Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

Kutana na Mtabibu wa Nyota Duniani Maalim Fadhil Rashid Kutoka Comoro Kwa sasa Yupo Tanzania

$
0
0
KUTANA NA MTABIBIBU WANYOTA DUNIANIKOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE ANADAWA ZA KI COMRO DAWAZAKE HABAHATISHI MUONE HARAKA AKUSAIDIE TEZI NAUVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABI MALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI ZAMAJINI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YAKUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NAUMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWAHARAKA KUZUIYA CHUMAULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI KARIBUNI WOTE TIBA NIKWADINI ZOTE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO DUNIANI

CALLING +255719362806/

WHATSAPP CALLING +255785786436

Siwezi Nikawa Kwenye Ndoa Nikabanabana Nitamzalia Uchebe Kidume- Shilole

$
0
0
Siwezi Nikawa Kwenye Ndoa Nikabanabana Nitamzalia Uchebe Kidume- Shilole
STAA wa Muziki wa Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa, kwenye ndoa yake aliyofunga hivi karibuni, atamzalia mumewe, Ashiraf Uchebe mtoto mmoja wa kiume.

Akizungumza na Star Mix, Shilole au Shishi Trump alisema, hawezi kusema kuwa hatazaa wakati tayari yupo ndani ya ndoa.

“Natarajia kumzalia mume wangu kidume mmoja maana siwezi kuwa kwenye ndoa nikabanabana,” alisema Shilole.

Shilole na Uchebe, wameisogeza mbele sherehe yao ya harusi iliyokuwa ifanyike Desemba 20 hadi Desemba 28, mwaka huu.

Jike Shupa Atokwa Povu Kisa Wanaume Mashoga

$
0
0
Jike Shupa Atokwa Povu Kisa Wanaume Mashoga
MUUZA nyago aliyejipatia umaarufu kupitia Wimbo wa Jike Shupa wa mwanamuziki Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, Zena Mustapha ‘Jike Shupa’ amewatolea povu watu wanaomsema kuwa anapenda kuishi na wanaume tata ‘mashoga’.


Akizungumza na Star Mix, Jike Shupa alisema kuwa, ni ajabu kwa mtu kumuandama, kisa amekuwa karibu na mashoga badala ya kuendelea na maisha yake na kutatua shida zake.



“Jamani naona watu wananishangaa kuwa karibu na mashoga, lakini wakumbuke kuwa ni watu kama walivyo watu wengine, wala siwezi kuwaacha hata kidogo, endeleeni na maisha yenu niacheni,” aliwaka Jike Shupa.

Wolper Atoboa Siri ya Gharama ya Jino Lake la Silva

$
0
0
Wolper Atoboa Siri ya Gharama ya Jino Lake la Silva
HII ikufikie wewe mpenda ubuyu kuwa, lile jino la shaba ‘silva’ la staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe lililoleta gumzo mitandaoni, mwenyewe amelifungukia kuwa, limemgharimu kiasi cha dola elfu 3 za Kimarekani (zaidi ya Sh. Mil.6 za Kibongo).

Akichonga na Star Mix, Wolper aliwashangaa wanaosema na kuweka picha zikimuonesha akiwa na mapengo wakati alifanya hivyo kwa makusudi na kuweka la silva ili kuwa na muonekano tofauti wa meno yake.

“Watu wanaongea tu bila kujua. Pengo hili nimelipandia ndege kwa makusudi na kwa taarifa yao tu hili jino la silva nililoliweka limenigharimu dola elfu 3 (Mil.6),” alisema Wolper.

Barnaba Afuata nyayo za Diamond Aajiri Bodigadi

$
0
0
Barnaba Afuata nyayo za Diamond Aajiri Bodigadi
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva nchini, Barnaba Elias, ‘Barnaba Classic’ ameamua kuajiri bodigadi wa kumlinda kwa ajili ya kujiongezea thamani.

Barnaba akizungumza na Showbiz alisema kuwa, ameamua kuongeza ‘value’ kwenye kazi zake na pia kuepukana na rapsha zisizo za lazima.


“Kuwa na bodigadi ni kuongeza value ya kazi yangu lakini pia kama wasanii kuna rapsha mbalimbali ambazo tunakutana nazo kutoka kwa watu ambao hawatutakii mema. Mashabiki wangu wasiniogope na kunitenga kwa sababu ya mlinzi wangu,”alisema Barnaba.

Hatimaye Mashindano ya Miss Tanzania Yafutwa Rasmi

$
0
0
Hatimaye Mashindano ya Miss Tanzania Yafutwa Rasmi
WAANDAAJI wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Kampuni ya Lino International Agency Limited,  wamesema  kwamba hakutakuwa na Fainali za Taifa za shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2017.

Katika taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo leo imeeleza kuwa sababu kubwa ya kuahirishwa kwa shindano hilo ni ukosefu wa Wadhamini ambao kwa njia moja au nyingine huwezesha kufanyika kwa mashindano hayo kwa kulipa gharama mbalimbali ikiwemo zawadi za washiriki.

Aidha waandaaji hao pia wamesema kuwa kuchelewa kupata kibali cha kuanza mchakato wa Miss Tanzania 2017, ambacho kilitolewa na BASATA mwezi Septemba mwaka huu pia kimechangia kukosa kwasababu muda ulikuwa umeshaenda.

Mashindano ya kutafuta warembo wa Miss Tanzania yamekuwa yakifanyika kila mwaka na baadae kuibua mastaa mbalimbali kama Wema Sepetu, Lulu Diva, Jokate Mwegelo na wengine wengi.

Jokate, Wema Sepetu Wapata Dili Wizara ya Maliasili na Utalii

$
0
0
Jokate, Wema Sepetu Wapata Dili Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amefanya uteuzi wa wajumbe nane kuunda kamati ya kitaifa ya kuandaa mwezi maalum wa maadhimisho ya urithi wa Tanzania  (Tanzania Heritage Month)

“Tumeongeza idadi ya wajumbe wa Kamati ya Mwezi wa Urithi wa Tanzania (Tanzania Heritage Month) ili kupata uwakilishi wa Zanzibar na Vijana. Kamati hii itafanya kazi ya kuweka sawa wazo hili na kusaidia utekelezaji wake” amesema Dkt. Kigwangalla.


Tundu Lissu: Bado Nina Risasi Moja Mwilini

$
0
0
Tundu Lissu: Bado Nina Risasi Moja Mwilini
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema mwili wake bado una risasi moja licha ya kutolewa nyingine 15, huku akiweka bayana kuwa kitu anachokikosa zaidi ni kazi yake ya ubunge.

Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari mara baada ya kufika nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, pia aligusia faraja aliyoipata baada ya kutembelewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi tangu Septemba 7 na ambaye huenda akahamishiwa nje ya bara la Afrika kwa matibabu zaidi, ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Azam, Baruan Muhuza.

“Hali yangu ya afya inaendelea vizuri bado nipo hospitali maana yake bado ni mgonjwa lakini niwaeleze Watanzania na wananchi wote wanaofuatilia afya yangu kwamba naendelea vizuri sana,” alisema na kuongeza,

“Hivi tunavyozungumza sina jeraha la risasi, risasi 16 ziliingia mwili mwangu na saba zilitolewa na madaktari hapahapa (Nairobi) na moja ipo bado kwenye mwili wangu lakini sina majeraha ya risasi na hali ni nzuri kuliko nilivyoletwa, nililetwa vipandevipande.”

Hiyo ina maanisha kwamba risasi nyingine nane, zilitolewa na madaktari wa Tanzania, saa chache baada ya shambulio hilo alipofikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General).

Huku akionyesha mkono wake wa kulia alisema, “Nilipigwa risasi hapa, upande huu na ikatokea hapa. Madaktari wanasema kwamba ilichakaza kabisa mfupa ilikopita, hakukuwa na mfupa. Ilibidi waungeunge kwa hiyo kuna chuma kinachounganisha mfupa wa huko mbele na nyuma kwenye mkono huu.”

Pia, aliukunja na kuunyoosha mkono wake wa kushoto na kusema kuwa hawezi kuunyoosha sawasawa kwa sababu kwenye kiwiko alipigwa risasi iliyosambaratisha mfupa.

Alikumbuka Bunge

Lissu ni miongoni mwa wabunge wanaoibua hoja nyingi na kuibana Serikali bungeni, jambo ambalo aliliweka bayana katika mahojiano hayo na kusisitiza kuwa ndicho kitu anachokikosa zaidi.

“Mimi napenda kazi ya ubunge. Kuna watu wanapenda ubunge kwa sababu una pesa na manufaa, unaitwa mheshimiwa na unakuwa wa kwanza kwenye foleni, hukai katika foleni. Mimi napenda ubunge, mle ndani (ukumbi wa Bunge) yale mapambano ya kisiasa na kiitikadi, unamkaba waziri mpaka anakosa pa kukimbilia,” alisema.

Aprili 4, 2015 Lissu alitoa hoja 22 za kupinga vifungu vya Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa mwaka 2015 na kusababisha kikao cha 14 cha Bunge kuvunja rekodi ya kutumia muda mrefu baada ya kumalizika saa 6:15 usiku.

Mvutano wa kisheria kati ya Lissu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju na mawaziri ulianza saa 12:30 hadi saa 5:30 usiku na baadaye Waziri Mkuu wa wakati huo, Mizengo Pinda akatumia muda uliosalia kuahirisha Bunge.

Katika mahojiano hayo na Azam Lissu alisisitiza, “Hakuna kazi ninaimisi kama ya ubunge bungeni, niende ofisini kwangu nijiandae nikasome ili kesho nikizungumza Watanzania wasikie, ndio kazi ninayoipenda.”

Alisema kitendo cha kulazimika kukaa miezi mitatu hospitalini, kulala kitandani muda wote kinamfanya akose mapambano ya bungeni, “Mtu akisema hii ni kutafuta kiki nafikiri aidha hanifahamu au akili zake haziko sawa.”

Kuhusu viongozi waliomtembelea alisema, “Makamu wa Rais alikuja wakati wa kumuapisha Rais Uhuru Kenyatta na kabla ya hajaondoka alitafuta nafasi ya kuja kuniona hospitali. Nilifurahi sana kwa uungwana. Ukiwa mgonjwa hakuna kitu cha faraja kama kupata mtu wa kukujilia hali. Aliniambia kwamba ametumwa na Rais John Magufuli kuja kunitazama, nikamjibu kamwambie Rais namshukuru sana kwa kukutuma kuja kuniona.”

Wanaohama upinzani

Kiongozi huo pia aligusia hamahama ya wanasiasa na kubainisha kuwa wapo wengi walioondoka lakini Chadema bado imebaki imara.

“Watu kwa sababu mbalimbali, aidha hawajui, wanasahau au wanajisahaulisha na historia yetu ya zama za vyama vingi,” alisema.

Alibainisha kuwa mbunge wa kwanza kuhama Chadema alikuwa Dk Aman Walid Kabourou ambaye alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa chama hicho, baadaye makamu mwenyekiti na mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama hicho.

“Aliondoka lakini aliishia wapi? Alihamia CCM kwani Chadema ilikufa? Said Arfi, alikuwa makamu mwenyekiti wa Chadema na mbunge wa Mpanda Mjini alirudi CCM je, Chadema ilikufa? Dk Willbroad Slaa alikuwa mbunge kwa vipindi vitatu mfululizo aliondoka je, Chadema ilikufa,” alihoji.
Chanzo: Mwananchi

Mijadara Yaibuka Baada ya TBC Kuonyesha Matangazo ya Moja kwa Moja Mikutano ya CCM

$
0
0
Mijadara Yaibuka Baada ya TBC Kuonyesha Matangazo ya Moja kwa Moja Mikutano ya CCM
Hatua ya vituo vya televisheni nchini hususan ya Taifa (TBC) kurusha moja kwa moja matukio na mikutano inayowahusisha viongozi wa Serikali na CCM, imeibua mjadala miongoni mwa jamii.

Katika mjadala, wapo waliogusia kuzuiwa kuonyeshwa mijadala ya Bunge moja kwa moja (live), kwa kigezo cha kuelemewa gharama na kubainisha kuwa kama viongozi hao wanaonyeshwa, hata vipindi vya Bunge vinapaswa kuonyeshwa kama ilivyokuwa zamani.

Wakati baadhi yao wakidai matangazo hayo yanalenga kuwazima viongozi wasio wa Serikali na vyama vya upinzani wanaokosa nafasi za kuonekana moja kwa moja, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi ametoa ufafanuzi akibainisha kuwa katika matukio ya kitaifa, vituo vya televisheni huombwa kurusha matangazo hayo.

Alisema, “Hivi ni TBC tu? Televisheni zote zenye uwezo wa kuonyesha huwa zinaonyesha. Suala la TBC kuzidi au kutozidi hiyo si hoja. Mfano mkutano mkuu wa CCM, televisheni nyingi zilionyesha.”

Dk Abbasi alisema katika matukio ya kitaifa, akitoa mfano wa maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, pia huwa vivyo hivyo.

Katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Desemba 17, mjini Dodoma, vituo kadhaa ikiwamo TBC viliuonyesha moja kwa moja kuanzia asubuhi hadi jioni.

“Kuhusu matukio mengine kuonyeshwa, hapo uziulize hizo televisheni zenyewe zitakuwa na majibu. Mimi nasimamia maonyesho ya kitaifa,” alisema.

Dk Abbasi alisema ikitokea Waziri Mkuu akaenda Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuzindua kitu halafu televisheni ikaonyesha tukio hilo, huenda kukawa na makubaliano kati ya televisheni husika na benki.

“Wakati mwingine tatizo si kuonyesha, pia mtazame mhusika mkuu wa tukio hilo ni nani,” alisema.

Januari mwaka jana, Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati huo, Nape Nnauye ilitangaza kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja matangazo ya mijadala ya Bunge ikieleza kuelemewa na gharama ambazo TBC inalipia.

Nape alitoa sababu nyingine ya kusitisha matangazo hayo wakati wa Bunge la 10 kuwa ni mpango wa Serikali kuanzisha studio yake.

Alisema Serikali ilikuwa ikitumia Sh4.2 bilioni kurusha mikutano minne ya Bunge kwa mwaka. Kwamba shirika hilo limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa kulipia matangazo hayo kwa kutumia matangazo madogo ya biashara.

Alisema asilimia 75 ya vipindi vya TBC hutumika kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani hivyo, TBC iliona ni vyema kubadilisha mfumo ili kukabiliana na kuzidi kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Ingawa hatua hiyo ilipingwa na wabunge wa upinzani na mashirika ya haki za binadamu, Serikali ilishikilia msimamo wake na kufafanua ni kwa nini ilifikia uamuzi huo.

Ni kama maelezo hayo hayajakata kiu kwani kina linapoibuka suala linalohusu kurusha matangazo ye televisheni live, suala hilo limekuwa likijirudia.

“Sijui kama wahusika wanalipia au la, hasa katika chombo cha habari cha umma,” alisema Dk Onesmo Kyauke wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) katika maoni yake.

“Nadhani vyama vyote vya siasa vipo sawa na tulishuhudia katika kampeni za uchaguzi mwaka 2015 vyama vingi vilionyesha matangazo yake moja kwa moja. Jambo hili likifanyika katika televisheni binafsi huwezi kuhoji sana ila televisheni ya Taifa yatasemwa mengi, ni lazima ulipe.”

Dk Kyauke aligusia mikutano ya Bunge, akisema umefika wakati wa kuruhusu ionyeshwe moja kwa moja ili wananchi kushuhudia wawakilishi wao wanachokifanya bungeni.

Mtazamo wa Profesa wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Saut), Mwesiga Baregu ni kwamba kuongezeka kwa matukio hayo kuonyeshwa moja kwa moja kuna lengo la kuwazima wengine akitoa mfano wa viongozi wa vyama vya siasa.

“Unaweza kujiuliza ni kwa nini wazuie matangazo ya Bunge, kwa nini wao ndio waonekane kila siku...? Viongozi waliopita walijitahidi kutenganisha shughuli za chama na Serikali,” alisema Profesa Baregu ambaye pia mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Alisema, “Ni kutaka kuonekana zaidi tu kuliko wengine, huwezi kusema mtumishi wa umma amsikilize na kumheshimu mwanachama wa CCM, sasa siku chama hiki kikitoka madarakani itakuwaje?”

Mhadhiri wa uandishi wa habari na mawasiliano ya umma wa Chuo Kikuu Tumaini, Kizzito Noya alisema, “Kurushwa ‘live’ matangazo inategemea na tukio husika. Huwa hairuhusiwi kurusha muda mrefu tukio ambalo halina masilahi kwa umma, “Hairuhusiwi kurusha matangazo kwa masilahi ya mtu mwenye pesa maana unawanyima watu wengine demokrasia na uhuru wa habari,” alisema.

“Mfano katika gazeti, matangazo yanatakiwa kutozidi asilimia 60, hata katika televisheni pia ni vivyo hivyo. Mfano kuruhusu mtu alipie pesa kuonyesha harusi yake kwa saa zaidi ya tatu. Hii si sawa.”

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco), Gaudence Mpangala aliungana na Profesa Baregu na kufafanua kuwa huenda kuna mkakati wa kuimarisha jambo fulani kutokana na matukio ya urushwaji matangazo moja kwa moja kuongezeka.

“Mikutano ya Bunge lenye wawakilishi wa wananchi halionyeshwi live lakini matukio mengine, hata ya chama tu yanaonyeshwa moja kwa moja.”

Akatwa Masikio Akituhumiwa Kulawiti Mtoto

$
0
0
 Akatwa Masikio Akituhumiwa Kulawiti Mtoto
KIJANA Msigala Salum (24), mkazi wa Kata ya Ndala mjini Shinyanga, amenusurika kifo kutokana na kufumwa akimlawiti mtoto wa miaka mitatu, baada ya baba mzazi wa mtoto huyo kuchukua kisu na kumkata masikio yote kisha kukimbia kusikojulikana.


Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi katika maeneo ya Majengo Mapya Kata ya Lubaga mjini Shinyanga, wakati kijana huyo akiwa katika shughuli zake za kuosha magari, ndipo alipodaiwa kumrubuni mtoto huyo akiwa na wenzake akicheza na kwenda kumfanyia ukatili huo.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule, alisema baada ya kijana huyo kutenda unyama huo na kukatwa maskio, jeshi lilipewa taarifa na kufika eneo la tukio na kufanikiwa kumtia nguvuni.

Alisema baada ya kumkuta mtuhumiwa akiwa katika hali mbaya, walimpeleka kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kamanda Haule alisema upelelezi juu ya suala hilo unaendelea na kwamba utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Aidha, alisema Jeshi pia linamtafuta baba mzazi wa mtoto huyo kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa baada ya kumkata masikio yote mawili,  alikimbia kusiko julikana.

Haule alisema mtoto aliyefanyiwa unyama huo alipelekwa kuchukuliwa vipimo na kupatiwa tiba kwenye hospitali ya mkoa.

Katika tukio lingine, jeshi hilo liliua Bahati Peter (28) mkazi wa Kata ya Oldshinyanga, anayetuhumiwa kuwa jambazi wakati akiwatoroka askari polisi waliomtia kizuizini kwenda kuwaonyesha wezake walipo.

Alisema askari walimpiga risasi na kufariki dunia wakati akijaribu kukimbia.

Kamanda Haule alisema tukio hilo liltokea Desemba 19, mwaka huu, majira ya saa 4:30 usiku katika eneo la Kata ya Ndala mjini Shinyanga, mahali alipokuwa ameficha silaha aina ya Shotgun yenye namba 006096210 TZ CAR 98454 ikiwa na risasi nne na alipoamriwa akaonyeshe wenzake ndipo akaanza kukimbia na kupigwa risasi.

Alisema kabla ya kuuawa, mtu huyo alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na mali za wizi ikiwamo Laptop HP, simu aina ya Samsung na alikili kuiba mali hizo zikiwa kwenye gari eneo la Club ya Level Four, jengo la NSSF mjini Shinyanga.

Haule alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufani ya  Mkoa wa Shinyanga, huku juhudi za kuwakamata majambazi wenzake zikiendelea kwa kuhusisha taarifa za kiitelenjensia.


Uchunguzi wa Chanzo cha Mauaji ya Kimbari Rwanda Wakamilika

$
0
0
Uchunguzi wa Chanzo cha Mauaji ya Kimbari Rwanda Wakamilika
Majaji wa Ufaransa wamemaliza upelelezi juu ya shambulio la kombora ambalo lilisababisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Ofisi ya mwendesha mashitaka sasa wataamua ikiwa waipeleke kesi mbele ya mahakama. Majaji wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba rais wa wakati huo wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana.

Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari. Upelelezi umesababisha sintofahamu kati ya mataifa haya mawili, kiasi cha Rwanda kuvunja uhusiano wa kidplomasi a na ufaransa mwaka 2006.

Uhusiano huo ulirejeshwa miaka mitatu iliyopita.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0
HARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670 

Hata Nape Aona Vyuma Vimekaza?

$
0
0
Hata Nape Aona Vyuma Vimekaza?
Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kuandika jambo ambalo linawachanganya wananchi wengine wakihisi na kudhani amekubali kuwa kweli mtaani vyuma vimekaza huku wengine wakiwa na maana tofauti juu ya kauli hiyo.


Nape kupitia mtandao wake wa Instgram jana aliandika  "Ni rahisi kuchukulia poa kwasababu kwako mambo yanaenda, lakini sio hata kidogo" jambo ambalo liliwafanya wananchi waanze kueleza hisia  

Wiki kadhaa zilizopita Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa anachukizwa sana na kitendo cha watu kutafsiri kauli zake anazozitoa kwenye mitandao ya kijamii na kuzihusisha na kumsema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Maguifuli.

Dewji ‘Mo’ Aanza Kazi Rasmi ya Kuihudumia Klabu ya Simba.

$
0
0
Dewji ‘Mo’ Aanza Kazi Rasmi ya Kuihudumia Klabu ya Simba.
MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameanza rasmi kazi ya kuihudumia Klabu ya Simba.

Mo ameanza kuihudumia klabu hiyo baada ya kupita kwenye mchakato wa kumtafuta muwekezaji wa Klabu ya Simba kwa ofa yake ya shilingi bilioni 20 na kupata hisa kwa asil­imia 50 huku 50 zikibaki kwa wanachama. Hata hivyo, bado kuna majadiliano na serikali ambayo inataka mwekezaji wa klabu asizidi asilimia 49.

Awali, mfanyabiashara huyo alikuwa anaihudumia timu hiyo kama mwanachama kabla ya kukabidhiwa na wanachama klabu hiyo na kuwa mwekezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka ndani ya timu hiyo, mfanyabiashara huyo ameanza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo mshahara, posho na mahitaji mengine.

Mtoa taarifa huyo alisema, kambi ya maan­dalizi ya mechi ya hatua ya pili ya Kombe la FA dhidi ya Green Warriors aliwezesha yeye kwa kuiweka timu ya Escape Two Hotel, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

“Ameanza kutoa hu­duma hiyo kwa kuanzia mechi dhidi ya FA kwa ku­fanikisha baadhi ya ma­hitaji muhimu ikiwemo kambi ya timu iliyoweka Escape Two Hotel.

“Pia anafanikisha baa­dhi ya mahitaji mengine ikiwemo mshahara na posho za wachezaji tuki­wa katika matayarisho ya mechi hii ya FA tu­takayocheza kesho (leo) dhidi ya Green War­riors,” alisema mtoa taarifa huyo.

Jumla ya Bilioni 3.1 Kutumika Kwenye Uchaguzi wa Marudio

$
0
0
Jumla ya Bilioni 3.1 Kutumika Kwenye Uchaguzi wa Marudio
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kuwa jumla ya Sh bilioni 3.1 zitatumika kwenye uchaguzi wa marudio ambao kampeni zake zimeshaanza.

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Januari 13 mwakani, kampeni zake zilianza tangu juzi kwa majimbo ya Singida Kaskazini na Longido wakati Jimbo la Songea Mjini kampeni zitaanza leo.

Kampeni hizo zitakamilika Januari 12 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika. Akizungumza na HabariLeo jana, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima alisema kuwa gharama hizo zitahusu majimbo matatu na kata sita.

Wakati Tume ikieleza gharama hizo za Sh. bilioni 3.1 za uchaguzi mdogo, jana Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alinukuriwa akisema kuwa serikali imeokoa Sh bilioni 156 ambazo zingetumika kugharamia uchaguzi wa marudio endapo serikali ingeshindwa kesi 53 zilizofunguliwa kupinga matokeo ya ubunge wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Fedha hizo zimeokolewa kutokana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufanikiwa kushinda kesi 52 na kushindwa kesi moja na hivyo kuokoa mabilioni hayo ya fedha. Akizungumzia uchaguzi katika majimbo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro ambayo pia yapo wazi kutokana na wabunge wake kujiuzulu, Kailima alisema mipango ya kuitishwa kwa uchaguzi ipo katika hatua za mwisho.

Alisema tayari NEC imeshapata barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kuieleza kuwa majimbo hayo yapo wazi na hivyo taratibu za kufanya uchaguzi wa marudio kwenye majimbo hayo zinaendelea. Alisema tume hiyo itakutana baadaye kutoa utaratibu kuhusu kufanyika kwa uchaguzi kwenye majimbo hayo mawili kwa kuwa kwa sasa wajumbe wengi wa Tume wako mikoani kikazi.

Alisema haitachukua muda mrefu utaratibu huo kutolewa kwani wanatarajia kukutana kati ya mwezi huu na Januari mwanzoni. Uhaguzi wa marudio kwa Jimbo la Longido unatokana na Maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Onesmo Ole Nangole.

Kwa Jimbo la Singida Kaskazini, uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa Mbunge Lazaro Nyalundu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujivua uanachama wa chama hicho pamoja na kujiuzulu ubunge wake na kujiunga na Chadema, wakati Jimbo la Songea Mjini uchaguzi unafanyika kutokana na aliyekuwa Mbunge jimbo hilo, Leonidas Gama kufariki dunia mwezi uliopita.

Jimbo la Kinondoni lipo wazi kufuatia aliyekuwa Mbunge wake, Maulid Mtulia (CUF) kujivua uanachama wa chama hicho na kujiuzulu nafasi zake ikiwemo ubunge Desemba 2, mwaka huu. Kwa jimbo la Siha aliyekuwa Mbunge wake, Dk Godwin Mollel naye alijivua uanachama wa Chadema na kujiuzulu nafasi zake zote ikiwemo ubunge na kujiunga na CCM hivi karibuni.

Sakata la Airtel, TTCL Lazidi Kupamba Moto Airtel Yafunguka Mazito

$
0
0
Sakata la Airtel, TTCL Lazidi Kupamba Moto Airtel Yafunguka Mazito
Wakati TTCL ikisema mchakato wa kuirudisha Airtel mikononi mwake utakuwa ni vita kubwa, kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa nyingi za kampuni hiyo ya simu za mkononi, imejitokeza na kusema, “Uwekezaji wetu ulifuata na kuzingatia sheria na taratibu kabla haujapata baraka zote za Serikali ya Tanzania.”

Jana, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Omary Nundu akiwa ameambatana na menejimenti ya shirika hilo alizungumza na vyombo vya habari na kusema: “Tunaenda vitani na tunajua hii ni vita kubwa.”

Mbali ya taasisi hizo mbili, mwandishi wetu alizungumza na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya Airtel Tanzania, Jaji Joseph Warioba kuhusu mzozo huo wa hisa na kusema Serikali ndiyo inayopaswa kuulizwa juu ya suala hilo kwani ndiyo yenye mkataba.

Juzi, Rais John Magufuli alimuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kufuatilia utata uliopo kwenye umiliki wa Airtel akisema kampuni hiyo ni mali ya Serikali.

Jaji Warioba aliyeiongoza bodi iliyovunja uhusiano uliokuwapo kati ya TTCL na kampuni ya Celtel na kuunda kampuni mbili tofauti alisema: “Hayo mambo iulizwe Serikali kwa sababu ndiyo ilikuwa na mkataba. Bodi haikutengeneza mkataba, ilichofanya ni kutekeleza makubaliano kati ya Serikali na Airtel.”

Mgogoro wa umiliki wa kampuni ya Airtel unatokana na uamuzi wa wakurugenzi sita waliohudhuria kikao cha bodi ya TTCL kilichoketi Agosti 5, 2005 pamoja na wawakilishi wawili wa menejimenti ya kampuni hiyo.

Akimwakilisha Jaji Warioba, kumbukumbu zilizopo ambazo Mwananchi imezithibitisha, zinaonyesha kiliongozwa na Omari Issa aliyekuwa mwenyekiti. Wajumbe wawili wa bodi hiyo walihudhuria ambao ni Yona Killagane na Agnes Bukuku huku Werner Ruessel akishiriki kwa njia ya masafa ya mtandao (teleconferencing).

Licha ya Jaji Warioba, wajumbe wengine wawili wa bodi hiyo walituma wawakilishi wao. Tito Alai aliwakilishwa na Moez Daya huku Edward Mwakyembe akizungumza kwa niaba ya Felix Mrema. Pamoja nao, alikuwapo aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TTCL, George Mbowe na mwanasheria wa kampuni, Gilder Kibola.

Nusu ya wajumbe wa bodi hiyo walioteuliwa kwa mujibu wa sheria wakishirikiana na wawakilishi wakurugenzi waliokuwa dharura, siku hiyo walipitisha uamuzi ambao miaka 12 baadaye umeishtua Serikali.

Kwa mujibu wa wajumbe hao, mustakabali wa TTCL uliandaliwa, na Jaji Warioba anasema mkataba uliojadiliwa ulikuwa kati ya Serikali na kampuni ya Airtel.

Kumbukumbu

Kikao hicho kilikuwa ni matunda ya uwekezaji uliofanywa mwaka 1998, TTCL ilipoanzisha kampuni tanzu ya Cellnet ambayo ilifanya kazi mpaka Mei 7, 2001 ilipobadilishwa jina na kuitwa Celtel Tanzania huku umiliki wake ukiendelea kuwa chini ya TTCL kwa asilimia zote.

Mtaji wa Dola milioni tano za Marekani (zaidi ya Sh11 bilioni za sasa) uliwekezwa. Lakini, January 31, 2002 ikiendelea kuwa chini ya umiliki wa TTCL ilikopa Dola za Marekani 82 milioni (zaidi ya Sh180.4 bilioni) ili kukuza mtaji.

Wakati mkopo huo unachukuliwa, TTCL ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na kampuni ya Mobile System International Celluler Investments Tanzania (MSI) ya Uholanzi. Serikali ilikuwa na asilimia 65 ya hisa zote na mbia huyo asilimia 35 zilizosalia.

Miaka mitatu baadaye, mwaka 2005 mabadiliko yalifanywa kwenye bodi ya wakurugenzi wa Celtel na kuunda kampuni mbili tofauti, Celtel ikitenganishwa na TTCL.

Kutokana na mabadiliko hayo, Celtel iliwekwa chini ya umiliki wa MSI ambayo Septemba, 2007 iliuza hisa zake kwa Zain ambayo nayo baada ya miaka mitatu, iliziuza kwa Bharti Airtel, June 8, 2010.

Bodi mpya

Kukamilika kwa kikao hicho kulimaanisha kuvunjwa kwa bodi ya wakurugenzi na kuundwa kwa uongozi mpya utakaosimamia shughuli za Celtel.

Makubaliano yaliyoafikiwa yanaeleza kuwa wajumbe wapya walitangazwa na kuchukua majukumu ya menejimenti na ilipewa miezi sita, pamoja na mambo mengine, kupendekeza meneja atakayesimamia shughuli za kila siku za kampuni hiyo mpya ya mawasiliano nchini ya Celtel.

Kama mkataba ulivyokuwa unasema; Serikali ilimteua Agnes Bukuku, Profesa Mathew Luhanga, George Mbowe na Amina Salum Ali huku MSI ikimteua Jaji Warioba kutetea masilahi yake ndani ya kampuni hiyo.

Hata hivyo, Serikali haijaridhishwa na namna umiliki ulivyobadilishwa baada ya Celtel kutenganishwa na TTCL kwani ilipewa hisa chache tofauti na ilivyostahili jambo linalomaanisha mbia mwenza aliyepo hivi sasa, Bharti Airtel, ndiye anayenufaika zaidi na uwekezaji uliofanywa.

TTCL

Msimamo wa shirika hilo la mawasiliano Tanzania kwa mujibu wa Nundu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano katika Serikali ya Awamu ya Nne ni kwamba hivi sasa hawahitaji tena mgao, bali wanataka Airtel irudishwe katika kampuni ya Serikali.

Kwa kutambua hadhi na weledi wa baadhi ya wajumbe walioshiriki kufanya uamuzi unaoonekana ulikiuka taratibu pamoja na ukubwa wa mbia mwenza, mwenyekiti huyo wa TTCL anaona mchakato wa kuzirudisha hisa hizo ni sawa na vita.

Ni vita ambayo Waziri Mpango atatakiwa kuandaa mazingira ya kuishinda baada ya kupewa agizo la kufuatilia umiliki huo na Rais Magufuli na kuhakikisha Airtel inarudi mikononi mwa Serikali.

Ili kuhakikisha kwamba vita hiyo inafanikiwa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema menejimenti na wafanyakazi wa kampuni hiyo watatoa ushirikiano na ushahidi unaohitajika kuhakikisha Airtel inarudi mikononi mwao.

Alifafanua kwamba, endapo kampuni hiyo ingekuwa mikononi mwa TTCL tangu mwanzo, mpaka leo ingekuwa imetoa mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania kwa kutoa gawio serikalini, ajira kwa wananchi na kukuza mchango wa sekta ya mawasiliano nchini.

Akitoa mfano alisema, katika robo mwaka iliyoishia Septemba, TTCL ilipata faida ya Sh2.6 bilioni kabla na Sh1.8 bilioni baada ya kodi na mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, inatarajia kutoa gawio la Sh1 bilioni kwa Serikali.

“Faida hiyo ni ya TTCL, tungekuwa pamoja na Airtel tungekuwa mbali kiuchumi,” alisema.

Kutokana na ushahidi aliosema kampuni yake inao, Kindamba aliitaka menejimenti ya Airtel kuirudisha Airtel mikononi mwa TCCL kwa kuwa upatikanaji wake haukuwa halali.

“Kampuni yoyote iliyoanzishwa kwa njia haramu haiwezi kuendelea kuwa halali. Tunataka wairudishe bila kukwaruzana na kama wanataka hivyo tutapita huko.

“Ila hatutaki tufike huko, Watanzania wajue. Tunaitaka kwa njia bora kampuni hii irudishwe,” alisema.

Juzi, akizindua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Rais Magufuli alisema kwa taarifa alizonazo, Airtel ni mali ya Serikali chini ya umiliki wa TTCL.

“Palifanyika mchezo wa ovyo, sasa sitaki kuzungumza mengi, fuatilia hilo (Waziri wa Fedha, Dk Mpango). Nchi hii ilikuwa ya maajabu sana, unachukua share (hisa) leo, kesho inauzwa kwa Dola moja, maajabu,” alisema.
CHANZO:MWANANCHI

Dudu Baya Ameiomba Serikali Kuwachukulia Hatua Kali za Kisheria Gigy Money, Amber Lulu Kabla ya 2018

$
0
0
Dudu Baya Ameiomba Serikali Kuwachukulia Hatua Kali za Kisheria Gigy Money, Amber Lulu Kabla ya 2018
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Dudu Baya ameitaka serikali kupitia Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kuwachukulia hatua wasanii wote ambao wameenda kinyume na maadali kwa mwaka 2017 ili mambo hayo yasije kujirudia mwaka 2018.

Dudu Baya akizungumza na E-Newz ya EATV amesema baadhi ya wasanii kwa mwaka huu wameitumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuweka picha zisizo na maadili kitu ambacho kimefanya jambo hilo kujadiliwa kuliko muziki wao.

“Watu kama kina Nuh Mziwanda wanapiga picha za uchi uko na Shilole kipindi kile uko bafuni unaoga kuna aja gani kuonyesha mashabiki wako, kuna mtu gani asiyeoga hapa duniani. Ukija kama suala la mdogo wangu Young Dee namkubali sana lakini alipiga picha na Amber Lulu za kumshika makalio, huo ni ujinga,” amesema Dudu Baya.

Dudu Baya ameendelea kwa kusema wasanii watumie mitandao kwa manufaa ya kibiashara na endapo wakishindwa basi sheria ichukue mkondo wake.

“Nabahatika nakutana na Amber Lulu au Gigy Money namwambia ebu kaza kwenye kipaji chako ebu achana na upuuzi, sasa hivi mabinti wanaotaka kuingia kwenye movie au muziki wasije kwa njia walizopitia Amber Lulu na Gigy,” amesema.

“Kama 2017 yamefanyika sana, ni serikali au Basata kuja na tamko, hao ni watu wa kutolea tamko atakayeenda kinyume basi sheria ifuate mkondo wake, siyo wakati wakuonyana ni wakati wa tamko kabla ya kuingia 2018,” amesisitiza.

Serikali Kuzifutia Leseni Kampuni 12 za Madini

$
0
0
Serikali Kuzifutia Leseni Kampuni 12 za Madini
Serikali imewashukia wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambao hawalipi kodi na imelenga kufuta leseni zote kwenye migodi hiyo isiyolipa kodi Serikalini.

Hadi hivi sasa kampuni  12 za wachimbaji hao wa madini ya Tanzanite, zinadaiwa  zaidi ya Sh3bilioni na zitakazoshindwa kulipa kodi hiyo zitafutiwa  leseni zao na wizara ya madini.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema leo Desemba 22  mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, wakati akizungumza na wafanyabiashara na wamiliki wa migodi ya madini ya Tanzanite.

Mnyeti alisema Serikali haiwezi kung'ang'ania kampuni moja ya TanzaniteOne pekee kwenye kuingiza kodi ili hali zipo kampuni nyingine ambazo hazilipi kodi kwa kisingizio cha kutozalisha madini hayo .

Alisema wachimbaji hao wanamiliki kampuni za uchimbaji na wanachimba kwa teknolojia kama kampuni ya TanzaniteOne lakini hawalipi chochote serikalini.

"Serikali inanyonya kwenye TanzaniteOne kuingiza mapato hawa wengine hawalipi kodi, sasa ni lazima tukubaliane madeni hayo yanalipwaje na watakaoshindwa watafutiwa leseni, zao," alisema Mnyeti.

Alisema kampuni itakayoshindwa kulipa kodi itapisha eneo hilo kwani miaka yote wanachimba hawalipi kodi ya serikali na mapato yote wanaondoka nayo kwa kisingizio kuwa hawajapata chochote.

"Tuliunda tume ya kuchunguza hizi kampuni na tukabaini hazilipi  kodi, sasa sisi serikali tukishindwa kusimamia kodi ili wananchi wapate maendeleo ni bora tukalale nyumbani na kulima viazi kuliko kushindwa kukusanya kodi," amesema  Mnyeti na kuongeza.'

"Mapato yote wanayopata wanaondoka nao na serikali haipati chochote ukimuuliza eti hajawahi kupata sasa kama haujapata ni bora uondoke , kamishna wa madini nadhani unanisikia vizuri, nitakuletea majina ya wanaoshindwa kulipa kodi ufute leseni zao," amesema

Hata hivyo, alisema madini ya Tanzanite yanapaswa kuwa baraka na siyo laana hivyo yanatakiwa kutumika kwa ajili ya kuwatetea maendeleo ya watanzania na kuleta tija kwa Taifa.

Naibu Waziri wa Madini Ladslaus Nyongo amesema  wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuona wajibu wa kufuata sheria za nchi ikiwemo kulipa kodi za serikali na mrabaha kwa uhuru na uwazi kabisa.

Nyongo amesema  serikali imelenga kufanya mji mdogo wa Mirerani kuwa kitovu cha biashara ya Tanzanite duniani.

Alisema wadau wa madini wanapaswa kuwekeza kwenye huduma muhimu kama vile hoteli za kisasa, mabenki, maduka ya kisasa na huduma nyingine.

Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne, Hussein Gonga amesema anashukuru uamuzi wa Rais John Magufuli kuagiza mnada wa madini kufanyika eneo linalochimbwa madini hayo.

Gonga amesema  jamii inayozunguka eneo hilo imenufaika kupitia mnada huo kwa kufanya biashara mbalimbali kwa wadau wa madini ikiwemo nyumba za kulala wageni, vyakula, vinywaji na mengineyo.

Shahidi wa Akiri Kumpigia Kura Lema Ingawa Yeye ni Mwana CCM

$
0
0
Shahidi wa  Akili Kumpigia Kura Lema Ingawa Yeye ni Mwana CCM
Shahidi wa pili katika kesi ya kudaiwa kumdhalilisha Rais John Magufuli inayomkabili mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kuwa ingawa yeye ni mwanachama wa CCM, mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu alimpigia kura mshtakiwa huyo.

Shahidi huyo Masoud Rajab (41) mkazi wa Kata ya Muriet aliieleza Mahakama kuwa Juni 22 2016 akiwa mwanachama wa CCM alihudhuria mkutano uliotishwa na mbunge huyo kama mwananchi wa kawaida.

“Sina kumbukumbu na nambari ya kadi yangu ya CCM na sikumbuki niliichukulia wapi, lakini mwaka 2015 nilimpigia kura Lema,” alisema shahidi huyo.

Akijibu swali aliloulizwa na wakili wa upande wa utetezi, John Mallya kwamba alikwenda kutafuta nini katika mkutano huo uliofanyika Kata ya Ngarenaro ihali yeye ni mkazi wa Muriet, alisema alipata taarifa kuwa kuna mkutano.

Rajab aliieleza Mahakama hiyo kuwa alipofika katika mkutano huo alishtuka kusikia maneno yakitamkwa na mbunge wake yanayosema Rais Magufuli anabana demokrasia na kwa kubana demokrasia atasababisha umwagaji wa damu.

Alidai maneno mengine aliyosikia ni kwamba endapo ataendelea watu vifua vitawajaa na ipo siku vitalipuka na siyo jeshi au polisi wataweza kuzuia.

Akijibu swali kutoka kwa wakili Mallya kwamba anaelewa nini kuhusu maneno vifua vitawajaa na umwagaji wa damu, shahidi huyo alisema anaelewa ni hasira na kuchuruzika kwa damu.

Rajab alidai kuwa baada ya kusikia kauli ya umwagaji wa damu, alikosa amani na kuamua kwenda kituo kikuu cha polisi saa mbili usiku kufungua jalada la mashtaka.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images