Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Kutana na Mtabibu wa Nyota Duniani Maalim Fadhil Rashid Kutoka Comoro Kwa sasa Yupo Tanzania

0
0
KUTANA NA MTABIBIBU WANYOTA DUNIANIKOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE ANADAWA ZA KI COMRO DAWAZAKE HABAHATISHI MUONE HARAKA AKUSAIDIE TEZI NAUVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABI MALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI ZAMAJINI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YAKUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NAUMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWAHARAKA KUZUIYA CHUMAULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI KARIBUNI WOTE TIBA NIKWADINI ZOTE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO DUNIANI

CALLING +255719362806/

WHATSAPP CALLING +255785786436

Kesi ya Wema Sepetu Kuendelea Tena January 10 Mwakani

0
0
Kesi ya Wema Sepetu Kuendelea Tena January 10 Mwakani
Kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili, msanii wa filamu Wema Sepetu ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini haikuweza kusikilizwa kwa sababu wakili wake hakuwepo.

Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ambapo Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alieleza kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa mashahidi wawili.

Wakili wa utetezi, Devotha Kiangakwa upande wake alieleza kuwa anamuwakilisha Wakili Peter Kibatala ambaye anamtetea Wema na wenzake ambaye amekwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenye kesi namba 85 ya mwaka 2016, hivyo anaomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi January 10, 2018.

Kijana Maarufu Ambaye Mpanda Majengo Marefu Afariki Baada ya Kuanguka China

0
0
Kijana Maarufu Ambaye Mpanda Majengo Marefu Afariki Baada ya Kuanguka China
Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amefariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.
Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.
Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.

Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.

Kihama cha Wasanii Wavaa Nguo za Utupu Chaja JPM Aagiza Washughurikiwe

0
0
Kihama cha Wasanii Wavaa Nguo za Utupu Chaja JPM Aagiza Washughurikiwe
Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amekerwa na mamlaka zinazohusika na maadili kutochukua hatua dhidi ya wasanii wanaoimba majukwani wakiwa na mavazi ya utupu.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne wakati akufungua mkutano mkuu wa tisa wa jumuiya ya wazazi CCM utakaofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.

Rais Magufuli amehoji vyombo vya habari, wasimamizi wa maadili, wizara na taasisi zinazodhibiti zimeshindwa kushughulikia maadili ya vijana.

Msingi wa kauli hiyo ilikuwa ni kumtaka kiongozi wa jumuiya hiyo atakayepatikana kuhakikisha anakwenda kusimamamia maadili ya vijana na Taifa kwa ujumla.

Rais Magufuli aliwataka wazazi hao kusimamia maadili ya Watanzania.

"Hii ni jumuiya ya wazazi lakini maadili yameanza kupotea na jumuiya ipo kwa ajili ya kukemea, mimi nimekuwa shabiki mzuri wa muziki, wanaovaa utupu ni wanawake, wanaume wanacheza wakiwa wamevaa, sana sana wataachia kifua wazi tu ili waonekane 'six pack', lakini wanawake, walio wengi wanaachia viungo vyao,”

"Jumuiya imefika wakati wa kukemea, tunawafundisha nini, je akicheza bila kuvua nguo hata furahisha wimbo? Sasa ni jukumu lenu jumuiya ya wazazi, kwa kumtanguliza Mungu kwa sababu hata Adam alipotenda dhambi alijikuta yupo uchi, lakini kwenye muziki hawajioni wako uchi na wanacheza hadharani.”

Rais Magufuli amesema wakati umefika bila kujali itikadi za vyama kuungana katika ujenzi na ulinzi wa maadiili ya Watanzania.

Shilole Afunguka Siri ya Kufunga Ndoa Kimyakimya

0
0
Shilole Afunguka Siri ya Kufunga Ndoa Kimyakimya
Mwanamuziki Zuwena Mohammed maarufu Shilole amesema aliamua kufunga ndoa kimyakimya baada ya kushauriwa na viongozi wa dini.

Pia, ameeleza alivyopata upinzani kutoka kwa dada yake ambaye hakutaka aolewe na mwanamume aliyemchagua.

Ndoa ya Shilole ilizua gumzo baada ya kufanyika katika hali ya kushtukiza licha ya kuwa aliahidi angefunga kwa uwazi na kufuatiwa na sherehe kubwa.

Shilole akizungumza na mwandishi wa mtandao wa Millard Ayo, amesema aliamua kufunga ndoa kimyakimya na mpenzi wake Uchebe baada ya kuambiwa ndoa haitangazwi kwa sababu inaweza kukaribisha uadui.

“Niliambiwa si kila mtu anapenda kusikia jambo jema kama hilo, wengine wanaweza kukufanyia husuda usifanikishe kwa hiyo nikaamua kuwasikiliza lakini haimaanishi kuwa sitafanya sherehe,” amesema.

Akizungumzia familia yake kumzuia kufunga ndoa amesema, “Unajua hayo ni mambo ya kifamilia, nina watoto wawili halafu ananichagulia mwanamume wa kuolewa naye?”

Shilole amesema anatarajia kufanya sherehe kati ya Desemba 25 na Desemba 27,2017.

“Sherehe ya kukata na shoka nitaitangaza siku mbili hizi. Itakuwa ya aina yake kwa kuwa watu watakula, kunywa na vingine kubeba. Itakuwa ya kihistoria,” amesema.

Oscar Pistorius Ajeruhiwa Akipigana Gerezani

0
0
Oscar Pistorius Ajeruhiwa Akipigana Gerezani
Aliyekuwa mwanariadha mlemavu raia wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amejeruhiwa kwenye mzozo wa gerezani, chini ya wiki mbili baada ya kifungo cha kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kuongezwa zaidi ya mara mbili.
Inadaiwa kuwa mwariadha huyo alikuwa kwenye vita vya kupigania simu kwa mujibu wa msemaji wa idara ya mahakama.
Pistorius ambaye amefungwa miaka 13 na miezi mitano aliripotiwa kupata jeraha.
.
Inaripotiwa kuwa alikuwa kwenye majibizano na mfungwa mwingine kuhusu kuitumia simu ya umma katika kituo ambapo wafungwa hao wote wamefungwa.

Idara ya mahakama imeanzisha uchunguzi kujua ukweli na kuchukua hatua zinazohitajika.

Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia, baada ya kudai kuwa alimpinga risasi Bi Steenkanp akidhani kuwa ni jambazi mapema siku ya wapendanao mwaka 2013.
Lakini mahakama ya rufaa ilibatilishwa uamuzi huo mwaka 2015 na kumpata na hatia ya kuua.
Pistorius alikatwa miguu yake yote miwili akiwa mtoto.

Ujumbe wa RC Makonda kwa Wema Sepetu "Karibu Nyumbani "

0
0
Ujumbe wa RC Makonda kwa Wema Sepetu "Karibu Nyumbani"
Baada ya Wema Sepetu kutangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuanzia mwishoni mwa weekend iliyopita ameonekana akiwa katika picha tofauti tofauti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda.

Sasa leo RC Makonda ameandika ujumbe kwa kwenye moja ya picha walizopiga pamoja. Kupitia ukurasa wake wa Instagram RC Makonda ameeleza kuwa Wema amechagua fungu jema katika maamuzi aliyofanya.

Serikali ni sawa na Mzazi ambaye siku zote huwaza mema kwa watu wake. Umechagua fungu jema karibu nyumbani tujenge Nchi imara na wala siyo upinzani imara kwani Nchi kwanza vyama baadae

Kabla ya RC Makonda, Wema naye aliandika; “I never knew you well until I hated you, & now that I met you, I thank God to have Found you… Every Dark Cloud possesses a Silver Lining”.

February 24 mwaka huu Wema alijiunga na Chadema akitokea CCM na December Mosi akatangaza kurejea CCM.

Dkt Shika Afunguka Ukweli Kuhusu Babu Seya

0
0
Dkt Shika Afunguka Ukweli Kuhusu Babu Seya
Dr. Luis Shika amesema hamjui mwanamuziki Babu Seya na Papii Kocha ambao wametoka jela kwa msamaha wa Rais wa  Jamhuri ya  Muungano  wa  Tanzania John Pombe  Magufuli katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika.

Dr. Shika amesema wakati Babu Seya anaingia nchini Tanzania  yeye alikuwa nje ya nchi hivyo hajawahi kumuona lakini anafahamu nyimbo zake ambazo aliwahi  kuimba.
''Simfahamu Babu  Seya, wakati anaingia nchini  tayari nilishaondoka nchini muda mrefu, lakini nafahamu nyimbo zake ile aliyoimba baba na mwana tunaimba na kucheza ndio haswa naifahamu vizuri'', amesema.

Pia Dr. Shika amempongeza Rais Magufuli kwa kuwatoa wafungwa mbali mbalimbali  na kutumia vizuri fursa ya uongozi kama mkuu wa nchi. ''Nampongeza Rais Magufuli kwa tukio hili la kuwatoa wafungwa  na kuwapa uhuru wakaanze maisha yao upya'', ameongeza.

Nguza Viking maarufu kama ''Babu  Seya'' na Johnson Nguza ''Papii Kocha'' walipatikana na hatia ya kubaka na kunajisi watoto na walihukumiwa kwenda jela maisha tangu mwaka 2004 kabla ya kupata msamaha mwaka huu wakiwa wamedumu gerezani kwa miaka 13.
 

Dudu Baya Amchana Mr Nice "Mr Nice Asiwe Kama Kunguru"

0
0
Dudu Baya Amchana Mr Nice "Mr Nice Asiwe Kama Kunguru"
Rapa mkongwe ndani ya tasnia ya bongo fleva, Dudubaya amemtaka msanii mkongwe mwenzake Mr. Nice asiwe kama Kunguru ambaye alikatwa mabawa na watu wengine na kutafuta sababu kuonekana Young D ndiye aliyemkata mabawa hayo.

Dudubaya amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV baada ya kusikia kuwa Mr Nice amemlalamikia Young D kuchukua baadhi ya mistari yake ya wimbo wake wa zamani.
Dudubaya amesema kitendo alichofanya Young D kuchukua mistari ya wimbo wake na wimbo wa Mr Nice ni kizuri kwani ameboresha zaidi na kufanya kazi kubwa hivyo uwepo wa kazi hiyo unamfanya hata Mr Nice na yeye kusikika kwenye muziki.
Aidha Dudubaya alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa Mr Nice ameonyesha kulalamika kwa sababu anatafuta sababu ya kutaka kulipwa na Young D kwani amekwama kiuchumi ndiyo maana amelitolea macho jambo hilo.

Huyu Hapa Bingwa wa Magonjwa Sugu Kama Vile Pumu, Vidonda vya Tumbo, Busha, Kisukari na Nguvu za Kiume

0
0

BABU MADUHU NI BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU YANAYOSUMBUA KAMA VILE PUMU, VIDONDA VYA TUMBO, BUSHA, NGUVU ZA KIUME, KISUKARI, MIVUTO YOTE, KUSAFISHA NYOTA, KURUDISHA MALI, NK.

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni NYASOSE MIX, Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,Hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa    dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

MHESHA POWER Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ITINYA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SUPER POWER,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

BABU MADUHU ANAPATIKANA MAGOMENI MOROCCO HOTEL/KANISANI
SIMU NO 0652 102 152/0755 684 297/0788 330 105.

HUDUMA HII UNAWEZA KUIPATA/KULETEWA MAHALI POPOTE NCHINI

 

Nani Yupo Sahihi, Afande Sele au Mrisho Mpoto

0
0

Maneno Makali ya AFANDE SELE kutoka Instagram Kwa MRISHO MPOTO na Majibu ya MPOTO kwa AFANDE SELE...

Afande Sele King - Rafiki yangu mkubwa mjomba mpoto kama ni kweli wewe ndio ulikua kinara ktk kusimamia utayarishaji wa wimbo maalumu wa kuhamasisha uzalendo kwa taifa halafu ukashawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii wazawa ndani ya wimbo huo na badala yake ukampa nafasi rafiki yetu christian bella kushiriki ktk wimbo huo unaowahusu watanzania wkt ukijua wazi kuwa bella pamoja na ukweli ni rafiki yetu sana lkn bado yeye sio mtz bali ni mcongoman....ktk hili mjomba umetukosea sana watanzania wenzako na kwa hakika kama ingekua kitendo chako hicho umekifanya kwa nchi zilizoshiba uzalendo na zisizovaa joho la unafki mjomba ulistahili kukatwa nywele zako na kupigwa risasi angalau tano kichwani kwa uchache tena hadharani kwani ulichofanya ni usaliti kwa nchi yako na ni aina flani ya uhaini...

Majibu

Mrisho Mpoto Akijibu - Kaka yangu @afandeseleking Bado narudia kusema kwamba heshima nnayokupa inatoka Mbali sana kwenye chumba cha nne cha moyo Wangu... Sihitaji kupoteza wino Mwingi kukukumbusha tofauti iliyopo kati ya UZALENDO, UZAWA na URAIA kwasababu nina uhakika unazifahamu vyema isipokuwa huenda leo haujaamkia ule ubavu sahihi na ule wa ukarimu wako ulionao siku zote, mpaka ukakataa uwepo wangu hapa Duniani Kwa kunichagulia adhabu ya kupigwa risasi tano tena za kichwa... kwakua hukuniuliza hili jambo kabla Itoshe kusema hunitaki tena...hivyo basi kabla sijapigwa hizo risasi tano nitakachofanya ni kukupa maelezo machache yatakayokufanya uipate picha ya UZALENDO.. Hivi unajua kama John Okello alipigania uhuru wa Zanzibar!? Majeshi yetu yamepigania uhuru wa msumbiji na hata Chegu sio mcuba na alipigania uhuru wa Cuba na Congo pia.. Na je unajua kama kuna wazawa wanaoangamiza maslahi ya nchi na kuna wazalendo wasiobagua!? Kaka, Afrika ni moja na waafrika wote ni ndugu zetu ( umajumui Afrika, tena ukichimba huko sana kwa hapa nchini utakuna na Prof Shivji) .. na ndio maana hata mwenge wa uhuru uliwekwa juu ya mlima kilimanjaro ili kumulikia nchi nyingine.. Kumbuka hiyo mitizamo ya KIUZAWA Mwalimu aliita mitizamo membamba.. kwa maana ya kwamba ipo kwa ajili ya Kuiangamiza afrika

Na mwisho ningependa kukuuliza--->Je umezisikia shangwe za wazalendo na wazawa leo hapa dodoma baada ya kusikia Babu Seya na familia yake wamepewa msamaha wa rais!!? Wewe ni RASTA kaka.. kumbuka siku zote CHUKI HUMUUMIZA ANAYEIHIFADHI.. #AfrikaUnite ✊


Nani yupo sahihi kati ya hawa mafahari wawili? 
Je kuwa Mzalendo ni lazima uwe mzawa wa nchi husika?

Utafiti..Wapenzi Wanaovaa Nguo za Kufanana Huwasaidia Kutunza Kumbukumbu

0
0

MAHUSIANO: Utafiti wa Jarida la HuffPost umebainisha kuwa wapenzi wanaopendelea kuvaa nguo zinazofanana(Sare) huwasaidia kutunza kumbukumbu pale mmoja anapokuwa mbali.
-
Jarida hilo linasema asilimia 58 ya vijana waliohojiwa wamethibitisha kukumbuka zaidi siku walizovaa sare wakiwa na Wenza wao.
-
Je, upi ni mtazamo wako katika hili, kuna ukweli wowote?

Kijana Aliyejizolea Umaarufu Kwa Kujipiga Picha Akiwa Kwenye Majengo Marefu Afariki Dunia

0
0

CHINA: Pichani ni Wu Yongning aliyejizolea umaarufu kwa kuonekana kwenye Video fupi akiwa juu ya majengo marefu na kupiga picha kwa mtindo wa 'Selfie'.
-
Bwana Wu Yongning alipotea kwenye mitandao kwa muda na sasa imethibitika kuwa alifariki baada ya kuanguka kutoka katika jengo la ghorofa la 62
-
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo ambao ungemuwezesha kushinda pesa nyingi

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

0
0

MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Jeshi la Tanzania Kuendelea Kulinda Amani DR Congo Licha ya Kupoteza Wanajeshi 14

0
0

Jeshi la Tanzania kuendelea kulinda amani DR Congo licha ya kupoteza Wanajeshi 14
-
Hatua hii itaimarisha uhusiano wa kidiplomasia pamoja na shughuli za kibiashara
-
Wiki iliyopita wanajeshi 14 wa Tanzania na 5 wa DR Congo waliuwawa na wengine zaidi ya 44 walijeruliwa katika shaumbulio linalotajwa kuwa baya tangu mapigano dhidi ya waasi yaanze katika ukanda wa mashariki mwa nchi hiyo hasa eneo la Kivu ambalo kwa sehemu kubwa linazungukwa na makundi ya waasi.
-
Kwa mujibu wa Umoja wa Taifa (UN) unasema shambulio hilo lilitokea Desemba 7 mwaka huu katika kambi ya jeshi ya ulinzi wa amani (MONUSCO)
-
Waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) walivamia kambi ndogo iliyopo eneo la daraja la mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamanga mpakani mwa Uganda Kaskazini Mashariki ya Wilaya ya Beni, jimbo la Kivu Kaskazini
-
Siku chache baada ya shambulio hilo serikali ya Tanzania kupitia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema shambulio hilo limeleta madhara makubwa lakini kikosi chao kilichopo huko kina uwezo wa kutekeleza majukumu kwa uweledi na umahiri stahiki.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

0
0
THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.

Pele wa Brazil Amewahi Kuitembelea Yanga ?

0
0
Pele wa Brazil Amewahi Kuitembelea Yanga ?
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga wamethibitisha kuwa waliwahi kupata nafasi ya kutembelewa na klabu ya Santos ya Brazil pamoja na mfalme wa soka duniani Pele, japo ziara hiyo haikukamilika.

Kupitia ukurasa wa klabu wa Instagram wameweka picha inayoonyesha nguo aina ya Kanga yenye maneno yanayoashiria kuwa ilikuwa ni sehemu ya maadalizi ya kuipokea Santos pamoja na Pele. “Pele na Santos, Wageni wa Yanga”, imeandikwa Kanga hiyo.
Maelezo ya picha hiyo yameeleza kuwa ziara hiyo ilikuwa mwaka 1972 ambapo klabu kongwe ya Santos yenye mafanikio katika soka la Brazil na duniani ikiwa na historia ya kuwatoa nyota wakali duniani kama Pele, Robinho na Neymar Jr ilitakiwa kufika nchini lakini ilishindikana.

“Hii ilikuwa 1972, Baadae ziara ya timu hiyo kutoka Brazil ikaahirishwa na @santosfc kuishia Nairobi kisha kurejea kwao. Unajua ni kwasababu gani? Usikose toleo la pili la Yanga Magazine”, ni maneno yaliyoandikwa chini ya picha hiyo.
Huenda undani wa safari hiyo ukajumuishwa kwenye mwendelezo wa Jarida la klabu hiyo (Yanga Magazine) katika toleo lijalo kama ilivyoelezwa na labda tunaweza kushuhudia safari hiyo ikapangwa upya na klabu hiyo ikaja nchini.

Askofu Aliyetaka Katiba Mpya Ipewe Kipaumbele Ahojiwa na Uhamiaji Kuhusu Uraia Wake

0
0
Askofu Aliyetaka Katiba Mpya Ipewe Kipaumbele Ahojiwa na Uhamiaji Kuhusu Uraia Wake
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Rulenge, Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61), amehojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na uraia wake. Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Askofu Niwemugizi alisema mara ya kwanza alihojiwa Novemba 28 mwaka huu na mara ya pili alihojiwa Desemba 4, mwaka huu.
“Mara ya kwanza niliitwa na kufika ofisi za uhamiaji Ngara, Novemba 28 na mara ya pili niliitwa Desemba 4.
“Niliombwa kibali kinachoniruhusu kuwa nchini, nikashangaa, nikasema mimi ni Mtanzania, nikaambiwa nilete document (nyaraka).
“Nilipeleka hati ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura na cheti cha kuzaliwa, wakasema wataniita tena.
“Baada ya kuitwa mara ya pili, nilipewa fomu ya kujaza ambayo bado naendelea kuijaza hadi sasa.
“Waliniita tena wakasema bado wanataka kujiridhisha ndio maana wanataka nijaze fomu, ninaendelea kuifanyia kazi mpaka nitakapokuwa nimeikamilisha yote,” alisema Askofu Niwemugizi ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC).
Mahojiano kati yake na Mwandishi wa Mtanzania yalikuwa hivi.
Swali: Je, ulizaliwa wapi?
Jibu: Nilizaliwa katika Kitongoji cha Kayanza, Kijiji cha Kabukome, Kata ya Nyarubungo, Wilaya ya Biharamulo.
Swali: Ulizaliwa tarehe ngapi?
Jibu: Nilizaliwa Juni 3, mwaka 1956.
Swali: Ulibatizwa wapi?
Jibu: Nilibatizwa katika Parokia ya Katoke, Biharamulo.
Swali: Elimu ya Msingi na Sekondari ulisoma wapi?
Jibu: Nilisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo na Shule ya Sekondari Nyakato Bukoba (O-level).
Baada ya kumaliza ‘O-level’ niliingia Seminari Kuu ya Ntungamo Bukoba halafu nikatoka hapo nikaenda Kipalapala Tabora.
Swali: Wazazi wako walizaliwa wapi?
Jibu: Walizaliwa sehemu mbalimbali, mama alizaliwa Lusahunga na baba alizaliwa katika Tarafa ya Nyarubungo, Kijiji cha Kabukome Kitongoji cha Kayanza.
Swali: Katika maisha yako yote je, ulishawahi kuhisiwa kuhusu uraia wako?
Jibu: Sijawahi kuulizwa, muda wote nimetumia passport (hati ya kusafiria) ya Tanzania na hakuna aliyewahi kuniuliza suala la uraia.
Swali: Je, unafikiri kwanini hili linajitokeza sasa?
Jibu: Baada ya hivi karibuni kutoa ushauri, kwamba ni vizuri mchakato wa Katiba ukarejewa, watu wali-react, sasa naweza kupata picha nini kimesababisha nianze kuhojiwa.
Swali: Je, Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC) wana taarifa kwamba umeitwa uhamiaji?
Jibu: Sijawataarifu kwa sababu suala hili lilionekana bado liko chini chini, lakini nafikiri nitatafuta namna ya kuwafahamisha juu ya jambo hili.
Swali: Je, mbali na kuwa Askofu, uliwahi kushika nafasi gani katika Kanisa Katoliki?
Jibu: Niliwahi kuwa Rais wa TEC, kuanzia mwaka 2000 hadi 2006 na baadaye nikawa Mkamu wa Rais kuanzia mwaka 2012 hadi 2015.
Swali: Je, una hofu yoyote juu ya usalama wako?
Jibu: Mimi sina hofu na usalama kwa sababu ninajua kufa ni mara moja. Kwa hiyo, ninabaki kivulini, ninazungumza tu ninavyowajibika kama askofu.
UHAMIAJI
MTANZANIA lilizungumza na Msemaji Mkuu Idara ya Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda, ambaye alikiri askofu huyo kuhojiwa.
“Ni kweli anahojiwa na ofisi yetu ya Wilaya ya Ngara, ni suala tu la tuhuma si kwamba ni kweli au la, hivyo itakapothibitika basi itajulikana,” alisema Mtanda.

Mbunge Chadema Amkumbuka Jakaya Kikwete

0
0

Mbunge Chadema Amkumbuka Jakaya Kikwete
Baada ya kuwepo kwa taarifa za kuhojiwa kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenga, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61) na Idara ya Uhamiaji kuhusu uraia wake, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amesema utawala wa Rais Kikwete,

makanisa yalisimama na kukosoa.
Heche amesema kwamba utawala wa Kikwete Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati ya serikali na waka hakuwahi kushuhudia viongozi wa dini wakihojiwa na kususitiza kwamba watu wasimame imara kupinga kuporwa kwa uhuru
"Kanisa lilisimama imara kukosoa mambo kadhaa wakati wa utawala wa Kikwete, sikuona kiongozi anahojiwa uraia wake naamini ingekuwa kipindi hiki kanisa lingefutwa wangesema sio kanisa la Kitanzania, tusimame imara kupinga uhuru wetu kuporwa, hakuna alie salama" Heche .
Taarifa zinadai kwamba Askofu Niwemugizi alihojiwa mara 2 na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na Uraia wake kati ya mwezi Novemba na Disemba
Mwishoni mwa mwezi Septemba , Askofu Niwemugizi alisema kuwa  imefika wakati nchi inahitaji kuwa na dira nzuri ambayo pia italetwa na Katiba Mpya na kusisitiza kwamba

Zaidi ya Wanafunzi 9000 Wakosa Nafasi za Kuingia Kidato cha Kwanza Mwaka 2018

0
0
Zaidi ya Wanafunzi 9000 Wakosa Nafasi za Kuingia Kidato cha Kwanza Mwaka 2018
Zaidi ya wanafunzi 9000 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mkoani Katavi wamekosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za halmashauri tatu za mkoa huo.

Akitangaza matokeo ya mtihani huo katika kikao maalumu cha uchaguzi wa wanafunzi Afisa Elimu mkoa wa Katavi Ernest Hinju amesema jumla watahiniwa 7,190 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa.
Aidha watahiniwa 162 hawakuweza kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali hali iliyopelekea wadau wa elimu kujadili changamoto za kushuka kwa elimu, kwani kulinganisha na mwaka uliopita mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya 9 kitaifa kutoka nafasi ya 2 mwaka uliopita
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi Bwana Gideon Marandu amezitaka halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi waliokosa nafasi wanapata nafasi ifikapo Februari mwaka 2018

Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images