Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Awaonya Wanachama CCM

$
0
0
Rais Magufuli Awaonya Wanachama CCM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Dk John Magufuli ameendelea kusimamia azma yake ya kumaliza rushwa ndani ya chama hicho.

Dk Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano amesema CCM haitasita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo itabainika rushwa imetumika.

Akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo Jumatatu Desemba 18,2017 Rais Magufuli amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa.

Amewataka wajumbe wa mkutano kuchagua watu waaminifu na wenye mapenzi ya dhati na CCM.

“Msichague watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,” amesema.

Rais Magufuli amewataka wanachama wa CCM kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho ulioanza Aprili, 2017.

“Vunjeni makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza makundi,” amesema.

Irene Uwoya Afunguka Anavyopambana na Changamoto Anazokumbana Nazo

$
0
0
Irene Uwoya Afunguka Anavyopambana na Changamoto Anazokumbana Nazo
Ikiwa leo ni birth day ya Irene Uwoya, Muigizaji huyo amefunguka baadhi ya vile ambavyo anavipitia katika maisha yake.Irene amesema licha ya yote anayopitia bado yeye ni mwanamke jasiri kwa namna ambavyo amekuwa akikabiliana na changamoto zake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

I am a strong woman…Everything that’s hit me in life I’ve dealt with on my own. I’ve cried my self to sleep…Picked my self backup and wiped my own tears.I have grown from things meant to break me.I get stronger by the day And i have God to thank for that.Happy birthday to me…🙏🏽🙏🏽🙏🏽🥂 make-up

November 14 mwaka huu Irene alifiwa na aliyekuwa mume wake, Hamad Ndikumana ambaye alikuwa akicheza mpira nchini kwao, Rwanda.

Bushoke Ajipanga Kufanya Ngoma na Papii Kocha

$
0
0
Bushoke Ajipanga Kufanya Ngoma na Papii Kocha
Baada ya muimbaji, Papii Kocha kurudi uraiani na kukutana na rafiki yake Bushoke, wawili hao wanajipanga kuingia studio kwaajili ya kuandaa kazi mpya za muziki.

Bushoke amesema amefurahi sana rafiki yake huyo kuwa huru huku akiahidi kuanza kufanya mchakato wa kumrudisha kwenye game rasmi.

“Nafikiria kufanya naye kolabo,” Bushoke aliliambia Gazeti la Mwanaspoti. “Mungu akijalia ziwe nyingi,  nikifanya shoo napenda ashiriki na vitu vingi napenda nimsaidie ila ziwezi kuviweka wazi,”

Papii Kocha pamoja na baba yake waliachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Pombe Magufuli.

Yanga Waja Juu Wataka Mzee Akilimali Afutiwe Uanachama

$
0
0
Wanachama Yanga Waja Juu Wataka Mzee Akilimali  Atimuliwe
KLABU ya Yanga imeonyesha hali ya kuchoshwa na tabia ya Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali za kupinga mabadiliko ya klabu hiyo hivyo imewalazimu kutoa mapendekezo ya kumfuta uanachama.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alitangaza rasmi nia ya klabu hiyo kuanza mchakato wa kwenda katika mfumo wa hisa jambo ambalo baadae Akilimali alisikika akipinga mfumo huo na kuomba Yanga wamtake radhi.


Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya Yanga Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Uhuru, Kaisi Edwin alisema, wamekutana wenyeviti wote wa matawi na kukubaliana kuandika barua kwa uongozi huo ili wamfutie uanachama mzee Akilimali.

Ni kwa Nini Suti Bado Inapendwa Sana?

$
0
0
Ni kwa Nini Suti Bado Inapendwa Sana?
Katika mji wa London kuna duka la Henry Poole & Co lililo katika mtaa maarufu kwa suti za wanaume.

Kampuni hiyo ni tangu mwaka 1806. Miaka iliyofuatia mitido ya suti ya Uingereza ilipata umaarufu duniani.

Kufuatia bei ya suti ya Henry Poole & Co kuwa takriban dola 5,300, itakuwa rahisi kufikiria kuwa suti ni vazi la watu wa hadhi ya juu lakini meneja wa kampuni hiyo Simon Cundey hakubaliani na hilo.

Wanaume bado uhisi vizuri zaidi na wakiwa wametulia wakati wamevaa suti, na ufurahi pia wakiwa wamevaa vazi linalowatoshea vizuri.

Kwa Picha: Mitindo ya mavazi katika tuzo za Emmy
Watu wengi katika ulimwengu wa sasa wanashughuli nyingi na hawana muda mwingi wa kuingia duka hili au lile kujaribu kupata nguo ambayo inaweza kuwatoshea vuzuri.

Suti ni ghali lakini kama unaweza kuangaliwa gharama yake kwa miaka 10 ambao ni muda inaweza kudumu, basi hiyo inaweza kuwa sababu muafaka ya bei yake.

Suti imekuwepo tangu karne ya 17 na imekuwa ya mshono mmoja tangu mwanzo wa karne ya 20. Kuonekana kwake pia kumekuwa kwa nia moja kote duniani wakiwemo kwa watu wenye hadhi ya juu na wanaume wa kawaida, na hatimaye kwa wanawake ambao na wameanza kuvaa suti za aina tofauti.

Mkurugenzi wa taasisi wa mitindo mjini New York Valeria Steel, anaamini kuwa suti imedumisha nguvu zake.

Wanawake watakiwa kuvalia nadhifu Uganda
Kwa mtu ambaye anafahamu mawili au matatu kuhusu kuchimbuka kwa suti, ni mchora mitindo Sir Paul Smith ambaye amewavisha watu maaruuf kama Pink Floyd na David Bowie.

"Ninavaa situ kila siku, hata wikendi, anasema Smith. "Nimegundua kuwa zinanifanyia kazi nzuri sana, anasema akiwa kwenye studio

Martin Pel ambaye ni mwanamitindo huko Royal Pavilion eneo la Brighton anaitaja suti kuwa kitu cha kusawazisha. Suti inasabisha mtu kutofikiria hali ya mtu au anatokea wapi.

Akiguzia kazi ya Anne Hollander, Valerie Steele anasema kuwa moja ya sabubu ya suti kuwa maarufu kwa kupindi kirefu ni kuwa kwa ghafla imefanya mwili kuhisi shwari.

Wakati wa vita miaka arobiani wanawake walichukua nyadhifa za wanaume na kuanza kuvaa suti pia.

Wanaume walikuwa vitani ndipo wanawake wakapata fursa ya kuvaa suti, lakini hawakuvaa suruali bali sketi.

"Sidhani kama suti inaweza kutoweka anasema Martin Pel. Nafikiri kuwa ni nguo muhimu sana. Hata kama tutaivaa kila siku au wakati wa shughuli maalum suti haitatoweka.

Vile Paul Smith anasema: unaweza kwa na miaka 13 au 100 au mtoto wa shule lakini suti ni vazi bora

Takukuru Yakanusha Kuachana na Ushahidi wa Nassari, Lema

$
0
0
Takukuru Yakanusha Kuachana na Ushahidi wa Nassari, Lema
Mkurugenzi  wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru )  , Valentino Mlowola  amekanusha  kuwa wametupilia mbali ushahidi wa Mbunge wa Arumetu Mashariki, Joshua Nassari  na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema juu ya tuhuma za kununuliwa kwa baadhi ya madiwani katika Chama chao na kuhamia Chama cha Mapinduzi  (CCM ).

Akiongea na Bongo5 leo, Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa Taasisi hiyo ina mamlaka sheria ya kuchunguza tuhuma zote zinazohusiana na rushwa nchini.

“Taasisi hii kisheria ina mamlaka sheria ya kuchunguza tuhuma zote zinazohusiana na rushwa nchini na jukumu hilo linaendelea kufanywa kwa kufuata taratibu za kisheria kwahiyo uchunguzi wa tuhuma zote za rushwa unaendelea mpaka tunapo jidhihirisha kuwa kosa limefanyika au halijafanyika”

“Hakuna kitu kama hicho, uchunguzi madamu kama unahusu tuhuma za rushwa lazima unaendelea tu suala la kwamba tunatupilia mbali tumetupilia mbali nini utaratibu tukishamaliza uchunguzi tunapeleka jalada kwa Mwanasheria mkuu wa serikali ana tathimini ule ushahidi kutoka hapo anapendekeza au anachukua hatua anazopaswa kuchukua.”

Awali kulikuwa na taarifa zikienea kuwa, Taasisi hiyo imefuta jalada liliwasilishwa na wabunge hao kwa kile kilichodaiwa kuwa wamevuruga uchunguzi na kuweka kila kitu hadharani wakati bado taasisi hiyo ikiendelea na uchunguzi.

Rais Magufuli Amshukuru Kikwete

$
0
0
Rais Magufuli Amshukuru Kikwete
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoangalia rushwa wala urafiki pindi alipomchagua kugombea urais na kutaka wanachama wake kuchagua wajumbe wa Halmashauri Kuu wenye mapenzi ya dhati na chama.


Dkt. Magufuli ameonya hayo wakati  akifungua mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma leo ambapo  amesema chama hicho kimedhamiria kupambana na rushwa na kwamba kama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete angeangalia hayo basi yeye asingepata nafasi alonayo

“Msichague watu kwa urafiki au kwa sababu ya rushwa, binafsi napenda nimshukuru mzee Kikwete (Jakaya) yeye hakuangalia rushwa nadhani angefanya hivyo huenda mimi nisingepita,” amesema.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka wanachama wa chama chake kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa chaguzi wa ndani wa chama hicho.

“Vunjeni makundi chaguzi zimekiwasha tujikite kwenye kukiimarisha chama. CCM haitamvumilia mtu mwenye kuendeleza makundi,” amesema

Pamoja na hayo Dkt. Magufuli ameweka wazi hatosita kutengua matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu iwapo itabainika rushwa imetumika.

Takukuru Yakanusha Kumshikilia Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba

$
0
0
Takukuru Yakanusha Kumshikilia Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU imekanusha taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa wanamshikilia aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Nehemia Mchechu.


Akiongea na East Africa Television leo, Afisa habari wa TAKUKURU Musa Misalaba amesema wanashangaa taarifa hizo zimetoka wapi na wao kama taasisi hawamshikilii Mkurugenzi huyo aliyesimamishwa na Waziri Lukuvi wiki iliyopita.

“Hizo taarifa sijui zimetoka wapi, lakini sisi hatuna huyo mtu, hatujamkamata saa tunashindwa kuelewa watu wanazusha kwa lengo gani”, amesema Misalaba.



Aidha msemaji huyo ameongeza kuwa wao kama taasisi hawajapokea agizo lolote la kumkamata na kumfanyia uchunguzi ndugu Nehemia Mchechu hivyo hawana sababu ya kumkamata.

Nehemia alisimamishwa kazi na Waziiri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi siku ya Jumamosi wiki iliyopita. Jana jioni kwenye mitandao zilisambaa taarifa za kukamatwa kwake ambavyo leo TAKUKURU imekanusha.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0

HARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670  

Sala ya Ukiwa Unamsikiliza Mpenzi Wako Akikudanganya Wakati Ukweli Unaujua

$
0
0

“Mungu baba uliyetuweka hapa duniani na kutupa kitabu cha kutuongoza katika njia iliyonyooka naomba unipe uvumilivu kama uliompa Nuh wakati anawaambia watu wapande meli kuna mafuriko yanakuja wakamcheka nisije mkata huyu mtu kofi lililonyooka likampandisha mashua na mafuriko yakamjia ndotoni akiwa kazimia, naomba unipe moyo wa huruma kama wa Adam kumsamehe Hawa baada ya kumlisha tunda nisije kumlisha ngumi akatembea kwenye garden nyuma ya nyumba yetu uchi, naomba unipe uwezo wa nabii Issa bin Mariam kunyanyua mikono juu na kushuka na samaki na mikate kwakua uongo wa huyu mtu umenipa njaa na ntakuja nimpasue sasaivi kama Samson alivyodondosha lijumba. Kwa hayo machache naomba usinipe nguvu ya kumuangalia maana kwa hii simu nimeshika ntamzabua kama Daud alivyomteremsha Goliath, AMINNNNNN..
.
By @idrissultan

Mange, Shika, Wema Mtaji wa Watawala -Niki wa Pili

$
0
0
Mange, Shika, Wema Mtaji wa Watawala -Niki wa Pili
Niki wa Pili amefunguka na kusema uwepo wa taarifa nyingi za matukio ya watu maarufu ambazo zinabebwa na kupigiwa makelele kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya jamii ni mtaji mkubwa kwa watawala kuwasaulisha watu juu ya matatizo ya nchi.

Niki wa Pili amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema kuwa matukio ya Weusi, Wema, Mange Kimambi na kina Dr. Shika ndivyo vitu vinavyowafanya Watanzania kusahau kuhusu matatizo ya ajira nchini, umasikini na ukosefu wa viongozi kwani badala ya wananchi kuanza kuhangaika na matatizo hayo muda wote wanakuwa wakihangaika na matukio ya watu maarufu.

"Sasa hivi ni rahisi kuwasahaulisha watu juu ya ukosefu wa ajira, umaskini, ukosefu wa viongozi nakadhalika, kwa kuwa Media, Social Media kila siku inatupatia utajiri wa taarifa nyingi tukio baada ya tukio. Weusi, Wema, Mange, Dr. Shika, Hamorapa, Meli ya wa china, Trump, Nyimbo mpya, Videos, Karuchi. Utajiri huu wa taarifa na matukio ni jambo jema sana kwa watawala duniani. Na wapigaji wengine ambao ni wananchi tuko bize na taarifa na matukio na bila kujuwa tunakuwa tuna kubaliana na hali ilivyo hakuna pressure wala muda wa kujadili au kupigani ajira, umaskini, Demokrasia, elimu nakadhalika" alindika Niki wa Pili

Mbali na hilo Niki wa Pili amesema kuwa maendeleo ya Teknolojia ni mazuri ila yanaweza kuja kwa njia mbili hasi na chanya.

Kinana Apewa Shavu Hili na Rais Magufuli

$
0
0
Kinana Apewa Shavu Hili na Rais Magufuli
Katibu mkuu wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana leo ameteuliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais John Pombe Magufuli  kuendelea kuwa katika nafasi yake kwa kipindi kingine.


Akiongea katika mkutano wa 9 wa Chama hicho unaoendelea mkoani Dodoma amemshukuru kwa kazi yake nzuri  kwa muda wote ambao amekuwa  katika nafasi hiyo huku akiweka wazi kuwa ni lazima aendelee kufanya nay kazi kwasababu ameridhishwa na utendaji wake wa kazi.

''Namshukuru ndugu Kinana kwa msaada wake mkubwa alionipa kwa kipindi chote hicho nafikiri  anafaa kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi kingine,'' amesema Magufuli. Kauli ya Rais Magufuli inaondoa tetesi zote zilizokuwa zinadai kuwa Kinana ameandika barua ya kuomba kujiudhuru katika nafasi yake kwa kilichodaiwa kuwa haridhishwi na utendaji wa Mwenyekiti wake Rais Magufuli.

Baada ya kupata nafasi  hiyo Abdulrahman Kinana amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini pamoja na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kukijenga chama hicho pamoja na nchi  kwa ujumla.

Kinana aliwahi kuwa mtumishi wa Jeshi la Tanzania kwa miaka 20 pamoja na kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi 2006, amechaguliwa kuwa Katibu mkuu wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu 2012.

Ndoto ya Odinga Kuapishwa Bado Ipo Pale Pale Amtaka Kenyatta Aache Kumtisha

$
0
0
Ndoto ya Odinga Kuapishwa Bado Ipo Pale Pale Amtaka Kenyatta Aache Kumtisha
Kiongozi wa Muungano wa Nasa nchini Kenya, Raila Odinga amesema ataapishwa kuwa rais wa wananchi kama walivyopanga akitaka Rais Uhuru Kenyatta kuacha kumtisha.

Akizungumza alipohudhuria mkutano kujadili kuundwa kwa bunge la wananchi eneo la Pwani, Odinga amesema hakuna atakayemzuia kuapishwa.

“Nitainua Biblia. Hakuna atakayenizuia kuinua Biblia. Ni bora kusimama na ukweli na kufa kwa jambo kuliko kukosa kufanya jambo,” amesema Odinga.

Wiki iliyopita muungano wa Nasa ulitangaza utarejea katika shughuli za kubuni bunge la wananchi baada ya kuahirisha mipango ya kumuapisha Odinga.

Odinga jana alizungumzia suala hilo kwa mara ya kwanza na kutaka Rais Kenyatta kutotoa vitisho kuhusu mipango yake ya kuapishwa.

Amesema hatatishwa na yeyote na kuwa Kenya ni kubwa kuliko yeyote. “Hakuna anayeweza kuja na kuwatisha Wakenya,” amesema.

Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa katika kaunti ya Kilifi, ofisa mkuu mtendaji wa ODM, Oduor Ongwen amesema ratiba ya kumuapisha Odinga katika mkutano wa kitaifa imekamilika.

Hata hivyo, hakutoa tarehe ambayo Odinga ataapishwa. “Tutamuapisha wapende wasipende. Hatutafanya shughuli hiyo kama mzaha, itakuwa katika kongamano la kitaifa na ataanza kutawala mara moja,” amesema Ongwen.

Mkapa Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti Ili Kuongoza Uchaguzi

$
0
0
Mkapa Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti Ili Kuongoza Uchaguzi
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameteuliwa muda huu mjini Dodoma kuwa mwenyekiti wa muda wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuongoza uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Hatua hiyo inatokana na Rais John Magufuli kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho tawala, ili kupisha taratibu za uchaguzi wa nafasi hiyo.

CCM hufanya chaguzi zake, ikiwa ni pamoja na kumchagua mwenyekiti kila baada ya miaka mitan

Msichana Aliyevuliwa Nguo na Polisi Kenya Kulipwa Dola 40,000

$
0
0
Msichana Aliyevuliwa Nguo na Polisi Kenya Kulipwa Dola 40,000
Mahakama nchini Kenya imempa msichana wa shule dola 40,000 baada wa kuvuliwa nguo na polisi waliokuwa wakitafuta madawa ya kulevya katika kisa kilichotokea mwaka 2015.

Picha za msichana huyo zilidaiwa kuchukuliwa na polisi na kisha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mahakama ilisema kuwa haki za msicha huyo wa miaka 18 wa shule ya upili zilikiukwa.

Gazeti la Standard linasema kuwa msichana huyo alipiowa picha akiwa nusu uchi na picha hizo kufuja kwa mitandao ya kijamii.

Msichana huyo kisha akapeleka kesi mahakamani akisaidiwa na shirika moja la kupigania haki za watoto akisema kuwa picha hizo zilimuathiri ambapo alitaka alipwe dola 70,000.

Gazeti la Standard lilisema kuwa msichana huyo alikuwa miongoni mwa wanafunzi wengine 44 waliakamawa katika kituo kimoja cha biashara kaunti ya Nyeri.

Kiongozi Upinzani Amuangukia Rais Aomba Msaada wa Milioni 60

$
0
0
Kiongozi Upinzani Amuangukia Rais Aomba Msaada  wa Milioni 60
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda amepiga goti na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli aweze kukisaidia chama chake cha Ada Tadea milioni 60 ili waweze kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge unaotegemewa kufanyika mapema 2018


Shibuda ameomba hilo leo Disemba 18, 2017 akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema endapo Rais akiwasaidia milioni 20 kwa kila jimbo hivyo wataweza kushiriki uchaguzi wa marudio wa Ubunge katika majimbo matatu ambao unategemewa kufanyika Januari 13, 2018.

"Nakuomba utombee kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli atutazame tupate ruzuku vyama visivyo pata ruzuku ili tuwe sawa na wale unaowapa ruzuku lakini hawapendi kushiriki katika masuala ya uzalendo na utaifa, lakini chonde chonde nakuomba utuombee" alisema Shibuda

Baada ya maombi yake hayo Rais Magufuli alimuuliza kama yeye na chama chake atashiriki katika uchaguzi wa marudio wa wabunge ndipo hapo aliporudi na kuomba apewe milioni 20 kwa kila jimbo.

"Naomba nisaidie milioni 20 kwa kila jimbo ili niwezeshe kwenda kugombea kwa hiyo kwa majimbo matatu tusaidie chama milioni 60 kwa sababu unaowapatika ruzuku hawakwenda kushiriki" alisisitiza Shibuda.

Baadhi ya Vyama vya siasa vya upinzani nchini Tanzania kikiwepo CHADEMA, CUF, TLP, CHAUMMA pamoja na ACT Wazalendo vimejitoa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa marudio wa nafasi ya Ubunge ambao unategemewa kufanyika Januari 13, 2018 kwa kile walichodai kuwa uchaguzi wa madiwani uliofanyika karibuni haukuwa wa haki na ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na kanuni za uchaguzi.

Mtoto wa Gadafi Ajitokeza Kugombea Urais wa Libya 2018

$
0
0
Mtoto wa Gadafi Ajitokeza Kugombea Urais wa Libya 2018
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi, anatarajia kugombea urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2018.


Taarifa za Saif al-Islam kutaka kugombea nafasi hiyo ambayo baba yake alikuwa ameishikilia kwa muda wa miaka 42, ilitolewa na msemaji wa familia Basem Hashimi Soul.

"Saif al-Islam atagombea urais kwenye uchaguzi ujao ambao unaweza ukafanyika katikati mmwa mwaka 2018,ana dhamira ya kuongeza ulinzi zaidi na utulivu kulingana na jografia ya Libya, kwa kushirikiana na makundi yote ya Libya, hivi karibuni anatarajia kuweka wazi tarahe ya kujitangaza rasmi kwenye vyombo vya habari", amesema msemaji Basem Hashimi Soul.

Nchi ya Libya hivi karibuni imekuwa isiyo ya utulivu, kutokana na vurugu zinazoendelea, huku mtoto huyo wa Gaddafi akiwa na imani kubwa Umoja wa Mataifa utakubaliana nae katika kipindi hiki kigumu ambacho nchi hiyo kinaipitia, cha kutafuta utulivu.

Saif al-Islam ni mtoto wa pili wa Muammar Gaddafi ambaye alitolewa madarakani na kuuawa mwaka 2011, na pia ni mwanasiasa mwenye utaalam wa uchumi.

Nassari: Niliwapa Takukuru Kila Aina ya Ushahidi Walioutaka Ila Ushahidi wa Rushwa Ukiletwa na Mwanasiasa Rushwa Inabadilika Rangi?.

$
0
0
Nassari: Niliwapa Takukuru Kila Aina ya Ushahidi Walioutaka Ila Ushahidi wa Rushwa Ukiletwa na Mwanasiasa Rushwa Inabadilika Rangi?.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa aliwapa Takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka kuhusu tuhuma za kununuliwa kwa baadhi ya madiwani wa Chadema na kuhamia Chama cha Mapinduzi(CCM) huku akihoji kuwa tuhuma na ushahidi wa rushwa ukiletwa na mwanasiasa rushwa inabadilika rangi?.

Mh. Nassari ametumia ukurasa wake wa Instagram kuyaeleza hayo huku akisema kuwa aliwapa Takukuru moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa.

“Niliwapa takukuru kila aina ya ushahidi walioutaka”
niliwapa takukuru mpaka moja ya kifaa nilichotumia kurekodi baadhi ya vikao vya ununuzi na ushawishi wa rushwa. Na wakasema wana teknolojia ya hali ya juu ku-retrieve kazi zote, muda na wakati ambapo video hizo zilichukuliwa, bila kukosea. Teknolojia ambayo mimi pia ninayo.
Cha ajabu hawajaona UHALISIA au UONGO uliopo kwenye ushahidi, badala yake wameona siasa. ni kweli ilikuwa lazima waone siasa kwa sababu hata ununuzi wenyewe ulikuwa ni rushwa ya ki-mfumo (systemic corruption ). Na aina hii ya rushwa ni mbaya sana kama itaachwa ikasambaa kwenye mfumo mzima wa Siasa za nchi. TAKUKURU wanasema iliingizwa siasa, swala la kujiuliza, “Hivi kumbe tuhuma na ushahidi wa rushwa ukiletwa na mwanasiasa rushwa inabadilika rangi”?

Hivi karibuni kuliibuka na tuhuma kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa(Takukuru) kuwa wamefuta ushahidi wa Mbunge huyo kwa kile kilichodaiwa kuwa wameharibu uchunguzi wa chombo hicho kwa kueleza kila kwa vyombo vya habari.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Rais Magufuli awatoa wasiwasi Watanzania Kuhusu Ukomo wa Uongozi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. John Pombe Magufuli amewatoa wasiwasi wananchi kwa kusema wazi kwamba anatamani siku moja ifike naye aitwe mzee mstaafu wa taifa hilo kama alivyo Kikwete na wengine.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua uchaguzi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama NEC Taifa, mkoani Dodoma akiwakaribisha na kuwatambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wakiwemo Marais wastaafu.

''Natamani siku moja na mimi nistaafu, niitwe mzee mstaafu kama mzee Kikwete niwaachie wengine,'' amesema.

Vipindi vya ukomo kwa sheria iliyopo kwa nafasi ya Rais ni miaka 10 , sheria inaruhusu kila baada ya miaka mitano kufanyika kwa uchaguzi mkuu ili kuwapa demokrasia wananchi kuweza kuchagua kiongozi anayefaa.

Mwezi Julai, 2017 kuliibuka mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii kujadili kauli ya Rais mstaafu ya awamu ya pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi, aliyoitoa katika Baraza la  sikukuu ya Iddi aliyosema  kama isingekuwa matakwa ya kikatiba angetegemea kuona Rais aliyepo madarakani John Pombe Magufuli akipewa nafasi ya kutawala bila kikomo.

Mkutano huo wa leo utakipatia viongozi wapya wa ngazi ya juu chama hicho ikiwemo Mwenyekiti taifa na Mwenyekiti baraza la mapinduzi Zanzibar.

Tayari Rais magufuli amethibitisha kuwa katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana ataendelea na nafasi yake.

Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images