Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Bendi ya Msondo Ngoma Waijia Juu WCB Yataka Ilipwe Milioni 300 Kisa ‘Zilipendwa’

0
0
Bendi ya Msondo Ngoma Waijia Juu WCB Yataka Ilipwe Milioni 300 Kisa ‘Zilipendwa’
Hii ni habari mbaya kwa kambi ya WCB inayoongozwa na Diamond kama ni ya kweli, kwani wanasheria wa Bendi ya Msondo Ngoma ametaka mteja wao kulipwa tsh milioni 300 na WCB kwa madai wametumia kionjo cha melody ya saxaphone cha wimbo wa bendi hiyo bila hurusa katika wimbo wa WCB, ‘Zilipendwa’.

Alhamisi hii zilianza kusambaa barua mtandaoni zikidaiwa kutoka kampuni ya sheria ya bendi hiyo, Maxim Advocate huku barua hiyo ikionekana kupitia Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) pamoja na COSOTA.

Bado WCB hawajazungumza chochote kuhusu tukio hili. Angalia barua hizo hapa chini


Magufuli na Museveni Waweka Historia kwa Kuweka Jiwe la Msingi Bomba la Mafuta Uganda

0
0
Magufuli na Museveni Waweka Historia kwa Kuweka Jiwe la Msingi la Bomba la Mafuta Uganda
MARAIS John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda waliweka historia jana baada ya kuzindua kituo cha pamoja cha forodha kitakachochochea ukuaji wa biashara kwa nchi zote mbili.

Kituo hicho cha aina yake, kipo katika mpaka wa Tanzania na Uganda, eneo la Mtukula.

Magufuli (maarufu JPM), ambaye yuko nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, alisema wakati wa ufunguzi wa kituo hicho na mwenyeji wake, Museveni,  kuwa wafanyabiashara waliokuwa wakitumia muda mrefu kutoa mizigo katika eneo hilo sasa wataondokana na adha hiyo.

Alisema kumekuwa na ukwamishaji wa maendeleo baina ya viongozi na wafanyabiashara wanaopeleka na kuingiza bidhaa ndani ya nchi hizo kwa kufanya ukaguzi wa muda mrefu  unaomfanya mtu kutumia zaidi ya dakika 20.

Rais Magufuli alisema  kituo cha Mtukula  kilikuwapo tangu mwaka 2011 na kuanza kufanya kazi mwaka 2015, huku kikitoa huduma kwa muda mrefu ili kukamilisha utaratibu.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, kituo hicho kimegharimu Sh. bilioni 7.16 hadi kukamilika kupitia fedha iliyotolewa na Trademark East Afrika kupitia ufadhili wa Canada na Uingereza.

Naye Rais Museveni alisema katika  kupanua sekta ya uchumi na maendeleo, shughuli za kilimo, ufugaji, viwanda ni nguzo katika kutoa ajira kwa wananchi wa Uganda na Tanzania.

Katika ziara hiyo ambayo Rais Magufuli ameongozana na mke wake, Mama Janeth Magufuli, yeye pamoja na Museveni walifungua walifungua  kituo cha pamoja cha huduma za mpakani (One Stop Border Post - OSBP) kilichojengwa kwa lengo la kurahisisha taratibu za kiforodha, uhamiaji na kuharakisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Sambamba na kufungua kituo hicho, marais hao jana waliweka jiwe la msingi katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la kuanzia Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Sherehe hizo zilifanyika katika kijiji cha Luzinga, kilichoko katika mkoa wa Rakai nchini Uganda.

Yanga Yalalamika Kusimama kwa Ligi Bara

0
0
Yanga Yalalamika Kusimama kwa Ligi Bara
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema haifurahishwi na kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusimamisha mechi za Ligi Kuu Bara ili kupisha michuano ya Kombe la Chalenji na kuongeza kuwa uamuzi huo "unaua" morali ya timu na kuwapa hasara.

Bodi ya Ligi Kuu imetangaza kuwa Ligi Kuu itasimama baada ya michezo ya raundi ya 10 ili kutoa nafasi kwa timu ya Tanzania Bara
"'Kilimanjaro Stars" kupata nafasi ya kujiandaa na kushiriki michuano ya Chalenji ambayo itaanza kufanyika kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 9 mwaka huu jijini Nairobi, Kenya.

Akizungumza baada ya mazoezi ya jana asubuhi ambayo alihudhuria, Katibu Mkuu huyo wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema kusimama kwa ligi huyo kutawaathiri na kutapunguza morali ya wachezaji wake ambao tayari imeimarika.

"Kuna haja ya kuliangalia upya jambo hili, TFF inapopanga ratiba ya ligi iangalie na matukio kama haya, inapaswa timu kujua mapema ratiba hii, kusimama kwa ligi si vizuri, hata ligi yenyewe inakosa msisimko," alisema Mkwasa.

Kocha huyo wa zamani wa Yanga, Ruvu Shooting na Twiga Stars, alisema kuwa ana uhakika kusimama kwa ligi hiyo kutaziathiri pia timu nyingine na si Yanga peke yake.

Alisema itawalazimu kuwapa mapumziko wachezaji wao ambao hawatakuwa kwenye vikosi vya timu za taifa kama Kilimanjaro
Stars (Bara) au Zanzibar Heroes mpaka pale mashindano hayo ya Kombe la Chalenji yatakapomalizika.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, aliiambia Nipashe jana kuwa wamelazimika kuisimamisha ligi baada ya TFF kuthibitisha kuwa mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kushirikisha nchi 12.

“Wakati tunapanga ratiba ya ligi kuu, Cecafa walikuwa hawana uhakika wa kufanyika kwa mashindano haya, ndio maana hatukuweka kwenye kalenda yetu, kwa bahati mbaya au nzuri mwaka huu yanafanyika kwa hiyo ilikuwa lazima tufanye hivi,” alisema Wambura.

Wakati huo huo, Mkwasa, alisema kuwa hana habari ya kutokuwapo nchini kwa mshambuliaji, Donald Ngoma, ambaye amekwenda kwao Zimbambwe kwa ajili ya kupata matibabu.

“Mimi sifahamu, Ngoma alikuja ofisini kwangu kuomba ruhusa ya kwenda kwao kupata matibabu ya majeraha yake, lakini nilimwambia anatakiwa kwanza azungumze na kocha na meneja wa timu kabla ya kuja kwangu, lakini nimesikia kaondoka,” alieleza Mkwasa.

Lui Adata na Papa wa Gigy Money

0
0
Lui Adata na Papa wa Gigy Money
Baada ya kufanya vizuri katika cover ya ngoma ya Patoranking na Diamond ‘Love You Die’, Msanii Lui ametaja ngoma nyingine ya Bongo Flava ambayo angetamani kufanya cover yake.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘1 on 1’ ameitaja ngoma ya Gigy Money ‘Papa’ kama ngoma ambayo ingeweza kufanya hivyo endapo muda ungeruhusu.

“Ni wimbo wa Gigy Money, ni wimbo ambao kila sehemu ninapoenda naukuta, ukienda club watu wanarudika, ukianza tu haulizi unaruka, kajitaidi sana ingawa sasa hivi muda wake umepita kidogo lakini hadi sasa hivi ni ya moto lakini siwezi kuifanyia tena cover” Lui ameiambia Bongo5.

Kutana na Mtaalam na Bingwa wa Magonjwa Sugu Kama Pumu, Vidonda vya Tumbo, Kisukari na Mengine Mengi

0
0
MTALAAM NA BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU NAYALIYOSHINDIKANA KAMA VILE PUMU, VIDONDA VYA TUMBO, BUSHA, NGUVU ZA KIUME, KISUKARI,MIVUTO YOTE, KUSAFISHA NYOTA, KURUDISHA MALI, NK.

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni SUPER SAYI 3,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

SUPER SAYI 4 Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR ULIMWENGU ANAPATIKA DAR ES SALAAM MAGOMENI MOROCO

HUDUMA HIZI UTAZIPATA MAGOMENI

SIMU NO 0745387469, 0652121197

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.

Uchumi wa Tanzania: Hussen Bashe Afafanua Mwenendo wa Uchumi Nchini....Ukweli Mchungu

0
0
Nimemsikiliza kwa makini sana Hussein Bashe kwa uchambuzi mzuri alioufanya kuhusu trend ya uchumi hapa nchini, inasikitisha sana tena sana. sasa nikajiuliza Hivi ingekuwaje maneno haya angeongea Zitto Kabwe?

VIDEO:

Mbunge Sugu Kweli Sugu Awachana Wabunge wenzake Kisawasawa...Alaani Airport Kujengwa Chato Badala ya Butiama

0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amekosoa mpango wa kujengwa kwa Uwanja wa Ndege wilayani Chato mkoani Geita na kusema kwamba hauna faida yoyote kwa Taifa kwani Rais Magufuli akishatoka madarakani hakuna ndege itakayokuwa inakwenda huko.

Akizungumza leo bungeni wakati wa kujadili mipango ya maendeleo ya taifa, Mh. Mbilinyi amesema kwamba suala la kwamba wakikosoa kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato ni kuchukulia kama suala binafsi bali ni suala la Mipango.

"Mipango bila utaratibu haiwezi kuwa mipango, Mh. Mwenyekiti. Namna ambavyo Airport ya Chato ilivyokuja haikuwa na mipango. Mipango kama hii inanikumbusha Rais Mobutu ambaye alijenga Ikulu kijijini kwao kipindi cha utawala wake na sasa hivi Ikulu hiyo imegeuka nyumba ya popo" Mbilinyi.

Mh. Mbilinyi ameongeza.  Tukianza kuongea hivi kuna watuu wanawaka lakini mkumbuke hii siyo 'personal' bali nazungumzia 'Principal'. Mnashindwa kwenda Butiama kwa Baba wa Taifa mtaenda Chato?

Pamoja na hayo Mh. Mbilinyi ameitaka serikali itumie mbinu ya waliyoitumia kwenye kukuza biashara ya Korosho itumie mbu hizo pia kwenye kukuza bei ya mazao mengine nchini kama mbaazi, Tumbaku na mazao mengineyo.

Hata hivyo Mbilinyi amewaasa mawaziri kutoshindana kutoa matamko ambayo wanajua hayawezi kutekelezeka bali watumie nafasi zao katika kumshauri Rais ili kusonga mbele kutekeleza mipango.

Badili Mwonekano wake na Kuweka Mwili Safi Kwa Kutumia Kessy Products

0
0
PENDEZA NA KESSY PTODUCT: BADILI MUONEKANO WAKO NA KUWEKA MWILI WAKO SAW KWA PRODUCT ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI, MATOKEO NI KWAARAKA* 🍇🌾🌳
1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _100,000/
2) KUREFUSH NYWELE NA KUZUIAKUKATIKA 90,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO KUWA NA UMBO ZURI (HIPS & BATAKS)KUNADAWA AINA TATU (@)JELI KUPAK_100,000/(B) KUNYWA (C)VIDONGE_130,000/
4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, KIUNONI NA MAPAJAN_80,000/
5)TOA KITAMBI KABISA(@) KUPAK 10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING MAJAN 130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE NA MANYAM YOTE
@) DAW YA MAJINI_100,000/NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME BILA KUVAA SIDIRIA_80,000/
8)KUONGEZA MAZIWA NA SAIZI NZURI_80,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA (kifaru)_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO YAKAWAIDA NA UZAZ_80,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_70,000/
13) KUWA MWEUPE WAKUPENDEZA KWA DAW(@) VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU VINYWELEO MWLINI _80,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA JELI PAMOJA NA VIDONGE VYAAIN ZOT _100'000
16) ENGEZA MAUMBIL YA KIUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_ 120,000 /
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUFIKA KILELE_80,000/
18) RUDISH(BIKRA) 100,000/
19)ONDOA MAFUTA USONI _80,000/
20)ONDOA MIKUNJO USON_70,000/(21) ENGEZA MGUU_80,000/🍍🍉🌾 *TUNAPATIKAN DAR E SALAAM* *NAKWA *MIKOANKOTE* UTAPATA *PIA* *NA NCHI ZOTE PIGA CM* (+255)0719955528
0756259180
0785371237
@dr_kessy_product*
*Delivery POPOTE ULIPO,*

"Watanzania Watakuwa Vibarua tu" - Zitto

0
0
"Watanzania Watakuwa Vibarua tu" - Zitto
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka na kudai kwamba utekelezaji wa miradi kupitia serikali ya awamu ya tano inaharibu uchumi wa nchi bila kujali maslahi ya Taifa na wananchi wake.
Zitto ametoa hayo ya moyoni kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kwamba Mkataba ambao serikali ya awamu ya tano imeingia na Uturuki katika ujenzi wa reli haujawazingatia Watanzania wenye viwanda vya chuma ambacho ni kitu kinachohitajika katika mradi huo wamenyimwa na badala yake wamekabidhiwa kampuni ya Uturuki.
Mh. Zitto ameongeza kwamba Mkataba ambao serikali umeingia na Waturuki hao hauwalazimishi kutumia malighafi za nyumbani ingawa wameingia mkataba wa sh. Triliomi 7.
"Kwa masikitiko makubwa nawaambia Watanzania kuwa Mkataba wa Ujenzi wa Reli waliyopewa kampuni ya Uturuki haukuzingatia maslahi ya Taifa.... . Watanzania wenye viwanda vya kuzalisha Chuma kitu  kinachotakiwa kwenye sehemu ya mradi wamenyimwa kazi hiyo na badala yake kampuni za Uturuki ndio wamepewa kazi hizo. Hata kokoto wamepewa kampuni ya Uturuki. Watanzania watakuwa vibarua tu" . Zitto.
Ameongeza kwamba "Naisihi Serikali itazame hii miradi mikubwa na kuifungamanisha na mkakati wetu wa Viwanda ili kufikia malengo yetu na azma yetu ya kuondoa umasikini nchini kwetu. Hii Serikali ya Awamu ya Tano inaharibu uchumi wetu. Inatekeleza miradi bila kujali maslahi ya nchi yetu. haina maarifa ya kuendesha uchumi,"
Mbali na hayo Mh. Zitto amefafanua kwamba kama nchi ingekuwa na mipango thabiti basi Tanzania ingekuwa wazalishaji wakubwa wa Chuma na na hata uzalishaji wa chuma cha kujengea reli kwenye eneo la Mashariki mwa Afrika na Maziwa Makuu.
"Nchi yetu ina chuma kingi sana kule Mchuchuma na Liganga, na pia tuna makaa ya mawe ya kuchenjua chuma hiki ili kupata chuma cha pua (steel). Mradi huu wa reli peke yake ungeweza kuchochea maendeleo makubwa kwenye sekta ndogo ya migodi na viwanda vya Chuma. Iwapo tungekuwa na mipango thabiti, ".

ICC Yatoa Idhini kwa Mahakama Kuanza Kufanya Uchunguzi

0
0
Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, wametoa idhini kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Fatou Bensouda, kuanza uchunguzi wa tuhuma za uhalifu wa kivita nchini Burundi.

Majaji hao walitoa idhini hiyo Oktoba 25 mwaka huu, ikiwa ni siku mbili kabla ya Burundi kutangaza kujitoa katika Mahakama hiyo Oktoba 27.
Katika uamuzi wao Majaji wamebaini kwamba, kuna sababuz a msingi za kufanyika kwa uchunguzi huo kuhusiana na uhalifu dhidi ya binadamu.
Takriban watu 1,200 wameuwawa katika machafuko nchini Burundi tangu mwaka 2015, ambao taarifa za idhini hiyo zilichelewa kutolewa ili kutoa muda wa kuweka mazingira ya kuwalinda waathirika na mashahidi.

Bwana Harusi Apigwa Risasi Sehemu za Siri Katika Sherehe ya Harusi Yake

0
0
Bwana Harusi Apigwa Risasi Sehemu za Siri Katika Sherehe ya Harusi Yake
Bwana harusi nchini Misri amejeruhuwa vibaya kwa kupigwa risasi katikati ya sherehe ya harusi yake.
Bwana harusi huyo aliyetambulika kwa jina la Osman al-Alsaied alipata majeraha mabaya katika sehemu yake ya siri, Kiunoni na Mkononi katikati ya sherehe ya harusi yake ambapo mtu huyo aliyempiga alikuwa anafyatua risasi kama kitendo cha kusherehekea harusi hiyo .

Osman al-Alsaied (28) alikuwa akisherehekea harusi yake ndipo mwanaume mmoja alikosea kufyatua risasi badala ya kuelekeza juu silaha hiyo yeye alielekeza chini na kumjeruhi bwana harusi.

Maafisa wa polisi mjini Cairo wamethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa bunduki hiyo ilifyatuliwa mwananume mwenye umri wa miaka 26 .

Hata hivyo, Polisi  wamesema kuwa mtuhumiwa huyo aliyefyatua risasi alikamatwa na kuhojiwa muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea.

Tukio hilo limeibua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii nchini Misri wengi wakitaka tamaduni hiyo ifutiliwe mbali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa BBC zimeeleza kuwa bwana harusi huyo anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo na tukio hilo limetokea wiki iliyopita.

Video; Nitakufilisi ya Queen Darleen

0
0
Video; Nitakufilisi ya Queen Darleen
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB Wasafi Tanzania, Mwajuma Abdul a.k.a Queen Darleen amedondosha mkono mpya kabisa unaokwenda kwa jina ‘Nitakufirisi’ chini ya utayarishaji wa Producer Laizer Classic katika studio za Wasafi Records.

Ikiwa ni kazi ya pili kutoka kwa Queen Darleen chini ya usimamizi wa WCB Wasafi, baada ya ile ‘Kijuso’ aliyoshirikiana na Rayvanny. ‘Nitakufirisi’ umetimiza ahadi ya Queen Darleen iyotoka katikati ya mwaka huu katika mahojiano na Dizzim Online kuwa mwishoni mwa mwaka huu ataanza kuachia kazi zake rasmi.
Hata hivyo Queen katika ngoma hii mpya ameuzungumzia mfumo na hali ya kimahusano wa akina dada(kwa kuuvaa uhusika) na wanaume wenye kuiamini nguvu ya pesa katika kujiridhisha kimapenzi kwa kuwapa jibu kuwa kwa mwendo huo atawafirisi ‘Nitakufirisi’.



Hatimae Elimu ya Shule ya Msingi Kuwa Miaka Sita

0
0
Hatimae Elimu ya Shule ya Msingi Kuwa Miaka Sita
Serikali inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa elimu hapa nchini ambao elimu ya msingi itakuwa inatolewa kwa miaka 6, tofauti na ilivyo sasa ambapo hutolewa kwa miaka 7.

Akijibu swali linalohusu watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu elimu ya sekondari, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Joseph Kakunda ametolea ufafabuzi suala hilo na kusema kwamba mfumo huo mpya utatoa fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea ukiwa ni mwaka mmoja na sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni lazima.
“Napenda kutoa majibu sahihi waliopata mkanganyiko, nilisema sera mpya ya elimu huko tunakoelekea inabadilisha mfuo wa sasa wa elimu ambao utahitaji mtoto aanze chekechea mwaka mmoja, elimu ya msingi miaka 6, sekondari miaka minne na itakuwa ni lazima”, amesema Mheshimiwa Kakunda.
Mheshimiwa Kakunda ameendelea kwa kueleza kwamba kutokana na mfumo huo mpya ambao utaruhusu mwanafunzi kusoma kwa muda mfupi, na baada ya kuhitimu ndio utakuwa kithibitisho pekee kwamba binti amemaliza elimu ya sekondari na ndipo ataruhusiwa kuolewa.
Hivi karibuni Waziri kakunda alitoa taarifa ikisema kwamba ili mtoto wa kike aweze kuolewa atahitaji kuwa na cheti cha kuhitimu sekondari, suala ambalo liliibua mjadala kwa wananchi.


Trump: Hatutakubali Biashara Inayowapendelea Wengine

0
0
Trump: Hatutakubali Biashara Inayowapendelea Wengine
Rais Donald Trum wa Marekani amesema kuwa Marekani haitavumilia biashara yenye upendeleo, katika hotuba yake iliojaa malalamishi katika mkutano wa mataifa ya bara Asia na yale yaliopo katika bahari ya Pacific{Apec} mjini Vietnam.
Amesema kuwa Marekani imejiandaa kushirikiana na mataifa ya Apec iwapo kutakuwa na bishara yenye kutopendelea upande wowote.
Bwana Trump alisema kuwa biashara huru iliathiri kazi za mamilioni wa raia wa Marekani na sasa anataka usawa kutekelezwa.
Tayari ameitembelea China na Japan katika zaira yake ya mataifa matano ya bara Asia.Apec unaleta pamoja uchumi wa mataifa 21 kutoka eneo la Pacific ambao ni asilimia 60 ya uchumi wote duniani.
Tangu achukue mamlaka rais Trump ameiondoa Marekani katika muungano wa Trans-Pacific, ambao unahusisha mkataba mkubwa wa kibishara unaoshirikisha mataifa 12 ya Apec akidai kwamba utaathiri uchumi wa Marekani.

Katika hotuba yake siku ya Ijumaa rais Trump alilishutumu shirika la biashara duniani WTO ambalo hutengeza sheria za biashara duniani na kusema haliweza kufanya kazi zake vyema iwapo wanachama wake hawataheshimu sheria hizo.
Alilalamika kuhusu ukosefu wa usawa wa kibiashara akisema Marekani imeondoa vikwazo vya kibishara huku mataifa mengine yakikataa kufanya hivyo.
''Vitendo kama hivyo vinaathiri watu wengi katika taifa langu'', aliwaambia viongozi wa kibishara na wale wa kisiasa katka mkutano huo.
Lakini hakuyalaumu mataifa ya Apec na badala yake kulalamikia watawala wa awali wa Marekani kwa kutoingilia swala hilo na kurekebisha hali.

Yanga Kumuwajibisha Ngoma Baada ya Kutoweka Bila Taarifa

0
0
Ngoma Kupewa Adhabu Kali Baada ya Baada ya Kutoweka Bila Taarifa
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesisitiza kuwa ni lazima wampe adhabu na onyo kali mshambuliaji wao Mzimbabwe, Donald Ngoma kwa utovu wa nidhamu wa kutoweka bila taarifa

Mkwasa amesema hayo, wakati akizungumza na Kipenga ya East Afrika Radio jana baada ya kuulizwa swali katika mahojiano maalumu kuhusiana na timu ya Yanga kuelekea michezo ijayo ya ligi kuu.
Japo Yanga wenyewe kupitia kwa katibu mkuu wake Mkwasa wamekiri kutofahamu chochote kwa sasa juu ya nini kimemsibu mchezaji huyo wala wapi aliko, lakini taarifa za kidukuzi ambazo Kipenga imezinyaka zinasema kuwa, mshambuliaji huyo aliondoka nchini kimya kimya na kurejea nyumbani kwao Zimbabwe bila ya kutoa taarifa kwa viongozi wake.
Mkwasa amesema, hawana taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji huyo aliyekuwepo nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu na nusu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.
“Hatuna taarifa za kuondoka kwa Ngoma na kama ameondoka basi atakuwa kafanya makosa kwani hakutoa taarifa kwa uongozi.
“Hivyo, kama akirejea nchini na kujiunga na klabu ni lazima tumchukulie hatua za kinidhamu ikiwemo adhabu kwa kitendo alichokifanya,” amesema Mkwasa

Polisi: Mnunuzi wa Nyumba za Lugumi Alitumwa na Lugumi Mwenyewe

0
0
Polisi: Mnunuzi wa Nyumba za Lugumi Alitumwa na Lugumi Mwenyewe
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa Dk. Louis Shika ambaye alishinda mnada wa ununuzi wa nyumba za Said Lugumi na baadae kuzua kizaa-zaa, alitumwa na Lugumi mwenyewe.

Dk. Louis ambaye alifunga mnada wa nyumba hizo kwa kuahidi kulipia shilingi milioni 900, alishindwa hata kutoa robo ya kiasi hicho kwa mujibu wa masharti ya mnada hali iliyopelekea kufikishwa katika kituo cha polisi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi hilo linahisi kuwa alitumwa na Lugumi kutokana na mazingira ya tukio husika.

“Aliwekwa na Lugumi ili kukwamisha mnada,” Mambosasa anakaririwa na Mwananchi ingawa aliweka angalizo kuwa hana vielelezo kuhusu hilo.

“Ingawa sina facts (vielelezo) kuthibitisha hilo, lakini alichokuwa anafanya kinatufanya tuamini hivyo. Kwasababu alikuwa anapandisha bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,” aliongeza.

Alisema kuwa hata muonekano wa mnunuzi huyo ulikuwa unatia shaka na kwamba Jeshi hilo linaendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi.

Kutana na Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed Kutoka Bagamoyo...Ana Dawa za Kurudisha Mapenzi na Zingine Nyingi

0
0

MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

USHAURI: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.

Dr Slaa Aajiriwa Kwenye Duka la SuperMarket Canada

0
0
Aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, imebainika.

Dk. Slaa, kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2015.

Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa Karatu, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo – Supermarket.

Supermarket ya Costco anayofanya kazi Dk. Slaa akihudumu kama Mshauri wa Mauzo (Sales Advisor), akilipwa Dola za Marekani 10 (zaidi ya Sh 20,000) kwa saa, ina hadhi kama Nakumat, Shopers, Imalaseko, Game na maduka mengine makubwa nchini.

Akizungumza na Gazeti la Mtanzania jana kwa simu , Dk. Slaa alisema kuwa kwa sasa anaishi kwa kazi ya mikono yake  kwani ili aweze kuishi anahitaji kufanya kazi zaidi ya mbili hadi nne kwa siku.

“Niko, ninafuatilia matukio Mutukula (ziara ya Rais Dk. John Magufuli jana). Siku zote nimesema ninaishi kwa jasho na kazi ya mikono yangu. Canada ili uishi vizuri, unahitaji kazi zaidi ya mbili au tatu mpaka nne. Hayo nimeweka wazi, sijui jambo jipya kama mtu alikuwa hafuatilii.

“Mimi ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza masomo yangu hasa Interpersonal Communication. Costco ninakofanya kazi ina members (wanachama) 10,000.  Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya 5,000 hadi 7,000,” alisema Dk. Slaa.

Mbali na hilo, alisema kuwa pia anafanya kazi nyingine ikiwa ni pamoja na ushauri (Consultancy).

Alisema kila mara amekuwa akiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mtandao wala propaganda.

“Canada ni kazi, Profesa wa Chuo Kikuu anafanya kazi ya Uber. Sijui kama Uber inafahamika Tanzania, ni dereva Taxi kwa kutumia gari lake binafsi. Ofisa wa Serikali usiku anaosha vyombo hotelini.

“Ndiyo maana familia ina magari mawili au zaidi, TV, nyumba ya kisasa, chakula cha kisasa. Wanatekeleza sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa matendo. Nadhani nimekupa taarifa za kutosha ikiwa ni pamoja na kujibu propaganda kuwa nilihongwa mabilioni.

“Niwahakikishie tena, wakati wa kusoma nilikuwa na scholarship, tangu nianze kazi ninaishi kwa jasho la mikono yangu. Mke wangu yeye ameingia Chuo Kikuu cha York baada ya Diploma yake na bado anapata scholarship.

“Ndiyo maana tuna uwezo wa kuwa na magari mawili aina ya Jeep na Dodge, ukifanya kazi utaishi vizuri. Hii ni pamoja na kugharamiwa bima ya afya (Health Insurance), watoto kusomeshwa na Serikali ya Canada,” alisema Dk. Slaa.

Mei mwaka huu, Dk. Slaa, alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.

Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

“Sina tabia ya kuyumbishwaa, sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,” alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie, ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Credit: Mtanzania

Hii ndio sababu ya kulazwa rumande kwa mnunuzi nyumba za Lugumi

0
0
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtuhumu Dk Louis Shika kutumwa na mfanyabiashara, Said Lugumi, kukwamisha mchakato wa kuziuza nyumba zake kwa mnada.

Akizungumza na Mwananchi leo (Ijumaa), Novemba 10, Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema mazingira ya mnada na jinsi alivyokuwa akifika bei ya kununua nyumba hizo yamelifanya jeshi hilo lihisi ametumwa kukwamisha uuzaji huo.

“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyie ingawa sina fact (vielelezo) za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana top (anapandisha) bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,

Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” amesema  Mambosasa

Mwananchi lilipotaka kujua iwapo mtuhumiwa huyo amemtaja Lugumi katika mahojiano ya awali, Kamanda Mambosasa amesema upelelezi unaendelea na umma utapewa taarifa utakapokamilika.

Source: Mwananchi

Wanachama 50 wa CHADEMA Wahamia CCM

0
0
Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya kuondokewa na wanachama 50 mkoani Geita ambao wamehamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Vijana  hamsini wanachama wa CHADEMA kutoka kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu wa UVCCM wilayani Geita Bw. Ali Rajab alisema vijana hao wamehama Chadema na kujiunga na CCM kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli.

Katika kampeni hizo  Bw. Rajab amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi CCM kwa ujumla kwani bila kufanya hivyo .

Naye Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani Geita Bi. Mazoea Salim, amesema CCM inatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo mdogo katika kata ya Senga kutokana na uwezo wa mgombea ambaye wamemsimamisha.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images