Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

JE Wajua Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo ya Kiume?

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE MADOGO?
Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia ,hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wenzao,kwakawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6_8 vinginevyo mtu huyu ana matatizo.



Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo baadhi ni,upungufu wa vichocheo (hornes) za gestrojen ambapo mwanaume anapobalehe vichocheo hivi (hormones)huchochea ujuaji wa uume.chango ambalo hushambulia nerve ambapo huharibu kabisa ukuaji wa uume, Punyeto ambayo huasili misuli ya uume,pia ngiri ambayo huleta maumivu ya tumbo kuunguluma na kujaa gesi,korodani moja kuvimba,kutopata choo vizuri,sababu hizi na nyinginezo hufanya uume kulegea na kisinyaa nakuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu zakiume (hamu ya tendo landoa hupungua au kuisha kabisa).NSUMBU,Nidawa inayozalisha hormones za gestrogene na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.NZAGI,Ni dawa ya kurudisha nguvu za kiume ,hutia hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha nakuponya kabisa tatizo hilo. Pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk 15 nakuendelea kwa tendo la kwanza.kumbuka dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji.Natunatibu kisukari,bp,ngiri,miguu kuwaka moto,namengine mengi.

WASILIANA OSTADHI JUMA KWA SIMU NO,0784002216 AU 0769597778


Mrithi wa Robert Mugabe Kuapishwa Ijumaa

$
0
0
Mrithi wa Robert Mugabe Kuapishwa Ijumaa
Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulisababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, anatarajiwa nchiuni humo siku ya Jumatano.

KIongozi huyo baadaye anatarajiwa kuapishwa rasmi Ijumaa, kulingana na shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC).

Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini , kulingana na Zanu-PF.

Kuondoshwa kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Bwana Mugabe.

Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.

Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa manane

Tizeba Ameagiza Kampuni Kutoa Mikataba Inayotambulika

$
0
0
Tizeba Ameagiza Kampuni Kutoa Mikataba Inayotambulika
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ameitaka Kampuni ya Mkonge ya China State Farms Agribusiness, inayofanya kazi zake mkoani Morogoro kuhakikisha inatoa mikataba inayotambulika kwa watumishi wake.

Dkt. Tizeba ametoa agizo hilo alipotembelea kiwanda cha Mkonge cha kampuni hiyo kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, baada ya kuapata malalamiko ya watumishi kukosa mikataba pamoja na kuwa wametimiza vigezo.
Baada ya kutembelea kiwanda hicho Dkt. Tizeba alipata nafasi ya kuonanan na wafanyakazi ambao walimweleza kero zao ambazo ni pamoja na mishahara duni, ukosefu wa mikataba na mazingira magumu ya kazi.
Kwa upande mwingine Waziri Tizeba, amewataka wawekezaji wa zao la Mkonge kutumia teknolojia itakayotoa faida zaidi na kuleta tija katika zao la Mkonge nchini sambamba na ukuaji wa pato la taifa kupitia zao hilo.
Katika mfululizo wa ziara zake mkoani Morogoro wazir Tizeba pia amepata nafasi ya kutembelea kiwanda cha Sukari cha Mkunazi 2 na kuwataka wawekezaji wa kiwanda hicho kuhakikisha kuwa uendeshaji wake hautaongeza bei ya Sukari bali utoe ahueni kwa wananchi wa hali ya chini kuweza kumudu bai za sukari.

Mahakama Imemuhukumu Miaka 20 Jela kwa Kukutwa na Kucha 17 za Simba

$
0
0
Mahakama Imemuhukumu Miaka 20 Jela kwa Kukutwa na Kucha 17 za Simba
Meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater ambae leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam imemuhukumu kwenda jela kwa miaka 20 baada ya kupatikana na hatia.

Pater amehukumiwa kwenda jela miaka 20 au kulipa faini ya Shilingi Milioni 534 baada ya kukutwa na kosa la kupatikana na kucha 17 za Simba.

Hukumu hiyo imetolewa leo November 22, 2017 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, ambapo amesema amesikiliza ushahidi uliotolewa na Mashahidi wanne wa upande wa mashtaka, vielelezo vitatu na utetezi wa Mshtakiwa mwenyewe.



Hakimu Mkeha amesema Mahakama imemkuta na hatia Mshtakiwa huyo baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi hiyo pasipo kuacha shaka na kueleza kuwa vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani hapo ni kucha za Simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo mshtakiwa alishindwa kulipa faini na kupelekwa gerezani.

Picha: Irene Uwoya Akiwa Kwenye Kaburi la Ndikumana, Aandika Ujumbe Huu

$
0
0
Picha: Irene Uwoya Akiwa Kwenye Kaburi la Ndikumana, Aandika Ujumbe Huu
Mume wa zamani wa Mwigizaji Irene Uwoya, Hamad Ndikumana alifariki ghafla wiki iliyopita huko Rwanda sekunde chache baada ya kuomba soda ya baridi na kunywa ambapo Irene alifanikiwa kusafiri mpaka kwao kwenda kutoa pole kwa familia.

Baada ya taarifa hizo Irene Uwoya alifunga safari baadae na kwenda kutoa pole kwa familia ya Ndikumana ambapo ameonekana akiwa na Mtoto wao Krissh juu ya kaburi la Ndikumana na kuandika “My trust is in you …R.I.P baba krissh”

Kwenye hizi picha hapa chini anaonekana akiwa nyumbani kwa kina Ndikumana na ndugu zake na juu ya kaburi la Ndikumana pia ambapo  Irene alipewa baraka na Baba Mzazi wa Ndikumana



Davina Awatetea Viben Ten " Mapenzi Hayachagui Umri"

$
0
0
Davina Awatetea Viben Ten " Mapenzi Hayachagui Umri"
LICHA ya wengi kuwaponda wanawake wenye umri mkubwa wanaokuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wadogo kiumri ‘viben’ten’, staa wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amewatetea kwa kusema siyo vibaya kwani mapenzi hayana umri.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Davina alisema licha ya kutowahi kuwa na kiben’ten, haoni tatizo kwa wanaokuwa na uhusiano na wanaume hao wadogo kwa kuwa siku zote mapenzi hayachagui umri, dini wala kabila bali mtu hujikuta amependa tu.

“Sijawahi kuwa na kiben’ten huwa naona ni bora kuwa na mtu ambaye tunalingana kiumri au amenizidi kidogo, wanawake wanaokuwa na wanaume hao wadogo siwezi kuwalaumu au kuwacheka kwa sababu mapenzi ni kitu ambacho hakizuiliki wala hakichagui,” alisema Davina.

Makamu wa Rais wa Zimbabwe Akataa Kurudi Nyumbani

$
0
0
Makamu wa Rais wa Zimbabwe Akataa Kurudi Nyumbani
Wakati Emmerson Mnangagwa alipofutwa kazi wiki mbili zilizopita hakuwa makamu wa rais wa pekee nchini Zimbabwe
Phelekezela Mphoko ni makamu wa rais mwengine ambaye anajulikana kwa kumuunga mkono mkewe rais Mugabe na kulingana na sheria anapaswa kumrithi Mugabe.
Hatahivyo chama cha Zanu PF kimsema kuwa Mnangagwa ataapishwa kufuatia uamuzi uliochukuliwa na kamati yake kuu siku ya Jumapili.
Bwana Mphoko alikuwa ameondoka katika taifa hilo wakati Jeshi lilipochukua mamlaka wiki moja iliopita, na kulingana na gazeti la NewsDay hajarudi nyumbani kwa kuwa anahofia kukamatwa.
Gazeti hilo limenukuu duru akisema kuwa amebadilisha mipango yake ya usafiri.
Alitarajiwa kurudi nchini zimbabwe kufikia siku ya Ijumaa , kutoka Tokyo Japan.
Lakini duru zimesema kuwa anataka tiketi zake za usafiri kubadilishwa ili aelekee Zambia au Msumbiji .
Anajua anaogopa kukamatwa kwa sababu anatakikana kwa kuzuia haki na kufanya ufisadi.

Waziri Mwijage Aweka Jiwe la Msingi Katika Kiwanda cha Usambazaji Vifaa vya Ujenzi

$
0
0
Waziri Mwijage Aweka Jiwe la Msingi Katika Kiwanda cha Usambazaji Vifaa vya Ujenzi
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijange, leo ameweka jiwe la msingi eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ambapo kiwanda hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwijage ameipongeza kampuni ya CNBM ya China kwa namna ambavyo imedhamiria kuwekeza hapa nchini kwa kuanzisha kituo cha usambazaji wa vifaa hivyo.

Alisema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.

Aliwapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.

Alisisiza kwamba kituo hicho kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho.

Naye Balozi mpya wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, alimpongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu

Tanzia:Meya wa Jiji Dar wa Zamani Amefariki Dunia.

$
0
0
Meya wa Jiji  Dar wa Zamani Amefariki Dunia.
Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Kleist Sykes amefariki dunia.
Familia imesema Sykes amefariki dunia leo Jumatano Novemba 22,2017 asubuhi na mipango ya mazishi inaendelea kufanyika.
Skyes aliyekuwa meya mwaka 2000-2005 amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Dully Sykes ambaye Kleist ni baba yake mkubwa akizungumza na Mwananchi amesema meya huyo wa zamani amefariki dunia leo saa mbili asubuhi.
“ Yaah, kweli amefariki na sasa familia tumeanza kukutana kujua mazishi yatafanyika lini,” amesema.
Meya wa sasa wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na Mwananchi amesema hivi karibuni alimtembelea hospitalini alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.
Mwita amesema kuna wakati Sykes alimtembelea ofisini kwake na alimpa ushauri kuhusu utendaji kazi.
“Ni mtu tuliyeelewana, amewahi kuja hapa ofisini kwangu kama mara mbili na kunishauri haya na yale kuhusu kazi zangu,” amesema.
Kleist Sykes aliyekuwa diwani wa Kivukoni mwaka 2000 hadi 2005 anatoka katika familia ambayo ni miongoni mwa zenye wanasiasa walioshiriki katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Dully Sykes Awatupia Lawama Wasanii wa Bongo Fleva

$
0
0
Dully Sykes Awatupia Lawama Wasanii wa Bongo Fleva
Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes amewalalamikia wasanii wadogo kiumri kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa kukosa upendo na umoja baina yao kwa kutokupeana sapoti kwenye kazi zao.

Dully amesema Wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye muziki ambao amewaita madogo hawana upendo wala umoja katika kusapotiana na kudai kuwa sio tu kwa wasanii wakongwe bali hata hao wenyewe kwa wenyewe na kuwafananisha na mdudu Kaa.

“Vijana wa sasa hivi wanatakiwa wajifunze kupendana, vijana wa sasa hivi hawapendani yaani hawana mapenzi, hawana ule upendo wamekuwa kama Kaa, Mimi nilijaribu kutuma posti yangu (ya wimbo mpya) juzi nikitegemea kupata nguvu nyingi kutoka kwa vijana lakini imekuwa tofauti na nilivyofikiria kwani wazee wenzangu ndio wamenipa sapoti akina Rich One, akina Mwana FA ndio walinisapoti na ndio walikuwa na furaha, kuna vijana wengine mpaka wanasema  kwamba nimetoa wimbo lakini hawajui  kama mimi nimetoa wimbo, wengine wanasema nitakupostia lakini hawaposti.“amesema Dully Sykes kwenye mahojiano yake na Radio Free Afrika Kwenye kipindi cha New Chapter na kuwapa ushauri wasanii hao

“Sasa mimi naomba tu kuwambia wale vijana ambao wanahisi labda muziki ni wa kwao peke yao hapana.. Unajua Mungu sisi wengine sisi ametupa utofauti mimi nakula majani kama Twiga wakae watulie, hao watakula majani chini kama Mbuzi, mimi nitakula ya juu, Wakae watambue kuwa wasishindane na Tembo wataumiza makalio.”

Soma na Hii – Hili ndio jibu la Dully Sykes kwanini wimbo wake mpya kauita ‘Bombardier’

Dully Sykes kwa sasa anafanya vizuri kwenye Media na wimbo wake wa Bombardier ambao umewavutia watu wengi kwenye aina ya uandishi hadi video ya wimbo huo.

Mhasibu Aliyeondolewa kwa Vyeti Feki Adaiwa Kutumia Funguo Bandia Kuiba Fedha Hospitalini

$
0
0
Mhasibu Aliyeondolewa kwa Vyeti Feki Adaiwa Kutumia Funguo Bandia Kuiba Fedha Hospitalini
Mhasibu aliyeondolewa kazini kwa vyeti feki, anashikiliwa na polisi akituhumiwa kuiba fedha katika Hospitali ya Mkoa wa Singida akitumia funguo bandia kuingia ofisi ya uhasibu aliyowahi kufanya kazi.

Edith Talasi (49), mkazi wa Minga mjini Singida anayetuhumiwa kuiba Sh873,000 imeelezwa alifanya kazi hospitalini hapo kwa muda na baadaye alirejeshwa katika kituo chake cha kazi ambacho ni Manispaa ya Singida.

Talasi anashikiliwa pamoja na Anthony Felix (51), ambaye ni mlinzi wa nyumba yake ya  kulala wageni iitwayo Nandau.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 22,2017 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea jana Jumanne Novemba 21,2017 saa 6:30 usiku katika hospitali ya mkoa.

Akielezea tukio hilo, amesema muuguzi wa zamu Shamir Omari (27) alipotoka mapokezi akielekea wodini alimwona mtu akiwa amesimama jirani na ofisi ya mhasibu ambaye baada ya kumsalimia aliondoka.

“Muuguzi aliamini mtu aliyemwona huenda  alikuwa mgonjwa au ndugu wa mgonjwa lakini aliporudi alimwona tena eneo lilelile hivyo alimshuku kuwa si mtu mzuri,” amesema Kamanda Magiligimba.

Amesema muuguzi alitoa taarifa kwa mlinzi wa zamu wa hospitali hiyo, Abubakari Jumanne ambaye alimweka chini ya ulinzi mtu huyo ambaye ni mtuhumiwa Felix.

Kamanda Magiligimba amesema mtu huyo alijitetea kuwa alifika hospitalini kuchoma sindano akionyesha dawa alizokuwa nazo.

“Wakati wanaendelea na mahojiano waliona makufuli mawili ya mlango wa nje wa chuma yapo chini na mlango ukiwa wazi. Mtuhumiwa alieleza bosi wake kwa wakati huo alikuwa ndani ya ofisi ya mhasibu amejifungia ndani,” amesema.

Amesema polisi walipatiwa taarifa na kufika eneo la tukio ambako walikutwa mlango ukiwa umefungwa kwa ndani.

Kamanda Magiligimba amesema mhasibu wa hospitali alipoamriwa afungue mlango kwa kutumia funguo zake, mtuhumiwa Edith akikutwa akiwa amejibanza kwenye kona ya mlango.

Amesema watumishi wa hospitali hiyo walimtambua kuwa aliwahi kufanya kazi hapo.

Alipohojiwa ameingiaje ndani, Kamanda Magiligimba amesema alionyesha funguo saba na zilipojaribiwa zilifungua milango yote ya ofisi ya mhasibu.

Amesema mbali ya wizi wa Sh873,000, imeelezwa Aprili,2017 wahasibu wa hospitali hiyo walibaini upotevu wa Sh1.8 milioni na Oktoba mwaka huu walibaini upotevu wa Sh3.6 milioni.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk David Mwasita amekiri kutokea upotevu wa fedha hizo na kwamba wahasibu walilipa kwa fedha zao za mishahara.

Dk Mwasita amesema wahasibu walilazimika kutoa fedha zao binafsi hivyo wasingeweza kutoa taarifa ya upotevu kwa kuwa milango na sefu ilikuwa imefungwa kama kawaida.

Kamanda Magiligimba amesema  wanaendelea kuwahoji watuhumiwa na baada ya mahojiano kukamilika watafikishwa mahakamani.
Chanzo: Mwananchi

Serikali Kutoa Ajira za Uhakika Sekta ya Uvuvi

$
0
0
Serikali Kutoa Ajira za Uhakika Sekta ya Uvuvi
Serikali  imesema inampango mkakati mzuri katika kuendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi na kutoa ajira za uhakika kwa Watanzania ambao wanafanya shughuli hiyo.

Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta amesma hayo akiwa Soko la Samaki Msasani wakati akifunga maadhimisho ya Siku ya Mvuvi ambayo iliambatana na utoaji wa zawadi kwa wavuvi waliofanya vizuri katika mashindano yakuvua samaki kwa vitumbwi na ngalawa yalioandaliwa na taasisi ya Tuna ambapo mshindi wa kwanza alipata tsh 400,000, wapili tsh 300,000 na wa tatu tsh 200,000.

Alisema serikali  imesema  inampango na mkakati mzuri katika kuliendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi ili sekta hiyo iweze kufanya vizuri na kusonga mbele zaidi

Meya alisema wavuvi  wanapaswa kuwa wabunifu ili kusaidia sekta hiyo kufanya vizuri zaidi

Afisa Uvuvi wa Manispaa Kinondoni Bi Grace Kakama akizungumza katika kilele hicho amesema kama kuwa watahakikisha wavuvi wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili waweze kuinuka kwa kipato zaidi.

Mamba Mweupe Mwenye Umri Mkubwa Aonekana Mtoni

$
0
0
Mamba Mweupe Mwenye Umri Mkubwa Aonekana Mtoni
Kuonekana kusiko kawaida kwa mamba mweupe mwenye umri mkubwa kumewasisimua wanaofanya shughuli za utalii katika eneo la Kaskazini mwa Australia.

Mnyama huyo wa jamii ya wanyama watambaao , aliyepewa jina la bandia -Pearl, alionekana katika ziwa Adelaide River katibu na eneo la Darwin siku ya Jumapili

Mtu mmoja aliyemuona, ambaye ni mwanaharakati wa hifadhi ya mazingira , alikadiria kuwa mamba huyo alikuwa na urefu wa mita takriban 3 za urefu.

Muonekano wa weupe wa rangi wa mnyama huyo umetokana na hali ya hypomelanism - inayosababishwa na ukosefu wa madini ya mwili yanayotengeneza ngozi melanin, kulingana na wataalam wa masuala ya wanyama..

Wakazi wa eneo lililo karibu na mto Adelaide wanaamini mnyama huyo ana uhusiano na mamba mwingine anayefahamika kuwa na hali hiyo ya afya ya mwili ambaye aliwahi kumuua mvuvi mnamo mwaka 2014.

"Kila mmoja anaelezea furaha yake ," alisema rais asiye rasmi wa kikundi cha uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja kama Broady.
"Nilishinda siku nzima nikitokwa na machozi ya furaha nikimtazama."

Muwindaji alaliwa na kuuwawa na ndovu Zimbabwe
Mamba mkubwa Big Daddy kufanyishwa ndoa Mombasa
Alama ya SOS huenda ikapata ufumbuzi Australia


Ni Kwanini mamba ni mweupe?

Wengi miongoni mwa mamba nchini Australia wanarangi za kijivu na kijani, jambo linalowawezesha kutoonekana kwa urahisi



Hitilafu ya kimwili ya Mamba Pearlhuenda ilistokea kupitia Jeni ama wakati wa kutengenezwa kwa yai , alisema Adam Britton, mtafiti msaidizi katika chuo kikuu cha Charles Darwin University.

"Wakati wa kutotoa kama mayai yatakuwa moto zaidi kiasi , inaweza kusababisha hitilafu katika kitengo cha seli na hivyo kusababisha kumeguka ," Alisema Bwana Britton.

Alisema matokeo yake yanaweza kuwa ni pamoja na "kuondolewa kwa rangi ya mwili au sehemu nyingine ya magamba kwenye mwili ".

Ni hali ya nadra ?

Mamba hao si " ni wa kawaida kuonekana'' wakiwa na umri mdogo wanapokuwa na umri mdogo, hususan katika hifadhi ya mamba, kwa mujibu wa Bwana Britton.

However, it is difficult for a pale juvenile to steer clear of predators.



"Ni jambo lisilo la kawaida kidogo kumuona mamba mwenye umri mkubwa akiwa na rangi nyeupe kiasi hicho ," Bwana Britton alisema.

"Nimeisha waona mamba kama huyu kila mara, lakini si mkubwa kiasi hiki mwituni

Kujiuzulu kwa Mugabe: Kimya Kirefu cha Rais Zuma Chawashangaza Wengi

$
0
0
Kujiuzulu kwa Mugabe: Kimya Kirefu cha Rais Zuma Chawashangaza Wengi
Kimya kirefu cha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma pamoja na chama chake tawala cha ANC kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe kinashangaza.
Kinaonyesha ushawishi wa kisaikolojia aliyokuwa nao kwao na walishangazwa sana na hatua aliyochukua.
Kile afisi ya rais Zuma ilichosema ni kwamba hatoweza tena kuelekea nchini Zimbabwe kama alivyokuwa amepanga ili kupatanisha kbal ya rais Mugabe kutangaza kujiuzulu.
Ziara hiyo sasa imeahirishwa hadi tyangazo jingine , taarifa ilisema.
Lakini badala yake chma cha upinzani nchini Afrika Kusini DA kilijibu na hivyobasi kuungwa mkono na raia weusi pamoja na wazungu kiliposema:
Huu ni ushindi wa raia wa Zimbabwe ambao wametaabika chini ya uongozi wa Mugabe .Habari ya bwana Mugabe sio geni na kwamba inaendelea katika bara la Afrika.Mtu aliyekuwa shujaa wa taifa lake , Mugabe alisababisha migawanyiko, ukosefu wa udhabiti na kuharibika kwa uchumi wakati alipobadilika kutoka kuwa mpiganiaji wa uhuru hadi kuwa dikteta.Hilo sio tu kwa Mugabe bali hata Zanu -PF chama ambacho amekitawala kwa kutumia nguvu kwa kuchukua mamlaka tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.Chama cha ANC kinaonyesha ishara kama zile za Zanu-PF, kimekumbwa na ufisadi mkubwa na ghasia huku pande pinzani zikipigania madaraka katika serikali kwa lengo la kujitajirisha badala ya kuwahudumia wananchi.Baada ya kuchukua madaraka miaka 23 kutoka kwa wazungu ,ANC sasa kinakabiliwa na changamoto ya kujiimarisha au tishio la kuangamiza uchumi wa Afrika kusini kama Zanu-Pf kilivyofanya kwa miaka 37.

EXLUISIVE: Mtoto Wa Tajiri Mtata Dr Shika Afunguka

$
0
0
EXLUISIVE: Mtazame Anayesemekana ni Mtoto Wa Tajiri Mtata Dr Shika Akifunguka



Aliemlipa LULU Michael Pesa kabla ya Kwenda Jela Afunguka Mazito

$
0
0
Isike Samweli ni Mwigizaji na Mkurugenzi wa kampuni ya Halisi Filamu ambapo kwenye hii video amezungumzia taarifa za kwamba amekua na uchungu wa fedha zake alizomlipa Mwigizaji Lulu ambaye hivi karibuni alihukumiwa kwenda jela miaka miwili. VIDEO:

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

$
0
0


THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.

Huyu Ndio Rais Mtarajiwa wa Zimbabwe.. Amewasili Harare Kwa Ajili ya Kuapishwa

$
0
0
Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerudi nchini humo kutoka Afrika Kusini.

Anatarajiwa kutoa hotuba yake katika makao makuu ya chama cha Zanu-PF mjini Harare.

Katambi Amjibu Mbowe, Amwambia Hanunuliki

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amesema tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba amenunuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hazina ukweli.

Katambi ambaye jana alitangaza kujiunga na CCM ametoa kauli hiyo kipindi ambacho kumekuwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake  ikiwamo ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba ameshawishiwa na akakubali.

Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 22, Katambi amesema hakuna mtu yoyote anayeweza kumnunua huku akisema Chadema kimepoteza dira hivyo wenye uelewa wataondoka.

“Nimesikia mengi, nitafanya mkutano na waandishi wa habari, nilidhani wangejitathimini katika ukweli ili kusaidia vijana, chama na taifa lakini kama wanaamua kushambulia mtu kwa uongo bila ushahidi, nitasema ukweli waziwazi,” amesema Katambi

Kuhusu tuhuma za rushwa, Katambi amesema ‘’Katambi hanunuliki wala hana bei naishi katika Principle…kwa wenye akili wangejua dira imepotea watafute upya masafa.”

Awali leo asubuhi, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni akizungumza  na Mwananchi kuhusu kuondoka kwa Katambi amesema;

"Badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashwishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa."

Mwananchi:

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe akutana na rais Jacob Zuma Afrika Kusini

$
0
0
Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amekutana na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati ambapo anasubiriwa kurudi nyumbani leo.

Bwana Zuma alitarajiwa kuwasili atika mji mkuu wa Harare leo ili kuwa mpatanishi wa mgogoro uliokuwa ukiendelea lakini akafutilia mbali zaiara hiyo baada ya rais Mugabe kujiuzulu.

Afisi ya rais Zuma ilituma ujumbe wa Twitter wa picha za mkutano wao.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images