Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Meya Ubungo, Temeke Wakunjana Mashati Wakati wa Kuhesabu Kura

$
0
0
Meya Ubungo, Temeke Wakunjana Mashati Wakati wa Kuhesabu Kura
Mameya wa Ubungo, Boniface Jacob na wa Temeke, Abdallah Chaurembo wanadaiwa kukunjana mashati wakati wa kuhesabu kura za uchaguzi wa naibu meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Katika uchaguzi huo, aliyeibuka mshindi, Mussa Kafana wa CUF alifikishwa kupiga kura akiwa mgonjwa. Kutokana na hali yake, alipigiwa kura na mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea.
Ilishuhudiwa katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee ulikofanyikia uchaguzi huo leo Jumatano Januari 3,2018 Chaurembo na Jacob wakikunjana mashati.
Vurugu inaelezwa ilitokea baada ya Chaurembo wa CCM kupinga kura mbili alizodai zilipigwa nje ya utaratibu. Picha za wawili hao zilisambaa mitandaoni zikiwaonyesha wanavyokunjana.
Hata hivyo, Jacob amekanusha madai ya kupigana akisema alikuwa analinda kura zilizotaka kuchukuliwa na Chaurembo jambo ambalo hakutaka litokee na alifanikiwa.
Jacob alisema Chaurembo alivamia meza ya kuhesabia kura akitaka kura kwa ajili ya kuziharibu.
“Si kweli kwamba tumepigana mimi nilikuwa wakala, wakati kazi ya kuhesabu kura ikiendelea Chaurembo akaona kura za Chadema zinaongezeka ikiwa na maana kuna watu wa CCM walitupigia kura,” amesema.
Jacob amesema, “Kuona hivyo akavamia meza akitaka kunipora zile kura lakini nilikuwa nimezishika vizuri hivyo hakuweza kuzichukua na alidhibitiwa, hivyo kazi ya kuhesabu kura iliendelea kama kawaida na ndiyo kama hivyo tumeshinda,” amesema Jacob.
Wakati akisema hayo, Chaurembo amesema, ‘’Utaratibu wa uchaguzi haukufuatwa, kuna kura mbili zilipigwa nje ya kiboksi ambazo maana yake zimeharibika, lakini nilipohoji tu huyo jamaa (Meya Jacob) kama mnavyomjua, akanishambulia.”
“Akanirukia, akanikaba shati na kunichania, mimi nilikuwa napinga kura hizo kujumuishwa kwa kuwa zilikuwa zimeharibika,” amesema.


Mvua Zaongeza Theluji Mlima Kilimanjaro

$
0
0
Mvua Zaongeza Theluji Mlima Kilimanjaro
Kuongezeka theluji katika Mlima Kilimanjaro kumekuwa kivutio kwa wananchi ambao baadhi wamekuwa wakipiga picha mandhari ya mlima huo.
Hata hivyo, baadhi wamekuwa wakihoji iwapo hali itaendelea kuwa hivyo.
Akizungumzia hali hiyo, Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Paschal Shelutete amesema hali hiyo inatokana na mvua iliyonyesha Januari Mosi,2018.
Shelutete amesema leo Januari 3,2018 kuwa mvua inayonyesha kwenye uwanda wa juu kuanzia mita 3,500 kutoka usawa wa bahari inakuwa katika mfumo wa theluji.
Amesema hali hiyo inatokana na kiwango kidogo cha joto ambacho kwa usiku hufika hasi (sentigredi sifuri au chini).
“Theluji hii huyeyuka kukiwa na mabadiliko ya hali ya hewa hasa kiangazi (kunapokuwa na jua). Upande mwingine kukiwepo na mvua endelevu na mabadiliko ya hali ya jua na joto theluji huungana na kuwa barafu ya kudumu,” amesema.
Mwongozaji watalii katika kampuni ya Zara Adventures Tours ambaye pia ni mwenyekiti wa waongoza watalii katika Mlima Kilimanjaro na Meru, Faustine Chombo amesema theluji imeongezeka lakini ni ya muda kutokana na mvua iliyonyesha.
Amesema hali ya hewa katika Mlima Kilimanjaro kwa sasa ni ya mvua ndiyo maana ukiuangalia mlima kutokea Moshi mjini unaonekana kuwa na theluji nyingi.
Amesema wamejipanga kupanda miti kila mwaka katika maeneo ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ili kusaidia jitihada za kuulinda na kuuhifadhi.
Chombo amesema kuna haja ya wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhamasishwa kupanda miti kwa wingi katika maeneo ya hifadhi hiyo hatua itakayosaidia theluji kuendelea kuwapo.


Emmanuel Eboure Ataka Kujinyonga Kisa Mapenzi

$
0
0
Emmanuel Eboure Ataka Kujinyonga Kisa Mapenzi
Nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboure ameweka bayana jambo lililomfanya afikirie kujinyonga kutokana na matatizo yanayomkabili.

Nyota huyo aliweka bayana suala la kutalakiana na mkewe, Aurelie ambaye mahakama kuamuru umiliki wote wa mali zitahamishiwa kwa mwanamke huyo ni mambo ambayo amesema yanamvuruga akili.

Eboue alisema kwamba amevumilia kuwa nje ya soka kwa takribani mwaka mzima lakini kubwa linalokoroga ni matatizo yaliyotokana na talaka na mkewe, pia anakabiriliwa na majonzi baada ya kufiwa na ndugu zake wawili wa karibu.

Alisema mambo hayo yameharibu mfumo mzima wa maisha yake jambo amablo limemfanya kuishi kama ombaomba, huku akiweka bayana kwamba hakuwahi kuwa na elimu ya kutunza fedha zake vyema.

Mkongwe huyo mwenye miaka 34, aliitumikia Atsenal tangu mwaka 2004 hadi 2011 kabla ya kuhamia Uturuki ambako alikuwa akiichezea klabu ya Galatasaray.


Basata Yaafunguka Kuhusu Mavazi ya Kubana na Nguo Fupi kwa Wanawake

$
0
0
Basata Yaafunguka Kuhusu Mavazi ya Kubana na Nguo Fupi kwa Wanawake
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mngereza, amesema wanawake wanaovaa nguo fupi mbele za watu hawako sahihi, kwani licha ya kuwa wana uhuru wa kufanya hivyo, lakini wanavuka mipaka ya uhuru huo.


Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mngereza amesema kwamba kuvaa nguo fupi maeneo ya watu wengi na mchana kweupe ni kuvunja maadili ya Mtanzania, hivyo wasilalamike watu wanapowafanyia vitendo viovu.

Akiendelea kuzungumzia suala hilo, Mngereza amesema licha ya watu hao kufanya makosa ingawa si ya kisheria, lakini watu wanaowachukulia hatua ya kuwachania nguo zao na kuwadhalilisha wanavunja sheria, kwani hakuna sehemu kwenye sheria ya nchi inayowaruhusu kufanya hivyo.

Benki Tano Zafutiwa Leseni za Biashara na BOT

$
0
0
Benki Tano Zafutiwqa Leseni za Biashara na BOT
Benki Kuu ya Tanzania(BOT) imezifutia leseni za biashara benki tano ambazo ni Covenant Bank for Women(Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera farmers cooperative Bank Limited, na Meru Community Bank Limited na


kuziweka chini ya ufilisi.

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa benki hizi zina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.

BOT imesema upungufu huu wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

Hii imetokea ikiwa ni siku moja tu tangu Gavana wa Benki Kuu Tanzania Prof. Beno Ndulu akabidhi ofisi kwa kumaliza muda wake na Gavana mpya kuchukua madaraka.

Soma taarifa yote hapa chini

Maskini Wastara Bado Mzimu wqa Sajuki Wamtesa

$
0
0
Maskini Wastara Bado Mzimu wqa Sajuki Wamtesa
Mzimu wa Sajuki Unavyomtesa Wastara Miaka mitano tangu kifo cha Sajuki, mkewe, Wastara Juma bado analia kuteswa na mzimu wa mumewe huyo, kutokana na jinsi walivyokuwa wakipendana na kuishi kwa amani.

Sajuki alifariki miaka mitano iliyopita na kumuacha Wastara mjane, ambapo licha ya kutoka na wanaume kadhaa, Wastara bado analia kuteswa na mapenzi, pengo la Sajuki halijazibwa mpaka leo.

Baba Daimond Awachana Zari na Hamisa Mobetto

$
0
0
Baba Daimond Awachana Zari na Hamisa Mobetto
Wamebutuliwa! Ndiyo msemo unaoweza kuusema baada ya Mzee Abdul, ambaye ni baba mkwe wa wanawake wawili, Zarinah Hassan ‘Zari The Bossy Lady’ na Mwanamitindo Hamisa Mobeto ambao waliumaliza mwaka jana kwa kuchafuana mitandaoni, mmoja akimuita mwenzake mchawi na mwingine akidaiwa kuwa ni changudoa mzee, jambo ambalo mzee huyo hakupendezwa nalo.



Akizungumza na Amani juzikati, Mzee Abdul alisema anachukizwa na kitendo cha wanawake hao ambao wote wamezaa na mwanaye, kuvuana nguo mitandaoni wakati kila mmoja ana haki sawa.


Mwanamitindo Hamisa Mobeto.

MSIKIE MZEE ABDUL

“Ninawasihi hawa wanawake waache malumbano katika mitandao ya kijamii, kwa sababu kila mmoja amezaa hivyo wote wana nafasi na haki sawa kwa vile hakuna aliyeolewa hadi sasa.

“Maneno wanayotoleana mitandaoni ni mabaya na yananichukiza mno, sasa naomba niwaase vijana wangu waache mara moja kwani wote wana haki sawa, mwanangu bado hajaoa na huenda mmoja wao akaolewa lakini na mwingine akapewa heshima yake kama mzazi, lakini pia bado wote wawili wanaweza kuolewa kwa vile imani ya dini ya mwanangu inaruhusu.”



AWATAKA KUNYAMAZA

Mzee huyo alienda mbali zaidi na kuwasihi Zari, aliyezaa watoto wawili na Hamisa mwenye mtoto mmoja, wanyamaze wakati kila mtu akisubiri uamuzi wa kijana wake.

“Kitu ambacho nina uhakika nacho ni kuwa kila mmoja kwa kitendo cha kuzaa na mwanangu, ataambulia chochote kitu kwani wana haki.


Zarinah Hassan ‘Zari The Bossy Lady’ .

“Unajua wasichokijua ni kuanika siri zao mitandaoni wanajiabisha na kutukanana vile wanajiabisha, kwetu sisi wazazi tunaonekana hatuna busara kuendelea kunyamazia ugomvi huo, mimi ninachoweza kusema ni kuwaomba wanyamaze, kila mmoja afanye mambo yake, atakayeendelea kulumbana na mwenzake ndiye ataonekana ana matatizo, lakini atakayekaa kimya, huyo ndiye atakuwa mwanamke wa kuoa,” alisema.



AMTAKA MAMA ESMA KUWA NA BUSARA

Mzee Abdul aliamua kumchana mzazi mwenzake, Mama Esma kwa kumtaka kuwa na busara kwa vile anaonekana kuchagua upande mmoja ambao anauunga mkono kupitia mitandao, kitu alichodai siyo sahihi.

“Namwambia mama Esma awe na busara, yeye ni mzazi, tabia yake ya kuchagua upande na kuendeleza vijembe siyo nzuri kwani anajua wazi kuwa mtoto wa Mobeto pia ni wetu, siyo vizuri, yeye kama mzazi angewashauri nina uhakika wangemsikiliza lakini nashangaa amechagua upande mmoja wa Zari,” alisema Mzee Abdul.



TUJIKUMBUSHE

Mwishoni mwa mwaka jana, Zari na Mobeto walirushiana vijembe vikali kwenye mitandao ya kijamii kila mmoja akimponda mwenzake. Wakati Zari akidai Mobeto hana hadhi ya kushindana naye, mwenzake huyo alimponda kuwa ni changudoa mzee, kitu kilichomchafua zaidi mama huyo wa watoto watano.

Kufuatia madai hayo, Zari alirusha kombora kwa kumuita mwenzake mchawi, akidai ‘ndumba’ zake alizotumia kumuibia mpenzi wake zimeisha nguvu na akijinadi kuwa yeye ni changudoa mzee mwenye mafanikio.

Kabla ya hapo, wawili hao walifanya shoo siku moja nchini Uganda katika maeneo yaliyo jirani, kitu ambacho kilionesha dhahiri kuwa bado wana bifu.
Chanzo: Global Publishers

Simon Msuva Ametua Nchini kwa Mapunziko

$
0
0
Simon Msuva Ametua Nchini kwa Mapunziko
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Difaa El Jadidi ya nchini Morocco, Simon Msuva ametua nchini kwa mapunziko ya muda mfupi huku akiwa na hari na hamasa kubwa ya kuhakikisha anacheza soka lakulipwa barani Ulaya.



Msuva ambaye awali alikuwa akiitumikia klabu ya Yanga kabla ya kusajiliwa nchini Morocco kwa kulipwa mshahara mnono unaokadiriwa dola 4,000 (takribani Sh milioni 9) amesema kuwa bado lengo lake kubwa ni kuhakikisha anacheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Hii Hapa Ahadi ya Eddy Kenzo kwqa Mashabiki Zake

$
0
0
Hii Hapa Ahadi ya Eddy Kenzo kwqa Mashabiki Zake
Je unatamani kuitazama video ya ngoma yake mpya ‘The Heat’ ya Eddy Kenzo?
Basi unatakiwa kukaa mkao wa kula kungoje hilo. Msanii huyo ameahidi kuachia video ya ngoma hiyo iliyotoka mwezi August mwaka muda si mrefu.
Kenzo amethibitisha hilo kupitia mtandao wake wa Twitter kwa kuandika, “New MUSIC video The Heat drooping soon.”

Mamlaka ya Hali ya Hewa Yatoa Angaalio ya Mvua Kuba Zinazotarajiwqa Kunyesha

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Yatoa Angaalio ya Mvua Kuba Zinazotarajiwqa Kunyesha
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo ya kunyesha kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia leo Alhamisi na kesho Ijumaa.

Taarifa ya TMA imebainisha mikoa itakayokubwa na mvua hizo ni Pwani ya Kusini ambayo ni Lindi na Mtwara, Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mbeya, Iringa, Songwe na Rukwa, Dar es Salaam na Pwani.

“Upepo wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini; kwa kasi ya Km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza;

“Hali ya Bahari, inatarajiwa kuwa mawimbi madogo hadi makubwa kiasi na matazamio kwa siku ya Ijumaa Januari 5,2018, kuongezeka kwa mvua katika mwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi.”

Hata hivyo, tayari mvua hizo zimekwisha kuanza na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani mvua ilinyesha jana Jumatano usiku katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.



Baada ya Babu Seya na Mwanaye Kwenda Ikiulu Mjadara Mkari Waibiuka

$
0
0

Baada ya Babu Seya na Mwanaye Kwenda Ikiulu Mjadara Mkari Waibiuka
Inawezekana ilikuwa ni nia njema kwenda kumshuku Rais kwa kumpa msamaha uliomuepusha na kifungo cha maisha, lakini kitendo hicho cha Nguza Mbangu Viking na wanawe kimepokelewa kwa hisia tofauti.

Nguza, ambaye ni mtunzi wa wimbo maarufu wa “Seya” uliomfanya apachikwe jina la Babu Seya katika kesi ya kubaka na kulawiti wanafunzi wenye umri kati ya miaka sita na nane, na mwanae Johnson Nguza au Papii Kocha, walisamehewa na Rais John Magufuli pamoja na wafungwa wengine 8,150 siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Alikuwa kitumikia kifungo cha maisha baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kubaka na kulawiti watoto hao, na juhudi za kupangua hukumu hiyo Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na nyuingine za nje hazikuweza kufanikiwa.

Lakini msamaha wa nadra kutokea kwa wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha na wenye makosa ya kubaka na kulawiti, ulimuepusha nyota huyo maarufu kwa kupiga gitaa la solo na mara tu alipotoka alisema angependa kuonana na Rais kwa ajili ya kumshukuru na akapata nafasi hiyo juzi.

Lakini kupokelewa kwake kumeibua hoja tofauti.

Wako wanaowaangalia waliofanyiwa vitendo hivyo miaka 13 iliyopita, ambao kwa sasa ni wasichana, na wengine wanaoangalia nafasi waliyoipata tofauti na wengine walionufaika na msamaha huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watu waliohojiwa na gazeti hili walisema tukio la kwenda Ikulu halikupaswa kupambwa, pamoja na ukweli kwamba Katiba inampa Rais mamlaka ya kusamehe wafungwa wa aina yoyote.

“Sikuona haja ya Ikulu kulikuza suala la wanamuzi hao kwenda kuonana na Rais. Baada ya kusamehewa kwa nini wanageuzwa kama mashujaa?,” alihoji Wakili Onesmo Kyaule.

“Inawezekana kabisa hilo likawa na picha tofauti kwa watu waliofanya au watakaofanya makosa kama yao.”

Ikulu ilisambaza picha za Nguza na familia yake wakiwa wanatembea kuelekea Ikulu na baadaye wakiwa kwenye mazungumzo na Rais na nyingine zinazoonyesha wakisalimiana na baadaye wakitoka.

Dk Kyauke alisema licha ya sheria kumpa Rais mamlaka ya kusamehe, wanamuziki hao walipaswa kurejeshwa kwao baada ya kusamehewa.

Naye wakili mwingine wa kujitegemea, Alloyce Komba wa kampuni ya Haki Kwanza, alipinga kitendo cha wanamuziki hao kwenda Ikulu kwa maelezo kuwa licha ya kusamehewa kwao, bado wana hatia ya ubakaji.

Alisema lingekuwa jambo la maana kama wangeitisha mkutano na waandishi wa habari na kumshukuru Rais kuliko kwenda Ikulu na suala lao kutangazwa.

“Rais akisamehe wafungwa anakuwa na vigezo vyake ila katika hili la kina Babu Seya, nimeshtuka kidogo,” alisema.

Alibainisha kuwa Papii Kocha na Babu Seya walitiwa hatiani na hata walipokata rufaa walishindwa.

“Kwa kuwa tunaheshimu utawala wa sheria na Mahakama ndio yenye uamuzi wa mwisho na wahusika wameshindwa kwenye hizo ngazi zote, tunatakiwa tuheshimu,” alisema.

“Kwenda Ikulu kuna heshima, hawa heshima hii wameipata wapi? Aaah sisi tunaomuamini Mungu tunasema sawa ila katika sheria, sheria ni sheria.”

Alisema msamaha huo unaweza ukawa kikwazo kwa vyombo vya Serikali vinavyopambana kudhibiti makosa ya ubakaji na mengineyo.

Naye Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Saut) alisema: “Sikutegemea kama wangeenda Ikulu kwa sababu msamaha wa Rais haufuti hukumu. Hauondoi jinai waliyofanya.

“Sijasikia kama wameomba radhi nasema hivi kwa sababu watoto waliotendewa vitendo hivyo pamoja na wazazi wao bado wapo na wanaliona suala hili.”

Alisema kama wanamuziki hao wangekaribishwa Ikulu sambamba na waliotendewa vitendo viovu walau ingeeleweka, “hata Serikali kufikiria fidia kwa waliotendewa vitendo vile nayo ingeweza kueleweka”.

Kwa upande wake, Dk James Jesse wa Shule Kuu ya Sheria Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) pia alisema msamaha haujafuta kosa.

“Unapopewa msahama sio kwamba kosa lako linafutwa. Rais ana mamlaka ya Kikatiba kufanya alichokifanya na kama watu watawaza tofauti huwezi kuwazuia,” alisema.

Matonnya Aliyepata Msamaha wa Magufuli Naye Ataka Kwenda Ikulu

$
0
0
Matonnya Aliyepata Msamaha wa Magufuli Naye Ataka Kwenda Ikulu
Wakati Babu Seya na mwanaye wakiwa tayari wametimiza azima yao ya kumuona Rais, Mganga Matonya, aliyeepushwa kifungo cha maisha, analalamikia hali yake kuwa imemzuia kusafiri kwenda Ikulu kumueleza jambo Rais John Magufuli.

Matonya, ambaye alikuwa mfungwa mwenye umri mkubwa kuliko wote kati ya walioachiwa huru, alikuwa anatumikia kifungo cha maisha baada ya awali kupata msamaha wa adhabu ya kunyongwa kutokana na kupatikana na hatia ya kuua na ameishi gerezani miaka 43.

“Mtakumbuka nilikuwa mtu wa kwanza kati ya tuliotoka gerezani niliyetamka kutaka nimuone Rais, lakini hadi sasa nashindwa kumuona,” alisema Matonya ambaye aliiambia Mwananchi siku alipotoka kuwa ana neno la kumueleza Rais na asipopata nafasi, atakufa nalo.

“Siko tayari kumwambia mtu mwingine zaidi ya Magufuli kipenzi changu,” alisema.

Akizungumza kwa simu kutoka Kijiji cha Wiliko, Matonya alisema taarifa za wanamuziki hao alizipata kutoka kwa mtoto wake na kwamba zilimliza kwani angepata nafasi hiyo kabla hajafa, angejisikia huru katika nafsi yake.

“Alipokuja (Rais Magufuli) kwenye mkutano wa CCM Dodoma niliwaomba watoto wangu wanipeleke. Tatizo wanaona kama nimechanganyikiwa lakini siyo kweli,” alisema Matonya.

Mzee huyo aliomba taasisi na mashirika mengine kumsaidia kumuona Rais Magufuli.

Mtoto wake, Aron alisema aandike ujumbe wake hata magazetini na Rais atauona.


Moto Wazuka Ghafla Kwenye Nyumba ya Clinyon

$
0
0
Moto Wazuka Ghafla Kwenye Nyumba ya Clinyon
Moto uliozuka ghafla katika makazi ya rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton umezua hali ya tafrani lakini hata hivyo ulidhibitiwa mapema.

Wazima moto karibu na mji wa New York walikimbia nyumbani kwa kiongozi huyo Clinton kukabiliana na moto uliozuka jana Jumatano jioni.

Msemaji wa familia ya Clinton ambaye hakutajwa jina lake alieleza kuwa moto huo ulizuka kwenye nyumba iliyotumiwa na maofisa wa kitengo cha ujasusi cha Secret Service.

Alisema nyumba anayoishi Bill na mkewe Hillary Clinton ambaye wakati fulani alikuwa waziri wa mambo ya nje haikuguswa na moto huo. Nyumba ya Clinton na maofisa usalama zimekaribiana.

Ripoti zinasema kuwa wakati moto huo ukizuka Rais Clinton na mkewe hawakuwepo huku msemaji huyo akifafanua kuwa "kila kitu kiko shwari." Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Familia ya Clinton imekuwa ikiishi katika mji wa New Castle, takribani kilomita 64 kaskazini mashariki mwa mji wa New York.



Penny Afunguka Kuwa na Gundu la Ndoa kwa Mwaka 2017

$
0
0
Penny Afunguka Kuwa na Gundu la Ndoa kwa Mwaka 2017
MTANGAZAJI wa Runinga ya Magic Swahili kupitia kipindi cha Harusi Yetu, Penniel Mungilwa ‘Penny’amefunguka kuwa, kuna uwezekano alikuwa na gundu la kutoolewa mwaka 2017 lakini anaamini mwaka huu, 2018 ataolewa kwa uwezo wa Mungu.

Akizungumza na gazeti hili, Penny alisema mwaka huu yuko tayari kwa ndoa na kwa mwanaume sahihi kwani ameomba vya kutosha.

“Mwaka huu ni wa baraka kwangu na gundu nyingi zimeshaondoka 2017, mwaka huu kwangu ishallah shela litakaa mwilini mwangu, mwanaume yupo tayari,” alisema Penny bila kumtaja jina mwanaume wake.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Hizi hapa sababu za Roberto Carlos kuamini CR7 ni bora kuliko Messi

$
0
0
Mjadala mkubwa katika soka ulimwenguni kwa sasa ni juu ya uwezo wa wachezaji wawili mmoja anakipiga Real Madrid na mwingine yuko Barcelona pale, ndio ni Cristiano Ronaldo na Lioneil Messi.

Mjadala wa Messi na Ronaldo unaonekana mpana sana na kila mtu ana sababu zake kumkubali huyu na kumkataa huyu, na hata kwa beki wa zamani wa Brazil Roberto Carlos naye ana sababu za kumkubali zaidi CR7.

Carlos anaamini kwamba Cristiano Ronaldo ni bora zaidi ya Lioneil Messi kwani amekuwa akimuona Ronaldo mazoezini jinsi amekuwa akijituma na pia juhudi zake mazoezini anavyozionesha uwanjani.

Carlos anasema tofauti kati ya Messi na Ronaldo ni kwamba Ronaldo anajituma sana akiwa uwanjani na pia mazoezini kiyu ambacho Lioneil anaonekana kukikosa na zaidi anaamini katika kipaji chake.

Carlos amewahi kuichezea Real Madrid kwa miaka zaidi ya 14 kabla yakuondoka kutoka kwa wababe hao wa Hispania mwaka 2007 ambapo alikwenda kujiunga na klabu ya Fernabache ya nchini Uturuki.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0
SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

Hofu Yatanda United, Mourinho Aanza Kupaki Mabegi yake Tayari Kuondoka

$
0
0
Mwishoni mwa mwaka jana na mwanzo wa mwaka huu kocha wa Manchester United amekuwa habari kubwa, wengi wanaona Jose Mourinho amekosa raha na mambo yanayoendelea EPL.

Inasemekana kwamba uhusiano wa Mourinho na CEO wa Manchester United Ed Woodward hauko vizuri na hii inatokana na Jose Mourinho kutokubaliana na sera za usajili ambazo anafanya Woodward.

Mbaya zaidi Woodward na Mourinho wamepishana kuhusu manunuzi ya beki Danny Rose ambaye ilitajwa kwamba anakaribia kutua United lakini Manchester wanaonekana kugoma kutoa pesa za kumnunua.

Inadaiwa pia kwamba Mourinho hakai tena Manchester kama zamani na muda wake mwingi huwa anautumia London ambako ndiko nyumba yake ilipo huku Manchester akiwa anaishi katika hoteli.

Kivuli cha Pep Gurdiola nacho kinatajwa kumsumbua sana Jose Mourinho kwani sasa inaonekana wazi kwamba Man City wanaelekea kubeba kombe la EPL jambo ambalo linamfanya Mou kujiona mnyonge.

Tayari PSG wameshatajwa kama sehemu ambayo Mourinho anaelekea, na tayari Mou anasema jiji la Paris ni mahala pazuri kuishi kwani alizisikia sifa za mji huo kutoka kwa mwanaye ambaye amewahi kukaa katika mji hio.

Waandishi wengi na wachambuzi wa masuala ya michezo nchini Uingereza wametabiri kwamba Jose hatakuwa na United katika msimu ujao wa ligi na k

Kitu Msuva kaandika Baada ya kusikia Mahadhi Kapiga Magoti Kuomba Msamaha

$
0
0
Siku moja baada ya Juma Mahadhi kuomba msamaha kwa viongozi wa Yanga na mashabiki ambao wamekuwa wakilalamika kuwa ameshuka kiwango kwa uzembe.



Mshambuliaji wa zamani wa Yanga ambaye anacheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe huu baada ya kuona Juma Mahadhi kaomba msamaha kwa kupiga magoti.



“#Neno Msamaha , Nisamehe sio Ujinga muhimu umejua wapi umeteleza Naimani Unakipaji kikubwa sana Endelea kuamini kwamba unaweza No time to waste Brother Hongera kwa kutambua ilo naimani wewe ni Champion Endeleza mapambano Mdogo wangu usonge mbele uje ufike Nilipo na Zaidi Nafasi bado Unayo @jumamahadhi21 Twende tuisogeze Tanzania Yetu 💪“

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Juma Mahadhi Jumanne January 3 2018 aliandika ujumbe wa kuomba radhi mashabiki na baadae wakati wa game ya Mapinduzi Cup ya Yanga dhidi ya Mlandege alifunga goli na kupiga magoti ikiwa ni ishara ya kuomba msamaha mbele ya mashabiki uwanjani hapo.

Museveni Amuandikia Barua Rais Magufuli

$
0
0
Museveni Amuandikia Barua Rais Magufuli
Rais wa Uganda Kaguta Museveni leo Januari 4, 2018 amemuandikia ujumbe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumpa salamu za mwaka mpya pamoja na kuzungumza juu ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.


Ujumbe huo wa Rais Museveni umewasilishwa Ikulu ya jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Sam Kutesa ambapo pia Waziri huyo amefanya mazungumzo na Rais Magufuli.
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images