uchunguzi dhidi ya vigogo na maofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wanaotuhumiwa kutafuna mabilioni ya shilingi kutokana na mbinu mbalimbali ikiwamo ya kujilipa posho ya ukarimu, imefahamika.

Agosti 31, mwaka jana, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikipitia taarifa za fedha za bodi hiyo kwa mwaka 2014/15, ilibainika imetumia Sh. bilioni 15 kwa shughuli za uendeshaji huku kiasi kikubwa kikiwa posho.

Kutokana na 'madudu' hayo, kamati hiyo iliitaka bodi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuhakikisha ulipaji wa posho
unazingatia sheria na miongozo ya serikali.

Kabla ya kupitiwa kwa taarifa za fedha za bodi hiyo na PAC Februari 16, mwaka jana, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.
Joyce Ndalichako, alitangaza kusitisha mkataba wa ajira wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, George Nyatega, pamoja na kuwasimamisha kazi wakurugenzi watatu kutokana na kile alichokieleza siku hiyo kuwa matatizo ya kiutendaji na matumizi mabaya ya fedha za umma yanayofanyika ndani ya bodi hiyo.

Prof. Ndalichako alisema taasisi hiyo imeonyesha utendaji usioridhisha kiasi kwamba kumekuwa na matatizo mengi na yanayojirudiarudia kwa wateja wao.

“Mikopo kwa wanafunzi imekuwa ikichelewa kuwafikia bila sababu za msingi kiasi kwamba imejengeka taswira kwa wanafunzi kwamba hadi walalamike wizarani ndipo matatizo yao yashughulikiwe, hivyo tatizo si ukosefu wa fedha bali ni uzembe wa watendaji katika kuwapatia wanafunzi mikopo yao kwa wakati," Prof. Ndalichako alisema.

Watumishi wa bodi hiyo waliosimamishwa kazi siku hiyo ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusuph Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo, Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo, Onesmo Laizer.

Prof. Ndalichako alizitaja baadhi ya sababu za kufukuzwa na kusimamishwa kazi kwa watumishi hao kuwa ni kufanya malipo yasiyo sahihi kwa baadhi ya wanafunzi wanaosoma ndani na nje ya nchi pamoja na udhaifu uliobainika katika mifuko ya fedha.

Wakati Prof. Ndalichako akichukua hatua hiyo, Takukuru nayo imekiri inaichunguza taasisi hiyo yenye jukumu la kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Nipashe ilimtafuta jijini Dar es Salaam Ofisa Uhusiano na Habari wa Takukuru Makao Makuu, Mussa Misalaba, ambaye alikiri kuwa wanaichunguza taasisi hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali za rushwa na ufisadi zinazowakabili vigogo na maofisa wake.

"Si hilo tu (la posho za mabilioni ya shilingi), tuna mambo mengi ambayo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu tunaichunguza. Wana tuhuma nyingi ambazo tunazifanyia kazi ili wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa," alisema Misalaba.

Hata hivyo, Misalaba hakuwa tayari kuziweka wazi tuhuma zingine ambazo vigogo na maofisa wa HESLB wanachunguzwa nazo.

Lakini habari za uhakika ambazo Nipashe inazo, Takukuru inachunguza pia HESLB kwa malipo ya mikopo kwa wanafunzi hewa na ulipaji wa mikopo mpaka minne kwa mwanafunzi mmoja.

Nipo Mbioni Kupata Mtoto Nataka 2018 Niitwe Mama- Gigy Money

$
0
0
Nipo Mbioni Kupata Mtoto Nataka 2018 Niitwe Mama- Gigy Money
Msanii wa muziki ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nampa Papa’, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, amedai kuwa yupo mbioni kupata mtoto, baada ya mastaa mbalimbali kufanikiwa kupata watoto hivi karibuni.

Msanii huyo anayefanya vyema na kibao chake hicho, amesema amefikia wakati wa kuitwa mama na Mungu akipenda mwakani anatamani hilo litimie.

“Kuitwa mama ni baraka na hakuna mwanamke ambaye hatamani hilo, kikubwa ni mipango tu kwa kuwa huwezi kukurupuka, halafu kingine mtoto ni mipango ya Mungu, unaweza kupanga hivi ikawa vile, sasa naona na mimi ni wakati wangu wa kutimiza hilo,” Gigy aliliambia Gazeti la Mtanzania.

Alisema pamoja na malezi kuwa na changamoto zake lakini ni jambo ambalo lazima alipitie na amejipanga vyema kutimiza azma yake hiyo aliyojiwekea na mpenzi wake.

Gigy alisema anatarajia kupata mtoto na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye wote kwa pamoja wameridhia jambo hilo.

Hamisa Mobetto Anyakua Tuzo ya ‘People Choice Awards’.

$
0
0
Hamisa Mobetto Anyakua Tuzo ya ‘People Choice Awards’.
Mwanamitindo kutoka Tanzania,  Hamisa Mobetto amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya Starqt Awards katika msimu wake wa nne kupitia kipengele  cha ‘People Choice Awards’.

Mrembo huyo aliyekuwa ana wakilisha Tanzania na Afrika Mashariki alikuwa akiwania vingengere viwili ambavyo ni ‘People Choice Awards’ na ‘Super Mum’ ila amefanikiwa kuibuka kidedea katika kipengele kimoja tu.

Starqt Awards ni tuzo zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine. Na zoezi la ugawaji tuzo hizo lilifanyika Novemba 4 mwaka huu katika ukumbi wa Bedford View City Hall, mjini Johannesburg nchini South Afrika.


Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..


JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.

Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

Kama hii ni Kweli basi Wanaume wengi Tunachekwa sana Vitandani

$
0
0
Inasemekana kwamba ukiwa unafanya mapenzi / unabaiolojiana na Mwanamke yoyote yule halafu pale unapomaliza mshindo wako / unapiga bao lako la Kichuya au Ajib halafu ukaona Yule Mwanamke hakukumbatii kwa kukubana kwa nguvu kabisa hadi hata unashindwa kupumua vizuri na kutikisa kabisa mwili wako na Fito zako ( miguu ) basi jua ya kwamba hapo 100% hujamfikisha / hujamtosheleza Kimahaba na ulichokifanya Kisayansi wanasema work done zero.Ila ikitokea kinyume chake basi jua kwamba Mwanamume umeshughulika na Mwanamke kafika katika Kilele chake cha Utamu na Raha ya Mkuyenge wako.

Je kuna Wanabaiolojia wenzangu hasa Wanaume wenzangu je hapa kuna ukweli wowtote labda? Hii habari / taarifa nimeipokea kwa mshtuko mkubwa mno hadi nimeshakosa raha kwani kusema kweli Mimi binafsi nakumbuka kabisa mwaka wa mwisho Kukumbatiwa hivyo kama ilivyobainishwa hapo juu nadhani ilikuwa ni mwaka 2000.

Sasa nawaza tu mwenyewe ( Am just thinking aloud ) kwamba kumbe inawezekana kabisa GENTAMYCINE tokea mwaka 2001 hadi sasa 2017 Wanawake / Mademu wote niwaowabandua / ninaobaiolojiana nao nafanya tu hiyo work done zero? Kwani sijawahi Kukumbatiwa hivyo kama hao Wataalam wa Mapenzi / Mahaba wanavyosema hapo juu.

Na sijui kwanini na Mimi niliamua kumuhoji hili swali huyu Mtaalam kwani hayo majibu yake sasa yamekuwa ni maumivu na mateso makubwa sana moyoni mwangu ila moyo wangu utatulia pale labda na Wataalam wengine wa JamiiForums watakapoliweka hili sawa. Yaani nawaza kwahiyo kumbe kujipinda Kwangu kote tokea 2001 hadi sasa 2017 nafanya Kazi bure tu / work done zero mbele ya Mbunye?

Nawasilisha.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Breaking News: Mlipuko wa Bomu Watokea Ngara na Kuua Wanafunzi watatu na Kujeruhi Kadhaa

$
0
0
Takribani wanafunzi 3 wameripotiwa kufariki dunia mpaka sasa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu wilayani Ngara.

Diwani wa Kata ya Kibogora wilayani humo, Ndg Adronizi Burindoli ameeleza kuwa jitihada za kuokoa uhai wa majeruhi zinaendelea..

Taarifa zaidi zitafuata.

Kocha Afunguka Kuhusu Atakayeziba Nafasi ya Mbwana Samatta

$
0
0
Kocha Afunguka Kuhusu Atakayeziba Nafasi ya Mbwana Samatta
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga ameweka wazi kuwa nafasi ya nahodha wa kikosi hicho Mbwana Samatta itazibwa na wachezaji ambao amewaita ndani ya kikosi hicho.
Samatta ambaye anakipiga kwenye ligi ya Ubeligji katika klabu ya KRC Genk ameumia misuli ya paja hivyo kulazimika kukaa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita kwaajili ya matibabu.Hiyo inamaanisha Samatta ataukosa mchezo wa Novemba 12 dhidi ya Benin.
Kocha Mayanga amekiri kuwa ni pengo kumkosa nahodha huyo lakini kama timu hawana budi kukubali na kutafuta namna ya kuziba nafasi yake kupitia wachezaji 24 ambao amewaita kwenye kikosi hicho.
“Ni kweli tumepata pengo kumkosa Samatta ambaye ni nahodha lakini hatuna namna lazima tukubaliane na hali halisi, lakini tunaowachezaji wanaoweza kuziba nafasi hiyo wakiwemo vijana tuliowaita kutoka timu za vijana”, amesema Mayanga.
Taifa Stars itasafiri kuelekea Benin ambako itacheza mchezo wa kalenda ya shirikisho la soka la kimataifa FIFA, Novemba 12.

Lavalava Asimulia Yaliyomkuta Baada ya Kugundulika Nyumba Aliyokuwa Anakaa Mwanamke Alipangiwa na Mpenzi Wake

$
0
0
Lavalava Afunguka Kukaa Kwenye Nyumba ya Mwanamke Aliyopangiwa na Mpenzi Wake
Msanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Lavalava amefunguka ishu ya kuishi katika nyumba ya mwanamke ambaye alimchukulia kama mpenzi wake wakati haikuwa hivyo

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Tuachane’ amesema baada ya kuisha pamoja alikuja kugundua nyumba wanayoishi na mwanamke huyo kapangiwa na mpenzi wake.

“Mwezi mmoja kabla sijaachia Tuachane nilikuwa na mpenzi wangu ambaye tulikuwa tumepanga mipango mingi sana kwamba kuna siku nitafika, nitakuwa hivi na kufanikiwa na kuweza kukuhudumia akawa ananiitikia, fresh kumbe hata pale alipokuwa anakaa kulikuwa kuna mwana kampangia” amesema.

“Mimi nakaa humo humo najiachia, mchizi akarudi hiyo siku nilikuwa kama nihisi kufa kufa hivi, akaniambia bwana nimerudi hapa kwangu” Lalava ameiambia Radio Free Africa.

Ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya hilo kutokea waliongea na kujitetea kwa kutoa maelezo ambayo yatakuwa sawa kwa pande zote na kilichofuata ni kwenda kutoa ngoma ‘Tuachane’.

Zari Aliamsha Dude "Ukizalishwa Songa Mbele na Maisha Yako,Tupe Nafasi Bibi! Usitubane Bane"

$
0
0
Zari Aliamsha Dude "Ukizalishwa Songa Mbele na Maisha Yako Tupe Nafasi Bibi Usitubane Bane"
Kimenuka tena! Ndivyo unavyoweza kusema, siku chache baada kushambuliana kwa maneno kisha ukimya kupita, mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameibuka upya na kumshambulia vilivyo mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Zari aliliamsha dude upya Jumapili iliyopita ambapo alifanya hivyo baada ya kuchokozwa na baadhi ya mashabiki ambao wanaaminika ni wa upande wa Mobeto.
Zari akiwa na mrembo mwenzake aliyeaminika kuwa ni shosti yake, ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alianza kurusha madongo kupitia Instagram katika kipengele cha kurusha matukio moja kwa moja (live).

“Kama yeye ni mwanamke kweli kwa nini ahangaike kulea mtoto? Mimi mwenzake mtu akinizingua nalea mtoto mwenyewe. Ukizalishwa, songa mbele na maisha yako. Tupe nafasi bibi, tupe nafasi. Tiffah anahitaji nafasi, usitubane bane,” alisikika Zari.

Katika video hiyo, Zari alisikika akitema maneno mengi ya kebehi huku shosti yake aliyekuwa amekaa pamoja naye akishadadia kwa maneno ya kumpampu Zari.
Baada ya kuupata ubuyu huo ukiwa wa motomoto, Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Hamisa bila mafanikio kufuatia simu yake kutopatikana hewani.

Hata hivyo, alipatikana mama mzazi wa Mobeto, ambaye alisema wao kama familia hawasikilizi habari za mitandaoni kwa sasa.

“Yeye awe amesema huko mtandaoni sisi hatujali hayo mambo kwa sasa na wala hayatuhusu, tunaangalia maisha yetu,” alisema mama Mobeto.
Hii ni mara ya pili kwa wawili hawa kutifuana mitandaoni tangu ilipobainika Mobeto kuzaa na mwanaume ambaye pia amezaa na Zari.

Awali, Zari aliposikia mzazi mwenziye amekiri kuzaa na Mobeto, alikinukisha kwa mrembo huyo kisha akakinukisha pia kwa mzazi mwenziye, wakamwagana kwa muda ambapo mrembo huyo wa Kiganda, alisema amemuachia mume Mobeto.
Baadaye Zari na mzazi mwenziye waliweka tofauti zao pembeni, wakaelewana kisha kikapita kimya cha muda mfupi kabla hajaliamsha dude upya juzikati.
chanzo: Global Publisha
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images