Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

Mamlaka ya Hali ya Hewa Yatoa Tahadhari Ujio wa Mvua Kubwa

0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Yatoa Tahadhari Ujio wa Mvua Kubwa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kuwapo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA iliyochini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema hayo katika taarifa ya utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo uliotolewa leo Ijumaa.

Mamlaka hiyo imesema katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Shinyanga, Rukwa, Mara, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera na Katavi kutakuwa na hali ya mawingu mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.

Imesema katika mikoa ya Mbeya, Njombe na Songwe kutakuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

Katika mikoa ya Iringa na Morogoro imesema kutakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Taarifa ya hali ya hewa imesema katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara kutakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Kwa mikoa ya Dodoma na Singida kutakuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kuhusu upepo wa Pwani TMA, imesema unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini -Mashariki kwa kasi ya Km 30 kwa saa na kutoka Kusini -Mashariki kwa kasi ya Km 40 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.

Mamlaka imesema kuhusu hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi hadi makubwa huku matazamio siku ya kesho Jumamosi kuwa na ongezeko la mvua maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini.


Tshishimbi Aanza Kufanya Mazoezi

0
0
Tshishimbi Aanza Kufanya Mazoezi
KIUNGO makabaji wa Yanga raia wa Congo Pap Tshishimbi Kabamba, kwa mara nyingine leo ameamsha molari ya wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuanza moja kwa moja mazoezi ya pamoja na wenzake yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Tshishimbi ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu wake aliyoyapata kwenye moja ya mazoezi yao  siku chache kabla ya Ligi Kuu Bara, kusimama kupisha michezo ya kimataifa.

Kanisa la Gwajima Labomolewa Ili Kupisha Barabara

0
0
Kanisa la Gwajima Labomolewa Ili Kupisha Barabara
Kufuatia zoezi la serikali la kupanua na kuboresha miundo mbinu mbalimbali nchini hususan ya barabara katika jiji la Dar es Salaam ambapo imelazimu baadhi ya maeneo kubomolewa ili kupisha zoezi hilo la upanuzi, Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima nalo limekumbwa na kadhia ya kubomolewa.

Kanisa hilo lililoko jirani kabisa na Barabara ya Morogoro ambayo serikali imepanga kuipanua ili kurahisisha usafiri na kupunguza foleni, lilitakiwa kubomolewa kutokana na kuwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara hiyo.

Mchungaji Biyagaza wa Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko chini ya Askofu Gwajima, ameeleza kuwa serikali iliwapatia notisi ya siku 30 ili wabomoe kipande cha jengo la kanisa hilo kilichopo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara.

“Ni kweli tunayo notice ya mwezi mmoja ya kuhakikisha kwamba eneo ambalo ni hifadhi ya barabara tunaliacha. Na hifadhi ya barabara ni mita 90 kuanzia katikati. Bahati nzuri wale waliokuja kuweka alama zao walipofika hapa na wahandisi , mafundi na baadhi ya watu wa kanisani walikuwepo. Basi tukawaambia wapime mita 90 zinapoishia. Kwa hiyo wakapima mita 90 zilipoishia wakaweka alama, wakasema basi nyie mnaweza mkabomoa upande huu na upande huu mkauacha kwa ajili ya hifadhi ya barabara,” alisema Mchungaji Biyagaza.

“Sisi baada ya hapo tukaona tujipange kwa ajili kuachia eneo la barabara ili shughuli nyingine ambazo ni mpango wa maendeleo ya serikali ziweze kuendelea na sisi tuweze kuendelea na eneo letu vizuri. Kwa hivyo kile kipande chote ambacho ni cha barabara na tukaongeza ndani kidogo chote tumekiondoa. Na hili eneo linalobaki tunapaimarisha ili nyumba ya Bwana iweze kufanya kazi yake ya kutoa huduma za kiroho,” aliongeza.

Mchungaji Biyagaza alieleza japokuwa eneo la jengo limepungua, eneo lililobakia linaimarishwa ili kanisa hilo liweze kuendelea kutoa huduma za kiroho kwa waumini wake.

Aidha kufuatia zoezi hilo la upanuzi wa barabara ya Morogoro ambalo linaenda sambamba na ujenzi wa barabara za juu (fly-over) katika makutano ya barabara eneo la Ubungo, umepelekea kubomolewa kwa majengo mbalimbali ikiwemo majengo ya wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na jengo la Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania ambayo yamebomolewa kufuatia agizo la Rais Dkt. John pombe Magufuli.

Hatimaye Jeshi la Polisi Lamshikiria Mwanamke Aliyevalishwa Pete na Mwanamke Mwenziye

0
0
Hatimaye Jeshi la Polisi Lamshikiria Mwanamke Aliyevalishwa Pete na Mwanamke Mwenziye
Sakata la mwanamke aliyemvisha pete ya uchumba mwanamke mwenzake limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwatia mbaroni watu wengine watatu akiwemo aliyevishwa pete.

Sura mpya ya kwanza ni mtuhumiwa Milembe Suleiman (36), anayedaiwa kumvalisha pete mwanamke mwenzake Janeth Shonza, aliyekuwa akishikiliwa na polisi mkoani Geita kuhamishiwa mkoani Mwanza.

Pili, jeshi la polisi pia limefanikiwa kumtia mbaroni mwanamke aliyevishwa pete, Janeth Shonza (25), mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa mafichoni eneo la Puma mkoani Singida.

Amewataja wengine wanaoshikiliwa na kutarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote uchunguzi utakapokamilika kuwa ni Richard Fabian (28), mkazi wa Buzuruga jijini Mwanza aliyepiga na kusambaza mitandaoni picha za wanawake hao wakivishana pete mitandaoni.


Kamanda Msangi amemtaja mwingine anayeshikiliwa kuwa ni Aneth Mkuki (24), mkazi wa Nyasaka jijini Mwanza, mpenzi mwingine wa Janeth aliyemsaidia kutoroka kukwepa kutiwa mbaroni na polisi baada ya video yao kusambazwa mitandaoni.
Chanzo: Mwananchi

JE, Una Upunguvu wa Nguvu za Kiume, Hamu ya Tendo Ndoa au Maumbile Madogo ya Uume?

0
0

JE, UNA UPUNGUVU WA NGUVU ZA KIUME, HAMU YA TENDO LA NDOA AU MAUMBILE MADOGO YA UUME?
SOMA HAPA👇👇.
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa limezidi kuongezeka kwa kasi duniani kote na limekuwa chanzo kikubwa cha ndoa nyingi na mahusiano kukosa uaminifu kutokana na wengi kutoka nje ya ndoa ili kupata mtu atakayemtosheleza na kumfikisha kileleni. Pia udogo wa maumbile ni tatizo kubwa na limekuwa likiwakosesha wanaume wengi uwezo wa kujiamini katika tendo na kusababisha tendo hilo kutokufanyika kwa usahihi. Hili pia huchangia kwa kiasi kikubwa wanawake wengi kwenda nje ya ndoa ( MAHUSIANO) kutafuta mbadala wake.
BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.

Kwa kutumia mimea na matunda bila kemikali 🍇🍍🍓🌿🍉🍒🍎🍑 @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 5.5 hadi 6 @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kuweza kurudia tendo ×3. @150,000/=
BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA KIAFYA NA ZIMETHIBITISHWA
NA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO).
KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
WEB:www.markbeauty.org
Wasiliana nasi Popote
ulipo duniani kwa (+255)
0767447444 na
0714335378
UTAPATA HUDUMA
NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

JE, Wajua Mkusanyiko Usiokuwa Halali Unaweza Kuanzia watu Watatu na Mkashtakiwa?

0
0

JE, wajua mkusanyiko usiokuwa halali unaweza kuanzia watu watatu na mtu yeyote ikithibitika amehusika katika mkusanyiko usio halali atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja?
-
Pia bila kujali kama mkusanyiko ulikuwa halali, iwapo wahusika watajiweka katika hali itayowafanya wengine waogope kutatokea uvunjifu wa Amani au watachochea wengine wavunje Amani utakuwa mkusanyiko usio halali.

Wanawake Wanaoshtakiwa Kwa Kushiriki Mapenzi ya Jinsia Moja Mwanza Wafikishwa Mahamani

0
0

Wanawake wanaoshtakiwa kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja Mwanza na kuvishana pete ya uchumba wamefikishwa Mahakama kuu leo.
_
Wamekana mashtaka yote waliyosomewa ambapo wamerudishwa rumande mpaka December 13 2017

Washtakiwa ni Milembe Suleiman (alievisha pete), Janeth Julius Shonza (alievishwa pete) na wengine ni Athen Mkuki alieshtakiwa kwa kosa kusimamia tukio la kuvalishana pete (MC)

Richard Fabian ameshtakiwa kwa kosa la kusambaza video fupi ya tukio hilo kwenye mitandao.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

0
0
THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.

Diva Afunguka Mapenzi Yalivyomponza Msanii Heri Muziki Hadi Kusababisha Kufeli Masomo

0
0
Diva Afunguka Mapenzi Yalivyomponza Msanii Heri Muziki Hadi Kusababisha Kufeli Masomo
Kumekuwa na tetesi kuwa mapenzi yanamfanya msanii wa Bongo Fleva, Heri Muziki kufanya vibaya kwenye masomo yake ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM). Sahau kuhusu hizo tetesi kwani tayari wote wawili yaani Heri Muziki na mchumba wake ‘Diva The Bawse’ wamezungumzia ukweli uliopo.

Heri Muziki amekataa kuwa kufeli kwake masomo kunatokana na mahusiano ya kimapenzi na mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse, kwa kusema kuwa kufeli kwa mwanafunzi yeyote ni jambo la kawaida na sio kitu cha kushangaa huku akikataa kuwa kufanya kwake vibaya kwenye masomo hakujasababishwa na mapenzi kama watu wengi wanavyodai.

“Unajua kupata sapu chuo ni kitu cha kawaida lakini hiyo stori ya sapu (Supplementary) nyingi ndio naisikia hapa leo but thats not a case siwezi nikasema thats a case… Nilikuwa nafanya muziki nipo shule na ikaongezeka pia na mahisiano vitu ambavyo kila kitu kilikuwa kinahitaji muda… And it was my first time kuwa kwenye mahusiano na mtu maarufu iliniyumbisha kidogo  kwa muda mfupi lakini nikarudi kwenye hali yangu baada ya kuzoea, lakini sio chanzo (cha kufeli).“amesema Heri Muziki kwenye kipindi cha Playlist cha Times FM.

Hata hivyo Bongo5 imemtafuta Diva kuzungumzia ishu hiyo ambapo Diva amekiri kuzisikia taarifa hizo na kusema kuwa yeye sio chanzo kwani huwa anamsaidia kwenye masomo yake kwa hali na mali.

Diva amesema kuwa huwa anamsapoti Heri Muziki kwani anajua umuhimu wa elimu katika maisha na anatamani siku moja mchumba wake nae apate cheti kama yeye.

“I have been very supportive about Heri na elimu yake. When it comes to me nimeenda shule na nimefika level ya Chuo pia so naelewa umuhimu wa elimu katika maisha . If you love someone huwezi muacha aharibikiwe katika shule au kazi anayofanya, utajitahid kumuelewesha hapa na pale na maamuzi huwa ni yake mwisho wa siku.”amesema Diva na kuzungumzia jinsi anavyosapoti muziki wake.

“Sihusiki na Heri kutoa au kutotoa muziki wake kwani ana management yake they know better, all in all i always try to tell him kipi kizuri na kibaya ila he has his own decisions to make in life. Na kingine I’m a fan of his work ni shabiki wake mkubwa sana hivyo would love to see him anafika kilele cha mafanikio. Im very proud of him, He is a smart, loving, caring and one of a kind human being. Hivyo i always wish him well regardless.“amesema Diva.

Heri Muziki jana ameachia ngoma yake mpya inayoitwa ‘Roho Juu’ akiwa ameshirikiana na Otuck William itazame hapa chini kisha dondosha maoni yako.

Mzee wa Miaka 70 Ajinyonga Kisa Mapenzi

0
0
Mzee wa Miaka 70 Ajinyonga Kisa Mapenzi
Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 katika kaunti ya Homa Bay nchini Kenya, amejitoa uhai baada ya kuachwa na mkewe wa pili kwa kumkimbia na kumuachia upweke wa hali ya juu.

Tukio hilo limetokea wiki hii baada ya mke wa mzee huyo Samuel Oloto Onjoga, kutoroka nyumbani katika hali isiyoeleweka na kwenda kuishi katika soko lililo karibu, kitendo kilichomuachia upweke na huzuni.
Chifu wa eneo hilo, Bw Joseph Ndege ameviambia vyombo vya habari kwamba Bw. Onjoga alijitia kitanzi kwa kutumia kamba ya mkonge kwenye mwembe ulioko nyumbani kwake.
"Tulimpata akining’inia kwenye mwembe ulio kando ya nyumba yake, alitumia kamba ya mkonge kujinyonga, mzee huyo alikuwa na upweke baada ya mke wake wa pili kumtoroka na kwenda kukodisha nyumba katika soko lililo karibu baada ya kuzozana,” amesema Chifu huyo.
kwa mujibu wa wanakijiji wenzake mke wa kwanza wa marehemu alifariki miaka mitano iliyopita, na kuoa mke huyo wa pili miaka miwili iliyopita, na kwamba huenda mzee huyo ambaye ni mfanya biashara wa mifugo alipatwa na matatizo ya kimawazo kwa kuishi peke yake nyumbani, ilhali alikuwa pia na matatizo ya kiafya.
Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Homa Bay, Bw Marius Tum, amesema polisi wameanzisha upelelezi kubainisha ukweli kuhusu kifo hicho, huku mwili wake ukihamishwa katika mochwari ya hospitali ya kaunti ndogo ya Rachuonyo kusubiri kufanyiwa upasuaji wa kubainisha chanzo cha kifo.

TFF Yamtangaza Yahaya wa Singida United Kuwa Mchezaji Bora kwa Mwezi Novemba

0
0
TFF Yamtangaza Yahaya  wa Singida United Kuwa Mchezaji Bora kwa Mwezi Novemba
Mchezaji wa timu ya Singida United ya Singida, Mudathir Yahaya amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) kwa mwezi Novemba.

Mudathir ametwaa tuzo hiyo baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Singida United mshambuliaji Danny Usengimana pamoja na beki wa Lipuli FC ya Iringa Asante Kwasi. Mudathir aliingia fainali ya kuwania tuzo hiyo ya mwezi Novemba msimu wa 2017/2018.
Kiungo huyo amepata tuzo hiyo baada ya mapendekezo kutoka kwa makocha na uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii kwenye kikao cha Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Singida United mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Oktoba hadi ya nne.

Singida United ilitoka 0-0 na Yanga, iliifunga Mbeya City mabao 2-1 na pia iliifunga Lipuli bao 1-0, ambapo Mudathir anayecheza nafasi ya kiungo alicheza dakika zote 270 sawa na michezo mitatu na hakuwa na kadi yoyote.
Mafanikio hayo yamemsaidia Mudathir kurudishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na ile ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, ambayo inashiriki michuano ya CECAFA Senior Challenge inayoendelea nchini Kenya.

Shule za Taasisi za Dini Zaonywa na Serikali

0
0
Shule za Taasisi za Dini Zaonywa na Serikali
Serikali imesema shule za taasisi za dini zimepoteza mwelekeo kwa kuwa zimeanza kuzalisha vijana wa vijiweni na baadhi zinatajwa katika suala la ushoga.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Maria Semakafu wakati akifungua mkutano wa umoja wa shule za seminari na binafsi uliofanyika mjini hapa.

Dk Semakafu alikemea tabia ya ushoga kuwa imeanza kuota mizizi kwani vijana wengi wa mitaani wakiulizwa mambo ya ushoga walijifunzia wapi wanazitaja shule za dini.

"Haya siyo maadili mliyokuwa mkifundisha tangu awali, kafundishe maadili ya kidini kama mlivyokuwa awali, tunapata malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na wanafunzi wanaosoma huko kuhusu tabia hizo chafu," amesema Semakafu.

Amesema kwa sasa shule hizo zimekuwa na maadili mabovu akaagiza warekebisha mienendo yao haraka kwani Serikali haitavumilia vitendo hivyo.

Aliyewai Kuwa Mchezaji wa Taifa Timu ya Wanawake Marekani Hope Solo Atangazwa Kugombea Urais

0
0
Aliyewai Kuwa Mchezaji wa Taifa Timu ya Wanawake Marekani Hope Solo Atangazwa Kugombea Urais
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Marekani Hope Solo, mwenye umri wa miaka 36 ametangaza rasmi kuwania nafasi ya Rais wa shirikisho la soka nchini humo (USSF) mwaka 2018.

Hope Solo ameweka wazi mpango wake huo wa kuwania nafasi hiyo ya kuongoza soka nchini Marekani huku akieleza moja ya sababu kubwa ni kuporomoka kwa kiwango cha timu za taifa za soka za wanawake na wanaume.
Rais wa USSF wa sasa Sunil Gulati ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo akitaja sababu kuwa ni kuwajibika baada ya timu ya wanaume kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi. Gulati mwenye umri wa miaka 58 amekuwa rais wa USFF tangu 2006.

 "Nilipokuwa msichana mdogo, kitu pekee nilichotaka ni kucheza soka na kuichezea timu yangu ya taifa katika ngazi zote na nimefanikiwa kufanya hivyo, kinachofanya ni kulitendea haki taifa langu na kurejesha heshima ya soka kwa kuwa rais wa USSF”, amesema Hope Solo.
Hope ameongeza kuwa katika muda wote ambao amekuwa mchezaji na hata baada ya kustaafu amekuwa akijifunza kutoka kwa marais wengine duniani hivyo ana uhakika amepata uzoefu wa kutosha kuweza kuisaidia nchi yake.

Wanawake Waliovishana Pete ya Uchumba Wafikishwa Mahakamani

0
0
Wanawake Waliovishana Pete ya Uchumba Wafikishwa Mahakamani
Wanawake wanaoshtakiwa kwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja Mwanza na kuvishana pete ya uchumba na video yao kusambaa mitandaoni, wamefikishwa Mahakama kuu Mwanza leo.

Washtakiwa wote wanne wamekana mashtaka yote waliyosomewa ambapo wamerudishwa rumande mpaka December 13 2017.

Washtakiwa ni Milembe Suleiman (alievisha pete), Janeth Julius Shonza (alievishwa pete) na wengine ni Athen Mkuki alieshtakiwa kwa kosa kusimamia tukio la kuvalishana pete (MC) huku Richard Fabian ameshtakiwa kwa kosa la kusambaza video fupi ya tukio hilo kwenye mitandao.

Rais Magufuli Awaonya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake ( UWT)

0
0
Rais Magufuli Awaonya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake  UWT
Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amewataka wajumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Wanawake CCM(UWT) kuchagua viongozi ambaye atakuwa anajali wanawake na siyo kujali tumbo lake.

Akizungumza na wajumbe hao leo Ijumaa wakati akifungua mkutano huo Rais Magufuli amesema watakapokuwa wanachagua viongozi leo Ijumaa wasiangalie wamepewa kanga kiasi gani, wala amelipiwa hoteli ya aina gani.

“Nataka mchague kiongozi wa kujali wanawake na sio kujali tumbo lake na awe mtetezi na shida zao wala habagui,” amesema Rais Magufuli.

Amesema anawapenda akina mama hivyo wachague mtu kwa matakwa yao.

“Viongozi wa jumuiya hii wanatakiwa kujua historia na kuipigania jumuiya hii muhimu kwa CCM,”

“Wanawake ndio wapigaji kura waaminifu na ukiahidiwa kura nao jua utashinda.”

Amesema, “Chama tunakata kiwe cha wananchi na sio cha mtu binafsi na kiongozi atakayechaguliwa aendane na mabadiliko ya ndani ya chama.”

Wanafunzi Waliofaulu Darasa la Saba Wapangiwa Shule Wote.

0
0

Baada ya kupata ufaulu mzuri na kuongoza kitaifa katika matokeo ya Darasa la saba mkoa wa Dar es Salaam,leo umetangangaza kuwa hakutakuwepo na wanafunzi wa chaguo la pili badala yake wanafunzi wote wamepangiwa shule moja kwa moja.

Akizungumza katika Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi kidato cha kwanza 2017 wa mkoa huo , Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mbando amesema kuwa katika matokeo ya Darasa la saba mwaka huu wanafunzi wote 58,573 walifanya sawa na asilimia 100% wote wamepangiwa shule na Wataanza kidato cha kwanza January 2018.

Amesema, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za ufaulu mzuri zaidi ni 68, wavulana 35 na wasichana 33.

Wanafunzi walio walio chaguzi wa shule za ufundi ni 74,wavulana 68na wasichana 6,shule za bweni kawaida no 24wavulana 12 na wasichana 12.

Aidha amesema, wanafunzi 1,931wamechaguliwa kujiunga na shule za mkoa zinazo chukua wanafunzi wa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo wavulana ni 850 na wasichana 1, 081.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika shule za serikali za wananchi ni 56,299 ikiwemo wavulana 27,035 na wasichana 29,264 huku wanafunzi wenye uhitaji maalum waliopangiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI ni 101wavulana wakiwa ni 58na wasichana 43.

Amefafanua kuwa, waliochaguliwa Manispaa ya Ilala ni wanafunzi 19,236,kigamboni 2,803,Kinondon 10,885 Temeke15, 323na Ubungo ni 10,326.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo Jumla ya nafasi 4,685 katika shule za pembenizomwajiji zimebaki wazi kwa sababu ya umbali uliopo kati ya shule ya msingi waliposoma wanafunzi na mahali shule zilipo, nafasi zizo baki kwa Manispaa ya Ilala ya Ilala (mjini) ni 887,kigamboni590, Kinondon 1,718 na Ubungo 1,490.


Akizungumzia asilimia, amesema wanafunzi waliojiunga na shule za secondari kwa waliofanya mtihani kwa mkoa ni asilimia 87.82%. katika Manispaa ya Ilala (mjini) ni asilimia 92.48.Ilala (Vijijini) asilimia 84.42.Manispaa ya Kinondoni 93.02%Temeke 81.74%.Kigamboni 91.10% na Ubungo ni 89.01.

Pamoja na hayo Mbando amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi kuwa peleka watoto wao shuleni waliopangiwa tarehe 8 January 2018bila kukosa, na kuwakumbusha wakuu wa shule 147 zinazo pokea wanafunzi kuzingatia waraka no 2 wa 2016 unao husu uendeshaji wa elimu bure bila malipo.

Umoja wa Mataifa (UN) Yathibitisha Kuuwawa kwa Wanajeshi 12 wa Tanzania Congo

0
0

Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa takribani wanajeshi 12 kutoka Tanzania waliokuwa wanalinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa vibaya baada ya kambi yao kuvamiwa na waasi mapema leo.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kupitia mtando wa Twitter imeeleza.

“Taarifa za awali katika eneo la shambulio mjini Kivu Kaskazini zinaonesha kuwa takribani walinda amani 12 kutoka Tanzania wameuawa  na wengine 44 kujeruhiwa vibaya.“amesema Guterres.

Bw. Guterres amesema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni huku akielezwa kusikitishwa na tukio hilo.

“Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.

“Natuma salamu zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa wanajeshi wa kulinda Amani na wanajeshi wa FARDCwaliouawa au kujeruhiwa,” amesema mwakilishi mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo ambaye ndiye pia mkuu wa kikosi cha walinda amani cha MONUSCO.

Duka lingine la Nakumat lafungwa Baada ya Kutimuliwa Kwenye Jengo la Biashara.

0
0

Mzigo wa malimbikizo ya deni la pango leo Ijumaa ulisababisha wamiliki wa duka kubwa la Nakumatt Supermarket Tanzania la mjini Moshi, kutimuliwa kwenye jengo walilokuwa wakiendesha biashara.

Hili ni duka la mwisho kufungwa nchini baada ya maduka mawili kutoka jijini Dar es Salaam na Arusha kufungwa kutokana na wawekezaji hao kushindwa kumudu gharama za kuendeshaji.

Ilikuwa kama sinema asubuhi ya saa 3:00 baada ya kuonekana gari mbili za polisi zikiwa zimeimarisha ulinzi katika duka hilo lililopo barabara ya Kaunda, katikati ya eneo la kibiashara mjini Moshi.

Wateja waliotaka kuingia katika lango kuu kwa ajili ya kwenda kununua biadhaa, walijikuta wakizuiwa na walinzi wa kampuni binafsi ya Intelligence Security, wakiwa hawaelewi nini kimetokea.

Ilipofika saa 4:00 asubuhi, kulionekana harakati za wafanyabiashara waliokuwa wamekodishiwa maduka na Nakumatt Supermarket, wakiondoa bidhaa zao katika vyumba hivyo vya biashara.

Meneja Nakumatt Supermarket Tanzania, Alfrick Milimo alipoulizwa na Mwananchi amekiri kujulishwa kufungwa kwa duka hilo na kwamba ndio alikuwa anaelekea hapo kujua kulikoni.

“Mimi sikuwepo kwa hiyo sijui nini kinaendelea nimepigiwa tu simu kwamba tumezuiwa kufanya biashara. Ndio naelekea huko lakini kwa sasa siwezi kusema lolote maana sijui,” amesema Milimo.

Hata hivyo, Meneja wa Majengo wa Kampuni ya Erncon Holdings Ltd, Thadey Mariki inayomiliki jengo hilo amesema wamelazimika kumuondoa mwekezaji huyo kutokana na malimbikizo ya pango.

“Hatukuwa na namna nyingine bali kuchukua jengo letu. Nakumatt Supermarket wamekuwa wakiendesha biashara hapa lakini hawajatulipa kodi ya pango zaidi ya mwaka mmoja,” amesema.

Mariki amesema hatua hiyo ya Nakumatt Supermarket kutolipa kodi hiyo, kuliifanya kampuni yao iwe na hali ngumu ya uendeshaji ikiwamo kushindwa kulipa mkopo waliokopa kujengea jengo hilo

“Tulikopa benki ili kujenga jengo hili lakini tunashindwa kurejesha kwa wakati na kulipa kodi za Serikali kwa sababu ya malimbikizo hayo ya kodi ya Pango,” amesema bila kutaja kiwango wanachodai.

“Kabla hatujalifunga leo tuliongea na wafanyakazi wote wa Nakumatt na kuwaeleza hali halisi na kwanini tumechukua hatua hii. Tunatafuta mwekezaji atakayetoa huduma bora zaidi.”

Duka la Nakumatt Supermarket ambalo linamilikiwa na kampuni ya Kenya, ndilo lilikuwa duka kubwa na lililokuwa na wateja wengi kulinganisha na maduka mengine.

Mwananchi.

Kesi ya Vigogo Uhujumu Uchumi Yaahirishwa

0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetaja tarehe nyingine ya kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya USD 3.7 milioni ambayo ni sawa na bilioni nane inayowakabili vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa upande wamashitaka, Jackline Nyantori kuieleza mahakama kuwa, upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika na wanajitahidi kukamilisha mapema iwezekanavyo.

Watuhumiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Six telecoms, Hafidhi Shamte, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mwanasheria na Mhadhiri na Mkurugenzi wa hiyo kampuni Dr ,Ringo Tenga, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.

Wakili wa utetezi Masumbuko Lamwai akizungumza mahakamani hapo amedai upelelezi wa kesi wanayokabiliwa nayo washtakiwa siyo mpya, kwani ilishafikishwa mahakamani hapo kama kesi ya uhujumu uchumi Namba 2 ya mwaka 2016.

Wakili wa utetezi amedai, upande wa mashtaka wanazo taarifa zote juu ya shauli hilo sababu mashtaka wanayoshtakiwa nayo yanahusu taarifa za simu ambazo ni electronic na ziko recodedi hivyo hamna ushahidi wowote ambao bado haujakamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 15 mwaka huu, washtakiwa wamerudishwa rumande.

Hatimaye Album ya Diamond 'A Boy From Tandale' Yawekwa Hadharani

0
0

Hakuna ubishi kwa mwaka huu mashabiki wengi wa muziki walikuwa wanasubiria kwa hamu kuipokea album ya ‘A Boy From Tandale’ ya msanii maarufu zaidi Tanzania, Diamond Platnumz ukweli ni kwamba album hiyo haitatoka mwaka huu tena badala yake itatoka mwakani.

Album ya ‘A Boy From Tandale’ itatoka tarehe 12 Januari 2018, na itakuwa na nyimbo 18, ambapo zaidi ya wasanii 13 kutoka Tanzania, Nigeria na Marekani watasikika kwenye album hiyo.



Wasanii hao ni Vanessa Mdee, P-Square, Mr Flavour, Young Killer, Tiwa Savage, Rayvanny, Davido, Jah Prayzer wengine ni Miri Ben-Ari,  Omarion, Rick Ross, Ne-Yo na Morgan Heritage wote kutoka Marekani.

Kupitia mtandao wa iTunes unaweza ku-order sasa hivi kabla haijatoka album hiyo kwa dola 6.99 sawa na tsh 15,666/=. Kumbuka bei hiyo ni kwa wale watakaonunua album hiyo kabla ya kutoka tar 12 Januari, 2017.

Tazama orodha ya nyimbo hizo hapa chini;


Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images