Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Manura Ajitangazia Ushindi Mechi Dhidi ya Libya

0
0
Manura Ajitangazia Ushindi Mechi Dhidi ya Libya
Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars” Aishi Salum Manula amesema kutokuwajua vizuri wapinzani wao Timu ya Taifa ya Libya hakutakuwa chanzo cha kutokufanya vizuri katika mchezo wa awali wa michuano ya CECAFA

Manula amesema mara nyingi Kocha hutoa mbinu kwa wachezaji wake kutokana na kuijua japo sio kwa undani timu wanayokutana nayo hivyo wanaamini Kocha anaifahamu Libya na mbinu walizofundishwa zitawasaidia kuweza kupambana nao ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo na inayofuata.
"Timu ya Libya siijui kwa hivyo lakini nadhani kwa vile ambavyo Mwalimu amatufundisha na mbinu ambazo ametupa kuelekea katika mchezo wetu wa kwanza nadhani tutafanikiwa kwani nadhani yeye ameweza kuifuatilia vizuri zaidi na kwaundani na kujua kwamba Libya ipo vipi ili atupatie mbinu gani na tuweze kuushinda mchezo huo, " amesema.
Aishi ameongeza kwa kuwataka watanzania kuendelea kuwapa sapoti ikiwa ni pamoja na kuwaanini kwani wao wakiwa ni wachezaji wanajua dhamana ya watanzania waliyoibeba.
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoondoka hapo jana kimeshawasili nchini Kenya na leo kimeendelea na mazoezi kwaajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Libya utakaopigwa siku ya Jumapili nchini humo

Calisah Akwama Kwenda Katika Mashindano ya Mister Africa Internation

0
0
Calisah Akwama Kwenda Katika Mashindano ya Mister Africa Internation
Mwanamitindo Calisah ameshindwa kushiriki mashindano ya Mister Africa International yanayofanyika Jumamosi hii Disemba 2 huko mjini Lagos Nigeria, licha ya kutumiwa barua ya mwaliko.


Calisah ameiambia Bongo5 kwamba licha ya kuwa mashindano hayo hutakiwa washiriki kutuma maombi yao ili washiriki lakini yeye aliombwa kushiriki na kampuni ambayo inaandaa mashindano hayo.

“Haikuwa bahati yangu kwa mwaka huu kwa kuwa nimechelewa kutumiwa mwaliko, nimepokea barua November 27 wakati mashindano yamenza wiki moja nyuma na fainali ni kesho (leo),” alisema Calisah.

Joshua Nassari Avamiwa Nyumbani Kwake Usiku na Watu Wasiojulikana Waliokuwa na Silaha za Moto

0
0
Joshua Nassari Avamiwa Nyumbani Kwake Usiku na Watu Wasiojulikana Waliokuwa na Silaha za Moto
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amedai usiku wa kuamkia Jumamosi hii alivamiwa na watu wasiojulika wakiwa na bundiki na kufyetua risasi nje ya nyumba yake.

Nassari amedai muda mchache baada ya tukio hilo yeye pamoja na mke wake walifanikiwa kufika kituo cha polisi na kutoa ripoti na tukio hilo.

“Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu,” alitweet Nassari.

Amedai watu hao baada ya kufyetua risasi walifanikiwa kumuuwa mbwa wake ambaye alikuwa nje ya nyumba.

Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara.

Mama Samia Awafunda Wanaume "Msipende Kuwana Wakubwa Wenzenu Hawana Ladha Katika Tendo la Ndoa"

0
0
Mama Samia Awafunda Wanaume "Msipende Kuwaoa Wakubwa Wenzenu Hawana Ladha Katika Tendo la Ndoa"
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu amewahasa wanaume wote wa Tanzania kutowaona wakubwa wenzao wamechuja katika tendo la ndoa na kuanza kuwataka watoto wadogo ambao ni watoto wao na taifa la kesho.

Akizungumza leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi ambapo pamoja na hilo amesema wapo baadhi ya wanaume ambao wanajua wameshaambukizwa bado wanaendelea kuwaambukiza watoto hao.

“Wanaume msipende kuwaona wakubwa wenzenu wamechuja hawana ladha ile ambayo mngependa kuipata, kwahiyo mna hamia kwa watoto wadogo ndugu zangu huu sio mwendo mzuri hawa ni watoto wetu, hili ni taifa la kesho tukiliteketeza leo, na wengine wanajua wameshaambukizwa na wakubwa wanaushifti kwa watoto wadogo ambao ambao hawawajui, ndugu zangu huu ni uuwaji wa makusudi na Mwenyezi Mungu hatawasamehe katika hili,” amesema Mama Samia.

Ongeza Hips na Makalio, Kuwa Softi na Mweupe, Ongeza Maumbile ya Kiume na Hamu ya Tendo

0
0
ONGEZA HIPS NA MAKALIO, KUWA MWEUPE NA SOFTI, ONGEZA MAUMBILE YA KIUME, NGUVU NA HAMU YA TENDO N.K
      @markson_beauty_pr Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kuthibitishwa kiafya. 
    NB. Matokeo ni uhakika na garantii.
🍉🍑🍌🍇🥒🍓🍎🍍
          BIDHAA ZETU:-
    
1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @150,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× ya kunywa @200,000/=
(b)Vidonge  @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @160,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- 
 (1)Mafuta  @150,000/=
(11)Vidonge @170,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka @150,000/= 
(b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @150,000/=
 (C)Handsome up original @250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula  @150,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/= 
(b)Mkanda wa kawaida @100,000/= 
(c)Micro-computer belt wa umeme @150,000/=
9.Kupunguza  maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @150,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @150,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120,000/=
12.Kubana uke na kuondoa uchafu @120,000/=
        Wasiliana nasi :- (+255)
             0767447444 au.        
                0714335378
  TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. 
👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
     Follow us instagram  @Markson_beauty_pr 
@Markson_beauty_pr
WEB:markbeauty.org

Hii Ratiba ya mechi za Kombe la Dunia: Urusi 2018

0
0
Hii Ratiba ya mechi za Kombe la Dunia: Urusi 2018
Robo fainali | Nusu fainali | Mechi ya kuamua nafasi ya tatu| FAINALI

Kundi A
Tarehe / saaMechiUwanja
14 Jun, 1500 GMTRussia - Saudi ArabiaLuzhniki, Moscow
15 Jun, 1200 GMTEgypt - UruguayEkaterinburg
20 Jun, 1800 GMTRussia - EgyptSan Petersburg
20 Jun, 1500 GMTUruguay - Saudi ArabiaRostov on Don
25 Jun, 1400 GMTSaudi Arabia - EgyptVolgograd
25 Jun, 1400 GMTUruguay - RussiaSamara

Kundi B
Tarehe / saaMechiUwanja
15 Jun, 1500 GMTMorocco - IranSankt Petersburg
15 Jun, 1800 GMTPortugal - SpainSochi
20 Jun, 1200 GMTPortugal - MoroccoLuzhniki, Moscow
20 Jun, 1800 GMTIran - SpainKazan
25 Jun, 1800 GMTIran - PortugalSaransk
25 Jun, 1800 GMTSpain - MoroccoKaliningrad


Kundi C
Tarehe/saaMechiUwanja
16Jun, 1000 GMTFrance - AustraliaKazan
16Jun, 1600 GMTPeru - DenmarkSaransk
21Jun, 1200 GMTFrance - PeruEkaterinburg
21Jun, 1500 GMTDenmark - AustraliaSamara
26Jun, 1400 GMTAustralia - PeruSochi
26Jun, 1400 GMTDenmark - FranceLuzhniki, Moscow


Kundi D
Tarehe/saaMechiUwanja
16Jun, 1300 GMTArgentina - IcelandSpartak, Moscow
16Jun, 1900 GMTCroatia - NigeriaKaliningrad
21Jun, 1800 GMTArgentina - CroatiaNizhni Novgorod
22Jun, 1500 GMTNigeria - IcelandVolgograd
26Jun, 1800 GMTNigeria - ArgentinaSankt Petersburg
26Jun, 1800 GMTIceland - CroatiaRostov on Don


Kundi E
Tarehe/saaMechiUwanja
17Jun, 1200 GMTCosta Rica - SerbiaSamara
17Jun, 1800 GMTBrazil - SwitzerlandRostov on Don
22Jun, 1200 GMTBrazil - Costa RicaSankt Petersburg
22Jun, 1800 GMTSerbia- SwitzerlandKaliningrad
27Jun, 1800 GMTSerbia - BrazilSpartak, Moscow
27Jun, 1800 GMTSwitzerland - Costa RicaNizhni Novgorod

Kundi F
Tarehe/saaMechiUwanja
17Jun, 1500 GMTGermany - MexicoLuzjhinski, Moscow
18Jun, 1200 GMTSweden - South KoreaNizhni Novgorod
23Jun, 1500 GMTGermany - SwedenSochi
23Jun, 1800 GMTSouth Korea - MexicoRostov on Don
27Jun, 1400 GMTSouth Korea - GermanyKazan
27Jun, 1400 GMTMexico - SwedenEkaterinburg

Kundi G
Tarehe/saaMechiUwanja
18Jun, 1500 GMTBelgium - PanamaSochi
18Jun, 1200 GMTTunisia - EnglandVolgograd
23Jun, 1800 GMTBelgium - TunisiaSpartak, Moscow
24Jun, 1500 GMTEngland - PanamaNizhni Novgorod
28Jun, 1400 GMTEngland - BelgiumKaliningrad
28Jun, 1400 GMTPanama - TunisiaSaransk
Group H

Kundi H
Tarehe/saaMechiUwanja
19Jun, 1200 GMTPoland - SenegalSpartak, Moscow
19Jun, 1500 GMTColombia - JapanSaransk
24Jun, 1500 GMTJapan - SenegalEkaterinburg
24Jun, 1800 GMTPoland - ColombiaKazan
28Jun, 1400 GMTJapan - PolandVolgograd
28Jun, 1400 GMTSenegal - ColombiaSamara

Hatua ya 16 bora
Tarehe / saaMechiUwanja
(1) 30Jun, 1400 GMTMshindi Kundi C - Wa pili Kundi DKazan
(2) 30Jun, 1800 GMTMshindi Kundi A - Wa pili Kundi BSochi
(3) 1 Jul, 1400 GMTMshindi Kundi B - Wa pili Kundi ALuzhniki, Moscow
(4) 1 Jul, 1800 GMTMshindi Kundi D - Wa pili Kundi CNizhni Novgorod
(5) 2 Jul, 1400 GMTMshindi Kundi E - Wa pili Kundi FSamara
(6) 2 Jul, 1800 GMTMshindi Kundi G - Wa pili Kundi HRostov on Don
(7) 3 Jul, 1400 GMTMshindi Kundi F - Wa pili Kundi ESankt Petersburg
(8) 3 Jul, 1800 GMTMshindi Kundi H - Wa pili Kundi GSpartak, Moscow

Robo fainali
Tarehe / saaMechiUwanja
(A) 6 Jul, 1400 GMTMshindi Mechi 2 - Mshindi Mechi 1Nizhni Novgorod
(B) 6 Jul, 1800 GMTMshindi Mechi 5 - Mshindi Mechi 6Kazan
(C) 7 Jul, 1400 GMTMshindi Mechi 7 - Mshindi Mechi 8Samara
(D) 7 Jul, 1800 GMTMshindi Mechi 3 - Mshindi Mechi 4Sochi

Nusu fainali
Tarehe / saaMechiUwanja
(I) 10 Jul, 1800 GMTMshindi Mechi A - Mshindi Mechi BSankt Petersburg
(II) 11 Jul, 1800 GMTMshindi Mechi D - Mshindi Mechi CLuzhniki, Moscow

Mechi ya kuamua mshindi wa nafasi ya tatu
Tarehe / saaMechiUwanja
14 Jul, 1400 GMTAtakayeshindwa Mechi I - Atakayeshindwa Mechi IISankt Petersburg

FAINALI
Tarehe/saaMechiUwanja
15 Jul, 1500 GMTMshindi Mechi I - Mshindi Mechi IILuzhniki, Moscow

Hawaii Nchini Marekani Yafanyia Jaribio King'ora cha Kuonya Kuhusu Shambulizi la Nyuklia

0
0
Kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita baridi jimbo la Hawaii nchini Marekani limefanyia jaribio king'ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia
Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na Korea Kaskazini mapema wiki hii.
Hawai kawaida ina ving'ora ambavyo huonya kuhusu majanga ya asili kama tsunami.
Kingora cha nyuklia kina mlio tofauti ambacho huwaonya watu kusalia manyumbani wakisubiri ushauri zaidi.
Lakini king'ora hicho kilisikika tena Ijumaa na kitarudiwa klila jumatatu ya kwanza ya mwezi.
Kombora linalorushwa kutoka Korea Kaskazini linaweza kushambulia Hawaii ndani ya dakika 20 baada ya kufyatuliwa.
Hivi majuzi Korea ilifyatua kombora mpya la masafa marefu ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia ndani ya Marekani.

Uzuri wa Nyumba Upambwa na Pazia Kuwa Mbunifu

0
0
Uzuri wa Nyumba Upambwa na Pazia Kuwa Mbunifu
PAZIA ni miongoni mwa mapambo yanayotumika  katika kupendezesha na kukoleza umaridadi wa ndani ya nyumba. Kama ilivyozoeleka, pazia zimekuwa zikitumika kupamba mlangoni na madirishani pia hasa maeneo ambayo chumba tunapoishi kinakosa faragha.

Lakini pia,  katika sehemu zenye joto kali ambazo mara nyingi madirisha yake huwa na  wavu au matobo, pazia imekuwa ikitumika wakati mwingine.

Halikadhalika, hata katika sehemu ambazo madirisha yake ni yale yasiyo na wavu, bado wanatumia pazia kama pambo la kupendezesha nyumba na miaka ya hivi karibuni limekuwa likitumika zaidi kuliko ilivyokuwa hapo zamani.

Na kwa sababu imezoeleka kwamba mwanamke ndiye anayesimamia mambo mengi nyumbani, pale inapokuwa haijapambwa na pazia ikapambika, huonekana kama hawajibiki ipasavyo katika majukumu yake kama mama na msimamizi wa uzuri na ubora wa makazi yake.
Mbali na nyumbani, pia pazia hutumika kupamba  ofisi, hotelini na sehemu nyingine nyingi. Pazia za ofisini zinafahamika na zile za hotelini kwenye sehemu za vinywaji nako ziko za kupapendezesha.

Kadri ukuaji wa sayansi na teknolojia unavyochukua nafasi yake, kadhalika maisha nayo yanabadilika ama kuboreka zaidi huku huduma na bidhaa zikiboreshwa kila wakati.

Siku hizi tofauti na miaka ya nyuma, baadhi ya familia hupendelea hata wakati mwingine ndani ya nyumba kunapokuwa na pazia ng’aring’ari zenye mvuto, hulazimika kugharimia kuweka kiyoyozi ili pazia zisivurugike katika mpangilio na kuharibu muonekano mujarabu wa ndani wa nyumba kwa kisa tu kutafuta hewa.

Kwa ujumla pazia katika kipindi hiki cha kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia, zinatengenezwa katika aina au mitindo yenye mvuto tofauti na hivyo kutoa fursa kila mtu kuchagua aina inayomfaa hasa kwa kuzingatia mandhari iliyopo ndani ya nyumba yake.

Zipo pazia zilizotengenezwa kwa kutumia kitambaa kizito zaidi, za vitambaa vyepesi, hariri, zipo za turubai, shanga, fimbo za plastiki  na hata za nyuzi.

Lakini pia zipo pazia ambazo zina matundu lakini zote kwa ujumla wake zimekuwa zikitumika kupamba  nyumba, ofisi ama hoteli kulingana na mahitaji ama mandhari iliyopo katika sehemu husika.

 Lakini pamoja na hayo uchaguzi wa rangi na aina ya kitambaa kwa wale wanaopendelea kushona, nalo ni jambo muhimu linalopaswa kuzingatiwa na wakati wa kufanya hayo yote kuzingatia aina ya rangi zilizopo katika nyumba unayoilenga kuanzia ukutani na vitu vingine vilivyomo ndani.

Kikubwa zaidi ambacho nimependa kuzungumzia pazia, ni kutokana na umuhimu wake katika kupendezesha makazi, ndiyo maana kuna umuhimu zaidi hasa kwa kina mama kuzingatia vigezo mbalimbali wanapofanya uchaguzi  wa pazia hizo.

Ni vema kutambua kuwa ubaya wa nyumba yako utatokana na namna unavyoitengeneza  na hata mvuto wake pia utatokana na namna unavyochagua na kupangilia  wewe mwenyewe.

Ni jambo la aibu kuona unasifia mvuto wa nyumba ya jirani eti tu ameweka pazia nzuri, wakati na wewe mwenyewe unaweza.

Naamini kila kitu kinawezekana ukijipanga  usitumie gharama kubwa katika kupata pazia bora  unazozipenda kama utajipanga na kudhamiria kuwa nazo.

Wapo wanawake na wanaume ambao wanaweza kutundika pazia zao ndani ya nyumba kwa kutumia kamba za kawaida na ikapendeza lakini nashauri kama inawezekana si vibaya kutumia fimbo ama vibanio vya  kutundikia pazia hizo vinavyouzwa madukani.

Fimbo hizi hupatikana kwa wingi katika maduka ambayo yanauza pazia kwa hiyo ni vema wakati unanunua pambo hilo ukatafuta na fimbo yake.

Ulizia fimbo au bomba ambazo rangi zake zinaendana na rangi iliyopo kwenye nyumba pamoja na iliyopo kwenye pazia. Mara nyingi bomba za kahawia, rangi ya maziwa na nyeusi isiyokolea hupendezesha.

Kwa kupata  matokeo epuka rangi zinazong'ara kupindukia  kwa sababu hazina utulivu, ni vema kuchagua rangi iliyopoa.

Zingatia kuweka pazia katika fimbo au bomba laini ambazo hazikwaruzi ili zisizisoharibu wakati unavuta kuziweka sawa ama unazitoa kuzifua ama kuondoa vumbi.

Zungumza na wataalamu wa urembo na mapambo ya nyumba ili kukupa ushauri zaidi. Suala la msingi ni kufahamu mbinu za uwekaji wa pazia. Kumbuka kuchanganya kama ni jepesi weka lenye lesi ndani.

Wakati mwingine ni vyema kubebesha pazi zito na lile la lesi ili joto linapozidi ulifungue mojawapo kupata hewa safi na mwanga.







Ngoma Awasili Nchini Awaangukia Viongozi Yanga

0
0
Ngoma Awasili Nchini Awaangukia Viongozi Yanga
SIKU chache baada ya kutokea taarifa za mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma aliyekuwa kwenye matibabu nchini Zimbabwe kuteuliwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo, nyota huyo amewasili nchini na kujitetea kwa viongozi.

Ngoma amewasili nchini juzi na kwenda kuonana na viongozi wa timu hiyo ambao walionekana kushangazwa na kukasilishwa na kitendo cha Ngoma kudanganya kuumwa huku akiitwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, akizungumza na gazeti hili jana, alisema Ngoma amerejea nchini na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na uongozi kuweka mambo sawa.

“Ngoma amerejea na mimi mwenyewe nimeongea naye, ameandika barua kwa katibu kuelezea safari yake kwenda Zimbabwe kwenye matibabu,” alisema Saleh.

Aidha, alisema kuwa mshambuliaji huyo alikataa kuwa ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo kilichokuwa kishiriki michuano ya Chalenji.

“Amesema hajaitwa kwenye timu ya taifa ila alionana na kocha wa timu hiyo na alimueleza kuwa yupo (Zimbabwe) kwa ajili ya matibabu,” alisema.

Suala hilo sasa lipo kwa viongozi na wanaendelea na mazungumzo.

Kwenye mtandao wa Chama cha Soka cha Zimbabwe iliandikwa kocha wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, Sunday Chidzambga, amemjumuisha Ngoma kwenye kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Chalenji.

Hata hivyo kwa sasa kuna taarifa Zimbabwe imejitoa kwenye michuano hiyo ya Chalenji inayoanza kesho kwa kile walichoeleza kuwa usalama Kenya ni mdogo.


Lema Amsindikiza Nassari Polisi Kutoa Taarifa ya Tukio la Uvamizi Nyumbani Kwake

0
0
Lema Amsindikiza Nassari Polisi Kutoa Taarifa ya Tukio la Uvamizi Nyumbani Kwake
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema wameenda kwenye kituo cha polisi Usa River kutoa taarifa ya tukio la uvamizi uliofanyika nyumbani Nassari usiku wa kuamkia leo Jumamosi.

Tukio hilo limetokea Kijiji cha Nkwanekori wilayani  Arumeru mkoa wa Arusha.

Katika ukurasa wake wa Twitter Nassari ameandika, “Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu.”

Baadhi ya majirani na viongozi wa Chadema wamefika nyumbani kwake kumjulia hali na baadaye kumsindikiza kituo cha polisi Usa River.

Mmoja wa majirani ambaye hakupenda kutajwa jina lake amesema alisikia milio ya risasi zaidi ya 12 na baadaye kimya kutawala.
Chanzo Mwananchi

Mzee Chilo Afunguka Sababu ya Bongo Movie Kujikita Kwenye Tamthilia

0
0
Mzee Chilo Afunguka Sababu ya Bongo Movie Kujikita  Kwenye Tamthilia
Muigizaji mkongwe nchini Mzee Chilo abainisha kuwa soko la filamu lipo ila filamu inachukua muda mrefu kuliko Tamthilia na ndiyo maana wamehamia huko, ila bado wanafanya filamu.

Pia Mzee Chilo aliyeanza kupata umaarufu kupitia tamhilia ya Jumba la Dhahabu ameeleza wamehamia huko pia ni suara la bajeti kwani filamu inachukua bajeti kubwa kuliko Tamthilia.

Ni Kweli Mange Amefuta Account Yake ya Intagramu na Kuamua Kuachana na Mitandao ya Kijamii??

0
0
Ni Kweli Mange Amefuta Account Yake ya Intagramu na Kuamua Kuachana na Mitandao ya Kijamii??
Mwanadada machachari ambaye amekuwa maarufu kupitia mitandao ya kijamii ususani Instagramu Mange Kimambi mtanzania Anayeishi Marekani Amewaacha mashabiki zake kwenye giza zito baada ya tetesi zinazoonekana kusambaa kwenye mitandao kuwa amefuta account yake na kuamua kuachana na mitandao ya Kijamii

Kuna Taarifa zinazosambaa kuhusu mange kwenye mitandao ya kijamii ambazo inasemekana ni taarifa kutoka kwa Mange zinasema "Nimetafakari sana juu ya nchi yangu ninayopoteza muda wangu kuipigania sana juu ya watu ninaowapigania, nimehatarisha maisha yangu na familia yangu lakini naona napoteza muda  bila sababuza msingi, nimeamua kufuta account yangu Instagramu na Kuachana kabisa na masuala ya mtandao"

Maamuzi hayo Magumu ambayo yamefanywa na mwanadada huyo ambaye amekua akiibua mambo mengi yanaoendelea nchini yamekuwa na maswali mengi huku watu wakihoji kuna ukweli kwenye hili???...

Je uamuzi wa wema Sepetu kurudi CCM ndio ulomfanya mange kujitoa katika mapambano aliyokuwa anayafanya katika mitandao ya kijamii.

Mange alijionyesha wazi kumpenda Wema na hata pale ilipotokea kuna mtu anamsema vibaya au kumuingiza kwenye tatizo wema Mange alikua kinara wa kumtetea kwa nguvu zake zote.

Wolper- Sipendi Mwanaume Mashine Napenda Mwenye Maumbile Madogo

0
0
Wolper- Sipendi Mwanaume Mashine Napenda Mwenye Maumbile Madogo
Muigizaji wa filamu bongo ambaye sasa anajihusisha zaidi na ujasiriamali, Jackline WOlper, amesema anapenda wanaume wenye maumbile madogo kwani yeye mwenyewe maumbile yake ni madogo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live Jackline Wolper amesema hana sababu ya kupenda au kusifia wanaume wenye maumbile makubwa wakati yeye maumbile yake ni madogo.
"Actualy siwezi kusema nachukuliaje wanaume wenye maumbile madogo, na ndio nawapenda pia, kwa sababu mimi mwenyewe mdogo, nitapendaje vitu vikubwa ambavyo siwezi kuvihimili? Unajua mwanamke anayesema mwanaume mashine namshangaa, mwanaume pesa bwana, mwanamke ambaye anajua maisha,  hawezi kusema mwanaume mashine, mimi mwenyewe siwezi kusifia mashine", amesema Wolper.
Pamoja na hayo Jackline Wolpler amesema kwa sasa hataki kujihusisha sana na masuala ya mahusiano, kwani amezipa kipaumbele kazi zake tu.

Omog Amtengenezea Mazingira ya Kubaki Simba Mavugo

0
0
Omog Amtengenezea Mazingira  ya Kubaki Simba Mavugo
WAKATI habari zikizagaa kwamba Simba ipo mbioni kuachana na straika wake, Laudit Mavugo, Kocha Joseph Omog wa timu hiyo ameenda mapumziko kwao Cameroon akisisitiza mchezaji huyo asiachwe ili kuepuka gharama za kuvunja mkataba wake.

Omog tayari yupo Cameroon tangu Jumatano ya wiki hii, inaelezwa ameacha ripoti kwa uongozi wa Simba inayowasisitiza kuliacha jina la Mavugo raia wa Burundi katika kikosi chake.

Mavugo hadi sasa amefunga mabao mawili tu katika Ligi Kuu Bara ambapo Simba ina mabao 23, hivyo uwezekano wa kuachwa ulikuwa mkubwa akiwa amejiunga na timu hiyo msimu uliopita akitoka Vital’O ya kwao Burundi.

Mmoja wa mabosi wa Simba, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Omog ameamua kumbakisha Mavugo kikosini si kwa sababu ya uwezo bali anataka amalize mkataba wake miezi sita ijayo ili awe huru kuondoka.

“Kweli kulikuwa na mipango hiyo ya Mavugo kuachwa lakini kwa sasa suala hilo limesitishwa kwa sababu Omog amependekeza asiachwe katika kipindi hiki bali hadi pale mkataba wake utakapomalizika.

“Kocha ameona afanye hivyo kwa sababu ya kutopoteza fedha za kulipa gharama za kuvunja mkataba maana anaweza kukataa kwenda kwa mkopo popote pale, tutabaki naye ili baadaye aondoke kwa amani,” alisema bosi huyo.

Habari kutoka Yanga zilisema, klabu hiyo ilikuwa ikimpigia hesabu Mavugo endapo angeachwa na Simba imuwahi kumsajili ikiamini bado ana makali isipokuwa hapati nafasi katika timu yake.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo


Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

0
0
MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Tupo Mbagala Rangi Tatu

Ujumbe wa Msando, Jerry Muro kwa Wema Sepetu Baada ya Kutangaza Kurudi CCM "Nyumbani ni Nyumbani"

0
0
Ujumbe wa Msando, Jerry Muro kwa Wema Sepetu Baada ya Kutangaza Kurudi CCM "Nyumbani ni Nyumbani"
Ujumbe wa alberto Msando kwa Wema sepetu baada ya kutangaza kurudi CCM Msando ameposti picha za mrembo huyo na kuandika kuwa "@wemasepetu we spoke and I repeat watakutukana, watajaribu kukudhalilisha, watatumia nguvu kuonyesha ufai, watakuombea mabaya, watatamani uanguke, watapenda uwe mnyonge, Ila ukweli wanajua ni suala la muda tu ukweli utajulikana. Muda ni kila kitu maamuzi haya ni sahihi na yeyote ambaye anakujari wewe kama rafiki ataelewa. Ni maisha yako,ni kesho yako, ni Tanzania yako @wemasepetu#forthosewholovetohate #hayawatanzaniauongowao #maamuzibinafsi #nabado #sindano #maumivuYakichwa #kuwangazisasabasi #theDon #hpolepole #sheIsback

Naye Jeri Murro ameandika hivi "Niliambiwa kuwa mtoto akinyea mkono huwezi kukata mkono always home is home "

Chadema Wamteua Patrick Sosopi Kurithi Nafasi ya Katambi

0
0
Chadema Wamteua Patrick Sosopi Kurithi Nafasi ya Katambi
BARAZA la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamefanya uteuzi wa viongozi wa Baraza la Vijana la Chama hicho (BAVICHA) ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kufuatia baadhi ya viongozi wao kukihama chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.
Katika uteuzi huo, Balaza hilo limemteua aliyekuwa Katibu wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti mpya wa BAVICHA, baada aliyekuwa mwenyekiti wa baraza hilo, Patrobas Katambi kuhamia CCM. Ole Sosopo ataitumikia nafasi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani 2018.
Aidha, chama hicho kimemteua ndugu Pambalu kuwa katibu wa Bavicha baada ya nafasi hiyo kuachwa wazi na Ole Sosopi aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa muda.

Ulimwengu Baada ya Kukaa Nje ya Uwanja kwa Muda Mrefu Sasa Hapiga Hatua

0
0
Ulimwengu Baada ya Kukaa Nje ya Uwanja kwa Muda Mrefu Sasa Hapiga Hatua
Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amezidi kupiga hatua za kurejea dimbani kutokana na kuendelea vizuri na mazoezi ya kujiweka sawa.

Ulimwengu anayekipiga katika klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden yuko katika mazoezi makali ya Gym, kuchezea mpira peke yake na mkufunzi pamoja na kukimbia ufukweni.
Mshambuliaji huyo alifanyiwa upasuaji wa goti katika hospitali ya Taasisi ya Sayansi ya Michezo mjini Cape Town, Afrika Kusini mapema mwezi Julai baada ya kusumbuliwa kwa mrefu na majeraha ya goti.

Ulimwengu hajafanikiwa kuitumikia kikamilifu timu yake mpya ya AFC Eskilstuna  tangu alipojiungana nayo mwezi Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Ngoma Akwaa Kisiki Yanga Hatima Yake Ipo Mikononi mwa Lwandamina

0
0
Ngoma Akwaa Kisiki Yanga Hatima Yake Ipo Mikononi mwa Lwandamina
YANGA imemuwekea ngumu straika wake Donald Ngoma kwanza kuendelea na kazi yake ya kuitumikia timu hiyo, pia mpango wa kwenda Singida United anakotakiwa na Kocha Hans van Der Pluijm.

Klabu hiyo imesema inamsubiri Kocha wao George Lwandamina arejee kutoka mapumzikoni Zambia, ndipo waamue hatima ya Ngoma aliyepitisha muda alioomba kuwa nje ya timu.

Ngoma hivi karibuni aliaga kwenda kwao Zimbabwe lakini alipitisha muda wa kuwa huo bila kutoa taarifa kwa uongozi, hivyo mabosi wake wanasubiri kukaa kikao cha pamoja na kocha ili kujua hatima yake.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema hawawezi kumtoa Ngoma kumpeleka Singida United kwani bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na timu yao.

“Ngoma bado ni mali yetu na kwa sasa tunataka kukaa naye kuzungumza naye tangu alipoondoka nchini na kwenda kwao Zimbabe kwa ajili ya kupata tiba ya majeraha yake.

“Mshambuliaji huyu bado ana mkataba wa mwaka na nusu hapa hivyo inakua ngumu kumuachia, tunataka amalize mkataba wake uliobakia,” alisema Mkwasa.


Akizungumzia kuhusu hatima ya Ngoma kikosini, Mkwasa alisema; “Inabidi tukae uongozi na kocha ili kujua tunamchukulia hatua gani Ngoma kwani alipitisha muda aliopewa kuwa nje ya timu bila maelezo, tutasikiliza kile anachosema sasa na tutapima kuhusu hatua za kumchukulia.”
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images