Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Wakuu wa Shule za Serikali Zilizofanya Vibaya Katika Matokeo ya Form Six Wawekwa Kikaangoni…Wapewa Mwezi Mmoja Kujieleza.

$
0
0
Wakuu wa shule za serikali zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu pamoja na Maofisa elimu wa Mikoa wamepewa muda wa mwezi mmoja ili kubaini chanzo cha  shule zao kuwa na ufaulu hafifu.

Baada ya kubaini chanzo hicho cha ufaulu hafifu wanatakiwa kutoa taarifa kwa katibu mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI.

Miongoni mwa shule ambazo wakuu wake wametakiwa kujieleza ni pamoja na shule ya Tambaza iliyopo jijini Dar es salaam na shule ya Iyunga ya Mkoani Mbeya, ambapo muda huo wa mwezi mmoja umeanza  leo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,  katibu Mkuu Tamisemi Jumanne Sagini amesema, kushuka kwa ufaulu kwa shule hizo kumewashtua  watu wengi, kwani shule hizo zimejengewa uwezo mzuri wa vifaa pamoja na miundombinu.

Hata hivyo Sagini amesema, idadi ya wanafunzi 22,685 waliofaulu masomo ya sayansi kwa mwaka  huu wa 2014  ni kubwa kwa  zaidi ya wanafunzi 3,939 ikilinganishwa na wanafunzi 18,746  waliofaulu masomo hayo mwaka jana.

Amesema kuwa ufaulu huo umeipa changamoto Serikali na imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi ambae amefaulu na kupata alama stahiki  katika masomo aliyoyachagua anapata shule.

Aidha amewataka wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamepangiwa kusoma masomo ya sanaa ilihali ufaulu wao ni katika masomo ya sayansi, kutokuwa na wasiwasi kwani serikali imebaini changamoto hiyo na kuifanyia kazi.

Batuli Ateswa na Dawa za Kulevya..Listi Ndefu ya Wanaosubiri Kunyongwa Yamuumiza

$
0
0
Na Gabriel Ng’osha
MWANADAFADA kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa anaumia kuona listi ndefu ya Wabongo wanaosubiri kunyongwa nchi mbalimbali kwa kukutwa na dawa za kulevya.

Batuli alisema kinachowaponza vijana wengi ni kupenda fedha za chapuchapu, matokeo yake wanaambulia kifungo cha maisha na wengine kunyongwa katika nchi zenye misimamo mikali.

“Inashangaza sana wasichana wanaingia katika biashara hii haramu, mbaya zaidi wanapoingiza madawa ya kulevya wanaharibu kizazi kilichopo, inaniuma sana maana vizazi na vizazi vinaendelea kuangamia,’’ alisema Butuli.

Kaburi la Adamu Kuambiana Latoboko Kimaajabu ni Baada ya Mauza Uza Kukutwa Kaburini kwa Recho

$
0
0
SIKU chache baada ya kukutwa mauzauza katika kaburi la mwigizaji Rachel Haule ‘Recho’, kaburi la mwigizaji Adam Kuambiana (pichani)limekutwa limetoboka kimaajabu.

Gazeti la Risasi Jumamosi toleo la Julai 19, mwaka huu lilikuwa na babari yenye kichwa cha habari kisemacho: ‘Uchawi kaburini kwa Recho.’ Kwenye habari hiyo, ilielezwa kuwa katika kaburi la Recho kulikutwa tunguri iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini.

Baada ya habari hiyo, siku mbili baadaye, chanzo kingine kiliwapigia simu waandishi wetu na kuwaeleza kuwa mbali na tukio la Recho, kaburi la Kuambiana limetoboka kimaajabu na kuzua mtafaruku miongoni mwa watu walioshuhudia kwa mara ya kwanza tukio hilo.

“Jamani haya ni mambo ya kishirikina, huwezi amini kaburi hili limetoboka ghafla kimaajabu maana juzi tu nilikuja kutembelea makaburi haya, lilikuwa halijatoboka,” kilisema chanzo hicho.

Mapaparazi wetu walifika katika makaburi hayo na kujionea kaburi hilo likiwa limetoboka huku watu wengi waliokuwepo eneo hilo walidai kuwa tukio hilo si la kawaida kwani limetokea wakati ambao mvua hazijanyesha.

Walisema kama tukio hilo lingetokea wakati ambao mvua zinanyesha basi wasingekuwa na mashaka lakini kwa jinsi ambavyo limetoboka wakati wa jua kali ni dhahiri kutakuwa na ‘mkono wa mtu’.
“Hapa bwana tusidanganyane kuna mkono wa mtu, haiwezekani kaburi lisitoboke kipindi kile cha mwanzomwanzo lije kutoboka sasa wakati kuna jua kali namna hii, lazima kuna mkono wa mtu tu,” alisema shuhuda mmoja.

Wengine walikwenda mbali zaidi kwa kuhoji kulikoni matukio hayo yawe kwa mastaa pekee na si kwa watu wengine?“Hii si bure hapa wachawi watakuwa na shida yao binafsi, haiwezekani iwe kwa mastaa tu ndiyo kunakuwa na mauzauza,” alisikika shuhuda mwingine.
Alipoulizwa mmoja wa walinzi wa eneo hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema hata yeye hajui kwa nini inatokea katika makaburi ya mastaa.“Mimi hata sijui kwa nini lakini yamefululiza, juzi tumeona kwa Recho na leo kwa Kuambiana, tumuombe sana Mungu atuepushe na mabaya,” alisema mlinzi huyo.

Hata hivyo, licha ya watu wengi walioshuhudia kaburi hilo kuamini katika uchawi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye alionekana ni mcha Mungu alisema hakuna uchawi wowote zaidi ya ardhi kutitia na kusababisha mmomonyoko wa udongo.

“Jamani siyo uchawi, hivi vitu vinatokea. Hapa itakuwa wakati wa kuzika, kulikuwa na uwazi umeachwa hivyo ardhi iliposhuka kuziba uwazi huo ndipo iliposababisha tobo,” alisema shuhuda huyo mcha Mungu.
Kuambiana alikutwa na umauti Mei 17, mwaka huu alipokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar baada ya kuugua ghafla akiwa hotelini alipokuwa amepanga kwa ajili ya kuandaa filamu.

Maajabu:Kijana Ang'olewa meno 232, Madaktari Watumia Nyundo na Tindo

$
0
0
Madaktari nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani .

Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.

Baada ya Miaka Miwili ya Ndoa, Aunt Ezekiel aanza kusaka Mtoto

$
0
0
Mwigizaji nguli katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel (pichani) anadaiwa kuanza kusaka mtoto ikiwa ni miaka miwili tangu afunge ndoa na Sunday Dimonte.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Aunt, siku si nyingi staa huyo atakwenda kuweka makazi ya muda kwa mumewe Dubai hadi atakapopata ujauzito.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, rafiki huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa kuogopa kusutwa na ‘matarumbeta’, alisema wengi wanadai mume wa Aunt yuko jela kwa hiyo ili kuwahakikishia kuwa kitu hicho hakipo ameamua aende kuishi Dubai kwa muda hadi atakaponasa ujauzito.

Kama mipango yake itakwenda vizuri, baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kupita ataondoka na safari hii atakaa sana Dubai hadi Mungu atakapomjalia kupata mimba ndipo atarejea Bongo. Lakini baadaye ataondoka tena kwani hata kujifungua amependa akajifungulie Dubai,” alisema rafiki huyo.

Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani lilimtafuta Aunt na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa alisema hapendi kuweka hadharani mambo yake na mumewe lakini kuhusiana na ishu ya kwenda kuishi Dubai, muda si mrefu ataondoka.

Nadhani unajua kuwa mke na mume Mungu akiwajalia afya njema ni muhimu ndoa ijibu kwa kupata mtoto, sasa kuhusu kwenda kuishi Dubai ndiyo mipango yangu.

“Nataka kuwakomesha wale wanaodai kuwa mume wangu amefungwa! Sitaki kuwajibu kwa maneno, nataka kuwajibu kwa vitendo,” alitamba Aunt.

Chanzo: Amani/Gpl

Baaya ya Brazil Kumtimua Kocha Capello Huyu Ndio Kocha Mpya wa Team Hiyo

$
0
0
Shirikisho la soka la Brazil CBF limemtangaza aliyekuwa mchezaji wa Brazil Dunga kuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya pili.
Dunga aliyeiongoza Brazil kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1994 aliwahi pia kuwa kocha katika mwaka wa 2006 hadi 2011.
Dunga amechukua pahala pake Luiz Felipe Scolari, ambaye alijiuzulu kufuatia kimbunga cha mabao 7-1 ambayo timu hiyo ililazwa na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali .

Sadfa ni kuwa Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 naye alifutwa kazi baada ya selecao kubanduliwa nje ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 katika hatua ya robo fainali.
Carlos Alberto Parreira ndiye aliyechukua pahala pake lakini hata naye haku dumu Scolari alipotajwa kuwa Kocha.
Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Brazil katika semi fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata kichapo kibaya cha mabao masaba kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la Dunia Ujerumani.

Dunga amewapiku mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
Wakati huohuo kocha wa Argentina Alejandro Sabella, 59, amesema kuwa atatangaza hatima yake juma lijalo baada ya kushindwa bao moja kwa nunge na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil mapema mwezi huu .
Wachezaji wanamtaka kocha Sabella kuiongoza timu hiyo katika kipute cha kuwania ubingwa wa mataifa ya Amerika ya Kusini yaani 2015 Copa America mashindano yatakayoandaliwa huko Chile.

Sakata la Viungo vya Binadamu kutupwa Dar, Chama cha Madaktari chataka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) Kifungwe

$
0
0
Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU)  sanjari na hospitali iliyo chini yake, vinastahili kufungiwa.

Tamko hilo la chama limekuja huku mamlaka mbalimbali zinazohusika na usimamizi wa karibu wa vyuo vikuu vya matibabu zikikiweka chuo hicho kiporo,  kusubiri uchunguzi wa tuhuma zinazokikabili za kutupa viungo vya binadamu jalalani, ukamilike kabla ya kuchukua hatua zinazostahili.

Kitendo hicho cha kutupa viungo vya binadamu jalalani kimetajwa na watu mbalimbali, wakiwemo wataalamu kuwa ni cha  ajabu kinachodhalilisha nchi na utu wa binadamu.

Rais wa MAT, Dk Primus Saidia alisema kitendo hicho  ni cha aibu na kwamba  kama ingekuwa nchi nyingine, walistahili kufungiwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema taasisi hiyo isingetakiwa kutoa mafunzo ya udaktari wala kufanya tafiti zozote, ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kutoa huduma za afya  katika hospitali yake.

Mwingine aliyezungumzia sakata hilo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Margareth Sitta aliyepongeza taasisi za serikali kwa hatua za haraka walizochukua kuhakikisha watu hao wanabainika mapema na kukamatwa.

Hata hivyo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa nyakati tofauti, walisisitiza nia yao ya kuchukua hatua dhidi ya chuo hicho, mara jopo linalochunguza sakata hilo litakapokamilisha kazi yake. 

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Kebwe Stephen alisema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho ambacho si cha kawaida.

Alitaka  upelelezi ufanyike haraka, adhabu stahiki ichukuliwe kutokana na kitendo hicho.

 “Baada ya kukamilika kwa upelelezi wa tukio hili na kupata taarifa za kwa nini walifikia hatua hii, naahidi wizara yangu itachukua hatua kali,” alisema Kebwe.

Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es  Salaam jana, msemaji  wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja alisema kutokana na kuwa jambo hilo ni jipya, wataangalia uwezekano wa kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema ingawa wizara yake haihusiki na usimamizi wa vyuo hivyo vinavyozalisha madakatri na kutaka waulizwe TCU, kwa mujibu wa Mwamwaja, kitendo walichofanya madaktari husika si cha kimaadili.

Alisema pamoja na kuwa kitendo hicho si cha maadili pia wanaangalia madhara ya kiafya kulingana na tukio hilo.

“Lakini pia ni vema kuangalia na jiji (Dar es Salaam) ni jinsi gani wanasimamia madampo yao, kwa nini inaruhusu kumwaga uchafu wowote bila kuwepo wakaguzi au ni utaratibu gani wanatumia kulinda afya za wananchi,”alisema  Mwamwaja.

Kwa upande wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yenye dhamana na vyuo vikuu, Katibu Mkuu wake,  Profesa  Sifuni Mchome alisema pia wanasubiri ripoti  ya timu iliyoundwa kuchunguza suala hilo wachukue hatua za haraka chini ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

“Kwa sasa uchunguzi unaendelea hivyo hatuwezi kuchukua hatua yoyote,” alisema Profesa Mchome. Katibu Mkuu alisema katika tume hiyo iliyoundwa na polisi, yumo  mwakilishi wa elimu kutoka TCU.

Alisisitiza wataangalia suala hilo na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kwa sasa hakuna sheria inayowabana kutokana na kuwa suala hilo ni jipya nchini.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Habari Mwandamizi wa TCU, Edward Mkaku alisema wanasimamia ubora wa elimu ya juu na suala lililotokea ni kesi ya chuo kwa asilimia 100.

Hata hivyo, alisema kwa kuwa Mkurugenzi wa Ithibati wa Elimu ya Juu katika tume hiyo yupo kwenye tume iliyoundwa, wataangalia hatua za kuchukua baada ya uchunguzi kukamilika.

Alisema TCU ni taasisi yenye utaratibu, hivyo itatoa uamuzi baada ya ripoti kwa kuwa sasa IMTU bado ni watuhumiwa na haipaswi kuhukumiwa.

“Tunasubiri tume imalize uchunguzi ndipo tutaona tutachukua hatua gani kulingana na  Sheria ya Vyuo Vikuu kwani kwa sasa sheria ya suala hilo haipo kutokana na kwamba ni jipya kutokea nchini,”alisema.

Wakili wa Kujitegemea kutoka MK Law Chambers, Karoli Mluge akizungumza nafasi ya sheria katika suala hilo, alisema hakuna sheria inayozungumzia kwamba kutupa viungo vya binadamu au mwili hadharani ni kosa.

Mluge alisema  jamii lazima itofautishe Sheria na suala zima la maadili na ubinadamu. Alisema kibinadamu na maadili, utupaji wa viungo vya binadamu si sahihi na ni jambo linaloshitua lakini  kisheria, haimtii mtu hatiani .

“Kimaadili si sawa, lakini suala hili ni la kiubinadamu  halina sheria,” alisisitiza. Alisema hata mtu anapokutwa na kiungo cha binadamu, hatiwi hatiani kwa maana ya kukutwa na kiungo husika isipokuwa, kinachotafutwa ni kujiridhisha ni kwamba amekipataje kutoka mwili wa binadamu.

“Si kosa kukutwa na kiungo cha binadamu…cha msingi, ni kuthibitisha umekipataje,” alisema. 

Kumekuwepo maswali juu ya ni namna gani vyuo vinapata miili ya kufanyia mafunzo kwa vitendo na baada ya mafunzo inapaswa iteketezwe namna gani. Hata hivyo katika kutafuta ufafanuzi wa maswali haya, taasisi hizo zinazohusika na usimamizi wa vyuo hazikuwa tayari kuzungumzia kwa undani suala hilo, kwa madai ya kusubiri matokeo ya tume iliyoundwa.

Tume hiyo iliyoundwa, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, itahakikisha inakuja na majibu, ikiwa ni pamoja na kujua idadi kamili ya watu wenye viungo hivyo.

Timu hiyo ya wataalamu ya watu saba inayohusisha pia Mkemia Mkuu wa serikali, itakuja na majibu viungo hivyo ni vya muda gani na zilitumika kemikali gani kuvikausha.

Jopo litabaini pia  kama ipo sheria na ni ipi  inavunjwa. Inalenga kubaini pia kama upo uzembe katika kulinda viungo vya binadamu na vinapatikanaje kwa ajili ya mazoezi.

Katika sakata hilo lililovuta hisia za watu na kuzua mjadala mitaani na kwenye mitandao ya kijamii, watu wanane wakiwemo Madaktari wa IMTU, walikamatwa juzi na Polisi kwa mahojiano wakituhumiwa kuhusika  katika  utupaji viungo vya binadamu jalalani.

Polisi ilisema mifuko ipatayo 85 yenye vichwa, miguu, mikono, moyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu, ilikutwa maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji, eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.

Miss K-Lyinn Ndani ya Mahaba Niue Siyo Cinema ya Bongo Movie Wala Siyo Tamthiiria ya Sunche na Kapeto

$
0
0


Ni mapenzi ya kweli haya wala siyo cinema ya bongo movie wala  siyo tamthiiria ya Sunche na Kapeto. Miss K-Lyinn ndani ya mahaba niue kama king na queen vile Safi sana

Ripoti: Ndege ya Algeria iliyobeba watu 116 imethibitishwa kuwa imeanguka

$
0
0
Ndege ya shirika la Algeria iliyokuwa imebeba abiria 116 ambayo awali iliripotiwa kuwa imepoteza mawasiliano kwa zaidi ya dakika 50 imethibitishwa kuwa imeanguka.

Kwa mujibu wa Aljazeera, maafisa wa Algeria wamethibitisha kuwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Burkina Faso kwenda katika mji mkuu wa Algeria, Algiers imeanguka Kusini mwa Mali.

Maafisa wa serikali ya Ufaransa wameeleza kuwa ndege hiyo AH5017 ilipotea kwenye radar katika eneo la Mali baada ya mvua kubwa kunyesha na inaelezwa kuwa vipande vya ndege hiyo vimeanza kuonekana baharini.

Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni binafsi ya Hispania inayofahamika kama Swiftair ilikuwa imebeba abiria 110 na wafanyakazi sita.

Kijana Apigwa Shoka la Kichwa Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu, Madaktari Wahaha Kumuokoa

$
0
0


Baada ya madoctor wa bugando kupambana kuokoa maisha ya jamaa aliye fumaniwa huko mwanza hatimaye wamefankiwa kumtoa shoka kichwani na hali yake bado mbaya yuko ICU kwa uangalizi zaidi mke wa mtu sumu 

Ali Kiba Leo Asubuhi Katoa Nyimbo Mbili Kwa Mpigo...Zidownload Hapa

$
0
0
Baada ya wapenzi wa muziki Tanzania kusubiri kwa muda mrefu sasa wamepata nafasi ya kujiburudisha na ngoma mpya kutoka kwa Alikiba. Tarehe 25 Julai, 2014 Alikiba ameachia single mbili mpya kwa wakati mmoja ziitwazo “Mwana” na “Kimasomaso”. Alikiba anajulikana ndani na nje ya Tanzania kwa hit zake kama Cinderella, Mapenzi yanarun dunia, Single boy, na Dushelele. Cinderela ndiyo wimbo ambao mpaka sasa umeweka rekodi ya kuuza copy nyingi katika Afrika Mashariki mwaka 2008. Mwaka 2012 Alikiba alishinda tuzo ya best Rhumba/ Zouk na wimbo wake wa “Dushelele” katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Alikiba anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kuimba na utunzi wa nyimbo pamoja na kuwa mburudishaji mkali sana katika show zake za live na mpaka sasa ametembea nchi nyingi sana duniani kuburudisha wapenzi wa muziki. Sasa unaweza kupata nyimbo mbili mpya za Alikiba katika tovuti ya www.mkito.com

Kimasomaso – https://mkito.com/song/kimasomaso/2194
Mwana – https://mkito.com/song/mwana/2195

Maimartha Amsuta Mtu Kwa Keki, Shampeni na Sare za Madira. Sikiliza Kisa Hapa

$
0
0
Wenyewe wamesema kuwa namna waliyoifanya wamemsuta mtu ki-technology mpya kutokana na namna yao mpya,unaweza kudhani ni filamu lakini Maimartha ameamua kumuelekeza kijana aliyeonekana mbeya.
Iliiandaliwa Keki na mpaka Shampeini imefunguliwa unaambiwa kumbe lengo lilikua kwa mtu mmoja sikiliza namna mpango ulivyokua.

Pati za Kajala za Kila Siku Zazua Jambo, Sidhani Kama Fedha za Sinema Zinaweza Kumpa Jeuri Hiyo

$
0
0
Na Musa Mateja
MAKUBWA! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ameangusha pati nchini China kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuibua minong’ono juu ya chanzo cha jeuri hiyo ya fedha.

Kufuru hiyo ya fedha ilianzia jijini Dar katika bethidei ya mwanaye (Paula) hivi karibuni ambapo awali alikwenda kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Shule ya Sinza Maalum kisha kuangusha bonge la sherehe katika Hoteli ya Sea Cliff.

Baada ya vurugu hizo ambazo kimsingi zilidaiwa kuteketeza milioni kadhaa, siku chache baadaye (Julai 22, mwaka huu), kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Kajala alitupia picha za sherehe yake ya kuzaliwa aliyoifanyia nchini China katika Mgahawa wa Waitaly uliyopo Guahnzu.

Chanzo kilichokuwepo katika sherehe hiyo kilisema, Kajala aliwaalika marafiki zake kibao wa nchini humo akiwemo mpenzi wake wa zamani, Petty Man ambapo walikula na kunywa kwa bili yake kitu ambacho wengi walihoji kuhusiana na alikozipata fedha hizo.

“Mh! Si bure kuna kitu, kufanya sherehe katika nchi za watu kama hivi si kitu kidogo lazima uwe na fedha za maana sasa hatujui mwenzetu ameitoa wapi hii jeuri,” alihoji mualikwa mmoja kupitia mitandao ya kijamii.

Kama hiyo haitoshi, shuhuda mwingine aliyechati na mwanahabari wetu alikwenda mbali zaidi kwa kuhoji juu ya kazi zake na pato analoingiza kupitia sinema.

“Nimefuatilia tangu alipoanza kuzitumbua fedha akiwa Bongo hadi huku China, sidhani kama fedha za sinema zinaweza kumpa jeuri hii, kutakuwa na mtu nyuma yake tu,” alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka kuchorwa jina gazetini.
GPL

Jokate Mwegelo Asaka Mwanaume wa Kumuoa

$
0
0
Katika kuonyesha amechoshwa na upweke, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameibuka na kusema kuwa sasa anasaka mwanaume wa kumuoa huku akitaja vigezo vya anayestahili kumuita mume.

Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Jokate alisema kuwa hana ‘mtu’ ila atakapotokea mwenye vigezo anavyotaka, hatakuwa na sababu ya kumkataa. “Kwa sasa sina mpenzi wala mchumba, akitokea sina kipingamizi ila mbali na vigezo vingine awe na mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Jokate.

Jokate amekuwa msiri sana katika maisha yake ya kimapenzi kiasi cha wengi kuamini ni msichana anayejiheshimu sana ila aliwahi kuwa na uhusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu, Hasheem Thabeet anayekipiga kwenye Timu ya Oklahoma City Thunder ya nchini Marekani.

Mchakato wa Ujenzi Barabara za Juu ‘flyover’ Tazara Waanza

$
0
0
Tatizo la foleni katika jiji la Dar es Salaam, limeanza kupatiwa dawa baada ya Serikali ya Tanzania na Japan kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu (flyover) katika makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere.

Akizungumza baada ya kutiliana saini, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk Servacius Likwelile alisema Japan imeiongezea Tanzania Sh5.64 bilioni, baada ya kiasi cha Sh52.55 bilioni kilichotolewa Juni 18, 2013 kutofikia kiwango kinachotakiwa na makandarasi kwa ajili ya ujenzi wa njia hiyo ya juu.

Sambamba na mradi huo, pia nchi hizo zimetiliana saini mkataba mwingine wa kuboresha usambazaji wa umeme katika jiji la Dar es Salaam kwa kujenga vituo vidogo katika maeneo ya Mwananyamala, Muhimbili na Jangwani Beach.

Miradi hiyo itakayogharimu jumla ya Sh77.5 bilioni na inafadhiliwa na Serikali ya Japan, chini ya Shirika la Maendeleo la Japan (Jica).

“Kama mnavyojua, barabara na nishati ndiyo nguzo katika ukuaji wa uchumi. Msaada huu utatuwezesha kuongeza kasi katika kuimarisha uwekezaji katika sekta ya hizi. Pia, zitachochea maendeleo katika maeneo mengine,” alisema na kuongeza kuwa kiasi kingine cha Sh71.9 bilioni kimetolewa kwa ajili ya kusaidia usambazaji wa umeme jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza na kukwamisha shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Kuhusu barabara hiyo, Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada alisema Serikali yake imeongeza fedha ili kukabiliana na upungufu wa bajeti uliosababishwa na kushuka kwa thamani ya fedha pamoja na ongezeko la bei ya vifaa vya ujenzi.

Alisema mkataba na mkandarasi unatazamiwa kutiwa saini Septemba mwaka huu na ujenzi wa barabara hiyo utaanza muda mfupi baadaye.

Mwakilishi Jica nchini, Yasunori Onishi alisema sekta ya usafirishaji ni moja ya shughuli kubwa wanazozifanya nchini ili kuleta maendeleo.

Alisema shirika lake limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam kwa miaka 30 sasa, ikiwamo ujenzi wa Daraja la Salenda ulioanza mwaka 1980. “Jica pia tulisaidia kuundwa kwa mpango mkuu wa sera na mfumo wa usafirishaji katika jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 na 2008. Hata hivyo, katika utafiti wetu, tulipendekeza kipaumbele kielekezwe katika makutano ya Tazara,” alisema Onishi.

Alisema mradi wa ujenzi wa barabara ya juu eneo hilo la Tazara, unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya watu milioni mbili wanaofanya safari zao kila siku kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwenda katikati ya jiji. Pia alisema barabara hiyo itapunguza kwa asilimia 30, muda unaotumika kusafiri katika umbali huo kutoka dakika 37 hadi dakika 25.

“Tumejipanga kikamilifu kutekeleza maazimio tuliyosaini leo. Naiomba Serikali pia itimize wajibu wake katika kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa zinatumika katika mambo yaliyokusudiwa,” alisema.

Onishi alisema Jica ina dhamira ya dhati kuisaidia Serikali ikiwamo upanuzi wa Barabara ya Bagamoyo (Mwenge - Tegeta) ambayo ujenzi wake utakamilika mwisho wa mwezi huu.

Wanaume Mnao Jisifia Mnajua Mambo Sita kwa Sita Mnaboa Wengi Si lolote..One Minute Man

$
0
0
Umekutana na Jamaa very Handsome...Very Smart..Kajazia misuli UKAMTAMANI...Yaani kila ukimwangalia Pichu inajaa udambwidambwi...Unampatia Picha Ukimpa Mzigo jinsi atakavyoimanua vizuri...SIKU YA SIKU UMEJIANDAA UMEMPA SHOO....Jamaa yuko bize anapiga mikelele ya shangwe kuita wazungu wakati wewe wala huoni anachofanya and ur wondering,"WHAT IS THIS NIGGA DOING ON TOP OF ME"
Imewahi kukutokea???
Halafu MBAYA ZAIDI baada ya kukuru kakara zisizo na faida yoyote kwako na kupakwa shombo la maana na kuwa disappointed jamaa linashuka na kukuuliza
"BABE HOW WAS IT"..Teh teh,Hapa wanaume tunapewaga jibu la kisiasa tu IT WAS FINE...halafu ananyanyua gagulo lake anaenda bafuni akirudi utasikia
"I think we should go,Nimekuta Missed call za Mum"
HUPEWI TENAAAAAA....Wanaume ukiona umepewa mara 1 ukiomba tena unazungushwa kama unafuatilia TIN NUMBER ofisi ya TRA ujue ULIFELI DAY 1...Akupe tena ili iweje??
UKIPEWA PAKUA HASWA..Ukishuka mtu alale kama masaa2 hivi ndo akumbuke kuna mama home...Sio mtu unashuka nae anabeba taulo..HUJAFANYA KITU BLOO!
poooooooo imejipost

Hii Picha ya Shilole ni Shidaaa Kama "RIHHANA"

$
0
0
Picha ya mwanamuziki wa nyimbo za mduara nchini, shilole mohamed aka SHISHI BABY iliyozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kama Insta na kuwaacha mashabiki midomo wazi wakijiuliza kama huyu ni shilole wa igunga au rihhana ,kutokana na muonekane wake HOT n SEXY kama binti Wa chuo.

Dida Afunguka, Simu Ndio Chanzo Cha Kuachana na Ezden, 'Alinichapa Mikanda', Azungumzia Mpango wa Ndoa Nyingine

$
0
0
Dida Shaibu, mtangazaji wa kipindi cha Mitikisiko ya Pwani amefunguka Exclusively kupitia Sunrise ya 100.5 Times Fm  inayoongozwa na Fadhili Haule na kueleza chanzo cha ndoa yake  na Ezden ‘The Rocker’ Jumanne kuvunjika. Ndoa iliyodumu kwa muda wa mwaka mmoja tu.

Dida ameeleza kuwa mzizi wa tatizo lililopelekea ugomvi mkubwa kati yao ni simu ya mkononi ya mumewe huyo wa wazamani baada ya kutaka kuitumia kucheza game na kugundua kuwa imewekewa password kwa mara ya kwanza katika uhusiano wao.

 “Tatizo kubwa la ugomvi wangu na X-Husband, tatizo kubwa lilikuwa ni simu. Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatano tumetoka kazini. Tukawa tuko kawaida, unajua sisi huwa tunataniana sana. Kwa hiyo aliacha simu yake kitandani, unajua mimi huwa nacheza game kupitia simu yake. Kwa hiyo mimi nikachukua simu yake nikakuta ameweka password kitu ambacho sio cha kawaida. Kwa hiyo mimi ikabidi nimuulize…nikamuita, tulikuwa tunaitana ‘mshikaji wangu mshikaji wangu’. Kwa hiyo alikuwa yuko bafuni anaoga, kwa sababu nyumba ni self-contained, kwa hiyo nikawa namwambia ‘duh mshikaji wangu mbona umeweka password?’ yaani kama utani tu, akaniamba ‘aah we iache simu yangu’.” Dida ameiambia Sunrise ya Times Fm

Amesema Ezden alishikilia msimamo wake kutomuonesha password kitu ambacho kilimpa hisia na wasiwasi kuwa huenda jamaa anamsaliti (anamichepuko) ameficha kupitia simu hiyo na kuanza kuongeza nguvu ya kuomba apewe password ili aondoe wasiwawasi wake lakini hakufaulu zoezi hilo.

Ameiambia Sunrise ya 100.5 Times Fm kuwa kitu kilichomfanya afikirie kuwa ameonewa kwa kunyimwa password ni uhuru aliokuwa nao mumewe huyo wa zamani kupitia application za kidijitali.

Amesema Ezden alikuwa na uwezo wa kuona kila kinachofanyika kwenye simu ya Dida hata  kupata jumbe zinazoenda kwenye simu ya Dida kabla mwenyewe hajazipata

“Simu yangu anauwezo wa kushika akakaa nayo, simu yangu anaweza kushika akadownload vitu vya kuweza kufatilia Dida anaenda wapi, Dida anafanya nini. Messages zangu za WhatsApp alikuwa anaweza kupata yeye kabla yangu mimi. Na kingine kikubwa ni kwamba alikuwa anaweza kudownload maongezi ambayo naongea na watu. Lakini hajawahi kukuta maongezi mabaya na watu….Nikiwa Kawe simu yake inamuonesha kuwa Dida yuko Kawe.” Ameeleza.

Hata hivyo, ametaja kuwa wasiwasi wa mumewe huyo wa zamani na mabadiliko yake katika matumizi ya simu yalitokana na ujumbe ambao alikuwa ametumiwa na mwanaume ambaye kwake yeye ni mteja.

Lakini ujumbe huo haukueleweka vizuri kwa sababu kuna kitu anadhani kilimiss kwenye ujumbe huo kilichosababisha ieleweke tofauti (Kama mtu anaechepuka nae).

Ameeleza kuwa alipoendelea kuomba zaidi password na hali ya kutoelewana kuongezeka akajikuta akipigwa vibao na hapo mambo yakazidi kuwa mabaya kwenye uhusiano huo.

“Alinipiga kibao, sio kibao tu, Vibao vya uhakika….baada ya kupigwa mimi nilishikwa na hasira kwa sababu alinipiga na baadae akaona kibao hakitoshi. Akachukua mkanda, mkanda huu wenu wa suruali lakini ulikuwa mzito akawa ananichapa nao ‘kwa nini unataka kupishika vitu vyangu’.

Anasema kutokana na kipigo hicho aliumia kichwani na kuelekea hospitali, lakini aliporudi nyumbani alikuta mwenzake ameshachukua vitu vyote alivyokuwa anavimiliki (alivyoenda navyo).

Alipoulizwa nani alimuacha mwenzake:

“Sitaki kusema nani kamuacha mwenzake kwa sababu mimi ndiye niliomba divorce. Katika maisha ya mwanadamu wanasema mwanamke hauwezi kumuacha mwanaume ila mwanaume anaweza kumuacha mwanamke. Lakini mimi nahisi kama tumeachana.”

Katika hatua nyingine, Dida aliulizwa kuhusu mpango wake wa baadae katika uhusiano wake kama ana mpango wa kuolewa tena.  Alisema hana mpango huo kwa sasa.

“Kwa sasa sina mpango wowote wa kuhusiana na suala la ndoa. Yaani sina na sitegemei. Na kama kuna mtu anafikiria kwa sababu napata maombi mengi sana. Washindwe na walegee. Kwamba labda naweza kusema mwenyezi Mungu amenijalia kuwa nabahati hiyo…Sio kupendwa yaani tuseme, unajua binadamu anakupenda mwingine anakujaribu. Sasa hivi watanifuata wanaume wengi sana kila mmoja atakuja kwa sampuli anayoijua yeye. Huyu atajifanya yeye ndiye ana mahaba kuliko Yule. Mwingine anasema ‘atapigaje mwanaume?’ kumbe yeye ndiye mdundindaji kwelikweli kuliko hata yule.

“Sitaki kuja kujutia maisha yangu, sitaki kuja kujutia maamuzi yangu. Huwa nafanya kitu kwa kuangalia mbele zaidi. Mimi nina biashara zangu, nina maisha yangu. Namshukuru Mungu amenijalia mtoto mmoja. Kwa hiyo nahitaji mtoto wangu awe na maadili fulani hivi ambayo ya kusema kwamba huyu ni mama..nahitaji kumsomesha, nahitaji awe hivi. Lakini sitaki mwanangu asipate matatizo haya ambayo labda mama yake nimepitia. Lakini hii yote nasema ni ujasiri. Nasema Mwenyezi Mungu labda ananionesha njia.”
Source:Times FM

Sikiliza Habari Kuhusu Barnaba Kutoka Kimapenzi na House Girl wa Wema Sepetu

$
0
0
July 25 Barnaba ametangaza kuwa ndiyo siku atakayotoa video yake ya Wahaladee ambayo imetengezwa kwenye ardhi mbili ya Tanzania na Kenya,Soudy Brown leo kaongea nae kuhusu msichana anayesemekana mpenzi wake kusimamishwa kazi alikokuwa anafanya kazi nyumbani kwa Wema Sepetu.

Bonyeza Kusikiliza:

Nyimbo ya 'Mdogomdogo' ya Diamond ni Advanced Version ya "Aye" ya Davido!

$
0
0

Japo nyimbo hz mbili zna maana tofauti,lakin zote zmepgwa kwa maadhi ya kiasili pia idea ya matukio na story ya video hz mbili ni ile ile!sema mkali diamond ktk sehemu ya familia ya mfalme ametupia wazungu,lakn mwisho wa siku wote waliopoa mabint wa kifalme na kuwachezesha midundiko ya kiasili!chukua hyo......!tazama vdeo zote mbili vzur ndo uje kuanza kubisha! tunakopy kidigital siku hizi,chezea diamond wewe!
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images