Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

VIDEO: “Sijatoa Mimba, Diamond Platnumz Namkubali tu” – Tunda

0
0
Video Queen maarufu wa Bongo aitwae Tunda amezungumza kuhusu yale maneno yaliyosambaa mitandaoni kwamba yeye ni Mjamzito huku akidaiwa kutoka kimapenzi na Mwimbaji Staa wa Bongofleva Diamond Platnumz.

Gumzo lake la kutoka na Diamond lilianzia pale alipoamua kuweka kwa siku kadhaa picha ya Diamond Platnumz kwenye sehemu ya Profile Picture ya Whatsapp yake, bonyeza play hapa chini kumtazama Tunda akiongea mwanzo mwisho

VIDEO:

BREAKING: Kauli ya Polisi Kilimanjaro Baada ya Kupiga Mabomu Mapokezi ya Lowassa

0
0
Polisi Mkoani Kilimanjaro leo imekiri kupiga mabomu ya machozi yasiyopungua manne kwenye mapokezi ya Mwanasiasa maarufu Edward Lowassa aliekua anakwenda kwenye kampeni kumnadi Mgombea Udiwani.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Hamis Isaah amesema wametumia mabomu hayo baada ya wananchi kufurika barabarani

 “Alikuwa anakuja katika mapokezi yake, wale waliokuwa wamejiandaa kupokea sasa ikawa ni fujo ikawa sio mapokezi, akakosa njia ya kupita na watu walivyokuwa wengi huwezi kuwaamini wote au kujua wengine wana nia gani”

“Kwa hiyo kilichofanyika pale palipigwa mabomu watu wakasambaa na akasindikizwa mpaka sehemu ya uwanja wa mkutano”

Msikilize Kamanda wa Polisi akiongea mwenyewe, bonyeza play hapa chini: VIDEO:

Simon Msuva Atemwa Kwenye Kikosi cha Challenge

0
0
Ammy Ninje hajamjumuisha winga Simon Msuva wa Difaa Hassan El-Jadida ya Morocco katika kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kuanzia Desemba 3, mwaka huu Jijini Nairobi, Kenya.

Badala yake, Ninje amemchukua winga wa Fanja ya Oman, Daniel Lyanga kwenye kikosi chake cha wachezaji 20 aliowataja leo mjini Dar es Salaam.

Katika kikosi hicho, Ninje mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameita makipa wawili tu, Aishi Manula wa Simba na Peter Manyika wa Singida United.

Mabeki ni Boniphace Maganga, Gardiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Kennedy Wilson.

Viungo ni Himid Mao, Hamisi Abdallah, Muzamil Yassin, Raphael Daudi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib na Abdul Hilal, wakati washambuliaji ni Elias Maguri, Mbaraka Yusuph, Yohana Nkomola na Daniel Lyanga.

Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A pamoja na ndugu zao, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya, wakati Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.

Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Rwanda.

Kili Stars itarudi uwanjani Desemba 7 kumenyana na Zanzibar Heroes, Desemba 9  na Rwanda kabla ya kumaliza mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na wenyeji, Kenya Desemba 11.

Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Desemba 12 na Nusu Fainali zitachezwa Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 itachezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali.

CECAFA Challenge ndiyo michuano mikongwe zaidi ya soka barani Afrika ambayo ilianza mwaka 1926 ikijulikana kama Kombe la Gossage hadi mwaka 1966, ilipobadilishwa na kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati hadi mwaka 1971 ilipobadilishwa tena na kuwa CECAFA Challenge.

Wadhamini tofauti wamekuwa wakiingia na kutoka kwa kipindi chote hicho, lakini taarifa zinasema kuanzia mwaka huu Televisheni namba moja Afrika Mashariki na Kati, Azam TV ndiyo wanakuwa wadhamini wapya ambao pia watakuwa wanarusha moja kwa moja michuano hiyo.

Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na Tanzania mara tatu.

Uganda, The Cranes pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.

Beki wa Real Madrid Ramos 'Ang'olewa' Pua

0
0
Beki tegemeo wa Real Madrid, Sergio Ramos akitoka nje kumpisha Nacho baada ya kushindwa kuendelea na mchezo dakika ya 46 kutokana na kuvunjika pua kufuatia kugongana na mchezaji wa Atletico Madrid, Lucas Hernandez katika mchezo wa La Liga wa mahasimu wa Jiji la Madrid usiku wa jana Uwanja wa Wanda Metropolitano uliomalizika kwa sare ya 0-0.

Mhe. Nassari Awachoresha Madiwani Waliojiuzulu CHADEMA na Kujiunga CCM

0
0
Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Joshua Nassari amemnadi mgombea udiwani wa Kata ya Ambureni, Dominick Mollel kwa kugawa CD anazodai zinaonyesha namna baadhi ya madiwani wa chama hicho wilayani Arumeru walivyoshawishiwa kupokea rushwa ili kujiuzulu Chadema na kujiunga na CCM.


Mhe. Nassari aliyekuwa ameambatana na mbunge wa Bunda, Esther Bulaya aligawa zaidi ya nakala 500 katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kwa Pole wilayani humo huku akiwataka  wananchi kutowachagua wagombea wa CCM kwa madai baadhi yao wanatuhumiwa kupokea rushwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Nassari amesema pamoja na kuwasilisha ushahidi wake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ameamua kugawa nakala hizo kuwafungua macho wananchi waelewe kwamba wagombea kutoka CCM hawafai.

Nassari amewambia wananchi waliofurika katika mkutano huo kwamba wagombea kutoka chama tawala hawastahili kuchaguliwa kwa kuwa baadhi yao walijiuzulu kwa kutuhumiwa kupokea rushwa. Pia alizungumzia kitendo cha baadhi ya wagombea wa CCM kutoa ahadi ya kuyakomboa baadhi ya mashamba yaliyotwaliwa na wawekezaji wilayani humo na kudai kwamba wakati wao wanatoa ahadi jukwaani wao wataingia shambani kudai haki.

“Wakati wao wanaahidi kushughulika na nyaraka sisi watatukuta shambani tunaendelea na kazi sawa.” amesema Mhe. Nassari.

Chanzo : Mwananchi

Tabia za Mwanamke Asiyewajibika au Mbovu Kitandani

0
0
Inasemekana wanawake wengi wenye ndoa wanakuwa na tabia zifuatazo zinazosababisha waume zao kwenda nje ya ndoa na wale wasio na tabia ya nyumba ndogo wanaishia kubakwa na waume zao

*Mwanamke asiyemtamkia kabisa mumewe kuwa anajisikia kuwa naye.
*Mwanamke ambaye baada ya mechi huwa haonyeshi dalili yoyote kama ameridhika na tendo au hakuridhika
*Mwanamke ambaye akiwahi kulala yeye mume akija hataki kuguswa
*Mwanamke ambaye mumewe akimgusa anakubali huku analalamika .. kama ulikuwa unataka kwa nini hukuwahi kulala unangoja nilale ndo unakuja kunisumbua..
*Mwanamke huyo hatingishiki kwenye mechi kata kidogo tena amenuna... anangalia kushoto au kulia anangoja goli liingie ... kama golikipa aliyekata tamaa ya kudaka penati......
*Mwanamke haweki kabisa maandalizi kama zana za kufanyia usafi baada ya mechi kama taulo, kitambaa nk

Ziko nyingine nyingi ambazo ni kero zinazowafanya wanaume kusononeka....na mara nyingine juamua kuzira na kuwa mwanzo wa mmoja kuhama chumba..... Wanawake wenye tabia hizi jirekebisheni

Naombeni Msinilaumu kwa Uamuzi Huu Niliouchukua kwa Mume Wangu

0
0
Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat, nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe

Tumeendelea kuishi na nilipopata mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo, napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe

wakati niko mjamzito mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl wangu ni wa mume wangu

kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote kuhusu huyo mtt.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na alionekana kweli amerigrate.
sasa cha kushangaza siku za karibuni amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama wa mtoto kwa siri haniambii chochote..

nilipoona mabadiliko niliamua kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena..
nikajaribu tena siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina maana kuna kitu zaidi ya mtoto.

Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo
1. Na mimi nimeamua kuwa na mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho, sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa atanisamehe tu ht akijua wl sijali, nipo tayari kwa lolote..
2. Sina mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio tunaojua ndani kukoje
3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani kwani sometime naona km nazidiwa mawazo vile

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo... 

0
0

MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Tupo Mbagala Rangi Tatu 

Breaking News: Chama cha Zanu-PF Kimemfuta Robert Mugabe Kama Kiongozi Wake

0
0

Chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF kimefuta Robert Mugabe kama kiongozi wake.

Kimemtua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.

Kufutwa kwa Bw. Mnangawa kumezua mambo mengi huku jeshi likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe 93, kumteua mke wake Grace kama makam wa rais.

Maelfu ya watu nchini Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Bw. Mugabe.

Bw. Mugabe anatarajiwa kukutana na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.

Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama kilikuwa kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe madarakani kama rais.

Profesa Lumumba Awakingia Kifua JPM, Kagame

0
0

MWANAZUONI maarufu barani Afrika, Profesa Patrick Lumumba, amesema Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Rwanda, Paul Kagame si madikteta bali wanachokifanya ni kuhakikisha kunakuwa na siasa za miiko na maadili.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana katika Mkutano wa Pan African Humanitarian wa mwaka huu ulioandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (Yuna) uliokuwa na kaulimbiu ya “amani inawezekana jana, sasa na kesho” na kuwakutanisha vijana kujadili nafasi zao katika kuleta amani barani Afrika.

Profesa Lumumba ambaye ni raia wa Kenya, alisema katika miaka ya hivi karibuni, wamekuja viongozi wenye mwelekeo na uchungu wa kuhakikisha mataifa yao yanaendelea, lakini baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwaita madikteta.

“Tunapaswa kujua hawa watu tunaowaita madikteta ni akina nani, kwa sababu kuna viongozi wameibuka katika miaka mitatu hadi 20 iliyopita, wakiwa na mwelekeo na kuona uchungu wa kuhakikisha mataifa yao yanaendelea, lakini baadhi ya watu wengine wanawaita eti ni madikteta,” alisema na kuongeza:

“Lakini viongozi hao ni watu wazalendo na wakereketwa wa maendeleo endelevu, hivyo watu kama hawa lazima tujiulize mienendo yao ni ya kidikteta? Au ni ya kuhakikisha mataifa yao yanapiga hatua za haja na hoja. Mfano wengine wanasema Kagame, Dk. Magufuli ni dikteta, sikubaliani nao kwa sababu kile ambacho wanakifanya, wanajaribu kusema kwamba lazima kuwe na siasa za miiko na maadili.

“Nakubali kwamba udikteta ni jambo ambalo halistahili, lakini ni muhimu kuhoji kwamba uhuni ndiyo demokrasia? Kwa sababu kumeibuka wimbi la watu ambao ni wababaishaji hata sio wapinzani, kila kitu anachokifanya (rais) wao kazi yao ni kupinga.”

Akizungumzia suala la amani, hasa katika vipindi vya uchaguzi, alisema ni wakati wa kujiuliza ni aina gani ya uongozi inahitajika barani Afrika ili kuwe na njia ya kubadilisha uongozi isiyoleta vurugu tofauti na ilivyo sasa.

“Pia tunapaswa kuangalia hivi vitu tunavyoviita vyama, ni vyama kweli au ni vikundi tu, genge tu la vibarua waliokuja kujitafutia nyadhifa ili kupora mali za Waafrika. Vijana ndio wataibua hoja hii na kutathimini kuwa mataifa yetu tunayaandaa kwa minajili ya kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema.

Pia alisema anaamini Afrika itakuja kuwa na amani na utulivu kwa sababu jitihada mahsusi zimeshaanza kufanywa na viongozi wake na tayari wamekwisha kutoa tamko kwamba kufikia mwaka 2020, lazima vitu vinavyoleta migogoro vitolewe na kila mtu anatakiwa kushiriki kwa nafasi yake.

Mtanzania

Mama Irene Uwoya Akesha Akimuombea Marehemu Ndikumana Aliyekuwa Mkwe Wake

0
0

Mama mzazi wa Irene Uwoya, Naima Uwoya, usiku wa kuamkia jana amekesha akimuombea aliyekuwa mkwewe Hamad Ndikumana katika Kanisa Katoliki Mbezi Jogoo, Dar es Salaam. Aidha Mama Uwoya akizungumza na chombo Kimoja cha habari amesema hakuwahi kuwa na tatizo na Ndikumana walikuwa Kama Mama na mwanae.Mama Uwoya amesema kipindi cha nyuma aliwahi kwenda nchini Israel na kufunga kwa Siku kadhaa ili Irene na Ndikumana warudiane lakini haikuwa bahati wao kuwa pamoja tena.
.
Akizungumza huku akilia kwa kwikwi kwa uchungu Mama Uwoya amesema
.
“Ndikumana mimi sijui nianzie wapi, alikuwa mkwe wangu kipenzi alikuwa kama rafiki, alivuka hata ukwe, Ndikumana mkwe wangu siku zote tumeishi nae vizuri, siku zote tumekuwa tukiwasiliana mpaka mwishoni hapa nilikuwa natoka safari, ananiambia mama naomba tuwe na moyo wa subira, mimi nitavumilia yote ya dunia lakini mimi ni mwanao mpaka naingia kaburini, na kweli mpaka anaingia kaburini, mwanangu mimi nilikuwa nampenda” alisikika mama yake Irene Uwoya ambaye alikuwa akilia kwa uchungu.
.
Akizungumza na Mtanzania alisema
.
“Sitaacha kumuombea marehemu mkwe wangu hadi siku naingia kaburini, nitaomba sana ili apumzike kwa amani hata kama ana kinyongo na familia yangu, tulimpenda familia nzima na naamini hata vizazi vyetu vijavyo vitampenda kwa kusikia matendo yake,” alisema mama Uwoya.
.
Alisema atahakikisha anampa faraja mzazi mwenziye (mama Ndikumana), kwa kuongea naye mara kwa mara kama alivyokuwa akiongea na marehemu na kumpelekea mjukuu wake ili amzoee na wajisike faraja ya kumuona mwanaye kupitia Krish.

Matokeo ya Yanga na Mbeya City Haya Hapa

0
0

DAR: Mechi imemalizika uwanja wa Uhuru kati ya Mabingwa Watetezi Yanga dhidi ya Mbeya City ambapo Yanga imeshinda kwa mabao 5 kwa 0.
-
Magoli ya Yanga SC yametiwa wavuni na Chirwa 19' 50' 59' pamoja na Martin 23'
Gadiel 80'.

Robert Mugabe Agoma Kula...Apania Kufa Akiwa Rais

0
0

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe inasemekana amekuwa akikataa kula na kuzungumza kwa siku kadhaa sasa akiwa amepania ‘kufa kwa ajili ya jambo sahihi’ wakati amewekwa chini ya ulinzi nyumbani kwake.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza limesema mpwa wa kiongozi huyo aitwaye, Patrick Zhuwao, alisema Jumamosi kwamba Mugabe yuko tayari kufa akipigania kile anachokiita ni sahihi.

Habari zingine kutoka nchini humo zinasema chama tawala cha ZANU-PF kitamwondoa Mugabe kwenye uongozi katika mkutano maalum unaotarajiwa kufanyika leo Jumapili. Mkutano huohuo unatarajiwa kumrudisha aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Munangagwa, ambaye alifukuzwa na Mugabe wiki mbili zilizopita.

Vilevile kuna uvumi kwamba kiongozi huyo ameikimbia nchi hiyo baada ya mamia ya maelfu ya watu kuandamana kupinga utawala wake. Waandamanaji hao walionekana wakichana matangazo yaliyo nje ya makao makuu ya Zanu-PF yakimwonyesha Mugabe.

Hata hivyo, Mugabe anategemewa kuzungumzia hatima ya kuondoka kwake madarakani na mkuu wa majeshi Constantine Chiwenga ambaye alimweka kizuizini nyumbani kwake.

Barnaba Ashindwa Kujizuia...Aandika Haya Kwa Mama Mtoto Wake Ambae Wameachana

0
0

Mwanamuziki anayefanya poa kwenye game ya Bongofleva Barnaba Classic ameshindwa kujizuia kwenye siku ya kuzaliwa mama wa mtoto wake Zuwena ambaye kwa sasa hawapo pamoja kwa kumshukuru kuwepo na kumpatia zawadi ya mtoto.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Barnaba amesema kwamba upendo wake juu ya zawadi mwanadada huyo aliyempati ipo palepale na kusisitiza kwamba anamuheshimu huku akimsisitizia kwamba anapenda kumuona akiwa furaha.

"Wewe ni rafiki Yangu na ndugu yangu Uvungu wa moyo wangu unakushukuru kwa kuwa daraja kwenye maisha yangu na nashukuru nimevuka salama matatizo ni sehemu ya kila mwanadamu upendo wangu juu ya zawadi uliyonipatia Iko pale pale/STEVE Na Kitu kizuri ninakuheshimu Sana mbali Na mambo Yote Na Kitu kingine Furaha Yangu kuona unaendela Kutabasamu Hata kama ilo Tabasamu Silitengenezi Mimi," Barnaba

Aidha Barnaba ameongeza kwamba anamtakia kila la kheri mwanadada huyo ambaye tayari amekwishaingia kwenye mahusiano na kumwambia anapenda yeye awe shuhuda wa maisha ya mzazi mwenzake huyo kwa kila jambo.

"Nakutakia maisha mema yenye baraka, nawaombea heri Katika Familia yako, nakuombea heri na uwahi uwe shuhuda wangu nami niwe shuhuda wako wa kila jambo heri ya siku yako ya kuzaliwa mzazi mwenzangu mama yake Steve, Zuunamela mama watoto ! Damu Ya yesu ikuangazie Amina,"  Barnaba

Rais Mugabe Apewa Masaa Kujiuzulu Urais Zimbabwe, Nguvu Yatangazwa Kutumika Endapo Atakaidi

0
0

Baada ya kuvuliwa nafasi ya kiongozi wa juu wa Chama cha Zanu- PF Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepewa masaa tu na Chama hicho kujiuzulu mwenyewe kwenye nafasi ya Urais wa nchi hiyo bila kutumia nguvu.


Chama tawala nchini humo leo baada ya kutangaza kuwa kimemvua uongozi Rais huyo mkongwe zaidi barani Afrika, Robert Mugabe, kimemwambia hadi kesho saa 6 mchana awe tayari ametangaza kujiuzulu nafasi ya Urais huku kikimuonya kuwa endapo atakaidi nguvu ya ziada itatumika kumng’oa madarakani.

“Rais wetu wa zamani, Robert Mugabe amepewa muda hadi kesho jumatatu saa 6 mchana awe ameshatangaza kujiuzulu nafasi ya Urais wa Zimbabwe la sivyo nguvu itatumika kumng’oa madarakani.”Imeeleza taarifa kutoka kwenye chama cha Zanu-PF iliyochapishwa kwenye ukurasa wao rasmi wa Twitter.

Nafasi ya Rais Mugabe itachukuliwa na kiongozi mkuu wa Chama tawala cha Zanu PF aliyechaguliwa leo kwenye kamati kuu ya chama hicho, Emmerson Dambudzo Mnangagwa ambaye pia alishawahi kuwa Makamu wa Rais wa Mugabe kabla ya kutimuliwa.

Dr.Cheni Amesema Habari za Lulu Kugomea Rufaa sio za Kweli

0
0

Dr.Cheni amesema habari za Lulu kugomea rufaa sio za kweli yeye hajazugumza na media yoyote Kama baadhi ya watu walivyosambaza mitandaoni. Amesema bado hajaongea na Lulu tangu aende Jela Segerea

Nahisi Ana Mwanamke Zaidi Yangu....Nataka Nimfumanie Kwa Suprise Visit Kwake

0
0
Nina age ya 22 nipo kwenye relationship na mwanaume kama miezi 3 saizi tatizo limeanza baada ya mimi kuwa mbali kama 3weeks hivi.

Nahisi anamwanamke zaidi yangu kwasababu hata namna ya kuongea
inanitia mashaka.

Kuna wakati akiongea na mimi anaongea vizuri sana but sometimes nikimpigia simu anaweza akaongea haraka haraka and mda huo najua yupo nyumbani kwahivo hayupo bize.

Nikimuuliza mbonahivo upo na nani? anakata simu then anafunga simu kabisa, kesho yake anaweza kuniambia simu imezima haikuwa na chaji au hapendi maswali yangu kwani
naonyesha kama simuamin.

Nataka nimfanyie suprise visit, sababu nimesharudi safari naye hajui kama nipo hapa mjini ili nijue kama kweli anakua bize au maswali yangu yanamkera na hamna kingine.

Je hii suprise ndio itaua kabisa mapenzi au nifanyaje?

Aliyezikwa Akidaiwa Mtu Mzima Abainika Kuwa ni Mwanafunzi Aliyekuwa Amepotea

0
0
Kama ni kuumbuka, basi walioidhinisha kuzikwa kwa maiti iliyodaiwa kuwa ni ya mtu mzima na mwenye ndevu, wameumbuka; maiti hiyo ni ya Humphrey Makundi, mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Scolastica ya Himo wilayani Moshi.

Hayo yalibainika baada ya kutekelezwa kwa amri ya kufukua maiti hiyo iliyotolewa na Hakimu Idan Mwilapo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na baadaye kufanyiwa uchunguzi. Uchunguzi umebaini kuwa maiti hiyo ni ya mtoto na hakuwa na ndevu.

Amri ya kufukua maiti hiyo ilitolewa baada ya Jamhuri kuwasilisha maombi kupitia kwa Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka ukitaka mwili uliozikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Novemba 12 kwa kukosa ndugu ufukuliwe. Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani juzi yakiambatanishwa na kiapo cha Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Doto Mdowe na Mahakama iliridhia ombi hilo.

Mwanafunzi huyo alitoweka shuleni katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6 na baadaye mwili wake ukaokotwa Mto Ghona, umbali wa mita 300 kutoka shule hiyo.

Kutokana na mwili huo kuharibika, polisi na daktari waliufanyia uchunguzi wa awali na kueleza kuwa haukuwa wa mtoto huyo bali ni wa mtu mzima na kuruhusu halmashauri kuuzika.

Ingawa haielezwi katika shauri hilo ni nani aliyetoa hoja mwili huo ufukuliwe, lakini RCO katika kiapo chake alitaka ufukuliwe ili uchunguzwe kama ni wa Humphery aliyetoweka Novemba 6.

Watu 11 wakamatwa

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah alisema wanawashikilia watu 11, akiwemo mmiliki wa shule hiyo iliyopo mji mdogo wa Himo kwa ajili ya mahojiano.

Kwa mujibu wa Kamanda Issah, ingawa mtoto huyo aliondoka Novemba 6 kutoka shule hiyo iliyozungushiwa ukuta na walinzi na kwenda kusikojulikana, taarifa za kutoweka kwake zilitolewa polisi Novemba 11.

“Mtoto alitoweka shuleni tarehe 6.11.2017 wao wakaendelea na taratibu zao hadi tarehe 10.11.2017 ndio walizifikisha taarifa hizo polisi. Tulianzia uchunguzi papo hapo,” alisema.

“Katika hatua za awali za uchunguzi tulimkamata mmiliki wa shule kwa usalama wake kwa sababu wazazi tayari walikuwa wanamtuhumu kuhusika na kifo cha mtoto wao.”

Kamanda Issah alisema wakati wakiendelea na uchunguzi, walipata taarifa kuwa kuna mwili wa mtu uliokotwa Novemba 7 na ukahifadhiwa Hospitali ya Mawenzi hadi Novemba 12 ukazikwa.

“Baada ya kupata taarifa ndipo tukaomba kibali cha kufukua huo mwili na wakati unafukuliwa wazazi walikuwepo. Nawahakikishia haki ya huyu mtoto haitapotea,” alisema.

Kamanda Issah hakutaka kuzungumzia kwa undani kuhusu kile kilichobainika katika uchunguzi huo, lakini alisema umefikia asilimia 50.

“Tunataka kujua ilikuwaje mwanafunzi akatoka shuleni na shule ina geti na ina walinzi. Hapo nje kuna mama lishe,” alisema kamanda huyo.

“Niwaonye wamiliki wa shule, wasimamie vizuri maisha ya wanafunzi.”

Mwili ulivyotambuliwa

Watu walioshuhudia ufukuaji wa mwili huo katika makaburi ya Karanga mjini Moshi juzi saa 8:30 mchana, walilieleza gazeti hili kuwa baba mzazi wa mtoto huyo, Jackson Makundi aliishiwa nguvu na kuanguka.

Taarifa zinasema kabla ya ufukuaji kuanza, maofisa wa polisi walimuuliza mzazi huyo ataje alama zitakazomfanya amtambue kuwa huyo ni mwanaye naye alitoa alama mbili ambazo ni jino moja kukatika nusu na kidole kimoja cha mkononi kuwa na kucha iliyong’oka, alama ambazo zilionekana.

“Baada ya mwili kufukuliwa na baba na ndugu wengine kutambua alama alizozisema, yule baba aliishiwa nguvu na kukaa chini ikabidi aondolewe eneo lile,” alisema mmoja wa walioshuhudia tukio hilo.

Kwa mujibu wa mtu aliyeshuhudia uchunguzi huo, mwili wa mtoto huyo umekutwa na jeraha kwenye fuvu la kichwa ikiashiria alipigwa na kitu kizito kichwani.

Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Alichosema baba mzazi

Jackson Makundi, baba mzazi wa mtoto huyo amedai kuna mchezo uliofanywa baina ya uongozi wa shule na polisi wa Himo ili kuficha ukweli kuhusu ukatili aliofanyiwa mtoto wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, baba huyo alidai alipewa taarifa za kupotea mwanawe Novemba 8, ikiwa ni siku mbili baada ya kudaiwa ametoweka shuleni katika mazingira ya kutatanisha.

Makundi alidai taarifa ambazo baadhi ya walimu wanazitoa kuhusu kutoweka kwa mwanafunzi huyo zinatofautiana na taarifa za wanafunzi.

“Baada ya mwili kufukuliwa nilijiridhisha kwa asilimia 100 kuwa mtoto ni wangu kutokana na kwamba vichwa vyetu vinafanana na nyuso zetu,” alisema.

Alidai taarifa alizozipata kutoka kwa wanafunzi wenzake ni kwamba mtoto wake aliondoka shuleni akiwa amevaa bukta, fulana na soksi.

Makundi amehoji iweje mwanafunzi atoweke shule halafu apewe taarifa baada ya siku mbili, wakati shule hiyo ina ulinzi na utaratibu mkali wa kuingia na kutoka.

“Ninaamini na dhamira ya moyo wangu inanituma kuamini uongozi wa shule na polisi wa kituo cha Himo wana jambo wanalificha kuhusu kifo cha mtoto wangu,” alisema.

Hata hivyo, alimpongeza Kamanda Issah na wasaidizi wake kwa namna wanavyompa ushirikiano katika uchunguzi, akiamini kila kitu kitajulikana.

Maswali kuhusu uchunguzi

Tangu kufukuliwa kwa mwili huo na kubainika ni wa Humphrey, kumeibuka maswali kuhusu namna polisi na daktari wa Hospitali ya Mawenzi walivyoruhusu mwili uzikwe.

Taarifa kutoka eneo ambalo mwili huo uliokotwa zilidai polisi hawakupiga picha pande zote za mwili huo ili iwe rahisi kwa mtu yeyote kuutambua.

Imeelezwa polisi walitafuta picha na kupata kutoka kwa mwananchi aliyezipiga kwa kutumia simu zikionyesha mwili huo ukiwa umelala kifudifudi.

“Ndiyo maana ukitazama polisi siku mwili unaokotwa wana picha moja ya marehemu akiwa amelala kifudifudi. Huu ndio utaratibu wa kiuchunguzi?” Alihoji mmoja wa wajumbe wa Serikali ya Mji wa Himo.

Swali jingine ambalo baadhi ya watu wamekuwa wakihoji ni jinsi polisi na daktari wa Hospitali ya Mawenzi walivyoruhusu mwili huo uzikwe wakidai ni wa mtu mzima mwenye ndevu wakati ni wa mtoto.

Pia, wanahoji ilikuwaje mwanafunzi atoweke shuleni tangu Novemba 6, lakini taarifa za kutoweka kwake zikafikishwa polisi siku tano baadaye.

Swali jingine ni kwanini polisi waliofika mahali sehemu ulipookotwa mwili huo, hawakuchukua sampuli za vipimo vya vinasaba (DNA) ili atakapojitokeza ndugu, waweze kuoanisha.

Utaratibu unataka maiti isiyojulikana inapookotwa yatolewe matangazo katika maeneo yote ya jirani, lakini katika tukio hilo, mwili ulichukuliwa na kupelekwa hospitali na baadaye kuzikwa.


By Daniel Mjema na Janeth Joseph, mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Kwanini Wanawake Wengi Wakishajifungua Wanakuwa Rahisi Kuchukuliwa na Vidume?

0
0
Katika pita pita zangu wale wadada wanajidai wana misimamo wanapozalishwa na wanaume na kuachwa alone huwa wanashuka chini na inakuwa rahisi kupiga sound ya kawaida na kuchukua mzigo ila kipindi kabla ilikuwa hata kusalimia watu ni tabu kwake.

Najiuliza kwa nini hulainika na kuwa na heshima pindi wanapo zalishwa?

Jinsi ya Kuzuia Chunusi na Mabaka Usoni

0
0
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.

Kwa lugha ya kidaktari chunusi huitwa Acne Vulgaris.Chunusi ndio ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni kumi na sa-ba..Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wa-kati wa balehe (adolescents) .

Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.

Chunusi ni ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na yenye mvuto.

Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo ambao huziba vishimo vya kutolea joto. 

Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo tunaviita chunusi.

Ukubwa wa kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.

Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.

CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;


UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana.
MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
USAFI WA MWILI- Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha chunusi

DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana.

Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi, dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi

MATIBABU
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.

Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.

DAWA ZA KUPAKA
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au pad.

Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream, Erythromycin,B-Tex na kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%) na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.

Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi.

Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.

DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.

Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi ,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin), Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide) Minocin (minocycline hydrochloride) na ”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”

Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.

MATIBABU MENGINE
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa baka.

MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.

Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi

MUHIMU
Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta mgando
Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
Punguza mawazo
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images