Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Novemba 16

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Novemba 16

Mbowe: Masha Hakuwahi Kuwa na Msaada Wowote Chadema

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema aliyekuwa mwanachama wao ndugu Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote ndani ya chama chao tokea alipojiunga akitokea CCM.

Chanzo: Gazeti la Nipashe!

Mabasi ya Kilimanjaro Express Yazuiwa na TRA baada ya Kushindwa Kulipa Kodi ya TSh 500 milioni

$
0
0
Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesitisha utoaji wa huduma za usafiri kwa kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express Limited baada ya kushindwa kulipa kodi ya Sh500 milioni.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo ameliambia gazeti la Mwananchi leo kuwa, wamefikia uamuzi huo baada ya majadiliano ya muda mrefu na kampuni hiyo kutokuzaa matunda.

Kayombo amesema biashara kwa kipindi cha hivi karibuni haikuwa nzuri kwani mabasi yake 26 yalipungua hadi kufikia 12 lakini si kigezo cha kutokulipwa kwa kodi ya Serikali.

“Ni kweli Kilimanjaro Express inadaiwa Sh500 milioni jambo ambalo lilitufanya sisi kusimamisha shughuli tangu Jumatatu (ya Novemba 13) hadi hapo atakapolipa kodi anayodaiwa,” amesema Kayombo

Kwa upande wake, mmiliki wa kampuni hiyo, Roland Sawaya amesema wamezuia mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini Moshi mkoani Kilimanjaro huku akieleza kuwa ni kweli anadaiwa lakini amekuwa akilipa deni hilo kwa awamu.

Amesema hivi karubuni alilipa Sh50 milioni na mwezi huu walitaka kulipa Sh35 milioni lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiasi chote kilichobaki cha Sh500 milioni huku akieleza kwamba mazungumzo yanayoendelea ana imani yatafikia mwafaka na kurejea kutoa huduma.

Chanzo: Mwananchi

Serikali yazipinga Kanuni za SUMATRA....

$
0
0
Serikali imefikia uamzi wa kusitisha kuanza kutumika kwa kanuni za leseni ya usafirishaji na kukiri kuwepo kwa mapungufu ya wazi ambayo yanahitaji marekebisho ili kuondoa kasoro zinazoweza kumuonea mmiliki wa chombo husika.

Uamzi huo umefikiwa leo kwenye mkutano wa wamiliki wa vyombo vya usafiri na Naibu waziri wa Uchukuzi na mawasiliano Atashasta Nditiye ambao kwa pamoja wamekubaliana kusitisha kuanza kutumika kwa kanuni hizo ili kuzipitia upya na kuondoa mapungufu.
Moja ya mapungufu ambayo Naibu waziri amekiri kwamba yapo kwenye kanuni hizo ni pamoja na kanuni ambayo inaeleza mmiliki wa gari kutozwa faini ya hadi ya shilingi laki mbili na nusu kwa makosa ya dereva.

Aidha Nditiye amedai kuwa ni kweli kanuni hizo zilizotolewa na mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA, zingeleta changamoto katika uendeshaji wa vyombo vya moto. Waziri Nditiye ameagiza kufanyika marekebisho ya kanuni hizo hadi kufikia Desemba 1 mwaka 2017.
Kanuni hizo zilipaswa kuanza kutumika hivi karibuni hali ambayo ilipelekea wamiliki wa vyombo vya usafiri kutangaza azima ya kuitisha mgomo kwa madai ya kutosikilizwa kila mara wanapotoa maoni yao juu ya kanuni hizo za usafirishaji.

Soma Nafasi za Ajira Zilizo Tangazwa Leo

$
0
0

Nyumba Anayoishi kwa Sasa Gigy Money Yazua Gumzo

$
0
0
Nyumba Anayoishi Sasa Gigy Money Yazua Gumzo
Msanii Gigy Money ambaye hivi karibuni amezua gumzo na kushangaza watu baada ya kuona mahali anapoishi, amesema ni kweli sehemu ambayo anaishi kwa sasa hapafanani na yale anayoyafanya, lakini hata hivyo hajutii hilo.

Akiongea kwenye 5SELEKT ya East Africa Television, Gigy Money amesema nyumba ambayo imeonekana anaishi sasa amehamia hivi karibuni baada ya nyumba aliyokuwa anaishi awali kujaa maji na kusomba vitu vyake, kutokana na mvua zilizoleta mafuriko hivi karibuni.
Gigy Money ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha mafuriko kusomba vitu vyake kimempa 'stress' kwani imemlazimu kuanza moja kwenye maisha, pamoja na kutafuta nyumba yoyote ile ili aanze maisha upya.
“Unajua nimetoka kwenye mafuriko, nyumba niliyokuwa naishi mwanzo maji yalijaa yakasomba vitu vyangu vyote, stress niliyonayo mimi mwenyewe ndo najua, yani naanza maisha moja ndio nikatafuta nyumba nikapata hapa, pale ninapokaa hata sistahili kukaa pale ndio naanza moja na mimi binadamu”, amesema Gigy Money.
Hivi karibuni kumeibuka minong'ono kwa baadhi ya watu wakionesha kushangazwa na kitendo cha Gigy Money kuishi kwenye nyumba ambayo haieleweki wakati mitandaoni anajitapa kuvaa vitu vya gharama kubwa zaidi.

Tajiri Salaah Amkana Irene Uwoya

$
0
0
Tajiri Salaah Amkana Irene Uwoya
Tajiri mmoja maarufu jijini Dar, anayefahamika zaidi kwa jina moja la Salaah, amemkana muigizaji Irene Uwoya ambaye amekuwa akijinasibu kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mpenzi wake.

Kumekuwa na habari zinazozagaa mitaani kuwa Uwoya, mke wa zamani wa mwanasoka Hamad Ndikumana, ndiye anayekula maisha na mfanyabiashara huyo na kuthibitisha hivyo, muigizaji huyo ambaye yupo levo ya daraja la juu (A List Female Artist) siku chache zilizopita alionekana katika kipande cha video katika mtandao mmoja akiwa amejichora tattoo yenye jina la mvulana huyo.

“Habari kubwa mjini ni kuhusu Uwoya, inasemekana jamaa amekufa ameoza kwa shostito na mwanamke jinsi anavyojua kuweka sawa mambo kachora hadi tattoo mgongoni mwake yenye jina lake,” kilisema chanzo chetu ambacho ni miongoni mwa wasiri wa muigizaji huyo.

Risasi lilijaribu mara kadhaa kumfikia kwa njia ya simu Uwoya bila mafanikio, kwani mara zote simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu, hakujibu lolote. Salaah ambaye anadaiwa kuwa kijana mwenye fedha na anayefahamika sana miongoni mwa mastaa kutokana na ukwasi mkubwa alionao, alizungumza na Risasi Mchanganyiko akiwa nje ya nchi na kudai hajui chochote kinachozungumza juu yake na msichana huyo. “Sikiliza, mimi hayo mambo unayozungumza siyajui na wala huyo unayemtaja simjui, ndiyo kwanza nakusikia wewe, tafadhali usinihusishe na hayo mambo mimi siyajui,” alisema kwa kifupi.

Majonzi Yatanda Rwanda Mazishi ya Ndikumana

$
0
0
Majonzi Yatanda Rwanda Msiba wa Ndikumana
Wananchi wa Rwanda pamoja na wapenzi wa soka wa Afrika Mashiriki siku ya jana walipokea kwa mshituko mkubwa kifo cha ghafla cha aliyekuwa kapteni wa timu ya Taifa ya Rwanda, Hamad Ndikumana ambaye pia alikuwa ni mume wa muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya.


Baba wa Marehemu
Mwili wa Ndikumana ukiwa umebebwa na wachezaji wa Rayon Sports, ukipelekwa msikitini kwaajili ya dua ya mwisho

Umati mkubwa watu ulijitokeza katika msikiti wa Qaddafi huko Nyamirambo Rwanda kwaajili ya kumuaga mwanasoka huyo mkongwe. Angalia picha.


Mama yake marehemu Ndikumana akilia kwa uchungu.

Ndikumana anadaiwa kufariki muda mchache baada ya kutoka mazoezi akiwa kama kocha wa timu ya Rayon Sports.


Afisa wa Soka Ajiua Baada ya Kuhusishwa Katika Kashfa ya Rushwa na FIFA

$
0
0
Afisa wa Soka Ajiua Baada ya Kuhusishwa Katika Kashfa ya Rushwa na FIFA
Afisa wa zamani wa soka nchini Argentina amejiua baada ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa iliyotajwa mjini New York.

Jorge Delhon amejirusha kwenye reli na kukanyagwa na treni kwenye mji mkuu wa Argentina Buenos Aires.

Baadhi ya viongozi wa soka nchini Argentina wameelezea kusikitishwa na tukio hilo na kusema limetia doa kwenye soka la nchi yao.

Kesi ya Delhon iliyofunguliwa siku ya Jumatatu inafuatia upelelezi wa muda mrefu uliofanywa na Marekani kwenye shirikisho la soka duniani FIFA.

AU: Hatua ya Jeshi la Zimbabwe ni Kama Mapinduzi

$
0
0
AU: Hatua ya Jeshi la Zimbabwe ni Kama Mapinduzi
Hatua ya jeshi la Zimbabwe ya kuchukua madaraka na kumzuilia Rais Robert Mugabe, inaonekana kama mapinduzi wa kijeshi, Muungano wa Afrika AU umesema.
Mkuu wake, Alpha Conde, alisema kuwa AU inataka kurejea mara moja hali ya kawaida.
Jeshi linakana kufanya mapinduzi ya kijeshi, na kusema kuwa Mugabe yuko salama, na kuwa hatua zao ni dhidi ya waalifu wanaomzunguka.
Hatua ya jeshi inafuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi Bw. Mugabe.
Makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa alifutwa kazi wiki iliyopita, na kuchangia mke wa rais Grace kuwa na fursa wa kumrithi Mugabe, hali iliyosababisha maafisa wa vyeo vya juu jeshini kuhisi kutengwa.

Bwana Mugabe 93, ametawala siasa za nchi tangu ipate uhuru kutoka Uinghereza mwaka 1980.
Akijibu yale yaliyotokea Bw. Conde ambaye pia ni rais wa Guinea, alisema kuwa wanajeshi wa Zimbabwe walikuwa wamejaribu kuchukua madaraka.
Mwandishi wa BBC aliye nchini Zimbabwe anasema kuwa Misri ilifukuzwa kutoka AU wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013, kwa hivyo jeshi la Zimbabwe linaweza kuwa linajaribu kuzuia hali kama hiyo kw kutaja hatua yao kuw isiyo mapinduzi ya kijeshi.

Kilichotokea kwa Mugabe ni Jambo Jipya Kutokea Katika Kipindi Hiki cha Demokrasia- Msekwa

$
0
0
Kilichotokea kwa Mugabe ni Jambo Jipya Kutokea Katika Kipindi Hiki cha Demokrasia- Msekwa
Sintofahamu iliyotokea Zimbabwe baada ya jeshi la nchi hiyo kutanda jijini Harare na kumuweka chini ya uangalizi Rais Robert Mugabe imeelezwa ni jambo jipya ambalo halijawahi kutokea.

Baada ya taarifa kusambaa kuwa jeshi linaidhibiti nchi hiyo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini mbali ya kueleza kuwa ni jipya, pia wameeleza kuwa ung’ang’anizi wa madaraka ni tatizo.

Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu kilichotokea Zimbabwe, makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa alisema ni jambo jipya kuwahi kutokea katika kipindi hiki ambacho nchi nyingi za Afrika zinafuata mfumo wa demokrasia wa kuchagua viongozi kupitia vyama.

Msekwa, ambaye pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge alisema anasita kuita mapinduzi kutokana na kilichotokea Zimbabwe kwa kuwa mapinduzi ya kijeshi huhusisha kuitoa Serikali iliyopo madarakani kisha jeshi kushika hatamu, jambo ambalo kwa nchi hiyo wanajeshi wametangaza kuwa hawako tayari kukamata madaraka.

“Katika kumbukumbu zangu sikumbuki kama hili jambo limewahi kutokea tangu miaka ya 60, kuna tofauti kubwa sana kuita haya ni mapinduzi ya kijeshi. Ni mapinduzi kwa sababu Serikali iliyokuwepo imetolewa lakini jeshi limesema halina nia ya kuchukua madaraka, ni jambo jipya sana kwangu ndiyo maana nasita kuita ni mapinduzi ya kijeshi,” alisema.

Hata hivyo, kada huyo wa chama tawala alisema kila jambo lina mwanzo wake pengine na hilo limekuja kwa makusudi ili watu wajifunze.

Msekwa alilipongeza jeshi hilo kwa kuhakikisha wanafanya mambo hayo kwa amani bila kumwaga damu.

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Profesa Gaudence Mpangala alisema jambo lililofanyika nchini humo ni matokeo ya ung’ang’anizi wa madaraka, ingawa nyuma Mugabe alisukumwa na chama kilichokuwa kikitaka kiendeee kutawala milele. “Sasa tupo katika utawala wa kijamhuri unaotaka kuwe na uchaguzi huru, ukimuangalia Mugabe alishafika umri wa zaidi ya miaka 90 na bado alikuwa anang’ang’ania madaraka ndiyo maana amepata aibu,” alisema.

Profesa Mpangala alisema Mugabe angejiwekea heshima kubwa kama angekubali kung’atuka mapema na kuandaa vijana ambao wangemrithi na siyo mpaka kusubiri jeshi ‘limpindue’.

Alisema tukio hilo ni funzo kubwa kwa nchi mbalimbali kwa kuwa si kiongozi pekee anayeng’ang’ania madaraka anachokwa, lakini pia chama kiking’ang’ania nacho kinajiweka katika wakati mgumu.

“Ni lazima kuwe na mfumo wa kubadilishana madaraka, hiyo ndiyo demokrasia unayotaka na ni lazima Serikali iweke mazingira ya ushindani sawa kwa vyama vyote vya upinzani,” alisisitiza Profesa Mpangala.

Akizungumzia suala hilo, mratibu wa Mtandao wa Wapigania Haki za Binadamu, Onesmo Ole Ngurumwa alisema Rais Mugabe amejitengenezea mwenyewe mazingira hayo.

“Kilichotokea ni matokeo ya kutoheshimu demokrasia, alikuwa na muda wa kutoka kwa heshima na kuandaa watakaomrithi lakini ameshindwa hilo na matokeo yake akafanya chama ni mali ya familia,” alisema.

Ole Ngurumwa alipongeza hatua hiyo na kusema kuwa ilifika wakati wake na kuwa wananchi walishachoshwa na kiongozi huyo ambaye alianza kuongoza mara tu baada ya uhuru wa nchi hiyo kupatikana kutoka kwa wakoloni wa Uingereza.

Hata hivyo, Ole Ngurumwa alilipongeza jeshi hilo kwa kitendo chake cha kutomwaga damu na kusababisha maafa kwa wananchi.

“Wakati mwingine tunashuhudia damu ikimwagika bila sababu za msingi, tunashukuru jeshi la Zimbabwe limefuata njia bora ya demokrasia ambayo haimwagi damu na kuheshimu watu,” alisisitiza Ole Ngurumwa.

Wezi Wachimba Njia ya Chini kwa Chini na Kuiba Pesa Kwenye Benki India

$
0
0
Wezi Wachimba Njia ya Chini kwa Chini na Kuiba Pesa Kwenye Benki India
Wezi katika mji wa Mumbai magharibi mwa India walitekeleza wizi kwenye benki moja inayomilikiwa na serikali baada ya kuchimba njia ya chini kwa chini ya urefu wa futi 25 (mita 8).
Walichimba njia hiyo kwa miezi kadha.
Polisi wameambia BBC kwamba pesa taslimu pamoja na vito vya thamani isiyojulikana viliibiwa.
Maafisa wanaamini kwamba wezi hao walikodisha chumba karibu na Benki ya Baroda kuwawezesha kuchimba njia hiyo.
Wanadaiwa kuendesha biashara ya kuuza mboga na matunda katika kiduka chao kuficha mipango yao.
Wezi hao walitoweka tangu Jumamosi usiku baada ya kutokea kwa wizi huo.
Haijabainika ni vipi wanaume hao walifanikiwa kuchimba njia hiyo kwa miezi kadha bila kugunduliwa.
Vyombo vya habari nchini India vimezungumza na wateja wa benki hiyo ambao vitu vyao vya thamani viliibiwa.
"Akiba yangu yote ilikuwa imewekwa kwenye sefu. Vito ambavyo tumemiliki kwa vizazi kadha, vimeibiwa," Dagdu Gavani, mmoja wa wateja aliambia Mumbai Mirror.
Wafanyakazi wa benki hiyo iliyo viungani mwa mji wa Mumbai waligundua wizi huo Jumatatu na kuwafahamisha polisi.
Polisi wameambia BBC kwamba sefu 30 kati ya 225 kwenye benki hiyo ziliporwa.
Washukiwa bado hawajatambuliwa.

Tangaza Biashara Yako Hapa

$
0
0

Mtu wangu wa nguvu unaweza Tangaza Biashara yako hapa nasi uweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa mara moja kupitia blog ya Udaku Special..

Piga simu 0714604974

Alivyoingia Grace Kwenye Ndoa Ya Robert Mugabe Na Sally..

$
0
0

Alivyoingia Grace Kwenye Ndoa Ya Robert Na Sally...

Ndugu zangu,

Grace Mugabe anatajwa kuwa ni moja ya chanzo cha anguko la Mugabe kisiasa. Inahusu mamlaka na mahaba.

Na huenda si wengi wenye kujua mahusiano ya kimapenzi ya Robert na Sally ya miaka hiyo ya nyuma yaliyopelekea ndoa na hata wakapata mtoto mmoja aliyekuja kufa kwa malaria akiwa na miaka mitatu tu.

Naam, ametokea wapi huyu Robert Mugabe, mwana wa pili kati ya wana watatu wa baba yake, fundiseremala wa kijijini, Mzee Mugabe?

Robert aliyezaliwa mwaka 1924 utotoni alikuwa mtulivu sana. Ndoto yake ilikuwa ama aje kuwa Mchungaji au Mwalimu wa shule.

Robert alishuhudia kaka yake Michael kwenye umri wa miaka 15, akifa kwa kula sumu ya majani wakiwa pamoja porini. Robert akabaki na mdogo wake tu.

Baba yake akaja kuitelekeza familia yao na Robert na mdogo wake wakalelewa na mama yao .

Hatimaye Robert akaja kuwa mwalimu kwenye shule ya msingi ya kijijini. Robert tangu utotoni amekuwa ni mwenye bidii ya masomo. Kwa sasa ni mwenye digrii saba na tatu kati ya hizo amezipata akiwa gerezani, mojawapo ni ya sheria.

Alivyoingia Sally kwenye maisha ya Robert..

Robert alikutana na Sally alipokuwa akisoma Ghana. Walipendana na wakaoana mwaka 1961. Sally ni raia wa Ghana.

Waliamua kuishi wote Salisbury ( Sasa Harare). Robert akaingia matatani kisiasa na kufungwa mwaka 1964 kwa miaka kumi.

Mwaka mmoja kabla ya kifungo, walimzaa mwana wao pekee, Nhamodzenyika ikiwa na maana ya nchi inayoteseka. Kwa kifupi walimwita Nhamo.

Sally ambaye alikuwa mcheshi na msomi alichangia sana kumjenga Robert hata kumsaidia kupata marafiki wa kuongea, maana, Robert ujanani alikuwa ni mkimya sana na asiyependa kujichanganya na watu.

Akiwa gerezani Zimbabwe, Sally alilazimika kukimbia Zimbabwe na kwenda kuishi kwao Ghana. Mwana wao Nhamo alifariki kwa malaria akiwa na miaka mitatu tu. Robert aliomba ruhusa ya bwana gereza ili akamzike mwanawe Ghana alikoishi Sally. Alikataliwa. Jambo hilo lilimhuzunisha sana Robert.

Mwaka 1974 Sally aliungana tena na Robert aliyetoka gerezani. Walikutana kwenye uwanja wa mapambano ya ukombozi Msumbiji.

Sally baada ya Uhuru wa Zimbabwe 1980, aliishi na mumewe Ikulu ya Harare. Sally alipendwa sana na Wazimbabwe. Wakazoea kumwita ' amai' ikiwa na maana ya mama yetu. Hata hii leo, Sally Mugabe anaonwa kama ' Mama wa Taifa' la Zimbabwe.

Alivyoingia Grace kwenye maisha ya Robert..

Grace Mafuru, msichana aliyeonekana mrembo aliyezaliwa Afrika Kusini, alifanya kazi ya Ukatibu Mukhtasi kwenye Ikulu ya Robert Mugabe. Ndipo hapo mahusiano ya kimapenzi kati ya Robert na Grace yakaanza huku Robert akiwa kwenye ndoa na Sally lakini wakiwa wapweke bila hata mtoto baada ya mwana wao Nhamo kufariki.

Grace akapata ujauzito wa Robert, 1988. Haikufanywa siri, Sally akajulishwa na akakubali hali hiyo mpya.

Mwaka 1992 Sally Mugabe alifariki kwa kuugua homa ya mapafu. Mwaka 1996 Robert na Grace wakafunga ndoa. Grace Mafuru akawa Grace Mugabe, First Lady.

Kuna ya kutafakari juu ya uongozi na mahusiano ya kimahaba. Wengi wanafikiri, kama angelikuwepo, kuwa Sally Mugabe angeliweza kumsaidia zaidi Robert Mugabe kiungozi na pengine Robert Mugabe asingefikia hatua ya kung'ang'ania madaraka.

Kuna mengi ya kusimulia juu ya mahusiano ya Sally na Robert na namna sally alivyomsaidia kumjenga Robert kisiasa katika ujana wao.

Kuna ya kusimulia pia, namna Grace alivyochangia kwenye anguko la Robert kisiasa.

Maggid Mjengwa,

0688 37 36 52 ( Whatsapp)

Breaking News: Mhasibu Mkuu wa Takukuru Alifikishwa Mahakamani

$
0
0
Breaking News: Mhasibu Mkuu wa Takukuru Alifikishwa Mahakamani
MHASIBU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai,  anayedaiwa kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.

Gugai amefikishwa katika mahakama hiyo baada ya taarifa iliyotolewa siku chache zilizopita na Naibu Kamishna wa Takukuru, Brigedia John Mbungo,  kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa ametoroka.  Mtuhumiwa huyo anatajwa kumiliki majumba na viwanja karibu kila mkoa nchini.

Breaking News:Boti ya Mv Julius Yazama Ziwa Victoria Watu 17 Waokolewa

$
0
0
Breaking News:Boti ya Mv Julius Yazama Ziwa Victoria Watu 17 Waokolewa
Watu 17 wameokolewa baada ya boti ya MV Julius kuzama katika ziwa Victoria.Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kubaini kama kuna waliosahaulika majini.

Hizi ni taarifa za awali fuatilia Habari zetu kufahamu zaidi.

Muda Mwingi Nalipwa kwa Kufanya Kiki -Gigy Money

$
0
0
Muda Mwingi Nalipwa kwa Kufanya Kiki -Gigy Money
Msanii wa muziki Bongo, Gigy Money amesema mara nyingi huwa analipwa ili kufanya kiki.

Gigy ambaye anatamba na ngoma ‘Papa’ amekiambia kipindi cha 5 Selekt, EATV kuwa kutokana na hilo kiki ni kitu ambacho kwake hakitaisha hadi kufa.

“Huwezi amini muda mwingi nalipwa kwa ajili ya kiki, mtu anakulipa kabisa nataka kujulikana anakutia kama ni laki tano mimi nafanya naye. Mimi hazikatakaa kuisha mpaka naingia kaburini, mimi mpaka siku nakufa ni kiki” amesema Gigy Money.

Katika hatua ngingine Gigy Money amesema watu wengi wanaamini pengine yeye ni mwanamke anayejiuza lakini ukweli ni kwamba yeye anapambana na maisha yake

Lawrence Masha Hakuwa na Msaada Wowote Ndani ya Chadema- Mbowe

$
0
0
Lawrence Masha Hakuwa na Msaada Wowote Ndani ya Chadema- Mbowe
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.

Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.

“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe

\Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola

Ndugai Awaamshia Duse Mawaziri "Waheshimiwa Acheni Kupiga Story Bungeni Wasikilizeni Wabunge"

$
0
0
Ndugai Awaamshia Duse Mawaziri "Waheshimiwa Acheni Kupiga Story Bungeni Wasikilizeni Wabunge"
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka mawaziri waache kupiga stori bungeni na kusikiliza wabunge wanapouliza maswali.

Ndugai ametoa agizo hilo leo Alhamisi asubuhi wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni.

“Kipindi cha maswali waheshimiwa mawaziri acheni kupiga stori… waheshimiwa mawaziri hamsikilizi,’’ amesema Ndugai

Kauli ya Ndugai imekuja baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Mwantumu Dau Haji kuuliza swali la nyongeza kuhusu kilimo cha umwagiliaji alilolielekeza kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.

Wakati akiruhusu naibu waziri kujibu swali hilo, Spika amesema kuwa swali hilo lilipaswa kujibiwa na wizara ya maji hivyo kumtaka naibu waziri wa wizara hiyo kujibu.

“Hilo swali lilitakiwa liende Wizara ya Maji, Naibu Waziri Maji, Mh Aweso (Jumaa),” Ndugai alimtaka Naibu Waziri wa Maji kujibu swali na kuongeza kuwa, “ndo shida mnakuwa mnaongea, hamsikilizi humu ndani, jibu swali.”

Baada ya hapo, Spika alimwambia Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, Kangi Lugola kujibu swali hilo. “Mh Kangi Lugola okoa jahazi’ alisema Ndugai ambaye alikuwa akiwasisitiza mawaziri kuwa makini kusikiliza.

Pia, Spika amewataka baadhi ya mawariri kujiandaa kutoa majibu mafupi katika maswali yanayohusu wizara zao, “Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Afya, Wizara ya Maji kwa majibu yanayokuja na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa majibu yanayokuja, ni marefu sana mawaziri wawe wanatoa majibu kwa ufupi,” amesema

Wazimbabwe Wasubiria Hatua za Jeshi

$
0
0
Wazimbabwe Wasubiria Hatua za Jeshi
Watu nchini Zimbabwe wanasubiri kuona hatua ambazo jeshi litachukua baada ya kutwaa madaraka ya nchi hiyo.
Rais Robert Mugabe yuko katika kizuizi cha nyumbani mjini Harare lakini ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa mke wake Grace ambaye alikuwa anataka kumrithi akimekimbia kwenda Namibia
Hatua za kijeshi zilifuatia kufutwa kwa Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambayr ni hasimu mkubwa wa Bi Grace Mugabe.
Mahala alipo Mnangagwa pia hapajulikani.
Lakini mzozo kuhusu ni nani anaweza kumrithi Mugabe kati ya Bi Grace Mugabe na Bwa Mnangagwa umekigawanya chama cha Zanu-PF miezi ya hivi karibuni.
Nchi za Jumuia ya maendeo ya kusini mwa Afrika (SADC) zinatarajiwa kufanya mkutano wa dharura nchini Botswana leo Alhamisi.

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Tendai Biti, aliiambia BBC kuwa anataka kuona serikali ya mpito madarakani.
Siku ya Jumatano wanajeshi wakiwa na magari ya jeshi walilizinga bunge na majengo mengine makuu ya serikali.
Saa kadha baadaye walichukua udhibiti wa makao ya kituo cha habari cha serikali ZBC na kutangaza kuwa walikuwa wanawalenga waalifu wanamzunguka Rais Mugabe.
Hata hivyo meja Jenerali Sibusiso Moyo alikana kuwa hakkukuwa na mapinduzi wa kijeshi.
Alisema kuwa Mugabe na familia yake walikuwa salama
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images