Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Naomba Ushauri: Nimezaa na Dada Yangu wa Damu

0
0
Moja kwa moja niende kwenye maada. Mkasa huu umenikumba nikiwa nafanya kazi mkoa flani kanda ya kati. Katika eneo ambalo nilikuwa naishi ni karibu na sehemu ambayo baba yangu alikuwa anafanyia kazi kabla ya kustaafu na kurudi nyumbani kwake namaanisha mkoa alikozaliwa yeye ambao upo kusini nyanda za juu. 

Wakati baba anastaafu na kurudi mkoa aliozaliwa mimi na nikabaki mkoa huo huo aliokuwa anafanya kazi sikuweza kuhama naye kwasababu nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni moja ya mawasiliano .

Katika kipindi alichokuwa anafanya kazi kumbe alizaa nje ya ndoa na mwanamke mmoja lakini baba hakuweza kumhudumia yule mtoto kitendo ambacho kilimfanya mama mtoto asimweke karibu na baba.

Hata yeye baba hakuwahi kutuambia kuwa aliwahi kuzaa nje ya ndoa. Katka kipindi chote hicho mama huyo na mwanaye walikuwa wakiishi mbali kidogo na wilaya yetu.

Basi katika mizunguko ya kazi hapa na pale nilikutana na dada huyu ambaye ndiye nimezaa naye pasina kujua ni dada yangu. Tulikutana kwenye semina mkoani Kilimanjaro kama ilivyo kawaida ya wanaume nikamuaproach yule dada na akaingia line. Tukaanza kujihusisha kimapenzi kwa muda wa mwaka mzima mpaka alipopata ujauzito.

Ikanilazimu niukubali ule ujauzito na nikatafuta wazee wa mtaa ninaokaa na kwenda nyumbani kwa mwanamke ili kujitambulisha. Yule mama mkwe ambaye ni mama mdogo kihalali alipoona majina yangu matatu akapatwa na wasi wasi japo barua ilipokelewa.

Ikabidi akanitafuta kwa kuniuliza kiundani nilipojieleza ndipo akasema huyu uliyempa mimba ni dadayako tena wa damu. 

Kwakweli niliishiwa nguvu akaanza kunisimulia kila kitu kuhusu baba yangu. Mpaka hapa ninapo andika mwanamke ameshajifungua na mtoto ana miezi 5.

Baba sijamwambia bado ila nataka nimpeleke huyu binti nyumban kwetu. Na hii siri naijua mimi na mama mkwe au mama mdogo. 

Sijajua nifanyeje mama mwenyewe ameshindwa afanye nini, tunaogopa kuwashirikisha watu aibu.

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Kwanini Wanawake Mkijifungua Mnakimbili kwa Wazazi Badala ya Kukaa na Waume Zenu?

0
0
Kuna kitu huwa kinanishinda kuelewa kusema ukweli kinachotokea kati ya wanaume na wanawake wa kisasa, hivi inakuaje mke umutie mimba wewe mwanaume then mimba alelee kwako nyumbani lakini ikifika kipindi cha kujifungua eti unataka akajifungulie nyumbani kwao. 

Kwa upande wangu mimi sioni logic yoyote ile eti mke kujifungulia kwao eti miezi mitatu sijui miwili ya mwanzo unataka akae kwao. Na nyie wanawake mnakubali vipi wakati mnajua kabisa mtoto kipindi cha mwanzo mwanzo anasumbua sana yaani kulia hakuishi sasa badala ukamlee na mumeo ili aone jinsi inavokuwa wewe unakimbilia kwa mama yako na baba yako kana kwamba yeye ndiye aliekupa ujauzito.

Tubadilike jamani tuyakubali majukumu yetu na wanawake juoni kuwa hicho kipindi ni cha mhimu kwa wanaume kushow love

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Baada ya Matokeo ya Kidato cha Sita Kutoka na Wanafunzi Wengi Kufaulu, Wadau Wasema Kuna Walakini

0
0
Wadau wa elimu nchini wameonyesha kushtushwa na matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kuonyesha kuwa asilimia 95.98 ya watahiniwa wamefaulu mtihani huo bila kuwapo na mikakati inayoonekana ya kuboresha kiwango cha ufaulu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wadau hao walisema pamoja na matokeo hayo kuonyesha ongezeko la ufaulu, wana wasiwasi iwapo matokeo yaliyoandikwa kwenye karatasi yanaakisi ufahamu wa wanafunzi.

Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo (Chadema) alisema hakuna mkakati wowote uliochukuliwa na Serikali kuhakikisha ufaulu unaongezeka, hivyo ni jambo la kushangaza kuona matokeo yanaonyesha wanafunzi wamefanya vizuri kiasi hicho.

“Hapo kinachooneka goli limepanuliwa ili magoli yaingie zaidi kwani kati ya mwaka jana na mwaka huu kitu gani kimefanyika. Ukaguzi wa walimu na wanafunzi haufanyiki, ufaulu unaongezekaje?” alihoji Susan.

Aliongeza kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kutaka kuwaridhisha wazazi ambao walikata tamaa kutokana na matokeo mabaya ya wanafunzi wao kwa miaka miwili iliyopita.

“Walimu wanajua kuwa hata wasipofundisha wanafunzi kuna mtu huko juu atawafaulisha tu,” alisema.

Mkurugenzi wa shirika la Uwezo linalojihusisha na masuala ya elimu, Ziada Mgalla alisema wanafunzi waliofaulu wanapaswa kupongezwa iwapo asilimia 95.98 ya ufaulu inawakilisha ufahamu wao.

Alisema historia inaonyesha kuwa wapo baadhi ya wanafunzi ambao walifaulu kwa kiwango kikubwa lakini hawakuwa na uwezo wa kufafanua kile walichokiandika kwenye mitihani jambo linalotia shaka kuwa huenda matokeo ‘yalichezewa’.

“Matokeo hayo hayatakuwa na maana kama wanafunzi waliofaulu hawawezi kuwa na ufahamu unaolingana na matokeo yao. Pia wastani unaozungumzwa lazima mwanafunzi awe amepata kuanzia alama 60 kuendelea kama amepata chini ya hapo hakuna sababu ya kushangilia,” alisema Ziada.

Akizungumzia sababu za shule za umma kufanya vibaya, mkurugenzi huyo alisema kuwa Serikali ijiulize kwa nini walimu wanaofundisha shule hizo wanafunzi wao hufeli, lakini wakienda kufundisha shule za binafsi, wanafunzi wao hufaulu.

“Suala siyo tu kuwa na walimu, wawasikilize wanapolalamika vinginevyo itafika wakati mwanafunzi wa sayansi ataonekana amefaulu lakini akifika kwenye upasuaji akashindwa kufanya kazi taifa likatia aibu,” alisema.

Meneja Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Boniventura Godfrey alisema wakati watu wanashangilia matokeo hayo yaliyotajwa kuwa ni mazuri yakilinganishwa na miaka iliyotangulia, wadau wa elimu wanapaswa kujiuliza kwa nini shule za umma zilizokuwa zikiongoza miaka ya nyuma zinazidi kufanya vibaya.

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Lulu Michael Afunguka 'Mimi Sipo Facebook Mnaibiwa Bure Tu na Anayejifanya Mimi'

0
0
STAA wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema hajawahi kufungua akaunti kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook ‘FB’ na kwamba aliyefungua kwa jina lake ana nia ya kuwaibia mashabiki wake.

Akizungumzia akauniti hiyo inayoonekana ni feki yenye sura ya kuwaingiza mjini mashabiki wake, Lulu alisema haitambui na wanaokubali kujiunga na ‘Lulu’ huyo wanataka kuibiwa.

“Hee nashangaa kwa kweli, yaani sielewi chochote kuhusu akaunti hiyo, sina akauti Facebook nashangaa sana kwa hilo swala wasitake kunichafulia,” alisema Lulu.

Makalio ya Mwigizaji Koleta Yadatisha Watu Mlimani City

0
0
Msanii wa filamu, Coletha Raymond ‘Koleta’ hivi karibuni aliibua gumzo maeneo ya Mlimani City jijini Dar kutokana na kivazi alichokuwa amevaa huku makalio yake yakionekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
Tukio hilo lilitokea juzikati wakati  Koleta alipokuwa akitoa kwenye lango kuu kuelekea ilipo ‘parking’ ya magari akiwa na mwanaume aliyeonekana kama mpenzi wake.

Wakiwa katika eneo hilo, wawili hao walionekana wameshikana mikono huku mdada huyo akitembea kwa mikogo na kudeka, akichezesha makalio yake hali iliyoibua minong’ono.

“Mh! Huyu si yule Koleta muigizaji, haya makalio yake daah! Au kishatumia Mchina maana…!” alisikika akisema kijana mmoja aliyekuwa akimsindikiza kwa macho huku wengine wakiendelea na mjadala juu ya kisuruali alichovaa na mwanaume aliyekuwa naye kama ni mpenzi wake ama laa.

Trafiki 27 Watimuliwa Kazi kwa Shutuma za Rushwa Barabarani

0
0
Askari  27 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani wamefukuzwa kazi ndani ya kipindi cha miezi sita kutokana  na kujihusisha na  makosa ya rushwa.

Kikosi hicho ambacho kimeonya dhidi ya unyanyasaji na ushawishi wa rushwa kwa waendesha pikipiki (bodaboda), kimesema mikakati ya uchunguzi na upelelezi imeimarishwa kwa lengo la kudhibiti matukio ya rushwa  miongoni mwa askari wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es  Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Taifa,  Mohamed Mpinga alisema askari hao wamekamatwa kutokana na kuimarishwa kwa  usimamizi wa nidhamu na mapambano dhidi ya rushwa.

Alisema, licha ya kufanya kazi kwa weledi,  upo usimamizi wa karibu kwa askari wake kwa lengo la kuepusha jeshi hilo na matukio ya aibu yakiwemo ya kujihusisha na rushwa.

“Pamoja na jitihada hizi tunaomba wananchi wote kutupa ushirikiano  kupambana na hali hii hasa kwa kutoa taarifa za askari wanawaomba rushwa,” alisema Mpinga.

Alisema taarifa zitawezesha kuwashughulikia kikamilifu  askari husika.

Kamanda Mpinga ameelekeza wananchi hao hususani madereva wanaoombwa rushwa na askari,  kuondokana na usiri kwa kuwafichua hata baada ya kuwapatia fedha.

“Kama askari akikuomba fedha zozote ni vizuri umpatie kama unazo. Na baada ya hapo, njoo utoe taarifa kwangu nami nitakurejeshea fedha hizo,” alisisitiza Mpinga akisisitiza kwamba wanao wapelelezi wa kubaini ukweli juu ya tuhuma dhidi ya askari wao.

Akilenga kujibu malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na waendesha bodaboda dhidi ya baadhi ya askari wa usalama barabarani, Mpinga alisisitiza, “kikubwa hapa ni ushirikiano wa kila upande, utakaowezesha tabia hii kukoma.”

Kajala Nalitaka Kumlipia Mume wa Florah Mbasha Hela ya Dhamana Mahakamani

0
0
Kama ulikuwa hujui basi chukua hii, staa wa filamu za kibongo, Kajala Masanja alitaka kumlipia dhamana mume wa mwimbaji wa muziki wa injili, Florah Mbasha aitwaye Emmanuel Mbasha shillingi za kitanzania million tano(5). 

Hata hivyo staa huyo alikuta tayari ndugu wa Emmanuel Mbasha wameshamlipia ndugu yao dhamana hiyo, hivyo zoezi lake hilo la kutoa msaada huo halikufanikiwa, hata hivyo mume wa Florah alimshukuru sana staa huyo kwa moyo wake huo wa upendo na huruma aliomuoneshea.

Halima Mdee'Nikiwa single Sina Bei-Mnao Ogopa Kumtokea Kisa ni Mbunge Wala Msiwe na shaka

0
0
Mbunge wa jimbo la kawe jijini Dar es Salaama katika tiketi ya Chadema Mh. Halima Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa huwa hana bei pindi awapo Single,

Mdee amesema hayo kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachokukutanisha na mtu maarufu katika tasnia fulani kila siku za Jumatano.
Halima Mdee alikuwa akijibu moja ya swali aliloulizwa na shabiki wa ukurasa huo aliehitaji kujua gharama zake za mali kama anahitaji kumuoa na kuwa mke wake
"Mhe Kama nataka nikutolee Mali niandae Tsh ngapi? Halima Mdee:Nashukuru..ila siko single. Kama ningekuwa single ,huwa sina bei kabisaa"
mbali na hilo Mdee ameweka wazi mpango wake katika jimbo la Kawe kwa mwaka 2015 kuwa anaweza kugombea katika jimbo hilo ikiwa mwenyezi mungu atamjalia uzima na kama ataona utumishi wake bado unahitajika katika jimbo hilo na wananchi, na kusema kuwa chama chake cha Chadema kipo imara licha ya changamoto mbalimbali walizopitia.
"Kawe nitagombea kama mwenyezi mungu ataniweka hai...na kama nikiona kwamba utumishi wangu bado unahitajika na wananchi.Ila Chama kiko imara,japo tumepita katika kipindi kigumu kwa kila mmoja wetu.Naamini tutaimarika zaidi..changamoto na misukosuko unaifanya taasisi au mtu kuwa imara zaidi.
MCHAKATO WA KATIBA
Maswali mengi yaliyoulizwa na mashabiki yalikuwa yakilenga katika kujua na kufahamu mustakabali wa mchakato wa Katiba na kujua kama Waakilishi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaweza kulejea bungeni kama ambavyo wamekuwa wakiombwa na baadhi ya viongozi wa Nchi kurudi kuendeleza mchakato huo,Mdee alisema kuwa kama wajumbe walio wengi wataacha kujadili rasimu ya Chama Cha Mapinduzi.
"Tutarudi kama walio wengi wataacha kujadili rasimu ya CCM....kilichotupeleka pale ni rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume....na si vinginevyo."
Shabiki mwingine alihitaji kujua kama Halima Mdee atakuwa teyari kukubaliana na suala la kubadili sheria ya mabadiliko ya katiba na jibu lake lilikuwa kama hivi
"Hatuwezi kuruhusu...itakuwa kuhalalisha matakwa ya kundi fulani kwa maslahi ya kundi husika. Sheria haina tatizo lolote...tunachotakiwa kama wajumbe wa bunge la katiba ni kutekeleza wajibu wetu kama sheria inavyotaka."

YATISHA: Kijana afyatuka, Amuua mtoto wa Miaka 9 na ‘Kutafuna Ubongo’ Kisha Kujikata Uume

0
0

Moshi. Mkazi mmoja wa Moshi amemuua mwanafunzi wa darasa la 3 kule Samanga leo na kisha 'kula ubongo' wa mtoto huyo katika tukio la kutisha lililostua wakazi wa mji huu.
Kijana huyu aliyefahamika kwa jina la Lawrence Mramba, 20, alimshambulia mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 kwa panga wakati akienda shule mnamo saa 1 asubuhi Ijumaa, akampasua kichwa na kisha akaanza kutafuna ‘vipande vya ubongo wake.’
Mara baada ya kitendo hicho cha kushtusha, Mramba, aliyeonekana kuwa na matatizo ya akili, alianza kujikatakata sehemu zake za siri na wembe, huku akitafuna vipande vya mwili wake mwenyewe, kimoja baada ya kingine.
Baadhi ya mashuhuda wanadai kijana huyo  ‘alionyesha kuwa na nguvu za ajabu’, huku wanakijiji wenzake wakishindwa kabisa kumdhibiti.
Wengi walilazimika kuketi kando wakimtazama jinsi anavyojikata wakishindwa kujua cha kufanya.
Iliwabidi polisi waingilie kati sakata hilo na hatimaye wakifanikiwa kumthibiti kijana huyo.
Hata hivyo, Mramba alifariki dunia muda mfupi baadaye katika hospitali ya Kilema wakati akipewa matibabu ya dharura kutokana na kupoteza damu nyingi.

Flora Lyimo 'Jamani Huyo Mange Nikiona Anavyotukana Wenzake na Kuwadharau Natamani Nimpandie Ndege'

0
0
Mbuta Nanga Aka Flora Lyimo Uvumilivu umemshinda baada ya leo Mange Kuweka post Akimponda Dada mmoja ambae inasemekana ndo alipeleka umbea kwa Mmiliki wa Bidhaa ambazo Mange amekuwa kiziuza bila idhini:
Jisomee Hapa alichosema Flora:

Wataalam 100 wa Ukimwi wafa Kwenye Ndege ya Malaysia iliyotunguliwa

0
0
Karibu watu 108 kati ya wahanga 298 wa ndege ya Malaysia iliyotunguliwa Ukraine Alhamisi walikuwa ni watafiti wa Ukimwi waliokuwa wakielekea Melbourne kuhudhuria Kongamano la 20 la Kimataifa la Ukimwi (AIDS 2014).

AFP imevinukuu vyombo vya habari nchini Australia vikisema kuwa, wakati wa mkutano wa maandalizi ya AIDS 2014 mjini Sidney, washiriki walielezwa kuwa wenzao 100 walikuwa wamepanda hiyo ndege iliyotunguliwa Ukraine Mashariki.

Kati ya waliofariki yumo mtafiti maarufu wa Ukimwi toka Uholanzi, Joep Lange, ambaye amewahi kuwa Rais wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ukimwi.

Vilevile, Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Glenn Thomas, pia amekufa katika mkasa huo.

Malaysian Airlines imetoa orodha ya wahanga inayoonyesha kuwa abiria 189 kati ya 298 walokuwa ndani ya ndege hiyo walitokea Uholazi, huku pia kukiwa na Wamalaysia 44, Waaustralia 27, Waindonesia 12, Waingereza tisa, Wajerumani wanne, Wabelgiji wanne, Wafilipino watatu, Mkanada mmoja na abiria mmoja toka New Zealand.

Utaifa wa abiria wanne waliobaki bado haujafahamika.  

UPDATE 1 - Hadi kufikia Ijumaa alfajiri, shirika la ndege la Malaysia limethibitisha abiria 298 wamefariki baada ya ndege yao namba MH17 kutunguliwa Ukraine Mashariki jana.

Kati ya wahanga wa zahama hilo, 150 walikuwa raia wa Uholazi walokuwa wakielekea Kuala Lumpur. Imethibitishwa pia kuwa Waaustralia 27 na Waingereza 9 wamefariki katika shambulizi hilo.

Shirika hilo la ndege limesema litatoa taarifa zaidi litakapokamilisha shughuli ya kuwatafuta ndugu wa marehemu, huku ikitangaza kusitisha safari zake zote Ulaya hadi hapo baadaye.

Wakati huo huo, Marekani pia imeyaonya mashirika yake yanayosafirisha abiria yasithubutu kuruka kwenye anga la Ukraine. 

FIRST POST - Kiev, Ukraine. Ndege ya Shirika la Malasyia jana ilitunguliwa mashariki mwa Ukraine na wanajeshi wanaoiunga mkono Russia na kuua watu 295 waliokuwa ndani, ofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine alisema.

Ndege hiyo ‘Malaysia Airlines’ ilikuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur na ilikuwa juu umbali wa futi 33,000 kutoka usawa wa bahari wakati ikitunguliwa.

Taarifa ya Kuungua kwa Jengo la Naura Springs Hotel Arusha.

0
0
Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii bila shaka utakuwa umekutana na picha ambayo inaonyesha hotel ya Naura ikiungua moto huku nyingi zikionyesha moto wake umeshika kasi kwenye kuwaka.
Baada ya kusambaa kwa picha hizo  tulimtuma Mwakilishi Wetu kutoka Arusha kwa ajili ya kwenda kupata uhakika wa taarifa hizi ambazo amesema kuwa si za kweli na hata uongozi na wafanyakazi wa hotel hiyo wameshangazwa na picha hiyo.
Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kujua haswa picha hiyo ilipoanzia kusambaa ili kuweza kuwatambua walioanza kuzisambaza picha hizo.

Samatta Aaga Team ya Mazembe, Sasa Kucheza Ulaya

0
0
ANAONDOKA! Ndiyo, unaweza kusema hivyo kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, aliyemuaga tajiri wa timu hiyo, Moisse Katumbi Chapwe, kwenda kukipiga barani Ulaya na amekubaliana na uamuzi wake.

Samatta amekuwa akidaiwa kunyemelewa na baadhi ya timu kutoka mataifa ya Ulaya kama vile Ufaransa, Ureno, Urusi na Ubelgiji, kutokana na kipaji kikubwa anachokionyesha cha kusakata kabumbu.

Samatta aliliambia Udaku kwa njia ya mtandao kutoka nchini Tunisia ilipoweka kambi Mazembe kuwa ndani ya miaka miwili ijayo amepanga kucheza soka kwenye ligi kubwa barani Ulaya na tayari ameshazungumza na Katumbi juu ya suala hilo na amekubaliana naye.

“Nimepanga ndani ya miaka miwili ijayo nicheze kwenye ligi kubwa ulimwenguni, nimezungumza na bosi wa timu, Katumbi kaniruhusu na kuniambia suala hilo halina tatizo, pia amesema ataniachia na hawatanibania timu ikija kunisajili,” alisema Samatta.

Katika hatua nyingine, Samatta alisema timu yao imeshindwa kuweka kambi barani Ulaya kwenye nchi ya Ubelgiji kutokana na baadhi ya wachezaji kukosa viza ya kuingilia nchini humo. Kwa sasa wapo nchini Tunisia wakijiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya Misri.

Kwa miaka mingi sasa Mazembe imekuwa ikidaiwa kuwabania nyota wake kujiunga na timu za Ulaya kwa lengo la kujiimarisha, lakini msimu uliopita ilimuuza nahodha wake, Tresor Mputu, kwenda timu ya Kabuscorp ya Angola aliyokuwa akichezea Mbrazil, Rivaldo,

Mazembe pia imemuuza beki raia wa Zambia, Stopilla Sunzu, aliyesajiliwa na Sochaux ya Ufaransa inayonolewa na kocha wa zamani wa Zambia, Herve Renard.

Samatta alijiunga na Mazembe mwaka 2011 akitokea timu ya Simba, iliyomuuza kwa dau la Dola za Kimarekani 100,000 (sawa na Sh. milioni 150 za Tanzania za wakati huo), huku yeye mwenyewe akipewa Dola za Kimarekani 50,000 za usajili.

Tudd Thomas ataja kiasi alicholipwa na Diamond na Ommy Dimpoz kufanya 'MdogoMdogo na Ndigushima'

0
0
Mtayarishaji wa muziki Tanzania Tudd Thomas ndiye aliyetayarisha wimbo wa Diamond ‘MdogoMdogo’ ambao unafanya vizuri sana  pamoja na wimbo wa Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’ ambazo zote zimepata nafasi kubwa huku wasanii hao wakilipa mamilioni kufanya videos.

Akiongea katika kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm na Fadhili Haule, Tudd amesema kuwa alilipwa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila wimbo katika nyakati tofauti.

“Kikawaida huwa wanasema sio vizuri kwa kuwa ni biashara lakini mimi niko real, ni two million kwa kila wimbo.” Alisema.

Ameeleza kuwa gharama za nyimbo hizo zilitokana na ukubwa wa nyimbo zenyewe na muda alioutumia kukaa studio na wasanii hao.

Tudd amesema wimbo wa ‘MdogoMdogo’ ulitengenezwa kwa muda wa miezi mitatu kwa kuwa ulikuwa wimbo mgumu kwao wote kwa kuwa ilikuwa idea mpya kwa wote, wakati wimbo wa Ommy Dimpoz ulimchukua miezi miwili kuukamilisha.

Wema Sepetu Amlipua Tena Kajala Baada ya Kumwita Mnafaki

0
0
Shakoor jongo na MUSA MATEJA

BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki.
Habari hiyo ya kuitwa mnafiki iliandikwa kwenye gazeti hili toleo lililopita iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘Kajala: Wema mnafiki’.

Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.

“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?

“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.

Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.

“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema Wema.

Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.

“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.

Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.
GPL

Mume wa Dida Edzen Ataja Sifa za Mwanamke Anaye Tarajia Kumuoa

0
0
Stori: Deogratius Mongela

BAADA ya kuachana na mkewe ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida,’ mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha TV1, Ezden Jumanne ametaja sifa za mwanamke atakayekuja kumuoa kama akitaka kufanya hivyo.

Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar, Ezden alisema kuwa kutokana na kupitia kipindi kigumu cha kuachana na aliyekuwa mkewe amedai kuwa hafikirii kuoa kwa sasa lakini kama akija kuoa tena atamhitaji mwanamke mcha-Mungu, mwenye heshima, asiyemlevi na atakayejitambua kama ni mke wa mtu.

“Sidhani kama nitaoa hivi karibuni, lakini kama nitaoa tena mwanamke ninayemtaka ningependa awe mwenye heshima, anayefuata dini, asiyependa ulevi na atakayejitambua kama mke wa mtu,” alisema Ezden.
GPL

Diamond Kununua Hummer ya Gwajima Kwa Mil 400

0
0
Kuna tetesi kuwa mwanamuziki diamond platnum amenunua hummer aliyokuwa akitumia mchungaji gwajima ambapo inasemekana kauziwa kwa bei ya kutupwa(haijajulikana bei gani). Tunasubiri tu baba ubaya atudanganye kaagiza ulaya milion 400.

Shilole 'Nafunga Ndoa na Nuhu Mziwanda Kuwafunga Midomo Wachonga Ng'ebe'

0
0
Shilole Amekanusha uvumi ulioenea kuwa amekatalaliwa Ukweni kwa Wazazi wa Mpenzi wake Nuhu kwa Vile ni Mkubwa Kimri, Shi shi Baby Amesema Alipokelewa vizuri sana na wala hakuna shida yoyote na anawashangaa wanaozusha maneno ya uongo, Shilole amesema kuwa hivi karibuni ataolewa na Nuhu Kuwakata Ng'ebe wasema Ovyo na Uongo..

Joyce Kiria 'Chid Benz, Edzen, Dudubaya na TID Mwanamke Hapigwi Ngumi, Mmeishiwa Sera, Kapiganeni na Matumla

0
0
Ukatili wa kijinsia haukubaliki hata kidogo, wengine tunapambana usiku na mchana kutokomeza vitendo hivi vya Ukatili na Udhalilishaji, cha ajabu watu maarufu sasaivi wamechachamaa kuendekeza vutendo hivyo..

mara Dudubaya akampiga Mke wake, mara Tid akamtukana RayC, Mara Chidbenz akampiga mzazi mwenzake, mara Ezden akampiga mkewe, mara Chidbenz kampiga RayC!!!! jamani jaman jamani kwanini mnachukua uamuzi huo wa kudhalilisha Wanawake???

ChidBenz, Tid, Ezden na Dudubaya nyie ni vioo kwenye jamii yetu, kwahiyo si vyema kufanya vitendo vya kuwapiga Wanawake na kuwadhalilisha...kwani nyie hamkoseagi? kuna siku mmepigwa? sisi sote ni watu wazima kwa hiyo kama tumeshindwana kila mtu anachukua 50 zake kwa Amani.....

Kuna msemo unasema kwamba Mwanaume wa kweli hapigi Wanawake wala kumdhalilisha Mwanamke kwa sababu Wanawake ni Mama zenu. vitendo mlivyowafanyia hao Wanawake mngependa Mama Zenu wafanyiwe???

ushauri: kama wewe unajiskia kupigana basi ni vyema ukaomba pambano na Matumla, Kaseba au Cheka ili tujue kama kweli wewe ni mpigaji..kinyume na hapo ni kuonea Wanawake na kuwadhalilisha kijinsia....

Nawaheshimu sana kama wasanii lakini naomba mjirekebishe tena kuanzia sasa muwe mabalozi wa Kupambana na vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji kwa Wanawake. na muwaombe radhi wale mliowapiga na kuwadhalilisha..

Nawakaribisha sana kwenye kipindi cha WanaumeLive ndani ya Wanawakelive tushirikiane sote kutokomeza vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji kw Wanawake..

Ney wa Mitego naomba useme na hawa mastaa wenzako ambao naona hawajasikia ule ujumbe wako kwamba Mwanamke hapigwi na mangumi na mateke...waeleze Mwanamke anapigwa na nini! nakuita pia Linex utukumbushe ule ujumbe wako kwamba ndoa haivunjwi na mwanamke pekee bali hata Mwanaume nae aweza vunja ndoa (mahusiano) si lazima uwe umefunga ndoa.

sasa inapotokea mmeshindwa kuelewana au kukubaliana haifai utumie Nguvu ndidi ya Mwanamke wako.. kama mkishindwana mnaachana kwa Amani, msiachane na kutuachia Mangeu...

Rayuu Akimbilia Sambawanga Kusafisha Nyota ya Ustaa Bongo

0
0
Msanii  anayefanya  vizuri  katika  tasnia  ya  filamu  nchini, Alice  Bagenzi  ‘Rayuu’  amesema  amekuwa  akisikia  maneno  ya  chinichini  kwamba  ameenda  Sumbawanga  Kuroga….

Tetesi  hizo  za  Rayuu  kwamba  ameenda  Sumbawanga  kuroga  zimeanza  kuvuma  baada  ya  watu  kuhoji  kuwa  jina  lake  linaonyesha  yeye  ni  Mhaya, lakini  chakushangaza  amekuwa  akienda  Sumbawanga  mara  kwa  mara….

Kumtafuta  mrembo  huyo  ambaye  amekuwa  akiandamwa  na  kashfa  ya  kutembea  na  waume  za  watu  na  kusambaza  picha  za  utupu ili  kujua  ukweli  wa  mambo  ambapo  msanii  huyo  alifunguka  kuwa:

Nawashangaa  sana  watu  wanaosema  nimekuja  Sumbawanga  kuroga, sio  kweli, huku  nimekuja  kusalimia.Naipenda  familia  yangu  ndo  maana  nimeitembelea na  ntakaa  kwa  muda  huku  kwani  huwa  nai  miss  sana  nikiwa  Dar
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images