Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Vanessa Mdee, Jux Wafanya Kufuru Harusi ya Shilole Wamwaga Minoti

0
0

COUPLE ya wakali wa Bongo Fleva, Juma Jux na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru baada ya kugawa minoti kwenye harusi, Shilole na Uchebe iliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam.




Katika harusi hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Couple ya Jux na Vanessa walipata fursa ya kutoa nasaha na kumpongeza Shilole kwa kufunga ndoa pia wakimpongeza Uchebe kwa kumpata mke aliye bora.

Kwa upande wa Jux alisema zawadi kubwa anayoitoa kwa Shilole ni kumsomesha mtoto wake mmoja kwa mwaka mmoja huku Vee Money akisema atamlipia muimbaji huyo kulala katika Hotel ya Nyota Tano ya Kilimanjaro.

Baada ya hapo, Jux alichana pochi na kumkabidhi Vanessa mkwanja ambapo aliwavagaa maharusi na kuanza kuwarushia pesa hizo kama zawadi.

Kakobe Aeleza A-Z Alivyohojiwa na TRA

0
0
Kakobe Aeleza A-Z Alivyohojiwa na TRA
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amewaelezea waumini wake jinsi alivyohojiwa na timu mbili zilizoundwa kwa nyakati tofauti na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Askofu Kakobe, ambaye ameingia kwenye mgogoro na mamlaka za nchi tangu aeleze kuwa ana utajiri mkubwa, alisema hayo wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisa lake lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya pili kuzungumzia sakata hilo kwa waumini wake tangu Desemba 31 mwaka jana.

Hata hivyo, Kakobe alisema kutoa mrejesho huo hakuwazuii TRA kueleza waliyobaini, lakini amesema ameona azungumze mapema na waumini wake kwa kuwa ndio watoa sadaka na wana haki kwa asilimia 100 kujua kinachoendelea kanisani kwao.

“Baada ya kuleta barua, Januari 2, kiongozi wa tume iliyoundwa awali na kikosi chake walifika na tuliwapa ushirikiano. Nilikuwa nao katika ofisi ya kiuchungaji kwa mahojiano, walikuwa na karatasi za maswali na majibu waliyaandika,” alisema.



“Waliuliza kuhusu utajiri wangu, niliwaambia nina nyumba moja tu duniani ipo Kijitonyama niliijenga kwa gharama ya Sh2 milioni na kiwanja nilinunua Sh30,000. Ni nyumba ya kawaida na ipo katika mtaa wa kawaida uitwao kwa Kakobe. Utafuteni mtaiona nyumba yangu.”



Askofu Kakobe alisema aliwaeleza wazi kuwa ana waumini wake ambao hawakuridhishwa na anapoishi, hivyo walitamani awe na sehemu nzuri itakayoweza kufaa kwa ajili ya wageni wa kimataifa wanaoweza kuwatembelea. Alisema walimshirikisha hilo na walijenga eneo jingine kwa michango yao miaka 10 iliyopita.



Alisema suala la akaunti za kanisa aliliweka wazi na kuwaambia kuwa kuna akaunti benki ya NBC na akaunti ya mfuko wa kitaifa wa FGBF iliyopo pia NBC Meru, Arusha.



“Niliwaambia wazi mimi wala mke wangu hatuna akaunti benki. Binafsi sina mradi wowote, sina shamba, sina kuku hata mmoja, paka na wala panya niliyefuga. Niliwaambia hata kanisa hatuna mradi wowote wa kiuchumi na hivi ndivyo tunavyoishi,” alisema.



“Mmoja akaniuliza kwa nini hamna mradi wa kiuchumi, nilimweleza huo ni wito wetu. Wakatoa karatasi moja ya kumbukumbu za TRA wakasema kuna shule moja inaitwa Full Gospel si yenu? Nikasema hatuijui ila ni neno ambalo linatumika kote duniani. Mkifuatilia vizuri mtajua wenye shule ni ya kina nani.”



Alisema walimuuliza iwapo ameajiri watu kanisani, akasema kuna watumishi zaidi ya 1,000 ambao hawalipwi wanafanya kazi ya Mungu na huo ndiyo mfumo wa kanisa.



Alisema walimuuliza kuhusu ukusanyaji wa sadaka, maisha yake bila ya kuwa na mradi wowote na baadaye waliitwa wakusanyaji sadaka kwa mahojiano zaidi.



“Wakauliza kutoka kwa hicho kikosi ‘bahasha za maombi maalumu ambazo huelekezwa kwa mchungaji zinakuwa nzito sana’, wakasema zinakuwa za kawaida tu. Wakaniambia kwa uzoefu wako kiasi gani huwa kinapatikana kwa mwezi, nikawaambia hufika hata Sh5 milioni lakini wakati mwingine kinaweza kwenda chini.”



Alisema baada ya hapo walihojiwa watoto na mke wake na kijana wake mmoja na majibu yakawa yaleyale. Alisema walichukua baadhi ya kompyuta na nyaraka muhimu kwa ajili ya uchunguzi na baadaye walitoa maoni yao.



“Kilichofuatia ndicho kilichonifanya nitoe mrejesho kabla ya TRA. Yule kiongozi niliyekabidhiwa na TRA alitoa ripoti inayoonyesha sina miradi wala vyanzo vya fedha, kinachosalia ni sadaka na wao hawahusiki nazo,” alisema Kakobe.



“Baada ya kiongozi huyo kutoa ripoti hiyo, aliondolewa katika hiyo kazi na hivi tunavyozungumza amepelekwa mkoani. Nikasema sasa nitamwaga mboga leo, nikasema hapa kuna hila, nitaitungua ndege kabla haijapaa.”



Askofu Kakobe alisema baada ya kiongozi huyo kutimuliwa ameletwa kiongozi mwingine na kazi imeanza upya, “Wamekwenda nyumbani kwangu wamekagua chumba kwa chumba, vyumba vyote nguo za wanangu, mke wangu; wanachambua nguo mojamoja yaani wanasagula kama mtumbani. Wamekuja ofisini hivyohivyo. Wameenda kwa viongozi wangu wamefanya hivyohivyo,” alisema.



Alisema wamehoji wapi anapeleka fedha na kuwapa mrejesho kuhusu safari zake za ndani na nje ya nchi lakini hawajaridhika.



“TRA sasa ipo ndani ya sadaka. Hii ni TRA kweli? au kuna jambo? Mimi leo nimemwaga mboga, hata (Askofu Josephat) Gwajima aliwahi kutoa mrejesho. Sasa Gwajima na Kakobe ni mapacha. Walikuja ofisini wanakagua chumba kimoja mara kingine nikasema watumishi tuwe macho wasijekutuwekea bangi,” alisema.



Aidha katika hatua nyingine, Askofu Kakobe aliwataka watumishi wa TRA kufuata utaratibu na ikiwa wataanza kukusanya sadaka basi wakusanye makanisa yote.



Alitoa onyo kwa watumishi hao na kusema wanamchonganisha Rais John Magufuli na wananchi wake kwa kuwa haamini kama wametumwa.



“Ninavyomjua Rais John Magufuli ana hofu ya Mungu. Nalikumbuka neno lake la ‘mniombee nisiwe na kiburi’ na sijayasahau. Leo kama anatuma TRA wachunguze sadaka sina imani hiyo. Tunajua kuna watu siku hizi wanatafuta kiki, wanatafuta kupanda vyeo, nakushauri Rais wanaotafuta vyeo kwa staili hii wageukie na uwatumbue,” alisema.

Kampuni ya mavazi, H&M Yafunga Maduka Yake Afrika Kusini

0
0
Kampuni ya mavazi, H&M Yafunga Maduka Yake Afrika Kusini
Kampuni ya mavazi, H&M imelazimika kufunga maduka yake kwa muda nchini Afrika Kusini baada ya kutokea uharibifu.
Hatua ya kufunga maduka hayo imekuja baada ya kundi la Economic Freedom Fighters (EFF) kuyalenga maduka takribani sita na kuyaharibu ikiwemo na bidhaa zake.

H&M wameachia taarifa ya kufunga maduka hayo kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Twitter, na kuelezea kuwa hatua hiyo imefanywa ili kulinda usalama wa wafanyakazi na wateja wao.



Wiki moja iliyopita kampuni hiyo ilichapisha T-Shirt iliyovaliwa na kijana mwenye asili ya Afrika na kuandikwa “Coolest monkey in the jungle”, kitendo hicho limetafrisiwa kuwa cha kibaguzi kwa watu weusi na kupelekea watu mbalimbali kulaani kampuni hiyo kwa kufanya kitendo hicho.

Ujenzi wa Barabara ya Njia sita Kuanzia Kimara Hadi Kiluvya Kuanza February

0
0
Ujenzi wa Barabara ya Njia sita Kuanzia Kimara Hadi Kiluvya Kuanza February
Ujenzi wa barabara ya njia sita kuanzia Kimara hadi Kiluvya, unatarajia kuanza mwezi ujao pindi mkandarasi atakapopatikana.

Nyumba takribani 2,000 zilizokuwa zimejengwa ndani ya mita 121.5 ya Barabara ya Morogoro zilibomolewa ili kupisha ujenzi huo ikiwa ni hatua ya awali ya utekelezaji.

Kazi ya ubomoaji iliacha vilio kwa wakazi wa maeneo ya Kimara hadi Kiluvya huku nyumba za kifahari zikiwamo za viongozi wa Serikali na wanasiasa maarufu akiwamo Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa J na nyumba ya mke wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa iliyopo Kibanda cha Mkaa Mbezi, zikibomolewa.

Ubomoaji huo pia, ulizikumba nyumba za ibada 32, vituo vya afya vitano, vituo vya mafuta sita majengo ya Serikali manne pamoja na Shule ya Msingi Kimara ambayo ilibomolewa nusu.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake juzi, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamkama alisema kazi ya ubomoaji wa nyumba zilizokuwa zimejengwa ndani ya hifadhi hiyo ya barabara imekamilika, hivyo kinachofuata ni maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo.

“Tumekamilisha ubomoaji, tunachofanya sasa tupo kwenye hatua ya awali ya kumtafuta mkandarasi ambaye tunatarajia hadi kufikia mwisho wa wiki hii, tuwe tumekamilisha hatua ya awali,” alisema Ndyamkama.

Alifafanua kuwa baada ya hatua hiyo, wanategemea mwezi ujao wawe wamempata mkandarasi na kumkabidhi kazi ya ujenzi.

Ndyamkama pia alisema kwa upande wa majengo ya Serikali likiwamo jengo la Tanesco, bado wanaendelea na ubomoaji lakini kuna baadhi ya nyumba chache za wananchi maeneo ya Kibo wanaendelea kubomoa wenyewe.

“Kwa sasa hatumshinikizi mtu kubomoa, wanabomoa wenyewe, maana asilimia kubwa ya ubomoaji imekamilika tunachofanya ni maandalizi tu ya kuanza ujenzi rasmi,” alisema.

Alifafanua kuwa ujenzi huo ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo imekuwa kero ya muda mrefu.   

Simba Mbioni Kumwajiri Kocha wa TP Mazembe

0
0
Simba Mbioni Kufikia Makubaliano ya Kumwajiri Kocha wa TP Mazembe
Tetesi kubwa kwenye soka hapa nchini zinazoendelea kusambaa ni zile zinazohusu klabu ya soka ya Simba kukaribia kufikia makubaliano ya kumwajiri kocha wa zamani wa TP Mazembe Hubert Velud.


Simba ambayo haina kocha mkuu kwa takribani wiki tatu tangu iachane na aliyekuwa kocha wake mkuu Joseph Omog, inadaiwa ipo kwenye maongezi na kocha huyo raia wa Ufaransa mwenye historia kubwa kwenye soka la Afrika.

Velud mwenye umri wa miaka 58, anatambulika vyema kwa mafanikio aliyowahi kuyapata nchini Algeria alipotwaa ubingwa wa ligi nchini humo kwa misimu tofuati akiwa na vilabu vya ES Setif mwaka 2013, 2014 akiwa na USM Alger na Super Cup ya Algeria mwaka 2013 akiwa na USM Alger.

Tayari inadaiwa kocha huyo ambaye msimu wa 2015/16 alikuwa anaiongoza TP Mazembe yupo jijini Dar es salaam na kama maongezi yataenda vyema atatangazwa kuanza kibarua ndani ya vinara hao wa ligi kuu VPL.

Akiwa kocha wa Togo, Velud anakumbukwa kwa tukio la kupigwa risasi kwenye mkono, wakati basi la wachezaji wa timu ya taifa ya Togo liliposhambuliwa na waasi nchini Angola wakati wanakwenda kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010.

Korea Kaskazini na Kusini Zaanza Mazungumzo Kuhusu Olimpiki

0
0
Korea Kaskazini na Kusini Zaanza Mazungumzo Kuhusu Olimpiki
Korea Kaskazini na Kusini wameanza mazungumzo kuhusu mpango wa kutuma timu kwa mashinndano ya msimu wa baridi yanayofanyika mwezi ujao nchini Korea Kusini.

Korea Kaskazini ilikubali wiki iliyopita kutuma ujumbe kwenda kwa mashindano hayo, na kupunguza msuko suko kati ya majirani hao wawili kutokana na mpango wake wa nyuklia.

Korea Kusini kisha ikapendekeza kufanyika mazungumzo makubwa Jumatatu kuhusi kushiriki kwa Korea Kaskazini.

Lakini Korea Kaskazini badala yake ikapendekeza kuhudhuria kwa kikosi chake cha sanaa katika mashindano hayo.

Korea Kusini imekuwa ikitaka Korea Kaskazini kushirikishwa kwenye mashindano hayo yaliyopewa jina olimpiki ya amani ikisema kuwa ni fursa ya kuboresha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Pande hizo mbili zinakutana eneo linalolindwa kati ya mataifa hayo la Panmunjom ambalo pia linafahamika kama truce village.

Wajumbe wawili kutoka kila upande walitarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo.

Wiki iliyopita wakati wa mazungumzo ya juu kati ya nchi mbili katika kipindi cha zaidi ya miaka mwilia, Korea Kaskazini ilisema kuwa itatuma wanariodha na mashabiki kwenda kwa mashindano hayo ya olimpiki ambayo yatafanyika kati ya tarehe 9 na 25 mwezi Februari mjini Pyeongchang.

Jux Ajitolea Kumsomesha Mtoto Mmoja wa Shilole

0
0
Jux Ajitolea Kumsomesha Mtoto Mmoja wa Shilole
Msanii wa viwango kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Juma Jux amejitolea kumsaidia msanii 'Shilole Baby' majukumu ya kumsomesha  mtoto wake mmoja kwa mwaka mzima ikiwa kama zawadi yake ya siku ya sherehe ya harusi iliyofanyika jana Jijini Dar es salaam.


Akizungumza jana katika sherehe Shilole na mume wake Uchebe, Jux amesema kwamba anafahamu kuwa mwanamke huyo ni mpiganaji na huwa hachoki kupambana katika kutafuta riziki yake mwenyewe na si tegemezi kwa mtu.

Akizidi kutoa sifa kwa Shilole kabla ya zawadi Jux amesema kwamba licha ya kuwa Shilole ni msanii mwenzake lakini pia wao ni marafiki ambao wanashauriana na kutaniana mambo mengi lakini pia anatambua kuwa ana mzigo wa majukumu ya kifamilia.

"Shilole ni mpambanaji sana sana. Ni mwanamke ambaye anaamini kwenye kutafuta kipato chake mwenyewe na siyo kupewa. Kwa kulitambua hilo nataka nimpunguzie mzigo kidogo dada yangu, Nitagharamia ada ya mtoto wake mmoja pamoja na mahitaji mengine kwa mwaka mmoja. Naamini nikifanya hivyo nitakuwa nimemsaidia yeye kuweza kusonga mbele katika mapambano mengine" amesema Jux.

Jana maeneo ya Masaki Shilole alifanya Sherehe ya harusi yake ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao wa filamu na muziki. Shilole alifunga ndoa ya kimya kimya  na mumewe Ashraf 'Uchebe' Mwanzoni mwa mwezi Disemba na jana ndiyo siku waliyoamua kufanya sherehe.

Bill Nass Awakana Wanawake Ma-superstar " Sijawahi Kuwa na Mahusiano na Mtu Yeyote Maarufu"

0
0
Bill Nass Awakana Wanawake Ma-superstar " Sijawahi Kuwa na Mahusiano na Mtu Yeyote Maarufu"
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bill Nass, amekanusha kuwahi kuwa kwenye mahusiano na wasanii wa kike wa hapa bongo, na kusema hajwahi kabisa kuwa nao.


Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Bill Nass amesema ana mahusiano yake na mpenzi wake wa muda mrefu, na ndiye anayemfanya asifikirie kuanzisha mahusiano na mtu yeyote hata kama ni msanii.

Bill Nass ameeendelea kwa kusema kwamba hata ikitokea amekorofishana na mpenzi wake huyo, mara nyingi hukaa mwenyewe na mpaka pale watakapomaliza tofauti zao.

"Sijawahi kuwa na mahusiano na msanii yeyote, iwe wa kuimba, wa kuigiza, presenter au kuwa na mahusiano na mtu yeyote ambaye ni celebrity, mtu ambaye nina mahusiano naye ni mtu ambaye nipo naye tangu tupo diploma, na mara nyingine tukiwa tunagombana nakuwa single tu , lakini mtu ambaye nipo naye nipo naye huyo huyo na si mwengine”, amesema Bill Nass.

Hivi karibuni msanii huyo aliwahi kukumbwa na skendo ya kuwa kwenye mahusiano na msanii wa kike Nandy  ambaye kwa sasa anafanya vizri zaidi kwenye game.

“Usimdharau Pengine Kesho Yake Ikawa Ndio Usalama Wako”- Dogo Janja

0
0
“Usimdharau Pengine Kesho Yake Ikawa Ndio Usalama Wako”- Dogo Janja
Mwezi mmoja umepita tokea Papii Kocha na baba yake Babu Seya waachiwe huru na kuona wakifanya baadhi ya shows na ngoma zao pendwa za zamani ingawa wameonekana studio wakiandaa kazi zao mpya ambazo bado hazijatoka.



Maswali yamekuwa mengi kwa baadhi ya mashabiki baada ya Dogo Janja kupost picha akiwa na Babu Seya pamoja na wanae na kuandika caption inayosema “Haijalishi mtu ana hali gani leo usimdharau pengine kesho yake ikawa ndio usalama wako…. #BabuSeya #PapiiKocha”

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.


NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.


MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA.


MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.


NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,


Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605


DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale

Godbless Lema: Afrika Kuna Matendo ya Kibaguzi ya sisi Kwa sisi Kuliko Matamshi ya Donald

0
0

Godbless E.J. Lema

"Africa inapiga kelele dhidi ya matamshi ya ubaguzi ya Donald Trump. Africa kuna matendo ya kibaguzi kuliko matamshi ya Donald Trump na ni sisi kwa sisi,unapotumia nguvu ya dola kuuwa demokrasia na haki,unapotumia nguvu kutesa na kuua wanao kukosoa, huu sio ubaguzi ? Tutafakari" Godbless Lema

Mwanaume Ajiua Kisa Penzi la Mkewe na Mchepuko..Aacha Ujumbe Huu Hapa

0
0

Ujumbe wa Yona Kabla ya kifo chake....

"Nimekuwa kwenye matatizo ya ndoa kwa miaka 4, kila wiki nikipambana na mke mlevi na mzinzi.
Tukio la jana usiku na leo asubuhi limenisononesha na kunitia simanzi kubwa. Nimekata tamaa ya kila kitu na kila jambo nangoja mapenzi ya Mungu tu. Nalazimika kutumia dawa za usingizi lakini wapi. Sasa nipumzike nimwache mke wangu Eng Mloelya na mchepuko wake Eng Lossy wa Idara ya Maji Mbeya waendee!" Yona

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

Wasiliana nasi +255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

RC Makonda Aingilia Kati Mgogoro wa Nyumba ya Mjane Ataka Isipigwe Mnada

0
0
RC Makonda Aingilia Kati Mgogoro wa Nyumba ya Mjane Ataka Isipigwe Mnada
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza mjane Bernadetha Ryewendera mkazi wa Tegeta Mtaa wa Upendo asibughudhiwe, aachwe aendelee kuishi kwenye nyumba yake ambayo ilipigwa mnada kinyume cha sheria bila yeye kuwa na taarifa rasmi.

Hayo yamejiri leo Jumatatu, Januari 15, kufuatia video ya mama huyo kusambaa mitandaoni ikimuonyesha akilalamikia baada ya nyumba yake kupigwa mnada, ambapo Makonda aliagiza mama huyo atafutwe na afike ofisini kwake leo saa tatu asubuhi jambo ambalo mama huyo ameliekeleza.

Mjane huyo ambaye anadai nyumba yake ilipigwa mnada January 12 mwaka huu kwa dakika tano bila yeye kupewa taarifa yoyote, amefika ofisini kwa Makonda leo ambapo baada ya kupitia nyaraka zake, RC Makonda ameagiza kusimamisha mnada wa nyumba hiyo aliouita ni batili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda amesema kuwa katika uchunguzi wa awali uliofanywa na wanasheria umeonyesha kuna utapeli mkubwa uliofanywa ambapo nyaraka zimegushiwa sahihi ya Bi Zainabu Kaswaka ambaye ni mmiliki wa eneo alilouziwa Bi Rweyendera. Imeelezwa pia kuwa nyumba iliyopigwa mnada ilikuwa na zuio mahakamani tangu mwaka jana.

Aidha Makonda ameagiza watuhumiwa wa utapeli huo kukamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria mara moja.

NIDA Yaanza Zoezi la Kuweka Pingamizi kwa Waliojiandikisha Vitambulisho vya Taifa

0
0
NIDA Yaanza Zoezi la Kuweka Pingamizi kwa Waliojiandikisha Vitambulisho vya Taifa
January 15, 2018 zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea kufanyika Mkoani wa Songwe ambapo wananchi wameonyesha mwamko wa kujitokeza kukamilisha jukumu lao la msingi la kujisajili ili kupata Vitambulisho ukiachia mbali mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani humo.

Afisa usajili wa Songwe Coletha Peter amesema kwasasa wanaendelea na Usajili katika Wilaya ya Mbozi na wako kwenye awamu ya 5 wanayotegemea kumaliza January 20, 2018.

Amesema baada ya kukamilika kwa awamu ya 5 wataingia katika awamu ya 6 itakayohusisha kata ya Nambizo, Magamba, Nanyala na Ruanda na kuwasititiza Wananchi wa kata zilizo katika awamu ya 6 kujiandaa kwa zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa Viambatanisho vya msingi vinavyohitajika katika zoezi la Usajili na Utambuzi.

Katika mkoa wa Songwe Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la mapingamizi ambapo wananchi wanapata fursa ya kuhakiki taarifa zao pamoja na kuweka mapingamizi kwa mtu yoyote wanayehisi si raia au si Mkazi wa eneo husika na amefanya usajili wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa, ambapo Coletha amewasihi Wananchi wa kata Ichenjezya, Vwawa na Mlowo ambazo ndo zimeanza zoezi hilo, kuwa wazalendo katika kufanikisha zoezi hilo.

Dk Mashinji Aeleza Tofauti Yake na Dk Slaa

0
0
Dk Mashinji Aeleza Tofauti Yake na Dk Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amezungumzia madai ya kupwaya katika nafasi hiyo, akibainisha kuwa kila kiongozi ana mikakati yake katika utendaji wa kazi.

Akizungumza leo Januari 15, 2018 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds, Mashinji amesema wapo wanaodai amepooza, mkimya na hana mikiki mikiki kama viongozi waliomtangulia walioshika nafasi hiyo.

Akitaja baadhi ya majukumu ambayo kwa sasa yanamtofautisha na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema, “Dk Slaa ilikuwa akizunguka mikoani, kuendesha mikutano, maandamano na harakati za matukio.

Katika uongozi wangu ninajenga  kanda za chama, kujenga uwezo wa chama ngazi za misingi(vitongoji).”

Amesema majukumu ya Katibu mkuu kwa sasa yamejikita katika utendaji wa kuimarisha mfumo, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa agenda ya chama hicho isemayo ‘Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli katika ujenzi wa Uchumi’.

“Sasa ukichanganya majukumu yangu na yale aliyokuwa akiyafanya Dk Slaa unaweza kuharibu mipango ya ujenzi wa kitaasisi. Watu  wanashindwa kuelewa hiyo tofauti, wanafikiria mfumo wa utendaji ni kama zamani,” amesema na kuongeza,

“Siyo kazi ndogo kujikita katika ujenzi wa kanda zetu inayotuelekeza kwenye Federal Government.”

Hata hivyo, amesema pamoja na mabadiliko hayo mazingira ya siasa kwa sasa nchini yamebadilika kutokana na hali ya ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na Serikali.

Amesema wakati Bob Makani (marehemu) alipokuwa Katibu Mkuu wa Chadema, majukumu yake yalikuwa ni ujenzi wa mfumo ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Amesemea baadhi ya kazi alizofanya tangu awe Katibu Mkuu ni  uandaaji wa Katiba ya Chadema, miongozo na kuweka misingi imara, mambo aliyodai kuwa yamemfanya asijulikane sana kwa Watanzania.

“Mbowe (Freeman-mwenyekiti wa Chadema) kwa wakati huo alikuwa maarufu kwenye umoja wa vijana. Makani hata leo wapo wasiojua kama alikuwa Katibu Mkuu wakati huo akiwa na mzee Mtei (Edwin-mwasisi wa Chadema),” amesema.

Dk Mashinji amesema kuanzia mwaka 2006 hadi 2010, uongozi wa chama hicho  ulikuwa na kazi ya kukijengea umaarufu kupitia shughuli mbalimbali za matukio,  yakiwemo maandamano, mikutano ya hadhara na vikao.

“Kwa sasa kazi iliyopo ni ku- consolidate chama, kukijengea uwezo wa kitaasisi zaidi, kama ni umaarufu Chadema inajulikana, tunajaribu kuziba maeneo yaliyokuwa na pengo katika mabadiliko ya Katiba kwa mwaka 2006,”amesema.

Amesema chama hicho kinashindwa kufanya aina ya siasa kama ilivyokuwa wakati wa utawala uliopita kutokana na katazo la kufanyika kwa shughuli za siasa.

“Amsha amsha bado ipo, hata waliozuia wanajua hilo, anajua hata akitoa dakika mbili tu sasa hivi, hapakaliki, sasa wanazuia kwa kutokujiamini,” amesema.

Jeshi la Polisi la Tanzania na Msumbiji Wasaini Mkataba wa Mashirikiano ya Ulinzi na Usalama

0
0
Jeshi la Polisi la Tanzania na Msumbiji Wasaini Mkataba wa Mashirikiano ya Ulinzi na Usalama
Jeshi la polisi Tanzania wakishirikiana na jeshi la polisi la Msumbiji  wamesaini mkataba wa mashirikiano ya ulinzi na usalama baina ya Nchi hizo mbili ili kudhibiti na kokomesha uhalifu mipakani pamoja uhamiaji haramu.

Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini dar es salam katika ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania

IGP sirro amesema,  mkataba huo wa mashirikiano ya ulinzi utasaidia kutunza na kudumisha aman kutokana na mashirikiano hayo,  na kuongelea mapigano ya majambazi ambao walikuwa wakipambana nao kibiti walikimbilia msumbiji na muungano huo utaleta mafanikio na kuwataka wote ambao wapo nchi msumbiji kuwa popote watakapo kimbilia bado hawatakuwa salama.

Aidha kwa upande wake IGP Bernadino Rafael wa msumbiji amesema makubaliano hayo yatawasaidia kuimarisha ulinzi na  kubadilishana na kujifunza mbinu mbalimbali ambazo jeshi la polisi la Tanzania wamekua wakizitumia ili kudhibiti uhalifu  na pia izi utazidi kuwa imara,  na madhaifu madhaifu ya polisi wa Tanzania

Aliyewazalilisha Watu Weusi kwa Kutoa Maoni ya Ubaguzi wa Rangi Atemwa na Mpenzi Wake

0
0
Aliyewazalilisha Watu Weusi Uingeleza Atemwa na Mpenzi Wake
Kiongozi wa chama cha UKIP nchini Uingereza Henry Bolton anasema kuwa amesitisha uhusiano na mpenzi wake baada ya yeye kuripotiwa kutoa maoni ya ubaguzi wa rangi kumhusu Meghan Markle.

Alisema kuwa mapenzi yao hayataendelea akiwa na wajibu kama kiongozi wa chama lakini hana nia ya kujiuzulu.

Jo Marney alikuwa ametuma ujumbe wa simu kuwa watu weusi wana sura mbaya na mpenzi wake Prince Harry ataichafua familia ya kifalme.

Mataifa ya Afrika yamtaka Trump kuomba msamaha
Bw Bolton alisema kuwa ilikuwa kinyume na katiba ya chama cha UKIP kuonyesha fikra zozote za ubaguzi wa rangi.

Mwanajeshi huyo wa zamani alichukua usukani wa chama cha UKIP kama kiongozi mwezi Septemba, na kuwa kiongozi wa nne katika kipindi cha miaka 18.

Trump asema atamshinda Oprah Winfrey 2020
Bw Bolton 54, alisema kuwa mwanamitindo huyo wa miaka miaka 25 alitimuliwa chamani mara moja baada ya chama kugundua kuhusu maoni yake.

Ujumbe huo ulitumwa wiki tatu baada ya wapenzi hao wawili kuanza uhusiano wao.

Refa Amrushia Teke Mchezaji Kisha Kumpa Kadi Nyekundu

0
0
Refa Amrushia Teke Mchezaji Kisha Kumpa Kadi Nyekundu
Mwamuzi huyo Tony Chapron alifanya hivyo baada yake kugongana na mchezaji huyo Diego Carlos.

Baada ya hilo, alimlisha mchezaji hiyo kadi ya pili ya manjano na kumfukuza uwanjani kufuatia kisa hicho muda wa ziada wa mechi.

Mwenyekiti wa Nantes Waldemar Kita amesema Chapron anafaa kupigwa marufuku kwa miezi sita kwa sababu ya uamuzi huo wenye utata.

PSG walipokuwa wanashambulia eneo la hatari la Nantes, Carlos alimgonga Chapron kwenye kisigino katika kile kinachoonekana kuwa ajali.

"Ni mzaha," Kita aliambia runinga moja ya Ufaransa.

"Nimepokea arafa 20 kutoka pande mbalimbali duniani kuniambia kwamba huyu mwamuzi ni mzaha tu.

"Nikizungumzia hili sana, nitaitwa kujibu maswali na kamati ya maadili. Hatuna haki ya kusema chochote."

PSG walishinda mechi hiyo yao ya kwanza baada ya mapumziko ya msimu wa baridi, bao lao pekee likifungwa na Angel di Maria dakika ya 12 uwanjani Stade de la Beaujoire.

Ushindi huo, bila mchezaji wao ghali zaidi Neymar aliyenunuliwa £200m - uliwaweka alama 11 mbele kileleni Ligue 1.

Meneja wa Nantes Claudio Ranieri alisema: "Jambo mbaya zaidi litakalomtendekea Diego Carlos ni kwamba atapigwa marufuku kucheza mechi moja. Ilikuwa mechi nzuri kwetu tukisahau bao ambalo lilikataliwa kwa sababu ya kuotea na pia yaliyomsibu Diego Carlos."


Lowassa Atoa Ufafanuzi Kuhusu Mazungumzo Yake na Rais Magufuli "Aliitwa Ikulu Akinitaka Kurudi CCM Ila Nilikataa"

0
0
Lowassa Atoa Ufafanuzi Kuhusu Mazungumzo Yake na Rais Magufuli "Aliitwa Ikulu Akinitaka Kurudi CCM Ila Nilikataa"

Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chama caha Demokrasiana na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa amesema kuwa alikwenda Ikulu baada ya kuitwa na Rais John Pombe Magufuli akimtaka arudi CCM lakini alimjibu kuhama kwake hakubahatisha.



Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images