Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

Makamo wa Rais Awasili Pemba kwa Ufunguzi wa Soko la Konde

0
0
Makamo wa Rais Awasili Pemba kwa Ufunguzi wa Soko la Konde
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili Pemba tayari kwa ufunguzi wa Soko la Konde ambapo alipokelewa na Waziri wa Kilimo,Mifugo,Maliasili na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid na viongozi wengine wa Chama na Serikali.


CCM Watafuta Diwani "Msaliti" Aliyewapa Kura UKAWA

0
0
Wajumbe wa CCM wanaoingia kwenye Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam, wamesema wapo katika hatua za mwisho za kumpata mjumbe mwenzao aliyesababisha wao kushindwa uchaguzi wa naibu meya wa jiji hilo.

Uchaguzi huo uliokuwa na mchuano mkali kutokana na kila upande kuwa na wajumbe kumi na moja, ulifanyika juzi katika ukumbi wa Karimjee na Mussa Kafana wa CUF akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) aliibuka kidedea kwa kupata kura 12 dhidi ya 10 alizopata Mariam Lulida wa CCM.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mjumbe baraza hilo CCM, Abdallah Chaurembo alisema tayari wanao ushahidi na wameshaanza kumbaini mjumbe ambaye alisababisha chama chao kushindwa katika uchaguzi huo.

“Tunataka kuirahisishia kazi kamati ya siasa ya mkoa kwa kumpata kwanza mjumbe huyu, halafu wao ndiyo watakaokuwa na jukumu la kumtangaza na kumchukulia anazostahili kwa mujibu wa makosa yake,” alisema Chaurembo.

Chaurembo ambaye pia ni Meya wa Temeke alisema walishaanza kumbaini mjumbe huyo kabla ya kazi ya kuhesabu halijakamilika na kudai kwamba hakuwa na nia ya dhati na CCM.

“Tulishakijua alichokuwa akikifanya, kwanza alikuwa anatetemeka wakati anaenda kupiga kura. Wakati yupo katika eneo la kupiga yeye ndiyo alitumia takriban dakika tano wakati wenzake nusu dakika.

“Hivi mtu unachukua takriban dakika tano nzima katika kupiga kura, una nini wewe, ina maana hujui kusoma wala kuandika? Alihoji Chaurembo. Nawaambia WanaCCM tutampata mtu huyo very soon (muda mfupi).

Alisema wameamua kushughulikia jambo hilo, ili iwe funzo kwa madiwani wengine wasiokitakia mema chama hicho na kwamba, hiyo itakuwa njia ya kuwaondoa wale viongozi wasio na masilahi na CCM.

Alieleza kuwa wajumbe wa CCM katika baraza hilo, wana imani wameshindwa katika uchaguzi kwa hoja mbili ambazo ni Ukawa kutumia utemi wakati kura mbili ziliharibika, na mjumbe mwenzao kuharibu kura na siyo kumpigia kura mgombea wa upinzani.

Katika uchaguzi huo, Chaurembo na meya mwenzake wa Ubungo (Chadema), Boniface Jacob nusura wazichape wakati wa shughuli ya kuhesabu kura kama si wajumbe wa uchaguzi huo kuwatenganisha.

Chaurembo aliendelea kwa kufafanua kuwa mjumbe huyo akishapatikana wajumbe wa CCM wa baraza ndiyo watakaokuwa mashahidi kwenye kamati ya siasa ya mkoa.

Naibu Meya asimulia alivyobebwa

Wakati Chaurembo akieleza hayo, naibu meya mteule, Kafana ameeleza namna alivyochukuliwa nyumbani kwake na kupelekwa kupiga kura akiwa mgonjwa.

Kafana alimweleza mwandishi wetu jana kwamba alikuwa katika hali mbaya kiafya kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na malaria, kifua na tumbo la kuhara.

Alisema baada ya kuwa na hali hiyo, alitoa taarifa kwa ofisi ya mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, ambayo iliamuru kutuma mwakilishi kwa ajili ya kuthibitisha kama anaumwa.

“Alikuja mwakilishi kutoka ofisi ya mkurugenzi ambaye alikwenda hadi katika zahanati niliyokuwa nikitibiwa na kupata uthibitisho, kisha akaja nyumbani kwa kupiga picha vyeti na kuniona,” alisema Kafana.

Alisema akiwa amepumzika baada ya kutoka hospitali, kadri muda ulivyokwenda simu zilikuwa zikipigwa kwa ndugu zake zikieleza kuwa anatakiwa kwenda kupiga kura hata kama ni mgonjwa na kwamba uchaguzi hauwezi kuahirishwa.

“Waliwapigia ndugu zangu kwamba wanakuja kunichukua na wakahakikishia nisiwe na wasiwasi kila kitu kitakwenda sawa. Haukupita muda alikuja Kubenea (Saed –Mbunge wa Ubungo) na vijana wengine kunichukua mkukuku.

“Ule mwendo haukuwa wa kawaida, gari lilikimbia sana kuhakikisha nashiriki uchaguzi. Ingekuwa jambo hili ni la mgombea binafsi nisingeenda kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya, lakini wajumbe wenzangu wa Ukawa wakasema haiwezekani lazima nishiriki hata kama mgonjwa,” alisema Kafana.

Hata hivyo, baada ya kuingia katika ukumbi wa mikutano Kafana hakuweza kupiga kura badala yake alisaidiwa na Kubenea ambaye alikuwa kiongozi kwa upande wa wajumbe wa Ukawa.

Kafana alisema alikuwa na uhakika wa kuibuka kidedea kutokana na idadi ya namba za wajumbe wanaounda Ukawa, lakini kutokana wajumbe wenzake kumhitaji ilimlazimu kuitikia wito huo huku akiwa taabani.

“Nilikuwa najiamini katika uchaguzi ule kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati yangu na wajumbe wa Ukawa na CCM. Ndiyo maana sikushangaa kusikia kupigiwa kura na mmoja wajumbe kutoka CCM,” alisema Kafana.

Kuhusu madai ya yeye kuigiza mgonjwa wakati ni mzima wa afya, Kafana alisema “ Mimi ndiyo mgonjwa, nawashangaa hao wanaosema mimi ni mzima. Isingekuwa wajumbe wa Ukawa kunitaka niende, binafsi nisingeshiriki. Kwenda na hali ile ni kujidhalilisha.”

Kafana aliwashukuru wajumbe wenzake kwa kumuwezesha kutetea nafasi hiyo na kwamba akisema wamefanya kazi kubwa.

Alisema awali, alijua kwamba uchaguzi huo ungekuwa wa kawaida lakini kwa hali ilivyokuwa, dhana hiyo ilikuwa ni kinyume chake.

Chanzo: Mwananchi

Hatimaye Rugemalira Awataja Wezi wa Fedha za Escrow Mbele ya Mahakama

0
0
Hatimaye Rugemalira Awataj Wezi wa Fedha za Escrow Mbele ya Mahakama
MFANYABIASHARA, James Rugemalira anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja aliodai ni wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyosema awali kwamba anawafahamu.

Watu hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,  baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Ruswa (Takukuru), Leonard Swai,  kueleza kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

 Baada ya kuelezwa hayo, wakili wa utetezi, Michael Ngalo, ameomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi wa kesi hiyo na kama hawawezi waiondoe mahakamani.

 Baada ya kuelezwa hayo, Rugemaliraa alinyoosha mkono ambapo alidai yeye ni mgonjwa wa kansa kwa miaka tisa sasa na amekuwa akipatiwa matibabu nchini India, lakini kwa sasa ugonjwa huo umejitokeza kwa njia ya uvimbe katika sehemu za siri.

 Akiiambia mahakama kuhusu suala la aliodai ni wezi, Rugemalira alidai alishawasilisha nyaraka za ushahidi kwa Takukuru kwamba ‘mwizi’ aliyeisababishia serikali hasara ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao waliisababishia  hasara ya Sh. trilioni 37.

Pia amedai kuwa watu hao aliowaita wezi hao ndiyo wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Sh. trilioni 16.

 Naye mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi, aliiambia mahakama hiyo kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana, pia yupo tayari kutoa ushirikiano wowote zikiwemo nyaraka ili kubaini ukweli wa kesi hiyo.

Baada ya kueleza hayo, wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemalira aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.

Akitoa ufafanuzi, Hakimu Simba alisema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia ameutaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu.

VIDEO: Babu Seya, Papii Kocha Kurekodi Wimbo Wanene

0
0
Wasanii Wakongwe Nchini, Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye, Johnson Nguza ' Papii Kocha' wakiambatana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza walitembelea studio za Wanene Entertainment zilizopo Mwenge, Dar es Salaaam.

Wasanii hao walipelekwa katika studio hizo na Waziri Shonza na kupokelewa na mmiliki wa Wanene, Dash ambapo walifanya mazungumzo ya pamoja yaliyolenga kurekodi nyimbo kwa wasanii hao na kusaidiwa kurudisha vipaji vyao ikiwa ni sapoti ambayo Wizara imeamua kuitoa kwa wasanii hao.

Serikali Yawasaidia Babu Seya na Wanae

0
0
Serikali Yawasaidia Babu Seya na Wanae
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewasaidia wasanii Nguza Viking 'Babu Seya' na mwanaye Johnson Nguza 'Papii Kocha' kwa kuwapeleka studio ili waweze kurudi rasmi katika kazi yao ya muziki.


Akiongea mbele ya waandishi wa habari Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amesema kuwa leo Januari 5, 2018 amefanikiwa kuwafikisha wasanii hao katika studio za Wanene ambapo hapo wataweza kurekodiwa kazi zao na kusaidiwa mambo mengi kama ambavyo ameweza kuongea na Mkurugenzi wa studio hizo.

"Tunajua kwamba hawa watu hawakuwa kwenye ulimwengu huu wa muziki muda hivyo wanahitaji 'support' kwani mtu anaporudi vitu vingi vinakuwa vipya hivyo nikaona ni vyeme kukutana nao na wamenieleza mpango wao ni kurudi kwenye tasnia ya muziki. Mimi kama Naibu Waziri nikaona ni vyema niwachukue na kuwaleta hapa studio za Wanene kwani tayari niliongea na Mkurugenzi wa studio hizi na aliahidi yupo tayari kuwasaidia kwa hali na mali" alisema Shonza

Aidha kwa upande wake Babu Seya ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa yote na kusema yeye sasa anachotaraji ni kufanya kazi tu na kusema kuwa mambo makubwa yatakuja mbele.

Babu Seya na Papii Kocha waliachiwa huru kwa msahama wa Rais Magufuli mnamo Disemba 9, 2017 na walitoka gerezani siku hiyo hiyo baada ya hapo walipumzika kwa wiki tatu na kuja kukutana na Rais Magufuli Ikulu Januari 2, 2018 ambapo walikwenda kumshukuru.

Babu Seya na Papii Kocha wametumikia kifungo kwa miaka 13 jela kufuatia kukutwa na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wadogo.

Watu Washtushwa na Muonekano Mpya wa Wowowo la Ruby

0
0
Watu Washtushwa na Muonekano Mpya wa Wowowo la Ruby
Jana msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Ruby kupitia ukurasa wake wa Instagram aliposti picha ikimuonesha mwenye umbo kubwa tofauti na muonekano wake wa siku zote.

Picha hiyo ambayo ni ya kwanza kwa mwaka 2018 kwa msanii huyo kuonekana, Ruby aliiweka na kuwatakia mashabiki wake Kheri ya Mwaka mpya.

Watu wengi waliotoa maoni kwenye posti hiyo wameonekana kushangaa mabadiliko hayo ya ghafla huku wengine wakidai ametumia dawa za kuongeza makalio wengine wakiamini kuwa ametumia App ku’edit picha hiyo.

utamu_baby Mchina ruby huo yaan unatudangny hvhv wakat ulikua mwembamba kama mwiko Wa pilau😂😂
fasamalsaid Kweli hii mwaka mpya mambo mapya , hongera kwa mchina #wowowo
koiyarachel@laur_de_patrique katoa wapi huu msambwanda jomoni katuzidi hadi sisi. Kweli kati ya kiboko na mamba, mamba ndio kiboko!!! pooohhhh…
mamukimwanyaMara paah 2018 kitako icho
officialsiahshoo1Kwel uchaw upo had 2018 🙊🙊unalala slim unaamka na bonge la wowowo
mdogo_wake_hamisakama ni vigodoro duuuh wew umezidi umeweka kochi zima
Ukweli ni kwamba Ruby hajatumia dawa ya kichina wala kuvaa kigodoro bali picha hiyo imefanyiwa editing  kupitia Application maalumu zinazofanya kazi hiyo ya kuongeza maumbo kwenye picha.


Picha Orijino ya Ruby aliyopiga kabla ya kueditiwa.

Kuna Applications kibao ambazo hutumiwa na wanawake kuedit picha kama ya Ruby ambazo kama hutakuwa mtundu wa mambo ya Picha huwezi kugundua hata siku moja kama picha imefanyiwa Editing.

Wachezaji Wanne Waongezewa Mkataba Manchester United

0
0
WachezajiWanne Waongezewa Mkataba Manchester United
Klabu ya soka ya Manchester United wamewaongezea mikataba wachezaji wake wanne ambao mikataba yao ilikuwa inafikia ukingoni.



Wachezaji hao ambao wameongezewa mikataba hiyo ni Juan Mata, Ander Herrera, Ashley Young na Daley Blind hadi mwisho wa msimu ujao. Wachezaji hao walikuwa wanatakiwa kuondoka bure mwishoni mwa msimu huu lakini United wamewapatia mikataba ya haraka wachezaji hao na kuimarisha ya maadili yao ya uhamisho kwa kuanzisha vifungu vinavyoongeza mikataba yao kwa miezi 12 hadi Juni 2019.

Mchezaji mwengine ambaye anatajwa kutaka kuongezewa mkataba ni Luke Shaw ambaye amewavutia sana mashabiki wa United kutokana na uwezo wake katika wiki za hivi karibuni na inawezekana kupewa mpaka mwisho wa msimu kuthibitisha thamani yake kabla ya uamuzi kufanywa juu yake.



Hata hivyo Marouane Fellaini amekataa kuongeza mkataba mpya na timu hiyo ambapo mwishoni mwa msimu huu atakuwa huru na timu ya Besitkas inaongoza katika mbio za kutaka kumsajili kiungo huyo wa Ubelgiji.

Mourinho hataki kumuuza Fellaini katika dirisha la uhamisho la majira ya baridi na amejiandaa kumpoteza wakati wa majira ya joto. licha ya matatizo yake ya sasa ya kuumia. Fellaini ameanza mechi moja tu tangu mwisho wa Septemba kwa sababu ya kuumia.

Aliyemuua Ndugu wa Rihanna Akamatwa na Kufikishwa Mahakamani

0
0
Aliyemuua Ndugu wa Rihanna Akamatwa na Kufikishwa Mahakamani
January 5, 2918 Mwanaume mmoja amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya Tavon Kaiseen Alleyne, 21 ambaye ni ndugu wa mwanamuziki wa kimataifa Rihanna.

Taarifa zilizotolewa na Nation News zimesema, “kijana huyo anafahamika kama Shawayne Dashawn Williams ana umri wa miaka 23, amefunguliwa mashtaka ya mauaji hayo ya Alleyne ambayo yametokea wiki iliyopita katika sikukuu ya Christmas.”

Shawayne amefikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kesi hiyo imeahirishwa na mtuhumiwa amerudishwa gerezani huku hukumu ya kesi hiyo ikipangwa kutolewa January 31, 2018.



Kabla ya tukio marehemu Alleyne alikuwa akitembea karibu na nyumba yake majira ya saa 1 usiku kabla ya kufatwa na mtu asiyefahamika na kisha kupigwa risasi. Hata hivyo Alleyne alikimbizwa hospitali ya Queen Elizabeth iliyopo Bridgetown lakini alifariki dunia.

Wakati huo huo marehemu Tavon Alleyne alikuwa na Rihanna saa moja kabla ya kufariki dunia wakisherehekea pamoja sikukuu ya Christmas.


Madiwani Wengine wa Chadema Watangaza Kujivua Uanachama na Kujiunga na CCM

0
0
Madiwani Wengine wa Chadema Watangaza Kujivua Uanachama na Kujiunga na CCM
Madiwani wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zakayo Chacha Wangwe wa kata ya Turwa wilaya Tarime, na mwenzake wa Kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa Mjini, Angelusi Mbogo wametangaza kujivua uanachama wa Chama hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa kimepoteza imani yao kwa wananchi huku pia kikiendeshwa kibabe hivyo wameamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuleta maendeleo na vita dhidi ya ufisadi.

Hali ya Kingunge Yaimarika Aendelea na Matibabu

0
0
Hali ya Kingunge Yaimarika Aendelea na Matibabu
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema hali ya mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, inaendelea kuimarika baada ya kuanza kupata matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa hospitalini hapo, Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Ngomuo amesema kwa sasa afya yake imeimarika.

"Anaendelea vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema Ngomuo.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete jana Alhamisi jioni alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mwanasiasa huyo.

Kingunge aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, alifiwa na mke wake Pares Mwiru jana Alhamisi saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa.

Neema amesema mke wa mwanasiasa huyo alifikishwa Muhimbili tangu Oktoba 3, mwaka jana.

Wakati Peras akifariki,  mumewe Kingunge anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

Awali mtoto wa Kingunge, Kinje Mwiru alisema kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

Wateja wa Benki Tano Zilizotangazwa Kufilisika Kulipwa Zaidi ya Milioni 1.5

0
0
Wateja wa Benki Tano Zilizotangazwa Kufilisika Kulipwa Zaidi ya Milioni 1.5
Bila kujali ni kiasi gani walitunza, wateja kwenye benki tano zilizotangazwa kufilisika, wataambulia si zaidi ya Sh1.5 milioni ya amana zao kwa mujibu wa sheria.

Jana, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu aliwaaga Watanzania baada ya kuiongoza taasisi hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa kwa miaka 10 mfululizo na kueleza kuwa tayari benki zilizofilisika zimekabidhiwa katika Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kwa taratibu za kisheria.

Kaimu mkurugenzi wa bodi hiyo, Richard Malisa alimhakikishia Profesa Ndulu kuwa taratibu za malipo hayo zitafanyika haraka iwezekanavyo huku kiwango cha juu kitakacholipwa kwa wateja kikiwa ni Sh1.5 milioni.

“Mwenye amana za Sh100,000 atalipwa kiasi hicho na mwenye Sh50,000 atalipwa hiyo ila kiwango cha mwisho ni Sh1.5 milioni. Kwa hiyo, kama wewe una Sh5 milioni utakacholipwa ni Sh1.5 milioni,” alisema.

Taasisi tano zilizotangazwa kufilisiwa ni Benki ya Wanawake Convenant na Efatha. Nyingine ni benki za wananchi; Njombe na Meru pamoja na Benki ya Wakulima Mkoa wa Kagera (KFCB) ambazo zinaungana na FBME, Twiga Bancorp na Benki ya Wananchi Mbinga zilizofilisika na kufutiwa leseni mwaka jana.

Nyingine tatu zimewekwa chini ya uangalizi ambazo ni Benki ya Ushirika Kilimanjaro, Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) na Benki ya Wananchi Tandahimba ambazo, endapo zitashindwa kukidhi vigezo, baada ya muda, nazo zitafilisiwa.

Kuhusu athari za kufungiwa na kufilisiwa kwa benki hizo Profesa Ndulu alisema jumla ya amana za benki zote nane ni Sh67.6 bilioni ambazo ni sawa na asilimia 0.38 ya benki zote 58 zilizopo nchini hivyo kutokuwa tishio.

“Hakuna athari zozote za kiuchumi zinazoweza kujitokeza kutokana na kufungiwa kwa benki hizi. Lakini, endapo tungeziacha ziendelee kujiendesha hivyohivyo, madhara yake yangekuwa makubwa,” alisema.

Profesa Ndulu alitaja sababu za benki ndogo kutofanya vizuri kuwa ni kutokana na kukosa mtaji, wigo mdogo wa biashara, ukubwa wa bodi zinazozisimamia pamoja na gharama kubwa za uendeshaji.

“Tumewashauri waungane, wawe shirikisho halafu hizo benki nyingine ziwe matawi kusaidia mfumo wao wa undeshaji uwe mmoja kupunguza gharama lakini utekelezaji umekuwa mgumu,” alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Benki za Kijamii (Cobat), Lukwaro Senkoro alikiri kupewa ushauri huo na BoT lakini akasema muda haukuwa rafiki kwao kuutekeleza ingawa hatua za makusudi zilichukuliwa.

Alisema katika jitihada hizo za kukamilisha mchakato wa kuziunganisha benki za wananchi, chama hicho kilianza kwa kukutana na bodi za wakurugenzi wa benki husika ambazo ziliafiki ushauri huo na kuahidi kwenda kuzungumza na wanahisa wao.

“Huko ndiko kulikosumbua,” alisema. “Benki sita zilikubali kuungana lakini tatu wanahisa wake wanahitaji muda wa ziada kufikiri kuhusu suala hilo,” alibainisha.

Alisema kwenye mkakati wao, walishafanikiwa kumpata mwekezaji atakayeiwezesha Benki ya Taifa ya Wananchi ambayo ingeanzishwa lakini baada ya benki tatu kutangazwa mufilisi, mchakato huo utakuwa umefika mwisho.

Alisema ushauri wa BoT ni wazo jipya lililohitaji kujadiliwa na wadau kabla ya kuridhia kuungana na kujiendesha chini ya mwamvuli mmoja hivyo kuhitaji muda wa kutosha wa uelimishaji.

“Ushauri ulitolewa Juni na tulipewa mpaka Oktoba tuwe tumekamilisha taratibu ili Novemba mwaka jana tuungane. Tumepambana mpaka mwisho lakini hatujafanikiwa. Kwa sasa mpango huo hautekelezeki,” alisema kwa masikitiko.

Dkt Shein Ataka Ofisi ya Takiwimu Kuandaa Sera ya Kusimamia Ukusanyaji wa Takwimu

0
0
Dkt Shein Ataka Ofisi ya Takiwimu  Kuandaa Sera ya Kusimamia Ukusanyaji wa Takwimu
Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein amesema ipo haja kwa ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali kuandaa sera ambayo itatoa muongozo wa kusimamia ukusanyaji wa takwimu kwa Tanzania Bara na visiwani.

Rais Shein ameyasema hayo wakati wa ufunguzi Jengo la Mtakimu Mkuu wa Serekali Mazizini Zanzibar, ambapo pamoja na hayo aliomba Mawaziri kushirikiana.

“Lazima tuandae policy ya statistics, tumebahatika tu kwa matatizo yaliyokuwepo tukatunga sheria kwanza, lakini ustaarabu wa suku hizi unatengeneza sera kwanza halafu unatengeneza sheria halafu kanuni sisi tulifanya kinyume kutokana na haja tuliyoifanya bado tunahitaji kutengeneza sera ya Takwimu,” alisema Dk. Shein.

Hata hivyo Dkt Shein aliwaagiza Mawaziri wanahusika na mambo ya Muungano kushirikiana katika mbalimbali kwa faida za pambe zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

0
0
MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na Nasi kwa Namba;0783140065 

Tundu Lissu Aitaka Jamii ya Kimataifa Kuingilia Kati Tanzania

0
0
Tundu Lissu Aitaka Jamii ya Kimataifa Kuingilia Kati Tanzania
Mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema Bw Tundu Lissu amesema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali.

Bw Lissu, akihutubia wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitalini, ameonekana kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwakandamiza wapinzani.

Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali.

Bw Lissu alikuwa akihutubu kutoka hospitali ya Nairobi jijini Nairobi ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa miezi minne sasa.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana.


Bw Lissu amesema kufikia sasa anaamini hakuna uchunguzi wa maana kuhusu kushambuliwa kwake mnamo 7 Septemba unaendelea.

Aidha, amesema Rais John Magufuli, ingawa aliandika ujumbe kwenye Twitter na pia kumtuma makamu wake Samia Suluhu Hassan, hajawahi kuzungumzia hadharani kisa cha kushambuliwa kwake.

"Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama. Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawawkilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela," amesema Lissu.

Bw Lissu amesema amepona na kwamba anashukuru Mungu na wote waliomtakia uponaji wa haraka.

Familia Yajipanga kumpa Taarifa Kiingune Juu kifo cha Mkewe

0
0
Familia Yajipanga  kumpa Taarifa  Kiingune Juu kifo cha Mkewe
Familia ya mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru imesema inasubiri baba yao apewe taarifa za msiba ili wajue taratibu za mazishi za mkewe Pares Mwiru.

Akizungumza na Mwananchi  leo Ijumaa Januari 5, 2017 nyumbani kwa Kingunge, mtoto wake Tonii Ngombale amesema baba yao hadi sasa  bado hajapewa taarifa ya kifo cha mkewe.

Amesema hali hiyo imetokana baba yao kuwa bado yupo  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na mbwa.

"Taratibu  za mazishi zitafahamika baada ya mzee (Kingunge), kupewa taarifa .Tunamsubiri atoe kauli kwa sababu yeye ndio mwenye mji wake na kiongozi  wa familia," amesema  Tonii na kuongeza kuwa

"Hatuwezi kufanya jambo lolote kwa sasa bila yeye kutoa kauli. Tunasikitika kumpoteza mama yetu, lakini wakati huo huo tunaomba dua hawezi kupokea taarifa hii  ya msiba katika hali  nzuri," amesema Tonii.


Tonii amesema jioni wazee wenzake  watajipanga na kwenda hospitalini kwa ajili ya kumpa taarifa za msiba wa mkewe kisha watatangaza utaratibu  wa mazishi hayo.

Pares Mwiru  alifariki dunia jana Alhamisi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.


Lissu Kusafirishwa Kesho Kwenda Nje ya Kenya kwa Matibabu Zaidi

0
0
Lissu  Kusafirishwa Kesho Kwenda Nje  ya Kenya kwa  Matibabu Zaidi
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amefunguka na kusema kuwa kesho Januari 6, 2018 atasafiri na kutoka nje ya Kenya kwenda kufanyiwa matibabu zaidi kufuatia shambulio la kupigwa risasi lililotokea mwaka jana.


Lissu amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa nje ya hospitali ya Nairobi na kusema kuwa amekuwepo hapo kwa takribani miezi minne akifanyiwa matibabu lakini sasa anakwenda kufanyiwa matibabu zaidi sehemu nyingine.

Mbali na hilo Tundu Lissu ameendelea kusema kuwa shambulio lake kupigwa risasi ni tukio la kisiasa ndiyo maana viongozi wa bunge wamekuwa wakishikwa na kigugumizi. Amesema Bunge limeshindwa kumhudumia na kumlipia matibabu kama ambavyo inapaswa kuwa lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa Bunge ambaye amethubutu hata kwenda kumuona.

"Leo nazungumza Bunge la Tanzania halijatoa hata shilingi moja wakati sheria ipo wazi, ndugu zangu wamewaandikia barua ya kuwaomba kupata haki ya matibabu lakini mpaka tunazungumza sasa hivi Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Bunge, Katibu wa Bunge wala hakuna kiongozi wowote wa Bunge aliyefika kuniona kwa miezi hii minne, walijua sitaweza kupona ndiyo maana hawakuwa na Plan ya kunitibu" amesema Lissu

Aidha Mbunge huyo ametoa maoni yake kuwa anaamini jaribio la yeye kutaka kuuawa mnamo Septemba 7, 2017 ni jaribio la kisiasa na amedai anaamini jeshi la polisi nchini Tanzania hawapelelezi juu ya tukio hilo.

"Maoni yangu kilichofanyika kilikuwa ni jaribu ya mauaji ya kisiasa moja kwa moja, mimi siyo mfanyabiashara, jeshi la polisi kwa maoni yangu hawapelelezi tukio hili kwa sababu sijawahi ona mtu anakuja kuniuliza, wanamtaka dereva wangu kwaajili ya kumkamata na sio kumhoji juu ya tukio hilo" amesema Tundu Lissu

Chege Akiri Kuathirika

0
0
Chege Akiri Kuathirika
Msanii Mkogwe kutoka TMK Chege Chigunda amekiri kuwa aliathirika kisaikolojia baada ya kundi la TMK Wanaume Family kuanza kuvunjika.


Chege ametoa kauli hiyo leo akiwa ndani ya Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kwamba boss wake ndiye aliyemtia  moyo nakumfanya azidi kupambana na kufikia mahali ambapo anapataka.

Akijibu swali la mtangazaji, Chege amesema kwamba "Nisiwe muongo kuvunjika kwa TMK Family kulinifanya niathirike kisaikolojia. Namshukuru sana Bosi wangu alinitia moyo na kuniambia kwamba nilikuwa pale kwa ajili ya kujitengeneza na siyo kumtegemea mtu aniimbie. Ujasiri wa maneno yale ndiyo yaliyonitia nguvu"

Akizungumzia kuhusu yeye na Temba kuonekana kuonekana maarufu ndani ya kundi kuliko wasanii wengine, Chege amesema kwamba kwenye kundi hakuwezi kuwa na watu maarufu wawili na kuongeza kwamba ndiyo maana yeye na Temba walibahatika.

Akizungumzia kuhusu wao wawili kuonekana na kusikika zaidi ikiwa ni pamoja na kutengeneza kombinesheni pamoja na Temba, Chege amesema kwamba muunganiko wao ulitengenezwa na wahindi ambao walipenda kazi yao na baadae kuamua kufanya kazi na muunganiko huo wa Chege na Temba.

Yanga na Azam Zapelekwa Mikoani

0
0
Yanga na Azam Zapelekwa Mikoani
Mabingwa wa kwanza wa Kombe la Shirikisho nchini Yanga SC watasafiri hadi mkoani Mbeya kucheza na Ihefu FC katika hatua ya 32 bora ya michuano hiyo ya (ASFC), kati ya Januari 31 na Februari 1.


Yanga ambao walitwaa kombe hilo lilipoanzishwa upya msimu wa 2015/16, wamepangwa na timu hiyo ya daraja la pili ambapo mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Klabu ya soka ya Azam FC yenyewe imepangwa kucheza na Shupavu FC ya Morogoro ambapo mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa CCM mjini humo. Wakati huo Green Worriors waliowatoa mabingwa watetezi Simba SC wamepangwa kucheza na Singida United kwenye uwanja wa Azam Complex.

Timu za ligi kuu ni Mbao FC ambayo itacheza na Kariakoo United huku Majimaji Rangers itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro. Maji Maji FC  wataikaribisha Ruvu Shooting huku Njombe Mji FC watacheza na Rhino Rangers.

Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya January 6

0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya January 6
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images