Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Jokate Awafumbua Macho Vijana

$
0
0
Jokate Awafumbua Macho Vijana
Mjasiriamali na Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amewataka vijana kutumia mitandao ipasavyao.

Jokate  amesema ni vema vijana wakatumia mitandao kuwa ajili ya kupata taarifa sahihi ambazo zitakuwa na manufaa kwao.

“Vijana wasitumie mitandao ya kijamii kujua Jokate amevaa nini leo au kaweka nywele gani inatakiwa watafute taarifa mbalimbali ambazo kila wakati hutolewa katika internet ili ziweze kuwapa ufahamu na pengine kuwasaidia” Jokate ameimbia EA Radio.

Katika hatua nyingine Jokate amesema ni vizuri kwa kijana kuwa na kazi yake binafsi ili aweze kujiamulia mwenyewe mambo yake kwamba leo afanye kazi gani nakadhalika.

Tiketi za Kushuhudia Kombe la Dunia 2018 Zaanza Kuuzwa na TFF

$
0
0
Tiketi za Kushuhudia Kombe la Dunia  2018 Zaanza Kuuzwa na TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea tiketi 290 kutoka kwa Shirikisho la Kimataifa la soka (FIFA) kwa Watanzania watakaotaka kwenda kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia mwakani 2018.

Tiketi hizo zipo kwenye makundi mbalimbali yaliyogawanywa kulingana na aina ya mechi na hatua mbalimbali za mashindano hayo ikiwemo hatua ya makundi na zile zinazofuata.

TFF inalo jukumu la kusimamia zoezi hilo la uuzwaji wa tiketi hizo kwa Tanzania ambapo mwisho wa zoezi hilo ni Januari 15, 2018. Kwa yeyote mwenye nia ya kununua tiketi awasiliane na Idara ya mashindano TFF.

Wakati huohuo, utaratibu wa kadi maalumu za kuingilia Uwanjani kwa waandishi wa habari kutoka Tanzania (accreditation) katika mashindano hayo ya Kombe la Dunia Russia uko tayari na waandishi wanatakiwa kujaza kupitia link maalumu inayosimamiwa na Idara ya habari na mawasiliano ya TFF.

Kwa mwana habari yeyote anayetaka kuripoti fainali hizo za kombe la Dunia awasiliane na Idara ya Habari na Mawasiliano TFF ili aweze kuthibitishwa FIFA ambapo mwisho wa zoezi hili ni Januari 15, 2018.

Kasimu Majariwa Aitaka AU Kufanya Uchunguzi wa Kina Vifo vya Wanajeshi 14 JWTZ Waliouawa DRC

$
0
0
Kasimu Majariwa Aitaka AU Kufanya Uchunguzi wa Kina Vifo vya Wanajeshi 14 JWTZ Waliouawa DRC
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania inautaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa kina, ulio wazi na wa ukweli juu ya vifo vya Wanajeshi 14 wa Jeshi la Wananchi waliouawa huko Jamhuri ya Congo December 8, 2017.

Amesema hayo leo December 14, 2017 wakati akiongoza mamia ya wanajeshi, viongozi wa serikali, na familia za Mashujaa hao na kueleza kuwa serikali inatumaini Umoja wa Mataifa utafanya hivyo haraka ili haki iweze kutendeka.


Ametoa pole kwa Jeshi, familia za wafiwa na Watanzania kwa ujumla na kuwaasa wanajeshi kuwa yaliyotokea DRC yasiwakatishe tamaa katika kutimiza wajibu wao huko Congo na kwingineko ambako wanatoa msaada huo.

Polisi Wakumbana na Chatu Mkubwa Wakipiga Doria

$
0
0
Polisi Wakumbana na Chatu Mkubwa Wakipiga Doria
Maafisa wawili wa polisi katika jimbo Queensland nchini Australia walipigwa na butwaa walipokumbana na chatu mkubwa wakipiga doria.
Ingawa walipigwa na butwaa mwanzoni, walitumia fursa hiyo kupiga picha na chatu huyo.
Picha ya mmoja wa polisi hao ilipakiwa mtandaoni na imezua hisia si haba.
"Nyoka huyo alikuwa na urefu wa zaidi ya mita tano, na kusema kweli si kiumbe ambaye unaweza kutafuta utepe useme utampima," polisi hao waliambia BBC.
Wachezea nyoka kuajiriwa chuoni Nigeria
Nyoka atafuta 'joto' kwenye kiatu
Picha hiyo iliyopakiwa na polisi hao kwenye mitandao ya kijamii Ijumaa imetazamwa mara zaidi ya milioni mbili, na kutolewa maoni mara 10,000.

Polisi hao walikutana na nyoka huyo karibu na Wujul Wujul, karibu 345km (maili 210) kaskazini mwa jiji la Cairns.
Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu
Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria
Chatu aina ya Scrub, ambao huwa ndio nyoka warefu zaidi Australia, wanaweza kufikia urefu wa hadi 7m (futi 23).

Polisi Wamshikilia Mwanamke Aliyejaribu Kuwauza Watoto Wake Pacha

$
0
0
Mwanamke Aliyejaribu Kuwauza Watoto Wake Pacha Akamatwa na Polisi
Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya madai kuwa alijaribu kuwauza watoto wake pacha wenye umri wa mwezi mmoja nchini Nigeria.
Ameshtaki kwa kuhusika katika bishara ya kuuza watoto lakini polisi wanasema kuwa mashtaka zaidi yataongezwa.

Mwanamke huyo alikamatwa wakati akijaribu kuuza watoto wake wasicha kwa dola 980 kwa mnunuzi ambaye aliwajulisha polisi.
Visa vya kuuzwa watoto wa kupangwa vimekuwa tatizo kwa muda mrefu chini Nigeria.

Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini.
Alipohojiwa mwanamke huyo alisema kuwa changamoto za kifedha zilisababisha afanye hivyo.
Nigeria ni mzalishaji mkuwa wa mafuta lakini asilimia kubwa ya watu milioni 170 wanaishi kwenye umaskini.

Mwaka 2013 wasichana wajawazito 17 na watoto 11 waliokolewa wakati polisi walivamia "kiwanda cha watoto" katika jimbo la Imo
Miaka miwili baada ya sakata hiyo, mwanamke mwingine alishikwa akipokuwa akijaribu kumuuza mtoto wake kwa dola 90 katika jimbo la Cross River.

Hivi Ndivyo Tukio la Kukamatwa Dola Milioni 1 Uwanja wa Ndege Lilivyokuwa

$
0
0
Hivi Ndivyo Tukio la Kukamatwa Dola Milioni 1 Uwanja wa Ndege  Lilivyokuwa
Polisi Kitengo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), inawashikilia watu wawili akiwamo raia wa Uganda kwa tuhuma za kukutwa na dola 1 milioni za Marekani.

Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi alisema jana kwamba fedha hizo zilikuwa zikitokea Uganda na ziliingizwa nchini kinyume cha taratibu.

Aliwataka watuhumiwa hao kuwa ni Wilfred Usangi, raia wa Uganda na mlinzi wa kampuni ya kusafirisha fedha ya SGA, Meshaki Sangwa.

Kamanda Mbushi alisema hayo jana baada ya kuulizwa na mwandishi wetu kauli iliyotolewa awali na Rais John Magufuli kuhusu fedha hizo alipokuwa akifungua tawi la Benki ya CRDB mjini Dodoma.

“Pia nataka mdhibiti matumizi ya dola, hivi ninavyozungumza kuna dola milioni moja zimekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, hakuna maelezo yoyote juu ya kuingia fedha hizo, ni lazima tuwe makini,” alisema Rais Magufuli.

Kamanda Mbushi alisema watuhumiwa walikamatwa Desemba 11, saa 2:30 usiku wakiwa eneo la ukaguzi uwanjani hapo.

Alisema raia huyo wa kigeni aliwasili nchini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya akitokea Uganda akiwa na fedha hizo ambazo alikuwa akizipeleka katika Benki ya Stanbic bila kuthibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). “Hawa wamekuwa na mazoea ya kusafirisha fedha mara kwa mara bila ya kufuata utaratibu. Alitakiwa achukue fomu, ajaze fedha walizokuwa nazo ili maofisa wa TRA wathibitishe lakini hawakufanya hivyo,” alisema.

Kamanda Mbushi alisema watuhumiwa bado wanashikiliwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

TFF Yawakingia Kifua Kilimanjaro Stars "Wachezaji Walibadili Jezi Airport"

$
0
0
TFF Yawakingia Kifua Kilimanjaro Stars "Wachezaji Walibadili Jezi Airport"
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesikitishwa na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwamba wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ walirudi nchini jana bila ya kuwa kwenye sare na badala yake kila mmoja alivaa nguo zake binafsi.

Taarifa hizo si za kweli na zimelenga kuwapotosha wa Tanzania na wapenda mpira wa miguu ama kwa makusudi au kwa sababu binafsi kwa wale wanaosambaza taarifa hizo.

Kilimanjaro Stars ilitua nchini saa 2.30 asubuhi kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) wachezaji wote wakiwa ndani ya sare.

Baadhi ya wachezaji waliomba kwa uongozi kwamba hawana mpango wa kwenda kambini badala yake walitaka kwenda kuungana na familia zao ambazo zilifika uwanjani kuwalaki. Uongozi uliwakubalia na hivyo kupata eneo la faragha Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ili kubadili sare husika na kuvaa nguo binfasi za kawida kabla ya kutawanyika.

Wachezaji walibadili sare hizo baada ya kufanyika utaratibu wote wa kuvunjwa kwa kambi na kwa kuwa kila mmoja alikuwa anarudi nyumbani kwake alikuwa na uhuru wa kuvaa mavazi anayoyataka.

TFF inachukuwa nafasi hii kukanushana kulaani taarifa hizo ambazo hazikuzingatia uweledi wa kuuliza upande wa pili na tunasisitiza kuwa wachezaji walirudi kila mmoja akiwa kwenye sare maalumu za timu kwa kuwa TFF siku zote tunaamini katika utaratibu na tumekuwa waumini wazuri wa kufuata utaratibu tunaojiwekea.

Breaking Newz: Mbunge wa Chadema Godwin Moleli Atangaza Kujivua Uanachama

$
0
0
Breaking Newz: Mbunge wa Chadema Godwin Moleli Atangaza Kujivua Uanachama
Mbunge wa jimbo la siha mkoani Kilimanjaro kupitia chama cha demokraisia na Maendeeleo Chadema Dkt Godwin Oloyce Moleli ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho.

Kutana na Mtabibu wa Nyota Duniani Maalim Fadhil Rashid Kutoka Comoro Kwa sasa Yupo Tanzania

$
0
0

KUTANA NA MTABIBIBU WANYOTA DUNIANIKOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE ANADAWA ZA KI COMRO DAWAZAKE HABAHATISHI MUONE HARAKA AKUSAIDIE TEZI NAUVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABI MALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI ZAMAJINI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YAKUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NAUMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWAHARAKA KUZUIYA CHUMAULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI KARIBUNI WOTE TIBA NIKWADINI ZOTE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO DUNIANI

CALLING +255719362806/

WHATSAPP CALLING +255785786436

Rais Magufuli Awamwagia Neema Walimu Awajaza Mapesa

$
0
0
Rais Magufuli Awamwagia Neema Walimu Awajaza Mapesa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendesha harambee na kuchangisha jumla ya milioni 60 ambazo watapewa wajumbe wa Chama Cha Walimu ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu CWT.

Rais Magufuli alianzisha zoezi hilo kwa kutoa milioni 10 ili wajumbe hao waweze kupata fedha za chakula na baadaye Rais kuanza kuwaita viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi za Serikali ili waweze kuchangia fedha za chakula ambapo kwa ujumla ziliweza kupatikana jumla ya milioni 60.
Katika zoezi hilo la uchagiaji wa fedha hizo za chakula kwa wajumbe 1200 wa CWT lilikuwa kama ifuatavyo
Rais Magufuli milioni 10
Waziri Mkuu  Milioni 10
Waziri wa Elimu, Ndalichako milioni 6
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama  milioni 6
Mama Magufuli Milioni 1
Mama Majaliwa  Milioni 1
Spika wa Bunge Job Ndugai Milioni 5
Katibu Mkuu Tamisemi Milioni 4
Naibu Katibu Mkuu Tamisemi  Milioni 4
Mstahiki Meya wa Dodoma Milioni 1
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Milioni 1
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mstaafu) George Mkuchika Milioni 3
Mkuu wa Chuo cha Dodoma Milioni 4
Mkurugenzi wa usalama wa taifa Milioni 4
Jumla ya fedha zilizopatikana zilikuwa milioni 60 hivyo Rais Magufuli aliagiza kuwa milioni 50 wapewe wajumbe wa CWT huku milioni 10 zikienda kwa walimu wanafunzi wa UDOM ambao walishiriki katika Mkutano huo. Lakini pia Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zifike kabla ya wajumbe hao hawajamaliza Mkutano wao. 

Haider Gulamali Afikishwa Mahakamani

$
0
0

Haider Gulamali Afikishwa Mahakamani
Haider Gulamali (46), aliyewania kuteuliwa kugombea ubunge Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Singida.

Gulamali aliyesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Flora Ndale jana Jumatano Desemba 13,2017 anasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu dhamana.

Baada ya kusomewa mashtaka jana alipelekwa rumande kutokana na mvutano wa kisheria kati ya mwanasheria wa Takukuru, Edson Mapalala na wakili wa mshitakiwa, Godfrey Wasonga kuhusu dhamana.

Gulamali aliyeshinda kura ya maoni kabla ya CCM kusitisha mchakato amezuiwa kugombea nafasi hiyo akituhumiwa kwa rushwa.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alitumia mamlaka yake kuitisha upya mchakato wa kumpata mgombea wa chama hicho na uchaguzi unafanyika leo Alhamisi Desemba 14,2017 na utafunguliwa na Kinana.

CUF ya Lipumba Yasimamisha Wagombea Ubunge Katika Uchaguzi Mdogo

$
0
0
CUF ya Lipumba Yasimamisha Wagombea Ubunge Katika Uchaguzi Mdogo
Chama cha Wananchi (CUF) upande unaomuunga mkono Mwenyekiti wa Taifa anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba umesimamisha wagombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa majimbo matatu.

Uchaguzi uliopangwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanyika Januari 13,2018 utafanyika katika majimbo ya Longido, Singida Kaskazini na Songea Mjini.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya amewataja wagombea hao na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni Delfina Mlelwa (Singida Kaskazini), Japhary Mneke (Songea Mjini) na Kisiongo Mayasek Olukuya (Longido).

Uteuzi huo umefanyika siku chache baada ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutishia kutoshiriki uchaguzi huo endapo NEC haitasitisha mchakato na kujadili dosari zilizojitokeza katika uchaguzi wa awali.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa niaba ya Ukawa, alisema uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 uliofanyika Novemba 26,2017 ulikuwa na dosari zinazopaswa kujadiliwa kabla ya kufanyika uchaguzi mwingine.

Wivu wa Mapenzi Wasabababisha Mwanamke Kumuua Mke Mwenzie na Kumzika Shambani

$
0
0
Mwanamke Amuua Mke Mwenzie Kisa Wivu wa Kimapenzi na Kumzika Shamani
mMwanamke mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara anatuhumiwa kumuua mke mwenza na kumzika shambani.

Kifo hicho kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi kimetokea katika Kata ya Kibimba mkoani Kagera ambako aliyeuawa alizikwa kwenye shamba la viazi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayenzi, Philipo Rutumbanya amesema Edina Joseph (28) anatuhumiwa kumuua Noelina Joseph (24).

Wawili hao ni wake wa Joseph Laurean (33), mkazi wa Kijiji cha Mayenzi wilayani Ngara.

Rutumbanya amesema mauaji hayo yalifanyika jana Jumatano Desemba 13,2017 saa 7:30 mchana na kwamba mtuhumiwa amefikishwa polisi.

Amesema Edina alihisiwa kuhusika na mauaji baada ya mumewe kumkuta akiwa na damu mwilini shambani.

Mwenyekiti huyo wa kijiji amesema Laurean  alipomhoji mkewe hakujibu lolote na alipofuatilia shambani aliona nguo za mkewe mdogo lakini yeye hakuwepo.

Amesema Laurian alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ndipo mtuhumiwa Edina alipohojiwa na alieleza alikuwa na chuki na mke mwenzake aliyeolewa miezi miwili iliyopita.

Mwenyekiti huyo amesema walimweka Edina chini ya ulinzi na aliwapeleka kwenye shamba la mume wake ambalo ni mali ya binamu yake John Shimimana alikoonyesha alikomzika mwenzake kwenye tuta la viazi.

Akizungumzia tukio hilo, mume wa wake hao, Laurian amesema ameishi na Edina kwa miaka 12 na wamejaliwa watoto watano; wa kike mmoja na wa kiume wanne. Pia ni mjamzito.

Laurian amesema mkewe mdogo alimpangia nyumba katika Kijiji cha Kanazi umbali wa kilomita sita kutoka Kijiji cha Mayenzi na alimpatia shamba ambalo alipewa na binamu yake Shimimana, ambaye ni diwani wa Kata ya Kibimba.

Amesema alipotoka matembezi kijijini alifika nyumbani kwa Edina alikokuwa amelala Jumanne Desemba 12,2017 lakini  hakumkuta.

Laurian amesema alikwenda kumuona mkewe mdogo Noelina aliyekuwa shambani ambako alimkuta Edina akiwa na jembe na mwili ukiwa na damu.

Amesema alipomhoji kuhusu damu alitetemeka na alipofuatilia alikuta nguo za Noelina lakini yeye hakuonekana.

"Tangu nioe mke wa pili kumekuwa na malumbano na malalamiko lakini niliona kawaida sikutarajia kama angechukua uamuzi wa kumuua mwenzake," amesema Laurian.

Polisi wilayani Ngara imefika eneo la tukio ambako Edina amekamatwa na baada ya kupata kibali cha Mahakama ya Wilaya ya Ngara mwili wa Noelina umefukuliwa.

Akizungumza wakati wa kufukua mwili ofisa upelelezi wa Polisi wilayani Ngara, Edward Masunga amewataka wananchi wakiwemo wanandoa kufuata utaratibu wa kufikisha malalamiko kwa viongozi wa vijiji badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Penzi la Rayvany na Mpenzi Wake Bado Njiapanda Aamua Kumtumia Ujumbe Huu Mwanae

$
0
0
Penzi la Rayvany na Mpenzi Wake Bado Njiapanda Aamua Kumtumia Ujumbe Huu Mwanae
Staa wa ngoma ‘Mbeleko’ Rayvanny aliyeko Marekani kikazi, baada ya kurushiana maneno yaliyoashiria kuwa amekosana kimahusiano na mama wa mtoto wake,  ‘Fayhma’ sasa ameonesha kuelekeza mapenzi mazito kwa kinachoweza kubaki kama kumbukumbu isiyobadilika kama hawatamaliza tofauti zao kwa suluhu ya wawili hao kurudiana.

Akiwa mjini Washington, Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha ya mwanae, Jaydany sambamba na maneno yayoambatana kwenye picha hiyo yaliyozungumza kuutamani ukaribu wake na mtoto wake huyo. Bila shaka mapenzi ya mzazi na mtoto yamechangia kumsukuma Rayvanny aoneshe hisia hizo. Aliandika Hivi "miss u jayvannboy @jayvannyboy

Katika hilo la wawili hao kutokauwa katika hali nzuri ya kimahusiano, inahesabika kuwa ni miezi isiyopungua miezi 7 tangu wawili hao walipokaribisha mtoto wao huyo wa kwanza kwakuwa taarifa za wawili hao kupata mtoto zilisambaa tarehe 19 mwezi Aprili mwaka huu.

Ofisi ya Taifa Takwimu:Tatizo la Ukosefu Ajira Lapungua Nchini

$
0
0
Ofisi ya Taifa Takwimu:Tatizo la Ukosefu Ajira Lapungua Nchini
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema tatizo la ukosefu wa ajiri nchini limepungua.

Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu, NBS Irineus Ruyoby amesema kwa mujibu wa takwimu walizonazo kwa sasa zinaonyesha tatizo la ukosefu ajira linaenda likipungua mwaka hadi mwaka.

“Takwimu ambazo tunazo zinaonyesha kiwango cha watu ambao hawaja ajiriwa kimepungua mwaka hadi mwaka, sasa hivi tupo katika kufanya tafiti nyingine tutaweza kujua hali halisi sasa ikoje” amesema.

Ameongeza kuwa uchumi wa Tanzania kwa sasa unaendelea kukua kwa kiwango cha wastani wa asilimia saba kwa mwaka na imekuwa hivyo kwa muda mrefu sasa.

Mjadara Mkali Waibuka Baada ya Mbunge wa Chadema Kujiudhulu

$
0
0
Barua na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza mbunge wa Siha (Chadema) mkoani Kilimanjaro, Dk Godwin Mollel amejiuzulu ubunge imezua mjadala.

Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema akizungumza na MCL Digital leo Alhamisi Desemba 14,2017 amesema naye ameona video na barua kwenye mitandao ya kijamii lakini hawana uthibitisho wowote.

"Mheshimiwa Mollel hakuwahi kuonyesha dalili yoyote kuwa yuko kwenye hilo wimbi na mimi nimeona hiyo barua na video kwenye mitandao. Bado kwangu nachukulia kama uvumi mpaka tutakapothibitisha," amesema.

Lema amesema kwa utaratibu alipaswa kumuandikia barua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe au viongozi wa Chadema.

Amesema akiwa katibu wa mkoa wa chama hicho hajapokea barua yoyote kutoka kwa Dk Mollel.

"Ukiangalia hata barua inayosambaa haijasainiwa na video inaonyesha ni mtu tu kajirekodi akarusha. Katika mazingira hayo hatuwezi kukurupuka kuzungumzia hilo jambo," amesema.

Taarifa inayosambaa kwenye mitandao ambayo haina saini inaonyesha kuandikwa na Dk Mollel akieleza ameamua kujivua uanachama wa Chadema kuanzia leo Alhamisi Desemba 14,2017.

Pia, ametangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge na kwamba huo ni uamuzi wake alioufanya akiwa na akili timamu na hajashinikizwa na mtu yeyote.

Wasiliana na The Great Maalim Hussein Mtaalam wa Kutatua Matatizo Yaliyoshindikana Kwa Kutumia Nyota na Dua

$
0
0
THE GREAT MAALIM HUSSEIN
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
Maalim Hussein ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO SAIDIA(Rudisha Mahusiano yako Ndani ya Saa 12 tu)

MAALIM HUSSEIN ni Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFATA MAELEKEZO YAKE..)

Je Unasumbuliwa na Mapenzi..?
Umeachwa na UMPENDAE Awe Mume/Mke na Bado Unampenda
Je Umejaribu Sehemu Nyingi Bila Mafanikio?
Mpigie Simu sasa Hivi Ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo..
Anauwezo wa Kurudisha Mahusiano yako na Kuimarisha NDOA Ndani ya saa 12 tu.
Je Umekimbiwa na Mumeo/Mkeo au Mpenzi na Anaishi na Mtu Mwingine..?
Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao (Mfarakano/Kimavi) Endapo Utafata Atakacho Kuelekeza.

Je Una Mpenzi wako ana Pesa na unataka Kumkamata? Muone Maalim Hussein Atamfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi..
Maalim Hussein Anatumia Jina La Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo..
Anatibu Kutumia QUR_AN DAWA ZA ASILI YA AFRICA, Dawa za KIARABU NA MAJINI..
ANATAFSIRI NDOTO. ANAPANDIKIZA NYOTA YA KUSHINDA BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUSKI NA VIFUNGO MBALIMBALI.

ZINDIKO ZA NYUMBA NA BIASHARA.. PETE ZA BAHATI.. HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA. HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA..
MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA..ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA  ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE..

Humaliza Kesi ya Aina Yoyote Ndani ya Siku 7 tu..
Hutoa Jini la MALI kwa wale Wanao Hitaji Utajiri Bila Masharti..
+255 674 835 107 WhatsAPP tu.

Picha: Rais wa Msumbiji Atua Nchini

$
0
0
Picha: Rais wa Msumbiji Atua Nchini
Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi amewasili mjini Dodoma kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.





Njombe Mjini Yasajili Nyota Wawili Waliyoshiriki AFCON U17

$
0
0
Njombe Mjini Yasajili Nyota  Wawili Waliyoshiriki AFCON U17
Klabu ya Mtibwa Sugar imewaruhusu nyota wake wawili Nickson Clement kibabage na Muhsin Makame Malima kujiunga na kikosi cha Njombe Mji kwa mkopo wa miezi sita.

Mchezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar na timu ya Taifa ya Serengeti Boys, Muhsin Makame Malima

Nickson Clement Kibabage anayemudu kucheza mlinzi wa pembeni na Muhsin Makame Malima anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wamejiunga na kikosi cha timu ya Njombe Mji kutoka katika mkoa wa Njombe.

Kwa takribani wiki moja wachezaji hawa wa kikosi cha Mtibwa Sugar walikuwa katika majadiliano na uongozi wa Njombe Mji na hatimaye makubaliano yamefikiwa na pande zote tatu ambazo ni wachezaji wenyewe , Klabu ya Mtibwa Sugar na Njombe Mji.

Wachezaji hawa waliokuzwa katika Academy ya Mtibwa Sugar yenye mskani yake Manungu wamejiunga na Njombe Mji kwa mkopo wa miezi 6 hivyo wachezaji hawa watadumu katika kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu wa 2017/2018.

Muhsin Makame Malima na Nickson Clement Kibabage ni kati ya vijana waliowakilisha taifa katika michuano ya AFCON chini ya miaka 17 kwa mara ya kwanza.

Mchuano Mkali CCM 22 Wachuana Nafasi Iliyoachwa Wazi na Nyalandu

$
0
0
Mchuano Mkali CCM 22 Wachuana Nafasi Iliyoachwa Wazi na Nyalandu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewaonya viongozi wa chama hicho ambao amesema wanawagawa wananchi.

Amesema endapo wataendelea kufanya hivyo watavuliwa uongozi.

Kinana amesema hayo leo Alhamisi Desemba 14,2017 akifungua mkutano wa halmashauri kuu ya jimbo unaopiga kura ya maoni kupata mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

Katika kinyang’anyiro hicho cha marudio wagombea 22 wamejitokeza kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Lazaro Nyalandu aliyejivua ubunge alioupa akiwa CCM na sasa amejiunga Chadema.

Amesema CCM ipo imara na wapambe wamepungua kwa kiasi kikubwa. Amewataka wagombea wafanye kampeni zinazofaa na mmoja akichaguliwa, wote wawe wamoja ili chama hicho kishinde kwa kishindo.

Kinana akizungumza katika mkutano huo unaofanyika Kijiji cha Ilongero, Singida amesema uchaguzi wa awali uligubikwa na vitendo vya rushwa ndipo uongozi wa juu wa CCM ulipoamua kufuta mchakato.

Ameagiza vitendo hivyo visijirudie akiwataka wajumbe wasirubuniwe kwa aina yoyote; na wagombea wakatae maombi ya wapiga kura ambao mara nyingi huwaambia unatuachaje.

Kinana amempongeza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Hassan Kilimba akisema amekuwa mwaminifu kwa chama hicho hata baada ya kuacha ubunge.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images