Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Baada ya Takukuru Kutangaza Donge Nono Hatimaye Mhasibu Wake Ajisalimisha

0
0
Baada ya Takukuru Kutangaza Donge Nono Hatimaye Mhasibu Wake Ajisalimisha
Aliyekuwa Mhasibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey John Gugai amejisalimisha katika taasisi hiyo.
Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 15,  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola amesema Gugai amejisalimisha na hatua za kisheria zinaendelea.
"Ni kweli amejisalimisha na yupo chini ya vyombo vya ulinzi na usalama na hatua zaidi za kisheria zitafuata" amesema Kamishna Mlowola
Mtumishi huyo anatuhumiwa kujipatia mali kinyume cha Sheria za Utumishi wa umma huku Takukuru wakidai kwamba kama atadhibitisha uhalali wa umiliki wake ataachiwa na akishindwa atachukuliwa hatua.
Gugai amejisalimisha ikiwa ni siku moja imepita tangu Takukuru ilipotangaza zawadi ya Sh 10 milioni kwa mwananchi yoyote ambaye angefanikisha kumtia nguvuni mtumishi  huyo.
Hata hivyo, Kamishna Molowa ameshindwa kufafanua kama amejisalimisha mwenyewe au kuna mtu katoa taarifa.

Shirika la Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Lafungiwa na Serikali

0
0
Shirika la Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Lafungiwa na Serikali
Ofisi ya msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali  (NGOs) imesimamisha shughuli za Shirika la Tanzania Social Support Foundation (TSSF) kuanzia tarehe 14/11/2017 ili kupisha uchunguzi.

Taarifa ya ofisi hiyo imesema kuwa serikali inafanya uchunguzi juu ya tuhuma zinazolikabili shirika hilo za kutapeli watu mbalimbali nchini kwa kisingizio cha kuwapatia mikopo kwa ajili ya elimu ya juu kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Aidha serikali imeagiza kusimamishwa kwa shughuli zote za shirika hilo ikiwa ni pamoja na kufunga ofisi zote za shirika hadi uchunguzi utakapokamilika.
Viongozi wa shirika hilo wameagizwa kufika katika Ofisi ya msajili mara moja wakiwa na nyaraka halisi za usajili wa Shirika ambavyo ni Cheti na Katiba kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.

Kadinda Afunguka Kuhusu Lipstick za Wema Kufungiwa "Hatuna Taarifa Za Kufungiwa kwa Sababu Vibali Vyote Vipo"

0
0
Kadinda Afunguka Kuhusu Lipstick za Wema Kufungiwa "Hatuna Taarifa Za Kufungiwa kwa Sababu Vibali Vyote Vipo"
Baada ya taarifa kuwepo kuwa bidhaa za lipstick ‘Kiss’ za Wema Sepetu kupingwa maarufu na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA), mtu wa karibu na mrembo huyo Martin Kadinda amesema hawana taarifa hizo.
Martin Kadinda  ambaye aliwahi kuwa meneja wa Wema ameiambia TV E kuwa wao walikuwa na vibali vyote vya kuuza bidhaa hizo na kwa sasa hawana tena bidhaa zozote kwani wameshauza.
“Hatuna taarifa kwa sababu vibali vyote vipo na hizo zilishaenda sokoni na zilishaisha, kwa hiyo sisi kama sisi hatuna tayari zipo sokoni” amesema.
“Kama ni mtu aliamka na kuamua kuandika all the best kwake, sisi mziko ulishakwisha alitengeneza product za kwanza now anakuja na product nyingine” amesisitiza.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

0
0
THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)
MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)
Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.
Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.
ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..
Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.
+255 746 757 102 Kupiga tu.

Mama Mzazi wa Irene Uwoya Amlilia Ndikumana Atoa Maneno Mazito

0
0
Mama Mzazi wa Irene Uwoya Amlilia Ndikumana Atoa Maneno Mazito
Mama mzazi wa msanii Irene Uwoya ambaye ni mkwe wa marehemu Hamad Ndikumana aliyefariki usiku wa jana kuamkia leo, ameshikwa na uchungu kwa kumwaga machozi mengi na kusema kabla marehemu hajafariki alikuwa anawasiliana naye na alimtaka kuwa na subira

Akiongea huku akilia kwa kwikwi na machozi yakimtoka, mama Uwoya amesema Ndikumana alikuwa ni zaidi ya mkwe kwake, na waliishi vizuri siku zote, na kumtia moyo kuwa atayavumilia yote ambayo alikuwa akiyapitia.
“Ndikumana mimi sijui nianzie wapi, alikuwa mkwe wangu kipenzi alikuwa kama rafiki, alivuka hata ukwe, Ndikumana wangu mkwe wangu siku zote tumeishi nae vizuri, siku zote tumekuwa tukiwasiliana mpaka mwishoni hapa nilikuwa natoka safari, ananiambia mama naomba tuwe na moyo wa subira, mimi nitavumilia yote ya dunia lakini mimi ni mwanao mpaka naingia kaburini, na kweli mpaka anaingia kaburini, mwanangu mimi nilikuwa nampenda”, alisikika mama yake Irene Uwoya ambaye alikuwa akilia kwa uchungu.
Ndikumana alikuwa mume wa ndoa wa msanii Irene Uwoya na baadaye walitengana, na kisha Irene Uwoya kuolewa na msanii wa bongo Fleva Dogo Janja.

Polisi Nchini Zimbabwe 'Wadhibitiwa' na Jeshi Harare

0
0
Polisi Nchini Zimbabwe 'Wadhibitiwa' na Jeshi Harare
Mwanasheria mmoja katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare amepakia kwenye Twitter picha inayoonyesha kundi la maafisa wa polisi wakiwa wameketi kwenye foleni, huku wakiwa chini ya uangalizi wa maafisa wa jeshi.

Fadzayi Mahere, ambaye anapania kuwa mbunge wa Mount Pleasant, Harare, anasema alipiga picha hiyo kupitia dirisha la afisi yake.

Haijabainika nini kilikuwa ninatokea kwenye picha hiyo.

Tuzo kwa Walimu Zazinduliwa Rasmi Kinondoni

0
0
Tuzo kwa Walimu Zazinduliwa Rasmi Kinondoni
Manispaa ya Kinondoni imefanya vizuri zaidi katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017 kwa kupata ufaulu wa asilimia 93.02, ambapo imekuwa halmashauri ya kwanza kitaifa.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika sherehe za uzinduzi wa kukabidhi tuzo kwa shule na walimu waliofanya vizuri meya mstahiki wa kinondoni Benjamin Sitta kama manispaa wameamua kufanya hivyo ili kuwapa motisha walimu na shule ambazo zimefanya vibaya mwaka huu ziweze kujipanga ili zifanye vizuri,


Aidha kutokana na mafanikio hayo manispaa ya Kinondoni kwa kutambua mchango wa walimu imeamua kutoa tuzo kwa walimu wote ambao masomo yao yamefanya vizuri kwa kufaulisha alama "A", hivyo kila A moja mwalimu wa somo husika amepewa sh.2500 ikiwa ni mwanzo na motisha kwa walimu.


Hivyo shule zote 78 zilizopata ufaulu wa juu kwa mwaka 2017 zimepewa tuzo ili kuzihimiza shule zote kuongeza juhudi na kuimarisha ufaulu wao kwa kasi zaidi.

 " Nachukua fursa hii kuwapongeza walimu wote wa shule za msingi, wazazi mkurugenzi, afisa elimu na Rais kwa jitihada wanazozifanya kwa kufanikisha mpango wa elimu bure ambapo unapelekea kupata matunda haya" alisema Sitta.

Kwa upende wake mkuu wa wilaya hiyo Ally Hapi amewapongeza walimu wote ambao shule zao zimefanya vizuri na kuahidi kuendelea kushilikiana nao ili kufikia lengo la ufaulu wa hali ya juu zaidi.

"Imekuwa ni kawaida yetu kufanya vizuri hivyo sio kitu cha ajabu sana kwa matokeo haya ambayo tumeyapata na tutaendelea kufanya hivi mpaka ufaulu ufike asilimia 100" alisema Hapi.

Msiba wa Ndikumana: Watu Mbalimbali Wakusanyika Nyumbani kwa Irene Uwoya

0
0
Msiba wa Ndikumana: Watu Mbalimbali Wakusanyika Nyumbani kwa Irene Uwoya
MASTAA na watu mbalimbali wanaendelea kufika nyumbani kwa mwigizaji wa filamu Irene Uwoya, Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam kuwafariji wafiwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mume wa staa huyo, Hamad Ndikumana, aliyefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao Rwanda kutokana na maradhi mbalimbali.
Kabla ya kifo Ndikumana alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Rayon Sports ya nchini humo  akiwa pia amewahi kuchezea timu mbalimbali za soka barani Afrika na Ulaya.
Kwa Irene Uwoya ameacha mtoto mmoja aitwaye Krish.

Rais Magufuli Atoa Agizo kwa Tanroads Kuweka X Jengo la Tanesco na Kuvunjwa

0
0
Rais Magufuli Atoa Agizo kwa Tanroads Kuweka X Jengo la Tanesco na Kuvunjwa
Rais John Magufuli amemwagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka alama ya X kwenye jengo la Shirika la Umeme (Tanesco) na sehemu ya jengo la Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili kupisha ujenzi wa daraja la juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea Chato alikokwenda baada ya kumaliza ziara ya siku tatu nchini Uganda.

Amewataka Tanroads kuwapa taarifa wahusika kuhusu kubomolewa kwa majengo yao ili wapate eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo unaolenga kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam.

“Sasa mimi nataka ikiwezekana leo au kesho muweke X jengo la Tanesco…muweke X sehemu ile ya mwanzo ya Wizara ya Maji,” amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na wananchi waliojitokeza katika eneo hilo.

Kiongozi huyo Serikali amesema kwamba Sheria ya Hifadhi ya Barabara ilianza tangu mwaka 1932, ikafanyiwa mabadiliko mwaka 1959, 1964 na 1967.

“Sheria ni msumeno, Serikali ikifanya kosa inasulubiwa, Rais akijenga kwenye Road Reserve (hifadhi ya barabara) anachukuliwa hatua hizo hizo,” amesema Rais Magufuli wakati wa ziara hiyo.

Wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, Rais Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi wakati huo aliagiza kubomolewa kwa jengo la Tanesco, hata hivyo, aliyekuwa waziri mkuu, Mizengo Pinda alizuia kubomolewa kwa jengo hilo na mengine yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara.

Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa ahamia CCM

0
0
Iringa. Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Frenk Mwaisumbe ametangaza kuhama chama chake na kujiunga na CCM.

Mwaisumbe ambaye alishika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita hadi alipoachia wadhifa huo Januari mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari mjini hapa leo Jumatano Mwaisumbe ametaja sababu za kujiunga na CCM kuwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli za kufufua uchumi wa nchi.

Mjue Zaidi Marehemu Ndikumana wa Uwoya Aliyefariki Ghafla

0
0
Klabu ya soka ya Rayol Sports imempoteza kocha wake msaidizi Hamad Ndikumana ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo ambapo ripoti za awali zinasema kifo chake kimesababishwa na matatizo ya Moyo.

Kifo cha Ndikumana sio tu kitawaumiza viongozi wa klabu hiyo bali ni wapenda soka wote wa Rwanda na ukanda wote wa Afrika mashariki na kati kutokana na umahiri wa Ndikumana alioujenga tangu mwaka 1998 alipoanza kuitumikia klabu ya Rayol Sports.
Ndikumana ambaye alikuwa anacheza nafasi ya ulinzi wa pembeni akicheza pande zote kulia na kushoto alijizolea umaarufu kiasi cha mashabiki kumpachika jina la Kataut kutokana na uwezo wake wa kupokonya mpira washambuliaji (Tackling).

Uwezo wake ulionekana kuwa mkubwa zaidi kwenye soka akiwa na umri wa miaka 19 tu kiasi cha kuzivutia klabu mbalimbali za Ulaya. Kataut alifanikiwa kuzichezea timu za KV Turnhout na KV Mechelen za Ubelgiji kati ya miaka ya 2000 na 2003.
Baadae alijiunga na klabu ya RSC Anderlecht ya hukohuko Ubelgiji kabla ya kucheza klabu zingine kadhaa kwenye nchi mbalimbali barani Ulaya hadi mwaka 2011 alipomalizana rasmi na klabu ya soka ya APOP Kinyras Peyias FC ya Cyprus ambapo alirejea nyumbani Rwanda na kisha kujiunga na klabu ya Stand United ya Shinyanga ambapo hakudumu sana.

Rayol Sports ilibaki kuwa nyumbani kwa Kataut kutokana na upendo wa mashabiki wa klabu hiyo kwake tangu akiwa mdogo ambapo baada ya kustaafu kucheza soka aliibukia kwenye majukumu ya ukocha akiwa kocha msaidizi wa Rayol Sports chini. August 8 aliiongoza Rayol Sports dhidi ya Simba kwenye Tamasha la ‘Simba Day’ ambapo walipoteza kwa bao 1-0.
Kwaheri Ndikumana zaidi na zaidi Watanzania hawatakukumbuka kwa kuwa mchezaji pekee kwani kila mpenda soka na burudani alimfahamu Ndikumana kama mume wa mwigizaji Irene Uwoya ambao walifunga ndoa mwaka 2007 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye ni Krish, lakini hadi anafariki walikuwa wametengena.

Sakata la Msondo Ngoma: BASATA yawashukia WCB Wasema Ukitumia kazi ya Mtu Bila Utaratibu Hiyo Moja kwa Moja ni Kosa

0
0
Baada ya Band ya Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya wimbo wake kwenye wimbo wa “Zilipendwa” Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza ameongea yafuatayo.

“Unaweza kuitazama katika mitizamo mbalimbali lakini unapoangalia kwamba wanaanza kushtakiana kimsingi ni taratibu ambayo inagusa sana mambo ya haki miliki, kabla ya kuitumia kazi ya mtu ni vizuri ukamuona mwenye kazi mkubaliane” AMEONGEZA NA KUSEMA

“Ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja kwa moja ni kosa, cha msingi hata kabla ya kumuweka Mwanasheria ili kudai haki yako ni vizuri ukawafata au ukawasiliana na alietumia kazi yako bila ruhusa…. katika hili linalojitokeza sasa hivi ni swala la kuamshana kwamba kazi ya sanaa ya mtu flani haina tofauti na mali ya mtu ya aina nyingine, huwezi kutumia gari la mtu bila ridhaa yake” – Mngereza

Mabasi ya Kilimanjaro yazuiwa na TRA

0
0
Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesitisha utoaji wa huduma za usafiri kwa kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express Limited baada ya kushindwa kulipa kodi ya Sh500 milioni.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema wamefikia uamuzi huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na kampuni hiyo kutokuzaa matunda.

Kayombo amesema biashara ya mmiliki huyo kwa kipindi cha hivi karibuni haikuwa nzuri kwani mabasi yake 26 yalipungua hadi kufikia 12 lakini si kigezo cha kutokulipwa kwa kodi ya Serikali.

“Ni kweli Kilimanjaro Express inadaiwa Sh500 milioni jambo ambalo lilitufanya sisi kusimamisha shughuli tangu Jumatatu (ya Novemba 13) hadi hapo atakapolipa kodi anayodaiwa,” amesema Kayombo

Kwa upande wake, mmiliki wa kampuni hiyo, Roland Sawaya amesema wamezuia mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini Moshi mkoani Kilimanjaro huku akieleza kuwa ni kweli anadaiwa lakini amekuwa akilipa deni hilo kwa awamu.

Amesema hivi karubuni alilipa Sh50 milioni na mwezi huu walitaka kulipa Sh35 milioni lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiasi chote kilichobaki cha Sh500 milioni huku akieleza kwamba mazungumzo yanayoendelea ana imani yatafikia mwafaka na kurejea kutoa huduma

Kilimanjaro ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Moshi na Arusha kwa zaidi ya miaka 20 ni kampuni tanzu ya Kilimanjaro Cargo Truck.

RC Makonda Awaahidi Neema Mabaharia

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda amewasihi  Mabaharia na nahodha wa meli kushirikiana na Serikali  kuwafichua wanaoingiza mizigo ya magendo na Dawa za Kulevya kupitia ukanda wa Bahari.

RC Makonda amesema hayo leo jijini Dar es salaam kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mabaharia ambapo amesema ushirikiano huo utasaidia kudhibiti uingizwaji wa mizigo ya magendo nchini.


Amesema kazi ya ubaharia ni kazi muhimu katika kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Taifa kupitia ukanda wa Bahari hivyo Mabaharia wanapaswa kuona wanalo jukumu la kuchangia Ukuaji wa Pato la Taifa.


Aidha RC Makonda amewaahidi Mabaharia kuwa atamfikishia Rais Magufuli changamoto  walizoainisha ikiwemo ya ugumu wa upatikanaji wa Ajira kwa mabaharia wazawa ugumu wa kupata Mafunzo kwenye meli, Ajira kwenye Meli za uchimbaji Mafuta na changamoto za Kisera na Sheria.

Kwa upande wake mmoja wa Mabaharia aliesoma Risala Bwana Aloyce Mpazi amesema watazidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha ukanda wa Bahari unakuwa moja ya nyanja zinazohusika kuchochea ukuaji wa Biashara.

Ndege ya Coastal Aviation Yaanguka Ngorongoro Ikiwa na Watu 11

0
0
Mapema leo Novemba 15 katika majira ya saa 5 kwa saa za Afrika Mashariki ndege ya Shirika la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) yenye namba 5H-EGG, Cessna Grand Caravan ikiwa na abiria 10 na rubani 1 imeanguka eneo la Empakaai wakati ikiwa safarini kuelekea Serengeti.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, hakuna mtu aliyeweza kufika eneo la tukio kujua hali ya ajali hiyo kutokana na kutokea katika eneo ambalo halifikiki kirahisi.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, timu za huduma za kwanza na mtukio ya dharura wanaendelea na utaratibu wa haraka wa njia ya anga na ardhi kufika eneo hilo ili waweze kutoa msaada.

Coastal wameeleza kuwa mamlaka zote zimepewa taarifa na kwamba wataendelea kuujuza umma wa watanzania kadiri watakavyoendelea kupata taarifa.

Dr Shika Afunguka Kwa Kirefu Maisha Yake...Tazama Hii Video Mwanzo Mwisho

0
0
AKIZUNGUMZA na Global TV Online leo na matangazo hayo kurushwa  jioni hii saa 10:30, Dkt. Louis Shika ambaye amepata umaarufu mkubwa baada ya kushiriki katika mnada wa nyumba za Said Lugumi jijini Dar es Salaam na baadaye ‘kukwaruzana’ na jeshi la polisi kutokana na mchakato wa mnada huo, amefunguka engi kuhusu maisha yake.

Katika simulizi hiyo, Dkt Shika ambaye hivi sasa ni maarufu kama ‘900 Itapendeza’ kutokana na mambo yaliyojiri katika mnada huo, alianza kwa kusema kwamba neno ‘daktari’ linalotangulia jina lake ni la kitaalam, yaani kweli yeye ni daktari wa binadamu akiwa alisomea taaluma hiyo nchini Urusi.

“Nilisomea utaalam huo nchini Urusi nilikokwenda mwaka 1984 kwenda kuchukua digrii ya kwanza ya miaka saba ambayo niliimaliza mwaka 1991,” anasema daktari huyo mwenye mwili wa kiasi na kimo kirefu.

Anaendelea kusema kwamba mwaka huohuo aliamua kuunganisha masomo apate digrii ya pili ya magonjwa ya kuambukiza (infectious diseases) ambayo alimaliza mwaka 1993.

Alishindwa kuchukua digrii ya tatu (PhD) kwani sehemu alikokuwa akisomea, kusini mwa Urusi, Chechnya, palizuka vita baina ya jimbo hilo na serikali, hali iliyomlazimu kukimbilia jijini Moscow kwenda kuendelea na digrii ya tatu.
Huko alifanikisha lengo lake hilo na kuanza kufundisha katika chuo hichohicho alichokuwa akisomea hadi akapata digrii ya nne.

Wakati akiendelea na shughuli za ufundishaji, aliangua kujingiza katika ujasiriamali na hivyo kufungua kampuni aliyoipa jina la Lancefort Ltd.  Hilo lilifanyika Julai 28, 1999 alipofungua kiwanda cha zana za madawa ya kilimo na kiwandani.

Akifafanua, alisema kiwanda hicho alikinunua kutokana na kuwekeza fedha alizokuwa anazipata kwa kufundisha na zingine alizoongezwa na marafiki.
Kiwanda hicho, alisema, kilitokana na mabaki ya viwanda vilivyoshindwa kufanya kazi wakati wa Ukomunisti na hivyo serikali ikawa inaviuza kwa waliovitaka.

“Nilinunua viwanda zaidi ya kumi vya kilimo,” anasema.
Kuhusu uangalizi wa viwanda vyake vilivyoko Urusi wakati yeye akiwa hapa, Dkt. Shika alisema hilo halimpi matatizo kwani kuna watu wenye uwezo wa kuviendesha wakati yeye akiwa hapa.

Pia alimtaja kiongozi wa zamani wa Urusi, Mikhail Sergei Gorbachyov, kuwa ni mmoja wa viongozi na wasimamizi wa viwanda vyake hadi sasa, hivyo hana wasiwasi wowote akiwa huku.

Kuhusu kilichomfanya kuja nyumbani Tanzania, mzee huyo alisema  alikuja nchini Januari Mosi, 2005 baada ya kutekwa na majambazi wa Kirusi mwaka 2004 wakimataka awake  dola milioni moja na nusu za Marekani.
Akifafanua, alisema majambazi hayo yalimshikilia kwa siku 28 katika sehemu ambayo hakuifahamu baada ya kumvizia alipokuwa akikaribia nyumbani kwake na kumteka.

Mateso makubwa aliyoyapata wakati wa kutekwa huko ikiwa ni pamoja na kupigwa, kuwekewa nyaya za umeme na kadhalika, ni pamoja na kukatwa vidole viwili vya mkono wa kushoto na kimoja mkono wa kulia, vyote kwa kutumia shoka.

Pamoja na kulazimishwa aiambie benki yake itoe fedha kwa ajili yake, yote hayo hayakufanikiwa kwa vile benki walihisi kulikuwa na njama za kumshurutisha kufanya hivyo.
Hata hivyo, baada ya mateso yote hayo, alifanikiwa kutoroka kutoka sehemu hiyo majambazi wengine walipoondoka na kumuacha mwenzao ambaye alilewa pombe kali na kujidunga madawa ya kulevya.
Baada ya tukio hilo ndipo alipoamua kurejea nyumbani ambako anaendelea kuishi hadi sasa.
Simulizi hii ya kusisimua inaendelea kesho Global TV Online,hivyo usikose kuiona.

NA WALUSANGA NDAKI | GLOBAL PUBLISHERS TAZAMA VIDEO HAPA:

Updates: Watu Wote 11 Waliokuwa Katika Ndege ya Coastal Aviation iliyopata Ajali Wamefariki Dunia

0
0

TANZIA:

Watu wote (11) waliokuwa katika ndege ya Coastal Aviation iliyopata ajali leo asubuhi wamefariki dunia.


Kuhonga Sio Ticket ya Kupendwa...Wanaume Shtukeni Acheni Kujipa Moyo Mtazidi Kufa Kwa Presha

0
0
Jamani tuongee ukweli,kuhonga hakuongezi kupendwa palipo penzi la dhati. Penzi la muda mfupi au la siku moja kuhonga kutaweza kukusaidia lakini kwa mwanamke au mwanaume anayekupenda haihitaji kuhonga. hii sio kwa wanaume tu hata wanawake wanaohonga.

Kwa uzoefu wangu huu penzi la kweli halipatikani kwa kuhonga bali kuridhiana na kupendana.

Usijidanganye wala kujipotezea muda na pesa zako kuhonga kutafuta penzi la dhati utajuta bure.

Ndio Mwisho wa siku mnakuja kufa kwa Presha Shtukeni wanaume

Karibuni wadau kuongezea elimu au kuniweka sawa.

Nimemfumania Mke wa Rafiki Yangu Kipenzi Guest House Akiwaa na Njemba Jingine Waki

0
0
Katika hali nisioitegemea tumegongana ana kwa ana Gest mi na shemeji yangu wa karibu ambae mme wake tunafanya kazi pamoja.

Mimi nikiwa nampeleka mgeni wangu kwenye chumba alichofikia mara ghafla chumba chumba cha pili mlango ulifungulia na kikatokea kichwa tu kugeuka tukagongana ana kwa ana huyo shemeji yangu ilichukua takriban sekunde 30 kukodoleana macho na baada kutoa salam sauti ya chini mimi niliingia chumba cha mgeni wangu kumuaga na kumtakia safari njema wakati natoka huku mwili ukiwa umekufa ganzi kwa kutoamin nilichokiona kwa shemeji yangu na kutambua alienipokea zamu ya lindo saa 12 jion mke wake ana madudu niliishiwa nguvu kabisa, alikuja mhudumu wa ile Gest akaniitia chemba baadae akaja jamaa ambae sikuweza kumtambua kutokana na mazingira na kunieleza kilichotokea muda mfupi uliopita anaomba iwe niifanye kuwa siri kwanza ametokanae mbali isitoshe ni mzazi mwenzie na akanikabidhi elfu 70 ambayo mi nilikataa kuipokea huku nikimwambia kwasasa nahitaji kuwahi nyumbani mambo mengine tutawasiliana kwa simu ili kukwepa ushaidi niliondoka lakini hatua chache baadae ilipigwa simkuingalia ilikuwa ya shemeji yangu akinisihi lile suala anaomba liwe siri kwa gharama yoyote ile na nimpe muda mfupi mtu wake anafanya michakato ya hela soon nitapata kwa njia ya M-pesa.

Kubwa kwangu jamaa tumetokanae mbali sana urafiki kwetu ni zaidi ya ndugu tumesoma shule ya msingi moja tumeachana Sec. tumeingia depo pamoja na kupangiwa kituo kimoja yaani kama bahati tu hofu yangu ni kwamba asikie hii isue najua alafu sikumpa taarifa atanionaje mimi?

Mpaka sasa natambua kwamba ameoa na ana watoto wawili huyu jamaa ameniambia kwamba ni mzazi mwenzie nashindwa kuelewa na proces zote za uchumba mi nilihusika na sikuambia kama amezaa, katika nyakati tofauti nimeingiziwa kwa mpesa zaidi mil. 1.2 

Nifanyeje? 

Kutana na Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed Kutoka Bagamoyo...Ana Dawa za Kurudisha Mapenzi na Zingine Nyingi

0
0

MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

USHAURI: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images