Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Vitu Vinavyofanya Wadada wa Kibongo Wapende Wanaume wa Kizungu

0
0
Kuna dada leo nilikuwa naongea naye ananiambia yeye anatamani sana aolewe na mzungu kwani ameshaona mambo yafuatayo ambayo a waname wengi wa kibongo hawana,

-Wanaume wengi wa kibongo anadai wanapenda sana michepuko

-Wanaume wengi wa kizungu wana real love japo wana ndoa za mikataba na nasema bora aishi kwa mkataba kuliko kuishi na mwanaume wa kibongo kwa muda mrefu ambaye kila siku hajui real love ikoje.

-Anadai ameona ndugu zake kibao ambao wameolewa na wazungu wanainjoi maisha kwa kuwa hakuna stree kwa maisha yao

-Anadai wazungu wengi wapo on time(wanaenda na muda)tofauti wa wanaume wengi wa kibongo hawana hata malengo kiufupi nikamuuliza lakini mbona wapo wanaume wa kibongo ambao wana real love akasema asilimia ndogo sana. Wengi wao ni wababaishaji na hawana future au hawana mbele au nyuma.

Haya sasa wanaume sikieni lawama hizo kutoka kwa baadhi ya mabinti wa kiafrika ambao wanashoboka na utandawazi.

Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Picha: Mtunisi Awachana "LIVE" Diamond na Wema Sepetu

0
0
Msanii mkongwe wa filamu nchini, nice mohamed aka mtunisi amewapa makavu live mastaa wenzie ,diamond pamoja na hawara yake wema sepetu aka mama ubaya ,kwa kitendo alichokifanya staa huyo wa filamu(wema) kufutarisha nyumbani kwake na kumkaribisha harawa yake(Diamond) pamoja na mama mkwe wake(haijulikani mkwewe kwa nani na kwa ndoa ipi) bi sanura kitendo ambacho mtunisi amekiona ni kinyume na dini yao hiyo ya kiislamu.
Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Mange Asutwa live na Mtandao wa Trebellawigs Baada ya kuiba Kazi zao na Kuzifanya Zake

0
0
Bi dada huyu amekuwa akiposti bidhaa zake kwenye account ya Insta inayoitwa @hollywoodshopaholics  anazodai anaziproduce yeye na kuziwekea price tag za madolare ya maana. Kumbe bwana sio bidhaa zake, bidhaa hizo ni za trebellawigs.

Amekamatwa live na ameshtakiwa insta na product alizoiba zimeondolewa na insta admn. Anachofanya ni kuchukua picha ya product na kufuta trademark ya Bela na kuweka hiyo ya hollywood sijui holic kwenye bidhaa za watu.

Jisomee Hapo chini:

Baada ya Kichambo hicho account hiyo ya Hollywoodshopaholics Ambayo inamilikiwa na Mange ilijitetea hivi kwa wateja wake:

Quote of The Day: “The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Irene Uwoya Azua Timbwili Kwa Mume wa Mtu

0
0

NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amesababisha tena ! Safari hii amekinukisha nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake ( jina tunalo) kufuatia jamaa huyo kufunga ndoa na mwanamke mwingine na kumfanya Uwoya kuendelea kuwa ‘ nyumba ndogo ’ . Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilichukua nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo, Sinza- Mori jijini Dar es Salaam.

MCHEZO ULIVYOKUWA

Chanzo kilidai kwamba , siku ya tukio , Uwoya akiwa na baadhi ya mastaa wenzake ( hawakutajwa) kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu mjini Bagamoyo , Pwani, alipokea simu iliyomnyetishia kuwa , mpenzi wake huyo amefunga ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza , kwa hiyo yeye aliye tu !

UWOYA ACHANGANYIKIWA

“Uwoya alipopata salamu hizo kwa njia ya simu alichanganyikiwa ! Alianza kusema maneno ya kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio . Mbaya zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema ndoa hiyo ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye maandalizi . “Akasema anaondoka kambini kumfuata jamaa yake na kwamba atamtambua kwani nia yake ilikuwa kwenda nyumbani kwake kumfanyia fujo na huyo mke mpya , ” kilisema chanzo hicho cha uhakika . Nyumba anayodaiwa kufanya fujo

AANZIA DUKANI

Chanzo kilizidi kudai kwamba, licha ya wasanii wenzake kumsihi asichukue hatua hiyo anaweza kuishia polisi , Uwoya hakukubali, aliondoka kwa hasira na breki yake ya kwanza ilikuwa kwenye duka kubwa la jamaa huyo lililopo Mikocheni , Dar ambapo alifanya fujo. “Kule alipogundua huyo mwanaume wake hayupo ndiyo akaondoka hadi nyumbani kwake, Sinza ambako aliendeleza fujo zake kwa kutukana na kutishia mambo mengi, ” chanzo kilisema .

HASIRA PEMBENI

Kwa mujibu wa chanzo, ni dhahiri kuwa , Uwoya aliondoka eneo hilo baada ya kuanza ‘ kujaza nzi ’ ( watu kuwa wengi ) ambapo aliondoka mdogomdogo na kama hana hasira utadhani si yeye aliyekuwa akichafua hali ya hewa .

MATEGEMEO YAKE

Habari za ndani ziliendelea kudai kuwa , Irene alishikwa na hasira za jamaa huyo kuoa kwa vile alikuwa akiamini zali hilo lingetua kwake baada ya ndoa yake na msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘ Katauti’ kwenda halijojo! “Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu ,” kilisema chanzo.

ALICHOAMINI

Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘ nyumba ndogo ’ jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo .

UWOYA HUYU HAPA

Baada ya gazeti hili kunyetishiwa filamu nzima, lilimsaka staa huyo na kubahatika kukutana naye maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba, alishaachana na mwanaume huyo. “Ilitokea, lakini nilishaachana naye . Unajua ishu si kwamba angenioa mimi , ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana , ” alisema Uwoya .

AMWANGA CHOZI

Katika hali isiyotarajiwa , msanii huyo alianza kumwaga chozi bila kusema sababu hata pale alipoulizwa kama chozi hilo lilitokana na kukumbuka tukio la jamaa yake kufunga ndoa kwa siri au la! Uwoya: “We niache tu , nina mambo mengi sana yanayoniliza mimi .” Kwa upande wake mwanaume huyo alipopatikana kwa njia ya simu na kueleza ishu nzima alijibu kwa kifupi: “Haiwahusu .” Kisha akakata simu.
GPL

Quote of The Day:
“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Penny:Jamani Msinishangae Mimi Kufunga Ramadhani Wakati ni Mkristo

0
0
MMTANGAZAJI wa Redio  EFM aliyewahi kuanguka kimahaba na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amewafungukia wanaomshangaa kuhusu kufunga mwezi wa Ramadhani na kuwataka watu hao wasimshangae kuhusiana na jambo hilo.

Akifafanua ishu hiyo mbele ya mwandishi wetu, staa huyo alisema kuwa amezaliwa katika familia yenye dini mbili japokuwa yeye ni Mkristo, lakini hufunga Ramadhani na Kwaresma sambamba na kusheherekea sikukuu zote kwa kuwa familia yao huamini Mungu ni mmoja

Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Baby Madaha'Naomba Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Uishe Maana sina Namna ya Kuingiza Fedha'

0
0
Na Rhoda Josiah

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umembana kiuchumi kwani kumbi nyingi za starehe zimefungwa kwa hiyo anashindwa kupata pesa.

Akipiga stori mbili tatu baada ya kuvutiwa waya na mwandishi wa gazeti hili, Baby Madaha alisema kwa upande wake michongo yake mingi ya hela anaipata kupitia kumbi za starehe hivyo kwa sasa fedha haingii kabisa.

“Naomba Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uishe maana mtonyo umekata halafu sina namna ya kuingiza fedha zaidi ya muziki hivyo hali si hali kwa sasa jamani,” alisema Baby.

Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Habari Njema Katika vita Dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi

0
0
Kuna uwezekano kuwa janga la ukimwi huenda likadhibitiwa ifikapo mwaka 2030, kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi.
Ripoti hiyo imesema kuwa idadi ya visa vya maambukizi mapya na vifo kutokana na HIV, vimeendelea kushuka.

Hata hivyo, shirika hilo linataka juhudi zaidi za kimataifa kufanywa kwani za sasa hazitoshi
Na shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.
Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 35 wanaishi na virusi vya HIV.
Ripoti hiyo ilionyesha visa vipya vya maambukizi milioni 2.1 vilitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.
Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.
Afrika Kusini na Ethiopia zimepiga hatua katika kupunguza vifo vya wagonjwa wa HIV.

Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Warembo: Kope za Bandia Zinaweza kusababisha Upofu

0
0
Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tunaouona kwa baadhi ya wasichana na wanawake ambao kwa hakika unaleta hamasa ya kuangalia.

Hata hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza kutolewa ushahidi kwa sasa.

Moja kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake wakikuangalia hasa mtoto wa kiume. Lakini hatari inayotokana na urembo huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi.

Wataalam wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji.

Gundi hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea kwenye mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa ‘kuona’. Endapo mtumiaji ataendelea kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta anakuwa na tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake ya baadae.

Hata hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda vinatumia vifaa vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika. Ukwepaji wa gharama ama kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza mrembo kwenye hatari zaidi.

Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.

Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Baada ya Kombe la Dunia FIFA Yatoa Orodha ya Viwango vya Ubora kwa Mwezi JULY

0
0
Shirikisho la soka duniani FIFA, hii leo limetangaza orodha ya viwango vya ubora wa soka, ikiwa ni juma moja baada ya kukamilika kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 huko nchini Brazil.

Orodha hiyo ambayo hutolewa kila mwezi, imezingatia matokeo ya michezo ya fainali za kombe la dunia, ambapo mataifa makubwa kama Uingereza yameonekana kutupwa mbali.

Wenyeji wa fainali za kombe la dunia Brazil nao wameonekana kuanguka kwa kiasi kikubwa, ili hali waliokuwa mabingwa wa fainali hizo mwaka 2010 Hispania wameporomoka kwa kasi ya ajabu wakitokea nafasi ya kwanza.

Mabingwa wapya wa fainali za kombe la dunia, Ujerumani wamekalia kiti cha orodha hiyo, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa walipokuwa nchini Brazil, ambapo walicheza michezo saba pasina kufungwa mchezo wowote.

Ifuatayo ni orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani kwa mwezi July mwaka 2014.

1. Ujerumani (+1)

2. Argentina (+3)

3. Uholanzi (+12)

4. Colombia (+4)

5. Ubelgiji (+6)

6. Uruguay (+1)

7. Brazil (-4)

8. Spain (-7)

9. Uswisi (-3)

10. Ufaransa (+7)

11. Ureno (-7)            

12. Chile (+2)            

13. Ugiriki  (+1)        

14. Italia (-5)              

15. Marekani  (-2)                

16. Costa Rica (+12)            

17. Croatia (+1)        

18. Mexico (+2)        

19. Bosnia na Herzegovina (+2)            

20. Uingereza (-10)    



AFRIKA MASHARIKI NA KATI

87. Uganda (-1)

95. Kenya (+13)

96. DRC (-12)

106. Tanzania (+7)

109. Rwanda (+7)

126. Burundi (+2)

Orodha kamili http://www.fifa.com/worldranking/rankingtable/

Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Post ya Hasheem Thabeet Kuhusu Wanaombeza Nakudhani Amesahau Lugha ya Kiswahili.

0
0
Hasheem Thabeet ame-post kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusu baadhi ya watu wanaodhani kwamba amesahau lugha ya kiswahili. Sasa hiki ndicho alichoandika Hasheem kwenye ukurasa wake wa facebook.
Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Maskini Happiness Magese Atumia Mipira Kupata Haja ndogo Baada ya Kibofu Kuwa na Hitilafu

0
0
Happiness Magese anasihi wanawake kucheki afya zao mara kwa mara wasije wakakutwa na tatizo kama lake la ugumba ambalo limeharibu na kibofu chake na kupelekea hata kushindwa kukojoa kwa njia ya kawaida na badala yake anatumia mipira, ni vema kuchek afya mara kwa mara.
Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

MARTIN KADINDA Afunguka Kuhusu Wanaume Wanaommemzea Mate Wakidhani ni SHOGA

0
0
Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda amesema kuwa amekuwa akikutana na changamoto kutoka kwa wanaume wengi wanaodhani kuwa yeye ni shoga na kufikia hatua ya kumtumia ujumbe wa kumtaka kimapenzi.

Kila mtu anakuwa na maswali yake anaya-raise kutokana na anacho kifikiria katika akili yake, Watanzania tunatabia ya ku-create situation katika akili zetu halafu we want everybody to accept.Kwamba mtu tu anaamka asubuhi may be ana matamanio na wewe anaanza ku-raise hilo swali aone jibu litakuwa ni nini. Wapo wengi (wananitamani) wako hivyo, facebook, Instagram mtu atakutumia namba yake, hakwambii lakini unaona kabisa huyu, nakukubali sana I wish siku moja uje nyumbani kwangu au can I come to your place, mimi sitakagi hata kwenda huko najua nitajiuliza imekuaje mpaka imefikia hivi, basi nasema sawa. Kwa sababu mimi facebook nakuwa mkweli sijawahi kujibu mtu tangu 2012, I have a person huwa anazipitia, akiulizia mtu maswala modelling mpe namba ya fulani, mambo mengine binafsi usiwajibu achana nao, kwa sababu mara ya kwanza nilikuwa ninadhani I should meet these people talk to them this is not right but nikaona unapoanza kuwa unajihusisha ndipo unapojikuta unaanza kuingia bila kujua” Martin Kadinda aliambia Sporah Show.

Pia Martin amesema kuwa ana mpenzi wake ambaye hapendi kumuweka wazi ili kulinda heshima yake.

Ukishakuwa maarufu na mtu wa karibu yako atakuwa maarufu, she’s not already kwa hiyo kitu yakuingia kwenye hiyo cycle kila siku wanamuona kwenye magazeti kwenye Instagram haiko hivyo. Ndiyo maana hata nikiweka picha yake Instagram nitaweka picha yake moja kwa miezi sita, yupo hata ukitaka kumuona kwenye Instagram yangu yupo, first lady wa martin huyu, lakini cycle yake na maisha yake siyo mtu wa kukaa kwenye media nadhani ni kwa sababu ya future ya kazi atayokuja kuifanya kwaiyo anajitaidi kuwa pembeni… Mara ya kwanza alishawahi kuniuliza alipita kwenye comment za watu kwenye blog fulani akasoma, akaniambia najua hii ni Watanzania walivyo, as long nakutambua mwanaume wangu ni mtu wa namna gani I don’t care about these people” Alimaliza Martin
Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Alikiba Asema Hana Chuki na Diamond, Ampongeza Lakini…’Sifikirii Kuongea Naye’

0
0

Wiki Ijayo Alikiba atakuwa mgeni katika kipindi cha runinga cha The Sporah show. Katika promo ya mahojiano yake na Sporah inayoendelea kurushwa kupitia Clouds TV, Alikiba amemzungumzia Diamond Platnumz ambaye huwa inasemekana wana-beef.

katika promo hiyo Sporah amemuuliza Alikiba kama Diamond ndiye amechukua nafasi yake kwenye muziki kwa kipindi alichokaa kimya, na majibu yake yanaongeza hamu ya kutokosa kukiangalia kipindi hicho.

Alikiba amejibu kuwa Diamond hajachukua nafasi yake, na kusindikiza jibu lake na mfano wa (nafasi yake) ni sawa na kiti kilichopata vumbi (kwa kutokaliwa siku nyingi) hivyo muda wowote akiamua kurudi anaweza kuamua kukifuta na kukikalia tena. Pia aliongeza kuwa Diamond amekaa kwenye kiti tofauti na yeye, lakini ni yuko ‘back seat’.

Kupitia 255 ya kipindi cha XXL pia leo Alikiba aliulizwa swali kuhusu yukoje sasa hivi na Diamond , haya ndio majibu ya hit maker wa ‘Cinderella’.

Mimi niko okay sana sema sifikirii kuongea naye tu basi lakini niko very okay yaani. Yaani sijawahi kufikiria si unajua kuwa na mtu okay ni kuzungumza na kuwa karibu unajua hivyo vitu, yaani sijawahi kufikiria hata hivyo. Mi niko okay na sina chuki na sana sana nampongeza lakini sina chuki, simaind yaani niko veeery okay”.

Quote of The Day:

“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

Kesi ya Mbasha imesomwa Tena Leo na Hiki Ndicho Kilichoamuliwa na Mahakama

0
0
Mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola Mbasha,Mr.Emanuel Mbasha leo amepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili yanayo mkabili ya ubakaji.
Katika kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Wilbert Luago,amelazimika kuhairisha kesi hiyo kwa muda wa nusu saa kwa hoja aliyoitoa Mbasha kwamba ana wakili wa kumtetea lakini alishindwa kufika kutokana na matatizo ya usafiri.
Kauli hiyo ya Mbasha ilimfanya Hakimu Luago kuhoji kama kweli alikuwa na nia ya kuwa na wakili au ana nia ya kuweka wakili kwani tangu kesi hiyo imeanza Mbasha hajapeleka wakili yoyote.
Mara baada ya nusu saa kupita Wakili wa mshitakiwa alituma muakilishi wake kuwakilisha barua za dharula ambazo zilionesha kuwa yupo safarini mkoani Arusha na kuomba kesi hiyo kuahirishwa.
Emanuel Mbasha ana kabiliwa na kesi mbili za ubakaji ambapo inadaiwa alitenda makosa hayo maeneo ya Tabata katika nyakati mbili tofauti,Mbasha alisindikizwa mahakamani na ndugu zake huku Mkewe Flora Mbasha kutoonekana Mahakamani na badala yake alionekana mdogo wake Flora ambaye ni shemeji yake Emanuel Mbasha.
Kesi hii imehairishwa mpaka July 23 mwaka huu.

Quote of The Day:


“The sky has never been the limit. We are our own limits. It’s then about breaking our personal limits and outgrowing ourselves to live our best lives.”

EXCLUSIVE!! Irene Uwoya Afunguka Juu ya Tuhuma za Kufanya Fujo Nyumbani Kwa Mume wa Mtu!

0
0
NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya amefunguka juu ya tuhuma za kufanya fujo nyumbani kwa mume wa mtu zilizoripotiwa na mitandao mbalimbali ya habari nchini hivi karibuni.

Akizungumza exclusively nasi, Irene amesema kuwa haelewi hizo tuhuma zimetoka wapi na wala hajui aanzie wapi kuzijibu maana siyo yote yaliyoripotiwa ni kweli.

Tuhuma hizo zilidai kuwa, mwanadada huyo mrembo alienda kuleta timbwili nyumbani kwa mume wa mtu huyo baada ya kusikia kuwa jamaa huyoa ameamua kuoa na kumoiga chini Irene aliyekuwa akitoka naye kipindi cha nyuma.



 “Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu,” Habari hizo ziliriripoti.

Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘nyumba ndogo’ jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo.

Akifafanua tukio hilo Zaidi uwoya alisema.

“Ilitokea, lakini nilishaachana naye. Unajua ishu si kwamba angenioa mimi, ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana,” alisema Uwoya.

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Ndege Nyingine ya Malaysia Yaanguka Ikiwa na Watu 295

0
0
Ndege ya Malaysia, Boeing 777 iliyokuwa inatoka Amsterdam kwenda Kula Lumpur imeanguka Mashariki mwa Ukraine karibu kabisa na mpaka wa Russia, leo, July 18.

Kwa mujibu wa CNN, waziri wa Malaysia anaehusika na mauala ya Usafirishaji amesema kuwa abiria 280 na wafanyakazi 15 waliokuwa kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha.

Tweet ya Malaysia Airlines imeeleza kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano baada ya kutoka Amsterdam.

Kumekuwa na taarifa za awali kuwa ndege hiyo ilipigwa na na Ukraine, taarifa ambazo zimekanushwa na raisi wa Ukraine.

Rais wa Malaysia ameeleza kupitia twitter jinsi alivyosikitishwa na tukio hilo na kudai kuwa wataanza uchunguzi wa tukio hilo haraka iwezekanavyo kufahamu chanzo.

Tukio hili linatokea wakati ambapo bado ndege ya nchi hiyo, Flight 370 iliyopotea March 8 Mwaka huu bado haijapatikana.

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Mange Vs Chagga Bibie:Hili ni Beef Baya Sana Mange Atumiwa Picha za Utupu za Chagga Bibbie na Kuziweka Insta

0
0
Haya jana yeye ndo alikuwa na raha na kicheko akishangilia anguko langu akajua kanimaliza nitarudi
upareni kulima…… Wapenzi hizi picha sijatumiwa na mwanamke, hizi picha nimetumiwa na mwanaume, imagine mwanaume ambae hatujazoeana tunafahamian tua, all he said to me was aliumia sana jana the way Stella tried to kill my business and told me to do as i pleased with the photos. I have almost 10 photos with me. Sasa naomba Stella anijibu huko Instagram nizirushe hizi picha au nisirushe? Yani hizo mnaazo ona hapo zimemstiri,naomba anipe jibu na kama anataka nirushe pia aniambie.

Yani in short I WANT HER TO DARE ME, YANI ANIAMBIE ‘MANGE I DARE YOU’ THATS ALL I NEED. Hili liwe fundisho kwa mbwa wote mnaonifatilia issue zangu, usidhani just because you hate then everybody else does, kuna wanaonipenda na hawapendi kuona mnaniharibia issue zangu bila sababu.
Hiyo mitit yake iliyolala ndo kabla ya plastic surgery ndo ile mititi ambayo Prezzo alilalamika imelala demu akapanick.Yani naandika hii huku natetemeka maana nna picha zinaanyesha nyapu kama ilivyo na hayo matatoo yake kama yalivyo na hiko choo kama kilivyo yani huulizi. Na wewe Linda achana na mimi nakuonya kuna siku ntakuja kutumiwa picha zako ulivyokuwa unatolewa mizigo (madawa) matakoni. Mnatafuta attention wenyewe, hivi mkikaa huko mkashona manguo yenu ya haloween mkanisahau mtakufa?
Source:BongoClan tz

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Mchungaji Mtikila Amfunguliwa Kesi Askofu Mokiwa Kwa Kumshika Makalio

0
0
Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk. Valentino Mokiwa.
Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.
Mtikila alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholous, usiku wa saa 03:00.
Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti. Baadae Askofu Mokiwa nae alisimama na kuungana na wenzie kuwakagua kina Mtikila baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.
Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.
Wakili wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa, "Mlalamikiwa alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna aliyebisha."
Alisema kisha akaendelea "Mshtakiwa (Mokiwa) alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya mlalamikaji".
Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.
Madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.
Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Agness Mchome.

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Siyo Bure Diamond Platnumz Kwa Hili Utakuwa Umelaaniwa, Huwezi Kumfanyia Baba Yako Hivyo

0
0
Stori: Erick Evarist na Gladness Mallya
Oooh! Nooh! Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.


Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.

BOFYA HAPA
“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo? 
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.

“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”

MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.

“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.

UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.

Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.

“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.

MATANUZI YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.

TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.

“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:

“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana.

“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”

BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.

“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.

“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.

DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.

MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao kifedha unapaswa kuendana na baraka za wazazi wa pande zote mbili. Vitabu vya Mungu vinatufundisha kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa duniani hivyo hata kama kuna kosa amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu. Hatutakiwi kumkosoa!

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Nape Kudhihaki Wanasiasa Wenzake kwa Kutumia Uzee Wao Sio Maadili ya Kiafrika Jitazame Upya!

0
0

Kila mara nyingi sasa nimemsikia Nape Nnauye katibu wa propaganda, itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi akidhihaki wanasiasa wa upinzani kwa uzee wao. Malengo yake ukiyachambua yamelenga kuwaaminisha wafuasi wa chama chake kwamba uzee dalili ya udhaifu na si lolote ktk utumishi wa kisiasa... Amediriki kuwaita mpaka majina kama Babu, wazee wanazeeka vibaya nk. Hivi ndani ya ccm, wazee wanajisikiaje kuona uzee ukitumika kama silibo na mbinu ya kueneza propaganda? Je, taifa lianze kuwaita wazee kama Mangula,salimu,kingunge nk majina anayotaka Nape. Sasa vijana wa ccm tuanze kuwaita wazee wetu majina kama, Babu mkapa,babu Mangula, babu wasira, babu Lowasa, babu Sitta, Babu kikwete, Babu Karume, Babu msuya nk?..... Jamani hata kama ni propaganda ya kuwabomoa wapinzani tusitumie utu wa binadamu kisiasa....mimi ninao wazee ktk uko nawaheshimu,nawaheshimu wazee wote bila kujali itikadi....wapinzani tupingane nao kwa hoja sio utu wao. Nasikitika Uvccm nao tumeambukizwa upuuzi huu! Nani kakwambia kutukana uzee ni turufu na ngazi ya kupandia kisiasa? Hio laaana! Nape kama huna mzee kwenu tafadhali sana wenye kujua thamani ya uzee utuache!....MWL NYERERE alithamini wazee kamwe hakuwahi kudhihaki uzee....uzee sio ugonjwa na ujana sio utakatifu..

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images