Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

Ali Kiba, Diamond Wafika Pabaya..Chanzo cha Ugomvi Wao Hiki Hapa

0
0
Na Sifael Paul
Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).

Kupitia Kipindi cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi wao.
Kiba alizungumzia sosi iliyotengeneza bifu kati yake na Diamond ambapo aliulizwa kama ana namba ya simu ya msanii huyo ndipo akatiririka:

“Nilikuwa nayo kipindi fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima wa kuwa nayo.
“Kuna kipindi alinikosea kwa sababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote ule Wimbo wa Single Boy, jambo ambalo halikuwa kweli. Halafu akasema mimi ndiyo nilimfuta.

“Diamond alinikosea kwa sababu kutokana na mimi ndiye nilifanya wimbo wake wa Lala Salama ambao upo kwenye album yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye, alichoniomba nifanye nilifanya kwa mapenzi yote na mimi namsapoti kila msanii wa Tanzania anayefanya vizuri, sikatai anaimba vizuri, sijui ukisema amekopi, mimi sijamaindi wala nini lakini usiseme kwa watu ukadanganya nikaonekana mimi sifai, siko hivyo mimi.

“Watu wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine wanampenda Ali Kiba. Wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini mimi nilimfuta kwenye wimbo wangu wa Single Boy lakini mimi wala, shahidi yangu ni produyuza Manecky (AM Records) kwani ndiye alitengeneza ule wimbo.

“Sikuwahi kwenda studio na Diamond, sikuwahi kufikiria kufanya wimbo naye. Ila alinipigia simu baada ya ule wimbo wa Single Boy kuvuja. Akaomba afanye na mimi, akanipa hadi idea (wazo) ya video, nikamwambia nimeshafanya na Jaydee (Judith Wambura).

Nikamwambia itapendeza zaidi tukifanya wimbo mwingine kwa sababu hii tukifanya mimi na wewe haita-make sense (haitaeleweka), inapendeza ikiwa single boy na single girl, hicho ndicho kitu nilimjibu.
“Baada ya kama wiki moja nikasikia kwenye mablog, nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta Diamond kwenye ule wimbo wakati yeye ndiye aliyenifuta katika wimbo wake, shahidi prodyuza wangu KGT.

“Kutoka hapo nikaona hakuna tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika wimbo wake. Mimi siyo shabiki wa Diamond ni shabiki wa muziki mzuri. “Kuna watu wanasema kachukua kiti changu? Labda kama ni kiti ambacho nilikuwa nimekaa kina vumbi na ninachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena, labda yeye yuko siti nyingine ila ya nyuma.

“Niliambiwa alisema vitu vingi, mara nilikopa fedha benki ili nimalizie nyumba na mambo kama hayo so siwezi kufanya naye kazi.” Baada ya Kiba kumchakaza, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond naye alijibu mapigo bila kutaja jina la Kiba ambapo aliandika: “Tatizo lako wewe unawaza kushindana na mimi ili nishuke…Wakati mwenzako nawaza kushindana na watu wa mataifa mengine ili nilete sifa na heshima nchini kwetu.”

Hata hivyo, baada ya hayo yote kuliibuka madai kwamba mbali na ishu za muziki, mastaa wa kike wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema Isaac Sepetu wanahusishwa kwenye gogoro hilo kisa wivu wa kimapenzi hivyo ishu hiyo bado ni mbichi. Tusubiri mwisho WAKE!
GPL

Matokeo ya Tuzo za AFRIMMA 2014 Alizokua Anawania Diamond Marekani

0
0
Wanaziita African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news kwa mujibu wa meneja Babu Tale ni kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.

Tuhuma za Mke wa Mbunge Kumuua Mfanyakazi wa Ndani: Mbunge Cyril Chami Atoa Ufafanuzi

0
0
Mimi Dr Cyril August Chami, Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM) napenda kueleza masikitiko yangu kwa taarifa za uzushi na za kutunga kuwa eti mke wangu asiye na jina amemuua mfanyakazi wetu Mwislamu kwa sababu "marehemu" alikataa kwenda kanisani.

Mimi sina mfanyakazi wa jina hilo la Mariamu. Wala sina mfanyakazi mwenye umri wa miaka 16. Hatuna tatizo lolote la mfanyakazi yeyote kupigwa, achilia mbali kuuawa.

Lakini taarifa hizo ambazo ni za uongo mtupu zimewashtua wengi kwa sababu zimejengwa katika misingi ya chuki za kidini. Mwandishi alilenga kuifanya jamii iamini kwamba mke wangu ambaye ni Mkristo anawalazimisha wafanyakazi wetu wasio Wakristu waikane dini yao na kuwa Wakristo. Alilenga kuibua chuki dhidi ya Waislamu na familia yangu. 

Kwa hakika, mikakati hii ya kuichafua familia yangu inasababishwa na harakati za ubunge Moshi Vijijini 2015. Wapinzani wangu wanajua wazi kuwa hawana hoja ya msingi ya kuwafanya wapiga kura wasinirudishe kwenye nafasi ya ubunge. Kwenye jukwaa na hata kwenye medani ya maendeleo wanakwama. Kwa mfano, kabla ya barabara za lami kuanza kujengwa walisema mimi sina ushawishi wa kuifanya Serikali kuzijenga. Sasa zimejengwa na zinaendelea kujengwa wanajenga hoja kuwa sihusiki wala Serikali ya CCM haihusiki, bali ni Benki ya Dunia inajenga!!! Wananchi wanawauliza kwani kabla ya Dr Chami kuwa mbunge Benki ya Dunia haikuwepo? Wanakosa hoja! Hivyo hivyo kwa mashule, maji, vyuo vya ufundi nk.

Kwa hiyo kwa upeo wao wanaona silaha pekee waliyo nayo ni kuzua kashfa dhidi yangu. Miezi michache iliyopita walizua nimeuza shamba la KNCU kwa shilingi bilioni 4 wakati mimi sina wadhifa wowote KNCU. Eti nimeuza nyumba mbili za Coffee Curing Moshi wakati mimi sina wadhifa wowote Coffee Curing.

Walipoona tuhuma hizo za kutunga hazijakubalika masikioni mwa wapiga kura wa Moshi Vijijini, sasa wamezua hili la mke wangu kuua ili Waislamu wa Moshi Vijijini wanione mtu nisiyefaa.

Sasa mimi napenda kuwauliza maswali haya:

Huyo mke wangu muuaji anaitwa nani? Inaingia akilini kweli kwamba mke huyo muuaji hafahamiki jina kwa hao "majirani" wetu wa kufikirika?

Binti Mariamu kauawa mji upi? Kwa nini majirani hao wenye uchungu hawajatoa taarifa kwa RPC wa mkoa au kanda husika?

Maiti kahifadhiwa hospitali ipi? Au "mke" wangu amekaa naye ndani baada ya kumuua na majirani wamekaa kimya tu?

Kwa desturi za dini ya Kiislamu binti huyo angeshazikwa sasa maana kwa mujibu wa habari hiyo ya kizushi, "aliuawa" usiku wa kuamkia jana. Je, kazikwa makaburi yapi na yako mji gani? Nani kahudhuria hayo mazishi? Kwa nini vyombo vya habari visituonyeshe hayo mazishi?

Kwa nini RPC mhusika asimkamate huyo mke wa mbunge fedhuli namna hiyo na muuaji asiyevumilika?

Kwa nini polisi hawajaniita mimi Dr Chami kunihoji kuhusu huyo "mke" wangu? Si wanajua niko jimboni Moshi Vijijini na RPC Boaz wa Kilimanjaro anafahamu niko jimboni, tena jana nimeutembelea msikiti mmoja kwa minajili ya kuutafutia umeme na maji? 

Sote tunafahamu kuwa kuna mkuu mmoja wa mkoa alimuua mtu kwa kumpiga risasi na alikamatwa akapelekwa mahabusu. Huyo mke wa Dr Chami ni maarufu kuliko Mkuu wa Mkoa? Kwa nini asikamatwe tuione sura yake magazetini?

Majibu ya maswali haya HAYAPO kwa sababu kila kitu kimetungwa kwa kujenga chuki tu. Hakuna Mariamu, hakuna kipigo, hakuna kifo. Ila kuna UBUNGE WA MOSHI VIJIJINI. Ndio unaopiganiwa, hamna kingine. 

Napenda kuwaasa wanasiasa wenzangu kuwa Watanzania wa leo si wa jana. Si jambo rahisi kuwaghilibu kwa staili hii. Waende kwa wananchi wachape kazi. Wasipofanya hayo wakadhani uongo wa mitandao utawapa ubunge watashangazwa mwaka kesho 2015.

Mimi naendelea kuwaahidi wapiga kura wangu utumishi wa dhati. Nawapa pole ndugu zangu wa Kiislamu kwa usumbufu walioupata. Waislamu wa Moshi Vijijini wananifahamu kama kiongozi nisiyewabagua kwa sababu ya dini yao. Wanafahamu kuwa nawapenda na nafahamu kuwa wananipenda sana. Ndiyo maana wengi wamejiuliza iweje tena mke wangu amwage damu ya Mwislamu kwa sababu iliyotajwa. Naendelea kuwaahidi Waislamu wote upendo na ushirikiano siku zangu zote za kuwatumikia.

Wasalaam

Dr Chami

Dr Slaa: Sina Mpango wa kugombea Urais 2015

0
0

DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa ktk kundi la UKAWA.Kila kitu kitafanywa kwa wakati muafaka, kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania umoja wetu wa UKAWA ili kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 2015.

Akizungumzia hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. Slaa alisema umoja huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, niaheshimu uamuzi wa Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.

UKAWA imebeba maoni ya wananchi na suala la kutengeneza Katiba sio suala la rais, serikali wala chama chochote bali ni la wananchi.

Serikali ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao ndio waliosaini rasimu ya Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio wanageuka na kutaka yajadiliwe mambo ambayo hayamo ndani ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba."

Barabara ya Lami Mabatini, Kijitonyama Haina Hata Mwaka, Nani Kala 10%?

0
0
Barabara hii inayopita karibu na kituo cha Polisi Kijitonyama, maarufu kama Mabatini, haina hata mwaka imeanza kumeguka vipande vipande.

Nani kala 10% hapo?

Diamond na Lady Jay Dee Waitoa Kimaso Maso Tanzania Tuzo za AFRIMMA 2014

0
0
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' ameendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki ndani na nje ya nchi baada ya kutwaa tuzo ya AFRIMMA 2014 ya Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki huku Lady Jaydee akinyakua tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki.

Tuzo hizo za Africa Music Magazine (AFRIMMA) zimetolewa leo alfajiri jijini Texas nchini Marekani.

Diamond alikuwa anawania tuzo katika vipengele vitano ambavyo ni: Msanii bora wa mwaka Afrika, Wimbo wa mwaka, Collabo bora, Video bora ya mwaka na Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki.

Kupitia ukaunti yake ya Instagram, Diamond ameandika hivi:


WASHINDI WA TUZO HIZO ZA AFRIMMA 2014 NI KAMA IFUATAVYO:

Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana)
Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya)
Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria)
Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania)
Best Male West Africa 2014- Davido (Nigeria)
Best Female East Africa 2014- Lady Jaydee (Tanzania)
Best Female West Africa 2014 – Tiwa Savage (Nigeria)
Best Male Central Africa 2014 – Fally Pupa (Congo)
Best Female Central Africa 2014- Gasha ( Cameroon)
Best Male Southern Africa 2014- Khuli Chana (South Africa)
Best African Group 2014- P-square (Nigeria)
Best Male Diaspora 2014- Fuse ODG (Ghana)
Best Female Diaspora 2014- Les Nubians (Cameroon)
Best Female Southern Africa 2014- Zahara (South Africa)
Best Dancehall Artist 2014 – Timaya (Nigeria)
Best Dance in a Video 2014- Iyanya (Lekwa Ukwu) (Nigeria)
Best Gospel Artiste 2014- Bahati (Kenya)
Best Traditional Artist 2014- Flavour (Nigeria)
Best Newcomer 2014- Stanley Enow (Cameroon)
Best Video Director 2014- Ogopa Dj’s (Kenya)
Music Producer of the year 2014- Dj Oskido (South Africa)
Best Dance Group 2014- Imagineto (Nigeria)
Best Rap Act 2014- Sarkodie (Ghana)
Best Collaboration 2014- Mafikizolo ft Uhuru (Khona) (South Africa)
Song of the Year 2014- Kcee (Nigeria)
Artist of the Year 2014- Davido (Nigeria)
Leadership in Music Award 2014- 2face Idibia
Legendary Award 2014- Yvonne Chaka Chaka
Transformational Leadership Award 2014- Chief Dr. Godswill Akpabio

Taarifa ya Kesi za Kusambaza Picha za Utupu, Kuuza Binadamu, Vitisho, Zilizofunguliwa Shidi ya Eto’o

0
0
Huu unaweza sio mwaka mzuri kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o, baada ya timu yake ya taifa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia, na akiwa hana timu ya klabu ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, sasa amefunguliwa kesi nzito mahakamani.
Kesi hizo za udhalilishaji kwa kusambaza picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu, udanganyifu, na vitisho zimefunguliwa kwenye mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon, na aliyekuwa mchumba wa mshambuliaji wa huyo za zamani wa Chelsea, Hélène Nathalie Koah.
Mapema wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana mashtaka hayo.
Hatua hiyo ya imekuja siku chache baada ya kusambaa kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook, ambazo mhudumu huyo wa zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi wake.
Eto’o amekanusha kuhusika na mchezo huo mchafu, na katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi mabaya ya fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi ya kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.
Mwanamke huyu alishawahi kuwaingiza kwenye beef mwanamuziki Fally Ipupa na Eto’o kwa kuwachanganya kimapenzi.

Manager wa Ney wa mitego ashangazwa na utajiri wa Ney.

0
0
Miezi miwili iliyopita msanii Ney wa mitego alianika utajiri wa ajabu zikiwemo nyumba nne na gari moja ya kisasa nissan murano!! Akichezesha taya na mwandishi wetu aliyekuwa manager wa ney amesema tangu aachane na ney miezi 7 iliyopita alikuwa hana hata nyumba moja ameshangaa kumuona ana nyumba nne ghafla lakini manager amesema inawezekana jamaa anatafuta kiki ili watu wanaomuita kwenye show wafikirie kumpa mpunga mrefu na si laki laki wanazolipwa kwenye fiesta! Amefunguka kwamba Ney kuwa na hizo nyumba basi itakuwa ni miujiza.

Ukweli wa idadi ya Tuzo Alizoshinda Diamond AFRIMMA Jana Usiku

0
0
Habari zenu ndugu ,wakubwa na wadogo
nataka niweke sawa kuhusu utata uliozuka kuwa diamond kashindatuzo ngapi,
kwenye AFRIMMA,ameshindatuzo mbili, mwanamziki bora East Afrika na Number 1 Remix ikishinda collabo bora ya Africa category iliyokuwa na ugumu kidogo kulingana na aliokuwa akishindanishwa nao:

2face ft Tpain- Rainbow ( Nigeria/ United
States)

Mafikizolo ft Uhuru-- Khona ( South Africa)

Dr Sid ft Don Jazzy /Phyno/Wizkid- Surulere
remix(Nigeria)

Amani ft Radio and Weasel – ‘Kiboko
Changu’ (Kenya/Uganda)

Jmartins ft DJ Arafat--- Touching body
( Nigeria/ Ivory Coast)

R2bees and Wizkid- Slow down ( Ghana/
Nigeria)

Kilichotokea ni makosa ya uandishi kwenye website ya Afrimma ambako ndiyo watu wamecopy ..
but wameahidi kulekebisha,kwa ufupi Diamond anarudi na tuzo mbili mkononi.
lakini nitumie nafas hii kuweka sawa kuwa,diamond kwa sasa,wasanii wakubwa wa nje wengi ndiyo wanoomba collabo yeye, sitosema mengi ila kwa uchache tu nimfano wa 
Mafikizolo waliomwomba Diamond nakumlipia na nauri ili abaki South ili tu collabo ikamilike,piakuna iyanya ailiomba colabo (siyo bumbum) but haijatoka bado, kuna Waghana, kuna mwanadada Waje wa Nigeria, hilo liliandikwa sana tu kwa wanokumbuka, all in all time will tell, kazi zitajieleza zikitoka.
Ahsanteni

Message To Ally Kiba..Hii Mwana Sijui Dsm Umepanick..Diamond Alipo Anachekelea Tu

0
0
Ukweli unauma...nasema hivi Talent pekeee haitoshi bila kujipanga...nikiwa kama shabiki wa Ali kiba,huu wimbo wa mwana kachemka..watanzania tuwe wakweli na sio watu wakurupuka tu..Kiba ana vocal za hatari hili halina ubishi ila nyimbo hamna kitu..chorus haina mvuto maneno hajajipanga..in short kapanic..na kama ndo alijichimbia na kutoa nyimbo basi alichemka Game imechange na ndo maana ata ukisikiliza nyimbo ya Fally ipupa kabadilisha style mpaka beat..My opinion ni kwamba Kiba huyu sio sawa na Kimasomaso..Kapanick yani kama huyu ndo competitor wa Dogo Dangoti alipo anacheka tu..kweli Kiba u lacking some Good PR,Management ambayo inajielewa ikupe ushauri,inauma kwasababu sauti yako ni untouchable ila wrong management..ni hayo tu..Naandika hivi ili watu wake wampelekee msg its such a waste of Talent.

Habari Kuhusu Watanzania Walioshikwa Kenya Kwenye Harakati za Kujiunga na Al Shabaab.

0
0
Wanajeshi wa kupambana na ugaidi nchini Kenya (ATPU) wanawashikilia raia watatu wa Tanzania waliokamatwa wakijaribu kuvuka mpaka wa Somalia na Kenya ili kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab.
Kamanda wa Polisi Lamu Mashariki amethibitisha kukamatwa kwa watatu hawa ambao wote wana umri chini ya miaka 22 ambao kwa sasa wanashikiliwa na maafisa wa kupambana na Magaidi Kiunga mpaka wa Kenya na Somalia ambapo baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa Mahakamani.
Kukamatwa kwa watatu hawa kunafikisha idadi ya vijana sita wa Kitanzania waliokamatwa nchini Kenya ambao wanatuhumiwa kujiunga na mtandao wa kigaidi ambapo wengine watatu wanashikiliwa kwenye gereza la Kamiti waliokamatwa Kiamboni.

Miongoni mwao ni Bakari na Daudi ambapo walipohojiwa wamesema >>> ‘Tumeambiwa kwamba Somalia kuna Waislamu na wako katika hali ngumu, kuna majeshi mengi yanawanyanyasa Waislamu kwa hiyo kama Muislamu inabidi uende kutoa support kwa ndugu zako, kutokana na imani yangu kujengeka katika dini ndio nikajikuta naunga safari’
Haya yanajiri baada ya vijana kadhaa wa Kenya kukamatwa mpakani walipokua wakifanya mpango kuvuka mpaka na kuingia Somalia vilevile msajili wa kundi la Al Shabaab amekamatwa akiwapeleka vijana wawili wa Mombasa kwenda kujiunga na Al Shabaab mjini Garisa.
Wakati huohuo Polisi wanawasaka vijana waliotumwa na Al Shabaab kwenye mataifa ya Kenya na Tanzania kusubiri kupewa maagizo ya kundi hilo kutekeleza mashambulizi.
Unaweza kuwasikiliza wakiongea hapa chini.

Mastaa wa Bongo Wasusia Arobaini ya Marehemu George Tyson

0
0


Jamani! Katika hali ya kushangaza, mastaa wa filamu Bongo wamesusia kumbukumbu ya siku 40 ya aliyekuwa muongozaji maarufu wa filamu nchini, George Otieno ‘Tyson’ aliyefariki dunia kwa ajali Mei 31, mwaka huu.

Shughuli ya 40 ya Tyson ilifanyika Alhamisi iliyopita nyumbani kwa aliyekuwa mkewe, Beatrice Shayo maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo mastaa mbalimbali walialikwa lakini hakuonekana hata mmoja hali iliyosababisha chakula na futari iliyokuwa imeandaliwa kubaki huku wasanii wa vikundi waliohudhuria wakirudia mara mbilimbili.

Akizungumza na gazeti hili, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba aliyekuwa kwenye shughuli hiyo alisema anashangaa mastaa wa filamu kukacha ishu hiyo kwani alimpa taarifa Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kwamba awaambie wahudhurie.

“Nimewaalika wasanii wote lakini hakuna aliyekuja hata mmoja, ukweli wasanii hatuna ushirikiano kwani Tyson ndiye mwanamapinduzi aliyeigeuza sanaa kutoka kwenye kuuza sura hadi kuwa biashara hivyo walipaswa kumpa heshima yake,” alisema Mwakifwamba.
GPL

Johari Akanusha Tuhuma za Kubatizwa Mara Mbili Kanisani

0
0
MKONGWE wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amedaiwa kubatizwa juzikati katika Kanisa Katoliki Nyalikungu wilayani Maswa, Simiyu lakini mwenyewe amekanusha.

Chanzo makini kilichodai kushuhudia ubatizo, kilieleza kuwa Johari alifika Jumapili kanisani hapo na watu kuhoji kwa nini achelewe kubatizwa? Alipotafutwa na mwanahabari wetu, Johari alitiririka:

“Kweli nilikwenda kwenye hilo kanisa lakini sikubatizwa kama alivyosema huyo mtu. Nitabatizwaje mara mbili? Mimi nilishabatizwa tangu utotoni.”

Miaka Sita ya Mahusiano na Sioni Dalili ya Ndoa…Nifanyeje?

0
0
Mimi ni msichana wa umri wa miaka 19. Nimekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na kijana mmoja  kwa muda wa miaka sita sasa.

Isitoshe sisi ni majirani wa karibu. Aliniahidi atanioa, lakini kwa jinsi muda unavyokwenda naona kama kuna tofauti. Nahofia kuachwa.

 Naombeni  ushauri  jamani

Mary

KATIBA MPYA: Wassira, Lipumba, Lissu ‘Wanyukana Live’

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira akiwakilisha CCM, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, jana walitoana jasho katika mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na East African Business and Media Institute.

Mdahalo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao 500, ulikuwa na mada inayosema: ‘Nani anakwamisha Upatikanaji wa Katiba Mpya.’ Kila upande ulitumia fursa hiyo kutupa shutuma kwa mwingine huku jazba na kelele vikitawala miongoni mwa waliohudhuria.

Hata hivyo, suala la muundano wa serikali ndiyo uliochukua nafasi kubwa katika mdahalo huo huku Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukiishutumu Serikali ya CCM kuwa ndiyo kikwazo cha upatikanaji wa Katiba Mpya nayo ikitupa mpira huo kwa Ukawa kwa kitendo chake cha kutoka katika Bunge Maalumu la Katiba.

Profesa Lipumba alisema wahafidhina wa CCM ndiyo waliomshauri Rais Jakaya Kikwete abadilike kimsimamo kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya.

“Rais Kikwete alikuwa na nia njema kabisa kuhusu Katiba Mpya lakini wahafidhina wa CCM wanaopenda madaraka walipoona muundo wa serikali tatu wakambana naye akabadilisha msimamo, tunamwomba abadilike, nchi hii ni yetu sote ili tupate katiba ya wananchi,” alisema.

Lissu aliongeza kwa kusema kuwa anayekwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya ni CCM ambao wanaweka maoni yao badala ya kujadili rasimu iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ndiyo maoni ya wananchi.

“Hatuwezi kurudi kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwenda kujadili rasimu ya CCM kwa sababu wanaonyesha hawana nia ya Katiba Mpya, bali wanataka kuwadanganya Watanzania, watawadanganya wananchi kwa kuleta Katiba ileile ila ikiwa na rangi tofauti,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema Ukawa hawawezi kushiriki katika udanganyifu wa aina hiyo na kwamba wameamua kuwaachia CCM ili wananchi waweze kuwahukumu kwa uovu watakaoufanya.

Alisema kati ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba katika Kundi la 201, wajumbe 166 ni wana CCM walioteuliwa ili kuongeza idadi ya watu.

“Humo kuna viongozi wa dini mashehe na maaskofu na waganga wa kienyeji ambao ni wana CCM ili wapitishe Katiba yenye masilahi yao binafsi,” alisema.

Hata hivyo, Wassira alisema hoja za Ukawa hazina mashiko na kumtaka Lissu kuwaomba radhi masheikh na maaskofu kwa kuwa hawakuteuliwa na Rais kutokana na kuwa wanachama wa CCM, bali ni mapendekezo ya taasisi wanazozitumikia.

“Namwomba Tundu Lissu akawaombe radhi masheikh na maaskofu kwa sababu kundi hili liliteuliwa kutokana na mapendekezo ya wahusika wenyewe pasipo shinikizo la Rais. Hapakuwa na uwezekano wa Rais kuwatambua wana CCM ili awateue wanaofaa. Kama ana ugomvi na Kingunge Ngombale Mwilu aseme.”

CHADEMA Imepoteza Ushawishi Kwa Watanzania

0
0
Kadri siku zinavyosonga chadema nayo inasonga kuelekea kaburini. Ilianza kwa kasi kama nguvu ya soda, ikatingisha, ikavuma,ikapendwa sana, ghafla ikafifia, ikasinyaa ikayumba ikapoteza kabisa umaarufu, ikapoteza ushawishi. Watanzania hivi sasa ukiwauliza, ukiwasikiliza hawaisemi tena chadema kama ni chama kilichobeba matumaini ya unyonge wao, umaskini wao na shida zao. Wako puzzled. 

Utafiti nilioufanya hautoi njia kwa chadema kupenya tena kwenye mioyo ya watanzania na kuwa chama pendwa, kimekuwa kama ilivyokuwa CUF ambayo hivi sasa ni chama zee zee, kuu kuu.

===nashauri ccm itumie vyema mwanya huu kujiimarisha, kuziba hili gape.

VICKY KAMATA Ajisalimisha Kanisani Kusafisha Nyota ya Mapenzi na Ndoa iliyochafuka

0
0
Msanii wa muziki na mbunge wa viti maalum wa jimbo la Geita kupitia CCM Vicky Kamata amejisalimisha kuombewa kanisa la EAGT kata ya Kalangalala wilaya ya Geita mkoani Geita ili kuondoa mikosi ya ndoa kuvurugika.
Jamani kusafisha nyota ya mapenzi si kwa waganga wa kienyeji tu bali kanisani ndo kwa uhakika zaidi kwingineko ni utapeli tu

Mrembo wa Kenya Huddah Monroe Atangaza Kumzimikia Ali Kiba

0
0
Udaku kutoka INSTAGRAM: Huddah Monroe Wa Kenya elezea hisia zake kuhusu .... Ali Kiba..Eti Anasauti Ya Kumtoa ...Pangoni....Soma alivyoandika..Then Niambie Ungekuwa Wewe Ndio Alikiba Unge Mfanyanini Huyu!!!!

Mtuhumiwa Amng’ata Mdomo Askari

0
0
KARANI wa Kampuni ya Mabasi ya abiria yaitwayo Happy African, Eliud Mwanyonga (40), amemng’ata mdomo askari wa kikundi cha ulinzi shirikishi aliyefahamika kwa jina moja la Ernest.

Tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita saa 12 alfajiri katika Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani wakati askari huyo alipokuwa katika shughuli zake za kila siku.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, James Zebedayo, aliliambia MTANZANIA Jumatatu kwamba, askari huyo aling’atwa mdomo baada ya kutaka kumkamata Eliud kwa kosa la 
kutovaa sare za kazi.

“Hawa mgambo walikuja asubuhi walikuwa kama sita hivi na walipofika hapa wakawa wamemuuliza kwanini hakuwa na sare.

“Yeye akawajibu siku hiyo ilikuwa ni Siku ya Mashujaa, kwa hiyo hakuwa na sababu ya kuvaa sare.

“Alipojibu hivyo yule askari wakachachamaa, wakasema lazima amkamate ili akaadhibiwe kisheria lakini yule mfanyakazi akakataa akasema hawezi kukamatwa mara mbili kwa kuwa alikuwa amekamatwa siku chache zilizopita kwa kosa lile lile.

“Baadaye huyo mtuhumiwa alifanikiwa kuwakimbia lakini askari hao walimkimbiza na walipomkamata, walimpiga kwa kutumia fimbo walizokuwa nazo. Walipokuwa wakimpiga, mtuhumiwa naye alijitetea na mwishowe akamng’ata askari huyo mdomo wa chini na kuuondoa kabisa,” alisema Zebedayo.

Kutokana na tukio hilo, askari wengine walifanikiwa kumdhibti mtuhumiwa huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi kilichoko kituoni hapo kabla ya kupelekwa Kituo cha Polisi Magomeni ambako alifunguliwa jalada lenye namba MAG/RB/7172/2014.

Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi Ubungo, Suphiani Masanga, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo ingawa hakutaka kulizungumzia zaidi kwa alichosema kuwa yeye siyo msemaji wa Jeshi la Polisi.

Nani Mkali kati ya Diamond na Ali Kiba? Wachezaji na Kocha wa Simba wabishana

0
0
Mjadala uliopo kwenye mitaa na baadhi ya maskani za watu wengi japo kwa dakika tano ni mpambano usio rasmi kati ya Diamond na Ali Kiba.

Mpambano huo unaotengenezwa zaidi na mashabiki umetua katika mazoezi ya Simba ambapo wachezaji maarufu wa timu hiyo waliweka nukta ya mazoezi kwa muda na kuanzisha mjadala ‘wa nani mkali’ mjadala uliomhusisha kocha wa timu hiyo, Selemani Matonya.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, wachezaji hao na Kocha wao walijikuta wakianza kubishana (debate isiyo na msimamizi) huku Suleiman Matola, Uhuru Selemani, Awadh Juma na Twaha Ibraahim wakiwa upande wa Mwana Dar Es Salaam Ali Kiba, wengine waliohusika kwenye mjadala huo walichukua upande wa MdogoMdogo wa Diamond wakiwemo Said Ndemla na Abdallah Sisem
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images