Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Maskini Jini Kabula Asimulia Matatizo Yake ya Ugonjwa 'Nilikuwa Kuzimu Sasa Nimerudi'

$
0
0
Maskini Jini Kabula Asimulia Matatizo Yake ya Ugonjwa 'Nilikuwa Kuzimu Sasa Nimerudi'
                                                                                                                                                                    MIRIAM Nyafulwa Jolwa ‘Jini Kabula’, msanii aliyekumbana na janga kubwa la kuugua ugonjwa uliotajwa kama ‘kichaa’ kuelekea mwishoni mwa mwaka jana, ameibuka na kufunguka kuwa kwa mapito aliyopitia mwaka 2017 anaona ni kama alikuwa kuzimu kisha kurejea duniani.



Pamoja na hilo, Jini Kabula amefungukia mengine mengi likiwemo suala la kudaiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Jini alizungumza hayo, baada ya mwanahabari wetu kumpigia simu kwa lengo la kumjulia hali na kutaka kujua kwa namna alivyojiandaa kuukaribisha mwaka mpya 2018, mazungumzo yalikuwa hivi:

Risasi Mchanganyiko: Jini vipi hali yako kwa sasa? Umepona kabisa?

Jini Kabula: Kabisa, si unaona tunaongea vizuri tu! Niko salama kabisa.

Risasi Mchanganyiko: Kwani ulikuwa unaumwa nini hasa?

Jini Kabula: (kimya cha muda mfupi), ndugu yangu wewe acha tu ni mapito ya duniani. Nashindwa kubainisha moja kwa moja nilichokuwa naumwa lakini nikiri ukweli kwamba sikuwa sawa kiakiki na kimwili, nilikuwa dunia ya peke yangu na ndiyo maana namshkuru sana Mungu kwa kunitoa jehanamu, maana ni sawa na nilikuwa kuzimu, ndiyo maana kwa sasa napumzika na hata hii simu nimepokea kwa sababu ni wewe, naongea na ndugu zangu tu.

Risasi Mchanganyiko: Kwani kwa sasa uko wapi?

Jini Kabula: Niko Mwanza kwa kaka yangu, niko mapumzikoni. Nauweka mwili wangu sawa kabla sijaanza tena mapambano ya maisha.

Risasi Mchanganyiko: Nini kilikuwa chanzo cha tatizo lako?

Jini Kabula: Tutazungumza tukikutana ana kwa ana lakini kwa sasa niseme tu kwamba kuugua kwa binadamu ni kawaida lakini wao walifurahi lakini Mungu ametenda na nitamtumikia hadi mwisho wa maisha yangu.

Risasi Mchanganyiko: Akina nani unaowasema walifurahi na Mungu ametenda?

Jini Kabula: (akilitaja jina la mwandishi) nimesema tutazungumza tukionana ana kwa ana lakini kwa sasa niseme watu wana visa sana.

Risasi Mchanganyiko: Kwa sasa umepona, kuna ndugu na marafiki waliokutenga wakati unaumwa? Kama wapo utachukua uamuzi gani?

Jini Kabula: Ni kweli kuna waliokuwa mbali na mimi lakini ni kawaida sana. Unajua mtu anapoumwa hususan ugonjwa wangu ule, ni vigumu watu kuwa karibu lakini ninawashukuru baadhi ya wasanii waliopambana kuokoa maisha yangu, hususan dada yangu Esha Buheti, Mungu ambariki sana na hakika maisha yake yamebarikiwa, ni mwanamke mwenye roho ya utu na uungwana uliopitiliza.

Risasi Mchanganyiko: Wakati unaugua kuna madai yalienea kwamba ulipimwa na kugundulika una Virusi vya Ukimwi, hili likoje?

Jini Kabula: Walisema hivyo? Jamani lakini nashukuru. Mimi ni mzima wa afya kabisa. Sina Ukimwi, tukionana nitakwenda kupima mbele yako.

Risasi Mchanganyiko: Umefikiria kuolewa sasa? Ni aina gani ya mwanaume unayemtaka?

Jini Kabula: Kuolewa? Lazima lakini siyo sasa hivi.

Risasi Mchanganyiko: Umeachana na maisha ya anasa? Kama pombe na starehe zingine?

Jini Kabula: Hapana kabisa. Mimi ni mtu wa Mungu na nimebadili mfumo wa maisha yangu, siwezi tena kufanya upuuzi huo.
Chanzo: Global Publishers

Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa

$
0
0
Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni kama baba mlezi wa msanii Dogo Janja, Madee Senesa, ametoa sababu iliyowafanya wafanye siri kufungwa kwa ndoa ya Dogo Janja na Uwoya.


Akizungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, Madee amesema walijua kuwa wawili hao ni maarufu, hivyo taarifa za ndoa yao ingewashangaza wengi na kuharibu mipango yote.

“Nilijua ni habari kubwa, ni habari ambayo ingeleta purukushani kwa wanahabari hata ndoa yenyewe isingefanyika, na hata wale ambao tumewaalika tulijua hawa wana marafiki zao ambao ni wana habari, hivyo tulichokifanya ni kutengeneza usiri wa ile shughuli, hata tuliowaalika tuliwaambia mnakuja hapa lakini simu zenu wekeni hapa, unangia unashuhudia tukio lakini hauna ushahidi wa kupeleka kwa wengine”, amesema Madee.

Madee ameendelea kwa kusema kwamba iwapo wasingefanya siri huenda wangetokea watu wa kuwashauri vinginevyo, na ndoa hiyo isingefungwa.

“Tungesema tuanze kuwaalika wangeanza kuwashauri usikubali kuolewa na yule au kumuoa huyu, ile ndoa ingekufa na sisi tungepata dhambi”, amesema Madee.

Mwezi Novemba mwaka 2017 msanii Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa, jambo ambalo  liliwashtua watu wengi, huku wengine wakisema ni kiki ya filamu.

Kiongozi wa Boko Haramu Apinga Kauli ya Buhari Alioisema Katika Sikukuu ya Mwaka Mpya

$
0
0
Kiongozi wa Boko Haramu Apinga Kauli ya Buhari Alioisema Katika Sikukuu ya Mwaka Mpya
Kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram Abubakar Shekau, ameonekana kwenye mkanda mpya wa video ikiwa ni saa 24 baada ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kutangaza hadharani kuwa kikundi hicho kimesambaratishwa.

Shekau amekiri kundi lake kuhusika katika matukio ya hivi karibuni nchini Nigeria katika maeneo ya Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo lile tukio la sikukuu ya Christimas katika kijiji cha Molai, mji mkuu wa Jimbo la Borno.

Shekau amejisifu kwa kusema kuwa askari wa Boko Haram wana afya njema na kwamba vikosi vya ulinzi nchini Nigeria haviwezi kufanya lolote dhidi ya wanamgambo hao.

Shekau ametoa tamko juu ya kukerwa kwake kutambuliwa kwa mji wa Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli tamko lililotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump.

Mapacha Walioungana Kuhamishiwa MuhimbiliiI Kwa Matibabu

$
0
0
Mapacha Walioungana Kuhamishiwa MuhimbiliiI Kwa Matibabu
MAPACHJA walioungana, Maria na Consolata wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa ajiri matibabu zaidi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Muhimbili Hospital.

Akizungumzia hatua hiyo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa wanakopatiwa matibabu, Dk Alfred Mwakalebela amesema pacha hao walilazwa hospitalini hapo Desemba 28,2017 na watapelekwa JKCI kwa matibabu zaidi.

“Hali zao zinaendelea vizuri lakini tumeona wanahitaji uchunguzi na matibabu zaidi ndiyo sababu tumeamua kuwapa rufaa. Uamuzi huo umelenga kuwawezesha pacha hao wanaosoma Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) cha mjini Iringa kufanyiwa uchunguzi na matibabu zaidi,” alisema Mwakalebela.

Nisha Afunguka Kuhusu Mapenzi 'Mabwana Waliniliza Mwaka 2017

$
0
0
Nisha Afunguka Kuhusu Mapenzi 'Mabwana Waliniliza Mwaka 2017
STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kuelezea kufurahishwa kwake na kumalizika kwa mwaka 2017 kwani ulimliza na kumfunza mengi katika suala la mapenzi baada ya mabwana zake wawili kuporwa na mastaa wenzake.



Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Nisha alisema kutokana na kufanyiwa kitendo hicho, mikakati yake mipya mwaka huu ni kumficha mpenzi wake.



“Wapenzi wangu wawili nililizwa wapenzi wangu wawili na hii ni baada ya kuwaanika hadharani hivyo kwa sasa sifanyi tena hayo mambo ya kumwanika hivyo itakuwa ngumu kumuiba kwa sababu wengi wana hila wakishajua flani yupo na mimi ndiyo wananifanyia makusudi,” alisema Nisha.

Rama Dee Afungua Mwaka 2018 kwa Furaha

$
0
0
Rama Dee Afungua Mwaka 2018 kwa Furaha
Mkali  wa R&B na mshindi wa tuzo mbalimbali, Rama Dee, aliyetamba na ngoma kali kama ‘kuwa na subira’, ‘Kipenda roho, na nyinginezo kibao, ameamua kufungua mwaka 2018 kwa kitu cha tofauti kabisa kinachokwenda kwa jina la ‘FURAHA YETU’.


Wimbo huo wa FURAHA YETU wenye staili kali na ya kitofauti unaotarajiwa kutoka rasmi ijumaa hii ya Januari 5, Rama Dee anasema alivyoangalia mahusiano ya watu jinsi yanavyoenda ndipo alipata wazo lake.

“Idea ya wimbo wa “tuwe na furaha” ilikuja baada ya kuona watu wengi kwenye mahusiano hawana furaha, si kwamba hawapendani no ila hawajui kama wanaishi kwa furaha kwa kuangalia na kuamini vitu vilivyo mbele ya camera”. Amesema Rama Dee

Pia kutokana na experience ya kuzungukwa na marafiki wanaopenda kuchukia kila kitu unachofanya, nako kulifanya wazo la wimbo huo kuibuka

“Lakini pia, niligundua marafiki wengi hawana furaha wana-hate kila kitu  kizuri wakifanyacho watu wengine, hawajiamini, hawakubali kuwa wapo kwenye ulimwengu wa furaha”. Kasema Rama Dee

Rama Dee ambaye ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 3 akitanguliwa na dada na kaka mmoja,  anasema lengo la kutumia staili hii ya twist ni kutimiza moja ya ahadi aliyowahi kumhaidi mama yake

“Marehemu Mama yangu alipenda sana muziki wa aina hii (twist), pia niliwahi kumwambia siku moja hii style nitaiweka kiujana ili iendelee kupendwa”. Amesema Rama Dee

Wimbo huo uliofanyika katika studio za  ‘Hometown studio’, Producer akiwa yeye mwenyewe kwa kushirkiana na  Elly Da Bway, Rama Dee anaamini wimbo huu sio kwaajili ya kucheza tu, bali ni maalum kwa kuwakumbusha watu kuwa maisha ni mafupi na tunahitaji kuishi kwa furaha.

Sugu Ahojiwa na Polisi kwa Kutoa Maneno ya Uchochezi

$
0
0

Sugu Ahojiwa na Polisi kwa Kutoa Maneno ya Uchochezi
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda Juu Kusini, Emmanuel Masonga wamehojiwa na Polisi wakidaiwa kutoa maneno yenye lengo la kuleta chuki baina ya wananchi na Serikali katika mkutano uliofanyika Desemba 30, mwaka jana.

Wawili hao walifika Ofisi ya Polisi Mkoa wa Mbeya jana saa nne asubuhi baada ya kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo (RCO) na walitoka saa 9:30 alasiri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga alisema jana kuwa, sababu za kuwahoji Sugu na Masonga ni kupata ukweli wa takwimu za mambo waliyoyazungumza kwa kuwa maneno hayo yanaweza kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi.

Kamanda Mpinga alisema, “Katika mkutano ule walizungumza kwamba watu wanauawa na kutupwa baharini mchana kweupe wakiwa kwenye viroba, lakini hawana ushahidi na jambo lenyewe sasa huku ni kuwachonganisha wananchi na Serikali.”

Alisema pia, walitamka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla anamsaidia Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kufanya shughuli zake Mbeya Mjini kwa ajili ya kumuandalia mazingira ya kampeni za ubunge mwaka 2020.

Kamanda Mpinga alisema baada ya kuwahoji waliwaachia kwa dhamana na watakapowahitaji wataitwa na kwamba Ijumaa wanatakiwa kurudi polisi.

Akizungumza baada ya mahojiano hayo, Sugu alisema madai ya polisi ni mwendelezo wa kunyamazisha hoja za upinzani katika kuikosoa Serikali.

Alisema yeye au wapinzani hawatanyamaza kwa namna yoyote ile katika kuikosoa Serikali na viongozi wake na kudai kwamba viongozi wa upinzani kukamatwa imekuwa kawaida hivyo haiwapi shida.

“Nimehojiwa kuhusu maneno wanayodai ni ya uchochezi katika mkutano wangu, nilihoji kuhusu hali ya usalama inayoendelea nchini, watu kupigwa risasi, kuuawa, kutekwa na kupotea katika mazingira tatanishi kwamba hayo yote hayawezi kumletea sifa nzuri Rais,” alisema.

Kwa upande wake Masonga alisema alichozungumza katika mkutano ni kuitaka Serikali kuchukua hatua kuhusu matukio yanayoendelea nchini kwa kuwa yanaleta hofu kwa wananchi.


Juma Mahadhi Apiga Magoti Kuiomba Msamaha Uongozi wa Yanga

$
0
0
Juma Mahadhi Apiga Magoti Kuiomba Msamaha Uongozi wa Yanga
Staa wa Yanga Juma Mahadhi ambaye amewahi kuonesha uwezo na kuitwa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, hivi karibuni baadhi ya mashabiki na wapenzi wa soka waliwahi kutuhumu uwezo wa mchezaji huyo kushuka kwa uzembe ukizingatia ana umri mdogo.

Jumanne ya January 2 2018 Yanga wakielekea kuanza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi wa Kombe la Mapinduzi Juma Mahadhi kabla ya mchezo alitumia ukurasa wake wa instagram kuomba radhi uongozi na mashabiki kwa kukiri kuwa aliteleza na anaahidi kuwa Mahadhi mpya.



Juma Mahadhi baada ya kuandika ujumbe huo wa wazi kupitia ukurasa wake wa instagram jioni ya January 2 alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mlandege na kupata ushindi wa magoli 2-1 huku Juma Mahadhi akifunga magoli yote mawili na kuwapigia magoti mashabiki akiomba msamaha.

Huu ndio Ujumbe wa kuomba radhi wa Juma Mahadhi aliyouandika saa chache kabla ya kucheza game na kuifungia Yanga magoli mawili dakika ya 6 na 36.



“Asalam alykum ndg zangu katika Imani haja yangu kwenu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapnz wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupitia nyinyi nawaomba sana radhi”
“Haja ya moyo wangu ni kutataka kufikia malengo yangu niliyojiweka lakini kwa mwaka huu ilikua ngumu sana kutokana na changamoto nilizokutana nao”
Sasa ombi langu kwenu Mashabiki,Viongozi na bench la ufundi ni kuwamba kijana wenu nahitaj msamaha kama niliwakosea bado nahitaji nafasi naamin siwez kurudia kosa kwani nimejifunza mengi naahidi kuwa Mahadhi mpya”

“Naomba Imani yenu kwangu na kama mnaona bado naitajika katika timu yangu pendwa Yanga SC, tumaini langu kilio changu kimewafikia nahitaji sasa kuanza mwaka mpya nikiwa kijana mwema na mpya Asanteni sana nawapenda wote”

Kutana na Mtabibu wa Nyota Duniani Maalim Fadhil Rashid Kutoka Comoro Kwa sasa Yupo Tanzania

$
0
0
KUTANA NA MTABIBIBU WANYOTA DUNIANIKOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO KWA SASA YUPO TANZANIA NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA NA KUWAKA MOTO PRESHA KISUKARI VIDONDA VYA TUMBO PUMU

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKINI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE ANADAWA ZA KI COMRO DAWAZAKE HABAHATISHI MUONE HARAKA AKUSAIDIE TEZI NAUVIMBE TUMBONI ANAUWEZO WAKURUDISHA MTUALIE POTEA KIMAZINGIRA (MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABI MALUM ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI NAKUMILIKI MALI ZAMAJINI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZAKIUME PIA ANAYO DAWA YAKUONGEZA HIPS SHEPU KUWA NAUMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (24) ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YA MVUTO WABIASHARA KUUZA MALIYAKO KWAHARAKA KUZUIYA CHUMAULETE KUSAFISHA NYOTA NAKUTOWA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI KARIBUNI WOTE TIBA NIKWADINI ZOTE UTAPATA HUDUMA POPOTE ULIPO DUNIANI

CALLING +255719362806/

Kikosi Kilichofanikisha Kurudisha Amani Kibiti Chapongezwa

$
0
0
Kikosi Kilichofanikisha Kurudisha Amani Kibiti Chapongezwa
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekipongeza kikosi maalum Kibiti kwa kazi waliyoifanya ya kulinda amani katika maeneo ya Kibiti, Rufiji, Mkuranga, na Mafia Mkoani Pwani.


Pongezi hizo zimetolewa na Kamanda Mambosasa mara baada ya kufanya ziara maalum kwenye kambi ya kikosi hicho kilichopo Wilayani Rufiji ikiwa ni sehemu ya ujirani mwema na kusema kazi inayofanywa na kikosi hicho matunda yake yanaonekana hadi nje ya mipaka ya Mkoa wa Pwani na kuwataka askari hao kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi.

"Chini ya usimamizi wa Mkuu wa Oparesheni, Naibu Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas Kibiti, Rufiji hali imekuwa shwari kwani awali hali ilikuwa mbaya. Hakuna asiyejua kuwa ilifika mahali watu wakawa wamekata taamaa na hata kukimbia maeneo yao na wengine wakisema Tanzania haijawahi kupitia maisha ambayo watu walikuwa wanapitia. Tunawapongeza sana kwa kazi nzuri" amesema Mambosasa.

Katika msafara huo Kamanda Mambo sasa ameongozana na makamanda wa mikoa ya kipolisi ya Ilala, Temeke, na Kinondoni, ambao wamesisitiza ushirikiano baina ya vikosi vya ulinzi bila kujali mipaka.

Mkoa wa Pwani ulikuwa ukikabiliwa na mauaji ya viongozi wa ngazi mbalimbali na pia raia wasio na hatia, ambayo yalikuwa yakitekelezwa na watu wasiofahamika huku mara nyingi yakihusisha uvamizi kwenye nyumba za wahusika na pia matumizi ya risasi.

Kutokana na kushamiri kwa mauaji hayo na vitisho vilivyokuwa vikitolewa na wauaji, baadhi ya watendaji walilazimika kukimbia makazi yao.

Tukio la mwisho kutokea wilayani Kibiti ni la Juni 27, ambapo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Michael Nicholaus na mtendaji wa Kijiji hicho kilichoko Kata ya Mchukwi, Mwilami Shamte, waliuawa kwa kupigwa risasi na kufanya idadi ya waliokwishauawa Pwani kufikia 37.

Hata hivyo hali ya kurejesha amani wilayani humo ilitokana na juhudi za jeshi la polisi nchini, chini ya IGP Simon Sirro, ambaye mara baada ya kuteuliwa alifanikiwa kukomesha mauaji hayo na polisi ilitangaza kuwaua watuhumiwa wa mauaji 13 waliodaiwa kutekeleza mauaji Kibiti, Mkuranga na Rufiji.

EWURA Yatangaza Bei Mpya za Petrol, Diesel na Mafuta ya Taa Kanzia Leo

$
0
0
EWURA Yatangaza Bei Mpya za   Petrol, Diesel na Mafuta ya Taa Kanzia Leo
January 3, 2017 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei mpya elekezi za Mafuta ya Petrol, Diesel pamoja na mafuta ya Taa kwa Mwaka. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia January 3.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, bei zitakazoanza kutumika leo Petroli imezidi kupanda bei kwa shilingi 8/lita, kupanda huku kumetokana na mabadiliko ya bei katika soko la Dunia.

Pamoja na kutaja bei kikomo za bidhaa mbalimbali za mafuta nchi nzima, EWURA wametaja mambo muhimu ya kuzingatia nakusogezea kama walivyotoa katika taarifa yao ya leo kama ifuatavyo.

Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Kwa mwezi Januari 2018, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 8/lita (sawa na asilimia 0.35), Shilingi 34/lita (sawa na asilimia 1.71) na Shilingi 89/lita (sawa na asilimia 4.57) sawia. Vilevile, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 7.56/lita (sawa na asilimia 0.37), Shilingi 33.97/lita (sawa na asilimia 1.81) na Shilingi 88.73/lita (sawa na asilimia 4.85) sawia. Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na ongezeko la gharama za usafirishaji (BPS Premiums).
Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga nazo zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Disemba 2017. Bei za Mafuta ya Taa hazijabadilika kwa sababu hakuna Mafuta ya Taa yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga katika mwezi wa Disemba 2017. Katika toleo hili, bei za rejareja za Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini zimeongezeka kwa Shilingi 60/lita (sawa na asilimia 2.78) na Shilingi 69/lita (sawa na asilimia 3.47), sawia. Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 59.68/lita (sawa na asilimia 2.93) na Shilingi 69.02/lita (sawa na asilimia 3.67). Ongezeko la bei za mafuta ya Petroli na Dizeli katika mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji (BPS premiums).
Ifahamike kwamba, sehemu kubwa ya shehena za mafuta yaliyopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam ni zile zenye bei za soko la dunia za mwezi Oktoba 2017 wakati shehena iliyopokelewa katika bandari ya Tanga ni ya bei za soko la dunia za mwezi Novemba 2017. Bei za mafuta katika soko la dunia kwa mwezi Novemba 2017 ziko juu kwa zaidi ya asilimia 6 ikilinganishwa na bei za mwezi Oktoba 2017.
Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika, zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.


Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na kanuni (formula) iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 216/2017 la mwezi Mei 2017.
Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.
Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta  yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahishisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mafuta ya petroli.


Nimekuwekea hapa chini bei za mafuta kwa nchi nzima kuanzia kesho Jumamosi July 1, 2017.

A: BEI ZA REJAREJA

MjiBei Kikomo
Petroli (Shs/Lita)Dizeli (Shs/Lita)Mafuta Ya Taa (Shs/Lita)
Dar es Salaam               2,167              2,018                   2,031
Arusha               2,263              2,115                   1,995
Arumeru (Usa West)                2,263               2,115                    1,995
Karatu                2,281               2,134                    2,013
Monduli                2,268               2,121                    2,000
Monduli-Makuyuni                2,273               2,125                    2,005
Ngorongoro (Loliondo)                2,347               2,200                    2,079
Kibaha               2,172              2,023                   2,036
Bagamoyo                2,178               2,029                    2,042
Kisarawe                2,175               2,025                    2,038
Mkuranga                2,177               2,028                    2,041
Rufiji                2,195               2,046                    2,059
Dodoma               2,226              2,077                   2,090
Bahi                2,233               2,084                    2,097
Chemba                2,252               2,103                    2,116
Kondoa                2,259               2,109                    2,122
Kongwa                2,223               2,074                    2,087
Mpwapwa                2,227               2,078                    2,091
Iringa               2,231              2,082                   2,095
Kilolo                2,236               2,087                    2,099
Mufindi (Mafinga)                2,241               2,092                    2,105
Njombe               2,259              2,110                   2,123
Njombe (Kidegembye)                2,280               2,131                    2,144


Ludewa                2,297               2,148                    2,161
Makete                2,290               2,141                    2,154
Wanging’ombe (Igwachanya)                2,257               2,108                    2,121
Bukoba               2,382              2,233                   2,246
Biharamulo                2,357               2,207                    2,220
Karagwe (Kayanga)                2,399               2,249                    2,262
Kyerwa (Ruberwa)                2,404               2,255                    2,268
Muleba                2,382               2,233                    2,246
Ngara                2,348               2,199                    2,211
Misenyi                2,391               2,241                    2,254
Geita               2,332              2,183                   2,196
Bukombe                2,321               2,172                    2,185
Chato                2,353               2,204                    2,217
Mbogwe                2,370               2,221                    2,234
Nyang’hwale                2,347               2,198                    2,211
Kigoma               2,398              2,249                   2,262
Uvinza (Lugufu)                2,410               2,261                    2,274
Buhigwe                2,387               2,238                    2,251
Kakonko                2,355               2,206                    2,219
Kasulu                2,384               2,235                    2,248
Kibondo                2,363               2,213                    2,226
Moshi               2,253              2,105                   1,984
Hai (Bomang’ombe)                2,256               2,108                    1,988
Mwanga                2,246               2,098                    1,977
Rombo (Mkuu)                2,269               2,122                    2,001
Same                2,239               2,091                    1,971
Siha (Sanya Juu)                2,259               2,112                    1,991
Lindi               2,226              2,077                   2,090
Lindi-Mtama                2,244               2,095                    2,108
Kilwa Masoko                2,201               2,052                    2,065
Liwale                2,247               2,098                    2,111
Nachingwea                2,255               2,106                    2,119
Ruangwa                2,257               2,108                    2,121
Babati               2,297              2,149                   2,029
Hanang (Katesh)                2,307               2,160                    2,039
Kiteto (Kibaya)                2,312               2,165                    2,044
Mbulu                2,310               2,162                    2,041
Simanjiro (Orkasumet)                2,329               2,181                    2,061
Musoma               2,346              2,196                   2,209
Musoma Vijijini (Busekela)                 2,386               2,237                    2,250
Rorya (Ingirijuu)                2,354               2,205                    2,218
Rorya (Shirati)                2,389               2,240                    2,253
Bunda                2,337               2,187                    2,200
Butiama                2,342               2,193                    2,206
Serengeti (Mugumu)                2,391               2,242                    2,255
Tarime                2,357               2,207                    2,220
Tarime (Kewanja/Nyamongo)                2,361               2,212                    2,225
Mbeya               2,274              2,125                   2,138


Chunya                2,284               2,134                    2,147
Chunya (Makongolosi)                2,298               2,149                    2,162
Ileje                2,287               2,138                    2,151
Kyela                2,290               2,141                    2,154
Mbarali (Rujewa)                2,258               2,109                    2,122
Mbozi (Vwawa)                2,284               2,134                    2,147
Momba (Chitete)                2,292               2,143                    2,156
Rungwe (Tukuyu)                2,283               2,134                    2,147
Morogoro               2,192              2,043                   2,056
Mikumi                2,208               2,059                    2,072
Kilombero (Ifakara)                2,230               2,081                    2,094
Kilombero (Mlimba)                2,252               2,103                    2,116
Kilombero (Mngeta)                2,242               2,092                    2,105
Ulanga (Mahenge)                2,241               2,091                    2,104
Malinyi                2,251               2,102                    2,115
Kilosa                2,211               2,061                    2,074
Gairo                2,211               2,061                    2,074
Mvomero (Wami Sokoine)                2,203               2,054                    2,066
Turiani                2,217               2,068                    2,081
Mtwara               2,240              2,090                   2,103
Nanyumbu (Mangaka)                2,288               2,139                    2,152
Masasi                2,265               2,116                    2,129
Newala                2,272               2,122                    2,135
Tandahimba                2,265                2,115                    2,128
Mwanza               2,317              2,168                   2,181
Kwimba                2,353               2,204                    2,217
Magu                2,325               2,176                    2,189
Misungwi                2,323               2,173                    2,186
Sengerema                2,350               2,200                    2,213
Ukerewe                2,377               2,227                    2,240
Sumbawanga               2,340              2,191                   2,203
Kalambo (Matai)                2,347               2,198                    2,211
Nkasi (Namanyele)                2,353               2,204                    2,217
Katavi (Mpanda)                2,375               2,226                    2,238
Mlele (Inyonga)                2,353               2,204                    2,217
Songea               2,291              2,141                   2,154
Mbinga                2,324               2,175                    2,188
Namtumbo                2,320               2,171                    2,183
Nyasa (Mbamba Bay)                2,326               2,177                    2,190
Tunduru                2,349               2,200                    2,213
Shinyanga               2,296              2,147                   2,160 
Kahama                2,310               2,160                    2,173
Kishapu                2,324               2,175                    2,188
Simiyu (Bariadi)                2,337               2,188                    2,201
Busega (Nyashimo)                2,330               2,181                    2,194
Itilima (Lagangabilili)                2,340               2,191                    2,204
Maswa                2,329               2,180                    2,192
Meatu (Mwanhuzi)                2,336               2,187                    2,199
Singida               2,258              2,109                   2,121
Iramba                2,270               2,121                    2,134
Manyoni                2,242               2,093                    2,106
Ikungi                2,253               2,104                    2,117
Mkalama (Nduguti)                2,282               2,133                     2,146
Tabora               2,321              2,172                   2,185
Igunga                2,275               2,126                    2,139
Kaliua                2,339               2,190                    2,203
Ulyankulu                2,333               2,184                    2,197
Nzega                2,286               2,137                    2,149
Sikonge                2,333               2,184                    2,197
Urambo                2,334               2,185                    2,198
Tanga               2,206              2,059                   1,938
Handeni                2,227               2,079                    1,959
Kilindi                2,242               2,094                    1,974
Korogwe                2,219               2,071                    1,950
Lushoto                2,228               2,080                    1,960
Mkinga (Maramba)                2,213               2,066                    1,945
Muheza                2,211               2,064                    1,943
Pangani                2,213               2,066                    1,945


B: BEI ZA JUMLA

Bei za Jumla – DSMPetroli (Shs/Lita)Dizeli  (Shs/Lita)Mafuta ya Taa (Shs/Lita)
Bei Kikomo2,056.411,907.121,920.00



Bei za Jumla –
TANGA

Petroli (Shs/Lita)Dizeli  (Shs/Lita)Mafuta ya Taa (Shs/Lita)
Bei Kikomo2,095.461,947.931,827.17
  Mhandisi Godwin Samwel

KAIMU MKURUGENZI MKUU

Atiwa Mbaloni kwa Kumuoza Mwanaye wa Miaka Minne

$
0
0
Atiwa Mbaloni kwa Kumuoza Mwanaye wa Miaka Minne
Mwanaume mmoja mwenye miaka 40 katika kijiji cha Kirimon anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya baada ya kujaribu kumuoza mwanaye wa miaka 4 kwa mzee wa miaka 70 jana January 2, 2017  baada ya mpango wake kushtukiwa na Tume ya Taifa ya Huduma za Watoto nchini humo.

Inaelezwa kuwa mpango huo ulivurugika baada ya mama wa mtoto na majirani kutoa taarifa kwa tume hiyo. Kwa mujibu wa Afisa wa tume hiyo Jane Kabiro, mwanaume huyo alitaka kupata ng’ombe 40 kwa kumuoza mwanaye huyo ili afidie ng’ombe aliowatoa kama mahari pindi alipomuoa mkewe ambaye ni mama wa mtoto huyo.

Kabiro alieleza pia kuwa siku za nyuma kidogo mwanaume huyo alitaka kuoa mke wa pili na mkewe alipokataa suala hilo alimfukuza na watoto warudi kwa mama mkwe wake. Baada ya mwanamke huyo na wanaye kwenda kuishi kwa mama yake alikwenda kuleta vurugu akitaka kumuoza mwanaye kama fidia ya mahari aliyotoa alipomuoa mwanamke huyo.

Msanii Huyu Kutoka Afrika Kutumbuiza Tamasha Kubwa Duniani la Coachella

$
0
0
Msanii Huyu Kutoka Afrika Kutumbuiza Tamasha Kubwa Duniani la Coachella
Tamasha kubwa la muziki duniani ambalo hufanyika kila mwaka nchini Marekani la Coachella jana usiku waandaji wa tamasha hilo wametangaza orodha ya majina kibao ya wasanii na Ma’DJ watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo.

Kwenye orodha hiyo kuna jina la msanii mmoja kutoka Afrika Kusini na sio mwingine ni Black Coffee ambaye pia muaandaji wa muziki na DJ.

Wasanii wengine wakubwa watakaotumbuiza  kwenye tamasha hilo ni Beyonce, Eminem, The Weeknd, French Montana, CardI B, CZA, kundi la Migos na wasanii wengine kibao.

Bodi Ya Mikopo Yawakalia Kooni Waajiliwa Yasema Ukitaka Usilipe Labda Ufe

$
0
0
Bodi Ya Mikopo Yawakalia Kooni Waajiliwa Yasema Ukitaka Usilipe Labda Ufe
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) imesema kuanzia Jumatatu ijayo, Januari 8, 2017 itaanza kukagua taarifa za mishahara za waajiri (payroll) ili kubaini waajiri ambao wanawasilisha kiwango kidogo cha mikopo ya wafanyakazi wao ambao ni wanufaika pamoja na waajiri ambao hawawasilishi kabisa pesa hizo kwenye bodi hiyo kwa mujibu wa sheria ili wachukuliwe hatua stahiki.



Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema wanufaika wengi wa mikopo, wakiwemo wadaiwa sugu, wameonesha ushirikiano mkubwa katika kurejesha mikopo yao, hivyo kurahisisha kazi ya kukusanya madeni ya mikopo hiyo.



“Kiasi cha pesa za wadaiwa sugu kilichoiva na kinachotakiwa kuwasilishwa ni Tsh. bilioni 285, hii inajumuisha kuaznia kazi hii ya kukopesha ilipoanza.



“Tangu mwaka jana mpaka sasa tumewapata wadaiwa sugu 26,000, tunashukuru wanufaika hawa wamejitokeza na wanawasilisha mikopo yao. Kuna baadhi ya waajiri wanawasilisha vizuri marejesho ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, wengine hawasilishi na wengine wanawasilisha kiasi kidogo tofauti na asilimia 15 kama sheria inavyotamka.



“Kuanzia Jumatatu, Jan. 8, 2017 tutaanza kukagua taarifa kwenye payroll za waajiri wote waliosajiriwa kubaini waajiriwa wao ambao ni wanufaika wa mikopo wanaodaiwa ili waweze kukatwa. Lengo la kufanya ukaguzi kwenye payroll za waajiri ni kubaini iwapo wana waajiriwa wanadaiwa na HESLB, waajiri wanaowasilisha kiwango kinachotakiwa, wanaowasilisha chini ya asilimia 15 na wanaokata pesa na hawaziwasilishi HESLB,” alisema Badru.



Hata hivyo, Badru amesema wamelazimika kufungua ofisi zao nchi nzima kwa ajili kusimamia malipo ya fedha hizo za mikopo, hasa wale waliotajwa kwenye orodha ya wadaiwa sugu ambapo wamewasambaza wakaguzi nchi nzima, kwa ajili ya kufuatilia waajiri wasiotekeleza wajibu wao wa kuwakata asilimia 15 wanufaika hao waliowaajiri.



Badru pia amewasisitiza watu wote waliowahi kukopa, kulipa wenyewe kwa hiyari kwani bila hivyo, watajikuta wakiingia matatizoni na njia pekee inayoweza kumuokoa mtu aliyekopa asilipe, nio kifo.

Hizi Ndivyo Dkt Shika Alivyofunguka Kuhusu Safari Yake ya Kwenda Marekani

$
0
0
Hizi Ndivyo Dkt Shika Alivyofunguka Kuhusu Safari Yake ya Kwenda Marekani
Mtanzania Dkt. Louis Shika amedai mara baada ya kumaliza mambo yake hapa nchini anatarajia kwenda nchini Marekani kufanya kazi Umoja wa Mataifa (UN) ambapo aliteuliwa kuwa balozi miaka mitatu iliyopita.

Dkt. Shika amekiambia kituo cha runinga cha Azam kuwa anachoshughulikia kwa sasa hapa nchini ni kuingiza fedha zake zilizopo nje ya nchi ili awe kufungua kampuni na itakapoanza kufanya kazi ndipo atasafiri.

“Basi nitakuwa nimemaliza kazi yangu kwa hapa Tanzania ninaondoka kwenda Marekani kuitumikia dunia, mimi ni balozi katika Umoja wa Mataifa uteuzi ambao ulifanywa 2014 na sikuripoti kazini lakini hawajakata tamaa miezi miwili iliyopita nimepandishwa cheo kwa ngazi ya juu,” amesema Dkt. Shika.

“Mwanzo niliteuliwa kuwa balozi wa wakimbizi kwa upande wa Afrika, sasa nimechaguliwa kuwa balozi wa wakimbizi ulimwenguni kote, kwa hiyo ofisi kutoka Nairobi inahama kwenda New York,” amesisitiza.

Utakumbuka umaarufu wa Dkt. Shika ulikuja baada ya kujitokeza katika mnada wa  kuuza nyumba za Lugumi ambapo aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800, kisha kudai anangojea fedha zake kutoka nchini Urusi.


Korea Kaskazini Yafungua Mawasiliano ya Simu na Korea Kusini

$
0
0
Korea Kaskazini Yafungua Mawasiliano ya Simu na Korea Kusini
Korea Kaskazini imefungua tena mawasiliano ya simu na Korea Kusini ili kuanzisha mazungumzo kuhusu kushiriki kwake katika mashindano ya msimu wa baridi.

Korea Kusini imethibitisha kuwa ilipata simu kutoka Kaskazini leo Jumatano.

Trump: Kibonyezo changu cha nyuklia kina nguvu kuliko cha Kim
Hii ni baada ya Kim Jong un kusema kuwa ataanzisha mazungumzo na Korea Kusini kuhusu kutumwa timu kwa mashindano ya msimu wa baridi huko Korea Kusini.

Mataifa hayo mawili hayajafanya mazungumzo ya juu tangu Disemba mwaka 2015

The North-South Korea hotline in the village of PanmunjomHaki miliki ya pichaEPA
Image caption
Korea Kaskazini yafungua mawasiliano ya simu na Korea Kusini
Mwaka uliofuatia Korea Kaskazini ilikata mawasiliano na kuacha kupokea simu kwa mujibu wa maafisa kutoka Kusini

Afisa kutoka Korea Kaskazini alitangaza kufunguliwa laini hiyo ya simu kwenye ujumbe uliopeperushwa mapema Jumatano.

Kim Jong-un: Kibonyezo cha silaha za nyuklia kiko kwenye meza yangu
Mkuu wa idara ya mawasiliano ya raia wa Korea Kusini Moon Jae-in, alisema kuwa kufunguliwa kwa laoni hiyo ya simu kuna umuhimu mkubwa

"Inabuni mazingira ambapo mawasiliano yatakuwa rahisi kila mara," alisema.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

Bond Afunguka Kuhusu Kuhusika Kwenye Ujambazi na Kuachana na Wastara

$
0
0
Bond Afunguka Kuhusu Kuhusika Kwenye Ujambazi na Kuachana na Wastara
MENEJA na aliyekuwa mpenzi wa msanii wa Bongo Muvi, Wastara Juma, Bond Suleiman amefunguka kuwa mwaka 2017 ulikuwa ni mchungu sana kwake, baada ya kuhusishwa na tukio la ujambazi na ishu ya kuachana na Wastara.


Wastara Juma akiwa na Bond Suleiman.

Akizungumza na Za Motomoto, Bond alisema kuwa kwenye uhusiano aliumia sana kumuacha Wastara hasa baada ya kumuona ni kama anataka mafanikio ya haraka wakati yeye uchumi ulikuwa umeyumba.


“Mimi ndiye niliyemuacha Wastara na kuamua kuondoka zangu na kwenda kufanya maisha yangu mengine kwa sababu niliona kama namkosesha amani na pia alitaka mafanikio ya haraka wakati uchumi wangu uliyumba. Pia ishu ya kuhusishwa kwenye ujambazi ilinitesa sana kwani nilikaa selo siku ishirini ila nashukuru polisi waliujua ukweli nikawa huru,”alisema Bond.

Snura Ajipanga Kuwaliza Watu Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

$
0
0
Snura Ajipanga Kuwaliza Watu Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa
MWANAMUZIKI nyota na mahiri kwa kukata viuno jukwaani, Snura Mushi amesema atawaliza watu watakaojitokeza katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa ambayo itafanyika mapema mwezi huu.

Snura aliiambia Za Motomoto News kuwa siku hiyo atawaimbia wimbo ambao utawaliza wote watakaoshiriki sherehe hiyo kwani wimbo huo una maneno ya kuhuzunisha ndani yake.


“Lazima kila atakayehudhuria bethdei yangu atoe chozi sababu nitawaimbia wimbo ambao una maneno ya kuhuzunisha na nitakuwa nauimba kwa mara ya kwanza kabisa kabla sijaurekodi na kuutoa.

Kituo cha Haki za Binadamu Yaijia Juu TCRA Kuhusu Kupiga Faini Vituo Vitano vya Televisheni

$
0
0
Kituo cha Haki za Binadamu Yaijia Juu TCRA Kuhusu Kupiga Faini Vituo Vitano vya Televisheni
IKIWA ni siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuvipiga faini vituo vitano vya runinga kwa kuvunja sheria za urushwaji wa matangazo na maudhui, Kituo cha Haki za Binadamu, LHRC kimeijia juu mamlaka hiyo na kusema hizo ni mbinu za serikali kukataa kukosolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen Kidjo Bisimba, alianza kwa kutoa pole kwa vituo vyote vilivyopigwa faini na kuongeza kwamba wapo kwenye mpango wa kuanzisha harambee ya kuvichangia vyombo hivyo vya habari kulipa faini.



Kuhusu makosa ambayo vituo hivyo viliyafanya, Bisimba anasema habari iliyoleta matatizo, haikuwa ya uchunguzi bali uchambuzi ambao kimsingi huwa hauhitaji mizania ya habari.
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live


Latest Images