Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kwa Spika wa Bunge Kufuatia Kifo cha Mbunge wa Songea Mjini

$
0
0
Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kwa Spika wa Bunge Kufuatia Kifo cha Mbunge wa Songea Mjini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri, Mhe Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Tutubert Gama.

Mbunge wa Songea Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Peramiho, Ruvuma.


Sethi wa IPTL na Wenzake Mambo Bado Magumu Warudishwa Rumande

$
0
0
Sethi wa IPTL na Wenzake  Mambo Bado Magumu Warudishwa Rumande
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo ijumaa Novemba 24 2017, imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara, James Rugemarila hadi Desemba 8, 2017, kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Upande wa mashtaka umemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa wanaomba upelelezi ukamilike kwa haraka kwasababu hali ya mshtakiwa mmoja si nzuri.

Harbinder Singh Sethi pamoja na Mfanyabiashara James Rugemarila, kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya zaidi ya Bilioni 3.

Waziri Mkuu Atoa Mwezi Mmoja Kwa Ofisa Ardhi Kutoa Fidia kwa Wananchi

$
0
0
Waziri Mkuu Atoa Mwezi Mmoja Kwa Ofisa Ardhi Kutoa Fidia kwa Wananchi
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ametoa mwezi mmoja kwa Ofisa Ardhi wa wilaya ya Namtumbo Bw. Maurus Yera kuhakikisha anatafuta ardhi ya kuwafidia wakazi wa kijiji cha Lwinga wilayani humo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Lwinga wilayani Namtumbo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.
“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya sikukuu ya Krismasi mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi wake waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa.”
Jumla ya wananchi 21 wanaidai halmashauri ya Namtumbo eneo lenye ukubwa wa ekari 101, ambazo mwaka 2008 zilitwaliwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupisha ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa Ruvuma kwa ahadi ya kulipwa fidia jambo ambalo halijatekelezwa hadi leo.
Waziri Mkuu amesisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtumishi ahakikishe anatumia taaluma yake vizuri kwa kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili kwa wakati.

Huyu Hapa Mwanamke Anayetunza Mayai Yake ya Uzazi Kwenye Barafu

$
0
0
Huyu Hapa Mwanamke Anayetunza Mayai Yake ya Uzazi Kwenye Barafu
Rita Ora amefichua kuwa aliweka mayai yake ya uzazi kwenye barafu baada ya miaka 20 alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Televisheni ya Australia .
Muimbaji huyo wa raia wa Uingereza, ambaye sasa ana umri wa miaka 26 alisemakuwa madaktari walimpenekezea upasuaji wa kuyaondoa mayai hayo mwilini mwake kwasababu " amekuwa akitaka kuwa na familia kubwa".

"Daktari alisema: 'una afya nzuri sasa na itakuwa vema, kwa nini usiyaondoe mayai yako ya uzazi uyatunze , halafu hautakuwa na hofu ya kuwakosa watoto tena ?'," alisema Rita.
Daktari Helen O'Neill, wa chuo kikuu cha London ,anasema: : " Ni bora kuondoa mwilini mwako na kuyatunza mayai yako ya uzazi mapema kuliko kusubiri."

Lakini ni ''hakikisho kamili'' la kupata ujauzuito na wasichana wengi hawawezi kugaramia garama ya upasuaji na utanzaji wa mayai ya uzazi ambayo ni Euro -£5,000 kila mzunguko mmoja wa hedhi.
Janet Jackson mja mzito akiwa miaka 50

Daktari O'Neil anasema : "Faida za kuyatunza mayai ya uzazi kwenye barafu ni kwamba unachukua jukumu la kutumga mimba mikononi mwako . Kama ukifanyiwa uchunguzi na ikibainika kwamba una uwezo mdogo wa kutpata ujauzito ni vema kuchukua hatua mapema."
Vibandiko vya njia ya uzazi vyadhuru wanawake

Anasema kuna upungufu mkubwa wa mayai bora ya uzazibaada ya mwanamke kufikia miaka 30 - na kwamba ubora huo huendelea kupungua kadri miaka inavyokwenda.
"Bahati mbaya watu wengi huanza kutunza mayai yao ya uzazi wakiwa na umri wa miaka 35, ambapo wanakuwa wamechelewa kidogo ," alielezea.


Nchini Uingereza , idadi ya wanawake wanaotunza mayai yao ya uzazi kwa ajili ya kupata watoto baadae imeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Mwaka 2014, wanawake 816 walitunza mayai yao kwenye barafu kwa ajili ya uzazi wa baadae ilipanda na kufikia hadi asilimia 25% mwaka 2013, kulinga na takwimu za hivi karibuni kutoka mamlaka ya inayofuatilia masuala ya uzazi wa kusaidiwa nchini humo (HFEA).
Hospitali ya wanawake ya London ya mtaa wa Harley, hivi karibuni iliripoti kuwa idadi ya wanawake wanaohudhuria kliniki zake za uzazi wa kusaidiwa fimeongezeka mara tatu kitika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kiwango cha uzazi wa kupozesha mayai kwenye friji kilikuwa ni sawa na 14% mwaka 2013, kulingana na mamlaka ya HFEA. Kiwango kilikuwa cha chini kwa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 38.
Bi Ora anasema alikuwa anatambua tayari kwamba mchakato huo haumaanishi kuwa ana uhakika wa kupata watoto baadae ,alisema : "Nafahamu watu wanaweza kusema , aah! lakini ana umri mdogo '. Nilitaka tu kuchukua tahadhari''.

Uongozi wa Simba Wampa Okwi Uangalizi Mzito

$
0
0
Uongozi wa Simba Wampa Okwi Apewa Uangalizi
KUFUATIA kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, Emmanuel Okwi kuwa majeruhi wa enka, uongozi wa klabu hiyo, umetoa rai kuhakikisha mchezaji huyo anapewa uangalizi wa hali ya juu kuona anafanikiwa kupona haraka kutokana na umuhimu wake katika kikosi hicho.

Okwi ndiye anayeongoza kwa kufunga mabao kwenye ligi kuu kwa sasa kutokana na kuwa na mabao nane akifuatiwa na Obrey Chirwa wa Yanga na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons ambao wote wana mabao sita.
Okwi alipata majeraha ya enka kabla ya mechi dhidi ya Prisons ya Mbeya ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu.


Taarifa ambazo Championi Ijumaa limezipata kutoka Simba ni kwamba uongozi wa timu hiyo umemkabidhi jukumu Dk Yasin Gembe kuhakikisha anakuwa na uangalizi wa hali ya juu kwa mchezaji huyo kutokana na majeraha aliyonayo.


“Uongozi umetaka Okwi awe chini ya uangalizi wa dokta kutokana na majeraha aliyonayo, kwa kuwa ndiye kinara wa mabao, hivyo ni vyema akaangaliwa ili aweze kupona kwa haraka na kurejea mzigoni,” alisema mtoa taarifa huyo.


Simba inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 22 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 20 ambapo timu zote zimeshuka dimbani mara 10, hali ambayo inaonyesha ni jinsi gani ligi imekuwa ngumu.

Breaking: Nyumba za Lughumi alizoshindwa kununua'' Dr. SHIKA'' zinapigwa mnada

$
0
0

Breaking: Nyumba za Lughumi alizoshindwa kununua'' Dr. SHIKA'' zinapigwa mnada

Dkt Slaa Afunguka Kuhusu Kuteuliwa Kuwa Balozi ' Nipo Tayari Kutoa Mchango Wangu'

$
0
0
Dkt Slaa Afunguka Kuhusu Kuteuliwa Kuwa Balozi ' Nipo Tayari Kutoa Mchango Wangu'
Aliyekuwa Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt.  Wilbroad Slaa amezungumzia hatua aliyoichukua Rais John Magufuli kumteua kuwa Balozi.

Dkt. Slaa amesema ubalozi ni nafasi ambazo zipo katika himaya ya Mkuu wa Nchi hivyo bila shaka hadi Rais kufikia hatua ya kumteua atakuwa na sababu za uteuzi huo.

“Hatimaye kama ni mapenzi wa Mungu namshukuru kwa uteuzi huo ninachoweza kusema katika hatua hii ni kwamba ni wajibu mkubwa katika kipindi hiki cha kujenga taifa letu. Kama ni kutoa mchango wangu nitakuwa tayari kutoa, Mwenyenzi Mungu akinisaidia” Dkt. Slaa amekiambia kituo cha runinga cha Azam.

Hapo jana November 23, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Magufuli alimteua Dkt. Wilbroad Slaa kuwa Balozi na inatarajiwa ataapishwa pindi taratibu zikikamilika.

Robinho Afungwa Miaka Tisa Jela Nchini Italia kwa Kosa la Ubakaji

$
0
0
Mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Real Madrid, Robinho
Mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Real Madrid, Robinho amefungwa miaka tisa jela nchini Italia kwa kosa la kushiriki kubaka msichana kutoka Albania.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa Robinho alishiriki katika ubakaji huo Januari mwaka 2013 wakati akiichezea klabu ya AC Milan inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia, maarufu kwa jina la Serie A.

Robinho, ambaye ameichezea timu ya taifa ya Brazil michezo 100, alipatikana na hatia ya kubaka msichana mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni raia wa Albania. Hata hivyo, nyota huyo wa zamani hakuwepo kortini.

Watu wengine watano pia walishtakiwa kwa kosa hilo, lakini hukumu yao bado haijajulikana.

AFP imekariri gazeti la kila siku la jijini Milan, Corriere della Sera, likisema kuwa Robinho na marafiki zake watano walimlewesha msichana huyo "kiasi cha kutojitambua na hivyo kutoweza kuwakatalia".

Baadaye walichangia kufanya naye ngono kwa kuachiana.

Je Dada Unapenda Kuwa Mrembo na Kaka Unakosa Hamu ya Tendo au Uume Mdogo?

$
0
0
BAADA YA UTAFITI TULIOFANYA MARKSON BEAUTY  TUMEGUNDUA KUWA  WANAUME WENGI DUNIANI HUSUMBULIWA NA MATATIZO KAMA👇👇
☆Kukosa hamu ya tendo.
☆Kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo.
☆Maumbile madogo ya uume.
☆Kuchoka sana wakati wa tendo na uume kusinyaa  nk.
      @markson_beauty_pr tumeandaa tiba bora kabisa kama ifuatavyo:-
1.HANDSOME UP OG_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @250,000/=
2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @150,000/=
3VigRX  CREAM_ Inaongeza uume inch 6.5 hadi 8 (wiki 2-3) @200,000/=
4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @150,000/=
5.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @150,000/=
     PIA KWA WANAWAKE WANAOPENDA KUWA NA MUONEKANO MZURI ZIPO ZA👇👇👇
☆Kuongeza hips, makalio na mapaja @200,000/=
☆Kushepu mguu (CHUPA YA BIA) @150,000/=
☆Kuwa mweupe bila sugu @150,000/=
☆Kurefusha nywele na kutokukatika ovyo @150,000/=
☆Kupunguza au kuongeza maziwa kuyasimamisha @130,000/=
*Kubana uke na kuzuia uchafu ukeni @130,000/=
*Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
     BIDHAA HIZI NI ZA MIMEA NA MATUNDA NA ZIMEPIMWA KTK MAMLAKA NA KUPATA KIBALI HIVYO NI SALAMA KWA 100%

    Wasiliana nasi Popote
  ulipo duniani kwa (+255)
           0767447444 au
              0714335378
        UTAPATA HUDUMA
    NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON BEAUTY CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
        Follow us
WEBSITE:- www.markworldbeauty.og
INSTAGRAM PAGE:-
@markson_beauty_pr

Nyumba za Lugumi Zakosa Mteja Wanunuzi Washindwa Kufikia Bei Elekezi

$
0
0
Nyumba za Lugumi Zakosa Mteja Wanunuzi Washindwa Kufikia Bei Elekezi
Jumba la kifahari la mfanyabiashara, Said Lugumi limekosa mteja wa kulinunua.

Katika mnada uliomalizika Leo mchana Novemba 24 Mbweni JKT, ulioendeshwa na Kampuni ya Udalali ya Yono, wanunuzi waliojitokeza wameshindwa kufikia bei elekezi

Mkurugenzi wa Kampuni ya Yono, Scholastika Kevela amesema wateja waliojitokeza wamefikia Sh510 milioni ambayo iko chini ya mategemeo.

"Tunahamia nyumba ya Upanga, kama atapatikana mteja leo tunaweza kurudi na tukamuuzia na masharti ni yaleyale kwamba lazima mteja akifika bei alipe hapa hapa asilimia 25 na asilimia 75 ndani ya siku 14," amesema Kevela

Nyumba hii imeshindwa kununuliwa kwa mara ya tatu baada Septemba 7 kujitokeza kama leo na Novemba 9 ambao unadaiwa ulivurugwa na 'Bilionea' Dk Louis Shika.

Tofauti na ulivyokuwa Novemba 9, leo kila aliyefika katika mnada huo alitakiwa kujiandikisha ikiwamo waandishi wa habari huku ulinzi ukiwa umeimarishwa  zaidi .

Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais Mpya wa Zimbabwe Mamia ya Watu Wajitokeza Katika Sherehe Hizo

$
0
0
Mnangagwa Aapishwa Kuwa Rais Mpya wa Zimbabwe Mamia ya Watu Wajitokeza Katika Sherehe Hizo
Raia wa Zimbabwe wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo mjini katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare kwa ajili ya sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa.
Emmerson Mnangagwa anatarajiwa kuapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kuondoka kwa rais kuondoka kwa Robert Mugabe madarakani baada ya miaka 37 ya utawala wa kiimla.

Makamu huyo wa zamani wa rais ambaye alirejea kutoka uhamishoni Jumatano -ataapishwa kaka uwanja michezo wa Harare.
Kufutwa kwake kazi mwezi huu kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang’atuke .
Upinzani unamtaka Bwana Mnangagwa, ambae amekuwa mmoja wa watawala kumaliza “utamaduni wa ufisadi”. Taarifa ya kuondoka madarakani kwa Mugabe mwenye umri wa miaka 93 hapo siku ya Jumanne iliibua sherehe kubwa kote nchini Zimbabwe.

Rufaa Yamponza Oscar Pistorius Mahakama Yamuongezea Kifungo Hadi Miaka 13

$
0
0
Rufaa Yamponza Oscar Pistorius Mahakama Yamuongezea Kifungo
Mahakama kuu ya rufaa nchini Afrika Kusini imemuongeza adhabu ya kukaa jela mwanariadha na mshindi wa Olimpiki Oscar Pistorius kutoka miaka 6 hadi 13 kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Hukumu iliyotolewa na mahakama asubuhi hii mjini Bloemfontein imebatilisha kutoka kifungo cha miaka 6 jela alichokuwa amepewa awali mwanariadha Oscar Pistorius hadi kifungo cha miaka 13 na miezi 5 jela.
Jaji wa mahakama hiyo ya rufaa Willie Seriti amesema kwamba Pistorius ilibidi ahukumiwe jela miaka 15 lakini mahakama imeangalia muda ambao tayari ameshakaa jela hivyo kumpunguzia hadi miaka 13.

Oscar Pistorius ambaye ni mlemavu wa miguu, alipatikana na hatia ya kumuua kwa kumpiga na risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp kwenye siku ya wapendanao mwaka 2013.

Hemedy PhD Amefunguka Kuhusu Watoto Wake Sita

$
0
0
 Hemedy PhD Amefunguka Kuhusu Watoto Wake Sita
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Hemedy PhD amefunguka mambo kadhaa kuhusu yeye kuwa baba wa watoto sita.

Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘January to December’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio katika watoto wake sita alionao wamepishana kila mmoja miezi miwili katika kuzaliwa.

“Mtoto wangu mkubwa ana miaka mitatu waliofuatia wote wanapishana miezi miwili miwili, sitaki drama kila mtu na mama yake lakini all in all nawapenda sana watoto wangu na itakuja siku nitaweka mambo yote wazi kama mnyama future” amesema.

Katika hatua nyingine Hemedy amesema wiki mbili zilizopita girlfriend wake alipata shida na alikuwa amebeba mapacha, hivyo sasa angekuwa na watoto nane akiwa na umri wa miaka 29.

Dkt Shika Akataa Kujirudia ya Mnada wa Nyumba za Lugumi Ahaidi Kukifadhili Chuo Lakini Akataa Kufatiliww

$
0
0
Dkt Shika Akataa Kujirudia ya Mnada wa Nyumba za Lugumi Ahaidi Kukifadhili Chuo Lakini Akataa Kufatiliwwa
Dk Louis Shika, ‘bilionea’ aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, bado anaendeleza vituko; safari hii amesema hataki kufuatiliwa.

Dk Shika alijizolea umaarufu baada ya kuibuka kwenye mnada huo na kutaja viwango vya juu vya fedha kuwapiku watu wengine waliojaribu kununua nyumba hizo.

Lakini akashangaza baada ya kushindwa kulipia hata asilimia 25 ya takriban Sh3 bilioni ya nyumba tatu alizoshinda mnada licha ya kuahidi kuwa angefanya hivyo ndani ya muda mfupi kwa sababu fedha zake ziko nchini Urusi.

Kauli zake katika mnada huo, hasa ya "900 itapendeza", ndizo zilizompa umaarufu kiasi cha kupata udhamini wa kampuni tofauti, lakini bado hajaisha vituko.

Akiwa mjini Kahama mkoani Shinyanga jana Alhamisi (Novemba 23,2017) kuhudhuria mahafali ya Chuo cha Afya, msomi huyo wa Urusi aliahidi kukifadhili chuo hicho Sh2.2 bilioni kila mwaka.

Hata hivyo, mtaalamu huyo wa utabibu wa binadamu ameutahadharisha uongozi wa chuo hicho, akiutaka kutomfuatilia kudai kutimiza ahadi yake kwa kuwa anataka kuepuke mambo ya mnada wa nyumba kujirudia.

“Inapendeza tu mkiamini kwamba mtakuwa mnapokea kiasi hicho cha fedha (dola milioni moja), kila mwaka,” alisema Dk Shika.

Dk Shika pia aliwatahadharisha waandishi wa habari kutomuuliza kuhusu kutimiza ahadi hiyo ya dola milioni moja kwa chuo ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa kwa sababu hana fedha taslimu hadi mchakato aliosema wa kuhamisha fedha kutoka Urusi utakapokamilika.

Akizungumza na jumuiya ya chuo na wageni waalikwa, Dk Shika ametaja sababu ya kuahidi msaada huo kuwa ni kukiwezesha kutoa elimu bora ya utabibu na masuala ya afya ambayo ni muhimu kwa jamii na maendeleo ya Taifa.

Dk Shika aliwasili Kahama kwa ndege iliyotua uwanja wa ndege wa Buzwagi na kupokewa na mkuu wa chuo hicho, Yona Bakungile, huku msafara wake ukiwa na magari zaidi ya 50 yaliyopita mitaa mbalimbali kabla ya kufika chuoni.

Chuo hicho kipo Kata ya Mwendakulima umbali wa takriban kilomita tatu kutoka mji wa Kahama.

Dk Shika, mbele ya mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ya kwanza, alitoa ahadi hiyo baada ya Bakungile kuzungumzia changamoto ya baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo kutokana na wazazi na walezi kushindwa kuwalipia ada.

“Baadhi ya wanafunzi pia wamekatisha masomo kwa kukosa ada baada ya wazazi au walezi wao kufariki dunia,” alisema Bakungile.

Akizungumzia ahadi ya Sh2.2 bilioni kwa chuo chake kila mwaka, Bakungile alisema anaamini na "itapendeza akizipokea" kwa sababu zitasaidia kuinua kiwango cha taaluma na ubora wa miundombinu chuoni.

Mkurugenzi wa Watumishi Housing Dkt. Fred Msemwa Apewa Mwezi Mmoja Kukamilisha Nyumba 35 za Walimu

$
0
0
Mkurugenzi wa Watumishi Housing Dkt. Fred Msemwa Apewa Mwezi Mmoja Kukamilisha Nyumba 35 za Walimu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi wa Watumishi Housing Dkt. Fred Msemwa kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa nyumba 35 za walimu ambazo kampuni hiyo imetakiwa kuzijenga.

Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo hii  leo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Nyumba za walimu na ujenzi wa shule za Sekondari  zilizopo kwenye wilaya ya Ilala  ambapo tayari Wizara imetoa kiasi cha shilingi  5.6  kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba hizo.
Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako ametembelea na kukagua shule ya Sekondari  Msongola, Nyumba za walimu,  shule ya Sekondari Mvuti na shule kongwe ya Sekondari Pugu zote zilizopo katika manispaa ya Ilala, mkoani Dar es salaam

CCM Yatoa Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo Mbunge wa Songea Mjini

$
0
0
CCM Yatoa Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo  Mbunge wa Songea Mjini
Chama Cha Mapinduzi, kimetoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekwa Mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya chama hicho Ndg Leonidas Gama kilichotokea usiku wa kuamkia leo.

Uongozi wa CCM chini  Mwenyekiti wa Chama hicho Ndg, John Pombe Magufuli umetoa salamu hizo kupitia kwa Katibu Mwenezi, Ndg Humphrey Polepole imesea kwamba chama kimepokea taarifa za kifo hicho kwa mshtuko mkubwa na huzuni.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kwamba kipindi chote cha uongozi wake marehemu Gama,  alikuwa sehemu ya viongozi wa kisiasa ambao waliamini katika uelewa wa pamoja na matarajio, siasa safi na za kimaendeleo, uongozi bora na umuhimu wa kuweka maslahi ya nchi na taifa mbele.
 Mhe. Leonidas Gama amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Peramiho, Ruvuma.

Robinho Akataaa Hukumu ya Miaka Tisa Jela Iliyotolewa na Mahakama ya Itali

$
0
0
Robinho Akataaa Hukumu ya Miaka Tisa Jela Iliyotolewa na Mahakama ya Itali
Baada ya kuhukumiwa miaka tisa jela na mahakama ya Italia kwa kosa la ubakaji, mchezaji wa soka wa Brazil, Robinho amesema hakubaliani na hukumu hiyo kwani hakusika na tukio hilo kama ilivyoelezwa.

“Nimeshachukua hatua zote za kisheria kwaajili ya kujitetea, sikuhusika kwa namna yoyote kwenye tukio hilo kama ilivyodaiwa na tumekata rufaa kupiga hukumu hiyo”, amesema Robinho.
Mahakama ya Italia jijini Milan jana ilimhukumu Robinho pamoja na wanaume wengine watano raia wa Brazil kwenda jela miaka tisa kwa kosa la kumbaka binti mmoja raia wa Albania mwaka 2013. Hata hivyo mahakama imetoa muda kwa Robinho na wenzake kukata rufaa kabla ya kuanza kutumikia kifungo hicho.

Mahakama ilidai kuwa wakati binti huyo anabakwa mwaka 2013 alikuwa na umri wa miaka 22. Tukio hilo linadaiwa kufanyika kwenye club moja ya usiku jijini Milan ambapo Robinho na wenzake walimnunulia pombe nyingi binti huyo na baada ya kulewa ndio wakamfanyia vitendo hivyo.
Robinho mwenye umri wa miaka 33, alicheza AC Milan kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Nyota huyo aliyeanza maisha ya soka kwenye klabu ya Santos ya Brazil pia amewahi kuzichezea timu za Real Madrid na Manchester City. Robinho kwasasa anachezea klabu ya Atletico Mineiro ya Brazil.

Mama Wema Aonywa na Hakimu Kisa Mwanae Kushindwa Kufika Mahakamani

$
0
0
Mama Wema Aonywa na Hakimu Kisa Mwanae Kushindwa Kufika Mahakamani
MAMA wa Miss Tanzania 2006 na msanii wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, Miriam Sepetu, leo alionywa na hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya mwanae huyo kushindwa kufika mahakamani ambapo anakabiliwa na kesi la matumizi ya madawa ya kulevya.

Katika kesi hiyo Wakili wa Serikali Agustino Michael aliitaja kesi hiyo mbele ya hakimu Simba kuwa ndiyo iliyokuwa ikitakiwa kuendelea lakini mama Wema alinyoosha kidole kuashiria kuwa na neno.

Hakimu huyo alimkaribisha mama Wema kusema jambo alilotaka kusema ndipo akaanza kutoa hudhuru na kuiambia mahakama hiyo kuwa Wema alishindwa kufika mahakamani hapo kufuatia kufiwa na shangazi yake.

“Mheshimiwa Wema amefiwa na shangazi yake hivyo ameenda kushughulikia suala la mazishi ndiyo maana hakuweza kufika hapa mahakamani mimi ndiyo  nimekuja kumuwakilisha” alisema Mama Wema.

Baada ya mama huyo kutoa hudhuru huo hakimu alianza kumbana maswali ambapo alimuuliza kama Wema amepatwa na msiba uliomfanya ashindwe kufika mahakamani imekuwaje yeye mama yake apate muda huo yeye ashindwe?

Aliuliza hakimu huyo kisha kumuonya mama Wema kwa kumuambia siku nyingine asichukulie masihara suala la mshitakiwa huyo kuripoti mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Desemba 14 mwaka huu.

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo...

$
0
0

MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Tupo Mbagala Rangi Tatu

Le Mutuz Ampa Makavu Ruge Kuhusu Tamasha la Fiesta "Acha Kushindana na Mamlaka"

$
0
0
Le Mutuz Ampa Makavu Ruge Kuhusu Tamasha la Fiesta "Acha Kushindana na Mamlaka"
Baada ya siku moja Mkurugenzi wa clouds Media Ruge Mutahaba kuzungumsa kuhusiana suala la muda wa tamasha la fiesta Mwanamitandao, William Malechela (Le Mutuz) ameibuka na kuanza kumkashifu Ruge.

Ameandika hivi kupitia ukrasa wake wa Instargram "The art of self Destructions again Ihave so much respect kwa ndugu yangu Joe Kusaga but ninashindwa kuelewa exactly what is Mkurugenzi wake trying to achieve kwa kuendelea kushindana na mamlakacause nimemsikiliza sana jana akiendelea kuiponda serikali just becauseanataka kupiga muziki leaders mpaka asubuhi... binafsiIhave worked so hard kujaribu kusaidia kulimaliza hili tatizo la mkurugenzi lakini naonahataki kusikia lolote isipokuwa analolitaka yeye tu...
Ninajua mamlaka imekubali kusogeza goli kidogo just to accomodate his rants kwa kumuongezea lisaa limoja mpaka saa saba lakini bado jana alikuwa anaiponda mamlaka kwamba inatakiwa itengeneze plain field ya kumaliza muziki iwe a unifrom kwa taifa nzima .... kuna wanaodai kuwa yule mkuu ni akili kubwazzz now ninashindwa kuamini kama anavyosema amepiga Tanzania nzima mpaka asubuhi huko kote anasahau aliruhusiwa na mamlaka ile ile inamwambia hapa tu dar  huwezi kupiga mpaka asubuhi basi mamlaka nzima haifai really?
Juzi mamlaka hiyo hoyo ilienda kuangaliana kumfariji na kuunguliwa kwa ofisi zake lakini leo mamlaka hiyo hiyo haifai kisa ni yeye tu apige muziki hadi asubuhi... mamlaka imempa option ya kupiga muziki wake uwaja wa karume tena ni bure hadi asubuhi  akitaka lakini hataki anataka leaders tu  na lazima iwe mpaka asubuhi ... I mean sawa mbona zamani tulikuwa tunapiga why now? anaambiwa kuwa kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na uwanja huo ambao wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu sana bila kusikilwa kwasababu hawana redio na Tv na wasanii kama yeye... infact mmiliki wa magorofa kupanga karibu na leaders wanalia hawana wapangaji ambao wanaogopa kelele za muziki ... at some point mkuu anajaribu kutishia mamlaka kwa kuigombanisha na wasanii anasahau kuwa  hii mamlaka ya mkoa imeshapigana na wauza unga, wauza shisha, na wakandarasi na wakatulia leo sembuseiwe wasanii? ... anasahau kua mamlaka hii  inaivunja jengo la Tanesco na wizara ya maji ili kuheshimu sheria zake namkumbusha tu AJIFUNZE KUHESHIMU MAMLAKA! bila SHURUTI"
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images