Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Ndugai Ampongeza Rais Magufuli kwa Kuweza Kusimamia Maoni ya Bunge na Wabunge

$
0
0
Ndugai Ampongeza Rais  Magufuli kwa Kuweza KusimamiaMaoni ya Bunge na Wabunge
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amempa pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kusikiliza maoni ya Bunge na wabunge kwa kutekeleza moja ya maombi yao kuigawa Wizara ya Nishati na Madini.


Ndugai ametoa pongezi hizo leo Januari 8, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Mashaka Biteko na kusema kwa miaka mingi walikuwa wakitaka Wizara hizo kugawanywa lakini ilikuwa inashindikana ila katika awamu ya tano Rais Magufuli ndiyo ameweza kufanya hivyo.

"Sisi Bunge tulikuwa tukishauri toka miaka ya nyuma kwa Serikali kwamba Wizara iliyokuwa inaitwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ni nzito mno, ilikuwa imejaza mambo mengi sana kwa wakati mmoja ushauri wetu ulikuwa ni vizuri kuzitenganisha na kuzisimika kila moja kivyake. Jambo hili Mhe. Rais umelitekeleza kabisaa kwenye awamu ya tano umeunda wizara mbili na hata tendo la leo linadhirisha kabisa jinsi ambavyo unazidi kuimarisha sekta ya Nishati na Madini kwa hili tunakushukuru sana kwani linaonesha dhamira yako ilivyo" alisema Ndugai

Mbali na hilo Ndugai amesema kuwa katika miaka ya nyuma katika sekta ya madini na nishati kama nchi tumeliwa sana hivyo anaamini kuwa katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli na wateule wake jambo hilo halitaweza kuendelea tena.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza mnamo Januari 30, 2018 Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.


Matokeo ya Darasa la Nne, Kidato cha pili Yatangazwa ..Wanafunzi 51,807 Washinwa Kuendelea Kidto cha Tatu

$
0
0
Matokeo ya Darasa la Nne, Kidato cha pili Yatangazwa ..Wanafunzi 51,807 Washinwa Kuendelea Kidto cha Tatu
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu Januari 8, Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.

Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.

Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Kiwanja Cha Kujenga Nyumba Kinauzwa Eneo la Mapinga Karibu na Bunju B

$
0
0

Kiwanja Chenye Ukubwa wa Mita 20 kwa 20 Kinauzwa Mapinga Bagamoyo Jirani na Bunju B, Kipo Karibu na Barabara ya lami ya kwenda Bagamoyo...Kina Ukubwa wa 20 Kwa 20 ...
Bei Sh Mil 8.5

Wasiliana na Namba hii 0714604974


Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.


NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.


MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA.


MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.


NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,


Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605


DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Rais Magufuli Awajia Juu Mawaziri Wake Awataka Kutenda Kazi Kama Atakavyo

$
0
0
Rais Magufuli Awaajia Juu Mawaziri Wake Awataaka Kutenda Kazzi kama Atakavyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewabadilikia baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano na kuwataka kutenda kazi kama atakavyo yeye kwani wasipofanya hivyo maana yake nafasi hizo haziwafai tena.


Magufuli amesema hayo leo wakati wa sherehe za kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Mashaka Biteko leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kudai kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Anjellah Kairuki pamoja na Naibu wake Stanslaus Nyongo na kuwataka kubadilika mara moja.

"Bado Wizara ya Madini haifanya kazi vizuri sana najua nikizungumza kwa kupamba nitakuwa mnafiki Mhe. Spika utatambua mwezi wa 7 Bunge lilipitisha sheria ya madini kubadilisha ile sheria iliyokuwepo mkapitisha sheria namba 7 ya mwaka 2017 ambayo Bunge na Watanzania wengi tuliamini kwamba kupitia sheria hii mambo mengi ya nchi yangenyooka ikiwa pamoja na kupata mlahaba na kupata faida na madini yetu. Ile sheria ilipofika nilisaini na kuwapa maelekezo watendaji wangu kuandaa 'regulations' lakini mpaka sasa ni miezi saba imepita regulations hazijasainiwa" alisema Rais

Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa kutokana na vitendo hivyo vya wateule wake ni wazi kuwa kuna matatizo makubwa ndani ya Serikali

"Unaweza kujiuliza kuwa tuna matatizo makubwa ndani ya Serikali, kwa sababu kama regulations zile hazijasaini mnategemea nini? Kuanzia mwezi wa saba hawakusaini leo tupo mwezi wa kwanza bado hazijasainiwa, usipokuwa na regulations mtu yoyote atakapo default atapelekwa kwenye mahakama gani? Kwa hiyo sisi Watanzania baadhi ya watendaji wa Serikali hawapo makini ninasema hii kwa uchungu mkubwa baadhi ya niliowateua bado hawajanielewa ninataka nini" alisisitiza Rais

Pia Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kutuma ujumbe kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ambaye sasa yupo likizo "unapokuja kukumbushwa kwamba kuna haya mabaya kwenye eneo lako na wewe upo maana yake ni kwamba hufiti, unatakiwa wewe uyagundue kabla ya watu wengine kuyagundua kwa hiyo Wizara ya Nishati mnachangamoto kubwa bado mengi hayajafanyika. Wizara ya Madini mkajirekebishe mfanye kazi kiukweli mpaka sasa Wizara ya Madini haija ni 'impress' na mumfikishie salamu hizi waziri bado haja ni 'impress' lakini nategemea mtabadilika" alisisitiza Rais

Simba Kibaruani Leo Dhidi ya URA Kombe la Mapinduzi

$
0
0
Simba Kutupa Karata Yake Leo Dhidi ya URA
Kikosi cha klabu ya Simba hii leo kitaingia Uwanjani kutupa karata yake dhidi ya timu ya URA katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar kuwania nafasi ya nusu fainali ya michuano hiyo.



Simba SC ambayo ipo nafasi ya tatu ya kundi A ikiwa na pointi nne, itahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika mchezo wa mwisho klabu hiyo ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wanaramba ramba timu ya Azam FC ambayo imeshatinga hatua hiyo kwa kuwa na jumla ya pointi 9 baada ya kucheza mechi nne huku ikiongoza kundi hilo.

Vita vikali hii leo ni kati ya wakusanya kodi wa Uganda , URA ambayo ipo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya pointi saba dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya tatu wakati timu za Mwenge na Jamhuri zikiwa zimesha toka katika mbio kinyang’anyiro cha Kombe la Mapinduzi.

Kwa matokeo yoyote yale yataifanya Simba SC kuyaaga mashindano hayo ya Mapinduzi Cup kwa mwaka huu na kuwa ni mashindano ya pili kupoteza baada ya yale ya FA.

Waandamana Kupinga Ongezeko la Bei ya Mkate

$
0
0
Waandamana Kupinga Ongezeko la Bei ya Mkate
Sudan imekumbwa na maandamano katika miji mbalimbali kutokana na ongezeko la bei ya mkate.

Habari zinasema gharama zimeongezeka mara mbili na sababu kubwa ni hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya vyakula uamuzi ambao umesababisha bei ya mkate kuwa mara dufu.

Maandamano yaliyofanyika magharibi mwa Darfur yamesababisha mwanafunzi mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kuzuka fujo.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya watu ambao walikuwa wamefunga barabara na kuchoma matairi katika barabara za mji mkuu wa Khartoum.

Lakini naibu waziri wa mambo ya ndani alisema maandamano hayo hayakutokana na ongezeko la bei na akaahidi kuwashughulikia wote waliofanya maandamano yenye fujo. Pia, Serikali imezuia kuuzwa mitaani magazeti yote yaliyokosoa ongezeko la bei.

Vyanzo vya uhakika vimezema uamuzi wa kuongeza bei ya mkate umefikiwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kufufua uchumi yaliyotolewa na IMF.

Mawaziri Walioachwa Kwenye Baraza la Rais Kenyatta Waduwaa

$
0
0
Mawaziri Walioachwa Kwenye Baraza la Rais Kenyatta Waduwaa
Hali ya mshangao imetawala kwa mawaziri wa Kenya ambao hawakutajwa kwenye baraza jipya la mawaziri la Rais Uhuru Kenyatta alilolitangaza Ijumaa iliyopita lililowaacha nje ya ofisi zao mawaziri sita aliokuwa nao kwenye awamu yake ya kwanza.

Baada ya kuapishwa, Rais Kenyatta ameanza kuunda Serikali kwa kutangaza baraza lake akiwateua mawaziri watatu wapya na kuwaacha wengine sita waliokuwapo awali.

Mawaziri wa zamani walioachwa kwenye nafasi zao ni pamoja na Fred Matiang’i (Mambo ya Ndani), Charles Keter (Nishati), Najib Balala (Utalii), Henry Rotich (Fedha), Joe Mucheru (Tehama) na James Macharia (Uchukuzi).

Hata hivyo, hatima ya mawaziri wengine ambao hawakutajwa bado haijajulikana licha ya kwamba wanaendelea kushika ofisi zao mpaka pale Rais Kenyatta atakapotangaza mawaziri wapya au kuwaacha wenyewe.

Baadhi ya mawaziri na wasaidizi wao wamekataa kukubali kwamba wameondolewa kwenye wizara zao wakisisitiza kwamba bado wanashikilia nafasi kwa sababu baraza zima la mawaziri bado halijakamilika.

“Rais hajanifukuza mimi, ametaja tu baadhi ya mawaziri ambao anapenda wabaki kwenye nafasi zao na kuteua wengine wachache. Mpaka mchakato wote utakapokamilika, huwezi ukasema amenifukuza. Naweza kupelekwa kwenye nafasi nyingine unajua,” alisema waziri mmoja ambaye si mmoja kati ya sita waliotajwa na Rais Kenyatta.

Ijumaa iliyopita Rais Kenyatta alitangaza mawaziri wapya watatu na kuwabakiza wengine sita kwenye nafasi zao.

“Napenda kutangaza kwamba ninawaacha watu wafuatao kwenye baraza langu la mawaziri na nitawapangia majukumu yao tena kwa mujibu wa Ibara ya 152(5)(A) ya Katiba na watu hao ni Fred Matiang’i (Mambo ya Ndani), Charles Keter (Nishati), Najib Balala (Utalii), Henry Rotich (Fedha), Joe Mucheru (Tehama) na James Macharia (Uchukuzi),” alisema Rais Kenyatta.

Juzi, kitu ambacho kinaweza kutafsiriwa kama kuwapunguzia msongo wa mawazo mawaziri ambao hawakutajwa, msemaji wa Ikulu ya Kenya, Manoah Esipisu alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akisema mawaziri wote bado wanashikilia nafasi zao mpaka pale mchakato wa kuunda baraza la mawaziri utakapokamilika.

Taarifa hiyo ya Esipisu ilikuwa ikimaanisha kwamba mpaka sasa hakuna waziri ambaye amefukuzwa kazi na Rais Kenyatta.

“Hii ni kufafanua kwamba mawaziri wote ambao bado wako ofisini wataendelea kutambulika kama ilivyoelekezwa kwenye waraka wa mkuu wa utumishi wa umma Desemba mwaka jana, mpaka hapo itakapoamriwa vinginevyo,” alisema Esipisu katika taarifa hiyo.

“Siku zijazo, Rais Kenyatta atahitimisha kazi yake ya kuunda timu ya ofisi kwa kuzingatia weledi, uadilifu na wanaoipenda kazi yao ya kuwahudumia wananchi kwa kufuata katiba.”

Kwa mujibu wa vyanzo viwili vya habari kutoka ndani ya Ikulu ya Kenya vimeliambia gazeti la The Standard kwamba, Rais Kenyatta amekuwa akifanya mambo yake kwa usiri na ulinzi mkubwa.

“Sikiliza, ngoja nikwambie. Serikali haifukuzi watu, inaondoa majina yao kwenye orodha ya wateule wa Rais. Nina uhakika mlishaliona hilo siku zilizopita. Kwa hiyo kama ndugu yake ametaarifiwa rasmi kwamba anataki kwenye baraza, nini kimebakia kwa mawaziri ambao bado wako ofisini?” kilisema chanzo kimoja cha habari.

Hata hivyo, msimamo huo ulitofautiana na chanzo kingine cha habari kutoka serikalini ambacho kilisema baadhi ya mawaziri ambao hawakutajwa Ijumaa akiwamo Eugene Wamalwa, Amina Mohammed, Mwangi Kiunjuri na Dan Kazungu wamefanya vizuri katika ofisi zao na kwamba wanaweza kubaki kwenye baraza la mawaziri.

“Kuna uwezekano baraza la mawaziri likaongezeka. Mawaziri sita waliotajwa na Rais wataendelea na nafasi zao isipokuwa Matiang’I ambaye anakwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Hiyo haimaanishi kwamba wale ambao hawakutajwa na Rais basi wamefukuzwa kazi,” kilisema chanzo hicho.

“Ina maana kwamba watu kama Amina, Eugene, Adan Mohammed, Kiunjuri and Kazungu watarudi lakini si lazima warudi kwenye nafasi wanazozishikilia sasa. Kwa kifupi ni kwamba mawaziri sita tu ndiyo wanajua nafasi zao.”

Rais Kenyatta na makamu wake, William Ruto wameweka usiri mkubwa katika chaguo la wateule kiasi kwamba hata wasaidizi wao wa karibu hawajui kitu.

Inafahamika wazi kwamba maofisa wa ngazi za juu waliokuwapo Ikulu wakati Rais Kenyatta akitangaza mabadiliko hayo hawakujua alikwenda kuzungumzia nini. Walijua atakwenda kuzungumzia mabadiliko kwenye sekta ya elimu.

Rais ameachana pia na utaratibu wa zamani ambao teuzi zake zilizingatia ukarimu, ukanda na urafiki. Si rahisi kwa sasa kutabiri nafasi chache za uteuzi zilizobaki.

Sambamba na hilo, Rais alifanya uteuzi wa kushtukiza kwa kumteua mkuu wa Mkoa wa Rift Valley, Wanyama Musiambo kuwa naibu mkuu wa utumishi wa umma akimaliza tetesi za watu waliotajwa kuchukua nafasi hiyo ambao ni Makati Wakuu Joseph Njoroge (Nishati), Karanja Kibicho (Mambo ya Ndani) na Monica Juma (Mambo ya Nje).

Watu wengi walitarajia Amina, Kiunjuri, Wamalwa na Kazungu kuachwa kwenye nafasi zao kwa sababu ni wanasiasa hodari na wachapakazi na walikuwa na mchango mkubwa kwa Kenyatta kuchaguliwa katika muhula wake wa pili.   




Hatimaye Mashabikii na Wapenzi wa Lulu Kuanza Kumuona

$
0
0
Hatimaye Mashabikii na Wapenzi wa Lulu Kuanza Kumuona
Zikiwa zimepita siku 54 tangu muigizaji wa filamu bongo,  Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela,  sasa mashabiki wake wataanza tena kumuona kupitia tamthiliya ya Sarafu inayotarajiwa kuanza kurushwa kuanzia Januari 10 siku ya Jumatano.

Sarafu ni moja ya tamthiliya zitakazoonyeshwa katika king’amuzi cha DSTV kupitia chanel yao ya Maisha Magic Bongo ambapo itakuwa inarushwa siku ya Jumatano na Alhamisi.

Katika tamthiliya hiyo ambayo msimu wake wa kwanza utaenda mpaka Machi mwaka huu, imesheheni waigizaji mbalimbali maarufu, ambapo mbali na Lulu wapo Funga Funga(Jengua), Mzee Chilo, Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Idris Sultan, Yusuph Mlela na mastaa wengineo.

Ndani ya tamthiliya hiyo Lulu anaigiza kama mtoto wa familia tajiri ya Mhandisi Sanga akiwa anatumia jina la Jack huku mama yake akiwa ni muigizaji wa siku nyingi Suzan Lewis 'Natasha'.

Uzinduzi wa tamthiliya hiyo uliofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, uliendana sambamba na uzinduzi  wa tamthiliya nyingine ya Sarafu ambapo baadhi ya wadau waliweza kushuhudia moja ya kipande alichoigiza Lulu, ambacho alionekana kukitendea haki.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliokiona kipande hicho walikuwa na maoni yao kuhusu namna walivyojisikia  baada ya kumuona msanii huyo akiwemo mrembo Wema Sepetu, ambaye alisema kipande hicho kimemuhuzunisha kwani alitamani naye angejumuika nao siku hiyo lakini kutokana na matatizo aliyoyapata imekuwa ngumu.

Kwa upande wa Natasha, amesema yeye sehemu hiyo ilipofika alitamani hata kutoka nje ya ukumbi, kwa kuwa yeye kama mama inamuumua kwa mtihani anaopitia Lulu kwa sasa ukilinganisha na umri wake mdogo aliokuwa nao.

Novemba 13, mwaka jana, Mahakama Kuu ilimhukumu kwenda jela miaka miwili Lulu kutokana na kukabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa  na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira.
Chanzo: Mwananchi

Gigy Money Kumbe Mjamzito!... Siri Yafichuka Baada ya Kutinga Basata Akiwa na Kibendi

$
0
0
Gigy Money Kumbe Mjamzito!... Siri Yafichuka Baada ya Kutinga Basata Akiwa na Kibendi
Baada ya kauli ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza kumtaka Gigy Money kufika Ofisini kwake  mwenyewe kabla ya Serikali haijamtafuta , Leo January 8 2018 nimezinasa Picha 10 za Gigy Money akiingia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) aliwasili na mpenzi wake Mo J, Good News ni kuwa Msanii huyo ni mjamzito

Sugu Afunguka Kuhusu Kupotelewa na Instruments za Nyimbo Zake

$
0
0
Sugu Afunguka Kuhusu Kupotelewa na Instruments za Nyimbo Zake
Kwenye taarifa za mitandaoni ambazo zimepewa nafasi kubwa ni pamoja na hii ya Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kutoa taarifa kwa yoyote ambaye anaweza kufanikisha kupata kwa instruments za nyimbo zake zote kwani anashindwa kufanya shows kwa hivi sasa.

Post yake ameandika>> ‘Taarifa: Nimepoteza beats (instrumentals) za nyimbo zangu zote, kitu kinachochangia nishindwe kufanya shows hivi sasa. Kama kuna yeyote anazo popote duniani naomba tuwasiliane kwa email yangu deiwaka14@gmail.com … Asanteni sana na nitashukuru sana kwani mtanisaidia kurudi jukwaani kitu ambacho nakimiss sana’. -Sugu.

Juliana Shonza: ROMA Aliitwa Basata Tumempa Miezi 6 Kurekebishe Wimbo Wake 'Kiba-100'

$
0
0
Juliana Shonza: ROMA Aliitwa Basata Tumempa Miezi 6 Kurekebishe Wimbo Wake 'Kiba-100'
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza ameongea na waandishi wa Habari baada ya kutangaza kumfungia Msanii wa Bongofleva Pretty Kind kutojihusisha na masuala ya sanaa kwa miezi sita.

Akiongea na waandishi wa habari Shonza amegusia pia suala la msanii ROMA ambapo amesema BASATA walimuita na kumuagiza akafanye editing katika wimbo wake wa KIBAMIA.

“Tumemuita ROMA miezi 2 iliyopita tumempa miezi 6 aurekebishe wimbo wake KIBAMIA na alikiri kweli ameimba vitu ambayo ni matusi, sisi hatuwezi mfuatilia kama amefanya editing au hajafanya, asipofanyia editing hizi sheria zitamhusu,”– Juliana Shonza

TRA Ykusanya Trilioni 7.87 kwa Nusu ya Mwaka wa Fedha 2017/18

$
0
0
TRA Ykusanya  Trilioni 7.87 kwa Nusu ya Mwaka wa Fedha 2017/18
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo January 8, 2018 imeeleza kuwa kwa mwezi July hadi December kwenye Mwaka wa Fedha 2017/2018 imekusanya jumla ya Tsh Trilioni 7.87 ikilinganishwa na Tsh Trilioni 7.27 ambayo ilikusanywa wakati wa kipindi hicho hicho kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ikiwa ni ongezeko la 8.46%.

Ripoti ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo imeeleza  kuwa kwa mwezi December 2017 pekee, TRA imekusanya Tsh Trilioni 1.66 ikilinganishwa na makusanyo ya December 2016 ya Trilioni 1.41 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 17.65.

Wanapenda Kuona Mauno Yangu Kama Nini- Snura

$
0
0
Wanapenda Kuona Mauno Yangu Kama Nini- Snura
Mwanamuziki Snura Mushi ' SnuSexy' yeye amekiri kwamba tayari alikwisha jipanga kukabiliana na mabadiliko ya serikali haswa katika kuzingatia sheria za mavazi pamoja na maneno kwenye nyimbo zake baada ya kuletewa shida kwenye wimbo wake wa Majanga.


Akizungumza na www.eatv.tv Snura amesema kwamba ameamua kubadilika na jinsi sheria inavyotaka ndiyo maana kuanzia video zake mpaka mavazi ya kufanyia show yamebadilika na wakati mwingine huwa anafanya uhakiki wa maneno yake kwa kuwauliza wahusika ili asipate matatizo.

Snura amesema kwamba wasanii wote wanatakiwa kujipanga kwa mabadiliko hayo ya sheria na kuwasisitiza kwamba sheria hizo hazijanza leo wala jana bali zilikuwepo tangu zamani na wahusika walikuwa wakizifungia macho ila sasa wameamua kuziangalia

"Mimi nilijua hivi vitu vitatokea baada ya kupata shida kwenye chura, maana nilipofika kule kila kipengele nilichokuwa naoneshwa kilionesha wazi nilikosea. Hivyo niwaombe wasanii wenzangu waweze kujipanga kwa hili na tuweze kufuata sheria kama jinsi ambavyo zinataka". Snura

Akiongeza Snura amesema kwama "Mashabiki pia inabidi wakubali mabadiko na matokeo ya kumuona Snura na nguo ndefu kwenye video ikiwa ni pamoja na kutoona viuno vikikatwa  maana na wao wanapenda kuona miuno kwenye video kama nini. Mashabiki waking'ang'ania kutuona kama zamani wataua muziki wetu"

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na Nasi kwa Namba;0783140065  

Malaria yamtesa Tambwe Arudishwa Dar

$
0
0
Malaria  yamtesa Tambwe Arudishwa Dar
Wakati klabu ya Yanga leo ikitarajia kuingia dimbani kucheza na Singida United kwenye michuano ya Mapinduzi, imemrejesha Dar es salaam mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwasababu ya kuugua.


Mshambuliaji huyo raia wa Burundi mchana huu amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam mchana huu kwaajili ya matibabu zaidi kufuatia kusumbuliwa na homa.

Daktari wa timu hiyo Edward Bavu amesema kuwa Tambwe amekuwa akisumbuliwa na Malaria kwa takribani siku nne. "Ana malaria, kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar es salaam ili apate matibabu zaidi'', amesema Dr. Bavu.

Mrundi huyo amekuwa katika msimu mgumu, akianza kukaa nje tangu Agosti 2017, kutokana na maumivu ya goti kabla ya kurejea mwezi Desemba, lakini mapema leo ameoondolewa tena kambini kwa sababu ya Malaria.

Kuugua kwa Tambwe kunazidi kuipunguzia nguvu safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ambayo pia inawakosa nyota wake Mzimbabwe Donald Ngoma na Mzambia, Obrey Chirwa.

Niyonzima Arejesha Matumaini Simba

$
0
0
Niyonzima Arejesha Matumaini Simba
WAKATI wenzake wakiwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi huko visiwani Zanzibar, kiungo mchezeshaji wa Simba, Mnyar­wanda, Haruna Niyonzima yeye yupo jijini Dar es Salaam akiendelea kujifua ufukweni.

Mnyarwanda huyo alibaki Dar ku­tokana na majeraha ya enka anayoen­delea kuyauguza yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili.

Kiungo huyo, alipata majeraha hayo akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo wakati kikosi hicho kikiwa na Mcam­eroon, Joseph Omog aliyesitishiwa mkataba wake hivi karibuni kabla ya msaidizi wake Mrundi, Masoud Djuma kukabidhiwa.

Akizungumza na Championi Ju­matatu, Niyonzima alisema ameanza programu hiyo ya kukimbia ufukweni kwa ajili ya kuiponyesha enka hiyo ili ipone kabisa.

Niyonzima alisema, wakati akien­delea na matibabu mengine atafanya mazoezi ya ufukweni kwani mchanga ni sehemu ya tiba kwa ajili ya jeraha hilo la enka linalomsumbua.

Aliongeza kuwa, hataki kuona akiendelea kusumbuka na jeraha hilo ambalo mara kwa mara linamtokea ili atakaporejea uwanjani lisijirudie.

“Mimi nipo Dar na sipo na timu Zan­zibar, kama unavyofahamu bado enka inanisumbua na hivi sasa nipo nafanya mazoezi ya kukimbia ufukweni huku nikiendelea kupata matibabu mengine hospitali.

“Na mazoezi haya ya ufukweni nayo ni sehemu ya tiba kwangu, kwani mchanga nao ni tiba kwa jeraha hili la enka inayonisumbua kwa muda mrefu,” alisema Niyonzima aliyetua kuichezea Simba katika msimu huu.

Serikali Yafunguka Kuhusu Bombardier, Meli ya Tanzania Iliyokamatwa na Dawa za Kulevya

$
0
0
Serikali yatoa neno kuhusu Bombardier na Meli ya Tanzania iliyokamatwa na dawa za kulevya

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa neno kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2018 kuhusu ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q400 iliyozuliwa nchini Canada na Meli ya iliyosajiliwa kwa namba za Tanzania iliyokamatwa huko Jamhuri ya Domica na Shehena ya dawa za kulevya.


Kuhusu Bombardier Serikali kupitia kwa Msemaji wake Mkuu, Dkt. Abbas Hassan amesema bado ratiba ipo vile vile kuwa ndege hiyo ya Bombardier na ile kubwa ya Dreamliner zote zitafika nchini kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

“Ishu ya ndege tutaizungumza itakapofika wakati wake lakini mara ya mwisho nilisema ndege zote za serikali ambazo tumenunua ratiba yake ni kufikia mwezi Juni- Julai mwaka huu ndege zote nne ikiwemo ile ndege ya ndoto yetu ya Boeing Dreamliner zitakuwa zimefika nchini.“amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.


Kwa upande mwingine Serikali imekiri kupokea taarifa za Meli yenye usajili wa Tanzania kukamatwa kwenye visiwa vya Jamhuri ya Dominika ikiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine.

“Suala la meli iliyokamatwa Dominika hili nalifahamu, nimelisikia kwa hiyo wenzetu wa wizara ya mambo ya nje bado wanafuatilia kujua usahihi maanake imeripotiwa hivyo kwa hiyo wizara ya nje tumeshazungumza nao na wanalifanyia kazi kwahiyo kama kutakuwa na taarifa zitatolewa.“amesema Dkt. Hassan Abbasi.

Mnamo Desemba 31, 2017 Jeshi la Maji nchini Uholanzi liliikamata Meli yenye usajili wa Tanzania ikiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine tani 1.6 ambapo Meli hiyo pamoja na wahusika waliokuwemo walishikiliwa nchini Jamhuri ya Dominika kwa uchunguzi zaidi.

Rais Magufuli Atoa Siku Tano kwa Wizara ya Madini

$
0
0
Rais Magufuli Atoa Siku Tano kwa Wizara ya Madini
Rais John Magufuli amemuapisha Doto Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini na kuiagiza wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha kanuni za sheria mpya ya madini namba 7 ya mwaka 2017 inasainiwa ifikapo Ijumaa, Januari 12, 2018.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya Biteko kuapishwa leo Jumatatu Ikulu jijini Dar es Salaam na ameelezea kutoridhishwa kwake na namna viongozi na watendaji wa Wizara ya Madini wanavyotekeleza majukumu yao polepole na bila kujali maslahi ya nchi.

“Sheria hii imepitishwa na Bunge na mimi nikaisaini tangu mwezi wa saba mwaka 2017, mpaka leo ni miezi saba bado hamjasaini kanuni zake ili sheria ianze kutekelezwa, na wahusika wote wapo, yaani mpaka leo hamjaelewa Watanzania wanataka nini? Amehoji Rais Magufuli.

Kutokana na hali hiyo amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kushirikiana na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu na Wakurugenzi wanaohusika katika Wizara ya Madini kuhakikisha kanuni hizo zinasainiwa.

Serikali Yawatoa Hofu Watanzania Kuhusu Tatizo la Umeme

$
0
0
Serikali Yawatoa Hofu Watanzania Kuhusu Tatizo la Umeme
Serikali yawatoa hofu Watanzania kuhusu tatizo la umeme na utekelezaji wa mradi wa treni ya umeme nchini ambao ujenzi wake unaendelea.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk Hassan Abass amesema jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha umeme wa kutosha unazalishwa nchini.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu jijini Dar es Salaam kuhusiana na utekelezaji wa ahadi za Serikali, Dk Abass amesema kazi ya kusanifu njia yote itakayopita reli hiyo ya umeme imeshakamilika.

"Suala la umeme sio tatizo Serikali inaendelea kutekeleza miradi zaidi ya  20 kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika,"

Dk Abass amesema Serikali kupitia kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco) inatarajia kununua vichwa 23 vya treni ya umeme na viwili vya treni ya dizeli kwa ajili ya kuboresha usafiri wa reli.

Sambamba na hilo inatarajia pia kununua mitambo 25 ya ukarabati wa reli na mabehewa 1,590 kati ya hayo 1,530 yakiwa ya mizigo na 60 ni ya abiria.



Dk Abass amesema zabuni za manunuzi hayo zinatarajiwa kufunguliwa ndani ya mwezi huu.

Amesema kati ya mabehewa 60 ya abiria 15 ni daraja la kwanza na 45 daraja la kawaida.

Kuhusu usafiri wa majini Dk Abass amesema tayari Serikali imenunua meli mpya mbili za mizigo katika ziwa Nyasa.

Meli hizo Mv Njombe na  Mv Ruvuma na zina uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja na zimeanza kufanya kazi wiki iliyopita.

Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images