Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Daaah! Inasikitisha. Soma Hii Story Huyu Dada Aliyekutana na Mwigizaji Shamsa Ford

$
0
0
Kupitia ukurasa wa mtandao mmoja wa kijamii leo hii, mwanadada mwigizaji Shamsa Ford amepost ujumbe huu kwa wale wadada wote wanopenda kutumia mikorogo kama njia ya kuwafanya waonekane warembo Zaidi. Hichi ndicho alichokisema.

“Leo nilikutana na mdada ambaye alikuwa ananiomba sana kukutana na mm.nilipokutana naye alikuwa amevaa hijabu kubwa sana yaani yalibaki macho tu.nikajua mfungo wa ramadhani.nilishangazwa sana baada tu ya kuketi akaanza kulia.baada ya kunitolea hijabu yake nilitamani kukimbia.Wasichana wenzangu na kina mama tujiamini na kile Mungu alichotuumba nacho..huyu dada alikuwa ananunua hii mikorogo inayotengenezwa na watu majumbani.matokeo yake amejichubua mpaka kabakisha ngozi ya mwisho.Na sababu kubwa iliyomfanya anitafute ni kunisihi kutochezea rangi yangu na kwasihi wanawake wanaojichubua waache coz madhara yake ni makubwa.na sasa hivi ana canser ya ngozi.Nilitamani kumpiga picture but alikataa.TUWENI MAkINI Dada zangu”

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Huu ni Ujumbe wa Kajala Kwenda Kwa Mtoto Wake Kwenye Siku ya Kuzaliwa Kwa Binti Yake Huyo.

$
0
0
Miaka 12 iliyopita sikuwahi kujua kama itafikia siku nitajisikia hiki ninachofeel siku ya leo.. nimepitia mambo mengi sana na wewe.. nimepata shida nyingi mno lakini sikukuacha wala kukutupa.. kwenye jua ama mvua, iwe usiku ama mchana katika mitihani yote niliyopitia nilikuwa na wewe tu mwanangu.. ulikuwa kama pochi yangu.. bila kujua kesho utakuwa NANI!! nilikupenda tangu siku ya kwanza nakuona.. nilikuthamini na kuahidi nafsi yangu kuwa nitakufa na wewe katika hali yoyote ile bila kujua wewe una hisia gani juu yangu... wala sikujua kama unaweza kuja kuwa faraja kwangu.. Paula!!! Mtoto wangu wa utotoni.. mtoto ambae nna historia kubwa na wewe..

LEO napenda kumshukuru sana MUNGU kwa kunipatia wewe.. sababu uwepo wako wa miaka 12 kwenye Dunia hii umenipa majibu yote ya maswali niliyokuwa najiuliza... Umekuwa faraja kubwa sana kwenye maisha yangu.. Pamoja na umri wako kuwa mdogo umeweza kusimama na mimi kwenye hali zote.. nimeshuhudia lililoniumiza likikuumiza pia.. umenifanya nione thamani yangu.. umenipa thamani kubwa sana kwenye maisha yako.. katika safari hii umenihakikishia kuwa nina mtu mmoja ambae hata Dunia nzima initenge na kunizomea.. YEYE ATABAKI KUWA NA MIMI!!! Tena kwa moyo mmoja na mapenzi... na mtu mwenyewe si mwingine yoyote.. ila ni WEWE mwanangu.. nakupenda sana Paula!! Na nakuombea MUNGU akukuze kwenye imani na akupe kila la kheri katika dunia hii.. nilikupenda jana ukiwa mikononi mwangu, ninakupenda leo ukiwa binti na naahidi kukupenda milele katika maisha yangu ukiwa kwenye hali yoyote ile.. ulikuwa wa kwangu na utaendelea kuwa wa kwangu mpaka mwisho wa maisha yangu.. HAPPY BIRTHDAY my daughter!!!! NAKUPENDA SANA!

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Linah Aelezea Wivu, Majivuno na Majungu Yanavyowatafuna Wasanii wa Kike Hapa Bongo

$
0
0
Idadi ndogo ya wasanii wa kike Tanzania waliofanikiwa kimuziki na mbio za baadhi yao kuishia sakafuni husababishwa na mengi, lakini kumbe wao binafsi ni sehemu kubwa ya sababu za kuwapunguza kwenye mkondo mkubwa wa muziki.

Akiongea na Tovuti ya Times Fm, msanii wa kike, Linah ambaye ni mmoja kati ya wasanii watano wa kike Tanzania wanaopiga hatua kubwa kimuziki na kuleta ushindani ameelezea wadudu wanaoshambulia maendeleo ya muziki ya wasanii wa kike Tanzania.

“Mimi nachoweza kusema ni wivu. Yaani sisi wasichana tuna wivu. Nakumbuka kuna wasichana kama wawili nilishawahi kuwafuata nikawaambia bana kuna wimbo huu hapa tufanyeje. Mtu aah sijui nini na nini…maneno pembeni ‘ah kwa sababu anaona mimi sasa hivi niko hivi na hivi’, yaani mambo kama hayo wasichana tunayo. Yaani hutaki mwenzio afanikiwe, unataka wewe tu ndio ukae na uwe wewe tu. Na ndio maana wasichana kwenye muziki tuko wachache kuliko wanaume. Yaani tuna ile tabia ya kwanini.” Ameeleza.

Amesema kwa upande wake alivyopata nafasi ya kwenda kufanya kazi Afrika Kusini alifikiria jinsi ya kuwavuta na wasichana wengine na kusafisha njia kama anavyofanya Diamond. Lakini badala yake wengi wameanza kumpiga majungu kuhusu safari yake.

“Kwa sababu kuna maneno nimeshayasikia, yaani hivi nakwambia nimerudi nasikia ‘oooh ana mabwana, sijui kapelekwa. Which is not true kwa sababu mimi niko kazini. Hata kama napelekwa niko kazini na kuna faida naipata. Wewe ambaye uko hapo na unafanya muziki umefanya kitu gani? Nimesaini mikataba mikubwa na kampuni kubwa na sio mchezo. Lakini mara ‘oh katika hayo makampuni aah mabwana’, unajua watoto wa kike. Kwa hiyo vitu kama hivyo vinaturudisha nyuma huwezi ukafanikiwa hata siku moja. Lakini ukivaa miwani ya bati ukasonga mbele basi unafanikiwa.”   Amefunguka Asterina  Sanga aka Linah.

Ameeleza kuwa wasanii wengi wa kike wa Tanzania hujivuna na ndio sababu ya kutokuwepo collabo za wasanii wakubwa wa kike.

“Angalia wenzetu Shakira na Rihanna wametoa wimbo unafanya vizuri, wanaonekana. Shakira na Beyonce walifanya wimbo. Sijui akina Kelly Rowland na wengine wengi. Hapa ulishasikia collabo ngapi za wasanii wakubwa wa kike kwa sisi tuliopo? Zaidi ya mimi na Khadija ambayo imetoka juzi

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Moto Wateketeza Nyumba Mwananyamala Hospitali

$
0
0
Moto mkubwa umeteketeza nyumba moja yenye vyemba 12 na mali zote zilizokuwa ndani yake katika eneo la hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Kamishina Msaidizi wa Polisi Camellius Wambura moto huo uliotokea majira ya saa tano na nusu asubuhi na kuteketeza nyumba ya zee Abdalah na kwamba hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu.

100.5 Times Fm imefika katika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda ambao walilalamikia kitengo cha zima moto na uokoaji kwa kushindwa kufika katika eneo la tukio kwa wakati.

Mashuhuda hao pia waliiomba seriakali kuhakikisha kunakuwa na huduma ya zima moto na uokoaji maeneo ya karibu.

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Baby Madaha: Wasanii Wengi wa Bongo ni Washirikina Wanalogana Sana

$
0
0
Staa  wa  kike  anayefanya  vizuri  katika  tasnia  ya  muziki  na  filamu  nchini, Baby  Joseph  ‘Baby Madaha’  amewatolea  uvivu  wasanii  wenzake  kwa  kuifumua  tasnia  hiyo  kuwa  asilimia  kubwa  ya  wasanii  ni  washirikina  na  wanalogana….

Msanii huyo  amewashutumu  baadhi  ya  wasanii  Bongo  kuwa  hawawezi  kufanya  jambo  lolote  muhimu  bila  kufanya  ushirikina  na  wengine  hawapendi   kuona  wenzao  wakitoka  kimaisha…..

Madaha  amefikia  hatua  ya  kufumua  ushu  hiyo  kwa  madai  kuwa  hata  kufilisika  kwake  ghafla  kumetokea  baada  ya  aliyekuwa  mpenzi  wake  raia   wa  Kenya  Joe  Kairuki  kupunguza  nguvu  ya  kumsaidia  kisanii  na  kwamba  ilitokana  na  rafiki  zake  kumpiga  juju….

“Wasanii  wenzangu  wameniloga.Walikuwa  wanaona  donge  sana  Joe  alipokuwa  akinisaidia.Kiukweli  wameniporomosha  kabisa.Nilienda  kwa  mtaalamu  akanithibitishia  hili.Hata  hivyo  nimepata  mfadhili  mwingine.Siwezi  kumtaja  wasije  wakanipiga  kipapai  tena,”  alifunguka  staa  huyo  wa  wimbo  wa  Summer Tyme.

Alisema  ushirikina  umeifanya  tasnia  ya  sanaa  kudumaa  kwa  kiasi  kikubwa  na  kwamba  imani  hiyo  imesababishwa  na  wsanii  wasio  na  elimu….

“Wasanii  wachawi  wapo  wengi  tu.Yaani  unamuona  msichana  mzuri  au  mvulana  mtanashati  msanii  kumbe  anakesha  kwa  waganga.

“Wengi  wanasafiri  sana  kwenda  mikoani  kuloga  wenzao.Sanaa  imejaa  uchuro  mtupu. Kama  si  kuelemewa  na  ushirikina  basi  tungekuwa  mbali  sana.

“Ushirikina  umesababisha  pia  fitina, majungu  na  visilani  miongoni  mwa  wasanii. Hatupendani  kwa  sabab  ya  mioyo  ya  kichawi,” Alisema  Baby  Madaha

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Shilole Awashangaa Wanao Kaa na Kuchonga Kuwa Mpenzi Wake Nuhu ni Serengeti Boy

$
0
0
Mwanamuziki na Staa wa Bongo Movies Mrembo Shilole Amehabarisha na Kusema kuwa Anawashangaa Sana watu wanao kaa Kutwa Kuchonga na Kusema Eti Mpenzi wake Nuhu Mziwandani ni Mdogo kwake kiumri , Shilole Amesema yeye na Nuhu Wanalingana Umri so kwake yeye ni sawa tu , Alizidi Kusema kuwa Kwanza Mapenzi huwa hayajali Umri Mnao kaa Kuchonga Mtachonga Sana.....

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Rachel:Sitoki Kimapenzi na TID na Wala Hajanifundisha Kutumia Madawa ya Kulevya (Unga)

$
0
0
Mwanamuziki Rachel Ambaye ni zao la THT na Aliyetamba na Single ya Kizunguzungu amejitokeza hadharani na kukanusha tetesi ambazo zilikuwa headlines week mbili zilizopita kuwa anatoka kimapenzi na TID na Pia Anatumia Madawa ya Kulevya baada ya TID kumfundisha..

Rachel Amekanusha uvumi huo na kusema "Jamini mimi sina mahusiano ya kimapenzi na TID kabisa maneno nayasikia tu mtaani na kwenye blogs ila si Mpenzi wangu na wala hajanifundisha kutumia madawa ya kulevya ,hizo stori sijui zinatoka wapi , mimi TID ninampango wa Kufanya nae kazi za music tu na si vingine"

Mkomo Kuchonga chongo Midomo Rachel kashasema Hapo Juu

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Wema Sepetu Atoa ya Moyoni na Kusema 'Nimemsamehe Penny'

$
0
0
STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu
amesema baada ya kutokuwa na maelewano
kwa muda mrefu na mtangazaji maarufu
Bongo, Peniel Mungilwa ‘ Penny’ , sasa
ameamua kumsamehe rasmi kwa heshima ya
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani .
Staa wa sinema za Kibongo , Wema Sepetu .
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Wema
alisema : “Kwa moyo mweupe , nasema
nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye
popote nitasalimiana naye kama kawaida .
Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti
wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu
ipokelewe vyema kwa Mungu

Kwa upande wa Penny alifunguka : “Siwezi
kusema nitamchukia Wema ila nimekubali
matokeo , sina tatizo naye tena ingawa najua
hatuwezi kuwa marafiki tena kama zamani,
lakini yaliyopita yameshapita .”
Wema na Penny walikuwa na bifu kwa muda
mrefu, chanzo kikiwa Penny kuingilia
uhusiano wa Wema kwa Mwanabongo Fleva ,
Nasibu Abdul ‘ Diamond ’

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Flora Lymo (Mbuta Nanga) yuko Mahututi Hospitalini, Apimwa Kansa ya Kichwa

$
0
0
Yule dada wa UK kwa jina florah lymo au mbutananga yuko hospitalini kwa matibabu baada ya kuhisi kizunguzungu na kuanguka ghafla. Taarifa zilizohakikiwa ni kwamba alifanyiwa kipimo cha Kansa ya ubongo. Majibu ya kipimo hiki ni Siri ya mhusika. Nimejisikia vibaya sana na kumuonea huruma. Seriously anahitaji Maombi Kama mwenyewe alivyoomba Huko IG .....tumuombee majibu yawe negative manake si ishu ya mchezo.

Updates :
Flora kwa sasa anaendelea vizuri na Baada ya Kupimwa Kansa haya ndo Majibu yake:


Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Le Mutuz: Thank You Jamiiforums I am A Big Star and Big Celebrity Cause of You Leo Nitaichangia Tsh. 200,000

$
0
0
Jamani heshima mbele sana, naomba kuwashukuru sana Jamiiforums I mean JF nimetoka nayo mbali sana na imenifikisha mbali sana na wala sio siri leo ninafahamika kila kona ya Tanzania kwa sababu ya kuanzia hapa JF, nilianza kwa majina ya bandia nikawa maarufu sana and then nikaamua kujitoa mwenyewe kama nilivyo na kuendelea kuwa maarufu, umaaurufu ambao kwa sasa unanilipa sana big time hapa mjini, sasa Mungu anasema ni muhimu sana kukumbuka ulipotokea ndio maana ndugu zangu nawapa shukrani zangu na leo nitaichangia JF Shillingi 200,000.00 za bongo.

- Again najua kwamba wengi wetu hapa tuna itikadi tofauti na sometimes tunakwaruzana sana, lakini najua kwamba wote tuna nia njema sana ya kulisimamia taifa letu, again naomba kuwaomba ,msamaha wale wote ambao nimewahi kuwakwaza kwa maneno yangu na nawasamehe wale wote walionikwaza ingawa mwendo ni ule ule tu, lakini again naomba kutoa heshima yangu kwa JF kwamba bila you JF nisingekuwa Le Mutuz making big bucks from online business najua wengi hivi karibuni wamekuwa wakiniombea kuwa Bilionea nawaahidi kwamba in 2 years tu nitakuwa kwa sababu nipo kwenye the right tracks.

MUNGU AIJALIE JF THIS IS MY HOME NA THIS IS MY BASE ALWAYS!! AND LUV YAH ALL!1

Le Mutuz Big Show
------------------------

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Mr Nice Afunguka Kuhusu Utajiri Wake wa Bilioni 1.5 na Jinsi Ulivyotoweka Ghafla

$
0
0
Mr.Nice akifunguka kuhusu utajiri wake ulivyotoweka ghafla!. Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview.

Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu. Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.

“Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema Mr.Nice.

“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana” 

Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.


Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda.

Ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake.

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Jokate Mwegelo Vs Vanessa Mdee Unamkubali Yupi Zaidi?

$
0
0
They are both smart,classic,intelligent,tale nted,educated and they both have natural beauty... Frankly speaking those chicks are cute but there is something ambacho mmoja kamzidi mwenzie je wewe unadhani ni kipi??? Na Unamkubali yupi zaidi?

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Steve Nyerere Alia na Watu Wanaomzushia Kuwa Yeye ni Shoga. Hichi Ndicho Alichosema

$
0
0
Mwenyekiti wa bongo movie Unity, Steve Nyerere amechukizwa na watu wanaotumia mitandao vibaya na kwa kumzushia kuwa ni shoga.

Steve Nyerere kupitia akaunti yake ya facebook ameandika:

Napenda kuchukua fursa hii kuongea machache na kama mtaboa mtu naomba samahani najua binadamu tumezaliwa tofauti sana kuna wale wanaogopa zambi na kunawale wanopenda zambi mimi daima nasema izo ni changamoto tuuu ok nimepata taarifa umu umu kwenye mitandao yetu ya kijamiii hususani huuu kwamba kuna binti anaitwa zainab ananichafua na kuniandika mambo ambayo ayana tija kwangu. Nazani ata kwake kwamba mimi shoga anauhakika hahahahaha nimecheka sana kupata izi taarifa nataka kuwapa taarifa ndugu zangu kuna msemo unasema mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe na mkanya mara moja aache mara moja kwani naimani anapoteza muda tu habari hizo si zakweli kabisa ila namtakia laheli kwahili jambo analonitendea mimi nasema namwachia mola akumbuke nafamily mke na watoto mama dada zangu kiukweli najisikia vibaya sana mi nasema asante”.

Baada ya kuandika kauli hiyo, Steve Nyerere ameuambia mtandao wa bongo5 kuwa kuna watu wameamua kumchufua baada ya kujionyesha wazi kwenye siasa.

Watu wananitumia meseji mbaya, eti mimi nimetumwa na viongozi, mara sijui mimi ni shoga, jamani hakuna mambo kama hayo, nawataka watanzania wajue hayo ni mambo za uzushi, sijui ata yametoka wapi” Alisema Steve Nyerere

Quote of The Day:

Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Tazama Matokeo ya Kidato cha Sita Mwaka 2014

$
0
0
Matokeo ya mtihani wa kidato cha 6
yaliyofanyika tarehe Mei 5 - 21, yametoka na
jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na asilimia
85.73 wamefaulu katika madaraja ya I- III.
Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia
95.98 ya watahiniwa waliofanya mtihani
kidato cha 6 wamefaulu. Wasichana
waliofaulu ni 12,080 na wavulana waliofaulu
ni 26,825
- Watahiniwa waliopata division IV ni 4,420
sawa na asilimia 12.54
- Watahiniwa waliopata zero (0) ni 612 sawa
na asilimia 1.74.
- SHULE 10 ZILIZOONGOZA
1. Igowole
2. Feza Boys
3. Kisimiri
4. Iwawa
5. Kibaha
6. Marian Girls
7. Nangwa
8. Uwata
9. Kibondo
10. Kawawa
- SHULE 10 ZA MWISHO
1. Ben Bella
2. Fidel Castro
3. Tambaza
4. MuhezaHigh School
5. Mazizini
6. Mtwara Technical
7. Iyunga technical
8. Al- falaah Muslim
9. Kaulia
10. Osward Mang'ombe

Click NECTA Kusoma Matokeo

Quote of The Day:

Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Audio: Diamond awapa baraka zote wanaotumia sura yake kufanya biashara

$
0
0
Diamond Platinumz’ ni jina ambalo linakubalika zaidi ama jina la msanii wa bongo flava mwenye mashabiki wengi zaidi nchini Tanzania, lakini umati wa mashabiki wanaompenda Diamond ni soko la wajasiriamali ambao wanalitumia kuingiza siku.

Hivi sasa wapo wafanyabiashara wanaouza fulana zenye jina au picha ya Diamond bila makubaliano yoyote na msanii huyo.

Hata hivyo, wafanyabishara hao hawatakiwi kuwa na hofu. Mwimbaji huyo amefunguka katika kipindi cha The Jump Off cha 100.5 Times Fm na kuwapa ruhusa wale wote wanaofanya hivyo.

“Kuwekwa tu pale kwangu mimi nimefurahi, nisiwe mnafiki. Siwezi kusema nimesikia uchungu eti kwa nini ametumia sura yangu hivyo. Yaani nimefurahi kwa sababu ninaona kama taifa limeni-appreciate kazi yangu na mtu katengeneza t-shits na kauza imeuzika kweli kwa sababu inaweza kuwekwa bwana ‘Salamu’ isiuzike (kicheko)…..mimi kwangu ni rukhsa” Amesema.

Ruhusa hii imepekwa hadi kwenye  saloon.

Hata hivyo, ametahadharisha kutotumia brand ya ‘Wasafi Classic’ kwa sababu hiyo ni brand yake. “Labda mtu atumie ‘Wasafi’, hapo tatizo lingine.”

Quote of The Day: Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Mtoto wa miaka 8 aiba benki kwa kutumia iPad!

$
0
0
Kuna baadhi ya matukio ya kivamizi tumezoea kuyaona kwenye filamu za kipelelezi huku yakituacha midomo wazi na sifa zote zinaenda kwa mtayarishaji, muongozaji na waigizaji wa filamu hiyo.

Lakini hili ni tukio halisi na sio filamu, unapodhani kuna usalama wezi hubuni mbinu ambazo hata hazifiriki kirahisi.

Maafisa wa Plainfield, New Jersey, Marekani walijikuta katika wakati mgumu wakimsaka mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye anadaiwa kuiba bank kwa kutumia iPad yake tu.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa sita mchana Jumatano June, 25 mwaka huu katika beki inayoitwa Greater Plainfield Bank & Trut. Maafisa walifika katika eneo la tukio haraka kuungana na walinzi kumsaka mtoto huyo baada ya kupigiwa simu na mkuu wa ulinzi wa bank hiyo ambapo awali walidhani alikuwa anatania.

Walipofika eneo la tukio, wafanyakazi wa benki hiyo walieleza jinsi ambavyo tukio hilo limetokea, ambapo mtoto huyo kwa utulivu alitembea hadi kwa mmoja kati ya tellers ambaye jina lake halikutajwa.

Alipofika kwa teller huyo kwa utaratibu tu alimpa iPad iliyokuwa na message juu iliyosomeka ‘giv me all of th money I hav a gun n my bookbag’. Kwa uoga mfanyakazi huyo ambaye aliishia kuuona mkono na iPad zaidi, alimkabidhi pesa zinazokadiriwa kuwa $12,000 na mtoto huyo alifanikiwa kuvuka mlango tu na kuchukua ‘motorized scoote’ akatoweka haraka kwenye jengo hilo.

Camera za jengo hilo zinamuonesha mtoto huyo aliyekuwa amevaa fulana nyekundu iliyoandikwa mbele ‘TURN DOWN 4 WHAT?’. Na anaonekana akitereza na begi lenye pesa begani kwake.

Hakuna shuhuda mwingine aliyeshtukia wakati wa tukio hilo zaidi ya mfanyakazi wa benki.

Kafulila:Ikitokea Nikifa Basi Serikali ya CCM Ndio Wahusika Wakuu wa Kifo Changu

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema endapo itatokea kwa namna yoyote akafa, mhusika mkuu wa kifo chake itakuwa “Serikali ya CCM” na ameagiza kuwa kamwe wasifike kwenye msiba wake wala kutoa rambirambi.

Wakati Kafulila akitoa tuhuma hizo nzito mkoani Kigoma, Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kutangaza zabuni kwa ajili ya kupata kampuni ya kimataifa kwa ajili ya kukagua akaunti ya escrow iliyofunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha kusubiri kumalizika kwa mgogoro ulio mahakamani baina ya Shirika la Umeme (Tanesco) na kampuni binafsi ya kufua nishati hiyo ya IPTL.

Kauli ya Kafulila inatokana na mbunge huyo wa tiketi ya NCCR-Mageuzi kudai kutishiwa maisha na Mwanasheria Mkuu Jaji Federick Werema. Jaji Werema anadaiwa kutoa vitisho hivyo baada ya Kafulila kumtaja ndani ya Bunge kama mmoja wa wahusika katika kashfa ya wizi wa Sh200 bilioni kutoka katika akaunti hiyo ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwa nyakati tofauti katika Uwanja wa Mwanga Center na Cine Atlas mjini Kigoma, Kafulila alisema amejitolea maisha yake kupigania rasilimali za taifa ambazo zinachotwa na genge la watu wachache kwa masilahi yao binafsi na kuwaacha Watanzania wengi wakiishi katika lindi la umaskini na huduma mbovu za kijamii.

“Mbunge wenu (Kafulila) nilisema ndani ya Bunge kwamba Sh200 bilioni zimeibwa katika akaunti ya escrow na waliozichota wapo na wanajulikana, lakini Serikali haitaki kuwachukulia hatua. Mbaya zaidi hata Spika wa Bunge (Anne Makinda) amekataa kuunda Kamati teule ya Bunge ili ichunguze kashfa hiyo,” alisema Kafulila.

“Matokeo yake nimeanza kutishiwa maisha yangu na Serikali imekaa kimya licha ya kuliwasilisha jambo hilo kwenye vyombo vya dola. Naomba nichukue nafasi hii kutoa tamko kwamba wakati wowote nikifa, mhusika mkuu wa kifo changu ni Serikali ya CCM na kamwe sitaki wafike kwenye mazishi na hata msiba wangu.”

Pia, alimlaumu Mkuu wa Polisi (IGP), Ernest Mangu kwa kukalia kimya jambo hilo, akisema amepoteza imani na jeshi hilo kwa vile linaonekana kumuogopa Jaji Werema kwa kushindwa hata kumuhoji.

“Nilipeleka malalamiko yangu kwa IGP, lakini hadi hivi leo (jana) ninapoongea hapa hajawahi hata kuitwa polisi atoe maelezo. Hili ni janga kwa utawala wa kisheria nchini. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa tulitarajia mtu mwenye hadhi ya jaji awe mtii na mtekelezaji wa sheria za nchi, lakini inapofikia jaji kutishia kuniua, hapo ujue mfumo wa sheria ni legelege na hauna nguvu kwa baadhi ya watu.”

Wakati wa Bunge la Bajeti, Kafulila alisema fedha hizo zilipitishiwa kwenye benki moja na kuchukuliwa zikiwa taslimu, tofauti na sheria za benki na kuwatuhumu vigogo wa Serikali kuhusika na akiomba Bunge liunde kamati huru kuchunguza tuhuma hizo.

Wakati Bunge hilo likiendelea, Jaji Werema alitumia neno “tumbili” kumhusisha na Kafulila na ndipo mbunge huyo wa Kigoma alipomwita mwizi na kusababisha tafrani ambayo iliepushwa na wabunge wengine waliomzuia Jaji Werema asimkaribie Kafulila.

Inataarifiwa kuwa akaunti hiyo ilikuwa na takriban Dola 250 milioni za Marekani, lakini baada ya kikao cha pamoja kati ya Kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), Tanesco na Wizara ya Nishati ilikubaliwa kuwa Dola 122 milioni kati ya hizo zitolewe kutoka akaunti hiyo na kulipwa PAP ambayo ni mmiliki mpya wa IPTL.

Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa tenda kwa kampuni za ukaguzi wa hesabu za kimataifa ili kufanya uchunguzi. “Serikali iache bla bla, itoe tamko kwa fedha hizo zaidi ya Sh400 bilioni. Wanasema siyo fedha za serikali, wakati nyaraka zote hizi nilizonazo zinaonyesha kuwa ni za serikali.

Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Kampuni ya Precision Air Yapata Hasara ya Sh 12.1 Billion

$
0
0
Hali ya kifedha ya kampuni ya usafiri wa anga ya Ndege ya Precision Air bado haijatengemaa baada ya kupata hasara ya Sh12.1 bilioni katika mwaka ulioishia Machi mwaka huu. Hata hivyo, hasara hiyo ni ahueni baada ya mwaka jana kupata hasara kubwa zaidi ya Sh30.1 bilioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya kifedha ya kampuni hiyo ya mwaka ulioshia Machi iliyotolewa jana kwenye vyombo vya habari, hasara hiyo ambayo bado ni mafanikio ya ukuaji wa asilimia 60, ilichagizwa na mabadiliko ya viwango vya kubadilishia fedha, riba katika mikopo ya ndege, uchakavu wa mali na malipo mbalimbali ya kampuni.

Hata hivyo, mafanikio hayo yanaonyesha jitihada za wazi za menejimenti kuiimarisha kampuni hiyo, ambayo mwaka jana ilijikuta ikihaha kutafuta fedha zaidi ya Sh50 bilioni ili kuongeza mtaji na ufanisi katika utoaji wa huduma zake.

Mwaka jana, Precision iliiomba Serikali iikopeshe kiasi hicho, lakini kilishindikana baada ya ombi lao kukataliwa na hivyo kutafuta njia mbadala ikiwemo kuliomba msaada Shirika la ndege la Kenya Airways, jambo ambalo hata hivyo halijawekwa wazi utekelezaji wake.

Moja ya mikakati iliyofanywa na Precision mwaka huo ni kuzirudisha ndege mbili zilizokuwa zikichangia hasara kwa kiasi kikubwa kwa wakodishaji wake, jambo lililosababisha idadi ya abiria wake kushuka kutoka 895, 654 wa mwaka wa awali hadi 687, 981.

Kutokana na hatua hiyo, taarifa hiyo ilisema kiwango cha mapato kilishuka kwa asilimia 22 hadi Sh141.1 bilioni kutoka Sh181 bilioni.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa Precision Air, Michael Shirima na afisa mtendaji mkuu, Sauda Rajab ilisema hata hivyo walipata faida katika kipengele cha uendeshaji kwa kupata Sh3.6 bilioni ikilinganishwa na hasara ya Sh18.1 bilioni ya mwaka ulioishia Machi, 2013 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 121.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mkakati wa kuiimarisha PW haukutelezwa kikamilifu hadi kipindi cha ukaguzi kilipokamilika.

Hata hivyo, ilisema kuwa mikakati mingine kama usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha, upangaji makini wa safari na ufanisi katika uendeshaji wa safari zake, viliwezesha mapato kwa abiria yaongezeke kwa asilimia 11 ukilinganisha na mwaka uliopita. “Matumizi ya moja kwa moja yalipungua kutoka Sh147 bilioni hadi Sh99 bilioni, hali kadhalika matumizi yasiyo ya moja kwa moja yalipungua kutoka Sh44.4 bilioni hadi Sh38.9 bilioni.

Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Ikulu: Wanaomkosoa Jakaya Kikwete Kuhusu Katiba Hawako Sahihi

$
0
0
Ofisi ya Rais imesema kuwa wanaomkosoa Rais Jakaya Kikwete kuhusu msimamo wake katika mchakato wa Katiba Mpya hawako sahihi kwa kuwa ni mlezi na ana haki ya kutoa maoni yake kama mkuu wa nchi na kama mwanasiasa.

Pia, imewataka wasiokuwa wajumbe wa Bunge la Katiba waiache kazi hiyo mikononi mwa Bunge hilo kwa sasa hadi hapo rasimu itakapowasilishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya kuikubali au kuikataa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salva Rweyemamu ikiwa ni siku moja baada ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), kutoa tamko zito kwa Rais Jakaya Kikwete ikiishangaa kauli yake ya kupinga mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya Watanzania.

Rais Kikwete amekuwa akilaumiwa na taasisi na watu binafsi baada ya kulieleza Bunge la Katiba kuwa kuna baadhi ya mambo kwenye Rasimu ya Katiba ambayo hayawezekani kutekelezeka, akitoa mfano wa muundo wa Muungano wa serikali tatu, jambo ambalo CCT ilisema jana kuwa alitakiwa alifanye wakati Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikimfuata kumweleza maendeleo ya kazi yao.

Hata hivyo jana, Rweyemamu aliliambia gazeti hili kuwa: “Kinachoendelea kwa sasa kwa baadhi ya makundi ya kidini kutoa matamko dhidi ya Rais si sahihi, kwa kuwa Rais ni mlezi na ana haki ya kutoa mtazamo wake kama mkuu wa nchi na kama mwanasiasa.”

Alisema kimsingi mchakato huo ni wa kisiasa na Rais ni mwanasiasa, pia ni mkuu wa nchi hivyo ndiye mwenye uwezo wa kutoa ushauri na kutoa angalizo pale inapohitajika, hasa anapoona kuna jambo lisilokuwa sawa, hivyo hakuna haja ya kuendelea kusimama kupinga kile alichokielekeza nje ya Bunge.

Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Wanawake Wengi Walioolewa ni Wepesi wa Kuchepuka..Yaani Simple Kama Kumsukuma Mlevi

$
0
0
Wanawake wengi walioolewa wamekuwa wepesi (achilia mbali vidada ambavyo havijaolewa, ingawa navyo ni majanga lakini, afadhali mitego yao kidogo ni negotiable).

Wengi wao huwatongozi ila watakutongoza wenyewe! Kundi risky zaidi ni la wamama wa nyumbani au wanawake ambao hawajasoma (I am sorry to say this)!

Unaweza kukuta mme wake ana fedha na kila kitu, lakini kwa sababu jamaa hajaajiriwa serikalini au kwenye taasisi au kampuni (kumbuka tulio wengi tunatamani kujiajiri!), mke wake anamchukulia kama mtu fulani ambaye hana hadhi nzuri ya kuwa mme.

Sumaku kali zaidi ambazo huwavuta wamama wa aina hiyo, ni wale vijana au watu wazima walioajiriwa, wanaotoka asubuhi, wamepiga tai, kiatu kiwi full time, wengine suti, halafu ni watu wa misheni town (wenye magari sijui inakuwaje, mtatuambia), (haata kama kazi zao ni kufagia au kuzunguka na mafile maofisini)!

Wanawake wa aina hiyo huanza kwanza kwa kutafuta ukaribu na mazoea na watu wa aina hiyo kwa udi na uvumba katika harakati za kufanikisha azma zao.

Licha ya uzoefu nilioushuhudia juu ya wamama hapo juu, hivi karibuni nimekumbana na majanga kadhaa yakihusisha wanawake walioolewa kwa ujumla, wengi wao wanaoonekana ni sex hungry moms au gold diggers. Nawapa tu mifano michache kuthibitisha haya ninayoyasema:

1. Mie nakaa mwenyewe mmama from no where akaanza kuniletea chakula (niliogopa sana), akaniambia naona unapata shida unakaa mwenyewe na wewe ni mwanaume huwezi kujipikia.

Siku ya kwanza sikukila (nilikiweka kwenye chombo changu nikampa sahani, baadaye nilikimwaga), maana niliona kama labda kaweka kitu. Siku nyingine akaleta na kuniambia tule wote! Hooooooooo, nikamwambia tutakula wapi?

Akasema kwako, usiogope mme wangu amesafiri! Sasa tukiwa tumekaa, alikuwa amejifunga kanga moja, anatawanya miguu na kuirudisha, nilijikaza sikufanya chochote, vituko anavyonifanyia mpaka sasa ni siri yangu.

2. Mwingine alipata namba yangu kupitia simu ya mmewe ambaye ni rafiki yangu, kila mara hasa usiku ana msgs kama hizi: "shem habari, nahisi wewe ni mcheshi, huna kiburi wala makuu, tena unachat na mimi bila shida, nina hamu siku moja nije Dar nikufahamu, au sio shem?"

Mara nyingi sijibu, akiona hivyo "shem nijibu basi, usiogope maana mme wangu hayupo sasa hivi". Vituko vyake siku hizi havisimuliki!

3. Mwingine, kutwa kulalamika kuhusu maisha yake na ndoa "Yaani shem, we acha tu, maisha magumu, rafiki yako naye kipato hakieleweki na mie sikusoma wala kubahatika kuajiriwa, maisha yanaenda tu kwa nguvu za Mungu, ningekuwa sio mvumilivu sidhani kama hii ndoa ingekwepo, shem unakaa wapi nije kukusalimia au una mke?" Mie najiuliza hivi wakati wa kufunga ndoa hakuapa kuwa na mmewe kwa shida na raha?

4. Mwingine ni mama jirani yangu, tena ni mtu anayejiweza, siku moja akaniita anaomba nimsaidie kurudishia taa imeungua, nilivyopanda juu ya meza alinipa taa - tube light mbovu, kuiweka haiwaki, akaniambia naomba simu yako nimpigie kijana fulani wa mtaani aniletee taa nyingine, nilivyompa kumbe alijipigia, halafiu akaniambia hapatikani, acha.

Tangu awe na namba yangu, utaona mida ya saa 4 usiku anatuma msgs kama vile "Mambo, Jumamosi hii twende tukatembee" au "Nina kitu nataka kukuambia ila tunahitaji faragha", Huwa namjibu, nina mambo mengi, labda siku nyingine.

Ni majanga mengi sana nakutana nayo yanayohusisha akina mama walioolewa. Mliooa kuweni makini na wake zenu, wengi ni washenzi sana na wana sophisticated means za kuwaengage wanaume wengine kwenye mahusaiano na wao! Pia najiuliza tatizo lao la kuzoeana na wanaume wengine na kujifanya wana hamu ya kuchat au kuwa karibu nao na sio waume zao ni nini?

NB: Nawaasa vijana kukaa mbali na mke wa mtu, maana mke wa mtu ni zigo la madawa ya kulevya.

Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images