Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Ujumbe Huu wa Diamond Kwa Mwanae Hatari Tupu...Kua Uje Kuwatembezea Jukumu Lako ni Kupita Nao Tu

$
0
0
Siku ya jana mtoto wa pili wa msanii Diamond, Nillan alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa baada ya kutimiza umri wa mwaka mmoja.
Katika kumtakia kheri ya siku hiyo muhimu kabisa maishani mwake, Diamond ameandika ujumbe wa ambao watu wengi wameshangazwa nao. Kupitia ukurasa wake wake Instagram Diamond ameandika;

Nasemaje! Kua Uje kuwatembezea Baba… We swala la Kutafta ela niachie mie… Jukumu lako ni moja tu, Kupita nao🔥…..Happy 1st Year Lanny!!! 🎂

Pia hapo awali mzazi mwenziye na Diamond, Zari The Boss Lady aliandika ujumbe mzuri kwa Nillani, Zari aliandika;

Ladies and gentlemen help me wish my hanshaaaaaam skwiiiiisshhhh a happy birthday. You surely growing up fast, i see you breaking girls’ 💔s soon b’coz this cuteness is overloaded …. Happy bday my toto @princenillan

Mr Nice Amruka Young Dee " Sijawahi Kumruhusu Binadamu Yoyote Kutumia Kazi Zangu Bila Makubaliano"

$
0
0
Mr Nice Amruka Young Dee " Sijawahi Kumruhusu Binadamu Yoyote Kutumia Kazi Zangu Bila Makubaliano"
Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva kwenye miondoko ya TAKEU, Mr. Nice, amesema hamjui msanii Young D ambaye ametumia wimbo wake, na kwamba hakubaliani na kitendo cha yeye kutumia kazi yake.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Teolevision, Mr. Nice amesema licha ya kutoruhusu mtu yeyote kutumia kazi zake, hajapata taarifa kutoka kwa Young D wala uongozi wake, na hajawahi kumjua kwenye maisha yake.
"Sijawahi kuongea wala kuruhusu binadamu yoyote kutumia kazi yangu yoyote bila makubaliano na ridhaa yangu mwenyewe iwe ni kwa kuniheshimu ama kunidhihaki, so far simjui huyo Young D at all , ndo namsikia kwako", amesema Mr. Nice.
Kwa upande wa Young D amesema suala hilo tayari uongozi wake unalishughulikia ili kumalizana na malalamiko ya Mr. Nice, hata hivyo aliamua kufanya kama kumpa heshima kutokana na kukubali kazi zake alizokuwa akizifanya.

Wolper Awahalika Harmonize na Mpenzi Wake Sara Kwenye Sherehe ya Siku Yake ya Kuzaliwa

$
0
0
Wolper Awahalika Harmonize na Mpenzi Wake Sara Kwenye Sherehe ya Siku Yake ya Kuzaliwa
Muigizaji wa filamu Bongo ambaye kwa sasa ni mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper amekiri kutokuwa na wivu na aliyekuwa mpenzi wake (ex-boyfriend) wake ambaye ni mwanamuziki kutoka kundi la WCB Harmonize na Kuwakaribisha katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Katika kuelekea birthday part ya wolper itakayofanyika leo decemba 7 ameamua kuudhihirishia umma kuwa hana wizu na wa kimapenzi na mpenzi wake wa zamani  ameamua kumualika harmonize pamoja na Sara katika part hiyo.

Wolper aliongeza kuwa amemtaka Sara kuwa rafiki yake na kumsaidia kumpa siri na nyendo za kuchepuka Harmonize

Kampuni ya Mwananchi Yatoa Tamko Kupotea kwa Mwandishi Wao Wataka Waliomchukua Wamrudishe Akiwa Hai

$
0
0
Kampuni ya Mwananchi Yatoa Tamko Kupotea kwa Mwandishi Wao Wataka Waliomchukua Wamrudishe Akiwa Hai
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Francis Nanai amesema kwamba japo hawana uhakika na sababu za kuchukuliwa na watu wasiojulikana kwa mwandishi wao Azzory Gwanda ila inawezekana hata kuandika habari za mauaji yaliyokuwa yanatokea Kibiti ikawa chanzo.

Akizungumza na wanahabari leo wakati wakisisitiza kupatikana kwa mwandishi wa kampuni yao aliyepotea wiki mbili zilizopita huko Kibiti mkoani Pwani, Nanai amesema hawajui sababu maalumu ya kupotea kwa mfanyakazi wao ila wanachoamini wakimpata akiwa hai watapata sababu za kutosha.

"Siwezi kusema sababu za kupotea kwa ndugu yetu Azorry, lakini inawezekana kutokana na ripoti alizokuwa akizifanya kutokana na mauaji yaliyokuwa yakifanyika Kibiti ikawa sababu ya kukamatwa kwake, lakini pengine tukimpata anaweza kutupa mwanga wa sababu za kukamatwa kwake".
Aidha Nanai ameongeza kwa kusema kwamba Mwandishi wao Azzory hakuwahi kuripoti kuhusu kutishiwa amani au kufuatiliwa kwa namna yoyote ndiyo maana hawajui sababu ya kuchukuliwa na watu hao ni nini.

"Tishio lolote kwa mwandishi ni kuingilia uhuru wa habari, tukio la kutekwa kwa huyu mwandishi ni kuingilia uhuru wa vyombo vya habari. Kama kampuni hatujawahi kupata taarifa kama alikuwa anafuatiliwa au aliwahi kutishiwa maisha kutokana na kazi  alizokuwa anazifanya". Ameongeza.
Mbali na hayo Nanani ameomba ushirikiano kutoka kwa vyombo vya usalama wakiwepo Polisi katika kuhakikisha Azzory anapatikana huku akiwageukia waandishi wa habari kuendelea kudumisha ushirikiano waliouonyesha siku ya leo.

Azzorry Gwanda alikuwa mwandishi wa kujitegemea wa kampuni ya Mwananchi Communication Ltd mwenye kituo cha kazi Kibiti- Pwani ambapo anadaiwa kuchukuliwa na watu wasojulikana tangu Novemba 20 mpaka leo hajulikani alipo.

Roma Aogopa Kujitabiria Kifo Baada ya Kuandika Mengi na Kutokea Kweli

$
0
0
Roma Aogopa Kujitabiria Kifo Baada ya Kuandika Mengi na Kutokea Kweli
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Roma amesema kutokana na mambo mengi anayoandika katika ngoma zake kutokea kweli muda mwingine hufikia hatua ya kuhofia.

Rapper huyo katika mahojiano na The Playlist, Times Fm amesema baadhi ya matukio kama Rais. John Magufuli kukalia madaraka hayo ni moja ya vitu alivyoandika toka miaka nyuma na kutokea kweli.

“Kuna muda mwenyewe nakaa napitia mistari yangu najitafakari naona mmmh! eeh Mungu vingine ambavyo nimeviandika visije vikatokea kweli, nisije nikaandika nafa kesho halafu walete” amesema.

“Roma kasema anaenda Zimbabwe lakini kitu kilichotokea Zimbabwe ni mfano wa nchi nyingi za Afrika, watu wanatamani kifanyike kitu kama kile” ameongeza.

Kwa sasa Roma anatamba na ngoma ‘Kiba_100’ ambayo ni yake na Stamina (Rostam).

Kigogo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Afungwa Miaka 15 Jela Kwa Kuiba SMG 8 za Mwajili Wake

$
0
0
Kigogo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Afungwa Jela Miaka 15 Kwa Kuiba SMG 8 za Mwajili Wake
Aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Mkoa wa Tabora, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Bhoke Bruno na wenzake saba jana Jumatano walihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kuiba bunduki nane aina ya SMG, mali ya mwajiri wao.

Wengine waliohukumiwa kifungo katika hukumu iliyosomwa na Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Sharmira Sarwatt ni Koplo Idd Abdalah, PC Mwinyi Gonga na Said Mgonela, wote kutoka kikosi cha FFU Tabora.

Kwa pamoja, waliokuwa waajiriwa hao wa jeshi la polisi kwa pamoja walitiwa hatiani kwa makosa matatu ya kula njama, kuiba na kushindwa kuzuia tukio.

Mahakama pia iliwapa adhabu kama hiyo washtakiwa wengine watatu Shaban Haruna, Shaban Kabanika na Idd Supu waliodaiwa kushirikiana na waliokuwa maofisa hao wa polisi.

Washitakiwa wengine watatu kati ya 10 waliokuwa wakishtakiwa, Charles Abihud, Emmanuel Festo na Nicholaus Mlelwa, waliachiwa huru baada ya ushahidi dhidi yao kukosekana.

“Ushaihidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri umeithibitishia Mahakama pasipo shaka kuwa washtakiwa saba kati ya 10 walihusika na makosa yanayowakabili, hivyo wanahukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kila kosa,” alisema Sarwatt.

Kutokana na adhabu ya makosa yote matatu yanaenda pamoja, washtakiwa watakaa magereza kwa miaka mitano.

Awali upande wa mashtaka ulioongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Juma Masanja uliiambia Mahakama kuwa kwa pamoja, wahtakiwa walitenda makosa hayo kati ya Aprili 2013 hadi Aprili 2014.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa washtakiwa kwa nyakati tofauti, walikula njama ya kuiba bunduki aina ya SMG zilizokuwa zikihifadhiwa katika ghala la kituo cha FFU mjini Tabora.

Upande wa mashitaka ulidai katika shitaka la pili kuwa katika kipindi hicho washitakiwa kwa pamoja washtakiwa bila kuwa na uhalali, walichukua bunduki nane kwenye ghala hilo, wakati shtaka la tatu likiwa ni kushindwa kuzuia uhalifu kutendeka ambalo.

Katika shauri hilo la jinai namba 104/2015, washtakiwa waliwakilishwa na mawakili Kelvin Kayaga na Mussa Kassimu wa mjini Tabora.

Waziri Atoa Siku 30 kwa Familia 59 Zilizo Ndani ya Eneo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Kuondolewa

$
0
0
Waziri Atoa Siku 30 kwa Familia 59 Zilizo Ndani ya Eneo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Kuondolewa
 Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ametoa siku 30 kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (Taa) kuziondoa familia 59 zilizo ndani ya eneo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).

Pia, ameitaka Taa kuhakikisha hatimiliki za ardhi za kampuni ya Puma Energy na Tanzanair zinafutwa kwa sababu ziko ndani ya uwanja huo ambao nao una hatimiliki yake.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutembelea kampuni hizo, Nditiye alisema haiwezekani kukawa na watu wengine wanaomiliki ardhi katikati ya uwanja huo na wana hatimiliki.

Pia, aliitaka mamlaka hiyo kuwaondoa watu wote waliojenga karibu na uzio wa uwanja huo bila kuacha mita tatu kama inavyotakiwa katika sheria ya ardhi au mita 10 kwa mujibu wa sheria ya viwanja vya ndege.

Naibu waziri huyo aliagiza viwanja vyote viwekewe mipaka na kwamba, vile ambavyo havina hatimiliki navyo vitafutiwe.

“Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba inazirudisha na kuzitambua mali zake zote. Hakikisheni viwanja vyote nchini vinakuwa na hatimiliki, mpaka sasa uwanja wa Mwanza hauna hatimiliki,” alisema. Nditiye aliitaka Taa kuhakikisha kwamba inapata taarifa zote za Puma Energy inayouza mafuta ya ndege ili waweze kukusanya tozo zao na pia kuimarisha usalama kwa usafiri wa ndege. “Wekeni watu wenu pale Puma kwa saa 24 ili mjue mafuta hayo yanatumikaje na mnapata stahiki yenu. Sasa kama mtu anaagiza mafuta na hakuna mtu anayemsimamia inakuwaje? Hiyo ni hatari hata kwa usalama,” alisisitiza.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Taa, Richard Mayongela alisema watatekeleza maagizo yote.Hata hivyo, alishauri kwamba mamlaka hiyo ipokee tozo zao bandarini wakati mafuta yakishushwa kama ilivyo kwa mamlaka zingine za Serikali kama vile TRA.

Alisema hatua hiyo itapunguza gharama nyingine na kurahisisha ukusanyaji wa mapato wanayostahili kupata kutokana na mafuta ya ndege.

Kuhusu fidia kwa wananchi, Mayongela alisema mamlaka yake kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji wameandaa ardhi kwa ajili ya kaya zaidi ya 1,000 zilizoathirika na mradi wa upanuzi wa uwanja na tayari wamelipa Sh3.7 bilioni.

Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba timu yake imekutana na Waziri Lukuvi ambaye amewataka kupeleka nyaraka muhimu kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi suala hilo.

Kuhusu Puma Energy na Tanzanair kumiliki viwanja katikati ya uwanja wa JNIA, Mayongela alisema zilipata ardhi kihalali kwa sababu Serikali haikuwa na utaratibu wa kupima maeneo yake na mengi yalianzishwa kwa matamko.

Alisisitiza kuwa taratibu za kufuta hatimiliki zao zinaendelea ili sehemu yote ya uwanja imilikiwe na Taa.   

Punguza Unene na Kutibu Magonjwa Kwa Kutumia Dawa za Edmark...Bonyeza Hapa

$
0
0
TUNA DAWA AMBAZO NI VIRUTUBISHO NA CHAKULA MBADALA ZIMEHAKIKIWA NA TFDA

Ni uhakika kwa afya yako, kupunguza uzito na Sumu mwilini, Mafuta/Sehemu Mbaya, Kitambi na Nyama Uzembe na kutibu MAGONJWA Mbali mbali yaliyoshindikana

Loose Weight Trainer ni Msaada wako Wasiliana Nasi Kwa WhatsApp 0713 777 470

Upate Suluhisho la Afya yako Bila Madhara pia unaweza kujiunga nami ili ufanye Biashara hii Nicheki


Intagram napatikana kwa jina @looseweight_trainer

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulet

Watu Wasijulikana Wafukua Kaburi za Mume wa Zari Kwa Lengo la Kuchukua Mali

$
0
0
Watu Wasijulikana Wafukua Kaburi za Mume wa Zari Kwa Lengo la Kuchukua Mali
POLISI wilayani Kayunda nchini Uganda inawatafuta watu waliojaribu kulifukua kaburi la marehemu Ivan Ssemwanga lililoko katika kijiji cha Nakaliro usiku wa Jumanne iliyopita ili kuutoa mwili wake. Ssemwanga alizikwa kijijini kwao huko Mei mwaka huu katika mazishi yaliyokuwa na shamrashamra kibao.

Habari zilizopatikana kutoka kwa mmoja wa ndugu zake zimesema waliofanya hivyo walikuwa wamelenga kulichukua fuvu lake. Kaburi lake lilikuwa likilindwa na polisi kuzuia watu wasilifukue na kuchukua fedha ambazo zilitupwa ndani ya kaburi hilo na marafiki zake waliokuwa wanajiita “kundi la matajiri”.

“Nilikuwa nikipita karibu na kaburi majira ya saa saba mchana na niliona shimo kwenye kaburi la Ssemwanga. Nilisogea karibu kuona nini kilikuwa kimetokea,” alisema Ali Wamala, mmoja wa ndugu wanaoishi nyumbani hapo. Hata hivyo, alidai kwamba huenda waganga wa kienyeji walikuwa nyuma ya njama za kuufukua mwili wa Ssemwanga.

Polisi walililinda kaburi hilo kwa zaidi ya mwezi mzima. Naye Naibu Mkuu wa wilaya hiyo, Yahaya Were, amesema upelelezi umeanza na watuhumiwa watakaokamatwa watafikishwa mahakamani. “Hili ni suala la usalama na polisi wameanza uchunguzi dhidi ya watu wanaotaka kuharibu amani ya wafu,” aliongeza Were.

Tangu kuzikwa kwa Ssemwanga, ndugu zake walikodi walinzi kulinda kaburi hilo lakini habari za kuaminika zimesema walishindwa kuwalipa mishahara yao kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa. Inasemekana walinzi hao mwezi wa kwanza walilipwa Sh. 600,000 mbali na kwamba walikuwa wamekubaliana kuwalipa Sh. milioni moja.

Rais Magufuri Kuhamia Dodoma Mwakani, Mama Samia Mwishoni mwa Mwaka Huu

$
0
0
 Rais Magufuri Kuhamia Dodoma Mwakani, Mama Samia Mwishoni mwa Mwaka Huu
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais John Magufuli atahamia Dodoma wakati wowote mwaka 2018 na si 2020 kama ilivyotangazwa awali na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan atahamia Dodoma mwishoni mwa mwaka huu kwa kuwa maandalizi yapo tayari.
Waziri mkuu amesema hayo leo Alhamisi  Desemba 7, 2017 wakati wa uzinduzi wa ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Dodoma ambapo amesema hadi sasa watumishi 2,346 kutoka wizara zote wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wameshahamia Dodoma.
Majaliwa jana Jumatano Desemba 6, 2017 alikagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais eneo la Kilimani mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya mkuu wa mkoa.
Rais John Magufuli alitangaza kuhamia mjini Dodoma  katika sikukuu za mashujaa zilizofanyika kitaifa kwa mara ya kwanza mjini humo mwaka 2016 tangu nchi ipate uhuru.
Uamuzi huo ulipokewa na Waziri Mkuu Majaliwa aliyetangaza ratiba ya uhamiaji wa Serikali katika kipindi cha miaka mitano baada ya yeye mwenyewe kuhamia Septemba Mosi, 2016.
Kwa mujibu wa Majaliwa, ratiba ya Serikali kuhamia Dodoma ilianza Septemba 2016 hadi 2020 wakati nchi itakapofanya uchaguzi mkuu.
Awamu ya kwanza iliyomhusisha yeye mwenyewe, mawaziri wote, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu wote na angalau idara moja au mbili ilianza Septemba hadi Februari 2017.
Awamu ya pili ilikuwa kati ya Machi 2017 hadi Agosti 2017 ambayo iliwahusisha watendaji wa wizara mbalimbali. Awamu ya tatu ilianza Septemba 2017 hadi Februari 2018 na ya nne Machi 2018 na Agosti 2018.
Majaliwa alisema awamu ya tano ambayo ni Septemba 2018 hadi Februari 2020 itakuwa kuhamisha watumishi wa wizara waliobakia jijini Dar es Salaam na ya sita itakuwa ni kati ya Machi 2020 hadi Juni 2020 ambapo Ofisi ya Rais ikiongozwa na Rais, Makamu wa Rais watahamia Dodoma.

Mambosasa Akanusha Kutupilia Mbali Kesi ya Dkt Shika "Kesi Ipo Pale Pale Tukitaka Kumpeleka Mahakamani Umma Utajulishwa"

$
0
0
Mambosasa Akanusha Kutupilia Mbali Kesi ya Dkt Shika "Kesi Ipo Pale Pale Tukitaka Kumpeleka Mahakamani Umma Utajulishwa"
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amekanusha taarifa za kuachana na kesi ya Dkt.Louis Shika, na kusema kwamba kesi yake bado ipo pale pale isipokuwa hawajaipa kipaumbele.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Kamanda Mambosasa amesema jalada la kesi ya Dkt. Shika bado lipo isipokuwa kesi yake haina mashiko kwani hajaleta madhara yoyote kwenye nyumba zilizokuwa zikipigwa mnada.
Kamanda Mambosasa amesema iwapo wataamua kumpandisha mahakamani Dkt. Sika kujibu mashitaka yake umma utajulishwa ili wajue kile kinachoendelea.
"Siyo kweli kama tumeamua kuachana naye kabisa, jalada lake lipo na likikamilika tutaamua nini kinafuata, Shika hakuleta madhara yoyote hivyo kesi yake haina public interest, nyumba ziko salama na hajadhuru mtu, tukiamua kumpandisha mahakamani tutaujulisha umma ili wajue", amesema Kamanda Mambosasa.
Dkt. Louis Shika amefunguliwa jalada la kesi kwa kosa la kuharibu mnada wa nyumba za Lugumi ambao upo kwa amri ya serikali, kwa kusema ananunua nyumba hizo kwa milioni 900 ilhali mfukoni hana pesa kabisa.

Dully Sykes: Nina Jina Kubwa Kuliko Kipato Changu

$
0
0
 Dully Sykes: Nina Jina Kubwa Kuliko Kipato Changu
Msanii wa muziki Bongo, Dully Sykes amefunguka sababu ya kutosimamia wasanii kwa sasa tofauti na hapo awali.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Bombardier’ ameiambia The Base, ITV kutofanya hivyo kunatokana na kipato kuwa kidogo licha ya kuwa msanii mwenye jina kubwa.

“Ilisimama kwa sababu hata kipato hakikuwa kikubwa, mimi siyo msanii labda mwenye kipato kikubwa, nina jina kubwa tofauti na kipato, kwa hiyo siwezi kusema jina langu lina uwezo wa kumchukua msanii no!!, nilitakiwa nipate kipato kwanza ndio nianze kumsimamia msanii wangu” amesema Dully Sykes.

Hata hivyo Dully ameongeza kuwa kwa sasa ana wasanii wawili tayari ambao ndio anataka aanze nao rasmi ingawa anajua anapoanza na msanii lazima kipato kidogo kiwepo kwa ajili ya kufanyia video, production nzuri na kusukuma wimbo (production).

Ukarabati Wamkwamisha Rais wa Zimbabwe Kuingia Ikulu

$
0
0
Ukarabati Wamkwamisha Rais wa Zimbabwe Kuingia Ikulu
Rais wa Zimbabwe,  Emmerson Mnangagwa bado anaendelea kuishi nje ya ikulu akisubiri ukarabati ulioanza ili kurejesha katika hadhi yake.

Mnangagwa aliapishwa hivi karibuni kuwa Rais wa Zimbabwe akihitimisha miaka 37 ya utawala wa Robert Mugabe aliyeongoza taifa hilo tangu uhuru.

Hata hivyo, licha kuapishwa kiongozi huyo ameshindwa kuhamishia makazi yake katika ikulu ya taifa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ikulu hiyo kuhitaji matengenezo makubwa.

Kulingana na msemaji wa rais, George Charamba ikulu ya Zimbabwe ilitelekezwa kwa muda mrefu na Mugabe aliyehamishia makazi yake katika jengo lake ambalo anaendelea kuishi hadi sasa.

Amesema kutokana na kutokaliwa kwa muda mrefu hali ya ikulu hiyo siyo nzuri na hivyo kumfanya Mnangagwa ashindwe kuhamia. Ukarabati unaofanywa ni pamoja kupaka upya rangi jengo nzima na kuweka mifumo mingine inayotakiwa. Pia, imeelezwa kuwepo kwa matengenezo muhimu ya lazima.

Baadhi ya ripoti zinasema Rais Mnangagwa amekuwa akiendesha shughuli zake katika ofisi iliyokuwa ikitumiwa na makamu wa rais wa zamani, Joice Mujuru lakini hakuna maelezo yaliyotolewa sehemu anakoishi.

Wiki iliyopita, rais huyo alitangaza baraza lake jipya la mawaziri huku akiwajumuisha baadhi ya maofisa wa kijeshi. Hata hivyo, siku mbili baadaye aliwapangua baadhi ya mawaziri na kumweka kando waziri aliyekuwa akishughulikia elimu ambaye alilalamikiwa kuwa chanzo cha kushuka kiwango cha elimu nchini humo.

Chuchu Hans Awananga Wauza Nyago Wanaosaka Umaharufu kwa Picha za Utupu

$
0
0
Chuchu Hans Awananga Wauza Nyago Wanaosaka Umaharufu kwa Picha za Utupu
STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans amewananga wauza nyago ambao wameibuka na picha za utupu kwa lengo la kusaka umaarufu na kusema kuwa, kitendo hicho madhara yake ni makubwa siku zijazo kwani wanaweza kukosa waume wa kuwaoa.

Akipiga stori na paparazi wetu, Chuchu ambaye amejituliza na kuzaa na muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’, alisema amekuwa akiona wasanii wengi wanaoibuka sasa kwenye sanaa hususan wanaojihusisha na umodo katika video za muziki, wakisambaza picha zao za utupu kwa lengo la kupata umaarufu bila kujua wanajiharibia.

“Niwatahadharishe tu wasanii wenzangu waachane na haya mambo, wengine hata nguo hawavai kisa kusaka umaarufu. Mwanamke ukiwa hivyo ukija kushtuka baadae utajikuta umeshajiharibia kila kona, hata mwanaume wa maana wa kutulia naye huwezi kupata, mimi nilipata umaarufu kwa filamu ya Roho Sita, sikuvaa nusu utupu,”alisema Chuchu.

Baba Apandishwa Kizimbani kwa Kufanya Mapenzi na Mtoto Wake na Kumsababishia Ujauzito

$
0
0
Baba Apandishwa Kizimbani kwa Kufanya Mapenzi na Mtoto Wake na Kumsababishia Ujauzito
Sadick Japhari, mkazi wa Tabora amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya mapenzi na binti yake mwenye umri wa miaka 16 hatimae kumsababishia ujauzito na kukatisha masomo yake akiwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Lwanzari Tabora mjini.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na kupandishwa kizimbani kwa mara nyingine tena shauri lake namba 49 la mwaka 2017 likiwa upande wa kutolea ushahidi kwa upande wa Jamhuri ambapo ilikuwa ni zamu ya kutoa ushahidi kwa Afisa mtendaji wa mtaa wa shule Kata ya Kaloleni, Christina Kitundu kuwasilisha ushahidi wake ambapo alieleza Mahakama kwamba mtuhumiwa Sadick ambaye alikuwa akiishi na binti yake katika nyumba yenye chumba kimoja na sebule alikuwa akifanya tendo la ndoa wakati binti yake akiwa amelala.

Christina ameiambia mahakama mbele ya mahakama Mkazi Mfawidhi wilaya ya Tabora mjini Jaktoni Lushwela kwamba mtuhumiwa baada ya kubaini tayari amekwisha msababishia binti yake ujauzito aliamua kumasfirisha ikiwa ni mpango wa kuficha ukweli.

Hata hivyo kwa kuwa Afisa Mtendaji wa mtaa ambaye alikuwa na jukumu la kufuatilia watoto wanaoacha masomo kwasababu mbalimbali akuchukua hatua ya kumrejesha Tabora binti huyo na hapo ndipo alipojiridhisha kuwa ni mjamzito na siku chache baadae akajifungua mtoto wa kiume.

Aidha mtoto huyo aliieleza Mahakama kuwa baba yake huyo amekuwa akimbaka mara kadhaa majira ya usiku tangu mwezi Januari 2017 wakati akiwa nyumbani huku akimtia kumdhuru endapo jambo hilo atalisema mbele za watu.

Mtuhumiwa huyo aliukana ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa daktari Disemba 19 mwaka huu, huku mtuhumiwa akiendelea kusota rumande.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

$
0
0

THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.

Mradi wa Ujenzi wa Barabara 6 ya Ubungo Unatarajiwa Kuanza Mwishoni mwa Desemba Mwaka Huu

$
0
0
Mradi wa Ujenzi wa Barabara 6 ya Ubungo Unatarajiwa  Kuanza Mwishoni mwa Desemba Mwaka Huu
Serikali imesema mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Ubungo hadi Kibaha Mkoani Pwani yenye urefu wa kilometa 16 unaotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa katika nchi jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Rasilimali Watu katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji Bi. Visensia Kagombora (katikati) kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ubomoaji wa majengo ya Wizara hiyo yaliyopo katika eneo la Ubungo maji Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale. (Picha na Maelezo)

Akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha inamaliza changamoto ya msongamano na kuziwezesha barabara zote za Jiji la Dar es Salaam kupitika katika majira yote yam waka.

Prof. Mbarawa alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mradi huo utakelezwa kwa ufanisi, viwango na ubora wa hali ya juu na kuwahakikisha wananchi waliopitiwa na mradi huo kuwa barabara hizo zitamaliza kero ya muda mrefu ya msongamano wa magari na hivyo hawana budi kuunga mkono juhudi hizo.

Kwa mujibu wa Prof. Mbarawa alisema tangu mwaka 1932 wakati wa utawala wa Gavana wa Kiingereza, Serikali iliweka sheria ya upanuzi wa barabara katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na kutambua ongezeko la idadi ya watu na msongamano wa magari ambayo ingekuwepo katika miaka ya sasa, hivyo zoezi la ubomoaji wa nyumba hizo ulikuwa haukwepeki.

“Katika kutekeleza mradi huu wa barabara za njia sita, majengo ya Serikali ikiwemo Ofisi za Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Wizara ya Maji pia yameondolewa katika maeneo ya hifadhi ya barabara ambapo mradi huu utapita, hivyo nasi wananchi hatuna budi kuunga mkono juhudi hizi” alisema Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa alisema wakati wa utekelezaji wa mradi wa barabara hizo unaotarajiwa kujengwa katika kiwango cha lami, na hakutokuwa na usumbufu kwa wananchi wanaotumia barabara hizo kwani Serikali imejenga njia mbadala za pembezoni mwa Jiji ili kurahisisha usafiri wa abiria na mizigo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale alisema Ofisi yake imejipanga kikamilifu kutekeleza mradi huo ili kuhakikisha kuwa Jiji la Dar es Salaam linaendelea kuwa kitovu cha uchumi na kiungo cha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi jirani.

Mhandisi Mfugale alisema katika kuondoa changamoto ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam, Ofisi yake imeiweka barabara ya Ubungo-Kimara katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo yao.

Naye Mwananchi wa Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam, Said Kilindo alisema wananchi wa maeneo hayo wamepokea kwa moyo mkunjufu utekelezaji wa mradi huo na kuiomba Serikali kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo ukosefu wa miundombinu ya vyoo katika maeneo mengi ya wafanyabiashara waliokuwepo katika maeneo hayo.

Takukuru Yawakalia Kooni Makada CCM Kuhusu Tuhuma za Rushwa

$
0
0
Takukuru Yawakalia Kooni Makada CCM Kuhusu Tuhuma za Rushwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, imeendelea kuwang’ang’ania viongozi na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendeleza uchunguzi dhidi yao kuhusu tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi uliomalizika Desemba 3,2017.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale leo Alhamisi Desemba 7,2017 ameieleza MCL Digital kuwa taasisi hiyo inaendelea kukusanya ushahidi ili kuwafikisha mahakamani au kuwaachia viongozi na makada hao ambao hata hivyo hakuwa tayari kuwataja.
Ninachoweza kukuthibitishia ni kwamba, tunaendelea na uchunguzi; ukikamilika tutawajulisha na hatua zingine za kisheria zitafuata,” amesema Makale.
Desemba 2,2017 maofisa wa Takukuru wilayani Ukerewe walilikamata na kulipekua gari la Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo alipokuwa katika kampeni za kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika Desemba 3,2017 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Akiwahutubia wana CCM baada ya kutangazwa mshindi kwa kura 555 dhidi ya kura 520 za mshindani wake wa karibu Saidi Mecky Sadiki, Diallo alielezea kitendo cha gari lake kupekuliwa hakikuwa cha kiungwana kwa sababu yeye ni muumini wa vita dhidi ya rushwa ambayo ni adui wa haki kupitia imani na ahadi yake ya mwana CCM.
Siku ya uchaguzi, maofisa wa Takukuru waliwakamata viongozi wanne wa CCM kutoka wilayani Ukerewe kwa tuhuma za kukutwa wakigawana Sh400,000 zikiaminika kuwa za rushwa kutoka kwa mmoja wa wagombea.
Makale alisema waliokamatwa, kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea ni Gabriel Gregory, diwani wa kata ya Bukindo na mwenzake, Nicholaus Munyoro wa kata ya Murutunguru; Steven Mzige, Mwenyekiti wa CCM kata ya Muriti na Katibu wa Uenezi wilayani Ukerewe, Musa Manka.


Takwimu: Watu Bilioni 1.7 Huugua Magojwa ya Kuhara

$
0
0
Watu Bilioni 1.7 Huugua Magojwa ya Kuhara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amesema kuwa Takwimu za shirika la Afya duniani linaonyesha kuwa kila watu wapatao Bilioni 1.7 huugua magonjwa ya kuhara ambapo watu bilioni 1.8 hupoteza maisha ikiwa ni sawa na kupoteza watu wanne kila dakika duniani kote.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo, mjini Dodoma katika uzinduzi wa Kampeni Taifa ya Usafi wa Mazingira awamu ya pili inayobeba jina la ‘Usichukulie poa – nyumba ni choo’

“Takwimu za shirika la Afya duniani linaonyesha kuwa kila watu wapatao Bilioni 1.7 huugua magonjwa ya kuhara, ambapo watu bilioni 1.8 hupoteza maisha, ikiwa ni sawa na kupoteza watu wanne kila dakika duniani kote takiwimu za hapa nchini zinaonyesha watu wapatao 30,000 na baadhi yao hupoteza maisha,” amesema Makamu wa Rais.

“Hali ya usalama wa haki za binadamu haiko vizuri, na tutarekebisha endapo tutazingatia usafi wa mazingira na nimefurahi sana kuwa idai kubwa ya watoto wa shule wapo hapa hawa ndio wanaopaswa kuyasikiliza haya kwasababu wanasema samaki mkunje angali mbichi.”
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images