Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Jeshi la Zima Moto Lafanikiwa Kuokoa Kituo cha Habari cha Clouds

$
0
0
Jeshi la Zima Moto Lafanikiwa Kuokoa Kituo cha Habari cha Clouds
Jeshi la zima moto limefika katika jengo la kituo cha habari cha Clouds Media Group jijini Dar es salaam, kudhibiti moto uliozuka katika mojawapo ya vyumba vya kurushia matangazo ya televisheni.
Tayari moto umeshadhibitiwa.
Sebastian Maganga, mkuu wa maaudhui na uzalishaji wa Cloud Media Group, ameiambia BBC kwamba, "moto umetokea kati ya saa tatu asubuhi hadi saa nne , athari saizi ni vigumu kuzijua. Eneo ambalo limeungua ni chumba cha kurushia matangazo ya televesheni."
Mojowapo ya vipindi vilikuwa vikuruka hewani hapo ambapo moto ulipozuka.
Pia Ambwene Mwakibete, Kaimu Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji, mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, amesema kwamba
"Tumeidhibiti moto ili usimbae kwenye vyumba vingine. Tumeona ni mfumo wa kiyoyozi ambao ni umeme ndio tumeona umeathirika kwa sehemu kubwa."
Hamna majeruhi wala vifo, na thamani ya uharibifu haijafahamika bado. Chanzo cha moto hadi sasa bado hakijafahamika.

Mahakama Yamuachia kwa Dhamana Mgombea Udiwani wa Chadema

$
0
0
Mahakama Yamuachia kwa Dhamana Mgombea Udiwani wa Chadema
Mgombea udiwani Kata ya Mhandu (Chadema), Godfrey Misana amepata fursa ya kushiriki kampeni za lala salama za uchaguzi mdogo wa Novemba 26, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kumwachia kwa dhamana katika shauri la kujeruhi linalomkabili.

Mgombea huyo pamoja na meneja wake wa kampeni, Charles Chinjibela na watu wengine wawili wanakabiliwa na kesi namba 540/2017 ya kumjeruhi meneja wa kampeni wa CCM katika kata hiyo, Thomas Warioba katika tukio lililotokea Novemba 14.

Washitakiwa wengine waliounganishwa katika shauri hilo leo Jumanne ni Dominic Izengo na Ebenezer Mathew.

Katika uamuzi wake Hakimu Mkazi, Ainawe Moshi amesema baada ya hoja za pande zote na kupitia vifungu vya sheria, Mahakama inakubaliana na hoja za upande wa utetezi unaowakilishwa na mawakili Gasper Mwanaliela na Paul Kipeka kuwa shtaka hilo lina dhamana na upande wa Jamhuri haujatoa hoja za kuishawishi Mahakama kuzuia dhamana.

“Baada ya kusikiliza ombi la upande wa Jamhuri la kuzuia dhamana na hoja za upande wa utetezi kupinga ombi hilo, Mahakama imejiridhisha kuwa hakuna hoja zenye uzito katika macho ya sheria za kuendelea kuwashikilia mahabusu washtakiwa, hivyo inawaachia kwa dhamana,” amesema Hakimu Moshi katika maamuzi yake.

Awali, Wakili wa Serikali, Elizabeth Barabara ametumia kifungu cha 148 (a) (d), cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kuomba dhamana za washtakiwa kuzuia kwa alichodai ni usalama wao.

Hakimu Moshi ametaja sharti la dhamana kuwa ni kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni kila mmoja. Shauri hilo limeahirisha hadi Desemba 7 mwaka itakapotajwa tena.

Man United Kuwanasa Bale, Griezman

$
0
0
Man United Kuwanasa Bale, Griezman
Manchester United inatarajia kuingia sokoni kunasa saini ya mshambuliaji mmoja.

Majina yanayotajwa kuwindwa na Man United ni Antoine Griezmann wa Atletico Madrid na Gareth Bale anayecheza Real Madrid.

Hata hivyo, kocha wa Man United, Jose Mourinho hajui atamsajili mchezaji gani kati ya Griezmann au Bale .

Washambuliaji wote wanamvutia Mourinho na atalazimika kuchagua mmoja ili kwenda kuongeza kasi katika safu ya ushambuliaji Man United.

Mourinho ana Romelu Lukaku na Zlatan Ibrahimovic aliyerejea uwanjani akitokea katika maumivu ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja miezi saba.

Mshambuliaji Griezmann na Bale mmoja kati yao anapewa nafasi ya kuvaa uzi wa Man United katika dirisha la usajili Januari, mwakani endapo mpango huo utafanikiwa mapema kabla ya majira ya kiangazi.

Bale amekuwa na maisha magumu Real Madrid baada ya kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara, lakini Griezmann tangu kuanza msimu huu hayuko fiti.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, amefunga mabao mawili katika mechi 10 alizocheza na mwishoni mwa wiki iliyopita alizomewa na mashabiki wa Atletico Madrid katika mchezo dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.

Msimu uliopita Griezmann alicheza kwa kiwango bora na aliwekwa sokoni akiuzwa Pauni 200 milioni, lakini Man United ilishindwa kumsajili baada ya Atletico Madrid kufungiwa na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kusajili.

Chadema Yabariki Uamuzi wa Aliyekuwa Mwenyekiti Wao wa Bavicha

$
0
0
Chadema Yabariki Uamuzi wa Aliyekuwa Mwenyekiti Wao wa Bavicha
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hakina mgogoro na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi ambaye ametangaza kujiunga na CCM kwa kuwa ni haki ya Kikatiba.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne baada ya Katambi kuhamia CCM, Dk Mashinji, “sisi kama chama msimamo wetu tuliuweka tangu madiwani walivyoanza kuondoka, tukaweka msimamo wazi kwamba, suala la mtu kuondoka kwenye chama au kubaki ni suala la Katiba ya nchi ambayo inampa mtu uhuru wa kuhama na kwenda kwenye chama anachotakana.”

Amesema kuwa haoni sababu ya kumzuia mtu kuondoka kwa kuwa mtu anapoamua kwenda sehemu yoyote anakuwa na matarajio.

Pia, Dk Mashinji amesema anamtakia heri (Katambi) na kuwataka CCM kumtumia katika sehemu ambavyo wanaona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote.

Soma: Katambi asema yuko tayari kuitwa msaliti

“Hatuna mgogoro wowote na kimsingi mimi nimtakie tu heri (Katambi) na wakipenda (CCM) wamtumie kwenye eneo watakaloona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote,” amesema

Hata Hivyo, Dk Mashinji amesema kuwa walikuwa wanamuandaa Katambi asaidie chama hicho kwenye kitengo cha sheria.

“Alikuwa anamalizia masomo yake ili awe wakili na tulikuwa tumeshaanza kumuandaa ili atusaidie kwenye kitengo cha sheria ndani ya chama,”

Katambi ametangaza leo kujiunga na CCM mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

$
0
0


THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.
+255 746 757 102 Kupiga tu. 

Mlipuaji wa Kujitolea Muhanga Wauwa Watu 50 Msikitini

$
0
0
Mlipuaji wa Kujitolea Muhanga Wauwa Watu 50 Msikitini
Takriban watu 50 wameuwawa katika shambulio la kujitolea muhanga katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa mji wa Mubi.
Wakuu katika eneo hilo wanasema kwamba watu zaidi ya kumi wamejeruhiwa, baada ya mtu aliyejitolea muhanga kujilipua ndani ya msikiti mmoja wakati wa sala ya alfajiri Jumanne.
Mubi ni mji ulioko katika Jimbo la Adamawa, mahali ambapo wanamgambo wa Boko Haram, wamekuwa wakitekeleza mashambulio ya mara kwa mara.
Shahidi Abubakr Sule aliambia AFP kwamba inaonekana kwamba mlipuaji huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakitekeleza ibada hiyo.
Hakuna mtu aliyetangaza kuhusika na ulipuaji huo lakini kundi la wanamgambo wa Boko Haram limekuwa likilenga makundi ya watu kaskazini mwa Nigeria.
Takriban watu 20,000 wameuawa katia kipindi cha miaka minane ya mashambulizi ya Boko haram.
Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid ameripoti kwamba wanamgambo wa Boko Haram wameimarisha mashambulio yao katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya jeshi kuyakomboa maeneo yaliokuwa yakidhibitiwa na kundi hilo.
Takriban watu 45 waliuawa katika shambulio la bomu la kujitolea muhanga katika jimbo hilo hilo mwezi Disemba.
Katika shambulio hilo wanawake wawii wa kujitolea muhanga walijilipua katika soko ambalo lilikuwa limejaa watu.
Wakuu katika eneo hilo wanasema kwamba watu zaidi ya kumi wamejeruhiwa, baada ya mtu aliyejitolea muhanga kujilipua ndani ya msikiti mmoja wakati wa sala ya alfajiri Jumanne.
Mubi ni mji ulioko katika Jimbo la Adamawa, mahali ambapo wanamgambo wa Boko Haram, wamekuwa wakitekeleza mashambulio ya mara kwa mara.
Shahidi Abubakr Sule aliambia AFP kwamba inaonekana kwamba mlipuaji huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakitekeleza ibada hiyo.
Hakuna mtu aliyetangaza kuhusika na ulipuaji huo lakini kundi la wanamgambo wa Boko Haram limekuwa likilenga makundi ya watu kaskazini mwa Nigeria.
Takriban watu 20,000 wameuawa katia kipindi cha miaka minane ya mashambulizi ya Boko haram.
Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid ameripoti kwamba wanamgambo wa Boko Haram wameimarisha mashambulio yao katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya jeshi kuyakomboa maeneo yaliokuwa yakidhibitiwa na kundi hilo.
Takriban watu 45 waliuawa katika shambulio la bomu la kujitolea muhanga katika jimbo hilo hilo mwezi Disemba.
Katika shambulio hilo wanawake wawii wa kujitolea muhanga walijilipua katika soko ambalo lilikuwa limejaa watu.

Lema Afunguka Haya Baada ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Kuamia CCM

$
0
0
Lema Afunguka Haya Baada ya Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Kuamia CCM
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kwamba kisasi cha CCM kuchukua wanachama wake kitasaidia kuwaondoa wavulana kwenye mapambano ya siasa za upinzani.

Lema ameyasema hayo ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, Patrobas Katambi kuomba kuomba ridhaa ya kuingia ndani ya Chama cha Mapinduzi leo katika kikao cha halmashauri Taifa.
Lema amesema kwamba CCM imekuwa na kisasi kikubwa baada ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili mstaafu na Mbunge wa Singida Kaskazini  Lazaro Nyalandu kuondoka CCM
"Baada ya Lazaro kuondoka CCM , CCM wamekuwa na kisasi kikubwa , ambacho kimsingi kitasaidia kuondoa wavulana ktk mapambano haya , bado Mameya wawili ? Na kijana mwingine aliyekuwa shupavu 2010-2015. Msiogope kwani wanawaogopa sana na ndio sababu ya matendo haya" Lema.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dr. Vicent Mashinji amesema kwamba "Ni muda wa kutofautisha kati ya wanaume na wavulana! wana CHADEMA msihofu tunazidi kuimarika. Kila abiria atashuka kwenye kituo chake lakini safari ya ukombozi inaendelea".
Hata hivyo juhudi za kumtafuta Lema kwa ajili ya kumtaja jina kijana huyo anayetarajiwa kuondoka Chadema hazijazaa matunda kwani simu ya Mbunge huyo haijapokelewa.

Mbunge wa Tarime, John Heche(CHADEMA) Aachiwa kwa Dhamana

$
0
0
Mbunge wa Tarime, John Heche(CHADEMA) Aachiwa kwa Dhamana
Mbunge wa Tarime, John Heche (CHADEMA) ameachiwa kwa dhamana leo baada ya kushikiliwa kwa siku mbili
- Alikamatwa kwa tuhuma za kufanya mkutano wa hadhara kwenye jimbo la Kilombero ambalo ni nje ya jimbo lake la uongozi.

Okwi Atoa Ahadi Hii kwa Wanasimba "Nitarejea Nikiwa Imara Zaidi"

$
0
0
Okwi Atoa Ahadi Hii kwa Wanasimba "Nitarejea Nikiwa Imara Zaidi"
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi amesema atarejea kwa kasi na uwezo zaidi baada ya kuwa nje kwa muda akiuguza majeraha aliyoyapata akiwa kwenye majukumu na timu ya taifa ya Uganda.

Okwi ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akielezea namna ambavyo ameukumbuka mchezo wa mpira wa miguu kutokana na kutocheza kwasababu ya kuwa majeruhi.
“Hakika nimeukumbuka sana mpira wa miguu, lakini nitarejea nikiwa imara zaidi baada ya kupona majeraha madogo yanayoniweka nje ya uwanja” ameandika Okwi".

Okwi ambaye ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu soka Tanzania bara akiwa na mabao 8 aliumia kwenye kambi ya The Cranes ilipokuwa ikijiandaa na mechi ya kukamilisha ratiba ya makundi kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Ghana.
Klabu ya Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama ya 22, ikifuatiwa na klabu ya Azam FC yenye alama 22, huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na mabingwa watetezi Yanga SC yenye alama 20.

Rais Magufuli Amemteua Edwin Rutageruka Kuwa Mkurugenzi TANTRADE

$
0
0
Rais Magufuli Amemteua Edwin Rutageruka Kuwa Mkurugenzi TANTRADE
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amemteua Bw. Edwin Novath Rutageruka kuwa Mkurugenzi wa TANTRADE.

Alichokisema Masha Baada ya Kuruhusiwa Kurudi CCM Leo

$
0
0
Lawrence Kego Masha, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema kuwa amefurahi sana kupewa ridhaa ya kujiunga rasmi na CCM leo, Novemba 21, na kwamba atahakikisha anakitumikia ipasavyo.

“Nimefurahi sana kwamba nimepewa ridhaa na mwenyekiti wa Chama  cha Mapinduzi pamoja na Halmashauri Kuu kurejea nyumbani, kurejea CCM. Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kufuata ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuhakikisha kwamba nakitumikia chama na kulitumikia taifa jinsi inavyotakiwa. Kidumu Chama cha Mapinduzi,” amesema Masha.

Wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu cha CCM kinachoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais Magufuli, Masha alieleza kuwa yeye ni kada wa CCM tokea zamani kwani alilelewa na kukulia CCM, hivyo yeye kurudi CCM ni kama kurudi nyumbani na anajuta kufanya maamuzi ya kukihama chama hicho huku akitaka kutumiwa ili kukiendeleza chama hicho na kukiletea maendeleo.

“Mwaka 2015 nilifanya maamuzi ambayo sina sababu ya kueleza sana, nimezaliwa ndani ya chama hiki, nilipohama ilibidi nimfiche mzee Masha, akanipigia simu akanuliza umefanya nini? nikamuuliza kwani wewe chama gani? akaniambia mimi nilifukuzwa we umehama, amefurahi sana juzi nilipomwambia narejea CCM, Mheshimiwa Mwenyekiti na kamati yako, naomba mnikubali, naahidi nitakuwa mwaminifu kwa chama cha Mapinduzi na serikali yake, ukinihitaji nitumie“, amesema Lawrence Masha.

Masha ambaye alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka 2015 akitokea CCM, alitangaza tena kukihama CHADEMA hivi karibuni kwa madai kuwa upinzani hauna nia ya dhati ya kutafuta nafasi ya kuunda serikali, badala yake umejikita katika kuikosoa serikali.

Orodha Nzima ya Makada Mbalimbali Kutoka Vyama vya Upinzani Waliojiunga na CCM Leo

$
0
0

Chama cha Mapinduzi (CCM) leo katika Mkutano wa Kamati Kuu unaofanyikia Ikulu, Jijini Dar es Salaam, kimepokea maombi ya kujiunga na chama hicho kutoka kwa makada mbalimbali wa vyama tofauti vya upinzani.

Pamoja na hayo, pia Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesoma hadharani barua ya maombi ya kurudishwa CCM ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Bi Sophia Simba aliyefukuzwa uanachama kwa tuhuma za usaliti.

Makada kutoka vyama mbalimbali vya upinzani walioomba ridhaa ya kujiunga na CCM ni pamoja na Prof. Kitila Mkumbo, aliyekuwa Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo na wakili wa kujitegemea Albert Msando na Lawrence Kego Masha.

Wengine ni aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Patrobas Katambi, aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa ya Chama Cha ACT-Wazalendo Samson Mwigamba pamoja na Katibu wa Kamati ya Programu za Kijamii Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Hlmashauri Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo Edna Sunga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauto katika mkutano huo, makada hao wameeleza kuwa sababu zilizowapelekea kuvihama vyama vyao na kuomba kujiunga na CCM ni pamoja na kuridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya Rais Magufuli, CCM kuirudia misingi iliyowekwa na waasisi, juhudi za kupambana na rushwa na ufisadi, nidhamu na uwajibikaji pamoja na jihudi za kutetea na kupambania maendeleo kwa wanyonge.

Makada hao wameahidi kuonyesha ushirikiano na kukitumikia CCM pamoja na kutoa ushauri katika maeneo mbalimbali ikiwamo kuwashawishi wengine kujiunga na chama hicho pia.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwa pamoja wameridhia kuwapokea wanachama hao wapya pamoja na kumsamehe Bi Sophia Simba aliyekuwa amefukuzwa uanachama kwa tuhuma za usaliti.

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo...

$
0
0
MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Tupo Mbagala Rangi Tatu

Breaking News: Rais Robert Mugabe Ajiuzulu Urais Kabla ya Bunge Kumuwajibisha

$
0
0
Spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu . Kumekuwa na shangwe miongoni mwa wabunge kufuatia tangazo hilo. harakati za kumuondoa madarakani rais huyo kupitia bunge kumesitishwa.

Katika barua iliyosomwa na spika kwa wabunge hao, mugabe amesema amejiuzulu ili kukabidhi madaraka kwa njia ya amani


Taarifa rasmi kutoka chama tawala cha Zanu PF inasema ndani ya saa 48 zijazo Makamu wa Rais aliyefukuzwa Emmerson Mnangagwa atakuwa kiongozi wa nchi hiyo

Majanga Yazidi Kuikumba Clouds FM...Yapigwa Faini na TCRA Kwa Kukiuka Maadili

$
0
0
Mamlaka  ya udhibiti wa mawasiliano nchini (TCRA) imekitoza kituo cha redio cha Clouds FM faini ya shilingi milioni 12 ikiwa ni pamoja na kupewa onyo kali kwa sababu ya kukiuka maudhu na kanuni za utangazaji kupitia vipindi vya Jahazi na XXL.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  jijini Dar, Makamu  Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema Clouds FM imetozwa shilingi milino tano kwa kosa la kukiuka misingi na maudhui ya utangazaji kupitia kipindi cha Jahazi kwenye kipengele cha Mastori ya Town, shilingi milioni tano kupitia kipindi cha Jahazi kipengele cha Najua Wajua na shilingi milioni mbili kupitia kipindi cha XXL.

“Hata hivyo, tunaitaka Clouds Media Group kuwaomba radhi wasikilizaji wa vipindi hivyo kwa siklu tatu mfululizo na pia tunautaka uongozi wa Clouds Media Group kuwachukulia hatua za kinidhamu watangazaji wanaokiuka maadili, miiko na kanuni za utangazaji,” alisema Mapunda VIDEO:

Edward Lowassa Afungukia Kuhamia CCM....Afunguka Haya

$
0
0
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lowassa alisema jana Jumanne  kuwa  amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," alisema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema  .

Alisema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.

"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," alisema

Hatma ya Zamaradi na Clouds Media Baada ya Kuolewa

$
0
0
Wambea wenzangu ebu nipeni ubuyu,

Hivi Zamaradi bado yupo Clouds FM baada ya kuolewa? Simsikii Kabisa

Maana kusema kweli alikua anajua sana kutangaza especially kwenye kipindi cha TAKE ONE na LEO TENA, alikua anapatia kweli. Kama aliacha sasa hivi sijui atakua wapi ila namshauri aende hata AZAM TV kutangaza, maana kipaji anacho..Asiache Kipotee Bure

Kumbe Ukosefu wa Makalio Makubwa Unawafanya Wanawake Wasijikubali

$
0
0

VIDEO:Kumbe Ukosefu wa Makalio Makubwa Unawafanya Wanawake Wasijikubali

Tazama Hapa Chini Wanawake wakijadili kuhusu swala hilo linalowapa shida mtaani:

Mwanamke Kama Unatabia Hii Basi Neno Ndoa Utalisikia Kwenye Bomba

$
0
0
Hivi unajua kwanini mahusiano mengi katika karne hii yanakufa sana ukilinganisha na miaka ya zamani? Nini ambacho kimetokea miaka ya hivi karibuni? Naomba utafakari kwa muda usiopungua dakika tano kisha majibu ubaki nayo.

Binafsi leo sikuja kwa leo ya kuzungumzia sababu hizo, ila leo nataka niseme  na wanawake wote wenye tabia ya kupenda ganda la ndizi kuteleza, unawajua wanawake wenye tabia za aina hii kwa watalam wa masuala ya mahusiano wamewapa jina jipya ambalo ni magolipa.

Wao kazi yao kubwa ni kusubiri wanaume zao waende kutafuta ili hali wao wamekaa nyumbani wakisubiri kuletewa, wanawake wa aina hii kiufupi ukiwachunguza kwa umakini huwa hawana uchu wa mafanikio na maendeleo hata chembe. Na wanawake wa aina hii huwa wana uhusiano mzuri na romote control za tv.

Nataka nikuibie siri wewe mwanadada mwenye tabia ya aina hii, hivi unajua wanaume wengi katika utawala huu wa sizonje  hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’? kama ulikuwa hujui basi leo nakupa makavu live.

Hivi unajua  Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa, kusugua miguu akimsubiria mwanaume arudi akutelee, sasa hivi imepitwa na wakati? Kama ulikuwa hujui basi leo nakupa ukweli wako bure pasipo kuchangia hata mia mbovu.

Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.

Kabla sijamaliza kicheni part ya  leo nataka kukwambia ya kwamba maisha ni kutafuta, punguza kufanya vitu visivyokuwa wa maana katika maisha yako,punguza muda wa kukaa vibalazan huku macho yakikutoka huku kazi ikiwa ni kuwasema watu wengine.

Wewe ni mtu mzima mwenye meno 32, una akili timamu buana, tafuta shughuli za kufanya ambayo itakufanya uweze kujikiingizia kipato, binafsi naamini unaweza kwani ule msemo wa wahenga wapya ya kwamba wanawake wanaweza upo kwa ajili yako.

Jifunze kupambana na hali yako kama young killer muhasisi ya hip-hop asemavyo. Kukaa ukimsubiri shemela akuletee sio mpango mzima pia nidhambi na chukuzi kwa mwenyezi mungu.

Tanesco Wapewa Onyo na Serikali

$
0
0
Tanesco Wapewa Onyo na Serikali
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa Tanesco kuhakikisha kuwa hawakati umeme bila sababu maalum na hivyo kuwaondolea wananchi adha ya kukosa nishati hiyo.

Mh. Subira ametoa agizo hilo leo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa TEDAP unaohusu upanuzi na ujenzi wa vituo vya kupozea Umeme na njia za Umeme vya Mbagala, Gongo la Mboto, Kipawa na City Centre.
Amesema, umeme ukatike pale inapostahili tu, na endapo tatizo linatokea kwenye mifumo ya Umeme ni muhimu Tanesco ikatoa taarifa mapema kwa wananchi,na kwamba kukosekana kwa nishati hiyo kunaathiri shughuli nyingi hasa za kimaendeleo na kiuchumi zinazowaingizia kipato wananchi.
Aidha Naibu Waziri amewaagiza watendaji wa Tanesco wanaosimamia mradi huo wa TEDAP jijini Dar es Salaam, kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika tarehe 15 Desemba, mwaka huu.
Mradi wa TEDAP unahusisha upanuzi na ujenzi wa Vituo Vipya 19 vya kupoza Umeme wa Msongo wa kV 132/33 na kV 33/11 pamoja na ujenzi wa njia za Umeme wenye Msongo wa kV 132, kV 33 na kV 11 katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Kilimanjaro na utagharimu Dola milioni 43 zilizotolewa na Benki ya Dunia .


Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images