Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live

Lijuakali Aachiwa kwa Dhamana Polisi Yafunguka Sababu ya Kumkamata

$
0
0
Lijuakali Aachiwa kwa Dhamana Polisi Yafunguka Sababu ya Kumkamata
Mbunge wa jimbo la Kilombero kupitia Peter Lijualikali ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa na maofisa wa polisi akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.

Kabla ya kuachiwa kwa dhamana Lijualikali ambaye anakabiliwa na kesi iliyoko mahakamani ya ushawishi na kuchoma moto ofisi ya serikali ya kijiji cha Sofi Malinyi amehojiwa kwa saa kadhaa katika kituo cha polisi mkoani Morogoro.

Akieleza leo Desemba 22  sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema anatuhumiwa kwa kosa la kimtandao ambalo ni kusambaza picha za mtu anayedai kuwa anataka kumuua jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kamanda Matei amesema kuwa baada ya kuhojiwa kwa kina wameamua kumuachia kwa dhamana hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tuhuma hizo na upo uwezekano wa kumfikisha mahakamani.

Lijualikali, Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Kilombero na wenzao 55 jana (Desemba 21) walifika mahakamani hapo ambapo wanashtakiwa kwa makosa nane likiwemo la kuchoma moto ofisi ya kijiji cha Sofi Malinyi Oktoba 26 mwaka huu.

Hii ni awamu ya pili Lijualikali kufikishwa mahakamani ambapo awamu ya kwanza alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kilombero kwa kosa la kufanya vurugu na baada ya kutiwa hatiani alihukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita.

Umoja wa Mataifa Wapuuza Vitisho vya Trump

$
0
0
Umoja wa Mataifa Wapuuza Vitisho vya Trump
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekaidi vitisho vya Serikali ya Marekani na kupiga kura ya ndiyo kuidhinisha azimio linalotupilia mbali tangazo la Rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel.

Nchi wanachama 128 zilipiga kura ya ndiyo dhidi ya kura tisa zilizopinga, huku nchi 35 zikijiondoa kupiga kura.

Baada ya kura, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley aliyashukuru mataifa 65 yaliyopinga azimio hilo, yaliyojizuia kupiga kura au hayakuwapo wakati wa kupiga kura.

Marekani, Togo, Honduras na Guatemala ni mataifa ambayo yalipiga kura kupinga azimio hilo.

Mataifa ya Canada, Mexico, Rwanda, Uganda, Poland, Jamhuri ya Czech na Romania hayakupiga kura.

Kabla ya kura, Marekani ilitishia kuzuia misaada kwa mataifa yatakayopiga kura kuunga mkono azimio hilo.

Haley amesema kura hiyo haitabadilisha kitu katika mipango ya Marekani kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem kutoka Tel Aviv.

Kim Jong-un Ajitapa Korea Kaskazini ni Tishio kwa Marekani

$
0
0
Kim Jong-un Ajitapa Korea Kaskazini ni Tishio kwa Marekani
Katika siku ambayo baraza la usalama la Umoja wa mataifa linapiga kura kuidhinisha vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea kaskazini, kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-un, amesema taifa lake linawakilisha tishio kubwa la nyuklia kwa Marekani.

Katika hotuba iliyoripotiwa na shirika la utangazaji habari nchini (KCNA) Kim amesema kuendelezwa kwa haraka kwa mpango wa nchi yake wa nyuklia kunashinikiza ushawishi muhimu katika siasa za kimataifa.

Azimio la hivi karibuni la baraza hilo la usalama katika Umoja wa mataifa linalenga kupiga marufuku usafirishaji wa bidhaa zote za mafuta kwenda Pyongyang na kuitisha kurudishwa kwa raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika nchi za nje katika muda wa mwaka.

CUF ya Maalim Seif Yapeta Mahakamani

$
0
0
CUF ya Maalim Seif Yapeta Mahakamani
Mahakama ya Rufaa Tanzania imekubali maombi ya Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho,Maalim Seif Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017 kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo kusikiliza shauri la msingi.

Taarifa hiyo ya maamuzi ya mahakama ya Rufaa, imetolewa mapema leo Disemba 22, 2017 kwa vyombo vya habari na Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF, Mbarala Maharagande.

“Mahakama ya Rufaa imeipa ushindi Maombi ya Bodi ya Wadhamini ya CUF chini ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017 (From Civil Application No.23/2017) kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo kusikiliza shauri la msingi tajwa hapo juu.

“Shauri hili ndilo linalohoji uhalali na mamlaka ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kumrejesha Lipumba katika nafasi ya Uongozi ndani ya CUF baada ya kujiuzulu na kukubaliwa kujiuzulu kwake na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF uliofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza Tarehe 21 August, 2017,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Jaji wa Mahakama ya Rufaa , Jaji Musa Kipenka amekubaliana na hoja za Mawakili Wasomi wa CUF Halfani Daimu, Juma Nassoro na Hashimu Mziray walizozitoa Mbele ya Mahakama hiyo.

Maharagande amesema, maamuzi hayo yanaipa nafasi mahakama kuu kuendelea kusikiliza shauri hilo ambalo Msajili wa Mahakama Kuu ameshalipangia jalada ambalo linasikilizwa mbele ya Jaji Wilfred Ndyansobera.

Dk. Tulia Ataka Mambo ya Siasa Zitengwe

$
0
0
Dk. Tulia Ataka Mambo ya Siasa Zitengwe

Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amefanya ziara katika baadhi ya maeneo wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya kutekeleza baadhi ya ahadi alizotoa na kusema kwamba lazima mambo ya maendeleo yatengwe mbali na siasa kwani rais wa nchi anapiga marufuku tendo hilo.


Dk Tulia amesema hayo wakati akitoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni tano katika shule ya sekondari Bujela

"Niwasihi jambo moja ambalo hata Rais Magufuli husisitiza, tusiingize siasa kwenye mambo ya maendeleo kwasababu  bila hivyo hatutapiga hatua, leo kama TULIA TRUST tuliahidi vifaa vyenye thamani ya Milioni tano na tayari tumetekeleza kwa kuja navyo vikiwemo bati, mbao, mchanga, saruji, chokaa, rangi, vioo, nondo," amesema Dk. Tulia

“Tunafanya haya yote kwa ajili ya kuhakikisha tunawatengenezea watoto wetu mazingira mazuri ya kujisomea na baadae watuletee maendeleo sisi wazazi wao hivyo niwaombe viongozi wote tushikamane,” Dk Tulia.

Pamoja na hayo Dk. Tulia alifika katika kanisa la Bujela ambalo liliharibiwa kwa upepo uliosababishwa na mvua na kuchangia jumla ya mabati 100 yenye thamani zaidi ya milioni mbili Kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa kanisa hilo ambalo tayari ujenzi wake ulianza kwa jitihada za waumini wenyewe.

Dk. Tulia amewahimiza waumini pamoja na viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa la Tanzania amani pamoja na kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kuiongoza nchi salama.

Mmh..... Hapa Ndipo Yalipofikia ya Zari, Mobetto Watunishana Misuri Waitana Mbu na Tembo

$
0
0
Mmh..... Hapa Ndipo Yalipofikia ya Zari, Mobetto Watunishana Misuri Waitana Mbu na Tembo
Usiku wa kuamkia leo kwenye jiji la Kampala Uganda kulifanyika Party mbili ambapo moja Hamisa Mobetto alihudhuria inaitwa Gal Power na nyingine ni ya Zari All White Party.

Sasa baada ya kumalizika kwa party hizo maneno ya Mashabiki yakaanza wengine wakiponda ya Zari na wengine wakiponda ya Hamisa kwamba ilikua na watu wachache.

Wao wenyewe wameandika vitu kwenye Snapchat zao na ikaonekana kama ni vijembe ambapo Zari ndio alianza kwa kuandika “Kuna tofauti kati ya Tembo na Mbu” ambapo Hamisa alijibu kwa kuandika “Tembo hana madhara sana kwa Binadamu ila mbu….. kila siku watu wanalazwa”


Diamond Atoa Ushauri Alioutoa “Ili Ufanikiwe ni Lazima Udhalilike Kwanza”

$
0
0


Diamond Atoa  Ushauri Alioutoa “Ili Ufanikiwe ni Lazima Udhalilike Kwanza”
December 22,2017 Mwimbaji wa Tanzania Diamond Platnumz ameandika maneno 53 ikiwa ni saa chache baada ya Mama Watoto wake Hamisa Mobetto na Zari kufanya party Kampala Uganda kwenye sehemu mbili tofauti ndani ya usiku mmoja.



“Ili ufanikiwe ni lazma Udhalilike kwanza… yaani lazima uwaonyeshe watu kuwa kitu fulani mie nakiweza… na katika kuwaonyesha huko kuna wengine watakudharau, watakubeza na kukucheka….ila kuna wengine watakipenda, watathamini, kukikubali na kukupa nafasi”

“Maisha ndio yako hivyo… Kadri unavyozidi kuogopa na kuona “watanichukuliaje” ndio unazidi kuchelewa kufikia ndoto zako…..amka sasa ukawaonyeshe”

kutoka na caption hiyo aliyoiandika Damond Platnumz imetafsiriwa kuwa ni maneno ya kumtia moyo mzazi mwenzake Hamisa Mobetto baada ya watu kusema party ya Hamisa haijajaza watu wengi kama party ya Zari the boss lady ambazo zote zilifanyika usiku wa December 21,2017.

Nimepokea Taarifa za Kuhuzunisha Kuhusu Bondia Floyd Mayweather

$
0
0
Bondia asiyepigika Floyd Money Mayweather hatimaye amekubali kufanya rematch na Conor McGregor ila safari hii haitakuwa boxing tena bali UFC kwa dau la 1 billion USD

Na hatoishia kwa Conor tu bali atapambana na mabondia wengine watatu wa UFC kwa dau lisilopungua pia 1 billion usd

Kiukweli natamani haya mapambano Floyd ayavunje tu hao jamaa wa UFC wanamtamani kweli kwa kuwa wamemshindwa kwenye boxing sasa wamemualika kwao kwa kumdanganya na dau nono na mwishoe Floyd amewakubalia.

Hizi tamaa za Floyd zimenikwaza sana mimi kama shabiki wake nambari moja ulimwenguni

Falsafa zake Floyd ipo siku zitamtokea puani , yeye husema kuwa haangalii sana kupoteza pambano yeye huangalia pesa atakazo ingiza baada ya pambano.

Lakini siku zote bwana pesa huisha ila heshima uliyojiwekea na kuitunza kamwe haiwezi kuisha au kushuka.

Sasa kwa mwendo huu naona kabisa ile record yake ya undefeated inaenda kupotea.

By Hance Mtanashati/JF

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0

MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na Nasi kwa Namba; 0783140065

Upelelezi juu ya Mauaji ya Kimbari Rwanda Umekamilika...Kagame Naye Katuhumiwa Kuhusika

$
0
0
Majaji nchini Ufaransa wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na Rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba Rais wa wakati huo wa Taifa hilo, Juvenal Habyarimana 1994.

Hii ni baada ya upelelezi juu ya suala hilo kukamilika. Upelelezi huo ulikuwa unafanywa na Majaji hao wa Ufaransa juu ya shambulio la kombora lililosababisha kifo cha Rais Habyarimana na baadaye kusabisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka huo huo.

Hata hivyo Rwanda nayo inawalaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari.

Upelelezi huu umesababisha mitafaruku kati ya Rwanda na Ufaransa jambo lililosababisha kuvunja uhusiano wao wa kidiplomasia mwaka 2006.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Hamisa Mobetto na Zari Warushiana Vijembe? Wapeana Majina ya Wanyama

$
0
0
Usiku wa kuamkia leo kwenye jiji la Kampala Uganda kulifanyika Party mbili ambapo moja Hamisa Mobetto alihudhuria inaitwa Gal Power na nyingine ni ya Zari All White Party.

Sasa baada ya kumalizika kwa party hizo maneno ya Mashabiki yakaanza wengine wakiponda ya Zari na wengine wakiponda ya Hamisa kwamba ilikua na watu wachache.

Wao wenyewe wameandika vitu kwenye Snapchat zao na ikaonekana kama ni vijembe ambapo Zari ndio alianza kwa kuandika “Kuna tofauti kati ya Tembo na Mbu” ambapo Hamisa alijibu kwa kuandika “Tembo hana madhara sana kwa Binadamu ila mbu….. kila siku watu wanalazwa”

Mambo ya Kufahamu DSM ”NO DISKO TOTO”, Kama Unapanga Kufyatua Fataki Wakati wa Mwaka Mpya Hii ikufikie

$
0
0
Kamanda wa Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa leo December 22, 2017 amezungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya usalama katika kipindi hiki cha sikukuu ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku Disco toto.

Ameeleza kuwa wamefanya utafiti na kugundua kuwa hakuna ukumbi hata mmoja unaokidhi vigezo vya kuingiza watoto kwa ajili ya disco na wakawa salama hivyo kwenye msongamano huo wa watoto madhara yanaweza kutokea.

“Tumetenga eneo la Tanganyika Peakers maalumu kwa kusherehekea kwenye usiku wa mkesha wa mwaka mpya na kwa wanaotaka kufyatua fataki wakafyatue kwenye eneo hilo kwa muda wa nusu saa baada ya saa sita kamili, watakaokiuka watachukuliwa hatua.” – Kamanda Mambosasa

Tazama VIDEO:

FULL VIDEO: Party ya Hamisa Mobetto Uganda GAL POWER 2017

$
0
0
AyoTV na millardayo.com usiku wa December 21 2017 zilinasa matukio yote yaliyofanyika katika party ya Hamisa Mobetto “Girl Power Women Empowerment Event” Kampala Uganda. VIDEO:

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0

HARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670  

Kisa Kuolewa na 'Kiben Ten' Mama Mobeto Ampa Makavu Mama Daimond

$
0
0
Kisa Kuolewa na 'Kiben Ten' Mama Mobeto Ampa Makavu Mama Daimond
MAMA mzazi wa Mwanamitindo maarufu Bongo Hamisa Mobeto, Shufaa Lutigunga amefunguka kuwa hayuko tayari kuolewa na “Serengeti Boy” wakati watu wazima wenzie wapo, kitendo ambacho kimetafsiriwa kuwa ni kumchana mama Esma.

Akizungumza na Risasi Jumamosi Mama Mobeto alisema kuwa, sasa hivi ameshakuwa mtu mzima na ni bibi mwenye wajukuu hivyo kuolewa na kijana mdogo ni kujishushia hadhi kama mama na bibi pia.

“Jamani mimi kama ni kuolewa basi nitaolewa na mtu mzima mwenzangu kwasababu Serengeti Boy kwangu haiwezekani, nahitaji kuolewa kweli ila nitaolewa na mzee mwenzangu ili wajukuu wapate babu,” alisema Mama Mobeto ambaye kwa kuongea hayo ni kama amemchana mama Esma amefunga ndoa hivi karibuni na kijana anayedaiwa kuwa ni Serengeti Boy kwake

Tukio la Shilole Kumwagiwa Pombe Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa Wakwe Wakelwa Wamjia Juu

$
0
0
Tukio la Shilole Kumwagiwa Pombe Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa Wakwe Wakelwa Wamjia Juu
SIKU ya kuzaliwa kwa msanii wa muziki Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alishtukizwa kwa kumwagiwa pombe na msanii mwenzake Irine Uwoya kitendo hicho kiliwashtua wakwe zake kwani ni watu walioshika dini ya kiislamu. Risasi Jumamosi baada ya kubaini hilo kutoka kwa sosi aliyekaribu na staa huyo na familia ya ukweni kwake lilimtafuta mume wa Shilole Ashrafu Uchebe ‘Uchebe’ ambaye alilifungukia suala hilo.

“Ni kweli mke wangu amemwagiwa pombe ni kwasababu alishtukizwa wazazi wamehoji na kushangazwa na hilo lakini nimewaelewesha kuwa yeye hakulitarajia alifanyiwa bila kujua, nashukuru wameelewa,” alisema Uchebe. Aidha Uchebe alisema kuwa hata hivyo anafanya kazi kubwa ya kumbadili mkewe Shilole, kwani alipomtoa ni mbali kwa vitendo na anaamini anabadilika kila siku, Mungu akijaalia atakuwa sawa na ataendana na yeye ambaye hanywi pombe.

“Mke wangu anakunywa pombe ingawa amepunguza sana kwa sasa, kwasababu ya mimi kumbadili ila bado naifanya kazi ya kumbadili siku hadi siku naamini atakaa sawa, nadhani hiyo ndio sababu ya wasanii wenzake kummwagia pombe,” alisema Uchebe.

Wajanja Wamshikisha Adabu Nisha, Wampokonya Mabwana Zake Wawili Wamshushia Mvua ya Matusi

$
0
0
Wajanja Wamshikisha Adabu Nisha, Wampokonya Mabwana Zake Wawili Wamshushia Mvua ya Matusi
MSANII maarufu wa Bongo Movie ambaye huitendea vyema tasnia hiyo hasa akicheza scene za komedi, Nisha ameibuka na kueleza kusikitishwa kwake na kitendo cha kupokonywa mabwa zake wawili kwa nyakati tofauti kisha mhusika kumshushia mitusi hadharani.

Nisha kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

“Halafu me nimepooza kweli, nimechukuliwa wanaume mara mbili nikanyamaza kimya, hata kuna aliyeniibia akajifanya mbabe kuja kunichamba kwenye page yangu eti kama wa kwangu kwa nini sijatangazwa naye

“Nikamnyamazia hajui niling’atwa na nyoka sikutaka na yule anipe sumu ingine ningekufa kwa kipindi kile kuweka mahusiano nje ni mimi sikutaka, na nilijua hata yake yake yasingedumu.

“Natamani 😂yangejirudia sa hivi nichambane,nitupiane vidongo km Tanzania na Uganda 😂 KUMBE INAWEZEKANA EE 😐bad lucky wa sasa simwaniki maana ndo nishapiga nanga musije mbeba naye 😐,” ameandika Nisha.

Aidha Nisha hajabainisha ni mabwana wapi aliyopokonywa na alipokonywa na nani.

 

Mr Poul Afunguka Chanzo cha Kuachana na Music

$
0
0
Mr Poul Afunguka Chanzo cha Kuachana na Music
Msanii wa muziki wa bongo ambaye ni miongoni mwa wasanii wachache walioanza na game ya bongo Fleva, Paul Mbena maarufu kama Mr. Paul, ameweka wazi sababu iliyomfanya yeye aache muziki.


Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live, Mr. Paul amesema kipindi ambacho wao walikuwa wanafanya muziki kulikuwa na changamoto nyingi ambazo alishindwa kuhimili, na kuamua kukaa pembeni kwa muda kufanya mengine.

“Kipindi ambacho sisi tunaanza muziki soko halikuwa kama sasa hivi, kuliwa na frustration nyingi, nikaachana nao kwanza nikarudi shule nikapiga degree kisha masters nikaingia ofisini, lakini sasa hivi naona vitu vimebadilika, watu wengi wana smart phones wanadownload nyimbo ikitoka tu, naona vijana wana chance kubwa ya soko”, amesema Mr. Paul

Mr. Paul ameendelea kwa kusema kwamba sasa hivi ana mpango wa kurudi kwenye game ya bongo fleva, na yuko tayari kushirikiana na wasanii wa sasa ili kupata kazi zenye ubora zaidi.

“Kama kuna uwezekano wa kuandikiwa muziki, nitawaacha waniandikie kama kuna masuala ya kulipa pesa nitalipa waniandikie ili niweze kwenda nao sawa”, amesema Mr. Paul

Mali za CCM Zamtokea Puani Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha

$
0
0
Mali za CCM Zamtokea Puani Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha
Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Ole Sabaya ambaye amesema alifunguliwa kesi nne kwa sababu ya kutetea mali za CCM na kudai wapo viongozi wa Chama na Serikali ambao wanahusika na ufujaji wa mali za Chama.


Lengai amefunguka hayo ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kuunda kamati itakayoweza kuchunguza mali za CCM, ambapo amesema yeye kupewa kesi za kufoji vitambulisho ni kwa sababu ya kupigania mali za Chama na kumshukuru rais kwa alichokifanya.

Lengai amesema kwamba akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha alitangaza kiama kwa wezi wa mali za UVCCM Arusha ambapo aanaamini katika wezi hao wapo viongozi wa CCM na Serikali

"Chama cha Mapinduzi ambacho kinajiita chama kikubwa kwa bara la Afrika na kiendelee kuomba omba kwa sababu tu kuna viongozi wameteka nyara mali zake. Rais tunamuheshimu sana kwa juhudi hizo muda unafika itajulikana ipi ngano na yapi magugu na hata sababu za ugomvi na migogoro kwenye UVCCM Arusha uliokuwepo" amesema Lengai

Sabaya ameongeza kwamba siku ya kwanza wakati akiwa anapelekwa mahakamani ni muda mchache aliokuwa ametangaza kiama kwa wezi wa mali za CCM na kuahidi kwamba Kamati iliyoundwa na Rais ikifika Arusha atawapa ushirikiano.

"Leo niseme ukweli Siku ya kwaza nipelekwa mahakamani siku ambayo muda mchache uliopita niliwatamgazia kiama wezi wa mali za UVCCM kwa Mkoa wa Arusha. Nilijua kwamba wapo viongozi wa Serikali na CCM wanahusika kwa kwa kushindwa kuzuia kwa nafasi zao, huo ni uzembe basi itakuwa walihusika moja kwa moja... ghafla nikashangaa ninaitwa kwa kesi za hovyo zisizo na kichwa wala miguu kuhusu vitambulisho. Tatizo halikuwa vitambulisho bali mali za CCM," Lengai
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live




Latest Images