Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live

Maneno ya Manara Baada ya Simba Kutolewa Michuano ya Azam Cup "Hii ni Aibu ya Mwaka Haivumiliki"

$
0
0
Maneno ya Manara Baada ya Simba Kutolewa Michuano ya Azam Cup "Hii ni Aibu ya Mwaka Haivumiliki"
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kitendo cha klabu yake ya Simba jana kufungwa kwa njia ya penati na kuondolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup ni aibu ya mwaka.


Haji Manara alisema hayo jana baada ya waliokuwa mabingwa watetezi wa (Azam Sports Federation Cup) Simba kupigwa na Green Warriors na kuondolewa katika michuano hiyo kwa penati 4-3

"Shame!! Aibu!!!Fedheha!!! Haivumiliki!!!Tumewakera fans wetu zaidi ya twenty millions... nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba..Aibu ya mwaka" aliandika Haji Manara
 

Patit Man Aweka Wazi Sababu ya Kumuacha Bill Nass

$
0
0
Patit Man Aweka Wazi Sababu ya Kumuacha Bill Nass
Aliyekuwa meneja wa Billnass amevunja ukimya baada ya kuiambia eNEWZ kuwa amejitoa kwenye lebo ya LFLG ambayo ni ndiyo iliyokuwa ikimsimamia mwanamuziki Billnass na kuanzisha lebo yake mwenyewe

Akiongea mbele ya camera ya eNEWZ Petit ametaja sababu kubwa ya kujitoa katika kundi hilo ni kuwa ameamua kuijitegemea na kuaanzisha  lebo yake mwenyewe inayojulikana kama "Roof Top" licha ya watu kusema kuwa yeye na Billnass wameachana kwa uhasama mkubwa.

"Ni kweli mimi simsimamii tena Billnass lakini tuko poa na hakijaharibika chochote wala hatuna ugomvi na yeye pamoja na Mchafu. Ni mfumo wa kazi tu umebadilika na hakuna chochote kibaya na maskani pale bado ninaenda kama kawaida. Nina kampuni ambayo naimiliki mimi na mtu mwingine anayeitwa John Tojo. Kwa hiyo "Roof Top" nimeingia nao 'share',"

Hata hivyyo Petit amesema kuwa bado ataendelea kumsapati Billnass kwa kuwa walikuwa ni washkaji toka zamani kabla hata hajaanza kumsimamia.

Wataka Rais Magufuli Aunde Tume Kuchunguza Ubinafsishaji Sakata la Airtel

$
0
0
Wataka Rais Magufuli Aunde Tume Kuchunguza Ubinafsishaji Sakata la Airtel
Sakata la hisa za Kampuni ya Airtel limeendelea kuchukua sura mpya baada ya Rais John Magufuli kushauriwa aunde tume huru ya kuchunguza ubinafsishaji uliofanyika ili watakaobainika wachukuliwe hatua kali.

Ushauri huo kutoka kwa wanasiasa umekuja siku mbili tangu mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Omary Nundu na menejimenti yake kuzungumza na wanahabari na kuitaka Airtel kurejeshwa TTCL na si vinginevyo.

Hata hivyo, kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa nyingi za kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu imetoa tamko ikieleza kuwa uwekezaji wake ulifuata na kuzingatia sheria na taratibu kabla haujapata baraka zote za Serikali ya Tanzania.

Jana, kwa nyakati tofauti, Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, waziri kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee na kada mpya wa CCM, David Kafulila walisema kuundwa kwa tume huru kutahitimisha mjadala na ukweli kujulikana.

Desemba 20, Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kufuatilia utata uliopo kwenye umiliki wa Airtel akisema ni mali ya Serikali.

Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini alisema kunahitajika kutazamwa mchakato mzima wa ubinafsishaji kwa kufanya ukaguzi maalumu wa sera ili kutoa mapendekezo ya kurekebisha makosa yaliyofanyika kwani jambo hilo linaweza kuzaa matunda mazuri zaidi. Alisema Serikali inaweza kuunda tume kutazama namna ubinafsishaji ulivyofanyika na kuchukua hatua za kisayansi baada ya matokeo ya kazi hiyo huku akidokeza kwamba akiwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walifanyia kazi sera ya ubinafsishaji.

“Katika kila taarifa yetu ya mwaka tulikuwa na sehemu maalumu iliyoeleza ufuatiliaji wetu wa utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji,” alisema Zitto kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa jana.

Zitto alisema ubinafsishaji wa TTCL ni suala walilolitolea taarifa mara kadhaa bungeni na ya mwisho ilikuwa Januari 2015.

“Ni ukweli usio na shaka kuwa kampuni ya Celtel (sasa Airtel) haikulipa chochote kuwezesha kumiliki hisa kwenye Celtel Tanzania na pia uuzwaji wa Celtel kwenda Zain na kisha Airtel, ulisababisha Tanzania kupoteza mapato ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax),” alisema.

Hata hivyo, alisema kunahitajika kushughulikia suala la Airtel kwa muktadha wa kazi nzima ya ubinafsishaji nchini.

Zitto alisema PAC iliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi baada ya ubinafsishaji wa mashirika kadhaa, ikiwamo Benki ya NBC na matokeo waliyawasilisha bungeni.

“Uuzwaji wa NBC nao ulikuwa ni wa bure na huwezi kushughulika na kampuni mojamoja bila kutazama muktadha mzima wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma,” alisema Zitto anaungwa mkono na Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe (Chadema) aliyesema suala la Airtel si jipya kwani iliuzwa kinyemela na walioiuza walilindwa hivyo umefika wakati wakawekwa hadharani.

“Kama dhamira ni kutaka kuanza kufanyia kazi kilichopigiwa kelele na kambi rasmi ya upinzani bungeni na iliyokuwa kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ni rahisi sana,” alisema na kuongeza, “Wote waliokuwa na dhamana ama katika shirika au wizara ambayo TTCL ilikuwa chini yake ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki katika mchakato huo wawekwe wazi na hatua zichukuliwe.”

Alisisitiza, “Mkataba wa mauzo uwekwe wazi ijulikane masilahi ya pande zote yalikuwa nini? Nani alipata au kukosa nini na kwa sababu gani na nani aliyesababisha hasara husika na kwa masilahi ya nani? Tunataka Watanzania wajue mbivu na mbichi kwa hoja zilizo mezani na sio kwa matamko.”

Kafulila ambaye ni mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisema, “Kuirudisha mali ni jambo moja na dogo, lakini waliosababisha hasara au kupindishwa kwa sheria na taratibu wanapaswa kujulikana.”

“Mimi nashauri iundwe kamati, Rais (Magufuli) aunde tume au kama Rais atashindwa, basi Waziri Mpango aunde kamati na yeye kama atashindwa basi Bunge liunde kamati teule ili kuchunguza kuanzia Celtel hadi Airtel.”

Kafulila alitolea mfano kamati iliyoundwa na aliyewahi kuwa waziri wa uchukuzi, Samuel Sitta (marehemu) kuchunguza mabehewa mabovu mwaka 2015.

“Ingawa ripoti yake haikusomwa bungeni lakini ilibaini wahusika na ndiyo hii ya Airtel na TTCL. Iundwe kamati ichunguze na ije na ukweli ili waliohusika wachukuliwe hatua,” alisema.

Waziri Kalemani Atoa Siku Kumi Jengo la Tanesco Libomolewe

$
0
0
Waziri Kalemani Atoa Siku Kumi Jengo la Tanesco Libomolewe
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la  Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro.

Waziri huyo pia  amewataka  watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo kuvunjwa.

 “Nataka kuanzia leo Desemba 22 ndani ya siku sita jengo hili lote libomoke  na kwasababu ni majengo mawili ndani ya siku kumi majengo yote mawili yawe yamebomoka kama mnaona vigumu kubomoa jengo lenu waambieni TBL ”amesema

Amesema  hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi  kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze tusiwakwamishe”amesema.

Amesema wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na kudai  Januari mosi ataenda  tena kukagua kuona kama agizo lake limefanyiwa kazi.

“Naimani wananchi hawatapata shida wakati wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya ,kwa hiyo asiruhusiwe mtumishi yoyote wa Tanesco kwenda nje ya ofisi yake wakati wa sikukuu zote mbili”amesema

 Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema wamelisikia agizo la Waziri na wataenda kulitekeleza kama lilivyo .

Siyumbishi na Ndoa Wanazofunga Waolewe tu Wakati Wangu Bado- Odama

$
0
0
Siyumbishi na Ndoa Wanazofunga Wakati Wangu Bado- Odama
MUIGIZAJI mwenye kiwango kizuri kwenye tasinia ya filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa ayumbishwi na ndoa wanazofunga baadhi ya mastaa hivi karibuni kwani wakati wake ukifika na
yake itafanyika.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Odama alisema kuwa hakuna kitu kizuri duniani kama wakati wa Mungu ambao ndio sahihi, hivyo hawezi kuona mtu amefanya kitu na yeye akatamani
kwasababu mwingine amefanya.

“Mimi naamini kabisa kila jambo lina wakati wake na wakati mzuri ni Mungu aliokupangia jambo husika, sio tu kukurupuka kwasababu mwingine kafanya,” alisema Odama

Lusekelo Atoboa Siri Chanzo cha Kuvunja Ndoa za Watu

$
0
0
Lusekero Atoboa Siri Chanzo cha Kuvunja Ndoa za Watu
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini DSM, Lusekelo 'Mzee wa Upako' amefunguka na kusema kuwa wachungaji wengi wanavunja ndoa za watu hasa pale inapofahamika kuwa mwanaume anatatizo la nguvu za kiume au mwanaume kupenda mtelezo.


Mchungaji Lusekelo alisema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji Joyce Kiria kwenye kipindi cha WANAWAKE LIVE na kusema kuwa wachungaji wengi wamekuwa wakivunja ndoa za wanandoa wengi ambao wanaume wanakuwa wamebainika kuwa na tatizo la nguvu za kiume.

"Sisi kuna kesi nyingi tumepata mfano watu walioana kumbe mwanaume hawezi tendo la ndoa, wachungaji ndoa za namna hii wanavunja nyingi tu, kwamba huyu bwana hawezi na hana nguvu za kiume wanavunja kabisa. Lakini pia yule mkatili kabisa kabisa anachengua watoto, hasomeshi watoto" alisema Mchungaji Lusekelo

Mtu Mmoja Atiwa Mbaroni kwa Kukutwa na Magamba ya Kakakuona na Nyama ya Simba

$
0
0
Mtu Mmoja Atiwa Mbaroni kwa Kukutwa na Magamba ya Kakakuona na Nyama ya Simba
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Ngerezya Chamukaga mkazi wa Kijiji cha Kanyara wilaya ya Sengerema kwa kukutwa na nyara mbalimbali za serikali, yakiwemo magamba 40 ya Kakakuona na vipande vitatu vya nyama ya Simba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi amesema Chamukaga alikamatwa Desemba 21 mwaka huu majira ya saa 1 usiku akiwa na nyara hizo za serikali.

Katika tukio jinine, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mukadam Mukadamu ameongoza oparesheni ya ukaguzi wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi za jirani katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Nyegezi, ambapo mabasi matatu yanayosafirisha abiria kuelekea jijini Dar es Salaam yamezuiliwa baada ya kubaini kuwa hayajakidhi vigezo.

Baadhi ya madereva wa mabasi yaliyofanyiwa ukaguzi wa leseni na kuwapima kilevi, wameupongeza utaratibu huo na kuomba uwe endelevu, huku abiria pamoja na wadau wengine wa usafiri wakisema ukaguzi huo wa kushtukiza unawafanya madereva wengi kuwa makini pindi wanapokuwa safarini na hivyo kupunguza ajali za mara kwa mara.

Mwanamke Auwawa Kikatili kwa Kuchomwa Moto Hadi Kufa Baada ya Kukataa Kuchumbiwa

$
0
0
Mwanamke Auwawa Kikatili kwa Kuchomwa Moto Hadi Kufa Baada ya Kukataa Kuchumbiwa
Maafisa wa polisi katika mji wa kusini mwa India wa Hyderabad wanasema kuwa wamemkamata mwanamume mmoja baada ya mwanamke mmoja kuchomwa hadi kufa wakati wa mgogoro.

Sandhya Rani, mwenye umri wa miaka 25 alikuwa anaelekea nyumbani wakati aliposhambuliwa siku ya Alhamisi , polisi iliambia BBC.

Watu walikimbia kumsaidia bi Rani lakini alifariki akielekea hospitalini.

Mshukiwa huyo , Karthika Vanga , 28, ni mfanyikazi mwenzake wa zamani.

Alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja na bi Rani hadi miezi michache iliopita, polisi liliambia ripota wa BBC Deepthi Bathini.

Wakati alipomkaribia siku ya Alhamisi wawili hao walionekana wakijibizana kabla ya mwanamume huyo kuchukua mafiua ya taa, na kumwagia mwilini na kumchoma moto , polisi walidai.

Walisema kuwa kulikuwa na madai kwamba bwana Vanga amekuwa akitaka kumchumbia bi Rani kwa kipindi cha miaka miwili.

Alikuwa amekataa mara kadhaa kuchumbiwa na bwana huyo ijapokuwa polisi wanasema haijulikani iwapo kulikuwa na malalamishi dhidi ya mtu huyo.

Mashambulizi dhidi ya wanawake nchini India yameongezeka tangu ubakaji wa gengi la mwaka 2012 na mauaji ya mwanafunzi katika basi moja mjini Delhi, na yamesababisha kuwekwa kwa sheria kali zinazolenga kukabiliana na mashambulio kama hayo.

Mobetto na Zari Ligi Bado Mbichi Wazidi Kurushana Roho Mobetto Amwambia Zari ''Ungejiamini Wako Angetulia”

$
0
0
Mobetto na Zari Ligi Bado Mbichi Wazidi Kurushana Roho Mobetto Amwambia Zari ''Ungejiamini Wako Angetulia”
Kutokana na kile ambacho kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kati ya Zari the bosslady  na Hamisa Mobetto ambao wanadaiwa kuwa wanarushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii kutokana na who wawili kuhost party usiku wa December 21,2017 Kampala Uganda na kusemekana kuwa Zari alijaza watu wengi kuliko Hamisa Mobetto.







Hamisa Mobetto aonyesha kuendelea kurusha vijembe kwa Zari kupitia mtandao wake wa snapchat ambapo Hamisa ameandika “Tembo gani anang’olewa pembe kila siku” na Zari kumjibu “vikatuni kumi wanakusanya michango ya kusaidia watoto, vinyago kwenye mitandao ya kijamii,walioshindwa na maisha wakajikusanya kumshusha mtu mmoja,lakini mkashindwa#TheGeneral”



Waziri Aagiza Wafanyakazi Kuongezewa Malipo

$
0
0
Waziri Aagiza Wafanyakazi Kuongezewa Malipo
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele (NARI) Dkt Omari Mponda, kuwaongeza malipo ya kazi wafanyakazi wa kituo hicho katika mradi wa kubangua Korosho.


Naibu waziri Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipotembelea kiwanda kidogo cha kubangua Korosho na kubaini wafanyakazi wanalipwa shilingi 600 kwa kila kilo moja ya korosho wanayobangua kiasi ambacho hakiakisi ufanisi wa kazi kubwa wanayoifanya.

Katika maelekezo yake Naibu Waziri huyo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho kuongeza kiasi cha malipo walau kufikia shilingi 1000 kwa kila kilo moja ili wafanyakazi hao waweze kupata malipo ambayo yatamudu gharama za maisha.

Katika hatua nyingine Mhe Mwanjelwa ameipongeza Taasisi hiyo kwa kufanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kutoa/kugundua na kusajili mbegu bora 54 za korosho kwa ajili ya matumizi kwa wakulima mwaka 2006 (Aina 16), Mwaka 2015 (Aina 22 mbegu chotara), na Mwaka 2016 (Aina 16 mbegu fupi).

Taasisi ya Utafiti wa kilimo Naliendele (NARI) imepewa jukumu la kufanya Utafiti ili kuongeza tija katika Kilimo katika kanda ya kusini mikoa ya Lindi, Mtwara na Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Nabii Amnunulia Zawadi ya Gali la Milioni 926 Mwanaye wa Miaka Minne

$
0
0
Nabii Amnunulia  Zawadi ya Gali la Milioni 926 Mwanaye wa Miaka Minne
NABII wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd Bushiri, amemfanyia sapraizi mwanayae wa kike, Israella Bushiri mwenye umri wa miaka 4, baada ya kumnunulia gari aina ya Maserati Levante lenye thamani ya Sh milioni 926, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.

Gari alilonunuliwa na baba yake.

Bushiri alitumia ukurasa wake wa Facebook ku-share picha na kuandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee aliyomjalia kumpata binti yake huyo.

Nabii huyo ambaye mara nyingi anafanya kazi zake za uinjilishaji nchini Afrika Kusini aliandika: “Ninaona baraka zako Mungu kwa zawadi hii ya pekee uliyonipa katika maisha yangu. Ninasherehekea kuzaliwa kwa Mungu wangu na mwokozi wangu Yesu Kristo, na kuzaliwa kwa binti yangu wa kwanza, Israella Bushiri.

“Ninaona ni kama jana tu wakati mtoto huyu alipozaliwa na kumbeba mikononi mwangu, lakini leo naweza kumweka mabegani mwangu na akatulia mwenyewe pasipo kushikiliwa, nitamsaidia kwa kila ninaloweza akue na kufikia malengo flani,” aliandika Bushiri.

Tanzia: Askari wa JWTZ Aliyeshambuliwa na Waasi Kongo Afariki

$
0
0
Tanzia: Askari wa JWTZ Aliyeshambuliwa na Waasi Kongo Afariki
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu.

Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC.

Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku.

Katika taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala.

Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na serikali ya Tanzania kutokana na msiba huo.

Sina Kinyongo na Wala Sijaumia Belle 9 Kuoa- Lulu Diva

$
0
0
Sina Kinyongo na Wala Sijaumia Belle 9 Kuoa- Lulu Diva
MSANII anayefanya poa kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kuweka wazi hisia zake kwamba anamzimikia msanii mwenzake, Abednego Damian ‘Belle 9’ ambaye amefunga ndoa ya siri siku chache zilizopita amesema kuwa, hana kinyongo na wala hajaumia na jambo hilo

Akizungumza na Mikito Nusunusu baada ya kuenea minong’ono ya wambea wa jiji kwamba kitendo cha Belle 9 kufunga ndoa kitakuwa kimemuumiza mrembo huyo alisema, hajaumia hata kidogo sababu kwa sasa Belle 9 ni rafiki yake wa karibu wala hawazi tena mambo ya mapenzi.

“Ni kweli niliwahi kuweka wazi hisia zangu kwamba namzimikia enzi hizo, lakini hayo yalipita Belle 9 tunaheshimiana kama marafiki tu, pia nashukuru alinialika kwenye harusi yake lakini mambo yalinibana nikashindwa kwenda, kikubwa nampongeza kufunga pingu za maisha,”alisema.

Ronaldo na Messi Kuonyeshana Ubabe wa Kufungia Mwaka Leo

$
0
0
Ronaldo na Messi Kuonyeshana Ubabe wa Kufungia Mwaka Leo
Leo ni vita ya kufunga mwaka kwenye ligi kuu soka ya Hispania maarufu kama La Liga, nyota wawili kutoka timu mahasamu Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona watakuwa wanawania kufunga mwaka wakiwa na mabao mengi zaidi.


Kwasasa nyota hao wana mabao 53 kila mmoja ambayo wameyafunga ndani ya mwaka huu wa 2017 katika mashindano yote. Wanaingia kusaka mabao mengine ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza mwaka wakiwa na rekodi ya kuwa na mabao mengi zaidi.

Kwa upande wa viwango timu hizo zote zinafanya vizuri pamoja na Real Madrid kuanza vibaya msimu, tayari imeshaanza kurejea kwenye ubora wake haswa ikipewa nguvu na ubingwa wa klabu bingwa ya dunia ilioupata wikiendi iliyopita.

Kuelekea mchezo wa leo utakaopigwa saa 9:00 alasiri, Barcelona ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 42 huku wakiwa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara saba tu katika mechi 16 huku Real wakiruhusu mabao 11 katika mechi 15 na wakishika nafasi nne wakiwa na alama 31.

Mechi ya leo ni El Clasco ya 237 katika historia ya timu hizo. Real Madrid imeshinda mara 95 huku Barcelona ikishinda mara 92 na kutoka sare mara 49. Messi ndio mfungaji wa muda wote wa El Clasco akiwa na mabao 24 akifuatiwa na Alfredo Di Stefano mwenye mabao 18 na Ronaldo akiwa na mabao 17.

Mwanasoka Nyota Kutoka Marekani Alexandra Morgan Atua Bongo Kuhamasisha Soka la Wanawake

$
0
0
Mwanasoka Nyota Kutoka Marekani Alexandra Morgan Atua Bongo Kuhamasisha Soka la Wanawake
Mchezaji mpira wa miguu maarufu wa Timu ya Taifa ya Wanawake Marekani Alexandra Morgan ambaye amekuja nchini kuhamasisha wanafunzi wa kike wanaopenda mpira wa miguu kucheza mpira wa miguu pamoja na michezo mingine wakiwa bado mashuleni ili kuwaongezea uwezo wa kufanya vizuri zaidi.

Ameeleza kuwa ameona wasichana wengi mashuleni wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka lakini hawafahamu hatima yao pindi wanapomaliza masomo yao na kuongezea kuwa mashuleni wasichana hawapewi nafasi sana kwenye soka la wanawake na ndio maana amekutana na TFF ili kuwashauri mazuri ya soka hilo la wanawake.

“Elimu ni kipaumbele, na hata kwangu ilikuwa kipaumbele na ndio maana nilicheza mpira na kupata kipato kutokana na kucheza mpira kwasababu ya elimu niliyokuwa nimepata, na hii ni kutokana na nidhamu niliyoiweka kwenye elimu na kucheza soka, na ndio maana nataka kuelezea uzoefu wangu jinsi nilivyofanikiwa kwenye hili.” – Alexandra Morgan

Huyu Hapa Bingwa wa Magonjwa Sugu Kama Vile Pumu, Vidonda vya Tumbo, Busha, Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0
BABU MADUHU NI BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU YANAYOSUMBUA KAMA VILE PUMU, VIDONDA VYA TUMBO, BUSHA, NGUVU ZA KIUME, KISUKARI, MIVUTO YOTE, KUSAFISHA NYOTA, KURUDISHA MALI, NK.

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni NYASOSE MIX, Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,Hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa    dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

MHESHA POWER Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ITINYA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SUPER POWER,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

BABU MADUHU ANAPATIKANA MAGOMENI MOROCCO HOTEL/KANISANI
SIMU NO 0652 102 152/0755 684 297/0788 330 105.

HUDUMA HII UNAWEZA KUIPATA/KULETEWA MAHALI POPOTE NCHINI

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

Kutana na Mtabibu wa Nyota Duniani Maalim Fadhil Rashid Kutoka Comoro Kwa sasa Yupo Tanzania

$
0
0
KUTANA NA MTABIBIBU WANYOTA DUNIANIKOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE ANADAWA ZA KI COMRO DAWAZAKE HABAHATISHI MUONE HARAKA AKUSAIDIE TEZI NAUVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABI MALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI ZAMAJINI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YAKUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NAUMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWAHARAKA KUZUIYA CHUMAULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI KARIBUNI WOTE TIBA NIKWADINI ZOTE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO DUNIANI

CALLING +255719362806/

WHATSAPP CALLING +255785786436

Wolper: Sijawahi Kumpeleka Kwetu Kwetu Kumtambulisha Mwanaume Yeyete

$
0
0
Wolper: Sijawahi Kumpeleka Kwetu Kwetu Kumtambulisha Mwanaume Yeyete
STAA wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema hajawahi kumpeleka mwanaume yeyote nyumbani kwao kumtambulisha licha ya kuwa kwenye na mahusiano na wanaume tofauti kwa nyakati tofauti tangu kuwa staa.

Wolper ameanika hayo wakati akifanya interview na Global TV Online usiku wa kuamkia leo katika shoo yake ya House of Stylish iliyofanyika katikaUkumbi wa High Spirit Lounge, jijini Dar es Salaam.

Diva huyo wa filamu ambaye amewahi kukiri mwenyewe kubanjuka na mastaa wakiwemo wa Bongo Fleva alisema mastaa wengi wanafanya mapenzi kujifurahisha tu wala si kwa ajili ya kutengeneza familia ama ndoa.

“Kwa kuwa nafanya vitu vya kijamii naepukana na baadhi ya mambo, mahusiano ya mnayoyaona kwenye mitandao ni kujifurahisha tu, ndo maana najiachia, lakini mama yangu angeuwa anatumia mitandao nisingejaribu kufanya hivyo, lazima niwaheshimu wazazi wangu.

“Sijaolewa na hamna aliyepeleka mahali nyumbani kwetu, kwa nini nimtambulshe mwanaume? Siwezi!” alisema Wolper.

Gabo Awatolea Uvivu Wasanii wa Bongo Movie

$
0
0
Gabo Awatolea Uvivu Wasanii wa Bongo Movie
Msanii Gabo Zigamba amefunguka na kuwatolea uvivu wasanii wa movie ambao wamekuwa wakijihusisha na mambo mengine yasiyohusiana na movie kama siasa na kusema kuwa hiyo ndiyo sababu kubwa inayopelekea bongo movie kushuka na wasani hao kushuka kisanaa.


Gabo alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz na kusema kuwa tasnia hiyo inapoteza nguvu kutokana na wasanii wake wengi kujikita kufanya kazi zingine zisizohusiana na sanaa.

"Nikizungumza kwa mapana sana inaweza ikawa inawagusa baadhi ya watu ila wasisikitike bali wachukue namna ya kujifunza, unapoacha kazi yako ukafanya kazi ya mwenzako ina maana unaharibu kazi yako. Kazi ambazo zilikuwa zinafanywa na wengi katika wao ambao walikuwa wanafanya kazi zisizokuwa za kwao zinawachanganya watu, unajua hata ukiwa si mwanachuo ukaenda kuzindua majengo ya chuo unaweza ukawachanganya wakashindwa kutambua wewe taaluma yako nini" alisema Gabo Zingamba

Aidha Gabo Zigamba amewashauri wasanii hao njia nzuri itakayosaidia tasnia ya filamu kusonga mbele na wao wenyewe kuwa na heshima katika kazi zao ni pamoja na kufanya kazi yao na kuachana na kazi za watu wengine.

"Itumike hekima na watu waridhike na kubaki katika kazi yetu ya sanaa tusiambatane sana na kazi ambazo hazituhusu basi kuna uwezekano wasanii wa filamu wakawa wamefanikiwa lakini hata wapenda taaluma yetu wakawa wamefanikiwa" alisisitiza Gabo
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live




Latest Images