Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Mh. Edward Lowassa, Mbowe wamjulia hali Mzee Kingunge

$
0
0
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa kumjulia hali Mzee Kingunge Ngumbare Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili anapopatiwa matibabu.

Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alifika hospitalini hapo kumjulia hali mzee huyo.

Hii ndio Benki Mpya iliyopewa Leseni ya Biashara na Benki Kuu ya Tanzania

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa taarifa kwa kwa umma kuwa, imetoa leseni ya biashara kwa benki mpya yenye jina, Guaranty Trust Bank (Tanzania) Limited.

Leseni hiyo inatoa kibali kwa taasisi hiyo kutoa huduma za kibenki nchini Tanzania kama benki ya kibishara na imetolewa kuanzia Januari 5, 2018.

Makao Makuu ya Benki hiyo yanapatikana Kitalu namba 4, Regent Estate, Barabara ya Bagamoyo, jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya Benki Kuu imekuja siku chache tangu ilipozifutia leseni za biashara, benki 5 ambazo ni Covenant Bank, Efatha Bank, Njombe Community Bank, Kagera Farmers’ Cooperative Bank, na Meru Community Bank.

Serikali yatoa neno kuhusu Bombardier na Meli ya Tanzania iliyokamatwa na dawa za kulevya

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa neno kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2018 kuhusu ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q400 iliyozuliwa nchini Canada na Meli ya iliyosajiliwa kwa namba za Tanzania iliyokamatwa huko Jamhuri ya Domica na Shehena ya dawa za kulevya.

Kuhusu Bombardier Serikali kupitia kwa Msemaji wake Mkuu, Dkt. Abbas Hassan amesema bado ratiba ipo vile vile kuwa ndege hiyo ya Bombardier na ile kubwa ya Dreamliner zote zitafika nchini kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.

“Ishu ya ndege tutaizungumza itakapofika wakati wake lakini mara ya mwisho nilisema ndege zote za serikali ambazo tumenunua ratiba yake ni kufikia mwezi Juni- Julai mwaka huu ndege zote nne ikiwemo ile ndege ya ndoto yetu ya Boeing Dreamliner zitakuwa zimefika nchini.“amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.

Kwa upande mwingine Serikali imekiri kupokea taarifa za Meli yenye usajili wa Tanzania kukamatwa kwenye visiwa vya Jamhuri ya Dominika ikiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine.

“Suala la meli iliyokamatwa Dominika hili nalifahamu, nimelisikia kwa hiyo wenzetu wa wizara ya mambo ya nje bado wanafuatilia kujua usahihi maanake imeripotiwa hivyo kwa hiyo wizara ya nje tumeshazungumza nao na wanalifanyia kazi kwahiyo kama kutakuwa na taarifa zitatolewa.“amesema Dkt. Hassan Abbasi.

Mnamo Desemba 31, 2017 Jeshi la Maji nchini Uholanzi liliikamata Meli yenye usajili wa Tanzania ikiwa na shehena ya dawa za kulevya aina ya Cocaine tani 1.6 ambapo Meli hiyo pamoja na wahusika waliokuwemo walishikiliwa nchini Jamhuri ya Dominika kwa uchunguzi zaidi.

Polisi yatumia Helikopta Kuangalia Kusalama Dar

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema wanatumia helkopta ili kuangalia maeneo ambayo yamepata madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kaimu kamanda wa polisi kanda kanda hiyo, Benedict Kitalika akizungumza leo Jumatatu amesema kutokana na mvua zilizonyesha jeshi hilo limeamua kutumia helkopta hiyo ili kujua ni maeneo gani yameathirika.

"Kuanzia sasa hivi tumeanza kuangalia sehemu mbalimbali kwa kutumia helkopta hivyo tutawajuza baadaye kama kuna madhara yametokea kutokana na mvua hizi zinazoendelea," amesema Kitalika.

Pia amewataka madereva wanaotumia barabara ya Morogoro wasipite Jangwani kutokana na maji yanayopita juu ya daraja.

Amesema njia wanayotakiwa kupita wakifika Magomeni usalama wapite barabara inayotokea Ilala na  barabara inayoelekea Kinondoni.

"Barabara inayotokea Kigogo haina madhara hivyo madereva waitumie isipokuwa ile ya Jangwani haipitiki," amesema Kitalika

BREAKING NEWS: Chid Benz akamatwa na madawa

$
0
0
Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz anashikiliwa tena  na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na hii inakuwa mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili.

Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP, Giless Muroto amesema kwamba ni kweli msanii huyo alikamatwa na taarifa kamili zitatolewa hapo kesho.

Kamanda Muroto amesema "Ni kweli Chidi Benz mnamo tar 30/12/2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zidhaniwayo kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani"

Aidha ameongza kuwa watuhumiwa wote bado wako mahabusu.

EATV.

Mashabiki wa Lulu Michael Kuanza Kumuona Jumatano hii

$
0
0
Zikiwa zimepita siku 54 tangu muigizaji wa filamu bongo,  Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela,  sasa mashabiki wake wataanza tena kumuona kupitia tamthiliya ya Sarafu inayotarajiwa kuanza kurushwa kuanzia Januari 10 siku ya Jumatano.

Sarafu ni moja ya tamthiliya zitakazoonyeshwa katika king’amuzi cha DSTV kupitia chanel yao ya Maisha Magic Bongo ambapo itakuwa inarushwa siku ya Jumatano na Alhamisi.

Katika tamthiliya hiyo ambayo msimu wake wa kwanza utaenda mpaka Machi mwaka huu, imesheheni waigizaji mbalimbali maarufu, ambapo mbali na Lulu wapo Funga Funga(Jengua), Mzee Chilo, Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Idris Sultan, Yusuph Mlela na mastaa wengineo.

Ndani ya tamthiliya hiyo Lulu anaigiza kama mtoto wa familia tajiri ya Mhandisi Sanga akiwa anatumia jina la Jack huku mama yake akiwa ni muigizaji wa siku nyingi Suzan Lewis 'Natasha'.

Uzinduzi wa tamthiliya hiyo uliofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, uliendana sambamba na uzinduzi  wa tamthiliya nyingine ya Sarafu ambapo baadhi ya wadau waliweza kushuhudia moja ya kipande alichoigiza Lulu, ambacho alionekana kukitendea haki.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliokiona kipande hicho walikuwa na maoni yao kuhusu namna walivyojisikia  baada ya kumuona msanii huyo akiwemo mrembo Wema Sepetu, ambaye alisema kipande hicho kimemuhuzunisha kwani alitamani naye angejumuika nao siku hiyo lakini kutokana na matatizo aliyoyapata imekuwa ngumu.

Kwa upande wa Natasha, amesema yeye sehemu hiyo ilipofika alitamani hata kutoka nje ya ukumbi, kwa kuwa yeye kama mama inamuumua kwa mtihani anaopitia Lulu kwa sasa ukilinganisha na umri wake mdogo aliokuwa nao.

Novemba 13, mwaka jana, Mahakama Kuu ilimhukumu kwenda jela miaka miwili Lulu kutokana na kukabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa  na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira.

Sheria ya Viboko 12 kwa Wanaume Yafafanuliwa

$
0
0
Uongozi wa kata ya Nyehunge Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, umetolea ufafanuzi taarifa za kuwepo kwa sheria ya kuwachapa viboko 12 mtu yeyote atakayekutwa amesimama na mwanafunzi wa kike, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv diwani wa kata hiyo Charles Kalam Mbogo, amesema taarifa hizo hazina ukweli kabisa, kwani hakuna kikao cha uongozi wa kata hiyo, kilichopitisha sheria hiyo.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa kata ya Nyehunge, wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwachapa viboko 12 au faini ya shilingi 10,000 wanaume wote watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike, kufuatia kukithiri kwa tatizo la wanafunzi hao kukatisha masomo kwa sababu ya kupata ujauzito.

EATV.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

"Nilimpa Nafasi Nandy Asikike ila Haniwezi"- Ruby Afunguka

$
0
0
Msanii wa kizazi kipya ambaye kwa sasa amerudi na ngoma aliyoipa jina 'Are U Ready' amejibu swali la wapenzi wengi wa burudani kwamba aliamua kuwa kimya kwa muda mrefu ili kumpatia nafasi msanii mwenzake Nandy na siyo kwamba alikuwa akimuogopa.

Akizungumza ndani ya Planet Bongo ya East Africa Radio, Ruby amesema kwamba ujio wa Nandy haukumpa Stress kwani anaamini msanii huyo ni mzuri na alikuwa akihitaji kusikika ndiyo maana hakutaka kukurupuka ili aanze kushindanishwa..

Aidha Ruby ameongeza kwamba anaamini kuwa Nandy anafanya aina muziki aliokuwa akifanya (Zouk) ndiyo maana hata watu wanadiriki kusema kwamba alikuja kuziba nafasi yake katika muziki na kuongeza kwamba tofauti yao ipo kwenye 'TONE' na 'SKALES' ndiyo maana aliamua kutulia ili kutafuta njia nyingine ili wasishindanishwe.

Pamoja na hayo Ruby amedai kwamba hapendi kushindanishwa na mtu yeyote na kwamba yeye katika maisha yake amezoea kujishindanisha mwenyewe.

Mbali na hayo Ruby ameongeza kwamba katika ukimya wake jambo lilokuwa likimuumiza sana ni jinsi ambavyo mashabiki zake walikuwa wakilalamika kwamba wamemmiss hali iliyokuwa inamfanya awe mnyonge na kushindwa cha kufanya.

Serikali yafunguka Kukamatwa Meli ya Tanzania

$
0
0
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amefunguka kuhusu meli inayodaiwa kuwa na usajili wa Tanzania iliyokamatwa Santo Domingo, Jamhuri ya Dominican siku ya Boxing day ikidaiwa kuwa na madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye ujazo wa tani 1.6

Dkt. Abbas akizungumza leo na waandishi wa habari amekiri kuwepo kwa taarifa hizo na kudai kuwa wao wanaifanyia kazi illi kujua ukweli juu ya sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa kwa siku kadhaa sasa.

"Suala la meli iliyokamatwa Dominica hili nalifahamu nimelisikia kwa hiyo wenzetu wa Wizara ya Mambo ya Nje bado wanafuatilia kujua usahihi, maana yake imeripotiwa hivyo kwa hiyo Wizara ya Mambo ya Nje tumeshaongea nao wanafanyia kazi kama kutakuwa na taarifa nyingine basi itatolewa" alisema

Taarifa za awali zilikuwa zinasema kuwa Jeshi la Maji la Uholanzi liliishtukia meli hiyo siku ya Christmas na kuikamata siku kesho yake ambayo ilikuwa siku ya boixing day na kuipeleka Santo Domingo, Dominican. Mnamo Disemba 31, 2017 Meli hiyo ilifanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa ilikuwa imebeba kilo 1600 ambazo ni sawa na tani 1.6 za madawa ya kulevya zilizokuwa zimefichwa kwenye matenki ya mafuta.

MC Pilipili Aipongeza Serkali kwa Kuwabana Wanoatupia Picha za UCHI Mitandaoni .....Aitaka Pia Imuhoji Idris na Kim Sasha

$
0
0
Baada ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumuita msanii wa Bongo Fleva Gigy Money na Mwanamitindo Sanchoka kwa mahojiano maalumu kuhusu kazi zao ambazo zinaonekana zipo kinyume na maadili hususani kwenye mavazi wanayovaa, Hatimaye Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, MC Pilipili ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kuishauri iendelee kuwasaka wengine wanaofanya hivyo.

MC Pilipili amesema amepokea taarifa hizo kwa mikono miwili ingawaje amesema kuna watu wengi mitandaoni wanafanya makosa kama hayo ya kuvaa nguo fupi au kuonesha maungo yao kwenye mitandao.

“Hiyo hatua mimi nimeipenda kwanza imeturudisha kwenye Maadili..Unajua hapa Bongo mtu anaweza akawa maarufu kwa kuposti maumbo yake tuu mtandaoni hii ni kinyume cha maadili,“amesema MC Pilipili na kuwataja watu wengine wanaokaa uchi mitandaoni

“Nilipatwa na maswali juzi Sancho ameitwa, Gigy Money kaitwa lakini pia kuna msanii mwingine alikuwa maarufu kwa kuposti picha kama hizo amejichora mitatuu anaitwa Agness, mwingine anaitwa Kim Sasha lakini wakati huo namuona Idris naye amevaa chupi hivi ile haihamasishi au naye aitwe?“amesema MC Pilipili.

Kiongozi Mkubwa wa Upinzani Kesho Kutimkia CCM. ....Ni Nani Huyo? Endelea Kuwa Nasi

$
0
0
CCM kupitia kwa Katibu Mwenezi Humphrey Polepole leo asubuhi wanasema watampokea kiongozi mkubwa wa Upinzani ambaye atajiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) .Je, ni nani huyo? Jibu litapatikana Kesho.

Usikose Kuitembelea Mpekuzi Blog mapema asubuhi  kwa habari motomoto

Serengeti Boy Awachonganisha Mama Diamond na Mama Hamisa Mobetto

$
0
0
Hivi karibuni umeibuka mzozo mkubwa kati ya mama mazazi wa mlimbwende Hamisa Mobeto, Shufaa Lutigunga na mama mzazi wa msanii Diamond Platinumz, Mama Sandra, kufuatia kitendo cha mama Sandra kudaiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na kijana mdogo ambaye angeweza kuwa mtoto wake.

Kufuatia kitendo hicho, mama Hamisa amemjia juu mama Diamond akimsema kuwa anakubali kuolewa na kijana mdogo kama mwanaye, jambo ambalo siyo zuri kwa maadili ya kitanzania.

Shufaa aliongeza kuwa kuolewa na kijana mdogo aliyemuita kwa jina ‘serengeti boy’ ni kujivunjia heshima kitu ambacho hawezi kukifanya, ikiwa ni kwa faida ya wajukuu wake.

“Jamani mimi kama ni kuolewa basi nitaolewa na mtu mzima mwenzangu kwa sababu Serengeti Boy kwangu haiwezekani, nahitaji kuolewa kweli ila nitaolewa na mzee mwenzangu ili wajukuu wapate babu,” alieleza Shufaa lipohojiwa.

Mama mzazi wa Diamond, amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na kijana ambaye kwa umri ni sawa na mtoto wake anayeitwa Rally Jones jambo ambalo limeibua sintofahamu na kuamshan hisia za watu wengi, huku kila mmoja akiwa na maoni yake juu ya jambo hilo.

Simba Aibu Tupu Yanyolewa Ndevu Mapinduzi

$
0
0
Simba imeyaanga mashindano ya Mapinduzi 2017/18 kwa aibu baada ya kutolewa katika hatua ya makundi kwa kufungwa 1-0 na URA katika mchezo wa mwisho wa Kundi A uliokuwa unaamua umu gani kati ya hizo itasonga mbele.

Simba ilikuwa inahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kufikisha pointi saba (sawa na URA) lakini watoto wa Msimbazi wangefuzu nusu fainali kwa tofauti ya magoli.

Kwa upande wa URA wao walikuwa wanahitaji sare tu ili kufikisha pointi nane ambazo zisingefikiwa na Simba kwa sababu wangesalia na pointi tano.

Ushindi dhidi ya Simba unaifanya URA ifikishe pointi 10 na kuongoza Kundi A mbele ya Azam ambao wanapointi tisa.

Katika mechi nne ambazo Simba imecheza katika hatua ya makundi, imeshinda mechi moja pekee, sare moja na kupoteza michezo miwili. Imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi A ikiwa na pointi nne nyuma ya Azam (pointi 9) na URA (pointi 10).

Msimu uliopita 2016/17, Simba ilicheza fainali na kupoteza kwa kufungwa 1-0 na Azam ambao walitangazwa mabingwa.

Kijana Akatwa Vipande Vipande Baada ya Kuuchapa Usingizi Kwenye Reli za Treni

$
0
0
INATISHA! Kijana mmoja maarufu kwa jina la Sharobaro mjini hapa, aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20, ameuchapa usingizi chini ya daraja la reli kisha kupoteza maisha baada ya kukatwa vipande viwili na treni.
Tukio hilo ambalo Ijumaa Wikienda lilifika punde baada ya kujiri, lilitokea kwenye daraja lililopo Barabara ya lringa- Morogoro, eneo la Msamvu, mchana wa Ijumaa iliyopita na kuibua masikitiko makubwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wasamaria wema waliishuhudia maiti ya kijana huyo ikiwa imekatwa vipande viwili ndipo wakatoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa huo ambao nao ulitoa taarifa polisi.


Inasikitisha sana.
Akilisimulia Ijumaa Wikienda juu ya tukio hilo la kutisha, mmoja wa mashuhuda hao, Mohamed Shukuru alikuwa na haya ya kusema:
“Kama unavyoona, chini ya daraja hili kuna reli na kunapita treni na juu yanapita magari kuelekea mkoani lringa.
“Sasa baadhi ya watu wa Stendi ya Msamvu hupenda kupumzika chini ya daraja hili na wengine hulala hapahapa.



“Kwa hiyo kinachoonekana, huyu jamaa alipitiwa na usingizi. Sasa treni ilipofika hakuisikia na kujikuta akigongwa kisha kupoteza maisha. Kiukweli ni tukio la kutisha sana.”
Shuhuda mwingine, Jumanne ldd alisema: “Huenda watu wamemuua na kuja kumtupa hapa relini kwa lengo la kupoteza ushahidi. Haiingii akilini, hata uwe chizi kiasi gani, huwezi kuja kulala relini. Vilevile hata ulewe vipi, mgurumo wa treni ni mkubwa hivyo lazima angeamka, binafsi siamini kama huyu kijana amegongwa na treni. “Hebu wahusika wafanye uchunguzi wao kwa kina ili tujue ukweli wa hili tukio.”

Ijumaa Wikienda liliwashuhudia Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa wa Morogoro wakiwa bize kupima eneo la tukio na baada ya kumaliza kazi hiyo waliuchukua mwili wa marehemu huyo na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kusubiria kama kuna ndugu watajitokeza kwani hakukuwa na yeyote aliyemtambua kwenye eneo hilo la tukio.

STORI: Dunstan Shekidele, Moro IJUMAA WIKIENDA

Kinguke Amkumbuka Tundu Lissu Aulizia Hali Yake

$
0
0
Kinguke Amkumbuka Tundu Lissu Aulizia Hali Yake
Mwanasiasa mkongwe , Kingunge Ngombale Mwiru ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili kufuatia kung'atwa na mbwa amemkumbuka na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amesafirishwa na kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi.


Kigunge amemjulia hali Tundu Lissu baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akiwa amefuatana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati Kuu Mhe. Edward Lowassa walipomtembelea leo Januari 8, 2018 katika hospitali ya Muhumbili.

"Vipi kuhusu Tundu Lissu? Nimeona mimi jinsi wanavyonifanyia hapa (madaktari) nimewauliza mimi tu niliyeng'atwa na mbwa mnanifanyia hivi Lissu mmemfanyaje maana majeraha yake yalikuwa makubwa" alihoji Kingunge

Baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA kumueleza Mzee Kingunge juu ya hali ya Tundu Lissu kwa sasa ilimpa faraja mzee huyo na kusema kuwa 'Aluta Continua'

MC Pilipili Aiomba Basata Kuwaita Idriss Sultani, Agness na Wengine Wanaoweka Picha za Utupu Mtandaoni

$
0
0
MC Pilipili Aiomba Basata Kuwaita Idriss Sultani, Agness na Wengine Wanaoweka Picha za Utupu Mtandaon
Baada ya Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumuita msanii wa Bongo Fleva Gigy Money na Mwanamitindo Sanchoka kwa mahojiano maalumu kuhusu kazi zao ambazo zinaonekana zipo kinyume na maadili hususani kwenye mavazi wanayovaa, Hatimaye Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, MC Pilipili ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo na kuishauri iendelee kuwasaka wengine wanaofanya hivyo.

MC Pilipili amesema amepokea taarifa hizo kwa mikono miwili ingawaje amesema kuna watu wengi mitandaoni wanafanya makosa kama hayo ya kuvaa nguo fupi au kuonesha maungo yao kwenye mitandao.

“Hiyo hatua mimi nimeipenda kwanza imeturudisha kwenye Maadili..Unajua hapa Bongo mtu anaweza akawa maarufu kwa kuposti maumbo yake tuu mtandaoni hii ni kinyume cha maadili,“amesema MC Pilipili na kuwataja watu wengine wanaokaa uchi mitandaoni

“Nilipatwa na maswali juzi Sancho ameitwa, Gigy Money kaitwa lakini pia kuna msanii mwingine alikuwa maarufu kwa kuposti picha kama hizo amejichora mitatuu anaitwa Agness, mwingine anaitwa Kim Sasha lakini wakati huo namuona Idris naye amevaa chupi hivi ile haihamasishi au naye aitwe?“amesema MC Pilipili.

Akamatwa kwa Tuhuma za Kujiunganishia Bomba la Mafuta Mali ya TPA Nyumbani Kwake

$
0
0
Akamatwa  kwa Tuhuma za Kujiunganishia Bomba la Mafuta Mali ya TPA Nyumbani Kwake
Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi wanamshikilia Samwel Kilang'ani(63) kwa tuhuma ya kutoboa bomba la mafuta ya dizeli mali ya TPA na  kujiunganishia hadi kwenye nyumba yake ambako ameweka mantanki makubwa ambayo ameyachimbia chini.

Msemaji wa TPA,  Janeth Ruzangi amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo huku polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikiendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.

   

Pretty Kind Baada ya Kufungiwa Miezi 6 Kisa Picha za Uchi Asema "Mimi ni Mtoto Shetani Alinipitia"

$
0
0
Pretty Kind Baada ya Kufungiwa Miezi 6 Kisa Picha za Uchi Asema "Mimi ni Mtoto Shetani Alinipitia"
Msanii wa filamu na video vixen, Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind baada ya kufungiwa na serikali kujihusisha na sanaa kwa miezi 6 kutokana na kupiga picha za uchi, amefunguka kwa kudai kwamba yeye ni mtoto hivyo kufanya tukio hilo alipitiwa na shetani.

Tunda Man Akwaa Skendo Mpya Adaiwa Kutapeli Mamilioni

$
0
0
Tunda Man Akwaa Skendo Mpya Adaiwa Kutapeli Mamilioni
MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva zao la Tip Top Connection, Tunda Man anadaiwa kutapeli mamilioni ya urithi ya msanii chipukizi, Asala Kipengele ‘Asala’.

Akizungumza na Full Shangwe, Asala alidai alitapeliwa fedha za urithi Milioni 30 alizompa Tunda Man ili amsaidie kimuziki lakini hadi sasa wamerekodi wimbo mmoja wa Subiri.

“Sitaki kumsikia Tunda kwa kile alichonifanyia, kanipiga sana hela za urithi kwa kujifanya meneja wangu lakini kumbe alikuwa amepanga kunitapeli,”alidai Asala na kuongeza;

“Kuna pesa kama milioni 30 ambayo nilimpatia kwa ajili ya muziki wangu lakini mpaka sasa sielewi chochote hata nikimpigia simu nyingi ni subiri, subiri.”

Full Shangwe lilimtafuta Tunda kujibu madai hayo alidai kwamba si kweli kwamba ametapeli hizo milioni 30.

“Hilo suala ndio nalisikia kwako wala mimi sijatapeli hizo milioni 30 unazoniambia.”
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images