Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Mapenzi Yamuhamisha Dini Kadja Nito Azidi Kumtibua Mama Yake

0
0
Mapenzi Yamuhamisha Dini Kadja Nito Azidi Kumtibua Mama Yake
MREMBO wa Bongo Fleva, Natasha Lisimo ‘Kadja Nito’ ambaye aliingia kwenye bifu zito na mama yake baada ya kubadili dini na kuwa Mkristo na kumsamehe kipindi alipokuwa mahututi akijifungua, amemtibua tena mzazi wake huyo kutokana na kukomaa kwenye dini hiyo.



Kwa mujibu wa chanzo chetu, kitendo cha mama yake Kadja kumsamehe alipokuwa mahututi leba, aliamini baada ya kurejea kwenye hali yake ya kawaida huenda angemtii na kurudi kwenye Uislamu lakini ndiyo kwanza, dini ya Kikristo imemkolea na sasa anajianika waziwazi hadi mitandaoni, jambo linalomchefua mzazi wake huyo.



Kutokana na ishu hiyo Kadja alipoulizwa alisema; “Kuna vitu sipendi kuviongelea sana kwa sasa, hususan mambo yangu na mama yangu ni masuala ya kifamilia, kama mnaona najianika kwenye Ukristo na nilibadili dini nikawa huko, sioni kama kuna haja ya kuzungumzia hilo kwa kina.

Chuchu Hans Afunguka Sababu ya Kumtoboa Mtoto Wake Sikio

0
0
Chuchu Hans Afunguka Sababu ya Kumtoboa Mtoto Wake Sikio
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans amefungukia madai ya kumtoboa sikio mtoto wao wa kiume Jaden mwenye umri wa mwaka mmoja akidai kuwa suala hilo limepokelewa ndivyo sivyo.

Akizungumza na gazeti hili, Chuchu alisema kuwa hakumtoboa kabisa sikio bali baba yake (muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’) ndiye aliyemvalisha kihereni cha kubandika na siyo kumtoboa moja kwa moja.

“Watu hawajatuelewa jamani hatuwezi kumtoboa sikio mtoto kwenye umri alionao tena wa kiume bali baba yake alimvalisha hereni ya kubandika tu, wasituzungumzie vibaya bwana,” alisema Chuchu.

Vanessa Mdee, Ray Kigosi, Millard Ayo Wametajwa Kuwania Tuzo Ghana

0
0
Vanessa Mdee, Ray Kigosi, Millard Ayo  Wametajwa Kuwania Tuzo Ghana
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ametajwa kuwania tuzo za The African Prestigious Awards (APA) 2017.

WhatsApp-Image-2017-08-23-at-16.46.10

Vanessa Mdee ametajwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha msanii bora wa kike wa mwaka 2017/18 ambapo atachuana na wasanii wengine kama Yemi Alade kutoka Nigeria na wengine wengi.

BEST FEMALE ARTIST AFRICA
-ANGHAM (EGYPT)
-ASMAE SALIM (LIBYA)
-BECCA (GHANA)
-CINDY LE COEUR (CONGO)
-GLORIA MULIRO (KENYA)
-HOPE MASIKE (ZIMBABWE)
-LATIFAH (TUNISIA)
 -LIRA (SOUTH AFRICA)
-LYRA-AOKO (KENYA)
-NABYLA-MAAN (MOROCCO)
-NANCY AGA (SUDAN)
-SOUHILA BEN LACHHAB (ALGERIA)
-VANESSA MDEE (TANZANIA)
-YEMI ALADE (NIGERIA)
-ZERITU KEBDE (ETHIOPIA)
Watu wengine waliotangazwa kuwania tuzo hizo ni Muigizaji wa filamu, Ray Kigosi, Monalisa na King Majuto ambao wametajwa kwenye vipengele vya Muigizaji bora wa kiume, Muigizaji bora wa kike na mchekeshaji bora wa mwaka 2017 barani Afrika.

Wengine ni DJ Sinyorita na Millard Ayo ambao wametajwa kwenye vipengele vya DJ bora wa kike na bloga wa mwaka 2017.

BEST BLOGGER AFRICA 2017.
-ALIAA MAGDA ELMAHDY (EGYPT)
-AMEYAW DEBRAH (GHANA)
-DANIEL BERHANE (ETHIOPIA)
-GARETH PON (SOUTH AFRICA)
-KENYA BUZZ (KENYA)
-LINA BEN MHENNI (TUNISIA)
-LINDA IKEJA (NIGERIA)
-MAMA CONGO (CONGO)
-MILARD AYO (TANZANIA)

Iyobo Afunguka Kuhuzu Kunyimwa Unyumba na Aunt Ezekiel

0
0
Iyobo Afunguka Kuhuzu Kunyimwa Unyumba na Aunt Ezekiel
DANSA maarufu Bongo, Moses Iyobo, amesema kuwa kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa amenyimwa penzi na mzazi mwenzie Aunt Ezekiel hajaona kama kuna tatizo ingawa aliandika kama utani.

Akizungumza na gazeti hili, Iyobo alisema kuwa yeye na Aunt ni watu ambao wanataniana sana japokuwa tayari ni wazazi kwa hiyo hata alipoandika juzikati Instagram, alikuwa kwenye kuendeleza utani japo mashabiki wao wameipokea vibaya.

“Unajua watu wanashindwa kuelewa lakini mimi na mama Cookie (Aunt) tunataniana sana kwa hiyo hata kuandika vile ni kumtania tu sasa watu hawakuelewa naona wametoa povu kweli,” alisema Iyobo.

Iyobo alikomenti kwenye video aliyoposti Aunt ikimuonesha akitembea akisindikiza na ujumbe wa neno ‘fresh’:

“Umeninyima penzi halafu uposti fresh?” alikomenti Iyobo

Mzee Majuto Anaumwa Tena Alazwa Muhimbili kwa Matibabu

0
0
Mzee Majuto Anaumwa Tena Alazwa Muhimbili kwa Matibabu
Mchekeshaji Amri Athuman aka Mzee Majuto Jumatano hii amelazwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es saalam kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari wa Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni.


Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii Asifa Habari huyo, Masoud kaftany, amesema muigizaji huyo alipelekwa hospitali hapo siku ya jana baada ya kuzidiwa.

“Ni kweli Mzee Majuto anaumwa na sasa hivi tupo naye hapa Muhimbili anaendelea na matibabu,” alisema Masoud kaftany. Kusema anaumwa nini ni mapema zaidi lakini baadae tutatoa taarifa rasmi baada ya kupokea taarifa ya madaktari,”

Afisa huyo amekiomba Chama cha Waigizaji, wadau wa filamu Tanzania na wa Tanzania wote wamuombee muigizaji aweze kupona haraka

Daktari wa Timu ya Olimpiki Marekani Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 175 Jela

0
0
Daktari wa Timu ya Olimpiki Marekani Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 175 Jela
Aliyekuwa daktari wa timu ya Olimpiki Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana michezo.

Katika kesi hiyo mashahidi 160 wamewasilisha ushahidi wao huku Nasser mwenyewe alikiri makosa kumi.

Alikuwa tayari akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha ngono za watoto kinyume cha sheria.

Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine.

'Nataka ukae jela maisha yako yote'. Hata hivyo baada ya hukumu hiyo mmoja wa waathirika amesisitiza kuwa washirika wa daktari huyo wanapaswa kushitakiwa pia.

Muda mfupi baada ya kutolewa hukumu hiyo, mkuu wa chuo kikuu cha jimbo la Michigan (MSU) alikokuwa anafanya kazi Nassar kati ya mwaka 1997 na 2016, amejiuzulu.

Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.

Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.Haki miliki ya pichaAFP
Image caption
Lou Anna Simon amekuwa akikabiliwa na shinikizo kujiuzulu.
Bi Simon alikana taarifa kuwa MSU ilifahamu kuhusu tuhuma hizo za unyanyasaji lakini kilishindwa kuchukua hatua.

Katika taarifa yake alisema: "kwa waathiriwa, samahani yangu haiwezi kutosha, kuwa daktari aliyeaminika, aliyefahamika alikuwa ni mtu muovu kwa kweli, aliyewadhulumu kwa kutumia kigezo cha kuwatibu."

"Ushahidi wa wahanga wa unayanyasaji wa Nassar ni wa kusikitisha, kuvunja moyo na binafsi unaonitia kichefu chefu," aliongeza.

"Ushahidi wa wahanga wa unayanyasaji wa Nassar ni wa kusikitisha, kuvunja moyo na binafsi unaonitia kichefu chefu,"

Takriban wasichana 140 wamewasilisha kesi dhidi ya Nassar, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya daktarihuyo miaka kadhaa ya nyuma.

Taasisi hiyo ya michezo na chuo hicho zimekana kuwa kulikuwa na chochote cha kufichwa.

Hukumu ya Larry Naser inafuatia wiki ya ushuhuda kutoka kwa wanawake takribani mia moja na sitini, wakiwemo washindi wa medali ya dhahabu ya olympiki Biles, Aly Raisman, Gabby Douglas na McKayla Maroney

Mnangagwa: Nitampa Mafao Mazuri ya Kustaafu Robert Mugabe

0
0
Mnangagwa: Nitampa Mafao Mazuri ya Kustaafu Robert Mugabe
Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameiambia BBC kuwa, atampa malipo mazuri ya kustaafu Rais aliyeng`olewa mamlakani Robert Mugabe na mkewe.

Amesema kuwa Mugabe ataendelea kupokea mshahara wake na mafao mengine kama kawaida ikiwemo kusafiri katika kiwango cha kwanza kwenye ndege (first class), pamoja na kusafiri kwa gharama ya serikali.

Lakini Rais Mnangagwa amesema kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na asiyeweza kushtakiwa.

Na Amesema kuwa Zimbabwe itajiunga tena hivi kariubuni na mataifa ya jumuia ya madola.

'Hatujampa kinga mtu yoyote isipokua ambacho nimeahidi kwa rais aliyetangulia na baba wa taifa letu, rais Robert Mugabe ni kwamba tunampatia mafao na mshahara wake kama alivyokua akipata awali, usafiri, ofisi, ulinzi, na serikali yangu itamuwezesha kuenda Singapore kwenye matibabu, na vyote hivi mke wake pia ataviapata''.

Mnangagwa amesema pia serikali yake mpya inafanya jitahada kubwa za kupambana na rushwa.


'' Msimamo wangu ni kwamba Rushwa haiwezi kuvumiliwa hata kidogo, hatuwezi kabisa kuvumilia jambo kama hili , na kama mnafatilia mambo yanayotokea Zimbabwe kwa sasa , watu wengi wenye wadhifa mkubwa wamefikishwa mbele ya mahakama, na ni ndani ya miezi miwili tuu tayari tunawashughulikia watu wenye makossa ya rushwa''.

Mskini Wastara Bado Anahitaji Mchango Ili Akatibiwe "Nateseka Jamani Naomba Mchango Wako"

0
0
Mskini Wastara Bado Anahitaji Mchango Ili Akatibiwe "Nateseka Jamani Naomba Mchango Wako"
Hujafa hujaumbika! Wakati staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma akiendelea kuomba michango kwa Watanzania ili akatibiwe mguu nchini India, mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sidonia Ntabashigwa mkazi wa Salasala jijini Dar yupo hoi kitandani akisema, anaamini mateso anayopata ni makubwa mno kuliko hata ya msanii huyo.

Akizungumza na Amani mama huyo alisema, anateseka kitandani kwa miaka miwili sasa na hawezi kutembea kwani mguu mmoja umevunjika na mwingine viungo vimehama sehemu yake.


Mama huyo anaeleza kuwa, miaka miwili iliyopita akiwa katika stendi ya daladala Mbuyuni, Tegeta Dar, gari liliacha njia na kumgonga, ambapo alivunjika mguu ambao baadaye ulikatwa kwenye eneo la juu ya goti huku mguu mwingine ukiwa umegeuka yaani viungo vyake vikahama sehemu yake halisi.



“Sikuwa ni hili wala lile, nimejikalia kituoni nasubiri daladala ndipo ghafla nikashangaa gari limekuja kunigonga na baada ya hapo sikujitambua tena hadi nilipojikuta hospitali,” alisema mama huyo ambaye anaishi kwenye chumba kimoja akiwa na wanaye sita.



Mama huyo kwa masikitiko alieleza kwamba, alilazwa kwa muda mrefu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na baadaye aliruhusiwa kurudi nyumbani akapewa magongo ya kutembelea, lakini hawezi kuyatembelea kwa sababu mguu mwingine bado una tatizo kubwa.



“Nateseka sana yaani mateso yangu ni zaidi ya Wastara kwani siwezi kutembea wala kufanya kitu chochote.

“Hapa nina watoto sita, tunaishi kwenye chumba hiki kimoja pamoja na baba yao ambaye hana kazi, yaani hata choo chenyewe ni mpaka tukaombe kwa jirani, nina mateso makubwa sana jamani,” alisema mama huyo na kuongeza:



“Mimi naweza kusema haya mateso ninayoyapata yanazidi hata ya Wastara maana nimesoma kwamba yeye angalau hata aliweza kuwekewa huo mguu wa bandia, akawa anaendelea na shughuli zake za kila siku.



“Mimi hapa kama unavyoniona. Sina mguu wa bandia, siwezi kufanya shughuli za kila siku. Hapa kama unavyoniona ni mtu wa kujilaza tu katika hiki kigodoro changu,” alisema mama huyo.



Mama huyo aliendelea kueleza kuwa pamoja na mateso hayo bado mguu mmoja anatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha viungo, lakini amekosa fedha zinazotakiwa shilingi milioni moja.



Kutokana na mateso yake mama huyu anawaomba watanzania wote walioguswa na mateso aliyonayo wamsaidie kwa chochote walichonacho.



Kutoa ni moyo na si utajiri, kama umeguswa na mateso ya huyu mama na una chochote cha kumsaidia wasiliana naye kwa namba 0653659379.

Wema Sepetu Amtolea Povu Mke Nabii Tito Baada Kumtaka Awe Mke Mwenzie

0
0

 Wema Sepetu Amtolea Povu  Mke Nabii Tito Baada Kumtaka  Awe Mke Mwenzangu
Katika hali isiyotarajiwa, imeelezwa kuwa msanii nyota wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, amemlipua mke wa ‘Nabii Tito’ baada ya mwanamke huyo kumshawishi kupitia mitandaoni aolewe na nabii huyo.

Chanzo chetu makini kilisema kuwa, msanii huyo amekasirishwa na kitendo cha mke huyo kumshawishi kuolewa na mumewe anayeitwa Onesmo Machija ‘Nabii Tito’ (44).

“Wema Sepetu nakupenda sana hata Nabii Tito anakupenda sana, kwanza mzuri, una shepu nzuri hata katika mambo ya Kiafrika unaongoza kwa uzuri.

“Nabii Tito huyo kwa watu wasiomfahamu wanasema sio nabii lakini kwa mimi ninayemfahamu na kuishi naye naona mambo ya kinabii anayofanya, nakuomba ukubali hata mimi nakupenda sana, kwanza una shepu nzuri.



“Uwe mke mwenzangu, ukubali kuwa mke wa Nabii Tito. Sikia kilio cha mke wa nabii,” amesikika kwenye video mke huyo wa Nabii Tito akimbembeleza Wema.

Naye Nabii Tito kwenye video hiyohiyo amechombeza kwa kubembeleza kwamba Wema akubali kuwa mkewe ili kanisa lao likuwe.

Alipotafutwa Wema na kuulizwa kuhusiana na video hiyo alisema, ameiona na amekasirishwa na kile walichokifanya nabii huyo na mkewe.

“Kiukweli wameniudhi sana kwa kunidhalilisha. Nawasiliana na mwanasheria wangu ili nimburuze mahakamani mwanamke huyo,” alisema Wema.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, mapema wiki hii lilimkamata nabii huyo na kumfanyia mahojiano kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya na limesema mtu huyo ana matatizo ya akili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gillesi Muroto amesema Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la Dk. William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.

Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba, baada ya hapo Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika Kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.



“Kwa msingi huo, jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Milembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dk. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo ya akili,” alisema kamanda Muroto juzi na kusisitiza kuwa wanaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.

Kwa nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.


NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.


MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA.


MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.


NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,


Je unamali yako unauza hupati wateja?

Wasiliana nami 0716-263605


DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale

Tausi Mdegela na Amigo Mahaba Motomoto .... Soon Kuolewa Mke wa Pili

0
0
Tausi Mdegela na Amigo Mahaba Motomoto .... Soon  Kuolewa Mke wa Pili
Msanii wa filamu wa Tanzania mwenye muonekano wa kipekee na kipenzi cha watoto, Tausi Mdegela, ameutaarifu umma kuwa anatarajia kuolewa kuwa mke halali wa mpenzi wake wa siku nyingi ambaye ni msanii wa muziki wa taarabu, Prince Amigo.


Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Tausi amesema suala la ndoa ni mipango lakini ni jambo ambalo lipo, kwani tayari wamekuwa kwa muda mrefu kwenye mahusiano na mpenzi wake huyo ambaye ni mwanamuziki wa taarab, ambaye tayari ana mke wa kwanza.

“Ndoa ni mipango mtuombee Mungu tufike mbali, ni muda mrefu tumeanza tunaishi pamoja, ila Amigo ana mke mkubwa, kwa hiyo mimi nasubiria kuwa mke mdogo, hapa akiongezeka watatu ndio itakuwa mtihani, wawili tushatosha wengi wa nini, hapo ndo tutapigana sasa, na tukigundua kuna wa tatu hapo ndio litakuwa lingine, na mke mkubwa kashakubali”, amesema Tausi.

Tausi ameendelea kwa kusema kwamba yeye hajali maneno ya watu wanayosema kuhusu mahusiano yake hayo, kwani anachoangalia ni maisha yake na sio watu wanasema nini.



Maskini Aslay Amkumbuka Mama Yake Amuandika Waraka Mzito...... "Juzi Nilitamani Nikupigie Simu Nikuambie Yanayonisibu Ila Namba Yako Haipatikani"

0
0
Maskini Aslay Amkumbuka Mama Yake Amuandika Waraka...... "Juzi Nilitamani Nikupigie Simu Nikuambie Yanayonisibu Ila Namba Yako Haipatikani"
Muimbaji Aslay Isihaka ameandika waraka mkubwa kwa marehemu mama yake akimuelezea ugumu wa maisha na muziki wake tangu kutoweka kwake duniani.



Barua kwa Mama yangu kipenzi pamoja na mashabiki zangu.

“Jina langu ni Aslay Isihack, jina hili alinipa Mama yangu mwenyewe Bi. Mozza kutokana na maisha niliyopita ya Muziki wengi wananifahamu kwa jina la Aslay.

Hellow Mama najua unanisikia mwanao tangu uondoke life its so complicated kuliko nilivyodhania, kila kitu kwangu tabu nakosa sana ushauri wako natamani kuongea nawe japo hata siku moja lakini nafahamu kwa mapenzi ya Mola haiwezekani nakuombea kila la heri huko ulipo.

Japo kwasasa nimepata kibinti pacha wako, jina lake nimemuita Mozza I wish ungemuona mmefanana sana. Kuna kitu Mama nataka kukugusia juu ya ndoto yangu bado sana natamani kuwa msanii mkubwa kama Kaka zangu na Dada zangu walionitangulia kwenye Muziki. Ndoto niliyokuwa nakusimulia kila wakati tukila Chakula cha jioni.

Mama Kila kukicha Wananirushia mawe nisifike niendapo. Mawe yote Mama nimeyaokota najengea barabara nifike niendapo, hakuna wakunifuta mimi machozi yangu nalia kilio cha mtu mzima maumivu ndani kwa ndani.

Juzi nilitamani nikupigie simu nikuambie yanayonisibu mwanao, Namba yako haipatikani labda umeweka call busy unaniombea dua njema. Nimuambie nani yanayonisibu ndani ya Moyo wangu juu ya Mziki wangu na maisha yangu?

Mashabiki wangu ndiyo wananipa Ujasiri wa kupambana na kukomaa hivo hivo. Sikufaidika na kile nilichokifanya kwa zaidi ya miaka 15
Hata mimi ukiniuliza ilikuwaje nakosa cha kukujibu Mama nataka tukae kikao cha dharura, tuone ilikuwaje.

I feel inferior, najihisi mnyonge, Nawaza nitaanzia wapi?. I just feel hopless and more hopeless day by day. I dont know. Kila ninaposhika panageuka mwiba mchungu kwangu.
Natamani kujua kama unafahamu nanyanyaswa kisa Muziki wangu .

Kiukweli Mama siwezi kulalamika sanaa maana hata wakati napokuwa mpweke mashabiki zangu huniliwaza kwa kusapoti kazi zangu wamekuwa ndiyo faraja kwangu.

Ndiyo wananifanya niwe jasiri wa kuwatengenezea Muziki mzuri kila kukicha. Sometimes nikiwaza mwanangu ataishije, na familia nitaitunza vipi, bila Muziki?

Natumaini utanijibu basi hata ndotoni Mama kama barua yangu utaipokea.

Nimekukumbuka sana mwanao
Aslay.
Nakupenda Mama.”

Vanessa Mdee Afunguka Kuhusu Kutoa Albamu "Nimejitoa Muhanga kwa Hili"

0
0
Nimejitoa Muhanga kwa Hili- Vanessa Mdee
Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee amesema amejisikia faraja kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki albamu japokuwa anahisi amejitoa muhanga kwa maana hafahamu kama itakuja kumlipa.


Vanessa amebainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya muda mchache kupita tokea alipomaliza kufanya mapitio ya albamu yake iliyopewa jina la 'Money Monday' na kusema amesikia kelele nyingi kwa baadhi ya wasanii kwamba albamu bongo haiuzi.

"Nimefanya 'research' kwa muda mrefu sana na nimekugundua kwamba hakuna mfumo unao-support mauzo ya albamu lakini nikasema kama ninataka kukamilika kama msanii huko ninapoelekea na vitu ninavyotegemea kufanya sitaweza kuvikamilisha bila ya kuwa na 'CV' ya kusema kwamba nami nina albamu", alisema Vanessa.

Pamoja na hayo Vanessa ameendelea kwa kusema "mwisho wa mwaka huu 2018 nategemea kuachia nyingine jumla nitakuwa nazo mbili 'so' sijaweka uoga mbele nimeweka vitendaji kazi, 'i want people to see' nina uwezo wa kufanya vitu vingi na nimefanya 'risk'kwa sababu bado sijajua kama itanilipa lakini mpaka sasa hivi naona kama malipo yapo".

Kwa upande mwingine Vanessa amewashauri wasanii wenzake waache kusikiliza kelele za watu zinazodai kuwa albamu bongo hazifanyi vizuri huku akiwaomba mashabiki wake kuendelea kumpa ushirikiano wa kununua kazi yake hiyo ambayo inauzwa kwa njia ya mitandaoni na mkononi.

Mwigulu Nchemba Afanya Maamuzi Magumu Aagiza Kukamatwa Wanaowapeleka Vijana Nchi Kutafuta Ajira

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza kutafutwa na kukamatwa mara moja kwa watu wote wanaohusika na uteswaji wa vijana wanaopelekwa nje ya nchi kutafuta ajira.

Dkt. Mwigulu amesema hayo leo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari baada ya kupata taarifa ya mateso wanayopata baadhi ya wananchi wa Tanzania wanaokwenda kufanya kazi tofauti tofauti nje ya nchi na kusema wameshafanya mawasiliano na Wizara zote zinazohusika na wameshakubaliana kila mmoja kuchukua hatua kulingana na wizara yake.

"Wale watu wanaoweka rehani vijana wetu, wamekuwa wakikimbia hapa na pale na ambao bado hawajakamatwa mpaka sasa waendelee kusakwa wote na wafikishwe katika mkono wa sheria ili sheria iweze kufuata mkondo wake kwa vitendo hivyo vya kinyama na kuwapeleka vijana wetu katika vitendo vya kinyama na kusababisha majonzi kwa familia husika",alisema Dkt. Mwigulu.

Pamoja na hayo na Waziri Nchemba amesema matatizo wanayoyapata vijana hao kwa kisingizio cha kupatiwa kazi nje ya nchi mpaka sasa yamekuwa makubwa mno.

"Tumeona vijana wakiwa wamefungwa miguu vichwa chini na mikono yote huku wakitandikwa viboko kwa madai ya kwamba miongoni mwao kuna aliyewapeleka kuwapa kazi nzuri ya kufanya lakini kwa bahati mbaya wakifika huko wanawekwa rehani kwamba hawataondolewa pale walipo mpaka wale waliowapeleka wakiwa wameshamaliza kupeleka fedha za dawa za kulevya", alisisitiza Waziri Mwigulu Nchemba.

Baada ya Kubwagwa na Heri Muziki Diva Anyapia Penzi la Soudy Brown

0
0
Baada ya Kubwagwa na Heri Muziki Diva Anyapia Penzi la Soudy Brown
Baada ya kubwagana na mpenzi wake Heri Muziki, Diva amefunguka mipango yake ya kuwa na Soudy Brown.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm amesema kwa sasa yupo tayari kubadili dini kwa ajili ya Soudy Brown ambaye ni mtangazaji mwenzake katika kituo hicho.

“Soudy Brown ndio kila kitu kwangu niseme hivyo, urafiki wangu uko karibu kupita kiasi like hakuna kama Soudy I think he my only true love,” Diva ameiambia Bongo5.

“Kwa sababu yeye ni mtoto wa kislam akiniongeza kwenye list nitabadilisha dini na nitaitwa Amina,” amesisitiza.

Hata hivyo ameongeza kuwa tayari anamjua mpenzi wake Soudy Brown ila kitu ambacho watakaa na kujadili. Diva kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Waambie’ ambao amewashirikisha  Mr. Paul na Mwana FA.

Mr Blue Akataa Tuzo za Tanzania " Kuna Tuzo Gani ya Kunipa Mimi"

0
0
Mr Blue Akataa Tuzo za Tanzania " Kuna Tuzo Gani ya Kunipa Mimi"
Msanii wa muziki Bongo, Mr. Blue amesema kwa sasa hataki tena kupatiwa tuzo kutoka Bongo kutokana na kunyimwa kwa muda mrefu.

Mr. Blue ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa amekuwa kwenye game kwa muda mrefu na hakupatiwa tuzo na alipofika kwa sasa kimuziki haoni kama kuna tuzo anaweza kupatiwa.

“Sitaki tena tuzo, yaani is too long nimesubiri kwa muda mrefu, Tanzania I don’t need any tuzo, kuna tuzo gani ya kunipa mimi, utanipa tuzo ya wimbo bora wa mwaka huu ‘Mbwa Koko’ hizo nyingine za nyuma unazifanyia nini?,” amesema.

“Kwenye game nimeanza toka nimekuwa mtoto mpaka nimekuwa na watoto bado nasubiri, siwezi tena kuwa na hamu ya kuitaka tuzo sasa hivi ninachoangalia ni mambo mengine, niwepo tu hata sifanyi tena kwa ajili yangu,” ameongeza.

Mr. Blue kwa sasa anafanya vizuri na ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Mbwa Mkoko.

Tundu Lissu: Nimemtolewa Risasi Nyingine Mwilini

0
0
Tundu Lissu: Nimemtolewa  Risasi Nyingine Mwilini
Siku 35 baada ya Tundu Lissu kusema mwili wake bado una risasi moja baada ya kutolewa nyingine 15, jana mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema) amelieleza Mwananchi kuwa madaktari wamemtoa kipande cha risasi kilichokuwa mwilini mwake.

Hata hivyo, mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 akiwa ndani ya gari lililokuwa nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7 mwaka jana, alisema chuma hicho ni tofauti na risasi iliyonayo mwilini, ambayo alielezwa na madaktari wa Hospitali ya Nairobi, Kenya kuwa iko sehemu mbaya, lakini isipotolewa haiwezi kumdhuru.

“Leo (jana) madaktari wamenitoa kipande cha chuma katika sehemu ya makalio ambacho nilipokuwa Nairobi (Kenya) madaktari walikiona lakini kilikuwa ndani ya nyama wakashindwa kukitoa,” alisema Lissu kwa njia ya simu kutoka Ubelgiji ambako alipelekwa Januari 7 kwa ajili ya tiba ya mazoezi.

“Kipande hiki kilisogea na wamekitoa. Ni tofauti na ile risasi ambayo iko mwilini mwangu.”

Akieleza kiundani kuhusu hali yake, Lissu alisema anaendelea vizuri.

“Huu mkono wa kushoto ambao ulikuwa na tatizo, wameunyoosha na kuufanyia mazoezi kweli kweli na huu mguu wa kulia ambao ndio wenye tatizo, unaendelea vyema,” alisema.

“Huku ni mazoezi tu. Kwa siku nafanya mazoezi kwa saa nne, Naingia saa 3:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi, narudi tena saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana. Mwisho naingia mazoezini saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 jioni. Hiyo ndiyo ratiba yangu kwa siku.”

Alisema katika mazoezi hayo anatumia magongo maalumu pamoja na kiti cha magurudumu.

“Mfano, huu mguu wa kulia natakiwa kuukanyagia kwa kilo 20 hadi 25 katika mzani na mimi nina kama kilo 90. Ninapoukanyagia ninaulizwa kama unauma, ikiwa sijasikia maumivu ina maana sijafanya kitu, kwa hiyo ni kazi kwelikweli,” alisema.

Kuhusu muda ambao anatakiwa kufanya mazoezi hayo mpaka atakaporejea katika hali yake ya kawaida, Lissu alisema bado hajajua.

“Ah bwana we, hapa madaktari wamegoma kunieleza hilo, lakini wameangalia katika maungio ya goti la mguu wa kulia kuna mfupa haujaunga vizuri, ni lini utaunga hilo sijajua,” alisema.

Mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya siku hiyo usiku.

Desemba 21 mwaka jana wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam, Lissu alisema madaktari wa Nairobi walimueleza kuwa risasi iliyokuwa imesalia mwili haina madhara.

Alisema risasi saba zilitolewa na madaktari hao, jambo lililomaanisha kuwa risasi nyingine nane, zilitolewa na madaktari wa Tanzania, saa chache baada ya kushambuliwa alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.   

Sugu na Wenzake Wamkataa Hakimu Anayesimamia Shauri Lao

0
0
Sugu na Wenzake Wamkataa Hakimu Anayesimamia Shauri Lao
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe Joseph Mbilinyi aka Sugu pamoja na mwenzake Emmanuel Masonga wamemkataa Hakimu anayesikiliza shauri lao kwa madai kuwa hawana imani naye baada ya kuwanyima dhamana kinyume cha sheria.

Kesi hiyo imeaihirishwa kwa saa kwaajili ya kusubiri uamuzi iwapo Hakimu huyo ataendelea nayo ama laa.

Siku ya jana Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Aikael Mbowe, alifika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli.

Walichosema TAKUKURU Baada ya Kukamilisha Upelelezi Kesi ya Malinzi

0
0
Walichosema TAKUKURU Baada ya Kukamilisha Upelelezi Kesi ya Malinzi
January 25, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake umekamilika.

Mbali ya Malinzi, wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga.

Wakili wa TAKUKURU, Leornad Swai alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa, pia jalada la kesi hiyo wameshalifanyia kazi ambapo upelelezi wamekamilisha.

Swai amedai kuwa jalada la kesi hiyo watalirudisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kama alivyowaagiza walirudishe kwake ili alikague tena baada ya upelelezi wao kukamilika.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi February 8,2018 kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418 na washtakiwa wote wamerudishwa rumande

Mwanza: Deogratius Kisandu Akamatwa na Polisi kwa Kosa la Kuandika Matusi ya Nguoni Facebook

0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limemkamata Deogratius Kisandu ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkolani kwa makosa ya kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuandika matusi.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutumia ukurasa wake wa Facebook kuandika matusi ya nguoni kwa takribani wiki nzima...Pia amekuwa akiandika ujumbe mbali mbali za uchochezi na zisizoeleweka kupitia mtandao huo

Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images