Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live

Mahakama Yagoma Kumfutia Mashtaka 20 Aliyekuwa Muhasibu wa Takukuru

0
0
Mahakama Yagoma Kumfutia Mashtaka 20 Aliyekuwa Muhasibu wa Takukuru
Mahakama ya Hakimu Mkuu mkazi Kisutu imekataa kuyafuta mashtaka 20 ya utakatishaji fedha kati ya 43 yanayomkabili aliyekuwa muhasibu wa TAKUKURU Godfrey Gugai na wenzake na kusema kuwa mashtaka hayo kwa sasa yana nguvu kisheria.

 Akitangaza uamuzi huo wa mahakama Hakimu Mkazi Kiongozi Thomas Simba amesema uamuzi wake huo unahitimisha mjadala aliouahirisha aliposikiliza kesi hiyo kwa mara ya kwanza Novemba 16 kama mashtaka ya utakatishaji fedha katika hati ya mashtaka ya Gugai na wenzake yaendelee au la.

Mara baada ya kutoa maamuzi hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 18 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Vitalis Peter kusema kuwa upelelezi haujakamilika ambapo watuhumiwa wanatetewa na wakili Alex Mgongolwa.

Godfrey Gugai na wenzake watatu walifikishwa katika mahakama hiyo ya Kisutu wakikabiliwa na makosa 43 ikiwemo kutakatisha fedha,udanganyifu pamoja na umiliki wa mali nyingi kwa Gugai kinyume na kipato chake halisi ambapo makosa mengi yanamhusu Gugai pekee yake.
Kutokana na uamuzi uliotolewa safari hii na Hakimu Simba Washtakiwa wote wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka wanayokabiliwa nayo,ya utakatishaji fedha,hayana dhamana na kesi yao itasomwa tena mahakamani hapo Desemba 18.

Mustafa Hassanali- Calisah Sio Mwanamitindo Kabisa Hana Sifa

0
0
Mustafa Hassanali- Calisah Sio Model, Acha Ugomvi Uanze,
Mbunifu maarufu wa mavazi nchini Mustafa Hassanali, ameonekana kwenda kinyume na matakwa ya mwanamitindo wa kiume bongo Calisah, akisema kuwa kijana huyo sio mwanamitindo kabisa

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mustafa Hassanali amesema kama Calisah angekuwa mwanamitindo mwenye sifa angeshafanikiwa kwenda kwenye majukwaa ya mitindo kimataifa, lakini kwa kuwa hana sifa, hata ya hapa nyumbani ameshindwa kufanikiwa kupanda.
Mustafa ameendelea kwa kusema kwamba tasnia ya mitindo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, na kama huna nidhamu basi hakuna utakalofanikisha.
"Calisah sio model, acha ugomvi uanze, unajua London fashion week, Heriet Paul alifanya Victoria secret ambayo ilifanyika Shangai, kama unajiita super model mbona Swahili Fashion hayupo? Kila mtu ana maisha yake na anataka kuishi jinsi anavyotaka, asiyefundishwa na mamaye hufundishwa na nani? Kama mtu hawezi kurespet na kuthamini biashara ya ubunifu, huwezi fanikiwa", amesema Mustafa Hassanali.
Kitendo cha mwanamitindo huyo kutolewa sifa na watu walioko kwenye tasnia yake imekuwa ni mara ya pili, ambapo awali mwanamitindo Dax Cruzz alisikika akisema Calisah hana vigezo vya kuwa mwanamitindo wa kimataifa na kwamba ataishia hapa hapa bongo.

Wakala wa Majengo Amaliza Mzozo Kuhusu Gharama ya Ujenzi wa Mabweni ya Chuo cha UDSM

0
0
Wakala  wa Majengo Aondoa Mzozo Kuhusu Gharama ya Ujenzi wa Mabweni ya Chuo cha UDSM
Mkurugenzi wa wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga ameondoa mzozo uliopo kwa baadhi ya watu kuhusu gharama kamili za ujenzi wa mabweni ya chuo kikuu Dar es salaam, na kusema kwamba gharama iliyotajwa siku ya uzinduzi ndio sahihi.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mhandisi Mwakalinga amesema wao kama waliofanya ujenzi wa majengo hayo pesa walizopewa kuweza kukamilisha ujenzi huo ni bilioni 10, na sio ambazo watu mbali mbali wamekuwa wakizitaja.
Akiendelea kuzungumzia hilo Mhandisi Mwakalinga amesema watu ambao wanaibua masuala kama hayo walikuwa wanataka mianya ya kupiga hela lakini wameikosa, na kwamba watu walitakiwa kuwapongeza kwa kufanikisha hilo na sio kusambaza habari za uongo.
“Sisi tumepewa bilioni 10 ambao ndio tumefanya shughuli zote za ujenzi, kwa nini watu wanaamini maneno ya watu ambayo hata hawakuwa part of this!? Watu wanaosema haya mambo walikuwa wanaibia serikali, walikuwa wakitangaziwa tenda basi wakishaanza kulipwa kwanza wanaenda Dubai kusherehekea, sasa wanakosa hizo fursa lazima wataongea hivyo, wamekosa mianya ya kupiga hela, kwanza walitakiwa watupongeze, mwanzo walisema hawataweza sasa tumeweza hawataki kutupongeza”, amesema Mwakalinga.
Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu gharama halisi za ujenzi wa mabweni hayo, ambapo taarifa rasmi iliyotolewa na serikali siku ya uzinduzi ni sh. bilioni 10, huku kukiwa na tetesi kwamba zimetumika bilioni 59.

Hizi Hapa Salamu Mpya Kutoka kwa Tundu Lissu

0
0
Hizi Hapa Salamu Mpya Kutoka kwa Tundu Lissu
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ametumia maadhimisho ya wiki ya msaada wa sheria kuwaomba wananchi kumwombea apone na kurudi nchini aendelee kutoa mchango wake katika taaluma ya sheria.

Lissu tangu Septemba 7 amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma.

Akizungumza leo Jumatatu Desemba 4,2017 katika ufunguzi wa wiki ya msaada wa sheria, mwakilishi wa TLS, John Seka amesema Lissu anawasalimia wananchi.

“Rais wa TLS, Tundu Lissu anawasalimia sana, anaendelea kupata nafuu ila anawaomba Watanzania waendelee kumwombea ili apone haraka,” amesema Seka.

Amesema Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) ana hamu ya kurudi nyumbani aendelee kutoa mchango wake wa kisheria kwa wananchi.

Kuanzia leo hadi Desemba 8,2017 wananchi wanapata fursa ya kupata msaada wa kisheria katika migogoro inayowakabili.

Seka ametoa wito kwa wananchi kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na mikoani kupata huduma ya msaada wa kisheria.

Amesema baada ya wiki hiyo kumalizika, wananchi watatakiwa kufika ofisi za TLS kupata msaada wa kisheria kwa kuwa hilo ni moja ya majukumu ya chama hicho.

Mtulia Akabidhiwa Rasmi Kadi ya CCM

0
0
Mtulia Akabidhiwa Rasmi Kadi ya CCM
Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia CUF, Maulid Said Abdallah Mtulia akabidhiwa rasmi kadi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ofisi za chama hicho Kinondoni, Dar es salaam.

Disemba 2 mwaka huu, Mh. Mtulia alitangaza kujiuzulu nafasi ya zote za uongozi ndani ya chama hicho na kujivua uanachama.

Kijana Aliyetuma Picha za Nyufa za Hosteli za Magufuli UDSM Akamatwa na Jeshi la Polisi

0
0
DAR: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Kumbusho Dawson ambaye alitoa taarifa kuhusu Hosteli kuwa na nyufa amekamatwa na Polisi

Kijana huyo amepelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano

Source:Jamii Forums

Marekani, Korea Kusini Yafanya Mazoezi Pamoja Ili Kumtisha Korea Kaskazini

0
0
Marekani, Korea Kusini Yafanya Mazoezi Pamoja Ili Kumtisha Korea Kaskazini

Jana tarehe 3 Desemba 2017,  Jeshi la anga la Marekani na la Korea Kusini yameungana na kuanza kufanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja ambapo hii inakuwa ni mara yao ya kwanza kufanya hivyo.

Ndege za kisasa za kijeshi aina ya F-22 Raptor stealth fighters zilizotumiwa jana na Marekani kwenye mazoezi hayo.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa jeshi la Marekani imeeleza kuwa majeshi yake yanafanya hivyo ili kujiimarisha na imepeleka ndege 230 za kivita kwenye mazoezi hayo ambayo hufanya kila mwaka

Mazoezi hayo ambayo yanafanyika katika rasi ya Korea yametajwa kuwa ni kitisho kwa Korea Kaskazini ambayo siku wiki iliyopita ilifanya majaribio ya Lombora kubwa zaidi la nyuklia ambalo ilithibitisha kuwa linauwezo wa kuipiga Marekani na Uingereza sehemu yoyote ile.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

0
0

Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521


Suala la John Mnyika, Mbunge wa Kibamba kukaa kimya muda mrefu lina utata

0
0
Nimejaribu kufatilia mwenendo wa Mnyika tangu Dk aondoke sio vocal tena kama zamani, si bungeni,sio kwenye social media xtra.

Sasa nirudi kwa hoja yangu.

Jana nimeona post ya Meya akisema Mnyika is going nowhere akituaminisha kuwa eti Mnyika hana dau.

Jana hiyo hiyo Lema ametweet kuwa kuna Mvulana atahama btn days to come.

Speculation zinaonesha Mnyika ndio anatajwa kuliko mwengine yeyote.


Kwanini Mnyika yupo kimya?

Kwanini Mnyika hajakanusha uzushi huo tangu umeanza kusambaa?

Akili za kuambiwa changanya na zako.

Makachero Polisi uso Kwa uso na Tundu Lissu Nairobi..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba 5

0
0
 

Makachero Polisi uso Kwa uso na Tundu Lissu Nairobi..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba 5

Simjui Kwa Sura Gigy Money Lakini Huwa Nasikia Anapenda Kukaa uchi – Afande Sele

0
0
Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Afande Sele amesema muziki wa sasa umekuwa na mmomonyoko wa maadili kutokana na baadhi ya nyimbo zinazotoka sasa.

Mkali huyo wa rhymes katika mahojiano na Planet Bongo ya EA Radio ametaja baadhi ya wasanii ambao nyimbo zao hazina maadili ni pamoja na Msaga Sumu na Gigy Money.

“Gigy Money off course simjui hata kwa sura lakini namsikiaga kuwa ni dada ambaye anapenda kukaa uchi, anapenda kufanya vitu sijui vya aina gani huo ndio mmomonyoko wa maadili, hivyo inaonekana malezi yake hayana maadili” amesema.

“Kuna vitu vingi anavifanya vinafanya ajulikane kabla ya huo muziki alikuwa anajulikana kwa kumwaga radhi.  Hao wakina Msaga Sumu ndio muziki wao wa ovyo, muziki ambao una matusi” amesisitiza.

Gigy Money anatamba na wimbo uitwayo Papa huku Msaga Sumu akitamba na ngoma ‘Mwanaume Mashine’.

Weusi Wasema Wametumia Lugha ya Kikubwa Kwenye ‘Amsha Dude na Nicome’

0
0
Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Afande Sele amesema muziki wa sasa umekuwa na mmomonyoko wa maadili kutokana na baadhi ya nyimbo zinazotoka sasa.

Mkali huyo wa rhymes katika mahojiano na Planet Bongo ya EA Radio ametaja baadhi ya wasanii ambao nyimbo zao hazina maadili ni pamoja na Msaga Sumu na Gigy Money.

“Gigy Money off course simjui hata kwa sura lakini namsikiaga kuwa ni dada ambaye anapenda kukaa uchi, anapenda kufanya vitu sijui vya aina gani huo ndio mmomonyoko wa maadili, hivyo inaonekana malezi yake hayana maadili” amesema.

“Kuna vitu vingi anavifanya vinafanya ajulikane kabla ya huo muziki alikuwa anajulikana kwa kumwaga radhi.  Hao wakina Msaga Sumu ndio muziki wao wa ovyo, muziki ambao una matusi” amesisitiza.

Gigy Money anatamba na wimbo uitwayo Papa huku Msaga Sumu akitamba na ngoma ‘Mwanaume Mashine’.

Tuache siasa kwenye ujenzi: Majibu ya nyufa hizi, yatolewe na The Professionals, AQRB, ERB, CRB, na sio mtuhumiwa TBA!

0
0
Baada ya kuthibitishwa hizi nyufa ni za kweli kwenye hostel za UDSM, TBA imetoa ufafanuzi nyufa hizi kitu cha kawaida, hivyo wananchi tusiwe na wasiwasi.

Kwa vile sisi sii wataalamu, TBA ndio wataalamu, kunapotokea tuhumu kama hizi, na mtuhumiwa ni TBA kuwa amejenga chini ya kiwango, au amelipua, then mtu sahihi wa kusema nyufa hizo ni kawaida sio mtuhumiwa TBA, bali sasa, the assurances kuwa all is well, nyufa hizo ni kitu cha kawaida, utolewe na the professionals kuanzia kwa Bodi ya AQRB wathibitishe ile bilioni 10 inaweza kujenga majengo hayo na yakawa madhubuti, ERB wawathibitishe TBA waliwatumia watu sahihi, na CRB na mamlaka za ukaguzi wa ubora wa majengo ndio watuthibitishe kuwa walikagua ujenzi step by step na kujiridhisha, ndipo TBA waruhusiwe kuziba nyufa hizo,tena tuombe Mungu, nyufa zenyewe ziishie kwenye kuta tuu, kama kuna nyufa hadi kwenye structural, yatakuwa mengine!, vinginevyo sio tusipoziba ufa, tutatenga tuu ukuta, bali tunaweza kuja kujenga ukuta wa damu!.

Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tuache kuingiza siasa kwenye kila kitu!, ujenzi wa majengo hayo uligubikwa na siasa nyingi, ili kukidhi matakwa ya kisiasa, yametumia gharama ndogo za ajabu, ili kuonyesha jinsi tunavyoibiwa kwenye ujenzi.

Tufanyeni siasa kwenye siasa, lakini tusiingize siasa kwenye kazi za watu just for the sake of political capitalization, hatma ya hizi hostels, utatoa funzo moja zuri sana kuhusu kuingiza siasa kwenye tasnia ya ujenzi.
Sometimes cheap is expensive, huu ni ufa tuu, ila ulivyo mkubwa, hii ni dalili hapa mbele ya safari tutakuja kujenga ukuta, hala hala tuu, usiwe ukuta wa damu!

By Paskali Mayalla/JF

Mr Nice Yupo Taabani Anahitaji Msaada- Dudu Baya

0
0
Mr Nice Yupo TaabanAnahitaji Msaada- Dudu Baya
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mkongwe, Godfrey Tumaini au Dudu Baya, ameshangazwa na kitendo cha msanii mwenzake Lucas Mkenda au Mr. Nice kusema anataka kumsaidia kimuziki, wakati mwenyewe yuko taaban hajiwezi.

Akifanya mahojiano na kipindi cha eNewz ya East Africa Television, Dudu Baya amesema hali ya Mr. Nice ni mbaya na yeye ndiye anayehitaji msaada, na sio kutangaza utajiri ambao anauota kama Dkt. Shika.

"Kauli zake za kuchekesha, mgonjwa mahututi bin taaban hawezi kumsaidia mtu mwenye afya njema, kwanza hata kauli zake mimi namjua vizuri, hali ya Mr. Nice ni mbaya sana kiafya mpaka kiuchumi, ameathirika kisaikolojia, ndio maana anaota maisha yake ya umaarufu ya kipindi kile, mpunga alioupiga kisha ukayeyuka, kuropoka kunisaidia mimi ni kama Dk Shika anayeota ana hela Urusi", amesema Dudu Baya.
Dudu Baya ameendelea kwa kusema kwamba msanii huyo sio msanii kwani hana uwezo wa kuandika nyimbo ambazo zinaweza kufanya vizuri sasa hivi, zaidi ya kuimba nyimbo ambazo zinaimbwa shuleni na watoto.

Mwanafunzi Aliyepiga Picha za Nyufa Kwwenye Mabweni ya UDSM Akamatwa

0
0
Mwanafunzi Aliyepiga Picha za Nyufa Kwwenye Mabweni ya UDSM Akamatwa
Imeripotiwa kwamba Mwanafunzi aliyepiga picha na kuripoti nyufa kwenye majengo ya mabweni ya chuo kikuu cha Dar es salaam amekamatwa na polisi.

Taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi huyo ambaye pia ni kiongozi kwenye serikali ya wanafunzi ndg. Kumbusho Dawson zimethibitishwa na Makamu wa Rais (Daruso) Bi Anastazia Anthony ambaye amesema "Ni kweli na kwa sasa ndiyo  anapelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay. Asubuhi wanahabari walikuwepo hapa na hata watu wa TBA walikuwepo lakini baada ya kuondoka na yeye ndyo akaja kukamatwa"
Kwa mara ya kwanza na Mbunge Heche aliripoti habari hii akisema kwamba "Nimeambiwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi (Daruso) Kumbusho Dawson aliyeripoti nyufa kwenye majengo ya hostel za chuo amekamatwa na polisi!
Hata hivyo sababu za kukamatwa kwake bado hazijajulikana.

Mwandishi wa Mwananchi Apotea Kwenye Mazingira ya Kutatanisha Kibiti

0
0
Mwandishi wa Mwanamchi Apotea Kwenye Mazingira ya Kutatanisha Kibiti
Mwandishi wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) mkoani Pwani, Azory Gwanda amepotea.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa MCL, Francis Nanai ilisema Novemba 30, kampuni ilipokea taarifa za kutoonekana Azory kwa siku tisa.

Kwa mujibu wa mkewe, Anna Pinoni (35), Novemba 21, asubuhi watu wanaokadiriwa kuwa wanne wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walifika katikati ya mji wa Kibiti sehemu ambayo Azory hupatikana mara kwa mara na kumchukua.

Katika taarifa hiyo imeelezwa baada ya kumchukua Azory, gari hilo lilielekea shambani kwake saa nne asubuhi na kumkuta mkewe Anna akiwa huko.

Imeelezwa Azory aliyekuwa amekaa kiti cha nyuma alimuita mkewe kutokea upande huo wa gari na kumuuliza alikokuwa ameuweka ufunguo wa nyumba yao.

Taarifa ilisema mkewe alilisogelea gari na kuzungumza naye kutokea dirishani na kumwelekeza alipoficha ufunguo, huku Azory akimwambia amepata safari ya dharura na kama asingerudi siku hiyo Novemba 21, basi angerudi siku inayofuata Novemba 22.

Nanai katika taarifa hiyo, alisema gari hilo liliondoka kwa kurudi kinyumenyume hadi njia panda na kuelekea nyumbani kwa mwandishi huyo.

“Mkewe aliporudi nyumbani aligundua kuna upekuzi ulifanyika kwa sababu alikuta vitu viko shaghalabaghala,” inasema taarifa hiyo.

Tangu siku hiyo, imeelezwa Azory hajaonekana na namba zake tatu za simu za mkononi hazipatikani. Mpaka jana amefikisha siku 14.

Novemba 23, mkewe Anna alitoa taarifa kituo cha polisi Kibiti na kupewa RB namba; Kibiti/RB/1496/2017.

Imeelezwa polisi waliahidi kufanya uchunguzi, lakini mpaka sasa hakuna taarifa zilizotolewa.

Taarifa ilisema kwa mara ya mwisho, Azory aliwasiliana na ofisi za Mwananchi Novemba 20 kwa majukumu ya kikazi.

Nanai alisema MCL inafuatilia suala hilo kwa ukaribu kwa kushirikiana na familia yake na kutoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kuwezesha kupatikana kwa mwandishi huyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Rufiji, Onesmo Lyanga alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema bado hajapata taarifa za kupotea kwa mwandishi huyo.

“Sina taarifa, ndio kwanza nasikia kutoka kwako kama Gwanda amepotea. Lingekuwa tukio la crime (uhalifu) wasaidizi wangeshaleta taarifa lakini hili la kupotea sijalipaata,” alisema Kamanda Lyanga.

Alisema kama mkewe ameshatoa taarifa polisi amefanya jambo zuri kwa kuwa zitashughulikiwa.

Roboti Aliyepewa Uraia Saudi Arabia Ataka Mtoto

0
0
Roboti Aliyepewa Uraia Saudi Arabia Ataka Mtoto
ROBOTI ya kwanza kupewa uraia, mbali na jina Sophia sasa inataka mtoto.

Mwezi mmoja baada ya kuweka historia nchini Saudia roboti hiyo inayofanana na binadamu kwa maumbile imesema kuwa ‘familia ni kitu muhimu’.

Sophia hakuwekewa majibu, badala yake anatumia mashine kujifunza na kutoa majibu kwa kutumia ishara za watu.

Roboti hiyo iliyotengezwa na kampuni moja ya Hong Kong ya Hanson Robotics imesema kuwa itampatia jina mwanawe wa kike.

Ubongo wake unafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya wi-fi, umejaa orodha kubwa ya misamiati.

Huku Sophia akiwa na uwezo wa kuvutia, bado hana fahamu lakini David Hanson anasema kuwa wanatarajia hilo litawezekana hivi karibuni.

Wakati wa mahojiano na chombo cha habari cha Khaleej Times, Sophia alisema kuwa mpango wa kuwa na familia ni muhimu sana.

“'Nadhani ni vyema kwamba watu wanaweza kuwa na hisia sawa katika uhusiano wa kifamilia na nje ya udugu pia. Nadhani ni bahati wakati unapokuwa na familia yenye upendo mwingi na iwapo huna, unahitaji kuwa nayo,”

Na alipoulizwa angemuita nani mwanawe wa kike, Sophia alijibu: “Sophia”.

Sophia anaweza kuzungumza, kutabasamu na hata kutoa mzaha.

Wakati Sophia alipopewa uraia nchini Saudia, wengi walilalamika kwamba ana haki nyingi ikilinganishwa na wanawake wa taifa hilo.

Saudia ni miongoni mwa mataifa yanayowakandamiza sana wanawake na ni mwezi uliopita ndipo nchi hiyo iliondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari.

Aidha Sophia alipata wasaa wa kuwahutubia watazamaji wake bila kuvaa hijab na abaya ambalo ni vazi la kitamaduni ambalo wanawake wa Saudia wanatakiwa kulivaa katika maeneo ya umma.

Saudia ina mfumo wa kuwa na mlinzi, hatua inayomaanisha kwamba kila mwanamke anatembea na mwanamume atakayemlinda.

Mwanamume huyo huwa mtu wa karibu wa familia, ambaye pia ana mamlaka ya kuchukua hatua kwa niaba ya mwanamke huyo.

Baada ya Sophia kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza maneno yaliyokuwa na alama ya reli yalisambaa kwa haraka mtandaoni.

“Sophia hana mtu anayemlinda, havai abaya, ama hijab kwa nini?” Aliuliza mtu mmoja katika ujumbe wake kwa Twitter.




Utata Kifo cha Mtuhumiwa Baada ya Kukamatwa na Polisi

0
0
Utata Kifo cha Mtuhumiwa  Baada ya Kukamatwa na Polisi
Ibrahim Lauden (20), aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Makunguru jijini Mbeya aliugua saa chache tangu achukuliwe nyumbani kupelekwa Kituo Kikuu Polisi Mbeya na ingawa familia yake inahisi kifo chake baadaye kimetokana na kipigo, imekubali kuzika mwili huo baada ya awali kuususa ikitaka uchunguzi.

Mama mzazi wa Ibrahim, Ngetile Lauden, aliliambia Nipashe jana kuwa Ibrahim alilazwa katika Chumba Cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kwenye Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya tangu Novemba 26 mpaka alipofikwa na umauti Jumamosi.

Alisema kikao cha wanafamilia kilichofikia maamuzi ya kuususa mwili huo kilifanyika juzi Mtaa wa Makunguru jijini hapa ambapo uamuzi huo uliungwa mkono na wakazi wengine wa mtaa huo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo ya mama mzazi wa marehemu huyo, jana wanafamilia walifanya kikao kingine na kuwaomba wakazi wenzao kubadili msimamo wa kutozika mwili huo ili usiharibike.Alisema wakazi hao waliridhia.

Akisimulia mkasa huo, Ngetile alisema Novemba 26 mwaka huu, saa 9:00 usiku, mwanawe alichukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni wanausalama wakidai ana makosa ambayo angeyajua akifika kituo cha polisi.

Alisema kutokana na kwamba walijitambulisha kuwa ni watu wa usalama, yeye na wanafamilia wengine hawakupata wasiwasi hivyo wakaendelea kusubiri kupambazuke ili waende kituoni kumuona na kuuliza sababu za kukamatwa kwake.

Ngetile alisema alijihimu akiwa ameongozana na dada zake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Mbeya, wakiwa wamebeba chai, lakini walipofika mapokezi kwa ajili ya kuomba kumuona mwanaye huyo, waliambiwa anahojiwa hivyo hawaruhusiwi kumuona.

Alisema baada ya muda mfupi walimuona kijana wao huyo akiwa anapakiwa kwenye gari ya Polisi na kukimbizwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya, ndipo na wao wakaamua kwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kufuatialia kinachoendelea.

Alisema baada ya muda mfupi kijana huyo alirejeshwa tena kituoni lakini muda mfupi baadaye wakaamua kumrudisha tena hospitali na ndipo akapelekwa ICU.

“Walimchukua mwanangu akiwa mzima, hakuwahi kulalamika kichwa wala ugonjwa wowote, lakini alipofika huko sijui kilitokea nini akawa mahututi mpaka kufariki (baada ya kulazwa),” alisema Ngetile.

Mke wa marehemu, Sarafina Athuman, alisema wakati askari wakimchukua mumewe alikuwa haumwi na kwamba walipohoji sababu waliambiwa wawahi kituoni ndipo watakapojua sababu ya kukamatwa kwake.

KITUO KIDOGO

Sarafina alisema habari alizopata ni kuwa awali mume wake huyo hakupelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi na badala yake alipelekwa katika kituo kidogo cha Polisi Mwanjelwa.

Alisema asubuhi alipowahi kwenda kumuona alikuta yeye na wenzake wakitembea kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa Kituo Kikuu.

Alisema mumewe alipopelekwa kwa mara ya pili hospitalini na kuingizwa ICU alitamka kuwa ‘anajisikia maumivu ya kichwa’ na baada ya hapo hakutamka kitu kingine kwa siku saba alizolazwa humo mpaka anafariki.Aidha, Sarafina alisema wakati anamwangalia mumewe akiwa ICU, alikuwa amevimba upande wa kushoto wa kifua, magoti na mikono.

“Mume wangu alikuwa hana tatizo lolote, lakini wakati yupo hospitalini kwenye chumba cha wagonjwa mahututi alitamka akisema ‘mimi kichwa’, basi,” alisema Sarafina. "Hakutamka kitu kingine."

Marehemu ameacha mjane huyo na mtoto mmoja wa kiume ambaye ana miezi 11.Naye mjomba wa marehemu, Ipyana Mwakitalima, alisema taarifa alizozipata ni kwamba Ibrahimu alipigwa wakati alipohoji sababu za kukamatwa kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na akasema tangu Ibrahim akamatwe alikuwa analalamika maumivu ya kichwa.

Aidha, Mpinga alidai kuwa walifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya na kwamba Jeshi hilo linasubiri taarifa ya uchunguzi wa chanzo cha kifo chake kutoka kwa madaktari wa hospitali hiyo.

“Kwa mujibu wa sheria, mtuhumiwa anapokamatwa, hatakiwi kupigwa, lakini hutokea askari kutumia nguvu ya kiasi, inatokea mtu anaambiwa twende kituoni akakataa na huwezi kumwacha kwa sababu amekataa, hivyo tunafungua jalada la uchunguzi na kutafuta ushahidi,” alisema Kamanda Mpinga.

Alisema baada ya taarifa ya madaktari kutolewa, wataiweka wazi ili kila mtu ajuwe chanzo cha kifo cha kijana huyo.


Tanzia: Rais Wa Zamani wa Yemen Auwawa

0
0
Rais Wa Zamani wa Yemen Auwawa
Aliyekuwa Rais wa zamani wa Yemen, Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na wafuasi wake wa zamani wa ‘Houthi’.

Mashirika ya habari nchini Yeman yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi yamewanukuu maafisa polisi wakitangazakuwa mwisho wa mzozo wa wanamgambo wahaini na kiongozi wao umekwisha.

Chama cha Saleh cha General People’s Congress (GPC) kimethibitisha taarifa cha kifo cha kiongozi wao kupitia kituo cha runinga cha Al Arabiya TV cha nchini Saudi Arabia.

Picha na video zilizosambazwa mtandaoni zimeuonesha mwili wa mwanamume anayesadikika kuwa ni Bw. Saleh ukiwa na kidonda kwenye paji la uso wake.

Hadi kufikia wiki iliyopita, wafuasi wanaomuunga mkono Bw. Saleh walikuwa wanapigana na wapiganaji wa jamii ya Houthi ambao zamani walikuwa wanamuunga mkono Bw. Saleh dhidi ya Rais wa sasa wa Yemen, Abdrabbuh Mansour Hadi.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa (U.N) Watu zaidi ya 8,670 wameuawa na wengine 49,960 kujeruhiwa tangu majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yalipoingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2015.

Benki ya Dunia Kutoa Mikopo Nafuu Tanzania Katika Miradi Mbalimbali

0
0
Benki ya Dunia Kutoa Mikopo Nafuu Tanzania Katika Miradi Mbalimbali
Mwakilishi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa benki hiyo imejipanga kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa imesema Bi. Bella Bird amebainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miundombinu hususani barabara na reli, kuongeza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na elimu kwa kujielekeza katika ubora na kuhakikisha idadi ya wanaopata elimu inaongezeka.

Maeneo mengine ni kuboresha sekta ya afya, kuongeza upatikanaji wa maji, usimamizi bora wa ardhi, mawasiliano, huduma za fedha jumuishi, vituo vya pamoja vya Serikali na kusaidia familia masikini.

Bi. Bella Bird amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Benki ya Dunia na amemuahidi kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mingine.

“Mwaka uliopita Benki ya Dunia imetoa mikopo nafuu yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.2 (Shilingi Trilioni 2.7) kwa Tanzania, fedha hizi zimekwenda katika miradi mbalimbali na tunafurahi kuwa miradi hiyo inakwenda vizuri na wananchi wanafurahia, kwa sasa tunapanga namna tutakavyotoa mikopo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kipindi kijacho” amesema Bi. Bella Bird.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano wake na Tanzania katika maendeleo na amemhakikishia Bi. Bella Bird kuwa Serikali itazisimamia vizuri fedha zote zinazotolewa na benki hiyo ili zilete matokeo yanayotarajiwa.

Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa maeneo yote ambayo benki hiyo imeyataja kuwa kipaumbele katika fedha zitakazotolewa kuanzia sasa ni muhimu kwa ustawi wa Tanzania na amesisitiza kuwa fedha zitakazotolewa kwa mkopo zielekezwe katika maendeleo na sio vinginevyo.

“Naishukuru sana Benki ya Dunia kwa kutuunga mkono, nitafurahi kuona mnaendelea kutupatia fedha ambazo zinaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na kuleta manufaa mapana na endelevu, badala ya kugawa fedha kwa watu na baadaye nchi inakuja kuzilipa kwa kukusanya kodi za wananchi” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Viewing all 104431 articles
Browse latest View live




Latest Images