Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live

Wakurugenzi, Watumishi Kukatwa Mishahara

0
0
Wakurugenzi, Watumishi Kukatwa Mishahara
Katibu mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Lauren Ndumbaro amewataka wakurugenzi, wakuu wa idara na watumishi wote kuwa wazalendo na kuwatumikia vyema wananchi.

Katibu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa manispaa ya Songea, ambapo ameeleza kuwa, ni lazima kila mtumishi atimize majukumu yake ili kurahisisha majukumu ya mwingine kwani idara nyingi zinategemeana kiutendaji.
“Kila mtumishi inabidi ajitathimini abadilike awe mwadilifu zaidi, awe mchapakazi zaidi, awe binadamu zaidi na awe mwaminifu zaidi”, amesema Ndumbaro.
Aidha Dkt. Dumbaro amewataka Wakurugenzi na Maafisa utumishi kushughulikia na kuyatatua matatizo ya watumishi na endapo hawatafanya hivyo basi wizara itasimamisha mishahara yao ili nao wapate usumbufu kama wanaopata watumishi wa kawaida.

Wakili wa Mobetto Akanusha Kufutwa kwa Kesi Iliyofunguliwa Kuhusu Matunzo ya Mtoto "Kesi Ipo Pale Pale"

0
0
Wakili wa Mobetto Akanusha Kufutwa kwa Kesi Iliyofunguliwa Kuhusu Matunzo ya Mtoto "Kesi Ipo Pale Pale"
Muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, upande wa watoto kuitupilia mbali kesi ya kukataa kutoa matunzo ya mtoto inayomkabili msanii wa muziki wa kizazi kipya, aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto, wakili wa upande wa mashtaka, Walter Goodluck amefunguka na kueleza kila kitu kuhusu kesi hiyo huku akisisitiza kwamba kesi ipo palepale.
Akizungumza na mtandao huu, Wakili Walter kutoka Kampuni ya Century Attorneys alisema watu wengi wanachanganya taarifa kuhusu kesi hiyo lakini ukweli ni kwamba kesi ya msingi ipo palepale na kwamba kulitokea tatizo dogo la kiufundi kwenye hati ya awali ya mashtaka, iliyosababisha pingamizi la upande wa mshtakiwa kupita.
“Kesi ya msingi ni baba kukataa kutoa matunzo ya mtoto, kilichotokea ni kwamba sekretari wetu alifanya makosa madogo ya kibinadamu wakati akichapa maelezo yetu ya msingi na ndiyo maana walipoweka pingamizi, mahakama ikawapa wao ushindi.
“Hata hivyo, hilo halibadilishi chochote kwa sababu kama nilivyosema, kesi ya msingi ipo palepale na jana baada ya mahakama kuifuta kesi, haraka tulirekebisha makosa yaliyotokea kisha tukaifungua upya ikiwa na marekebisho, kwa hiyo tunachosubiri sasa ni kupangwa kwa tarehe mpya ya kusikilizwa kwa kesi hiyo,” alisema Wakili Walter.
Alipoulizwa kama kiwango kinachoombwa na Mobeto kinaendana na sheria iliyopo, Wakili Walter alifunguka kwamba watu wengi hawajui sheria na ndiyo maana wapo wanaosema kwamba kiwango anachotakiwa kupewa ni kikubwa sana.
“Kwa kawaida, Sheria ya Haki za Mtoto ya Mwaka 2009 inaangalia uwezo na kipato cha baba kwa sababu hata katika maisha ya kawaida, uwezo wa baba ndiyo unaotoa tafsiri ya watoto watakula nini, kama baba anao uwezo, watoto wanaweza kuwa wanakula nyama hata kila siku. Kiwango hicho kinaendana na kipato cha baba yake.
“Kwa kawaida haya mapingamizi huwa yanawekwa kwa ajili ya kupoteza muda tu na kwa kawaida, kesi za namna hii huwa hazichukui zaidi ya miezi sita, kwa hiyo ni suala la muda tu.

TFDA Yafunguka Sababu ya Kufungia Lipstiki za Wema Sepetu

0
0
TFDA Yafunguka Sababu ya Kufungia Lipstiki za Wema Sepetu
Serikali imeanika sababu ya kuifungia lipstic ya mwanadada aliyewahi kuwa Miss Tanzania na Muigizaji wa Filamu Bongo, Wema Sepetu iitwayo Kiss.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Nchini (TBS),  rangi hizo hazina ubora kwa matumizi ya binadamu.

Kwa upande wa Meneja wa Wema Sepetu, Happy Shame alipotakiwa kuzungumzia suala hilo amefunguka na kusema kwamba taarifa za kufungiwa kwa bidhaa hizo yeye kama Meneja hajazipata bali anachofahamu mzigo ulikuwa haujaingia sokoni na kwamba muigizajin huyo alikuwa bado akifuatilia vibali kutoka mamlaka husika.

Rangi hizo za mdomo za muigizaji Wema Sepetu zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 usiku wa birthday yake.

Watu wa Nne Mbaroni kwa Kosa la Kumtukana Mke wa Mugabe

0
0
Watu wa Nne Mbaroni kwa Kosa la Kumtukana Mke wa Mugabe
Watu wanne wamekamatwa nchini Zimbabwe wakituhumiwa kumzomea mke wa rais wa nchi hiyo Grace Mugabe wakati akihutubia mkutano wa hadhara siku ya jumamosi iliyopita.

Gazeti linalomilikiwa na Serikali la The Herald limeripoti kwamba watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kupuuza mamlaka ya rais.
Kuzomea huko kuliibuka kati ya makundi mawili ndani ya chama tawala cha Zanu-PF yanayopambana juu na nani atakuwa mrithi wa rais Robert Mugabe ambapo kuna kundi linalimuunga mkono mke wa rais Grace Mugabe na lile linalomuunga mkono Makamu wa rais aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa.
Imedaiwa kwamba watu hao waliokamatwa ni wafuasi wa aliyekuwa Makamu wa Rais
Watu hao walikamatwa mara baada ya mkutano huo uliofanyika mjini Bulawayo,watuhumiwa hao inasemekana ni aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa .
Watuhumiwa hao waliokatwa ni wanaume watatu na mwanamke mmoja wako nje kwa dhamana.

Rais Magufuli Akosoa Uamuzi Uliotolewa na ICC

0
0
Rais Magufuli Akosoa Uamuzi Uliotolewa na ICC
Rais John Magufuli amelaani uamuzi ulitolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), ambayo imemuagiza mwendesha mashtaka wake kuanzisha uchunguzi dhidi ya mgogoro wa Burundi.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi Novemba 11,2017 akiwa mjini Masaka nchini Uganda kabla ya kuagana na mwenyeji wake, Rais Yoweri Museveni baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku tatu.

Rais Magufuli katika taarifa ya Ikulu amesema majaji wa ICC wametoa uamuzi huo Novemba 9,2017 na kumtaka mwendesha mashtaka wa Mahakama hiyo kuchunguza vitendo vya kihalifu dhidi ya binadamu vilivyotokea Burundi tangu kuzuka kwa mvutano miaka miwili iliyopita.

Rais Magufuli amesema, “Hatua hii inarudisha nyuma jitihada zilizochukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyounda kamati ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi inayoongozwa na Rais Museveni  na Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa.”

Amesema hali ya Burundi si mbaya kama inavyotangazwa kwa kuwa tayari wakimbizi wengi waliokuwa Tanzania wamerejea nchini humo, huku wengine wakiendelea kurejea.

Rais Magufuli amesema viongozi wanaosuluhisha mgogoro huo wamepanga kutana Novemba 23,2017 kuendeleza mchakato wa utatuzi.

Akizungumzia hilo, Rais Museveni ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) amesema ICC inaingilia mambo ya jumuiya hiyo bila kuwahusisha viongozi wake jambo ambalo si sahihi na linarudisha nyuma juhudi za kutafuta amani ya Burundi

Trump na Putin 'Waafikiana Kuuwashinda Islamic State Nchini Syria'

0
0
Trump na Putin 'Waafikiana Kuuwashinda Islamic State Nchini Syria'
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wamekubaliana kuhakikisha kundi la wapiganaji wanaojiita Islamic State (IS) wanashindwa nchini Syria, maafisa wa rais wa Urusi wamesema.
Ikulu ya Urusi imesema taarifa imeandaliwa na wataalamu baada ya viongozi hao wawili kukutana kwa muda mfupi pambizoni mwa mkutano wa viongozi wa nchi za Asia na Pasific nchini Vietnam Jumamosi.
Kwa jumla, viongozi hao wawili walikutana mara tatu katika kipindi cha saa 24 katika mji wa Da Nang.
Hakujakuwa na thibitisho lolote rasmi kutoka kwa Marekani kuhusu tamko hilo la Urusi.
Mkutano kati ya Rais Trump na Vladimir Putin ulitarajiwa kufanyika wakati wa mkutano huo wa Apec, lakini ni maelezo machache sana ambayo yametolewa.
Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza Julai katika mkutano wa G20 katika mji wa Hamburg nchini Ujerumani
Maswali kuhusu uhusiano wa Donald Trump na Urusi yamekuwa yakiulizwa mara kwa mara.
Wasaidizi wake wakuu wa zamani wanachunguzwa kwa tuhuma za kushirikiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2016.

Ingawa White House haijasema chochote kuhusu mkutano wa wawili hao, taarifa ya Kremlin iliyotolewa Jumamosi imesema viongozi hao "waliafikiana kwamba mzozo wa Syria hauwezi kutatuliwa kwa njia ya kijeshi".
Kadhalika, walikariri "kujitolea kwao kuwashinda Isis [jina jingine la IS]" na kuzitaka pande zote kushiriki mazungumzo ya amani ya Geneva.

Samatta Afanyiwa Upasuaji wa Goti la Mguu wa Kulia

0
0
Samatta Kafanyiwa Upasuaji wa Goti la Mguu wa Kulia
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta siku ya Jumamosi ya November 4 2017 katika uwanja wao wa Luminus Arena alikuwa uwanjani kuitumikia Genk lakini kwa bahati mbaya hakumaliza game.

Samatta aliichezea KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Lokeren mchezo ambao ulimalizika kwa sare tasa (0-0) lakini nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya Genk alishindwa kumaliza dakika 90 na kuishia kucheza kwa dakika 40.

Uchunguzi ulifanywa na jopo la madaktari wa Genk na kueleza kuwa Samatta atahitaji upasuaji wa goti lake la kulia baada ya kuumia goti hilo na atakuwa nje ya uwanja hadi mwanzoni mwa kipindi cha majira ya baridi, good news ni kuwa Samatta leo amethibitisha kuwa upasuaji wake umeenda salama.

Rais Magufuli Atoa Agizo Hili kwa Wazili

0
0
Rais Magufuli Atoa Agizo Hili kwa kwa Wazili
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutafuta fedha na kujenga barabara ya Mutukula – Minziro yenye urefu wa kilometa 6 ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 11 Novemba, 2017 katika Mji wa Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda baada ya kupokea kero za wananchi waliokusanyika jirani na geti la kuvuka mpaka huo ambao wamedai kukosekana kwa barabara hiyo kunawalazimu kutumia barabara ya kuzunguka Kyaka.

Pamoja na kumtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kujenga barabara hiyo, JPM pia amewataka viongozi wa Mkoa wa Kagera kufanyia kazi madai ya wananchi waliolalamikia kupata usumbufu katika kizuizi cha Kyaka jirani na mto Kagera.

Hata hivyo Dr. Magufuli amewataka wananchi wa Mutukula kutambua kazi ya ulinzi na usalama inayofanywa na vyombo vya dola na amewataka kutoa ushirikiano kwa viongozi na Serikali katika kuhakikisha mpaka huo unakuwa salama.

Amewataka pia wananchi hao kuongeza juhudi katika shughuli za maendeleo zikiwemo kilimo na biashara na amerejea agizo lake la kuutaka Mkoa wa Kagera kujenga soko la kimataifa katika maeneo ya jirani na mpaka huo ili wananchi wapate mahali pa kuuzia bidhaa zao kwa njia halali.

Je Wajua Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo ya Kiume?

0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE MADOGO?
Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia ,hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wenzao,kwakawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6_8 vinginevyo mtu huyu ana matatizo.


Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo baadhi ni,upungufu wa vichocheo (hornes) za gestrojen ambapo mwanaume anapobalehe vichocheo hivi (hormones)huchochea ujuaji wa uume.chango ambalo hushambulia nerve ambapo huharibu kabisa ukuaji wa uume, Punyeto ambayo huasili misuli ya uume,pia ngiri ambayo huleta maumivu ya tumbo kuunguluma na kujaa gesi,korodani moja kuvimba,kutopata choo vizuri,sababu hizi na nyinginezo hufanya uume kulegea na kisinyaa nakuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu zakiume (hamu ya tendo landoa hupungua au kuisha kabisa).NSUMBU,Nidawa inayozalisha hormones za gestrogene na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.NZAGI,Ni dawa ya kurudisha nguvu za kiume ,hutia hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha nakuponya kabisa tatizo hilo. Pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk 15 nakuendelea kwa tendo la kwanza.kumbuka dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji.Natunatibu kisukari,bp,ngiri,miguu kuwaka moto,namengine mengi.

WASILIANA OSTADHI JUMA KWA SIMU NO,0784002216 AU 0769597778

Mwanafunzi aliyefariki kwa kupigwa radi afaulu la saba

0
0
Buchosa. Aliyekuwa mhitimu wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Nyamanzugo, Charles Samson ambaye alifariki dunia kwa kupigwa na radi Oktoba 19, ni miongoni mwa wanafunzi 6, 500 waliofaulu mtihani wa darasa la saba katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.

Mwanafunzi huyo alipigwa na radi alipokuwa akijisomea na wenzake kujiandaa na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.

Jumla ya wanafunzi 8, 600 walifanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba katika Halmashauri ya Buchosa.

Ofisa Elimu wa Kata ya Nyanzenda, Leogratus Rutanywanilwa alisema kwamba Samson amefaulu kwa kupata alama A.

“Wenzake wawili aliokuwa akijisomea nao pia wamefaulu mtihani huo na wanasubiri kujiunga na elimu ya sekondari mwakani,” alisema Rutanywanilwa.

Ofisa elimu hiyo pia aliwataja wanafunzi walionusurika katika tukio hilo ambao wote wamefaulu kwa kupata alama B, kuwa ni pamoja na Claud Mussa aliyekuwa anasoma Shule ya Msingi Luchili na Lutema Shilaka wa Shule ya Msingi Nyamabano.

Wanafunzi hao watatu walipigwa na radi Oktoba 19, walipokuwa wakijisomea katika jengo la Kanisa la AGT katika Kijiji cha Luchili wilayani Sengerema.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu kufaulu kwao, mmoja wa watoto hao, Mussa aliyenusurika alisema kwamba hadi sasa bado wana kumbukumbu ya mwenzao.

Mama mzazi wa marehemu, Maria Mashauri aliwasihi watoto walionusurika katika tukio hilo kusoma kwa bidii na kufaulu kama njia ya kumuenzi mwenzao aliyetangulia mbele ya haki.

Wanne wakamatwa kwa kosa la kumzomea mke wa Rais

0
0
Watu wanne wamekamatwa nchini Zimbabwe wakituhumiwa kumzomea mke wa rais wa nchi hiyo Grace Mugabe wakati akihutubia mkutano wa hadhara siku ya jumamosi iliyopita.

Gazeti linalomilikiwa na Serikali la The Herald limeripoti kwamba watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka ya kupuuza mamlaka ya rais.

Kuzomea huko kuliibuka kati ya makundi mawili ndani ya chama tawala cha Zanu-PF yanayopambana juu ya nani atakuwa mrithi wa rais Robert Mugabe ambapo kuna kundi linalimuunga mkono mke wa rais Grace Mugabe na lile linalomuunga mkono Makamu wa rais aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa.

Imedaiwa kwamba watu hao waliokamatwa ni wafuasi wa aliyekuwa Makamu wa Rais
Watu hao walikamatwa mara baada ya mkutano huo uliofanyika mjini Bulawayo,watuhumiwa hao inasemekana ni aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa .

Watuhumiwa hao waliokamatwa ni wanaume watatu na mwanamke mmoja wako nje kwa dhamana.

Rais Magufuli Amaliza Ziara ya Siku Tatu Uganda Tayari kwa Kurejea Nchini

0
0
Rais Magufuli Amaliza Ziara ya Siku Tatu Uganda Tayari kwa Kurejea Nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemaliza ziara ya siku 3 ya kiserikali nchini Uganda na kurejea rasmi nchini Tanzania.

Aliyemtupiaga Rais Mstaafu George Bush Viatu Kwenye Mkutano....Atolewa Gerezani

0
0
Aliyemtupiaga Rais Mstaafu George Bush Viatu Kwenye Mkutano....Atolewa Gerezani
Mwandishi wa Habari wa Iraq, Muntadhar Al-Zaidi aliyemtupia viatu rais mtaafu wa Marekani George W.Bush, wakati wa mkutano wa waandishi wa habari wa Iraq mnamo tarehe 14 Desemba 2008 ameachiwa huru.

Katika tukio hilo la kusisimua, Bush alilazimika kukimbia, akiepuka kugongwa na viatu hivyo.

Kiatu cha pili kilichorushwa na mtu huyo, kilipiga bendera ya Marekani ambàpo wakati huo, Al-Zaidi anacheka.

Baada ya tukio hilo, haraka walinzi walimkamata na kumtoa katika chumba. Matukio ya aina hii yalikuwa yakitokea mara kwa mara kwa kiwango cha kimataifa.

Nimezaliwa Kufunga na Kuvunja Rekodi - Lukaku

0
0
Nimezaliwa Kufunga na Kuvunja Rekodi - Lukaku
Mshambuliaji wa Manchester United Romelo Lukaku amesema amezaliwa kufunga na anaamini ataendelea kufanya hivyo pamoja na kuvunja rekodi ufungaji bora nchini Ubelgiji kabla ya mwaka huu kuisha.

Lukaku ameyasema hayo baada ya kuifikia rekodi ya Paul Van Himst na Bernard Voorhoof ya mabao 30 katika timu ya taifa ya Ubelgiji, ambapo ameeleza kuwa bado ana nia ya kufunga zaidi.
“Nimezaliwa kwa ajili ya hili na nitaendelea kufanya hivyo", amesema Lukaku ambaye sasa anahitaji bao moja tu kuweza kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wa nchini ya Ubelgiji.

Lukaku alifunga mabao mawili kwenye sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mexico hivyo kufikisha mabao 30 sawa na Paul Van Himst na Bernard Voorhoof ambao wanashikilia rekodi hiyo.
Lukaku anafanya vizuri msimu huu akiwa na Manchester United ambapo tayari amefunga mabao saba kwenye ligi kuu soka nchini England. Lukaku anaweza kuvunja rekodi siku ya jumanne ambapo Ubelgiji itacheza mechi ya kirafiki na Japan. 

Mc Pilipili Ampongeza Dogo Janja Kufunga Ndoa "Amefanya Uchaguzi Mzuri Bila Kuangalia Watu Wanasema Nini"

0
0
Mc Pilipili Ampongeza Dogo Janja Kufunga Ndoa "Amefanya Uchaguzi Mzuri Bila Kuangalia Watu Wanasema Nini"
Baada ya msanii wa Bongo Flava Dogo Janja kufunga ndoa na Irene Uwoya, Mc Pilipili amesema msanii huyo amefanya uchaguzi mzuri.
Amesema Dogo Janja amefuata moyo wake bila kuangalia watu watasema nini kwani toka zamani alikuwa anampenda Irene.

“Ningemsifu Dogo Janja kwa ajili ya uchaguzi mzuri wa bila kuangalia watu wanasema nini, bali kaangalia yeye anapenda nini” amesema.

“Dogo Janja tangu akiwa mdogo amekuwa anampenda sana Irene Uwoya na hata post zake zimekuwa zikionyesha kuwa anampenda toka zamani that is very nice kwa sababu anakuwa na msichana ambaye anamfikiri” Mc Pilipili ameiambia Bongo5.

Raia wa Korea Kaskazini Aiomba China Kutorudisha Nyumbani Familia Yake

0
0
Raia wa Korea Kaskazini Aiomba China Kutorudisha Nyumbani Familia Yake
Raia mmoja wa Korea Kaskazini amemuomba rais wa China Xi Jinping kutomrudisha nyumbani mkewe na mwanawe wa kiume akisema kuwa watakabiliwa na kifungo jela au kifo iwapo watarudishwa Korea Kaskazini.
Mwanamke na mvulana wa miaka minne wanaeleweka kuwa miongoni mwa kundi la watu 10 wa Korea Kaskazini waliozuiliwa nchini China wiki iliopita baada ya kuvuka na kuingia nchini humo kisiri.
Mtu huyo ambaye alitaka kutambulika kwa jina la Lee pekee , alitorokea Korea Kusini 2015.
Alirekodi ombi lake katika mkanda wa video ambao uliwasilishwa kwa BBC.
Alisema kuwa mkewe na mwanawe watakabiliwa na hatia ya kifo ama kufungwa jela iwapo watarudishwa nyumbani Korea Kaskazini.
''Ningependa rais Xi Jinping na rais Donald Trump kumfikiria mwanangu kama kilembwekeza wao na kumleta mwanangu katika taifa huru la Korea Kusini '', alisema.tafadhali tusaidie.
''Okoa familia yangu kutorudishwa Korea Kaskazini. Mimi kama baba nawaomba viongozi hawa wawili kuisaidia familia yangu. Tafadhalini tusaidieni.Anasema kuwa anafuatwa na kiwiliwili cha mwanaye katika jela''.
''Nasikia sauti ya mwanangu ikiniita'', alisema.
''Namuona mwanangu katika jela ile baridi akimlilia babake, alisema.
''siwezi kusimama na kutochukua hatua yoyote''.

Noah ya Abiria Yagongana Uso kwa Uso na Lori

0
0
Noah ya Abiria Yagongana Uso kwa Uso na Roli
Taarifa ya ajali iliyotokea mchana huu kwenye mkoa wa Kilimanjaro eneo la kikavu kwa Sadala baada ya Gari la maji ya Kilimanjaro ambalo ndio chanzo cha ajali, kulipita gari jingine na kugongana uso kwa uso na Noah ya abiria iliyokua ikitokea Moshi Mjini kwenda Sanja Juu.

Inasemekana ni watu wanne wamepoteza maisha kwenye ajali hiyo lakini millardayo.com na AyoTV zinaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi kuthibitisha hilo, majeruhi wamepelekwa hospitali.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana

0
0

THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)
MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)
Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.
Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.
ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..
Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.
+255 746 757 102 Kupiga tu.

Mwanafunzi aliyeongoza darasa la saba apata shavu hili

0
0
Mwanafunzi  aliyeongoza mtihani wa darasa la saba Hadija Aziz amefunguliwa akaunti na benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya pongezi kwake.

Benki ya NMB imetoa Sh 500,00 na kumfungulia akaunti mwanafunzi huyo wa shule ya Sir John ikiwa ni kumpongeza kwa kuwa wa kwanza katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa darasa la saba nchini mwaka huu

Akizungumza leo Novemba 11 ,Meneja wa NMB Tawi la Madaraka, Victor Msofe amesema kuwa akaunti aliyofunguliwa mwanafunzi huyo ni aina ya Chipukizi ambayo itamsaidia katika kununua mahitaji yake muhimu awapo shule ya Sekondari.

“NMB Tawi la Madaraka tumefurahishwa sana kusikia taarifa kuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa ametoka Jijini Tanga, ni faraja kwa mkoa na wateja wetu kwa ujumla hivyo tukaona tumuunge mkono kwa kumfungulia akaunti” amesema  Msofe.

Meneja huyo amesema  hatua hiyo ya NMB ina lengo la kuwahamasisha wanafunzi wengine iwe wa shule za msingi au Sekondari kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuwataka wadau wengine kumchangia kwa kutumia akaunti hiyo .

Hadija ameishukuru  NMB kwa kumfungulia akaunti na kubainisha kuwa imempa nguvu na ari ya kufanya vizuri zaidi kwenye masomo ya Sekondari.

“Akili na mawazo yangu yote hivi sasa yapo kwenye masomo, nafikiria nitakwenda kusoma shule gani, na huko lengo langu ni kuhakikisha naongoza mitihani yote ili nifikie lengo langu la kuwa daktari baadaye” amesema  Hadija.

Mama wa mwanafunzi huyo, Jane Kihiyo ameshukuru NMB kwa kumpa nguvu mtoto wake  huyo na kusisitiza kwamba tukio la kumfungulia akaunti limewafurahisha.

Mtaalamu wa masuala ya bima jijini Tanga, Ramadhani Manyeko amewashauri wadau wa elimu kuangalia uwezekano wa kumtafutia shule itakayoweza kuendeleza kipaji chake cha akili darasani bila kujali ni ya Serikali au binafsi.

“Kwa nchi za wenzetu Hadija  na  wenzake walioshika nafasi ya pili hadi tano wangekuwa ni lulu kubwa, wangetafutiwa shule zenye uwezo wa kuwaendeleza vipaji vyao bila kujali ni ya Serikali au binafsi kwani ni faida kubwa kwa Taifa na wangelipiwa gharama zote ili wasome bila usumbufu” amesema Manyeko.

Mwananchi:

Kagasheki amvaa Kigwangalla kumhusisha na rushwa

0
0
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri wa sasa wa sasa wa wizara hiyo Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa ana mahusiano ya karibu na Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya rushwa.

Kupitia mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh. Kigwangalla amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na kuhusu rushwa aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu.

Balozi ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alinukuliwa kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja mimi kuwa karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu nilivogawa nikiwa Waziri na rushwa niliyopokea,"

Hata hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao

"Mhe. Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu sana. Tuongee kindugu nje ya hapa! Kuweka sawa ni kwamba 'sikukutaja!" Kigwangalla.

Hivi karibuni Waziri Kigwangalla aliweka wazi kwamba amewaondoa Askari wote wa kituo cha Geti la Kleins kwa kuwa wamekuwa wakitumika na mwekezaji huyo ambaye ana uhusiano wa Karibu na Prof. Songorwa (aliyemsimamisha kazi siku chache zilizopita) na alikuwa na uhusiano ya karibu na Prof. Maghembe, Lazaro Nyalandu, balozi Kagasheki na Mawaziri wa Maliasili na Utalii wa zamani.

Balozi Kagasheki aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika uongozi wa serikali ya awamu ya nne ambapo aliongoza wizara hiyo Mwaka  (2012-2013)
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live




Latest Images