Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

MAUSTADHI Watembeza Kichapo cha Mbwa Mwizi kwa Makahaba Wanaojiuza Kipindi Hiki cha Ramadhani

$
0
0
MAUSTADH jijini Dar es Salaam wamefikia uamuzi mzito wa kutembeza bakora kwenye vijiwe korofi vya warembo wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili almaarufu kama machangudoa au machangu kwa kile kilichodaiwa kuwa wanasafisha jiji kutokana na kero za vishawishi vya kuharibiwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa sosi aliyewasiliana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, maustadh hao walianza oparesheni yao waliyoibatiza jina la ‘Safisha Jiji’ maeneo ya Sinza kwenye mitaa ya Shule ya Msingi ya  Mapambano na jirani na msikiti uliopo maeneo ya Afrika Sana.

Wakati maustadh hao wakiwafungia kazi na kutembeza bakora, OFM ilifika maeneo hayo na kufanikiwa kunasa tukio zima ambapo iliwashuhudia warembo hao waliokuwa wakijiuza kwa madai ya kusaka fedha za sikukuu, wakipewa kibano cha kutosha.

Wakizungumza na OFM baada ya sakata hilo, maustadh hao walisema wamechoshwa na uchafu unaofanyika kwenye makazi yao huku wakifunguka kuwa mara kadhaa wanaporudi nyumbani wakitokea msikitini, machangu hao huwang’ang’ania wakiwashawishi kufanya nao ngono bila kujua wapo katika mfungo.

“Tumechoshwa na ufuska, mbaya zaidi hawa machangu wanafikia hatua ya kutung’ang’ania wakitulazimisha tuwanunue bila kujali kama tunatoka msikitini kuswali,” alisema mmoja wa maustadh hao na kuongeza kuwa wanauheshimu mwezi huu mtukufu ndiyo maana wameamua kutembeza bakora kwa machangu hao.
Warembo hao walishuhudiwa wakiwaomba msamaha maustadh hao na kudai kuwa wamekoma, hawatarudia tena kuwasumbua maustadh.“Jamani kaka zangu nawaomba msinichape sana nina ujauzito, naomba mnichape kwenye makalio nimekoma sitarudia tena,” alisema mmoja wa machangudoa aliyekuwa akitembezewa kichapo.


Tarajia Kumuona VJ Penny Kama Mtangazaji Kwenye Show Kubwa ya TV

$
0
0
Mambo yanazidi kumnyookea Ex wa Diamond Platnumz, Penniel Mungilwa aka VJ Penny kwakuwa licha ya kuvishwa pete na kumponya kidonda alichoachiwa na hitmaker huyo, ameendelea kupata deals baada ya deals. 

Penny akipitia script ya kipindi

Mtangazaji huyo wa redio na runinga, ataanza kuonekana hivi karibuni kwenye show inayohusu filamu za Tanzania itakayoonekana kwenye kituo cha TV cha kimataifa kinachoonekana Afrika Mashariki.

Penny na Rio Paul

Katika kipindi hicho, Penny atakuwa akishirikiana na mbunifu wa mitindo Rio Paul.

Mwanamuzi Bob Junior Naye Afikiria Kutembelea Nyota ya Diamond Platnumz

$
0
0
Msanii wa muziki na producer, Bob Junior amesema kuna uwezekano mkubwa wa kufanya kolabo na msanii aliyemtoa, Diamond Platnumz.

Akizungumza na Bongo5, Bob Junior aliyetayarisha nyimbo za Diamond zikiwemo ‘Kamwambie’ na ‘Mbagala’ amesema kwakuwa yeye ndiye aliyemtoa akiamua muda wowote wanaweza kufanya naye kazi.

“Kwa sababu nia bado ipo na sisi tupo hai hatuwezi kujua nini kitatokea, siwezi sema natamani ni kijana wangu ambaye nimemtoa mimi nikiamua siku nafanya naye nitafanya naye, haiwezi kuwa na ugumu,” amesema Bob Junior.

Mrembo Huddah Monroe Azidi Kutafuta Kick Kwa Kutupia Picha za Utupu Mtandaoni

$
0
0
Kwa Kile Kinachoonekana Mchuano mkubwa wa warembo wenye umaarufu Kenya kupitia maumbo yao mrembo huddah Monroe wa Kenya ambae siku za nyuma alikuwa Gumzo katika Mitandao Ameamua Kutupia Picha akiwa Uchi kitandani , Mrembo huyo kwa sasa si Gumzo tena Baada ya Kuibuka Warembo wenye Maumbo ya Kutatanisha kama Kina Vera Sadika na Miss Kwamboka....Kitendo hicho kimetafsiriwa ni kama kutafuta Kick kwa Nguvu
IN THE NAME OF INSTAGRAM: A Kenyan socialite, Hudaah Monroe posted this photo and captioned “Damn! Isn't it a beautiful day? And idle mind is a devils workshop”

Uchambuzi: ‘Kwenu Vipi’ ya Stamina na Nay wa Mitego ni ‘Part 2′ ya ‘Muziki Gani’

$
0
0
Muziki Gani ya Nay wa Mitego na Diamond Platnumz iliwakilisha majibizano kati ya wasanii wanaofanya hip hop na wale wanaofanya Bongo Flava. Lakini kwakuwa majibizano kama hayo yanaendelea kila siku baina ya wale wanaofanya hip hop ambayo sasa imegawanyika pia, Stamina na Nay wameamua kuyaweka kwenye wimbo mpya ‘Kwenu Vipi’.
Katika ngoma hii Stamina anawakilisha kundi la wasanii wa hip hop waliobaki na misimamo ya kufanya hip hop ngumu ambayo hutafsiriwa kama muziki usiokuwa rafiki na biashara wakati Nay wa Mitego akiwakilisha wana hip hop waliobadilika kidogo kwendana na soko na kulainisha muziki wao kwa kutumia beat zenye ladha ya Bongo Flava ama na wao kuimba kabisa.

Mara nyingi kundi linalowakilishwa na Nay wa Mitego limekuwa likitafsiriwa kama lenye mafanikio ukilinganisha na wale wanaoendelea kukaza kwa midundo migumu na mashairi ya kiufundi zaidi.

Katika mistari ya Stamina, anasikika akizitolea mfano ‘Nakula Ujana’ ya Nay na ‘Pombe Yangu’ ya Madee kuwa miongoni mwa nyimbo zisizoelimisha jamii na anadai kuwa zinabebwa. Naye Nay wa Mitego akiutaja wimbo wa Professor J ‘Kamiligado’ kuwa ulifanikiwa pamoja na kwamba mchawi huyo wa rhymes aliimba.

Katika mistari mingine Nay anasema rappers wenye misimamo ya hip hop ngumu wameendelea kuishi kwa wazazi wao kwakuwa muziki hauwalipi na huku Stamina akimpa dongo Nay kuwa alikimbia hip hop halisi baada ya kugundua anafichwa.

“Kwanza hamtambui kwamba huu muziki ni kazi, na ndio maana mnakatazwa na wazazi, unafanya muziki mwaka wa kumi huna hata Bajaj, nyie sio wasanii ni wasindikizaji,” anarap Nay wa Mitego. “Kwa kupost picha Insta (gram) hilo mnaongoza, utasikia mjengo wangu mpya kumbe umepanga unajiongeza,” anachana Stamina.

Nay anamjibu: Eti mnajifanya mnakaza huku mnakufa njaa, hakuna mnachopata zaidi ya sifa kwenye mitaa, kwanza mnatudhalilisha kutwa mnapiga mizinga Umarekani mwingi mpaka mnakula unga.”

“Si bora sisi unga kuliko nyie mapunga, hamna style, hamna swag wala hamjui kutunga, kwa kuongeza sifuri kwa hilo mnaujasiri hata video ya milioni 2 utaskia milioni 200,” anajibu Stamina.

Mwisho Godzilla anamalizia kwa outro na kusisitiza umoja kati ya wasanii wote bila kuzingatia muziki wanaofanya.

Usikilize wimbo huo hapa. Bongo5

Baada ya Ajali ya Malaysia Airline…Hii ni Taarifa ya Ndege Nyingine Kutoka Nchini Uganda

$
0
0
Baada ya habari za ndege ya Malaysia airline hivi sasa ajali nyingine imetoka karibu kabisa na Tanzania ambapo ni nchini Uganda. Ndege hiyo ambayo ilikuwa imebeba wanajeshi 6 wa Marekani wakitoka Entebe kuelekea South Sudan imetua kwenye barabara ya magari baada ya hitilafu kutokea ikiwa hewani. Lakini kwenye hii ajali hakuna aliyepata majeraha au kufariki kutokana na taarifa ya msemaji wa polisi nchini Uganda.

Alichoandika Peter wa P Square Baada ya Kuipotezea Harusi ya Kaka Yake.

$
0
0
Kama kaka yake ambavyo hakuhudhuria harusi yake, basi Peter Okoye na yeye amepotezea harusi ya kaka yake Jude Okoye. Ndugu hao walionekana  kwamba wamemaliza tofauti zao lakini baada ya Peter kupotezea harusi ya kaka yake mashabiki wamekuwa wakimwambia ayamalize na ndugu yake.
Mashabiki hao wanamwambia kupitia twitter lakini baadhi yao kinachowakuwata ni kuwa blocked. Peter alichukuwa muda wake kuandika maneno haya kuhusu hii ishu.


Hivi Chadema nani Kwenu hajawahi Kuitwa Msaliti?

$
0
0
Prof Baregu mulimtukana sana  kwa matusi ya wazi kabisa pale alipotoa ya moyoni juu ya mwelekeo wa chadema na siasa zake! Mlimshambulia huyu Mwl wangu na roho iliniuma sana kwa maana namjua msimamo wake!

Vijana wa Bavicha mulimvua nguo huyu Mzee wa watu na Kama kawaida yenu mulimuita Msaliti! Leo hii mnakaa mnasema uzee dawa? Haya maneno yanatoka moyoni au? Poleni sana!

Hivi ni yupi ambae hamjawahi kumuita msaliti ndani ya chama chenu? Mbowe alipompigia Magoti JK kumshukuru kwa kazi nzuri yaani mulimporomoshea mitusi ati msaliti mkubwa ndani ya chama!

Kazi mmnayo nyie kwenu kila mtu akinena baya basi ni msaliti ndani ya chama!

Swali, ni nani hamjawahi kumuita Msaliti ndani ya Chadema?

Kuna Siri Gani Wanawake (Wasichana Wengi) Kuwapenda Wanaume za Watu?

$
0
0
Hili suala najiuliza sana hivi inakuaje?au ni justification ya ule usemi ,"Raha ya mwanaume muwe watano"? 
Kwa My experience rafiki zangu wengi sana ambao wameoa inakua rahisi sana kuopoa msichana bomba kama akimchana live yeye ni mume wa mtu ,hii imenisababishia hadi mimi(censored) niwe najitambulisha ni mume wa mtu hapo aaah...
Sasa nauwaulizeni wadada wa JF nini mnachovutiwa na wanaume wa watu?hamuoni kama ni hatari?kwanini usipenda cha kwako mwenyewe? Au wanamiliki nini ambacho singleboys hatuna hopeful we can learn from them and u
Nawasilisha

Tapeli Lililojidai Kishoka wa Tanesco Ladakwa Live Mlimani City

$
0
0
TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa  tapeli huyo alifika asubuhi  akiwa na wenzake sita,  nyumbani kwake  wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo  wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung’oa mita, eti waliona kwenye GPS  yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu  Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa  vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuite Polisi,  basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme,  nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.

Ukikutana na Mwanamke wa Aina Hii Ukaingia Naye Mapenzini na Kuoa Basi Unalo

$
0
0
Kuna mdada mmoja nilisoma naye chuo miaka fulani hapo nyuma, sasa jana katika pilikapilika zangu mjini, tukakutana ghafla maeneo fulani, kwa hiyo tukaanza kusalimiana na tukaona ni vizuri tusogee pembeni kwenye mgahawa fulani tukakaa.Basi tukawa tunapiga story za kawaida na kila mmoja akimwuuliza mwenzio yuko wapi na anafanya nini sasa. Katika kukaa naye kwa muda mfupi usiozidi nusu saa, kila baada ya sekunde kama 3 hadi tano nasikia simu yake (Sumsung galaxy S5) ikilia ndii, njee, ngaa, etc., huku akiishikilia na kucheza nayo muda wote! Sasa ikabidi nimwuulize mbona simu yako haiishi milio? Akajibu ni msgs - watu wananitumia msgs kutoka social networks mbalimbali. Nikamwambia mmmhh, social networks gani hizo mpaka simu iwe busy muda wote? Akaniambia mie nipo (tena kwa madaha) karibu social networks zote halafu nina marafiki wengi sana, akaanza kunionyesha (sio kwamba sizijui, ila yeye alihisi mie ni mngoroko na sijui chochote kuhusu social networks), nami nikawa curious kufuatilia, maweeeeeeeeee! Mdada karibu kila social network unayoijua yupo na ni very active, halafu amejiunga na magroup kibao, singles, lovers without limit, love addicts, sijui magroup gani yaani basi:
- WhatsApp
-Viber
-Instagram
-Telegram
-Tango
-skype
-facebook
-Google+ (Google Talk)
-Twitter
-twoo
-flickr
etc.,
Kilichoniacha hoi ana contacts mpaka basi, yaani nimeona facebook ana marafiki wengi zaidi ya elfu, WhatsApp kama 3800 hivi, kwingine sikuendelea kuangalia.
Nikamwuuliza sasa hizi contacts zote unazitoa wapi? Akasema wengine tunakutana kwenye mishemishe lakini wengi ni kwenye mitandao.
Nikamwambia wewe hobby yako inaonekana kuchat! Akadakia "sana na kuangalia movie". Wakati naachana naye akawa anasisitiza nimpe namba ya simu tuwe tunawasiliana kupitia WhatsApp na social networks zingine, nikamwambia wewe nipe tu namba yako nikifika home nikatulia nitakuadd.
Natumaini wadada wengine wengi wa namna hii wapo!
Swali langu ni kwamba mwanaume ukikutana na mdada wa hivi ukaingia naye kwenye mahusiano, utakuwa na guts za kujipiga kifua kwamba utaweza kuclear strings na attachments zote alizozifanya? Watu wangapi amekutana nao, kutongozana nao na labda hata kusex nao?
Kwenye hizi social networks wanaume na wanawake mara nyingi hawaishii kuchat tu, bali hufikia hatua ya kutongozana na nimeona mahuasiano kadhaa ya ndoa au kiuchumba yaliyovunjika kwa wahusika kukutwa na msgs za kutongozana au kupeana miada ya kuchepuka!Ukitaka mahusiano yako yabaki kuwa ndoto au yaingie matatani wewe mruhusu mwenzi (au jiruhusu mwenyewe) wako awe anachat, mara kushare photos na videos na watu wa jinsia tofauti - hata kama akidai ni ndugu zake, sijui kaka/dada wa hiari, sijui nilisoma naye chuo/sekondari, sijui mfanyakazi mwenzangu bila sababu ya msingi, utakuja kuniambia!

Kahaba wa Kitanzania Aeleza Alivyosambaza UKIMWI

$
0
0
MWANAMKE mmoja wa Kitanzania aliyefanya ukabaha kwa miaka 18 katika miji mbalimbali ya Tanzania, likiwemo Jiji Kuu la kibiashara la Dar es Salaam na mingine ya Namibia, ameibuka na kueleza jinsi alivyotenda dhambi ya kusambaza Ukimwi kwa wanaume wakware.

Licha ya kukiri kufanya hivyo, akisema kwa siku alipanga hadi wanaume watano,tena bila ya kutumia kinga akisema alidhamiria kuusambaza ugonjwa huo hatari alioambukizwa akiwa katika shughuli za ukahaba.

Alijigundua ameathirika mwaka 2006. Hata hivyo, katika maelezo yake ameelezea kuijutia dhamira yake hiyo, akisema alisambaza kutokana na hasira aliyokuwa nayo dhidi ya mwanamume aliyemwambukiza.

“Nilimchukia sana kila mwanamume, yeyote aliyejiita mwanamume…nilishindwa tu kuwawinda na kuwaua, lakini dhamira yangu ilikuwa kutumia silaha yoyote kuua wanaume kwa sababu mmoja wao aliniua… “Ndani mwangu nilijisemea kamwe sitawaambia hali ya afya yangu, yeyote anayekuja kwangu nammaliza. Kwa namna walivyoambukiza lazima niwaambukize’. Sijui nimewaambukiza wanaume wangapi, lakini ni maelfu,” alisema mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32, alipotoa ushuhuda wake kanisani nchini Nigeria hivi karibuni.

Uongozi YANGA wamchana Ridhiwani KIKWETE…wadai sio Mwanachama wao

$
0
0
Uongozi wa Yanga umesema Mwenyekiti wa Kamati ya ujezi wa jengo la Mafia, Ridhiwani Kikwete siyo mwanachama wa klabu hiyo kwa kuwa hajalipa ada yake kwa miezi sita mfululizo.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa  vyombo vya habari na kusainiwa na Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ilieleza kitendo cha Ridhiwani kupinga hatua ya Wajumbe wa Bodi ya Udhamini na wanachama wa Yanga kwa pamoja kumuongezea muda wa mwaka mmoja, mwenyekiti wao, Yusuf Manji hayana uzito kwa kuwa siyo mwanachama.

“Ridhwani Kikwete hajalipa ada zake za uanachama kwa miezi zaidi ya 6 mfululizo na kwa mujibu wa Katiba ya Yanga ibara ya 13 kipengele cha pili ambacho kinasema kuwa endapo mwanachama hajalipa ada yake kwa muda wa zaidi ya miezi sita mfululizo atakuwa amekoma kuwa mwanachama wa Yanga.”

“Maoni aliyoyatoa hayana uzito wa mwanachama wa Yanga, labda alikuwa akitimiza haki yake ya kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaamini kama angekuwa ni Mwanachama hai wa Yanga angetoa maoni yake kwenye Mkutano wa dharura wa Wanachama  uliofanyika Juni Mosi. Pia angeweza kutoa  kwenye kitabu cha maoni ya kupinga maazimio ya Mkutano huo kilichowekwa hapa klabuni kuanzia Juni 23  hadi  27, hakuna aliyesaini zaidi ya mwenyekiti, Manji.

“Niwakumbushe wanachama wa Yanga sehemu ya kuchangia maoni yao ni kwenye vikao vya Wanachama na siyo kwenye vyombo vya habari,  wasitafute umaarufu kwa njia za kubomoa kuliko kujenga wala wasiwadhalilishe waliojitosa kwa hali na mali kuisaidia Yanga kuwa bora kama Mama Fatma Karume wenye historia ndefu Yanga, tunaona ni sawa na udhalilishaji kwake, kwa kweli inasikitisha sana.

Taarifa hiyo ya Yanga imekuja ikiwa ni siku moja baadaya Ridhiwani kukaririwa na gazeti hili akisema haridhishwi na mambo ya migogoro ya kikatiba yanayoendelea ndani ya Yanga.

Rose Ndauka na Charlz Baba "BIFU" Zito

$
0
0
Ni dhahiri kuwa sasa , staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka na Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘ Chaz Baba ’ wapo kwenye bifu zito. 

Habari kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa , chanzo cha bifu hilo ni fedha , ambapo Rose alikodisha gari la Chaz Baba kwa ajili ya matumizi yake lakini akalirudisha likiwa limeharibika na kumuomba Chaz alitengeneze kisha angemlipa fedha zake, lakini hakufanya hivyo . 

Staa wa filamu za Kibongo , Rose Ndauka “Alikodi gari kwa Chaz , lakini aliporudisha lilikuwa bovu, akamuomba Chaz alitengeze angemlipa , baada ya hapo akaingia mitini . Chaz alikasirika sana, maana hata Rose alipopigiwa simu alikuwa hapokei .

“Imefikia hatua Chaz ametoa kiapo kibaya , amesema hata akifa, maiti yake isizikwe mpaka Rose alipe fedha zake kwanza , ” kilitiririka chanzo hicho. Akizungumzia ishu hiyo , Chaz alisema , kitu alichokifanya Rose si kizuri na kamwe hawezi kumsamehe mpaka amlipe fedha zake . 

Huyu hapa anafafanua zaidi : “Unajua Rose alikuja kwangu na kukodi gari yangu aina ya Toyota Noah , akarudisha likiwa halitamaniki kabisa , nilipomwuliza akasema walipata ajali , nikamtaka akalitengeneze, akasema hana pesa kwa hiyo nitengeneze atanilipa .

Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba ’ “Tangu siku hiyo sijaona simu yake wala meseji, hata nikimpigia hapokei . Nimeingia hasara ya kwenda kutengeneza kwa shilingi laki tano, pesa yangu inaniuma , nataka anilipe . 

“Hata kama nikifa leo , maiti yangu isizikwe mpaka Rose alipe haki yangu kwanza . Akitangulia yeye utaratibu utakuwa hivyo sitokubali azikwe hadi ndugu zake wanilipe fedha zangu, ” alisema Chaz Baba .

Baada ya kupata habari hiyo Risasi Jumamosi lilimhoji Rose kulikoni ameshindwa kulipa deni la watu hadi mdai anatoa kiapo kibaya kama kile,akaruka vikali.

“Ni kweli kabisa mimi nilikodi gari ya Chaz nikawa natembelea na ilivyokuja kuharibika nililitengeneza mimi na kwenda kumkabidhi lakini hakuridhika na namna lilivyotengenezwa ndiyo maana anasema ananidai lakini mimi sijui hilo deni , ” alisema Rose .

Florah Mbasha na Mumewe "NGOMA NZITO"

$
0
0
Imebainika kwamba waimbaji wa muziki wa Injili nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emmanuel Mbasha hawajapatana kama ilivyodaiwa awali na taarifa zinasema kuwa mwanadada huyo ameanza maisha yake kivyake kwa kupanga nyumba nyingine mbali na mumewe.

Habari za kuaminika toka ndani ya familia ya Flora zinasema kuwa msanii huyo amekuwa na wakati mgumu wa kumsamehe mumewe kutokana na tabia zake chafu ambazo zimekuwa zikiutesa moyo wake na sasa anang'ang'ania kumchukua mwanaye.

"Hivi karibuni iliripotiwa kuwa wanandoa hao wamepatana lakini ukweli ni kwamba hakuna kitu kama hicho,mwanamke amepanga chumba chake hapa Dar es Salaam na kumwachia kila kitu mumewe ambaye sasa ana haha kumchukua mwanaye ili aishi naye," kilisema chanzo cha habari.

Lakini upande wa pili, mume wa msanii huyo hivi karibuni alieleza kuwa ugomvi baina yao ulianza kutokana na kuchepuka kwa mkewe, huku akipeleka shutuma kwa mchungaji wa kanisa la ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye ni maarufu kwa vitu ambavyo ni tofauti na huduma zake.

Emmanuel Mbasha tayari alishatoa waraka wa wazi kwenda kwa mchungaji huyo, akimtaka kukaa mbali na ndoa yake jambo ambalo bado halina mrejesho chanya kwani wawili hao Flora na Gwajima wameendelea kufanya kazi pamoja kitu kinachopelekea Emmanuel kuona bado kuna kitu kinaendelea kati yao.

Kutokana na hali hiyo, mume wa Flora amekuwa mgumu kumtoa mtoto wake akihofia kulelewa na mtu ambaye kwake anamchukulia kama adui wa familia yake.

"Imekuwa ngumu sana kwa Emmanuel kumwachia mtoto wake katika hali hii, hata kama ni wewe unamuachiaje mtoto wako kipenzi aende kwa mwanamke ambaye ni msaliti," alisema ndugu wa karibu wa Emmanuel Mbasha

Sakata la Flora Mbasha kunasa Mimba Gwajima Akimbia Nchi…Waumini Sasa kugawana Mpaka Mbao za Kanisa

$
0
0
Kufuatia  sakata  la  Flora  Mbasha  na  mumewe  likumuhusisha  moja  moja  kiongozi  wa  kiroho  Mchungaji  Gwajima, habari  tulizozipata  ni  kwamba  mchungaji  huyo  amekimbia  nchi….

Habari  toka  chanzo  cha  kuaminika  kilichopo  ndani  ya  kanisa  la  mchungaji  huyo  ni  kuwa  Gwajima  hivi  sasa  ameshauza  karibia  robo  tatu  ya  mali  zake  na  kwamba  moja  kati  ya  magari  yake  ya  kifahari  huenda  likanunuliwa  na  mwanamuziki  Diamond.

Jamaa  hivi  tunavyoongea  anaweza  akawa  ameshatoroka  tayari, maana  hili  sakata  limeanza  kumwendea  hovyo  na  wiki  iliyopita  kuna  madalali  walikuja  hapa  wakiitaka  gari  yake  aina  ya  Hammer, wakidai  kuwa  inataka  kununuliwa  na  mwanamuziki  Diamond,”  kilisema  chanzo  cha  habari  hii.

Kikaendelea  kumwaga  data  kuwa  karibu  wiki  zima  lililopita  mchungaji  huyo  alikuwa  kwenye  mipango ya  kuuza  baadhi  ya  nyumba  zake  na  kwamba  hata  familia  yake  hivi  sasa  haiko  kwenye   makazi  yake  anayoishi  siku  zote…

Hata  familia  yake  sijaiona  karibu  wiki  mbili  hapa  kanisani  na  taarifa  tulizonazo  karibu  waumini  wengi  tu ni  kwamba  jamaa  anataka  kuhama  nchi  lakini  hatujui  ni nchi gani  anayotaka  kwenda  kufanya  makazi  yake  tena  ya  kudumu,” alisema.

Habari  hizo  zinadai  kuwa  baadhi  ya  waumini  wamepanga  kugawana  mali  kadhaa  za  kanisa  pamoja  na  za  Gwajima  mwenyewe  endapo  itagundukia  kuwa  ametoroka  kweli….

Kuna  baadhi  ya  waumini  wamekerwa  sana  na  hii  skendo ya  Flora  Mbasha, wamekuwa  wakijiapiza  kwamba  hata  zile  mali  zake  ni  halali  yao  kwani  zinatokana  na  sadaka  wanazotoa  kila  siku, inasikitisha  sana  kwa  kweli.” alisema  mtoa  habai  hii.

Inasemekana  kuwa  mchungaji  Gwajima amepanga  kuwaaga  waumini  wake  kama  vile  anakwenda  kueneza  neno  katika mataifa  mengine, lakini  ukweli  ni  kwamba  anataka  kuondoka  ili  kukwepa  aibu  kutokana  na  mambo  yanayoendelea…

Jamaa  yupo  kwenye  hali  ngumu, hii  ishu  ya  Flora  Mbasha imemuweka  katika  wakati  mgumu  sana  kwa  sababu  amekuwa  akinyooshewa  vidole  sana, na  kuna  baadhi  ya  wazee  wamekuwa  wakimtaka  atoe  tamko  rasmi  ili  kukwepa  hiki  kikombe  cha  aibu,” kilisema  chanzo  hicho.

Mwandishi  alimpigia  simu  Gwajima  lakini  simu  yake  haikupatikana, na  hata  Diamond  naye  alipopigiwa  simu  ili  kujua  kama  kweli  anataka kununua  gari  la  Gwajima, simu  yake  iliita  bila  kupokelewa  na  hata  alipotumiwa  ujumbe mfupi  hakujibu  kitu

Aunt Ezekiel: Sijawahi kumvulia Chupi Diamond na Sifikirii Kumtongoza

$
0
0

Wakati  ikidaiwa  kuwa  mwanadada  Aunt  Ezekiel  anamzunguka  Wema  Sepetu  na  kula  Penzi  la  shemeji  yake  Diamond, sasa  ameamua  kufunguka  na  kudai  kuwa  kamwe  hawezi  kumsaliti  Wema  na  kikubwa  anachokiheshimu  ni  kwamba  anajua  Diamond  ni  mpenzi  wa  ndugu  yake…..

Aunt  alisema  hajawahi  kulala  na  Diamond, wala  kumuomba  kutoka   kimapenzi  kama  watu  wanavyodhani  bali  wao  ni  marafiki  wa  karibu  kwani  anatambua  kuwa  Wema  anampenda  Diamond, na  ndio  maana  wakati  wote  wanakuwa  pamoja  na  si  kwamba  yeye  ana lengo  la  kuchukua  nafasi  hiyo…..

Mimi  jamani  sijawahi  kutoka  na  Diamond  na  wala  sina  lengo  hilo,najua  yeye  ni  shemeji  yangu  kwa  Wema,sasa  inakuwaje  na  mimi  nijipeleke  wakati  najua  kinachoendelea?

“Hayo  mambo  siwezi  kufanya  na  ninachohitaji  kuwaambia  mashabiki  wangu  ni  kwamba  kila  mmoja  ana  mpenzi  wake  na  hatuwezi  kuibiana  wanaume  kama  inavyodhaniwa,”  alisema  Aunt.

Hata  hivyo  alisema kuwa  safari  zote  wanazokuwa  pamoja  ni  jibu  tosha  na  kama  angetaka  kufanya  hivyo  ni  wazi  wangegombana  na  rafiki  yake, kitu  ambacho  hataki  kiwe  hivyo.

Mr. Tanzania Adata na penzi la Jack Wolper

$
0
0
Modo  wa  Tanzania  anayejulikana  kwa  jina  la  Calisah  ambaye  amewahi  kushiriki  Mr.Tanzania  2013-2014  ameandika  picha  za  kimahaba  katika  picha  za  msanii  maarufu  wa  filamu, Jackline  Wolper  ‘Gambe’…

Umenifanya  nisitamani  mwanamke  yeyote  katika  dunia hii.Nakupenda  sana  Wolper  Gambe  wangu  coz  i get everything  from  you.I love  you  kamdoli  kangu, kichuna  changu,”  hayo  ndo  maneno  ya  kimahaba  aliyoyaandika  na  kumtumia  Wolper.

“Hata kama ni Mwezi wa Ramadhani, Haki ya Tendo la Ndoa lazima Nipewe”….Mume wa Jack CHUZ

$
0
0
Mume  wa  mcheza  filamu  za  kibongo  Jack  Pantezel, Gadna  Dibibi  amesema  kuwa  mwezi  mtukufu  wa  Ramadhani  ni  haki  kwake  kufanya  jambo  lolote  kwa  mke  wake  kwani  wao  ni  wanandoa, hivyo  hawawezi  kujinyima  haki  yao  ya  msingi….

Dibibi  amesema  kuwa  wamekuwa  wakikutana  na  mkewe  na  kulimenya  tunda  tamu  nyakati  za  usiku  baada  ya  kufuturu  lakini  si  mchana  kama  wengine  wanavyofanya, kwani  endapo  watakuwa  wanafanya  mchana  ni  wazi  kwamba  watakuwa  wanamkosea  Mungu  na  mfungo  wao  utakuwa  hauna  maana…

Hilo  suala  kwetu  si  jambo la  kushtua  sana  kwa  sababu  tupo  kwenye  ndoa, ni  lazima  nipate  haki  yangu  ya  ndoa  kama  inavyotakiwa  lakini  si  kufanya  jambo  hilo  mchana, nitakuwa  nakosea  sana  ingawa  wapo  wanaofanya  hivyo  kimakosa,”alisema  Dibibi

Muigizaji wa The Vampire Diaries aliyemtumia rais Obama Barua yenye sumu afungwa jela miaka 18

$
0
0
Muigizaji wa kike maarufu, Shannon Guess Richardson, jana (July 18) amehukumiwa kifungwa cha miaka 18 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumtumia rais wa Marekani Barack Obama barua yenye sumu.

Muigizaji huyo alikamatwa June, 2013 baada ya kutuma barua hiyo yenye sumu ambayo ilielekezwa pia kwa Mayor wa New York Michael Bloomberg na mwanasheria anahusikana na udhibiti wa silaha.

Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi, barua hiyo ilikuwa imebeba sumu kali aina ya ricin inayotengezwa kutokana na mbegu za mimea.

Uchunguzi unaonesha kuwa aliagiza mbegu hizo kwa njia ya mtandao na akajifunza jinsi ya kuzigeuza kuwa sumu kisha kutekeleza nia yake.

Muigizaji huyo ambaye alijifungua akiwa mahabusu alijitetea mahakamani hapo na  kudai kuwa yeye sio mtu mbaya na hakuwa na nia ya kumuumiza mtu yoyote na kwamba vilivyoko kwenye barua hiyo sio vya kwake.

“I never intended for anybody to be hurt. I'm not a bad person. I don't have it in me to hurt anyone.”

Shannon mwenye umri wa miaka 36 ni mkazi wa Texas Marekani na ameigiza series maarufu za TV kama The Vimpire Diaries, The Blind Side na filamu ya The Walking Dead.


Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images