Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Yaanika Kampuni Zenye Wadaiwa Sugu

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Yaanika Kampuni Zenye Wadaiwa Sugu
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imeanika majina 57 ya kampuni, shule, vyuo na mashirika ambayo waajiri wake hawawasilishi makato ya wanufaika wa mikopo kwa wakati.

Uanikaji wa majina hayo kupitia tovuti ya HESLB umekuja siku mbili baada ya kutangaza kufanya hivyo Jumatano iliyopita.

Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo, Phidelis Joseph alisema kabla ya kuanza kuwasaka wanufaika 119,497 ambao hawajarejesha mikopo yao, wataanika majina yao hadharani.

Miongoni mwa kampuni zilizotajwa ni pamoja na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la NSSF, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Puma Energy Limited, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Zipo pia shule za sekondari ambazo waajiri wake hawapeleki fedha kwa wakati licha ya kuwakata wafanyakazi wao.

Akifafanua kuhusu muda wa kuwasilisha fedha za makato ya wanufaika, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema kila mwajiri ana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha makato ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa Bodi ndani ya siku 15 baada ya mwisho wa mwezi.

“Baadhi ya waajiri wamekuwa hawafanyi hivyo na kuilazimisha Bodi ya Mikopo kuanza kuwasaka kwa nguvu.

“Katika msako huu hatutamuacha mtu au mwajiri yeyote anayekiuka sheria iliyoanzisha Bodi,” alisema Badru.

Kaimu Mkurugenzi wa Habariwa HESLB, Omega Ngole alisema kwamba idadi ya wanaokwenda kulipa madeni yao imeongezeka.

Alisema kwa kawaida ofisi zao za kanda zilizopo Arusha, Dodoma, Mwanza na Zanzibar hupokea wadaiwa wapya kati ya 15 hadi 25 kwa siku, lakini kuanzia jana wamepokea zaidi ya 50.

Akizungumzia zaidi kuhusu ofisi za makao makuu, Ngole alisema: “Tunapokea wadaiwa wapya wanaotaka kulipa zaidi ya 300 ambayo haikuwa kawaida, wapo na viongozi ambao majina yao yapo kwenye orodha ya wadaiwa, wamemaliza leo.”

Alisema kwamba wanawashukuru wote kwa kutimiza wajibu wao kwa kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwasomesha wahitaji wengine.


Baada ya Kuchumbiwa Wolper Aonyesha Pete Yake ya Uchumba Aliyovalishwa

$
0
0
Haatimaye Wolper Aonyesha Pete  Yake ya Uchumba Aliyovalishwa
Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper amethitisha kuvalishwa pete ya uchumba na kijana anayetambulika kwa jina la Engine.

Muigizaji huyo ambaye alikuwa kwenye mahusiano na kijana Brown mwezi mmoja na nusu iliopita, alisafiri na mpenzi wake huyo mpya mpaka mkoani Kimanjaro na kuvalishwa pete ya uchumba mbele ya wazazi wake.

“Mjivuni nachagua yakunifaa kwa hii kidole🔒#engagement #abouttobemrssomebody
#can’twaitformyweddingday,” aliandika Jack Instagram.

Naye mume wake huyo mtarajiwa ambaye anatambulika kwa jina la Engine, amesema ni kweli amemvalisha pete mrembo huyo wa Bongo Movie na kinachosubiriwa kwa sasa ni ndoa kwa kuwa tayari ameshalipa na mahari.

Pata Tiba ya Tatizo la Nguvu Za Kiume........Inasaidia Kukufanya Urudie Mara 5 na Kuchelewa Kwa Dakika 20

$
0
0
TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO LINATIBIKA.Baada ya utafiti wa mda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka DR Magise imekuletea tiba ya matatizo hayo kwa kutumia dawa za:


FULL POWER:Ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume,dawa hii inamchanganyiko wakutosha wenyekuzalisha vichocheo vingi vya Hemone za Gestrogen vikiwemo vitamin B6&B1,vitamini E,pamoja na madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi,na kuchelewa kufika kileleni zaidi dakka 20-30.


NYAMVA:Inarutubisha maumbile ya uume yani kurefusha na kunenepesha nchi 4-7 upana cm3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukiitumia maumbile yako yatabaki kuwa hivyo siku zote,Pia tunatibu Presha,kisukari siku7,ngiri,chango la tumbo tumbo kujaa gesi,kutopata choo vizuri

 TUPO TZ DAR ES SALAAM   MBAGALA RANGI TATU.HUDUMA HII UTALETEWA POPOTE ULIPO .WASILIANA NAMI 0783741788,0715741788 -DR MAGISE

BENKI KUFUNGWA: “Mamilioni yote yapo Benki, ndani nina elfu 20 tu sijui nitafanyaje na ada za watoto”

$
0
0
Baada ya Benki Kuu ya Tanzania kuzifunguia benki tano January 4, 2018 ikiwemo Meru Community Bank baadhi ya wateja wa benki hiyo wameiomba serikali kuwasaidia kupatikana kwa fedha walizokuwa wameweka katika benki hiyo ili ziweze kuwasaidia katika matumizi mbalimbali.

Mmoja wa wateja aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Munish amesema yeye aliwekeza pesa zake kwenye benki hiyo kwa sababu  aliamini ni Benki ya wananchi na ni sehemu salama kuweka pesa zake na hivyo taarifa ya kugungiwa ameipokea kwa masikitiko makubwa.

“Nimeweka pesa nyingi, ada za watoto zote nilikuwa nimeweka huku, hata Jumatatu sina ada ya kuwapeleka wanangu shule, nina watoto wa chuo na wa shule za English medium, sina hata senti tano na ndani nia shilingi Elfu ishirini tu.” – Elizabeth Munish

Lissu Akiri Kuwa na Deni Kubwa Nchini Kenya

$
0
0
Lissu Akiri Kuwa na Deni Kubwa Nchi ya Kenya
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amekiri kuwa ana deni kubwa na nchi ya Kenya kutokana na kuokoa maisha yake na kumpatia ulinzi kwa kipindi cha miezi minne aliyokuwepo nchini hapo akitibiwa.


Lissu ameyasema hayo asubuhi na mapema wakati akijiandaa kuondoka kuelekea nchini Ubelgiji anakoenda kufanya matibabu zaidi kwa ajili ya viungo vya mwili ili kumuwezesha kutembea kabisa.

Akiizungumzia Kenya, Lissu amesema kwamba hataweza kusahau fadhila za nchi ya Kenya pamoja na watu wake kwani, serikali hiyo ilihakikisha inampatia ulinzi wa masaa 24 alipokuwa hospitali hapo.

"Nina deni kubwa sana na nchi ya Kenya. Wakenya wameokoa maisha yangu na kunilinda kwa wakati wote. Ninashukrani kubwa kwa serikali ya Kenya na wananchi kwani madaktari wao na wauguzi wao wamehakikisha nakuwa hivi,".amesema Lissu.

Akizungumzia kuhusu Tanzania, Lissu amewashukuru madaktari wa Dodoma kwa kuokoa maisha yake baada ya shambulio na kipekee amemshukuru Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya kwa kuwa Kiongozi mkuu wa jopo la madaktari waliookoa maisha yake na watanzania kwa maombi na michango yao.

Lissu alifikishwa Hospital ya Nairobi Usiku wa Setemba 7 baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana kwenye viunga vya nyumbani kwake mkoani Dodoma majira ya saa saba mchana alipokuwa ametoka bungeni.

Diamond Kufungua Kiituo cha Redio na Television Wasafi FM, Wasafi TV.

$
0
0
Diamond Kufungua Kiituo cha Redio na Television Wasafi FM, Wasafi TV.
Rais wa WCB, Diamond Platnumz ametangaza habari njema kwa watanzania hasa hasa kwa wadau wa tasnia ya habari kwamba anatarajia kufungua Wasafi FM na Wasafi TV.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Waka’ akiwa amemshirikisha msanii wa muziki wa kufoka kutoka Marekani, Rick Ross, alitoa taarifa ya ujio wa redio hiyo na TV kupitia twitter yake Disemba 30 mwaka 2017 lakini muda mfupi baadae aliifuta taarifa hiyo.


Weekend iliyopita muimbaji huyo akiwa nchini Kenya katika show za kuufungua mwaka 2018 alifanya mahojiano na kituo cha runinga cha KTN na kueleza mpango wake huo wa kufungua Wasafi FM na Wasafi TV.

Hiyo ni habari njema kwa wadau wa habari kwani kuanzisha kwa kituo hicho bila shaka kitazalisha ajira za kutosha kwa watanzania.

Waziri Mkuu Abaini Madudu Kwenye Vyama Vikuu vya Ushirika Aagiza Vyama Viwili Vichunguzwe

$
0
0
Waziri Mkuu  Abaini Madudu Kwenye Vyama Vikuu vya Ushirika
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amebaini madudu kwenye vyama vikuu vya Ushirika vya Mbinga (MBICU na MBIFACU) na kuagiza uchunguzi ufanyike kuanzia leo.

Ametoa agizo hilo jana jioni Ijumaa, wakati akiwa anahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbinga, kwenye viwanja vya CCM, mjini Mbinga.

“Nikiondoka hapa jukwaani, Viongozi wote wa zamani na wa sasa waripoti kwa Mkuu wa Wilaya, na OCD hakikisha ofisi za chama hazifunguliwi hadi kesho asubui (leo)’ kazi itakapoanza, ili wasije kubadilisha nyaraka kwenye ofisi yao. Timu yangu ya uchunguzi ikohapa Mbinga, kesho waende wote kwenye ofisi hizoo,”alisema huku akishangiliwa na wananchi.

Alisema timu timu hiyo ya uchunguzi itakiangalia chama hicho na kukifumua chote, na wote wakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kinidhamu. Tunataka MBICU na madeni yenu yaliyoko kwa Msajili wa Hazina yajulikane, tunataka turudishe hoteli yetu, mashamba yetu na majengo yetu, alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kutembelea wilaya ya Nyasa ambako atazungumza na watumisHIi na madiwani, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Ally Hapi: Waiochukua Hela za Wananchi Ili Wasibomolewe Nyumba Natoa Masaa 72 Wazirudishe

$
0
0
Ally Hapi: Waiochukua Hela za Wananchi Ili Wasibomolewe Nyumba Natoa Masaa 72 Wazirudishe
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi leo January 6, 2018 amefanya ziara Kigogo na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo na kutoa maagizo kuwa wale wote wanaowadanganya wananchi kwa kuwaambia watoe fedha ili wasibomolewe nyumba zao wazirudishe ndani ya masaa 72 kwani huo ni ulaghai, tulishasitisha zoezi la bomobomoa.

“ Nimetaarifiwa na wananchi wa kigogo kuwa kuna watu wanapitapita kule wanakusanya hela kwa wananchi na baadhi ya watu ni viongozi, sasa nataka niwaambie sina mchezo na kazi yangu, kuna watu wananichezea,”– Ally Hapi

“Wale wote waliokusanya fedha za wananchi na wanaowatisha wananchi kwamba watakuja kubomolewa, wanatumia hicho kigezo kama njia ya kujikusanyia pesa  na baadhi yao ni wenyeviti wa serikali za mitaa, ninawapa masaa 72 wawe wamerudisha fedha zote walizokusanya“– Ally Hapi


Huu Hapa Ushauri wa Mwijage kwa Wanaotaka Kujenga Viwanda

$
0
0
Huu Hapa Ushauri wa Mwijage kwa Wanaotaka Kujenga Viwanda
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amewataka Watanzania  kabla ya kwenda kujenga viwanda wawafuate Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ili wapatiwe utaalamu wa mahitaji ya soko kwa sasa.

“Linapokuja swala la viwanda, usinisikilize mimi utaumia, ukitaka kujenga kiwanda kawaone SIDO, wala hupaswi kujua unahitaji kiwanda cha aina gani watakuelezea huko huko.” – Waziri Charles Mwijage

Maneno ya Kiingunge kwa Rais Magufuli "CCM ni Chama Changu na Nimekiunda Mimi"

$
0
0
Maneno ya Kiingunge kwa Rais Magufuli "CCM ni Chama Changu na Nimekiunda Miimi"
January 6, 2018 President Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa, akiwa katika kitanda cha hospitali amemwambia President JPM kuwa CCM ni chama chake na amekiunda yeye.

“CCM ni chama changu nimetoka tu, tumeachana lakini nimefanya kazi zote, nimekiunda mimi, hakiwezi kuwa kinyume changu,”– Mzee Kingunge

Waasi Washambulia Hospitali

$
0
0
Waasi Washambulia Hospitali
Wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Syria wanasema kwa siku kumi mfululizo, waasi wamekuwa wakishambulia hospitali katika maeneo wanayoyamiliki.

Mshauri wa masuala ya afya wa umoja wa mataifa aliyepo nchini humo Hamish de Bretton-Gordon mashambulizi hayo yanarudisha nyuma juhudi zao za kuwapatia watu huduma za afya.

Anasema hospital zimeharibiwa vibaya Mashariki mwa mji wa Ghouta na Damascus,na jimbo la Kaskazini la Idlib.

Bretton-Gordon amesema zaidi ya watoto 150 wanahitaji kuondolewa katika maeneo hayo ili kupata huduma kamili za afya.

Hali ya usalama nchini Syria imekua ya kuzorota kila kukicha kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya serikali na washirika wake dhidi ya waasi wanaopinga serikali ya Rais Bashar al-Assad

Maskini Kingunge Apokea Kwa Masikitiko Taarifa za Kifo cha Mkewe

$
0
0

Maskini Kingunge Apokea Kwa Masikitiko Taarifa za Msiba wa Mkewe
Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru leo Jumamosi amepewa taarifa za kifo cha mke wake Pares Mwiru ambazo imeelezwa kuwa amezipokea kwa mshtuko mkubwa.

Kingunge aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Kijitonyama, alifanyiwa upasuaji Januari 4 mwaka huu.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 6, mtoto wa mwanasiasa huyo Kinje Mwiru amesema wamempa taarifa baba yao saa tano asubuhi leo.

“Tumemfahamisha nusu saa iliyopita, ilikuwa ni vigumu sana wakati tunamfikishia taarifa hizo na amezipokea kwa ugumu sana. Haikuwa rahisi kwa yeye kupokea taarifa wakati tunamweleza,” amesema.

Kinje amesema kwa sasa wamemuacha apumzike ili aweze kuwapatia mwongozo nini kifanyike baada ya kifo cha mke wake.

Pares alifariki Januari 4 saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa, tangu alipofikishwa Muhimbili Oktoba 3, mwaka jana.

Akizungumza na Mwananchi leo, Ofisa Uhusiano wa MNH John Stephen amesema kwa sasa afya yake imeimarika.

Soma: Rais Magufuli afika Muhimbili kumwona Kingunge

 "Anaendelea vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema.


Mtulia Ateuliwa na CCM Kugombe Ubunge Kinondoni, Godwin Mollel Jimbo la Siha

$
0
0
CCM  Yawateua Wabunge Kutoka Upinzani Kugombe Ubunge Kilimanjaro, Siha
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewarudisha waliokuwa wabunge wa upinzani kugombea majimbo ya Siha na Kinondoni baada ya wabunge hao kuijiunga na chama hicho.



Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole imesema kuwa baada ya tafakuri na tathimini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Dk Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro na Maulid Mtulia kusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.



Imesema kuwa wagombea wa ubunge wanaelekezwa kufika katika ofisi za CCM katika mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM wa mikoa hiyo siku ya Jumanne, Januari 9 bila kukosa.

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0

Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.


NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.


MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 


MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.


NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,


Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 


DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

“Usiwe Mstaafu ukaenda kujenga kiwanda utakufa”- Waziri Mwijage

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amewataka Watanzania  kabla ya kwenda kujenga viwanda wawafuate Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) ili wapatiwe utaalamu wa mahitaji ya soko kwa sasa.

“Linapokuja swala la viwanda, usinisikilize mimi utaumia, ukitaka kujenga kiwanda kawaone SIDO, wala hupaswi kujua unahitaji kiwanda cha aina gani watakuelezea huko huko.” – Waziri Charles Mwijage VIDEO:

Baba Mzazi wa Mess Afunguka Kuhusu Mess Kuondoka Barcelona

$
0
0
Baba Mzazi wa Mess Afunguka Kuhusu Mess Kuondoka Barcelona
Baba mzazi wa nyota wa Barcelona Lionel Messi, Jorge Messi amesema, taarifa zinazosamba kuwa endapo jimbo la Catalonia litajitenga kutoka Hispania nyota huyo ataachana na klabu hiyo kuwa ni uongo.


Jorge ambaye pia ni wakala wa mfungaji huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano na 'Radio Red' ya Argentina na kufafanua kuwa hakuna kipengele kinachotaka Messi aondoke Barcelona endapo Catalonia itajitenga na Hispania

''Taarifa hizo ni za uongo, mkataba mpya wa Messi hauna kipengele hicho, ila tu kuna maelewano yanayotaka pande zote mbili kuzingatia kuwa Barcelona ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa kwahiyo inatakiwa kucheza ligi kubwa haijalishi ni ligi gani ila iwe moja ya ligi kubwa'', amesema Jorge.

Messi ambaye pia ni mfungaji bora wa muda wote wa Argentina mwezi Novemba mwaka jana alisaini mkataba mpya wa kusalia Camp Nou mpaka mwaka 2021 huku gharama ya kuuzwa ikiwekwa kuwa ni € 700 milioni ambazo ni takribani shilingi  bilioni 2.



Msimu huu Messi ana mabao 15 kwenye LaLiga, huku Barcelona ikiwa pointi 45, tisa juu ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili ikiwa 36.

Golikipa wa Simba Aishi Maanula Auanza Mwaka Vizurii Afaniikiwa Kufunga Ndoa Leo

$
0
0
Golikipa wa Simba Auanza Mwaka Vizurii AAfaniikiwa Kufunga Ndoa Leo
Idadi ya wachezaji soka makapera inazidi kupungua. Golikipa wa klabu ya soka ya Simba, Aishi Salum Manula amejiondoa mwenyewe katika orodha hiyo.



Mchezaji huyo amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu ajulikanaye kama Aisha.

Manula hakuweza kusafiri na kikosi cha Simba katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea huko visiwani Zanzibar kwa ajili ya kukamilisha shughuli za ndoa hiyo.

Waziri Majaliiwa Amaliza Mgogoro wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri

$
0
0

Waziri Majaliiwa Amaliza Mgogoro wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambao umedumu kwa miaka miwili.



Ametoa uamuzi huo jana jioni, wakati akizungumza na watumishina madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Mbinga kwenye ukumbi wa jumba la Maendeleo mjini Mbinga.

“Ninazo taarifa kuwa kuwa mnagombea mahali pa kujenga makao makuu ya Halmashauri hali mnataka kujenga kwenye chanzo cha maji. Hiyo haikubaliki. Kwenye vyanzo vya maji hakujengwi miji tena Afisa Maliasili nenda ukapande miti zaidi ili tutunze chanzo chetu,”alisema Waziri Mkuu.

Wataalamu wa Halmashauri hiyo walikuwa wakivutana na Madiwani juu ya makao makuu hayo kujengwa ,Ndengu ambako ni karibu na chanzo cha maji huku wengine wakitaka yajengwe Kigonsera kwa madai kuwa kote ni karibu na wananchi.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iligawanywa Julai 215 kwa kupata Halmashauri ya Mjiwa Mbinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na ilianza kazi Julai 2016.

Waziri Mkuu alisema Halmashauri hiyo si ya kwanza kuwa na migogoro kwa hiyo nimeamua mjenge hapa hapa mjini Mbinga. Mkijenga huko wanakotaka hawa mtagombana na mkijenga kule nako pia mtagombana lakini ugomvi wenu ni kwaajili ya nani? Kama sikuwaumiza wananchi mnaowaongoza ni nini?,alihoji Waziri Mkuu.

“Miaka yote mmekuwa mkipata huduma kutokea hapa hapa kabla Halmashauri hizi hazijatenganishwa. Tumeleta fedha mara mbili mara ya kwanza sh. milioni 500 na ya pili sh. milioni 400 lakini hazijatumika kwasababu ya migogoro yenu isiyo na tija. Kwa hiyo makau makuu yatajengwa hapa hapa mjini,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Polisi Wamshikilia Mtu Mmoja Anayeuza Viungo vya Binaadam

$
0
0
Polisi Wamshikilia Mtu Mmoja Anayeuza Viungo vya Binaadam
Polisi nchini Cyprus wanasema wanamshikilia raia mmoja wa Israel anayetuhumiwa kufanya biashara ya viungo vya binadam.

Moshe Harel amehusishwa kufanya biashara ya figo kwa matariji wa Israel takriban miaka kumi sasa.

Amehusishwa kuchukua figo za raia wa Kosovo pamoja na Uturuki na nchi nyingine kadhaa ambao mpaka sasa hajawalipa chochote.

Msemaji wa polisi nchini Cyprus amesema mtu huyo alikamatwa uwanja wa ndege wa Larnaca mwezi Desemba.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumanne kujibu mashtaka yanayomkabili.

Anahitajika kwa makosa kama hayo nchini Kosovo

Kamati Maalumu ya Kuhakiki Mali Yaanza Kuwachunguza Vigogo CCM

$
0
0
 Kamati Maalumu ya Kuhakiki Mali Yaanza Kuwachunguza Vigogo CCM
 Kamati maalumu ya kuhakiki mali za Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoundwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais John Magufuli, imetua Arusha na kuwahoji viongozi kadhaa, wafanyabiashara na wanachama.

Kamati hiyo inayoongozwa na Dk Bashiru Ally licha ya kuhoji watu hao, pia ilitembelea baadhi ya mali za CCM mkoani Arusha.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Wakili maarufu Arbert Msando akizungumza na mwananchi jana alisema wanaendelea vizuri na kazi za kuhakiki mali za chama na uchunguzi zaidi.

“Tumewahoji baadhi ya viongozi na wanaCCM, tunaendelea vizuri, ila siwezi kusema tumebaini nini hadi sasa kwa kuwa taarifa rasmi itatolewa,” alisema Msando.

Alifafanua kuwa baada ya kukamilisha kazi hiyo, mkoani Arusha kamati hiyo, itaelekea mkoani Mwanza.

Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Elias Mpanda alithibitisha ujio wa kamati hiyo, lakini hakuwa tayari kuelezea kazi ambazo zimefanyika.

“Muda huu tupo na kamati ya kuhakiki mali za chama hivyo, siwezi kusema lolote kuhusiana na masuala ya kampeni,” alisema alipotakiwa kuelezea kampeni za chama hicho Jimbo la Longido.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Lengai ole Sabaya wiki iliyopita licha ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuunda kamati hiyo, aliomba ifike mkoani humo kwa kuwa kuna mali za chama alizodai zinatumika kwa masilahi ya wachache.

Sabaya ambaye ni diwani wa Sambasha, alisema CCM mkoani Arusha ina mali nyingi, lakini viongozi waliopita wamekuwa wakinufaika na mali hizo, kupitia mikataba mibovu na kujimilikisha baadhi ya mali.

Hata hivyo, jana alisema amefarijika kuona kamati hiyo, imetua Arusha kuanza kazi ya uhakiki na akaeleza ana imani itafanya kazi kwa uadilifu.

Hivi karibuni Rais Magufuli alikutana na kamati hiyo baada ya kuiteua na kuitaka kuhakiki mali za chama na kuhoji mtu yeyote wakiwamo viongozi na wafanyabiashara ili kuhakikisha mali za CCM zinanufaisha Wanaccm wote.

Rais Magufuli pia alitaka kamati hiyo, kupewa ushirikiano ili kuhakikisha inafanyakazi kwa ufanisi.

Kwa miaka kadhaa kumekuwapo na malalamiko miongoni mwa wanachama kuhusu kutumika vibaya baadhi ya mali za chama hicho, ikiwamo maduka, viwanja, ofisi, magari ambazo zinamilikiwa na watu binafsi.



Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images