Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Kunuka Kikwapa na Weusi Katikati ya Mapaja Yangu Vinaninyima Raha

$
0
0
Naomba niombe msaada kwenu wadau,nina matatizo sijui niseme shida  ambazo kiukweli zinanikosesha raha,nimekua nikihangaika sana kutafuta dawa ya kumaliza harufu ya kikwapa,yaani ni kwamba nimejaribu kila aina ya deodorant,na perfumes za kila aina lakini harufu haiishi,itokee bahati mbaya nisahau kupata Deodorant jamani sio siri najisikia hata mimi mwenyewe jinsi ninavyotoa harufu kali,zaidi ya harufu makwapa yangu ni meusi,ajabu,niliambiwa deodorant za Forever Living zinasaidia kumaliza weusi makwapani lakini wapi sioni tofauti,nawaombeni mnisaidie jamani nakosa raha,kifupi harufu utadhani lile jasho wanalonuka wanaume,wakati mwingine nafikia hata kujinyanyapaa mwenyewe,kwa kutokwenda kwenye shuhuli,nahisi wenzangu wananisema,shida inakuja muda wa kazi,kwani siwezi kukwepa kwenda ofisini,kiukweli it is so embarrassing.

La pili,huohuo weusi,katikati ya mapaja nako hakufai,yaani nikipanua miguu utadhani nimesilibwa lami hapo kati,nimejaribu kutumia mikorogo,haikusaidia,cream zile za hospitali za ngozi,pia nimejaribu,angalau kidogo utaona natakata,tatizo lake baada ya muda yanatoka mapele kama vijipu nashindwa hata kutembea shauri ya friction,nilipata ushauri wa kuvaa skin tight ili kuepusha friction,lakini lile la weusi lipo palepale,wenzangu nawaomba,kama kuna mtu alishawahi pata  matatizo kama yangu,naomba msaada tutani,jamani siyo siri,pamoja na kutaka nionekane maridadi,lakini pia wakati wa majambos si mwajua kuna muda wa mahabuba kwenda down,sasa inapofikia hapo,dah,najisikia aibu kwa maana naona kama vile najichoresha,na jamaa yangu huwa hakubali bila kunipagawisha kwa njia hiyo,sasa nipo na wakati mgumu
.
Huwa napendelea sana kusoma story kila wikiendi ila wamama/wadada saa nyingine mna maneno makali ambayo yanatukatisha tamaa kuomba ushauri humu,nawaombeni jamani,wengine hatuna pa kusemea wala wa kutupa ushauri wa kweli,tusaidiane jamani,Samahani kama nimewakwaza

Serikali Yamtilia Shaka Dr Shika...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 18

$
0
0


Serikali Yamtilia Shaka Dr Shika...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Novemba 18

Ufafanuzi Kuhusu Sheria Mpya Ya Ttcl Kwa Vyombo Vya Habari

$
0
0
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) iliyotolewa kwenye magazeti ya Mwananchi na Uhuru ya tarehe 15/11/2017. Gazeti la Mwananchi liliandika, “Serikali ‘yaiua’ rasmi TTCL na gazeti la Uhuru liliandika,“TTCL ‘bye’ ‘bye’. Vichwa hivi vya habari vimewachanganya wasomaji na kuleta taharuki kwa wateja na wafanyakazi wa TTCL, wadau wa Sekta ya Mawasiliano na wananchi kwa ujumla.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewasilisha Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania katika mkutano wa Tisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 14 Novemba, 2017 mjini Dodoma. Bunge lilijadili na kupitisha Muswada na kutungwa kuwa Sheria itakayoanzisha Shirika la Mawasiliano Tanzania. Madhumuni ya Muswada yalikuwa ni kuanzisha Shirika la Umma la Mawasiliano nchini kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, kukuza uchumi na kutoa huduma za mawasiliano kwa ubora unaotakiwa. Pia, kulipa Shirika la Mawasiliano jukumu la kusimamia miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano nchini.

Sheria mpya itaiwezesha TTCL kutekeleza majukumu yake kama Shirika la Mawasiliano nchini. Hizi ni jitihada za Serikali kuimarisha TTCL na sio kuiua. TTCL bado ipo na itaendelea kutekeleza majukumu yake kama Shirika la Mawailiano nchini. Shirika litaendelea kutoa huduma kwa wananchi kwa ubora na ufanisi zaidi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
17 Novemba, 2017

Heche Amshukuru Spika Kwa Kumlinda Asikamatwe

$
0
0
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amekiri bila busara za Spika wa Bunge kutumika leo angekuwa amekamatwa leo na polisi wamedaiwa kutoka Morogoro waliokuwa eneo la Bunge kwa nia ya kumkamata.

Mh. Heche amweka hilo wazi jioni hii huku akikosoa matumizi mabaya ya rasilimali iliyotumiwa.

"Nimepokea barua ya polisi asubuhi leo wakinitaka kuripoti Morogoro eti kwa kosa la kumsindikiza na kufanya mkutano jimboni kwa Mh Lijualikali alipotoka gerezani mwezi wa 4" Amesema Heche na kuongeza;

"Kabla hata ya kuitikia wanataka kunikamata bila busara za spika wangenikata. Matumizi mabovu ya rasilimali"

Kabla ya taarifa hii kutoka Mapema leo Heche alikiri kupokea wito unaomtaka kwenda kuhojiwa Morogoro.

"Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.

Dkt Cheni Aweka Wazi Tetesi za Lulu Kugomea Rufaa

$
0
0
Dkt Cheni Aweka Wazi Tetesi za Lulu Kugomea Rufaa
Muigizaji wa muda mrefu nchini, Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni, amefunguka kuhusu tetesi zilizozagaa mitandaoni, zikimhusisha kuhusu kugomea rufaa kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Katika posti za watu mbalimbali mitandaoni, waliandika kuwa Dr Cheki alisema Lulu ambaye ameanza maisha ya gerezani, alikataa ndugu zake wasikate rufaa kwa kile alichosema, anataka kumaliza kifungo chake mapema ili awe huru kisaikolojia. Lakini juzi, Dk Cheni ambaye alikuwa staa pekee aliyekuwa akihudhuria mahakamani wakati kesi hiyo ikifanyika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alikanusha kuzungumza na Lulu, kwani hata siku ya hukumu hakuwepo kortini.

“Siyo kweli, mimi sijazungumza na Lulu tangu siku ile ya hukumu, kwanza sikuwepo mahakamani na hadi leo ninapoongea na wewe sijaenda kumtembelea gerezani, kwa hiyo hayo maneno siyo yangu,” alisema muigizaji huyo. Novemba 13, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilimhukumu Lulu miaka miwili jela, baada ya kumkuta na hatia ya kuua bila kukusudia, kosa alilolifanya April 7, 2012 baada ya kuwa ndiye mtu wa mwisho kuwa chumbani na muigizaji mwenzake, marehemu Steven Kanumba aliyefariki siku hiyo

Rais Mstaafu Jk Awapa Ushauri Huu Wasanii

$
0
0
Rais Mstaafu Jk Awapa Ushauri Huu Wasanii
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mabye pia ni kipenzi cha wasanii, Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka wasanii kufanya kazi zenye ubora zaidi ili kuweza kushindana na soko la kimataifa, la sivyo watabaki hapa hapa bongo.

Jakaya Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye ghfala ya uzinduzi wa Television Mpya ya Jason ambayo itakuwa inaonyesha filamu za kitanzania, na kusema kwamba ni wakati muafaka sasa kwa wasanii kuacha kulia lia kutaka serikali iwape msadaa, na badala yake wafanye kazi zenye ubora zaidi.
“Kama anavyosema Waziri isiwe sasa scene' ni hizo hizo tu, msilalamike tulindeni, mtabaki kibongo bongo tu, nyinyi mkitaka mtoke lazima muende beyond bongo, lazima muwe na product nzuri, na product nzuri mnaipata mkiacha ushindani, muhimu ni kusaidiwa mshindane vizuri, basi”, amesema Jakaya Kikwete.
Pamoja na hayo Jakaya Kiwete amesema amefurahishwa na muenendo wa tasnia ya sanaa ya filamu, ambayo kwa sasa imetoa ajira kwa watu milioni 6.

Mapokezi ya Odinga Yasababisha Vifo Vitano Nairobi

$
0
0
Mapokezi ya Odinga Yasababisha Vifo Vitano Nairobi
Imeripotiwa kuwa takriban watu watano wamepoteza maisha jijini Nairobi nchini Kenya na wengine kujeruhiwa wakati polisi nchini humo ikikabiliana na wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Maelfu ya wafuasi wa upinzani leo walikusanyika katika uwanja wa ndege kumpokea Raila Odinga ambaye alikuwa anarejea kutoka nchini Marekani.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo, George Kinoti amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kuwa vimetokana na mkanyagano wa Wafuasi hao na sio nguvu ya polisi kama inavyoelezwa.

Taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la Reuters zimeeleza kuwa Polisi walirusha mabomu ya machozi na vilipuzi kuwatawanya wafuasi hao huku gari moja la polisi likichomwa moto.

Raila Odinga alisusia kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 26 huku akitaka uchaguzi huo kuahirishwa kwa mara ya tatu lakini Tume ya Uchaguzi nchini humo ilikataa kufanya hivyo.

Jumatatau ijayo Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uhalali wa uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba ambao rais Uhuru Kenyatta alibuka mshindi.

Serikali Yajipanga Upya Mapambano ya Dawa za Kulevya Yawasilisha Mswada Bungeni

$
0
0
Serikali Yajipanga Upya Mapambano ya Dawa za Kulevya Yawasilisha Mswada Bungeni
Serikali imewasilisha bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na imeweka vifungu vikali vya kukabiliana na biashara ya dawa za kuelevya nchini.

Katika mabadiliko hayo ya sheria maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya sasa wataruhusiwa kumiliki silaha na kutumia silaha za moto inapobidi.

Katika muswada huo, Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Masuala ya Ukimwi imetaka wakati wa kutunga kanuni za sheria hiyo, Serikali iingize pombe aina ya viroba katika orodha ya dawa za kulevya.

Akiwasilisha muswada huo, waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenister Mhagama alisema mabadiliko hayo yataongeza ukali wa vita dhidi ya biashara hiyo.

Akizungumzia maofisa wa mamlaka kumiliki silaha, Mhagama alisema nguvu ya kifedha ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya inawafanya wamiliki silaha na kujiwekea kinga ya ulinzi.

“Hii inafanya mazingira ya kiutendaji kuwa hatarishi wakati wa ukamataji. Kwa sasa mamlaka inatumia polisi kwa ajili ya ulinzi wakati wa kufanya operesheni zake za ukamataji watuhumiwa,” alisema.

Mhagama alisema kuna wakati taarifa hupatikana usiku na kuhitaji utekelezaji wa haraka, hali ambayo hulazimu maofisa wa mamlaka kujitoa muhanga na kuhatarisha usalama wao au kuahirisha.

Chini ya mabadiliko hayo, mtu atakayemsafirisha mtu mwingine nje ya nchi kwa minajili ya kuwekwa rehani ili kufanikisha biashara ya dawa za kulevya, atahukumiwa kifungo cha maisha jela.

Mbali na hilo, sheria hiyo mpya imeongeza makosa yasiyostahili dhamana kuwa ni pamoja na kumiliki mitambo ya kutengeneza dawa za kulevya na kufadhili biashara hiyo ya dawa za kulevya.

Halikadhalika mtu atakayekamatwa kwa tuhuma za kuwaingiza watoto kwenye biashara na matumizi ya dawa za kulevya, hawataruhusiwa kupata dhamana watakapofikishwa mahakamani. Katika sheria hiyo mpya mtu atakayetiwa hatiani kwa makosa ya kujihusisha na biashara hiyo mali zake na za washirika wake ambazo alizipata miaka 10 kabla ya kutiwa hatiani zitataifishwa.

Mhagama alisema marekebisho hayo yameweka utaratibu mzuri wa kufanya makubaliano baina ya Tanzania na nchi za nje ya namna ya kusaidiana kutaifisha mali.

Alisema marekebisho hayo ya sheria yanampa uwezo kamishna jenerali wa mamlaka hiyo kushikilia akaunti za watuhumiwa benki ili kuimarisha na kuboresha uchunguzi.

Pia, marekebisho hayo yameweka kifungu kinachotambua kuwa itakuwa ni kosa kusafirisha isivyo halali kemikali zinazotumika katika kutengeneza dawa za kulevya.

Akitoa maoni na mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Ukimwi, Dk Jasmine Bunga alisema inakubaliana na marekebisho hayo ya Serikali ili kupanua wigo wa vita hiyo.

Dk Bunga alisema wakati wa kutunga kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo, Serikali ione umuhimu wa kuongeza kwenye orodha viroba na dawa nyingine za binadamu kama za kulevya.

Alisema dawa hizo nyingine za binadamu zipo zinazoweza kutumiwa kama dawa za kulevya na hiyo itasaidia kudhibiti mbinu mpya za kuzalisha dawa mpya za kulevya hapa nchini.

Vilevile kamati hiyo iliitaka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya idhibiti taarifa na ripoti za uchunguzi kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuondoa mazingira ya ubambikiaji kesi.

Dk Bunga alipendekeza mamlaka za Tanzania Bara na Zanzibar kutafuta mbinu za kudhibiti mianya ya kupenyeza dawa za kulevya Zanzibar kwa kuwa sheria inahusu Tanzania Bara tu.

Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa wizara hiyo, Masoud Salim alitahadharisha kuwaruhusu maofisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kumiliki na kutumia silaha kuwa ni hatari zaidi.

“Kuruhusu maofisa wa chini ya mamlaka hii kutumia silaha bila kueleza utaratibu wa mafunzo maalumu yanayotambuliwa kwa mujibu wa sheria ni hatari zaidi,” alisema.

Salim alisema sheria hiyo inamruhusu ofisa wa mamlaka kufyatua risasi au kutumia silaha kwa mtu anayehisiwa kutumia au kuuza dawa za kulevya anapotaka kukimbia au kuleta hatari.

“Ikumbukwe kuwa mwenye mamlaka ya kumkamata raia yeyote anayehisiwa au aliyetenda kosa kinyume cha sheria ni askari aliyepewa mafunzo,” alisema na kuongeza:

“Kitendo cha kuwaruhusu maofisa hawa ambao hawajaelezwa kama wanayo mafunzo ya kukamata au utaalamu wa kushughulika na wahalifu kuwapa mamlaka makubwa ya silaha ni hatari.”

Kambi hiyo ilitaka sheria hiyo iwe ke msisitizo wa kuwabana na kutoa mafunzo yenye tija ili kutoruhusu mwanya wowote wenye nia ovu kwa ofisa ambaye atakosa weledi katika majukumu yake.

Lazima Kuvuna Poindi Tatu kwa Mbeya City Bila Tshishimbi - Lwandamina

$
0
0
Lazima Kuvuna Poindi Tatu kwa Mbeya City Bila Tshishimbi - Lwandamina
LICHA ya kukosekana kwa kiungo wake nyota Papy Tshishimbi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City, Kocha wa Yanga George Lwandamina amesisitiza kikosi chake kitaibuka na ushindi.

Akizungumza na Nipashe, Lwandamina, alisema kuwa mchezo wa kesho ni muhimu kwao kushinda hivyo hata asipokuwepo nyota huyo ambaye ni muhimu kwenye kikosi cha Yanga wanapaswa kupambana kuvuna pointi tatu.

“Kila mchezaji anaumuhimu wake kwenye kikosi, hatupaswi kutegemea uwepo wa mchezaji mmoja, ni lazima tupambane kama timu kupata ushindi,” alisema Lwandamina.

Alisema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao wa kesho kwa kuwa na wao wamejiandaa na wamejipanga kushinda.

“Mchezo utakuwa mgumu, kwa sababu hata wao (Mbeya City) wamejiandaa, lakini kama wenyeji ni lazima tupambane ili tufanikiwe kupata pointi tatu,” alisema Lwandamina.

Aidha, amesema kutokana na matarajio ya ugumu wa mchezo huo, amewataka wachezaji wake kutumia vizuri kila nafasi watakayoipata kwenye mchezo huo.

Msimu huu Yanga imeonekana kupoteza makali yake ya upachikaji mabao baada ya kushuhudiwa kwenye michezo tisa iliyocheza kwenye ligi imefunga mabao 11 na kuruhusu kufungwa mabao manne huku ikiwa imejikusanyia pointi 17 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo.


Simba, Tanzania Prisons Hapatoshi Leo Uwanja wa Sokoine

$
0
0
Simba, Tanzania Prisons Hapatoshi Leo Uwanja wa Sokoine
VINARA Simba kutoka Dar es Salaam wanatarajia kushuka dimbani kuwakabili Tanzania Prisons "Maafande" katika mechi ya raundi ya 10 ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.

Mabingwa hao wa Kombe la FA wanashuka uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupata pointi tatu dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopita wakati wenyeji Tanzania Prisons wao walitoka sare ya bao 1-1 na Kagera Sugar ugenini Bukoba.

Akizungumza na Nipashe jana, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, alisema kuwa kikosi chake kiko tayari kwa mechi hiyo ambayo itakuwa na ushindani na changamoto kutoka kila upande.

Omog alisema kikubwa katika mechi ya leo ni wachezaji wake kuwa makini na kutumia vyema nafasi watakazozitengeneza huku akiitaja safu  ya ulinzi ya Tanzania Prisons ni imara na imefanya vizuri katika mechi zilizopita.

Mcameroon huyo alisema pia anataka kila mchezaji atakayepangwa kucheza kwa bidii na kujiongezea nafasi ya kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho ambacho kiko kwenye mchakato wa kujiimarisha  kuelekea mashindano ya kimataifa hapo mwakani.

"Ni mechi ngumu kama nyingine zilizopita, najua timu za jeshi huwa imara na wachezaji wake huitaji mbinu za ziada kufikia ubora unaotakiwa, wana nguvu, wanapumzi nzuri, lakini nasi tumejipanga kuwakabili ili tutimize malengo," alisema Omog.

Amewaambia wachezaji wake kuwa wanadeni la kuhakikisha msimu huu wanapata pointi zote sita jijini hapa kutokana na kuwapokea vizuri katika mikoa yote ya jirani waliyokwenda kucheza mechi za kirafiki.

Wakati safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Mganda Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya,  Mohammed Rashidi wa Tanzania Prisons mwenye mabao sita ndiye anatarajiwa kuibeba timu yake katika mchezo wa leo.

Mechi nyingine za ligi hiyo ya juu Tanzania Bara zitakazochezwa leo ni kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Ndanda FC, Njombe FC wao wataikaribisha Azam FC wakati Stand United itaivaa Mwadui na Majimaji watachuana na Mbao kutoka jijini Mwanza.

Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16 itaendelea tena kesho kwa mabingwa watetezi kuwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na "ndugu" Mtibwa Sugar watacheza na Kagera Sugar huko Manungu, Turiani Morogoro.


Bilionea wa Nyumba za Lugumi Afunguka Kuvutiwa na Wema Sepetu

$
0
0
Bilionea wa Nyumba za Lugumi Afunguka Kuvutiwa na Wema Sepetu
BILIONEA wa nyumba za Lugumi, Dkt Louis Shika amemfungukia ‘Tanzania Sweetheart’, Wema Issac Sepetu kuwa ni staa ambaye anamkubali ukiachana na huyo kwa upande wa muziki Ray C ni mmoja wa mwanadada ambaye anamkubali kupitia nyimbo yake ya nataka niwe na wewe milele.
Bilionea huyo ambaye amekuwa staa kwa muda mfupi kwa umaarufu wa Jina la 900 Itapendeza baada ya mnada wa nyumba za Lugumi bilionea akatambulika kwa jina hilo.

Rosa Ree Afunguka Fid Q Alivyomtosa kwenye Ngoma ya Fresh

$
0
0
Rosa Ree Afunguka Fid Q Alivyomtosa kwenye Ngoma ya Fresh
MWANAMUZIKI chipukizi anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva, Rosa Ree ameeleza jinsi alivyomtosa Fid Q kwenye kolabo ya ngoma ya rapa huyo iitwayo Fresh.

Akibonga na Mikito Nusunusu Rosa Ree alisema alipigiwa simu na Fid Q akimweleza nia yake ya kutaka kumshirikisha katika ngoma yake mpya, kitu kilichomfurahisha na kumtaka amtumie ‘beat’ ili asikilize na kuingiza kipande chake cha sauti.

“Fid Q alinitumia beat nikaingiza verse yangu, nilipomaliza nilimwambia autaarifu uongozi wangu (management) juu ya kazi hiyo, ajabu baada ya kumwambia hivyo, sikuiona tena simu yake, siku chache baadaye nikasikia ngoma ipo mtaani,” alimaliza Rosa Ree.


Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumamosi

Next: Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo... 13:29 MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo. Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa. Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako. Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065 Tupo Mbagala Rangi Tatu

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo... 13:29 MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo. Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa. Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako. Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065 Tupo Mbagala Rangi Tatu

$
0
0
MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Tupo Mbagala Rangi Tatu

Mama Kanumba Ahudhulia Uzinduzi wa Filamu ya Hamisa Mobetto

Previous: Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo... 13:29 MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo. Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa. Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako. Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065 Tupo Mbagala Rangi Tatu
$
0
0
Mama Kanumba Ahudhulia Uzinduzi wa Filamu ya Hamisa Mobetto
MWANAMITINDO  Hamisa Mobeto, usiku wa kuamkia leo amezindua rasmi  Quality Centre jijini Dar muvi ambayo ameshiriki kwa kiasi kikubwa inayoitwa, Zero Player, ambayo ilishutiwa katika ukumbi wa Suncrest Cineplex.
Muvi hiyo ambayo imeshutiwa nchini, South Africa, na Mobeto ameigiza kama Mhusika mkuu huku akitumia jina la Jack, imeandaliwa na Allan Upamba, huku ikishirikisha wa sanii machachari kutoka Bongo, akiwemo Mobeto na Seth Bosco.

Afande Sele Awapa Makavu Bongo Movie "Siwachukii Bongo Movie Bali Nachukia Tabia Zao Chafu Ambazo Zinaharibu Tasnia"

$
0
0
Afande Sele Awapa Makavu Bongo Movie "Siwachukii Bongo Movie Bali Nachukia Tabia Zao Chafu Ambazo Zinaharibu Tasnia"
Msanii mkongwe wa muzuki wa kizazi kipya, Selemani Msindi marufu kwa jina la Afande Sele, ameweka wazi juu ya chuki aliyonayo kwa tasnia ya filamu bongo (bongo movie).

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, Afande Sele amesema hawachukii wasanii wa bongo movie, bali huchukia tabia zao chafu ambazo zinaharibu Tasnia.
Afande Sele ameendelea kwa kusema kwamba wasanii wa bongo movie wana tabia chafu hasa za kuwanyanyasa wanawake kwa kuwatumikisha kingono, huku akimtolea mfano muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) ambaye amefungwa.

Mr Nice Aliamsha Dude " Dudu Baya ni Msanii Asiyejielewa Umri Ushaenda Hana Mahali pa Kuishi"

$
0
0
Mr Nice Aliamsha Dude " Dudu Baya ni Msanii Asiyejielewa Umri Ushaenda Hana Mahali pa Kuishi"
Msanii Mr Nice ambaye kwa sasa ameachia kazi yake mpya ya Yaya, amejibu tuhuma za msanii mwenzake Dubu Baya aliposema kwamba maisha yamemshinda na kukimbilia Kenya, na kumjibu kuwa Dudu Baya ni msanii asiyejielewa, ndio maana hana mahali pa kuishi.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Teleivison, Mr.Nice amesema ni wakati sasa Dudu Baya akomae na game kama anavyofanya yeye, kwani muda wa malumbano na kuchafuana hautamsaidia chochote, na hastahili kufanya hayo kwakuwa umri umeshamucha.
Mr. Nice ameendelea kwa kusema kwamba Dudu Baya ni mlevi na anaishi maisha ya kuigiza, hivyo kabla hajaanza kumuongelea vibaya ni vyema akaanza kujilinganisha naye kama wanafanana kimaisha.

Irene Uwoya Atua na Mwanaye Kigali Kuhani Msiba wa Aliyekuwa Mume Wake

$
0
0
Irene Uwoya Atua na Mwanaye Kigali Kuhani Msiba wa Aliyekuwa Mume Wake
Mrembo wa zamani wa taji la Miss Chang’ombe na mwigizaji maarufu nchini, Irene Uwoya amewasili jijini Kigali, Rwanda kuhani msiba wa aliyekuwa mumewe, Ndikumana Hamad.

Ndikumana aliyekuwa akijulikana kama Katatut, alifariki dunia ghafla siku chache zilizopita na kuzikwa juzi jijini Kigali.

Uwoya hakuwa jijini Kigali wakati wa mazishi na usiku wa kuamkia leo ametua jijini Kigali akiongozana na mwanaye, Klishy ambaye alizaa na marehemu. Pia aliongozana na mama yake mzazi.

Uwoya alijifunika sura muda wote wakati akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kanombe jijini Kigali.

Wakati anatua, ndugu wakiwemo mashabiki wa michezo na burudani, walijitokeza uwanjani hapo.

Kataut ambaye alicheza soka katika nchi kadhaa za Ulaya, mauti yalimkuta akiwa kocha msaidizi wa Rayon Sports na siku moja kabla ya kifo chake alikuwa mazoezini.

Kwa hapa nchini, Kataut aliwahi kuichezea Stand United kabla ya Kocha Patrick Liewig raia wa Ufaransa, kupendekeza aachwe.

Afrika Mashariki Kuja na Show Kama ya Big Brother Itakayoanza Mwakani

$
0
0
Afrika Mashariki Kuja na Show Kama ya Big Brother Mwakani
Show ya TV iliyopewa jina God Father East Africa itaanza kuonekana mwakani. Reality show hiyo itahusisha nchini za Afrika Mashariki – Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda.

Usaili utaanza kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao katika majiji ya Nairobi, Kigali, Kampala na Dar es Salaam. Washiriki watakaa kwenye jumba la God Father kwa kipindi cha miezi mitatu na mshindi ataibuka na kitita cha shilingi milioni 50 za Tanzania.

Show hiyo itaonekana kupitia NTV au Citizen TV ya Kenya. Kama ilivyo Big Brother, washiriki watarekodiwa na kamera saa 24 katika siku 7.

Manyika Jr Kiwango Chake Chapaa Amfunika Manura

$
0
0
Manyika Jr Apanda Kiwango Amfunika Manura
Golikipa wa Singida United Peter Manyika Jr ameendelea kuonyesha kiwango bora baada ya kucheza mechi saba bila kuruhusu nyavu zake kuguswa akiwa na klabu yake hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu.

Mechi ya jana ambayo Singida United walishinda bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC, imemfanya Manyika kufikisha jumla ya michezo saba bila kufungwa katika mechi 10 za VPL alizocheza msimu huu wa 2017/18.
Mtoto huyo wa golikipa wa zamani wa Yanga Peter Mantika sasa amefikia rekodi ya golikipa wa Azam Razak Abarola ambaye hajaruhusu goli katika mechi saba za VPL katika mechi tisa alizochezan hadi sasa msimu huu.

Golikipa mwingine ambaye amecheza mechi nyingi bila kuruhusu goli ni Aishi Manula ambaye ni golikipa namba moja wa klabu ya Simba na Taifa Stars, hajaruhusu goli katika mechi tano za VPL kati ya mechi tisa alizocheza hadi sasa.
Manyika tayari amecheza michezo 10 wakati Manula akiwa na mechi tisa huku leo akitarajiwa kucheza mechi yake ya 10 ambayo klabu yake ya Simba itacheza na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Manyika amejiunga na Singida United msimu huu akitokea Simba ambako alikosa nafasi ya kuchcza mara kwa mara lakini tangu ametua kwenye kikosi hicho cha kocha Hans Van Pluijm amejihakikishia nafasi ya kuanza.

Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images