Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live

Njoo Ushuhudie Miujiza ya Kamgambile na Bi Khadija, Wana Uwezo Mkubwa Katika Kutiba Magonjwa na Kurudisha Wapenzi

$
0
0

NJOO USHUHUDIE MIUJIZA YA KAMGAMBILE NA BI KHADIJA WANA UWEZO MKUBWA KATIKA KAZI ZAO JE? UMEACHWA NA MPENZI WAKO JE? NA HUJUI NAMNA YAKUMRUDISHA? WAONE HARAKA WAKUSAIDIE KAMGAMBILE NA BI KHADIJA HURUDISHA MAHUSIANO NDANI YA MASAA (12) TU

DAWAZAO NI NZURI ZENYE KUONYESHA MAFANIKIO KWAHARAKA ANATIBU KWAMITI SHAMBA NAKITABU CHA QUR AN TUKUFU WANA UWEZO MKUBWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE UVIMBE TUMBONI KIFAFA VIDONDA VYATUMBO TEZI PUMU KISUKARI MIGUU KUWAKA MOTO NAKUFA GANZI WANA UWEZO MKUBWA WAKURUDISHA MTU ALIE POTEA KIMAZINGIRA ( MSUKURE) KAMA UMEIBIWA AMA KUDHULUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASAA (72) TU PATA UTAJIRI USIOKUWA NAMASHARITI KWAYULE ANE TAKA DAWA YA LIMBWATA KUMTAWALA MPEZI WAKO UNAVYO TAKA DAWA YA NGUVU ZAKIUME WANAYO KUONGEZA UUME SAIZI UPENDAYO NCHI 5-6-7-8-9 NIWEWETU UNAVYOTAKA WANAKUSAIDIA KUSAFISHA NYOTA NAKUPATA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NANYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA MALI BILA YA MASHARITI HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO DUNIANI ACHAKUTESEKA

CALLING +255719866726

WHATSAPP CALLING +255768455841 KARIBUNI WOTE WANAO TAKA HUDUMA HII

Breaking Newz: Nabii Tito Afikishwa Mahakamani Mkoani Dodoma

$
0
0
Breaking Newz: Nabii Tito Afikishwa Mahakamani Mkoani Dodoma
Baada ya kumkamata na kudai huenda ni kichaa, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma leo limemfikisha mahakamani Onesmo Machibya maarufu kama Nabii Tito. Haijafahamika kosa analoshtakiwa nalo.

Nilipigiwa Simu na Nasbu ‘Diamond’ Akaniomba Nikamkubalia- Wema Sepetu

$
0
0
“Nilipigiwa Simu na Nasbu ‘Diamond’ Akaniomba Nikamkubalia- Wema Sepetu
MSANII wa filamu Bongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa alipigiwa simu na X wake ambaye ni Diamond Platinumz akimuomba afike Hyatt Regency Hotel kwa ajili ya kujumuika na watu wengine kwenye hafla ya kumtambulisha msanii mpya wa WCB, Maromboso ambapo hafla hiyo ilifanyika usiku wa kuamia leo.



“Nilipigiwa simu na Nasbu ‘Diamond’ akaniomba nije kwenye hafla ya kumtambulisha msanii wao mpya wa WCB, nikakubali nikamwambia haina shida nitakuja, akaniuliza idadi ya watu nitakaokuja nao nikamwambia nitafika na marafiki zangu na timu yangu. Hivyo nimefurahi leo kujumuika na WCB kuwapa kampani,” alisema Wema.

Mtulia Afunguka Kuhusu Uamuzi Wake wa Kuhama Chama "Nimefanya Maamuzi ya Kiume"

$
0
0
Mtulia Afunguka Kuhusu Uamuzi Wake wa Kuhama Chama "Nimefanya Maamuzi ya Kiume"
Mgombea wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Maulid Said Mtulia amesema amefanya maamuzi ya kiume ya yeye kuhamia chama hicho kwa sasa kwa maana wapo wengi wanataka kufanya hivyo lakini wameshindwa kwa madai wanasubiri kulipwa kiunua mgongo.


Mtulia ameeleza hayo wakati alipokuwa anaendelea kujinadi kwa wananchi wa jimbo la Kinondoni ambalo hapo awali alikuwa analishikilia yeye kupitia chama chake cha CUF kabla ya kujivua uanachama wake na kuenda kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kuijenga nchi.

"Kujiuzulu Ubunge sio mchezo, nimefanya maamuzi ya kiume maana kuna wenzangu wengine mpaka sasa hawawezi kutoka kwa sababu wanasubiri kiunua mgongo. Sasa kijana kama mimi nikae pale nisubirie kiunua mgongo hivi kweli ntaweza kuishi kwa kusubiri kiunua mgongo", alisema Mtulia.

Aidha, Mtulia amesema amejinusuru kwa mengi kukihama chama chake cha awali ili aweze kuwapigania wananchi wa jimbo hilo kwa maana hapo awali alikuwa anashindwa kuyafanya majukumu yake vizuri kutokana na mgawanyiko ndani ya chama chao.

"Wenzangu Wabunge 10 walifukuzwa uanachama CUF hamkujua, mlisubiri nifukuzwe au mna roho mbaya na mimi. Hivi nilipo hapa nimeruka kwa kujinusuru nashukuru nipo salama na nimesimama tena kwa wana kinondoni ninaomba kugombea Ubunge nyie mnanuna kitu gani au huo ndio usaliti. Lakini jambo jingine mimi nimekuja CCM kwa sababu nampenda Magufuli balaah", aliuliza Mtulia.

Pamoja na hayo, Mtulia aliwashangaza baadhi ya watu kwa kusema ametumikia Ubunge ndani ya miaka miwili na kushiriki vikao vyote vya Bunge lakini hakuweza kuwa na namba ya Rais Magufuli.

"Leo ninawaambia siri yangu, nilivyokuwa Mbunge miaka miwili namba ya Rais Magufuli sikuwa nayo lakini sasa namba ninayo. Hivyo wanakinondoni mnataka nini kama mnataka maendeleo ndio haya", alisisitiza Mtulia.

Kwa upande mwingine, Mtulia amewaambia wananchi wa Jimbo la Kinondoni endapo watamchagua yeye katika chaguzi hizo za marudio zilizopangwa kufanyika mapema Februari 17 mwaka 2018 basi watakuwa wametengeneza daraja la kujipatia maendeleo.

Jafo Atoa Agizo Hili kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri (DED)

$
0
0

 JafoAtoa Agizo Hili kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri (DED)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri (DED) kutunza siri za Serikali.

Jafo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 29,2018 mjini Dodoma alipofungua mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mikoa sita.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa ambayo yanatolewa kwa viongozi wa kada hiyo.

Waziri Jafo amesema ujenzi wa Serikali utakuwa mzuri iwapo viongozi hao watakuwa makini na kutunza siri.

"Hivi unakuwaje wewe mkurugenzi au mkuu wa wilaya unapeleka siri za Serikali kwenye mitandao ya kijamii na nyingi unaziona kwenye WhatsApp, inatia aibu sana," amesema Jafo.

Amewataka wakurugenzi kujipambanua na kusimamia miradi ya maendeleo katika kukusanya mapato na kuyatumia vyema na hasa ya ndani.

Jafo amesema tatizo kubwa kwa wakurugenzi ni kutofanya uamuzi kwa haraka

Kazi ya Mbunge si Kwenda Kumtetea Rais Bali Kutetea Wananchi Waliompa Kura- Sumaye

$
0
0
Kazi ya Mbunge si Kwenda Kumtetea Rais Bali Kutetea Wananchi Waliompa Kura- Sumaye
Waziri Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais hawakutambua majukumu yao.


Sumaye amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge.

"Kazi ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais. Watu ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona hayo mambo wewe kama umehama maana yake ulikuwa uelewi maana ya kuwa Mbunge" alisisitiza Sumaye

Mbali na hilo Sumaye alidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa hakijali tena maslahi ya wananchi wake kwa kuwa kimeshika madaraka kwa muda mrefu ndiyo maana wameweza kumrudisha Mtulia kugombea kwenye jimbo la Kinondoni bila kujali mtu huyo amesababisha fedha za wananchi zaidi ya bilioni moja ziteketee kwenye uchaguzi wa marudio wakati fedha hizo zingeweza kutumika katika kufanya mambo ya maendeleo kwa wananchi.

Watu Wengi Wajitokeza Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Kupata Msaada wa Kisheria

$
0
0
Watu Wengi Wajitokeza Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Kupata Msaada wa Kisheria
Wananchi hao wametoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, huku baadhi wakitoka Rufiji mkoani Pwani ambao wameandaliwa utaratibu maalumu.

Baadhi yao wamesema leo Jumatatu Januari 29,2018 kuwa migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na wenyeviti wa mitaa wanaopokea rushwa na kuwapendelea wenye fedha nyingi.

Mkazi wa eneo la Chasimba wilayani Kinondoni, Bakari Mussa amesema mgogoro kati yake na aliyevamia kiwanja chake uliamuliwa na Mahakama naye alishinda lakini amejitokeza mtu wa tatu anayedai aliuziwa eneo hilo na aliyeshindwa kesi.

"Tumekuja kupata msaada wa kisheria kuhusu masuala ya ardhi, tumeshindwa kuendeleza ardhi yetu kwa sababu ya zuio la Mahakama aliloweka huyo mtu. Ninatarajia kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa," amesema Mussa.

Kiongozi wa timu ya wanasheria, Georgia Kamina amesema mwamko wa wananchi ni mkubwa na waliojitokeza wote watasikilizwa.

Amesema timu yake ina wanasheria 150 kutoka Shule ya Sheria, ustawi wa jamii, maofisa kazi, Jeshi la Polisi na wanasheria wengine wa kujitegemea, hivyo wana uwezo wa kuwamudu wote.

Kamina amesema wengi waliosikilizwa wana matatizo ya ardhi, mirathi na ajira, ambao baada ya kusikilizwa hupewa ushauri wa kitaalamu wa namna ya kumaliza matatizo yanayowakabili.

"Tutatoa huduma wiki nzima kuanzia leo Januari 29 hadi Februari 2,2018. Tumejitolea kumsaidia mkuu wa mkoa kuifanya kazi hii," amesema.

Awali, akizungumza na wanasheria hao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka kutohukumu wananchi wanaowasikiliza badala yake watoe ushauri wa kitaalamu.

Amesema mwisho wa siku waandae ripoti kumshauri hatua za kuchukua zilizo ndani ya mamlaka yake na kubainisha njia nyingine zilizo nje ya mamlaka yake.

Meya wa Jiji Afunguka Kuhusu Dereva Wake Kudaiwa Kutaka Kufanya Fujo Ofisi za CCM

$
0
0
Meya wa Jiji Afunguka Kuhusu Dereva Wake Kudaiwa Kutaka Kufanya Fujo Ofisi za CCM
Moja ya Stori kubwa Leo January 29, 2018 ni inayomhusu Meya wa Dar es salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Isaya Mwita ambayo inahusiana na gari analotumia kuonekana katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) na kusemekana anakihujumu chama hicho.

‘Kuna tatizo limejitokeza baada ya gari yangu kukutwa kwenye ofisi za CCM Mkwajuni, sasa dereva wangu amejikuta katika sakata hili, nataka niwaambie wana-DSM wote kwamba kwanza ofisi za ccm zinatumika kulaza magari ya Umma, kiukweli hakukuwa nia yoyote ovu iliyokuwa imepangwa”-Isaya Mwita

Wahusika Wakuu Mpango wa Kumuapisha Odinga Kuongoza Kenya

$
0
0
Wahusika Wakuu Mpango wa Kumuapisha Odinga Kuongoza Kenya
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga amekuwa akisisitiza kwamba ataendelea na mpango wake wa kuapishwa kuongoza Kenya baada yake kutangaza kwamba hamtambui Bw Uhuru Kenyatta kama kiongozi aliyechaguliwa kwa njia halali.

Raila Amolo Odinga ni kiongozi wa muda mrefu Kenya ambaye amehusishwa na harakati za kupigania mageuzi ya kisiasa nchini humo.

Amewania urais nchini Kenya mara nne bila mafanikio, na ya tano ingawa alikuwa kwenye karatasi za kupigia kura, alisusia.

Aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa Kenya, wadhifa ulioundwa kufuatia Mkataba wa Kitaifa ulioafikiwa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, ambapo aligawana mamlaka na Rais Mwai Kibaki.

Mwaka 2017, Bw Odinga alikuwa miongoni mwa viongozi watano waliojiita Pentagon ambao wanaongoza muungano wa umoja wa vyama vya upinzani, National Super Alliance (NASA).

Bw Odinga aliishi kukamatwa na kuachiliwa mara kwa mara tangu mwaka 1982 hadi 1991 kwa harakati zake za kupigania mageuzi wakati wa muhula wa pili wa utawala wa rais Daniel arap Moi.

Odinga apendekeza serikali ya muda iundwe Kenya
Amekuwa akisema lengo lake kuu ni kufanikisha mageuzi ya kisiasa Kenya na pia kumaliza ufisadi.

Bw Odinga ni mwanasiasa anayesifika sana kwa ushawishi wake kisiasa na amekuwa katika msitari wa mbele kuunda vyama vya miungano na wanasiasa ambao, wengine wakati mmoja walikuwa mahasimu wake.

Agosti 2017, uchaguzi ulipofanyika, tume ya uchaguzi ilitangaza kwamba alikuwa ameshindwa na Rais Kenyatta.

Alipinga matokeo hayo Mahakama ya Juu na uchaguzi huo ukafutiliwa mbali na uchaguzi mpya kuandaliwa tarehe 26 Oktoba.

Lakini Bw Odinga alisusia uchaguzi huo akisisitiza kwamba mageuzi yalihitajika katika tume ya uchaguzi kabla ya uchaguzi huru na wa haki kufanyika.

Mahakama ya Juu ilipoidhinisha kuchaguliwa kwa Bw Kenyatta na baadaye akaapishwa tarehe 28 Novemba, Bw Odinga alisema kamwe kwamba hatamtambua kama kiongozi aliyechaguliwa na wananchi Kenya.

Kalonzo Musyoka ni kiongozi wa chama cha Wiper Democratic Movement of Kenya na kiongozi mwenza wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa).

Ni makamu wa rais wa zamani, ambaye alihudumu chini ya Rais Mwai Kibaki kati ya 2008 hadi 2013.

Alikuwa mgombea mwenza wa Bw Raila Odinga katika uchaguzi mkuu wa 2013 (Coalition for Reforms and Democracy - Cord) na tena mwaka 2017.

Marekani yamuonya Odinga dhidi ya kujiapisha Kenya
Aliwania urais mwaka 2007 kupitia chama cha ODM-Kenya lakini akashindwa.

Alikuwa amehudumu serikalini kama waziri wa mambo ya nje 1993 hadi 1998 na tena 2003 hadi 2004.

Alihudumu kama waziri wa elimu 1998 he na baadaye kama waziri wa utalii 2001 hadi 2002.

Musyoka alikuwa ameteuliwa kuwa waziri wa mazingira mwaka 2004 lakini 2005 akapinga rasimu ya katiba iliyokuwa inaungwa mkono na serikali ya Rais Mwai Kibaki na baadaye akafutwa kazi.

Amekuwa akisisitiza kwamba ni sharti Rais Kenyatta na Naibu Rais William Ruto wakubali kushauriana na serikali la sivyo mambo 'yatakuwa mabaya'.

Musalia Mudavadi
Musalia Mudavadi ndiye makamu wa rais aliyehudumu muda mfupi zaidi Kenya
Image caption
Musalia Mudavadi ndiye makamu wa rais aliyehudumu muda mfupi zaidi Kenya
Musalia Mudavadi ni kiongozi wa Amani National Congress (ANC) na aliwania urais mwaka 2013 lakini akamaliza wa tatu nyuma ya Bw Odinga na Bw Kenyatta.

Amekuwa mmoja wa viongozi wenza wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa).

Bw Mudavadi ni mwanasiasa wa muda mrefu nchini Kenya ambaye anashikilia rekodi ya kuwa makamu wa rais aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi tangu uhuru - miezi miwili.

Alihudumu kama naibu waziri mkuu mwaka 2008 hadi 2013.

Amewahi kushikilia nyadhifa mbalimbali katika baraza la mawaziri, zikiwemo Waziri wa Fedha chini ya Rais Daniel arap Moi.

Kwa muda mrefu, amekuwa akitazamwa kama watu walio katika nafasi nzuri ya kuwa rais nchini Kenya.

Bw Wetangula amewahi kuhudumu kama waziri wa mambo ya nje
Ni mmoja wa viongozi wenza wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa) ambaye amekuwa kiongozi wa walio wachache Bunge la Seneti tangu 2013.

Amekuwa akihudumu katika Bunge la Seneti kama seneta wa jimbo la Bungoma, magharibi mwa Kenya.

Awali, alikuwa kiongozi mwenza katika muungano wa upinzani wa awali wa Coalition for Reform and Democracy (Cord) ambao Bw Odinga aliutumia kuwania urais mwaka 2013.

Bw Wetangula amekuwa kiongozi wa chama cha Forum for the Restoration of Democracy-Kenya (Ford-Kenya) tangu 2011 ambacho 2013 kilikuwa kwenye muungano wa Cord na mwaka 2017 katika muungano wa Nasa.

Alijiingiza katika siasa mwaka 2003 alipochaguliwa mbunge wa Sirisia, magharibi mwa Kenya na kuhudumu tangu 2012.

Alihudumu kama maziri msaidizi wizara ya mambo ya nje kati ya 2003 na 2008 ambapo aliteuliwa waziri wa mambo ya nje hadi 2012.

Alikuwa mmoja wa wajumbe wakuu upande wa chama cha PNU chake Mwai Kibaki wakati wa mazungumzo yaliyoongozwa na Kofi Annan ya kumaliza mzozo wa baada ya uchaguzi wa 2017.
James Aggrey Bob Orengo ni wakili na mwanasiasa wa muda mrefu, ambaye alishiriki harakati za kupigania mageuzi ya kisiasa miaka ya 1980 na 1990 na aliwahi kufungwa jela wakati wa utawala wa Daniel arap Moi.

Alichaguliwa kuwa mbunge wa eneo la Ugenya akiwa na miaka 29, wakati huo akiwa mbunge wa umri mdogo zaidi kuchaguliwa. Alihudumu kama mbunge wa eneo hilo mara kwa mara.

Aliwania urais mwaka 2002 akitumia chama cha Social Democratic Party (SDP) lakini akamaliza wa nne.

Bw Orengo ni mmoja wa mawakili ambao walihusika sana wakati wa kesi ya Bw Odinga ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 Agosti, 2017.

Mara kwa mara hutumiwa kutoa msimamo wa muungano wa upinzani wa Nasa.

Raia wa Nigeria Akamatwa na Dawa za Kulevya Aina ya Cocaine

$
0
0
Raia wa Nigeria Akamatwa na Dawa za Kulevya Aina ya Cocaine
Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege jijini Dar es Salaam linamshikilia raia wa Nigeria akituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Christian Ugbechi (26), anadaiwa kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kwa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na pipi 59 zenye uzito wa zaidi gramu 800.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema leo Jumatatu Januari 29,2018 kuwa mtuhumiwa anaishi na kufanya kazi nchini Ufaransa.

Amesema alikuwa akisafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nchini Ufaransa.

"Tumemkamata mtuhumiwa akiwa na pipi 59, kati ya hizo 56 alizificha kwenye soksi na tatu amezitoa leo kwa njia ya haja kubwa. Yupo chini ya uangalizi maalumu,” amesema Mbushi.

Basi la Kampuni ya Tahmeed Lateketea kwa Moto

$
0
0
Basi la Kampuni ya Tahmeed Lateketea kwa Moto
Basi la kampuni ya Tahmeed ambalo linafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa Nairobi limeteketea moto katika kijiji cha Matumbi mkoani Tanga leo.


Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa hakuna abiria ambaye amepata madhara na moto huo ulioteketeza basi hilo.

"Ni kweli basi hilo limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kupata madhara yoyote kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiri ambao walikuwepo kwenye basi hilo kama 15 hivi wote waliweza kushuka mapema kabla ya moto kushika gari zima" alisema Wakulymba

Mmh! Zari Kiboko Ampa Ujumbe Huu Mama Diamond “Fanya Tuhame Guest House Tumuachie Mwanao”

$
0
0
 Mmh! Zari Kiboko Ampa Ujumbe Huu Mama Diamond “Fanya tuhame Guest House tumuachie mwanao”
Bado inaonekana ishu ya Diamond Platnumz kudaiwa kulala na wasichana wengine nyumbani kwake Madale, mama watoto wake Zari The Boss Lady hajaichukulia poa na inadaiwa kuwa amekasirishwa na tuhuma hizo zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.

Diamond siku kadhaa zilizopita alidaiwa kupeleka msichana mwingine na kulala nae nyumbani kwake Madale, ila baada ya kuenea kwa video clip ikimuonesha msichana huyo akiwa Madale, Zari alionesha kukasirishwa na kuandika snapchat “Ati Madale State lodge au Madale Guest house?”


Baada ya siku kadhaa kupita baadhi ya mashabiki waliamini inawezekana ishu hiyo imepita ila comment ya Zari katika post ya instagram ya mama Diamond inaonesha amekasirika bado, hiyo ni baada ya ku-coment katika picha ya Mama Diamond aliyopost na kuandika “Kubwa la maadui” ikimuonesha Mama Diamond akiwa Madale lakini Zari akacomment “Fanya tuhame Guest House tumuachie mwanao”

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Kiume ( Super Shafti)

$
0
0
DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO YA KIUME ( SUPER SHAFITI) NI DAWA YENYE UWEZO MKUBWA WAKUTIBU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


 (SUPER SHAFITI ni dawa ya asili yenye uwezo mkubwa wa kuogeza nguvu za kiume maradufu
(1) itakufanya uwe na nguvu za ajabu ukiwa unafanya ntedo la ndoa
(2) inaogeza hamu ya kurudia ntedo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka
( 3) itakufanya uchelewe kufika kileleni dani ya dk 30
( 4)  itaimalisha milija ya uume iliyo legea au kusinyaa
(5) lnarefusha na kunenepesha uume saizi utakavyo kuazia ichi 1-8 unene sm 2-4
 (6) itakupa nguvu za kusimamiasha uume wako barabara kama_ msumari wakati wa ntedo la ndoa
(7) inasaidia kusafisha mishipa. ya kwenye uume na hivyo kusaidia Katika kuongeza kasi ya msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume
(8) usaidia kuurudisha nje uume ulioingia ndani
(9) inasaidia kuogeza manii nyingi ambazo vina viini vya uzazi
(10)usaidia kutibu madhara ya punyeto ,matumizi makali ya  madawa ya kizugu mirungi bangi na sigara

KWA NINI BAADHI YA WANAUME WENGI WANA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA KUWA NA MAUMBILE MADOGO YA KIUME NINI CHANZO CHAKE?

ni kutokana na magonjwa megi kuongezeka yakiwemo kisukari presha ya kupanda na kushuka upigaji wa punyeto wa mda mrefu magonjwa ya moyo ngiri ya kuviba korondani vidonda vya tumbo
Msongo wa mawazo  tumbo kuuguruma kujaa ngesi kutopata choo vinzuri maumivu ya mgongo kiuno na tumiaji wa madawa makali ya kizungu ya kuongeza nguvu za kiume kuzaliwa na chango linaloshabulia neva za ukuwaji wa uume utumiaji wa mirungi bangi sigara na nk  tunapenda kuwatangazia wasomaji, wa makala zetu kuwa tunazo dawa nzuri za asili ambazo hazina mazala na zinazotibu na kuponyesha matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na maumbile ya kiume

NA TUNATIBU MAGONJWA YOTE SUGU KAMA KISUKARI PRESHA AINA YOTE UGONJWA WA MOYO SITRUKO KWIKWI KICHOMI MINGUU KUFA NGAZI ASIMA NK MZEE ISAYA ANAPATIKANA MAGOMENI MIKUMI KARIBU NA KANISA  TUMAINI HEBRAST CLINI NDIYO JIBU NA SULULISHO YA MATATIZO YOTE

PIGA simu 0745495181 au 0682644040

Kwa watu wa mikoa huduma utatumiwa na watu wa nje ya nchi utazipata dsm kama huna nafasi ya kufika ofisini kwetu utaletewa popote ulipo

BREAKING: Dk Wilbrod Slaa Akutana na Rais Magufuli leo Ikulu Jijini Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Mhe. Dkt. Wilbrod Peter Slaa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya Mazungumzo hayo Balozi Mteule Mhe. Dkt. Slaa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Balozi na ameahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Mhe. Dkt. Slaa amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora wenye maono na uthubutu wa kutekeleza mambo makubwa yenye maslahi kwa nchi ikiwemo miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), ujenzi wa daraja la juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela (Tazara), mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge) na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

“Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, na mimi Dkt. Slaa nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naona kuna upungufu.

“Leo ninasema ninafurahi yale niliyokuwa napigia kelele yanatekelezwa kwa sababu nimeyaona, sasa kitu kikubwa ni macho, ushabiki katika maendeleo hauna tija, ushabiki katika siasa nao hauna tija, kama nilivyowahi kueleza huko nyuma siasa ni sayansi, wapo wanaofikiri siasa ni upotoshaji na siasa ni udanganyifu lakini siasa ni sayansi, na siasa kama ni sayansi ina misingi yake inayohitaji kusimamiwa, na misingi yake ni nini kilikuwa ni tatizo na tatizo hilo linatatuliwa kwa misingi ipi, sasa haya tunayoyasema ni hivi, tulikuwa na tatizo la umeme, Stieglers’ Gorge inaanza kujengwa, na miradi mingine mikubwa inatekelezwa, haya ndio mambo ya msingi” amesema Mhe. Dkt. Slaa.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Dkt. Slaa kwa moyo wake wa kizalendo na amesema aliamua kumteua kuwa Balozi kwa kuwa anatambua kuwa ataweza kupigania maslahi ya Tanzania popote atakapopangiwa kuiwakilisha.

“Dkt. Slaa alinijulisha kuwa anakuja na akaomba akija angependa kuja kuniona na nikampangia leo, tumezungumza mambo mengi na ameniahidi kuwa atakwenda kufanya kazi yake vizuri kwenye nchi atakayokwenda kuwa Balozi.

“Mhe. Dkt. Wilbrod Slaa ni mtu safi, anazungumza kutoka moyoni na anaipenda Tanzania na mimi kutokana na moyo wake wa kuchukia ufisadi na kuchukia wizi nikaamua kumteua kuwa Balozi” Amesema Mhe. Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na maafisa wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wanastaafu baada ya kutimiza umri.

Walioagana na Mhe. Rais Magufuli ni Luteni Jenerali James Mwakibolwa aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na Meja Jenerali Michael Isamuhyo aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Wengine ni Brigedia Jenerali Aron Lukyaa, Brigedia Jenerali William Kivuyo, Brigedia Jenerali Elizaphani Marembo na Kanali Peter Samegi.

Akizungumza baada ya kuagana, Luteni Jenerali Mwakibolwa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na amesema anaondoka na kuliacha jeshi likiwa na nidhamu, utii, uzalendo na weledi.

Nae Meja Jenerali Isamuhyo pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli  amesema anafurahi kuiacha JKT ikiwa imeimarika katika majukumu yake yakiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo na kuimarisha mafunzo kwa vijana wazalendo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
29 Januari, 2018

Basi la Tahmeed Lawaka Moto Tanga

$
0
0

Basi kampuni ya Tahmeed  lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Mombasa, Kenya limeteketea kwa moto leo Januari 29, mwaka 2018  katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Handeni, William Nyero amesema polisi wapo eneo la tukio na hakuna madhara yoyote kwa abiria waliokuwa kwenye basi hilo.

Amesema dereva wa basi hilo baada ya kubaini kasoro aliliegesha pembeni na abiria kuteremka, kushusha mizigo yao.

"Abiria wote waliokuwa wakisafiri na basi hilo wapo salama. Baada ya abiria kushuka na kushusha mizigo yao basi liliwaka moto,” amesema

Kwa nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.


NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.


MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA.


MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.


NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,


Je unamali yako unauza hupati wateja?

Wasiliana nami 0716-263605


DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale

Vumbi Lazidi Kutimka Uchaguzi Mdogo Siha

$
0
0
Vumbi Lazidi Kutimka Uchaguzi Mdogo Siha
Chama cha Wananchi CUF, kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Siha kikiwataka wananchi kumchagua mgombea wake Tumsifuel Mwanri kwa kuwa ana uwezo wa kuwaletea maendeleo ya kweli.

Wakati CUF ikisema hayo, mgombea wa chama cha Sau ameahidi kutoa nusu ya mshahara wake kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hizo uliofanyika Miti Mirefu, naibu mkurugenzi wa ulinzi na usalama CUF, Masoud Omar alisema vyama vingine vilipewa dhamana ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Siha lakini vimeshindwa hivyo wamchague Mwanri kwa maendeleo yao.

“Tunawashangaa kwa kushindwa kuleta maendeleo na kuanza kugombana wao kwa wao, sasa CUF tumewaletea jembe la kuwaletea maendeleo, mchagueni alete mabadiliko Siha,” alisema.

Akiomba kura, Mwanri alisema endapo atapata ridhaa ya kuongoza, ataboresha maendeleo katika sekta ya elimu, kilimo na maji.

Alisema atawatafutia wananchi masoko ya bidhaa za kilimo na kwa wafugaji, soko la ngozi ili waweze kufanya biashara na kujikwamua kiuchumi. Pia aliahidi kutafuta mashamba kwa ajili ya kilimo kwa shule, lengo likiwa ni kuwapunguzia wazazi mzigo wa michango ya chakula.

Wakati mgombea huyo wa CUF akitoa ahadi hizo, mwenzake wa CCM, Dk Godwin Mollel amesema akiwa upinzani, alizuiwa na kuonywa mara kwa mara pale alipojaribu kuunga mkono mazuri yaliyofanywa na Serikali.

Alisema kauli ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuwa walioko upinzani wanaweza kumuunga mkono Rais wakiwa huko bila kuhama ni ya matumaini kwa viongozi wa chama hicho wakiwamo wabunge ambao wamekuwa na kiu ya kuzungumzia mazuri yanayofanywa na Serikali na kuhofiwa kuonywa na kuhojiwa.

Akijibu kauli ya Mbowe aliyoitoa hivi karibuni, Dk Mollel aliwaambia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana eneo la Zahanati ya Ormelili kwamba wamchague hata kama yeye ni gunia la misumari. Akimnadi mgombea ubunge wa Chadema katika Viwanja vya Ngarenairobi, Mbowe, alinukuliwa akisema kuwa Dk Mollel ni gunia la misumari.

Dk Mollel ambaye hivi karibuni alijivua ubunge wa Siha baada ya kujiondoa Chadema na kuteuliwa na CCM kugombea tena nafasi, alisema kama yeye ni gunia la misumari ni vizuri akapewa nafasi hiyo kwani atatumiwa kukamilisha miradi.

Akimnadi mgombea huyo, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, aliwaahidi wananchi wa Siha kuletewa maendeleo na Kata ya Endument kupewa ekari 4,000 kwa ajili ya makazi, endapo wataichagua CCM.

Katika kampeni zake, mgombea wa Sauti ya Umma (Sau), Mdoe Azaria alisema kuwa endapo atapata ridhaa ya wananchi, atatoa nusu ya mshahara wake katika halmashauri kwa ajili kutekeleza miradi.

Alisema fedha hizo zitakuwa zinasaidia wananchi wanaoshindwa kutoa michango inayohitaji na kutumika kwenye huduma za afya kwa ajili ya watu wasiokuwa na uwezo.

Alisema Siha imekuwa na migogoro mingi ya ardhi kutokana na baadhi viongozi kuwa mikononi mwa watu binafsi.

Nabii Tito Apandishwa Mahakamani Leo Kwa Shtaka la Kutaka Kujiua

$
0
0
Nabii Tito Apandishwa Mahakamani Leo Kwa Shtaka la Kutaka Kujiua
Tito Onesmo Machibya anayejulikana kama 'Nabii' Tito (44) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong'ona Manispaa ya Dodoma leo Januari 29, 2018 amepandishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya kwa shtaka la kutaka kujiua.


Nabii Tito amepandishwa kizimbani leo akidaiwa kutaka kujiua mwishoni mwa wiki jana ambapo alijichana chana na wembe katika baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati Jeshi la Polisi likifanya uchunguzi nyumbani kwake.

Januari 23, 2018 Nabii Titoo alikamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kufanya uchochezi na baadaye alipelekwa kupimwa akili katika hospitali ya wagonjwa wa akili (Mirembe) na kufahamika kuwa mtu huyo alikuwa na matatizo ya akili, hivyo jeshi la polisi liliendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake na siku jeshi hilo lilipokwenda kufanya uchunguzi nyumbani kwake ndipo alifanya jaribio la kutaka kujiua.

Vikao vya Bunge Kuanza Rasmi Kesho

$
0
0
Vikao vya Bunge Kuanza Rasmi Kesho
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, laweka wazi shughuli zitakazo fanyika katika mkutano wa 10 wa Bunge unaotarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 30 January mwaka huu.


Bodi ya Ligi Yapangua Ratiba Yafanya Mabadiliko ya Michezo Miwili

$
0
0
Bodi ya Ligi Yapangua Ratiba Yafanya Mabadiliko ya Michezo Miwili
Bodi ya ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) imefanya mabadiliko ya michezo miwili kutokana na sababu tofauti.

Mchezo wa kwanza ni baina ya Mbao FC dhidi ya Kagera Sugar uliyopangwa kufanyika tarehe 3 ya mwezi Februari katika dimba la CCM Kirumba Mwanza, ambapo kwa sasa utafanyika Februari 4  katika uwanja huo huo huku sababu ikitajwa kuwa ni kutokana na uwanja huo kuwa na shughuli nyingine ya kijamii.

Mchezo wa pili ni kati ya Ruvu Shooting na Kagera Sugar ambao awali ulikuwa umepangwa kupigwa Februari 7 mwaka huu, na sasa umesogezwa mbele kwa siku moja hadi Februari 8, mwaka huu.

Wakati wa muzungumzo na waandishi wa habari bodi ya ligi imesema kuwa  sababu za mabadiliko hayo ni kuipa nafasi timu ya Kagera Sugar kusafiri na kupata nafasi ya kupumzika kwa kuwa mechi yao ya Februari 3 jijini Mwanza imesogezwa mbele kwa siku moja.

Mzungo wa pili wa ligi hiyo unatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi ya Feberuari 3 kwa michezo sita kupigwa kama ifuatavyo:-

Azam FC vs Ndanda FC,

Lipuli FC vs Yanga SC,

Singida United vs Mwadui FC,

Stand United vs Mtibwa Sugar,

Majimaji FC vs Mbeya City,

Tanzania Prisons vs Njombe Mji.

Jumapili kutakuwa na mechi mbili ambazo ni:-

Mbao FC vs Kagera Sugar,

Ruvu Shooting vs Simba SC.
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live




Latest Images