Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Tetemeko Latokea Chamwino Mkoani Dodoma na Kuleta Madhara Katika Nyumba Zaidi ya 60

$
0
0
Tetemeko Latokea Chamwino Mkoani Dodoma
Wataalamu wa jiolojia wamesema kuwa tetemeko la ardhi limetokea Kata ya Aneti wilayani Chamwino usiku wa kuamkia jana lina ukubwa wa 5 katika kipimo cha richter.

Tetemeko lenye ukubwa wa 5.1 kipimo cha richter lilitokea Julai mwaka juzi katika kata hiyo na kusababisha nyumba zaidi ya 60 kupata nyufa.

Ofisa Mwandamizi wa Jiolojia katika Wakala wa Jiolojia Nchini (GST), Gabriel Mbogoni alisema tetemeko hilo limetokea katika maeneo lilipotokea mwaka jana Kusini

Mashariki wa mji wa Aneti.

Alipoulizwa kama tetemeko hilo lililotokea saa 9 limeleta madhara yoyote, Mbogoni alisema hajapata taarifa.

“Ukubwa wa 5 siyo la kawaida. Unakumbuka la Bukoba lilikuwa na ukubwa gani? Ni kama 5.7 tetemeko linaweza likawa na ukubwa wa tano hadi saba lakini lisilete madhara,” alisema.

Mbogoni alisema tetemeko linaweza likawa na ukubwa mdogo lakini likaleta madhara kutegemea na mpasuko wa miamba umetokea katika kina gani.

“Inategemea pia na eneo ambalo mawimbi yanapita, ile miamba iko namna gani,” alisema Mbogoni.

Alifafanua kuwa tetemeko hilo lilipiga kati ya sekunde nne na tano na kwamba likipiga kati ya sekunde 20 hadi 30 madhara yake ni makubwa sana.

Mbogoni alisema madhara hayo yanatokana na jengo kutikiswa kwa muda ambazo tetemeko linadumu.

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga alisema hadi jana mchana kulikuwa hakujaripotiwa madhara yoyote.

“Nimewasiliana na viongozi wa kule, diwani na mwenyekiti wa kitongoji wanasema ni kweli lilitokea lakini hadi sasa hakujaripotiwa madhara yoyote,” alisema.

Tetemeko kubwa la ardhi kutokea nchini lilitokea miaka tisa iliyopita katika eneo la Oldonyo Lengai ambalo lilikuwa na ukubwa wa 5.9 kwa kipimo cha richter.



Mnyika Afunguka Kuhusu Kujiuzulu Nafasi Yake Chadema

$
0
0
Mnyika Afunguka Kuhusu Kujiuzulu Nafasi Yake Chadema
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika amesema taarifa kwamba amejiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema -Bara hazina ukweli.

Mnyika ambaye amekuwa akitajwa tajwa kwamba atakihama chama hicho, ametoka kauli hiyo baada ya kuwapo taarifa kwamba  amejiuzulu wadhifa huo.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Desemba 5,2017 jioni kuhusu taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu; Mnyika amesema, ‘’Si kweli ni taarifa za uongo.’

Waziri Ummy Awapa Makavu Wazungusha Raundi Baa

$
0
0
Waziri Ummy Awapa Makavu Wazungusha Raundi Baa
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewaasa wanywaji  pombe kuacha kuzungusha raundi baa badala yake wawekeze kwa watoto kwa kuwawekea akiba benki kwa maisha yao ya baadaye.

Ummy alitoa rai hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa elimu ya fedha kwa ajili ya watoto na vijana iliyoandaliwa na Benki ya NMB.

NMB kupitia kampeni yake ya Wajibu inamaanisha ‘Wajibika’ ni mpango wa elimu kwa wanafunzi na wazazi unaojumisha akaunti tatu za akiba ikiwamo NMB Mtoto, NMB Chipukizi na NMB Mwanachuo.

 Ummy alisema kabla baba hajaenda baa kuzungusha raundi 10 za bia, anapaswa kujiuliza kama mtoto wake ana akaunti.

“Pia kwa mwanamke badala ya kumtunza shoga yako beseni lililosheheni vitu vya Sh. 200,000, hakikisha kwenye fedha hiyo unatoa ya kumwekea akiba mtoto wako.

“Watanzania tujifunze kuweka akiba za watoto wetu. Fedha unazotumia kwa mambo yasiyo na mpango  kwa ajili ya mtoto wako, njoo NMB fungua akaunti ya mtoto akaunti, Chipukizi au Mwanachuo Akaunti,” alisema.

“Hakuna mtoto wa taifa la kesho, kesho inaanza leo. Kwa hiyo kama inaanza leo, anza kuweka akiba kwa ajili ya kesho,” alisema Ummy.

Waziri huyo alisema takwimu zinaonyesha Tanzania ina watoto milioni 25 na  kama kila mzazi ataamua kumfungulia akaunti mtoto wake na kumwekea Sh. 50,000 ina maana watapata jumla ya Sh. bilioni 500.

Kadhalika aliipongeza benki hiyo kuhusiana na kampeni yao ya Jifunze, Jipange na Wajibika na kueleza kuwa ni ya umuhimu kwa sababu inawakumbusha wazazi namna ya kuweka akiba za watoto.

Alisema pamoja na kwamba serikali imeweka elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne haimaanishi kuwa mzazi hachangii chochote.

“Yapo baadhi ya mambo ambayo mzazi anaingia gharama kuchangia kwa hiyo kama mtoto akiwekewa akiba hakutakuwa na changamoto,” alisema.

Alisema amekubali kuwa balozi wa kampeni hiyo ya elimu ya fedha na kueleza kuwa katika kuhamasisha umma kuwafungulia watoto wao akaunti, ataanza na familia yake.

“Nitakuja kabla ya mwisho wa mwaka huu kufungua akaunti za watoto wangu wawili, mmoja nitamfungulia mtoto akaunti na mwingine chipukizi akaunti,” alisema.

Alisema takwimu za Benki Kuu Tanzania (BoT) zinaonyesha kuwa idadi ya wanaotumia huduma za kibenki zimeongezeka ambapo mwaka jana walikuwa asilimia 9.1 na mwaka huu wamefikia asilimia 16.7.

Katika hatua nyingine, Ummy ameiomba benki hiyo iweke utaratibu wa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili wakati wakihamasisha watu kufungua akaunti za watoto, wawe na utaratibu wa kuwawezesha kupata kadi za bima ya afya za ‘Toto Afya Card’.

“Ombi langu kwenu tukae pamoja na mfuko wa taifa wa bima ya afya ili tuhamasishe watu wakifungua akaunti za watoto, kuwe na utaratibu wakifikisha kiasi cha kufungulia bima ya afya, utaratibu ufanyike wapewe kadi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema akaunti hizo za aina tatu ni mahususi kwa vijana ambao wengi wao ni wale walioko mashuleni kwa ajili ya kuwasaidia wajiwekea akiba na kupanga matumizi yao.

Pia alisema benki hiyo inatambua kupanua elimu ya fedha ni muhimu ili kuweza kutumika kikamilifu kunufaisha uchumi jumuishi.

Kadhalika, alisema benki hiyo imeongeza uelewa kuhusu akaunti ya Chipukizi ili kuongeza kupatikanaji fedha kwa vijana ili kusaidia kutimiza malengo yao na kujijengea tabia ya kujiwekea akiba.


Trump Kuutambua Jerusalem Kuwa Mji Mkuu wa Israel

$
0
0
Mji wa JerusalemTrump Kuutambua Jerusalem Kuwa Mji Mkuu wa Israel
Maafisa wa serikali ya Marekani wamesema kuwa rais Donald Trump, leo atautambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Ikulu ya White House imethibitisha kuwa rais Donald Trump pia atazungumza kuhusu juu ya kutangaza rasmi kuhamishia kwa ubalozi wa Marekani Jerusalem.
Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya white house sarah sanders amesema kuwa Trump alizungumza na baadhi ya viongozi siku ya jumanne kuhusu mpango yake ya kuhamishia ubalozi huo kutoka Tel Aviv kuupeleka Jerusalem.
Kwa nini mji wa Jerusalem ni mtakatifu?
Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel
''Amezungumza na baadhi ya viongozi asubuhi ya jana na atendelea kuwa na majadiliano na wadau wanaohusika lakini atafanya maamuzi yenye umuhimu kwa Marekani''
Wakati huo huo viongozi wa Palestina, Misri, Jordan na Saudi Arabia, wametoa onyo kwa rais Trump kuwa kuhamishia ubalozi huo Jerusalem kutadhoofisha kabisa juhudi za kuleta amani mashariki ya kati.

Shamsa Ford Amuonya Wema Sepetu Kuhusu Kuhama Vyama

$
0
0
Shamsa Ford Amuonya Wema Sepetu Kuhusu Kuhama Vyama
KUFUATIA kuhama chama kutoka Chadema kwenda CCM kwa mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Wema Sepetu, msanii mwenzake, Shamsa Ford ameibuka na kumtahadharisha pamoja na wasanii wote kwa jumla.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Shamsa alisema wao siyo wanasiasa hivyo suala la Wema la kwenda na kurudi kwenye vyama vya siasa inawezekana anapata faida lakini cha muhimu asisahau kazi yake.

“Siwezi kuzungumzia sana suala la Wema kuhama vyama maana ni lake binafsi na huenda lina faida kwake, nawasihi tu wenzangu wasisahau kazi yao ya sanaa iliyowatambulisha kwa jamii,” alisema Shamsa.

Koleta Afunguka Kuhusu Maisha Ya Ndoa " Kudumu Kwenye Ndoa ni Mungu Tu"

$
0
0
MKONGWE wa filamu za Kibongo, Koletha Raymond amefunguka kuwa suala la kudumu kwenye ndoa ni la Mungu tu kwani kwa akili zake hawezi kujihakikishia kwa asilimia mia moja.

Koletha alisema hayo kutokana na ndoa nyingi za mastaa kutodumu ambapo alisema ingawa ana imani ndoa yake itadumu, lakini ni Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kulijua hilo kwa ufasaha.

“Kikubwa ni kumshirikisha Mungu tu kwa kweli na mimi mwenyewe kuchezea karata yangu vizuri, siwezi kusema ndoa yangu itadumu milele, ni kwa neema tu maana kuna mengine hayavumiliki,” alisema Koletha.

Diamond Platinums Aachia Video Mpya ya Wimbo wa Sikomi..Itazame Hapa

$
0
0
Diamond Platinums Aachia Video Mpya ya Wimbo wa Sikomi..Itazame Hapa

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumatano

Diamond Ampa DJ Wake Romy Jones Nyumba ya Milioni 100 Kama Zawadi ya Harusi

$
0
0
Habari Wadau..

Naona Rais wa WCB mambo ya vyuma vimekaza yeye hayamuhusu.. Maana hela anachukua kwa wateja wake waliopo dunia nzima...

Juzi Kamzawadia DJ wake wa Muda Mrefu Romy Jones Nyumba ya Milion 100

Mama Diamond nae kujibu mapigo kamzawadia Romy Jones kiwanja cha thamani ya milioni 80...

A boy from Tandale... Anawapenda sana wafanyakazi wake

VIDEO:

Punguza Unene na Kutibu Magonjwa Kwa Kutumia Dawa za Edmark...Bonyeza Hapa

$
0
0
TUNA DAWA AMBAZO NI VIRUTUBISHO NA CHAKULA MBADALA ZIMEHAKIKIWA NA TFDA

Ni uhakika kwa afya yako, kupunguza uzito na Sumu mwilini, Mafuta/Sehemu Mbaya, Kitambi na Nyama Uzembe na kutibu MAGONJWA Mbali mbali yaliyoshindikana

Loose Weight Trainer ni Msaada wako Wasiliana Nasi Kwa WhatsApp 0713 777 470

Upate Suluhisho la Afya yako Bila Madhara pia unaweza kujiunga nami ili ufanye Biashara hii Nicheki


Intagram napatikana kwa jina @looseweight_trainer

Sina Mpango wa Kuhamia CCM Kama Inavyodaiwa Mitandaoni- Kubenea

$
0
0
Sina Mpango wa Kuhamia CCM Kama Inavyodaiwa Mitandaoni- Kubenea
Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) na Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amesema hana mpango wowote wa kuhama Chama chake cha Demokrasia na Maendelea(CHADEMA) na kuhamia CCM kama inavyodaiwa mtandaoni.

Kubenea ameiambia Bongo5 leo, kuwa wananchi wanapaswa kupuuza taarifa hizo kwani yeye ataendelea kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama chake.

“Nadhani ni udhaifu wa watu kwasababu kama mtu anaandika taarifa kwamba Mbunge ana hama na aliyeandika taarifa hizo ni Mbunge bila kumuuliza Mbunge mwenzake bila kuwasiliana nae hiyo ni shida me naona is not fair,” amesema Kubenea.

“Wananchi wapuuze taarifa zozote zinazonihusisha mimi na kuondoka Chadema na kujiunga na CCM hizo ni za Uzushi mimi bado ni mwananchama wa Chadema na bado ni Mbunge wa Ubungo na sina mpango huo na sijawahi kuzungumza na mtu yoyote.”

Nimefurahi Sana Kutembelewa na Mzee Mwinyi Licha ya Umri Wake 93 Ametafuta Muda Kuja Kunipa Pole- Tundu Lissu

$
0
0
Nimefurahi SanaKutembelewa na Mzee Mwinyi Licha ya Umri Wake 93 Ametafuta Muda Kuja Kunipa Pole- Tundu Lissu
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema licha ya umri wa miaka 93 alionao Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi bado amediriki kufunga safari kwenda kumtembelea na kumpa pole.

Lissu, ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutembelewa na Mzee Mwinyi katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anaendelea na matibabu.

Lissu amelazwa hospitalini hapo tangu Septemba 7 anakotibiwa akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma akitokea kuhudhuria mkutano wa Bunge.

Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu kuhusu kutembelewa na Mzee Mwinyi, mwanasheria huyo wa Chadema pamoja na mke wake, Alice walisema wamefurahi kutembelewa na kiongozi huyo.

“Nimefurahi sana kwamba umri wote alionao wa miaka 93 si kidogo, ametafuta muda kuja kunipa pole hospitalini ni kitu kizuri sana, ni ubinadamu mkubwa sana,” alisema Lissu ambaye alionekana mwenye furaha.

Rais mstaafu Mwinyi anakuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa Serikali waliomtembelea Lissu kwani hivi karibuni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan naye alifika hospitalini hapo kumjulia hali.

Mzee Mwinyi akiambatana na mke wake na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya walifika hospitalini hapo kumjulia hali mbunge huyo na picha zinawaonyesha wawili hao wakizungumza huku nyuso zao zikiwa na tabasamu.
Chanzo: Mwananchi 

Ma-DJ Walipigwa Stop na Kupewa Hela Wasicheza Nyimbo Zangu- Baraka Da Prince

$
0
0
Ma-DJ Walipigwa Stop na Kupewa Hela Wasicheza Nyimbo Zangu- Baraka Da Prince
Msanii Baraka The Prince amedai kuwa kuna wakati ma-Dj walikuwa wanaambiwa wasicheze nyimbo zake.

Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘Sometimes’ ameiambia The Base, ITV hata hivyo taarifa zilikuwa zinamfikia kutokana anaishi na watu vizuri na si kama inavyokuwa ikienezwa.

“Kuna baadhi ya Dj’s walikuwa wanaambiwa wasicheze nyimbo zangu, wengine mpaka hela wanapewa kwa ajili ya kutopiga, unakuta mpaka Dj anakufuata anakuambia unajua nimepewa mpaka hela nyimbo yako nisipige” amesema Barakah.

“Kwa hiyo hicho ni kitu cha kushukuru ingekuwa watu hawanipendi nina matatizo na watu inavyokuwa ikienezwa sidhani kama hata kuna mtu angeweza kuthubutu kunifuata na kunipa taarifa kama hizo, it means napendwa na watu na tayari nina empire yangu” ameongeza.

Hata hivyo Barakah hajaweka wazi ni kina nani hasa walikuwa wanashinikiza hivyo.

Umati Wamuokoa Rais wa Zamani wa Georgia Kutoka kwa Polisi Ukrain

$
0
0
Umati Wamuokoa Rais wa Zamani wa Georgia Kutoka kwa Polisi Ukrain
Wafuasi wa rais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili wamemoukoa kutoka kwa gari la polisi kwennye mji mkuu Kiev baada ya kukamatwa kufuatia madai kuwa anasaidia kundi la kigaidi.
Bw Saakashvili 49, aliutaka umati kumuandoa madarakani rais Petro Poroshenko ambaye ni mshirika wake wa zamani.
Alipewa uraia wa Ukrain mwaka 2015 hatua iliyosababisha apoteze uraia wake wa Georgia.
Rais wa zamani wa Georgia aingia Ukrain kwa nguvu
Bw. Saakashvili amekuwa mkosoaji mkubwa wa Bw. Poroshenko.
Anamlaumu rais kwa kushindwa kumaliza ufisadi. Bw Porokoshenko amekana madai kama hayo hapo awali.
Georgian former President Mikheil Saakashvili flashes a victory sign after he was freed by his supporters in KievHaki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Umati wamuokoa rais wa zamani wa Georgia kutoka kwa polisi Ukrain
Akiwa na pingu kwenye mkono mmoja na akizungukwa na mamia ya watu, Bw Saakashvili aliwashauri wafuasi wake kutembea kwenda kwa bunge la Ukrain.
"Ninawashauri kuanza maandamano ya amani ya kumuondoa madarakani Poroshenko. Msiogope," alisema kwa njia ya vipasa sauti.
Ukrain: Urusi ilihusika na udukuzi wa mitandao
Maafisa hawazungumzi lolote kufuatia kukombolewa kwa Bw Saakashvili. Mapema maafisa waliokuwa wamejifunika nyuso walimkamata Bw. Saakashvili, 49 kutoka nyumbani mwake.
Bw Saakashvili anashukiwa kwa kupokea msaada ya kufedha kutoka kwa kundi lenye uhusiano na rais wa zamani wa Ukrain Victor Yanukovich.
Bw. Saakashvile anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela ikiwa atapatikana na hatia.


Waziri wa Furaha, Mahusiano ya Kifamilia Ateuliwa Nigeria

$
0
0
Waziri wa Furaha, Mahusiano ya Kifamilia Ateuliwa Nigeria
Serikali ya Jimbo la Imo nchini Nigeria imeteua waziri atakayeshughulikia masuala ya furaha na mahusiano ya kifamilia.

Uteuzi wa waziri huyo unaelezwa ni mkakati wa kuwasahaulisha wananchi adha za kisiasa na mapigano ya makundi haramu.

Gavana wa jimbo hilo, Rochas Okorocha amesema uteuzi huo ni wa kwanza kufanyika katika Taifa hilo lililopitia kipindi kigumu cha mashambulizi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram na hali mbaya ya kisiasa.

Okorocha amemteua ndugu yake, Ogechi Ololo kuwa waziri wa masuala ya furaha na mahusiano mema ndani ya familia.

Kabla ya uteuzi huo, Ogechi alikuwa msaidizi wa Gavana Okorocha na mshauri wake maalumu wa masuala ya nyumbani. Pia, anahusika na mapambo wakati wa sikukuu ya Krismasi.

Hata hivyo, msemaji wa gavana huyo, Sam Onwuemeodo hakutoa maelezo zaidi kuhusu majukumu ya waziri huyo.

Akizungumza na Shirika la Habari la AFP alisema, “Hakuna kitu kipya zaidi katika uteuzi huo.”

“Gavana ni mtu mbunifu ambaye kila wakati huanzisha vitu vipya serikalini. Jukumu kubwa la waziri huyu ni kuleta ubunifu ambao utaweza kuigwa na magavana wengine. Gavana anataka kuwafanya watu wawe na furaha kila wakati na ndiyo maana ameunda wizara hii kwa lengo hilo,” amesema.

ACT-Wazalendo Kufanya Maandamano Desemba 8

$
0
0
ACT-Wazalendo Kufanya Maandamano  Desemba 8
Idara ya vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo imesisitiza kuwa itafanya maandamano yake ya amani yenye lengo la kupinga vitendo vya utumwa wanavyofanyiwa vijana wa Afrika nchini Libya.

Pamoja na kutojibiwa barua yao ambayo wameliandikia jeshi la Polisi kwenye mkoa wa kipolisi Kinondoni kwaajili ya kuomba kibali cha maandamano hayo lakini wamesisitiza kuwa watafanya hivyo
“Polisi Kinondoni wanasema barua yetu ya maandamano ya tarehe 8/12/17 imetumwa KANDA na mpaka sasa majibu hawajaletewa, wanasema tuulizie tena kesho tunapenda kuujulisha umma kuwa ratiba ya maandamano yetu haijabadilika”, imesema Taarifa ya hiyo kutoka idara ya vijana ACT-Wazalendo.

Idara hiyo ya vijana imepanga kuandamana siku ya Ijumaa Disemba 8 kuanzia saa 4 asubuhi ambapo wataanzia eneo la Leaders Club jijini Dar es salaam na kuishia ofisi za Ubalazi wa Libya nchini zilizopo Upanga jijini Dar es salaam na watatumia barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Hivi karibuni nchini Libya kumeibuka vikundi vya watu ambavyo vinafanya biashara ya utumwa kwa baadhi ya wageni wanaoingia nchini humo hususani wale wahamiaji ambao hufika nchini humo kwa lengo la kuvuka na kuelekea barani Ulaya.

TCRA Kufanya Mapitio ya Leseni za Vituo vya Luninga

$
0
0
TCRA Kufanya Mapitio ya Leseni za Vituo vya Luninga
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema inafanya mapitio ya leseni za vituo vya luninga ili kufanyia utatuzi kasoro zilizojitokeza wakati wa kuhama kutoka mfumo wa analojia kuelekea digitali.

Aidha, imezitaka kampuni zinazorusha matangazo ya luninga kufuata sheria na kanuni za usajili zinazowataka kurusha bure matangazo ya chaneli za ndani.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba, aliyaeleza hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, alipofanya ziara katika ofisi hizo.

Kilaba alisema kuhama kutoka analojia kwenda digitali ilikuwa ni kazi kubwa ambayo lazima ingeleta changamoto ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi.

Alisema kampuni hizo zimekuwa zikikata matangazo ya chaneli za ndani pindi muda wa kifurushi alicholipia mteja kumalizika licha ya mkataba walioingia na TCRA kuelekeza kuwa huduma hizo zitatolewa bure kwa wananchi.

Alisema anatambua kuwapo mvutano kati ya kampuni za urushaji matangazo na watoa huduma wa kituo kuwa nani anapaswa kulipia gharama hizo na ni kiasi gani na kwamba wanalitafutia ufumbuzi suala hilo ili wananchi wapate chaneli hizo bure.

Chaneli zinazotakiwa kupatikana bure ni ITV, TBC, Star TV, Chanel Ten, Clouds TV na TV Tumaini.Naye Naibu Waziri huyo, aliwataka TCRA kusimamia kanuni na sheria hizo ili wananchi wapate huduma hizo bila malipo yoyote.

Aidha, Nditiye, aliitaka TCRA kufunga vibanda vyote vya kusajili laini za simu bila kufuata sheria.Alisema kumekuwapo na idadi ya vibanda na watu wakipita mitaani bila kuwa na vitambulisho na kusajili laini bila kuzingatia kanuni na taratibu za usajili hali ambayo inapelekea baadhi yao kuzitumia kufanya uhalifu.

“Tunataka kila mtu anayetumia laini awe anafahamika. Na taratibu zitumike kama ilivyopangwa kuwa vitambulisho vinavyotakiwa kutumika ni vya kupigia kura au cha uraia. Napendekeza ikiwezekana usajili uwe unafanyika kwenye ofisi za watoa huduma badala ya watu kusajili ovyo mitaani,” alisema.

Straika Mgana Kuchukua Mikoba ya Ngoma Yanga

$
0
0
Straika Mgana Kuchukua Mikoba ya Ngoma Yanga
WAKATI zikiwa zimebaki siku tisa pekee kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, Kamati ya Usajili ya Yanga chini ya mwenyekiti wake, Hussein Nyika, muda wowote ule kutoka sasa inajipanga kumtambulisha mshambuliaji mpya ndani ya kikosi hicho ambaye atachukua mikoba ya Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye ameonekana kuwa msumbufu.

Yanga kwa sasa inatumia nguvu kubwa kwa ajili ya kusaka mshambuliaji mwingine wa kimataifa ambaye atakuja kuungana na washambuliaji, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu kwa ajili ya kuimarisha safu yao hiyo.

Chanzo makini kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatano kuwa kwa sasa mwenyekiti wa kamati hiyo anajipanga kutambulisha mshambuliaji mpya ambaye anaweza kutokea Liberia, Burundi, DR Congo na Ghana ambapo hivi karibuni alipita kwenye nchi hizo kwa ajili ya kusaka mchezaji huyo.

“Muda wowote ule mkae mkao wa kula kwani kunaweza kukatokea jambo la kushangaza kwa kushushwa mshambuliaji mpya ambaye atakuja kuongeza nguvu kwenye eneo letu la ushambuliaji, ambapo mchezaji huyo ndiye atakuja kuchukua mikoba ya Ngoma ambaye yupo kwenye mstari mwekundu wa kuachwa.

“Atakayehusika na zoezi hilo ni mwenyekiti Hussein Nyika, ambaye hivi karibuni alikuwa anazunguka kwenye nchi hizo kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri na muda si mrefu mambo yote yatakuwa wazi,” kilisema chanzo hicho.

Championi Jumatano, lilimtafuta Nyika juu ya suala hilo ambapo alisema: “Tayari hadi sasa nimeshatangaza wachezaji wawili, Fiston Kayembe na Yohana Nkomola na siku chache zijazo kabla ya dirisha kufungwa basi nitaweka wazi kila kitu chetu.
“Hao ambao wanazungumziwa muda si mrefu mtapata majibu yake kama watakuja hapa au la, lakini kwa sasa subirini.”

Wema Sepetu Afunguka Baada ya Kutangaza Nia Yake ya Kurudi CCM "Inanivunja Moyo Najihisi Nimekatishwa Tamaa"

$
0
0
Wema Sepetu Afunguka Baada ya Kutangaza Nia Yake ya Kurudi CCM "Inanivunja Moyo Najihisi Nimekatishwa Tamaa"
Baada ya msanii wa filamu, Bongo Wema Sepetu kurudi CCM kutokea Chadema, hatimaye amezungumzia hilo.

Wema amesema hawezi sana kulizungumzia hilo kwa sababu maamuzi yalishafikiwa lakini anajihisi kukatishwa tamaa.

“Yaani it so complicated najikuta sipo kwenye position ya kuielezea in simple English or Swahili, siwezi lakini tubaki tu tunaomba Mwenyenzi Mungu kwamba everything it will be ok one day inshallah” Wema ameiambia K Fm, Rwanda.

“I am strong, nisingekuwa strong nisingekuwa hapa sasa hivi najaribu kusali kwa hii hali, muda mwingine kama bidamu inakuwa inanivunja moyo najihisi nimekatishwa tama, yaani ok!  acha nimuachie Mungu” ameongeza.

February 24 mwaka huu Wema alijiunga na Chadema akitokea CCM na December Mosi alitangaza kurudi CCM.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images