Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live

Ndugai Ametuma Salamu za Rambi Rambi kwa Waziri Ulinzi Kufuatiwa Kifo cha Askari wa JWTZ

$
0
0
Ndugai Ametuma Salamu za Rambi Rambi kwa Waziri Ulinzi Kufuatiwa Kifo cha Askari wa JWTZ
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ametuma salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, kufuatia vifo vya askari 14.

Spika Ndugai amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya askari hao ambao walikuwa wakilinda amani nchini Kongo, pamoja na wengine 44 waliojeruhiwa kufuatia mashambulizi yanayotekelezwa na askari waasi nchini humo.
Kufuatia tukio hilo, Spika Ndugai ametoa pole kwa familia za askari hao waliouawa, na kuwaombea wale waliojeruhiwa kupona haraka na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Nuh Mziwanda Afungukaa Uhusiano Alionao na Shilole "Bado Naawasiliana Nae"

$
0
0
Nuh Mziwanda Afungukaa Uhusiano Alionao na Shilole "Bado Naawasiliana Nae"
Msanii wa muziki Bongo, Nuh Mziwanda amesema bado anawasiliana na aliyekuwa mpenzi wake, Shilole.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Bao la Ushindi’ amesema huwasiliana iwapo kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

“Kwa sababu sisi ni binadamu, kuna kuumwa, kuna misiba kwa hiyo utashindwa kwenda kwenye msiba kwa sababu ninyi mlikuwa mmeachana ni vitu ambavyo havileti maana” Nuh ameiambia Bongo5.

“Mimi sina noma, hata sign ya studio yangu ukisikia nyimbo zangu hizi mpya za sasa hivi Bao la Ushindi, Anameremeta ni sauti yake. Kwa hiyo tupo kikazi kama tulivyofanyaga tour ile ni kazi, ikitokea tunafanya” amesema.

Shilole amefunga ndoa hivi karibuni na mpenzi wake, Uchebe na baada ya hapo Nuh alitoa kauli ambao ilitafsiriwa kama amerusha dogo katika ndoa hiyo.

Utafiti: Kunywa Glasi Moja ya Wine Kila Siku Kuna Manufaa Haya

$
0
0

Utafiti: Kunywa Glasi Moja ya Wine Kila Siku Kuna Manufaa Haya

Utafiti wa siku za hivi karibuni uliofanywa na wanasayansi wa nchini China umeonesha kuwa kunywa glasi moja ya mvinyo yaani ‘wine’ kila siku hupunguza hatari ya kifo cha mapema kwa mara tano.

Wanasayansi hawa pia wameeleza kuwa kukiuka unywaji huu unaoshauriwa kiafya kwa kunywa zaidi hatari ya kifo inaongezeka kwa asilimia 11 ikiwa ni pamoja na kuongeza hatari ya kufa kwa magonjwa ya saratani kwa asilimia 27.

Inaelezwa kwa matunda ya zabibu yanayotumika kutengeneza wine huwa na virutubisho vijulikanavyo kama ‘resveratrol’ ambavyo huongeza na kuboresha afya ya moyo, kusaidia kutoa kinga ya magonjwa ya saratani na kulinda macho dhidi ya uoni hafifu

Kwa mujibu wa Mwandishi Mkuu wa utafiti huo Professor Bo Xi, japokuwa unywaji wa kiasi husaidia kupunguza magonjwa yanayohusiana na moyo unywaji wa kupitilza huweza kusababisha kifo.

Picha: Huyu Ndiye Binadamu Mwenye Tattoo Nyingi Zaidi Duniani

$
0
0
Picha: Huyu Ndiye Binadamu Mwenye Tattoo Nyingi Zaidi Duniani
Mwanaume mmoja raia wa Uingereza Paul Allen anasemekana kuwa ndiye binadamu mwenye tattoo nyingi kuliko mtu yeyote dunia ambazo kwa sasa ziko 812 katika kila sehemu ya mwili wake hadi sehemu za siri na sehemu pekee kwenye mwili wake isiyo na tatuu ni ndani ya macho tu.

Ameeleza kuwa alianza kujichora tattoo hizo akiwa na umri wa miak 49 wiki moja baada ya mama yake mzazi kufariki na tangu hapo hajawahi tena kuacha wala kuridhika na wingi wa tattoo hizo zilizo mwilini mwake.

Ameongezea pia kuwa hadi sasa ametumia zaidi ya Euro 15, 000 (Takriban Tsh 40 milioni) kama gharama ya kuchora tattoo hizo.

Image result for paul allen tattoo
Image result for paul allen tattoo

Mamia Wafurika Dodoma Kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru

$
0
0
Mamia Wafurika Dodoma Kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru
Wakazi wa mji wa Dodoma na viunga vyake mapema leo Jumamosi, Desemba 9, 2017 wamejitokeza kushuhudia maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Taratibu za ukaguzi wa kiusalama, zilifanya misururu mirefu baada ya kutumika geti moja kuingilia ndani ya Uwanja wa Jamuhuri.

Hali hiyo ilifanya misururu mrefu kuanzia geti la kuingilia uwanjani kufika katika barabara inayoelekea Nkuhungu.

Mabasi makubwa yanayotoka katika wilaya za jirani yalionekana yakishusha watu tangu saa 11.00 alfajiri kuwahi foleni.

Watu walianza kuingia uwanjani huku vikundi mbalimbali vya burudani vikitumbuiza.

Saa 2:00 asubuhi, gwaride maalumu lililojumuisha vikosi vya ulinzi na usalama viliingia uwanjani.

Viongozi mbalimbali walianza kuwasili uwanjani kuanzia saa 1:00 asubuhi wakiwemo mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume, mke wa Rais ya Kwanza wa Tanzania Mama Maria Nyerere na aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais, Mohammed Gharib Bilal.

Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema ni baadhi ya viongozi wa kisiasa walioonekana uwanjani hapo.

Viongozi wengine waliofika asubuhi uwanjani hapo ni Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, mke wa Rais, Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, majaji wakuu wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Spika wa Bunge Job Ndugai, mawaziri na wabunge.

Tayari Uwanja wa Jamhuri umejaa na wananchi wamezuiwa kuingia katika uwanja huo na milango yote imefungwa.

Jeshi la Israel Limefyatua Makombora Eneo la Gaza, Palestina

$
0
0
Jeshi la Israel Limefyatua Makombora Eneo la Gaza, Palestina
Jeshi la Israel limefyatua makombora kadhaa kuelekea eneo la Gaza, Palestina ikilenga wapiganaji wa kundi la Hamas.

Jeshi hilo la Israel limeeleza kuwa katika mashambulizi hayo lilipiga maeneo ya viwanda vya uzalishaji wa silaha na maghala ya silaha ya Hamas, mapema leo. Hata hivyo, kwa mujibu wa Independent, makombora hayo yalileta madhara katika maeneo ya makazi yakigusa pia watoto.

Hamaki kati ya Israel na Palestina iliongezeka wiki iliyopita baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Israel imekuwa ikidai Jerusalem ni mji wake mkuu wakati Wapalestina wakiendelea kudai upande wa Mashariki mwa mji huo kuwa eneo lao muhimu lililotwaliwa na Israel katika vita ya mwaka 1967.

Jana, kiongozi wa Hamas, Fathi Hammad alisema kuwa Taifa lolote litakalohamishia ubalozi wake Jerusalem litakuwa ‘adui wa Wapalestina’.

Tanzania kupitia Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Maige imeweka wazi msimamo wake kuwa haitahamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem.

“Hatuna ulazima wa kuhamisha ubalozi wetu. Unapaswa kufahamu kuwa ubalozi wa Tanzania nchini Israel utabaki kuwa Tel Aviv na hakuna mpango wa kuuhamishia Jerusalem ingawa kumekuwa na jitihada za kutushawishi kufanya hivyo,” Waziri Maige anakaririwa na The Citizen.

Uamuzi wa Trump umepokelewa kwa hisia tofauti na mataifa mengi huku ikielezwa wazi kuwa utakwamisha mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.

Mzungu Ajivunia kwa Alikiba Asema Ndie Chanzo cha Kuimba Kiswahili na Kupata Mafanikio Makubwa

$
0
0
Ali Kipa Amhamasisha Mzungu Kuimba Kiswahili na Kumpa Mafanikio Makubwa
Msanii wa muziki kutoka Kenya mwenye asili ya Israel Gilard Millo, amesema msanii wa bongo fleva Alikiba ndiye aliyemu-'insipire' kuimba Kiswahili, kitu ambacho kimempa mafanikio makubwa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, Gilard ambaye hivi sasa ametua bongo, amesema wimbo wa 'Cinderela' wa Alikiba ndio ulimfanya azidi kupenda kuimba kwa lugha ya Kiswahili, baada ya kuona mashabiki wakimshangilia kwa nguvu alipoimba wimbo huo jukwaani. 
"Cinderela ndio wimbo ulionifanya mimi nianze kuimba Kiswahili, nilikuwa nauimba na band live, na ndio wimbo wa kwanza wa Kiswahili nilioanza kuimba, sasa nikiimba watu wakawa wanashangilia huyu ni mzungu lakini anaimba Kiswahili, nikapenda nikaanza kuimba na zingine kwa Kiswahili, na mpaka leo naimba nyimbo zangu kwa Kiswahili", amesema Gilard.
Gilard ana kazi mbali mbali ambazo zimemfanya achukue tuzo za kimataifa, ambazo zimeimbwa kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo Unajua, Nairobi Yangu, Mapenzi, Sema milele na nyinginezo.

Breaking News:Babu Seya Nguza Viking na Mtoto Wake Waachiwa Huru Kwa Msamaha wa Rais

$
0
0
Katika Maazimisho ya Miaka 56 ya Uhuru Tanzania Leo Rais Magufuli ametoa Msamaha Kwa Wafungwa Babu Seya na Mwanawe Ambao Walikuwa Wamefungwa Kifungo cha Maisha kwa kosa la kulawiti......

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Tupo Mbagala Rangi Tatu

Mwili wa Joel Bendera Waagwa Dar RC Mkonda Aongoza Mamia ya Waombelezaji Kuuaga Mwili Huo

$
0
0
Mwili wa Joel Bendera Waagwa Dar RC Mkonda Aongoza Mamia ya Waombelezaji Kuuaga Mwili Huo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaongoza mamia ya watu waliojitokeza  kumuaga aliyewahi kuwa kocha wa Taifa Stars, Joel Bendera katika Viwanja  vya Hospitali ya Lugalo jijini Dar  ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho Korogwe, Tanga.


Bendera  aliyefariki Jumatano wiki hii  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliwahi kushika nyadhifa tofauti serikali ikiwemo ili ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mbunge wa  Korogwe  Mashariki na Mjini na  baadaye kuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro na Manyara.

Yametimia....... Htimaye Babu Seya na Mwanaye Kusheherekea X- Mass Wakiwa Uraiani

$
0
0
Yametimia....... Htimaye Babu Seya na Mwanaye Kusheherekea Uhuru wa Tanganyika Wakiwa Uraiani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasamehe familia ya mwanamuziki Pappi Nguza Viking ambao walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha.
 
Rais Magufuli ametangaza msamaha huo leo mjini Dodoma kwenye sherehe za Uhuru wa miaka 56 ya Tanganyika.
“Nimeamua kusamehe wafungwa 8157, ambapo baada ya msamaha huu, 1828 watatoka leo, 6329 wamepunguziwa muda wa kukaa gerezani”, amesema Rais Magufuli.
Baada ya kutangaza hivyo rais Magufuli akaongeza kuwa katika msahama huu nimeamua kuisamehe familia ya Nguza Viking na kuanzia sasa wawe huru kulingana na taratibu za kimagereza.

Wafungwa 8,157 Wapata Msamaha wa Rais Magufuli... 1828 Watatolewa Kutolewa Leo.

$
0
0
Wafungwa 8,157 Wapata Msamaha wa Rais Magufuli... 1828 Watatolewa Kutolewa Leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 8,157 huku wafungwa 1828 watatolewa leo.

Akizungumza leo katika maadhimisho ya Miaka ya 56 ya Uhuru, Rais Magufuli huku akisema kuwa watu 6,329 watapunguziwa muda wa kukaa jela.

“Ninatoa msamaha kwa wafungwa 8,157 na wafungwa 1,828 watatoka leo na 6,329 watapunguziwa muda wa kukaa jela,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alieleza kuwa amesamehe watu 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Boss wa Ndemla Akwama Kumalizana na Simba

$
0
0
Boss wa Ndemla Akwama Kumalizana na Simba
BOSI wa Klabu ya AFC Eskelistuna ameshindwa kuwasili nchini wiki hii kumalizana na Simba kuhusu usajili wa timu hiyo, Said Ndemla baada ya mmoja kati anayehusika na ujio wake kupata msiba.

Kiongozi huyo alitarajiwa kuwasili nchini wiki hii kwa ajili ya suala la mchezaji huyo pamoja na masuala mengine ya kisoka lakini imeshindikana.

Ndemla alifanikiwa kufuzu majaribio mwezi uliopita katika klabu hiyo ya Sweden ambayo ilikuwa
 inashiriki ligi kuu na sasa imeshuka daraja.

Akizungumza na Championi Jumamosi, meneja wa Ndemla, Jamali Kisongo alisema kiongozi huyo ameshindwa kuwasili kutokana na matatizo hayo aliyoyapata mwenzao.

“Yule kiongozi alitakiwa kuwasili nchini wiki hii lakini imeshindikana kwa sababu mmoja kati ya watu anayehusika na ujio wake amepata msiba, hivyo sijafahamu baada ya hapo ratiba zake zitakuwaje.

“Lakini kama kutakuwa na lolote tutaweka wazi. Kwa upande wa mchezaji licha ya timu kushuka daraja lakini dili liko palepale, atajiunga nayo tu,” alisema Kisongo.

Wasanii Wapamba Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru Mkoani Dodoma

$
0
0
Wasanii Wapamba Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru Mkoani Dodoma

Baadhi ya Wasanii wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara,yanayoendelea kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.

Mtoto wa Babu Seya Afunguka Baada ya Familia Yake Kuachiw Huru " Mungu Mwaminifu "

$
0
0
Mtoto wa Babu Seya Afunguka Baada ya Familia Yake Kuachiw Huru " Mungu Mwaminifu "

 Mtoto wa Mwanamuziki wa dansi Nguza Viking ‘Babu  Seya’ Michael Nguza amesema anamshukuru Mungu baada ya Rais John Magufuli kutangaza familia yao ipo huru kuanzia leo Jumamosi.

 Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo, leo Jumamosi, Desemba 2017 akiwa mjini Dodoma wakati wa akihutubia  maadhimisho miaka 56 ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika.

Michael Nguza ambaye hivi sasa anajiita Nabii Michael baada ya kutoka jela  amesema : “Namshukuru Mungu, Mungu ni mwaminifu. Siwezi kuongea mengi kwa sasa, nitatoa taarifa baadaye.

“Tunatarajia kufanya kikao cha familia ili kujadili suala hili na baadaye tutaulezea umma baada ya majadiliano haya familia naomba kuweni wavumilivu,” amesema Nabii Michael.



Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRDC ), Wametoa Tamko na Kulaani Kupotea Gwanda

$
0
0
Image result for mwandishi wa mwananchi aliyepotea


Wadau wa habari kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC ), wametoa tamko na kulaani kupotea kwa mwandishi wa kujitegemea wa Mwananchi, Azory Gwanda.

Tamko hilo limetolewa baada ya wadau hao wa habari likiwamo Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na  THRDC kuunda kamati ndogo ya uchunguzi.

Gwanda alipotea tangu Novemba 21 mwaka huu katika mji wa Kibiti, mkoani Pwani alikokuwa akiishi na kufanyia kazi.

Akitoa tamko hilo leo Jumamosi, Katibu Mkuu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema tukio hilo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa habari.

Aliwaomba viongozi wa siasa na Bunge kuona haja ya kulijadili suala la utekaji na kupotea kwa Watanzania ili kuja na maazimio.

"Tunaviomba vyombo vya habari viendelee kuuhabarisha uma juu ya kupotea kwa ndugu yetu Azory Gwanda,” amesema.

Kajubi ameipongeza kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kwa kuweza kufuatilia kupotea kwa mwandishi huyo na kuvitaka vyombo vingine vya habari kuwa na moyo huo bila kujali aina ya mikataba ya waandishi wao.

Kwa upande wake mratibu wa Taifa wa THRDC, Onesmo Ole Ngurumwa alisema wanasikitishwa na ongezeko la watu kutoweka na kwenda pasipojulikana na hakuna chochote kinachofanyika kuzuia suala hilo linalozidi kuota mizizi kwenye jamii.

"Makundi ya watetezi, waandishi, wanasiasa na wasanii wamesharipotiwa kupotea na kutoweka, kati yao wapo waliookotwa wameumizwa vibaya, wapo ambao hadi leo hawajulikani walipo na wengine kurudi wakiwa na hofu kubwa," amesema.



Ole Ngurumwa amesema wanaliomba jeshi la polisi kutoa ulinzi ili kuweza kuandamana kwa amani hadi ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP )  kupeleka hoja na kilio hicho.

Aliongeza kuwa ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kuhakikisha Azory anapatikana.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai aliwashukuru wadau wa habari, vyombo vya habari na watetezi wa haki za binadamu kwa kusaidia jitihada za kumtafuta Azory.

Nanai amesema inasikitisha kuona kwamba wakati Tanzania ikisherehekea miaka 56 ya Uhuru bado hakuna uhuru wa habari.

Amesema hadi sasa hakuna fununu yoyote waliyoipata juu ya tukio hilo la kutoweka kwa Azory na kuomba nguvu zaidi katika kumtafuta.


Maneno ya Bushoke Baada ya Kuachiwa Kwa Babu Seya na Mwanaye "Sioni wa kum-replace Magufuli Ametimiza Ndoto Zangu"

$
0
0
Maneno ya Bushoke Baada ya Kuachiwa Kwa Babu Seya na Mwanaye "Sioni wa kum-replace Magufuli Ametimiza Ndoto Zangu"

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni rafiki kipenzi wa Papii Kocha mfalme mtoto wa Babu Seya, Bushoke Rutta, ameelezea furaha yake baada ya kusikia rafiki yake huyo ameachiwa kwa msamaha wa Rais, na kwamba ametimiza ndoto zao.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Bushoke amesema furaha aliyonayo hailezeki kwa alichokifanya Rais na haoni wa kuchukua nafasi yake, kwani alichokifanya ni kitendo cha huruma na upendo wa hali ya juu, kwa kutimiza tumaini ambalo walikuwa nalo rafiki zake hao vipenzi.
Bushoke ameendeleea kusema kwamba hivi karibuni rafiki yake huyo alimsikia akisema ana imani Rais wa sasa atawaonea huruma na kuwaacha huru, hata isingekuwa leo basi ingekuwa siku yoyote lakini waliamini hawatafikwa na umauti wakiwa jela.
Akiendelea kusimulia furaha yake Bushoke amesema aliposikia Rais anatangaza kumsamehe Babu Seya na familia yake, mwili ulimsisimka huku asiamini nachokisikia.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

$
0
0
THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.

Offer ya X-Mass..Pendeza Sasa Kwa Punguzu la Bei.....

$
0
0

🎁OFFER YA X-MASS.🎁
PENDEZA SASA KWA PUNGUZO KUBWA LA BEI.
KATIKA KUSHEREHEKEA MSIMU WA SIKUKUU @natural2162 TUNA PUNGUZO LA 20% KWA BIDHAA ZETU ZOTE, IKIWA NI SHUKRANI KWA KUTUUNGA MKONO.
BIDHAA ZETU ZOTE ZIMETENGENEZWA KWA MIMEA NA MATUNDA HAZINA KEMIKALI WALA MADHARA.
KWA WANAUME TUNATIBU👇👇
☆Kukosa hamu ya tendo.
☆Kuwahi kufika kileleni na kushindwa kurudia tendo.
☆Maumbile madogo ya uume.
☆Kuchoka sana wakati wa tendo na uume kusinyaa nk.
@natural2162 tumeandaa tiba bora kabisa kama ifuatavyo:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @220,000/=
2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @130,000/=
3VigRX CREAM_ Inaongeza uume inch 6.5 hadi 8 (wiki 2-3) @170,000/=
4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @140,000/=
5. MAXMAN 2-Hii ni vidonge vinavyoongeza nguvu za kiume pamoja na uume @220,000/=
6.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @140,000/=
PIA KWA WANAWAKE WANAOPENDA KUWA NA MUONEKANO MZURI ZIPO ZA👇👇👇
1.Kuongeza hips, makalio na mapaja @180,000/=
2.Kushepu mguu (CHUPA YA BIA) @130,000/=
3.Kuwa mweupe bila sugu kwa:-
(a)mafuta @130,000/=
(b) Vidonge @150,000
4.Kurefusha nywele na kutokukatika ovyo @130,000/=
5.Kuongeza hips, makalio na mapaja kwa vidonge (YODI PILLS ORIGINAL) @200,000/=
6Kupunguza au kuongeza maziwa kuyasimamisha @130,000/=
7.Kubana uke na kuondoa uchafu ukeni @120,000/=
8.Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
NB:Hakikisha unapata risiti yenye muhuri na garantii ili kukuhakikishia ubora na usalama wa bidhaa za NATURAL BEAUTY CO

Wasiliana nasi Popote
ulipo duniani kwa (+255)
0659618585 na
0759029968
UTAPATA HUDUMA.
👉🏻OUR WEBSITE:- www.naturalworldbeauty.og
👉🏻INSTAGRAM PAGE:-
@natural2162
@natural2162
@natural2162

Kituo cha Haki za Binadamu Champongeza Magufuli Kutoa Msamaha kwa Wafungwa

$
0
0
Kituo cha Haki za Binadamu Champongeza Magufuli Kutoa Msamaha kwa Wafungwa
Kitua cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwemo familia ya msanii Nguza Viking.

Pamoja na pongezi hizo LHRC, imesema itaendelea kumuomba Rais Magufuli abadili baadhi ya sheria ikiwemo kuondoa sheria inayotoa ruhusa ya adhabu ya kifo..
“Tunampongeza Mh. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 61 kati ya wafungwa 522 waliohukumiwa kunyongwa”. LHRC wameandika kupitia ukurasa wao wa Twiiter.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

LHRC imeongeza, “Tunamsihi Mhe. Rais kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta sheria zinazoruhusu uwepo wa adhabu ya kifo na kuifanya hukumu ya kifungo cha maisha kuwa adhabu mbadala”.
Katika msamaha huo Rais pia amemsamehe mzee Mganga Matonya ambaye ana miaka 85 akiwa amekaa gerezani miaka 37 pamoja na miaka saba aliyokaa mahabusu wakati akisubiri hukumu yake hivyo kufanya afikishe miaka 44 gerezani.
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live


Latest Images