Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Sikubaliani na Kupigwa Marufuku Mikutano ya Hadhara kwa Vyama vya Siasa – Dkt. Slaa

$
0
0
Sikubaliani na Kupigwa Marufuku Mikutano ya Hadhara kwa Vyama vya Siasa – Dkt. Slaa
Aliyekuwa Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt.  Wilbroad Slaa amefunguka baada ya katazo kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara.

Dkt. Slaa ambaye kwa sasa ni Balozi amekiambia kituo cha runinga cha Clouds kuwa hakubaliana na jambo hilo kwa sababu uwepo wa mikutano hiyo ni kitu ambacho kilipitishwa na bunge.

“Mimi sikubaliani na jambo la kupigwa marufuku kwa mikutano ya kisiasa kwa jambo lililopitishwa na Mhe. Rais kwa maneno tu sababu Rais hafanyi kazi kwa maneno na hili jambo lilipitishwa na bunge iweje sasa mtu mmoja azuie,” amesema.

Katika hatua nyingine Dkt. Slaa amesema yeye ni muumini wa Demokrasia na anapenda uwepo wa vyama vingi ila muelekeo wa kisiasa nchini kwasasa haumfurahishi.

“Mimi nilijiuzulu siasa ya vyama vingi pia katika tafsiri yangu huwezi kuachana na siasa sababu ni maisha, lakini nilisema kuwa nitakuwa tayari kupigia kelele jambo lolote lile lenye maslahi kitaifa,” amesema Dkt. Slaa.

Muonekano Mpya wa Nywele za Kijani za Ben Pol Zampa Dili Nono

$
0
0
Muonekano Mpya wa Nywele za Kijani za Ben Pol Zampa Dili Nono
Wakati wabongo wakiendelea kumshambulia mitandaoni kwa aina ya mtindo wa kupaka rangi za kijani kwenye nywele zake, Msanii Ben Pol ameneemeka na staili hiyo kwani ameshalamba dili nono na kampuni ya Green Telecom inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na IT.

Ben Pol amethibitisha taarifa hizo kwenye mahojiano yake na Bongo5 ambapo amesema ni kweli amepata dili hilo na tayari ameshasaini mkataba lakini maelezo mengine atayatoa baadae baada ya kumaliza baadhi ya vitu na kampuni hiyo.

“Ni kweli nimepata dili nzuri yenye mkataba kabisa na Green Telecom lakini kwa sasa bado kuna vitu vinamalizika halafu tutatoa taarifa kamili na wenyewe ila ni dili kubwa,“amesema Ben Pol.

Huu ni muendelezo wa mafanikio kwa Ben Pol kwani mwishoni mwa mwaka jana alipata dili kadhaa ikiwemo ya ubalozi wa MAÜA association.

Mwamuzi Aliyetakiwa Achezeshe Mechi ya Azam, Simba Abadirishwa

$
0
0
Mwamuzi Aliyetakiwa Achezeshe Mechi ya Azam, Simba Abadirishwa
Mwamuzi Jonesia Lukyaa aliyekuwa achezeshe mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Azam FC, amebadilishwa.

Simba na Azam FC ambazo zinachuana kileleni mwa Ligi Kuu Bara, zinavaana kesho katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.

Taarifa zinaeleza mwamuzi huyo mwanamama mwenye beji ya Fifa amebadilishwa na nafasi yake amepewa mwamuzi mwingine.

“Nafasi yake amepewa Emmanuel Mwandengwa, hivyo hatachezesha,” kilieleza chanzo.

Hata hivyo, hakukuwa na ufafanuzi kuhusiana na suala hilo la uamuzi wa kumbadili siku chache kabla ya mechi.

RC Mnyeti Ataka Ofisa Tarafa Asimamishwe Kazi

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amemtaka kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Arnord Msuya kumsimamisha kazi Ofisa Tarafa ya Dongobesh, Bayo Banka kwa madai ya kushindwa

kutekeleza wajibu wake kutokana na kuchanganya siasa na kazi.

Pia, amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambao hawaungi mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuacha kazi vinginevyo atawachukulia hatua kwa kutotimiza wajibu wao ipasavyo na kuingiza siasa kazini.

Mnyeti ametoa agizo hilo jana Februari 5,2018 wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo katika ziara yake ya siku saba.

Amesema Banka anapaswa kusimamishwa kazi hadi hapo atakapotoa maelezo ya kushindwa kutimiza wajibu wake kwa kuchanganya siasa na kazi.

Amebainisha kuwa CCM ilifanyika kampeni na kuinadi Ilani yake ya uchaguzi kwa wananchi, kwamba kinachofanyika sasa ni utekelezaji wa Ilani hiyo kwa watumishi kuwatumikia wananchi.

"Mnakaa ofisini na kulipwa mishahara na posho nyingi lakini mnashindwa kuwatumikia wananchi badala yake mnaingiza siasa chafu. Natoa onyo kwa wote msirudie jambo hilo hata mara moja nitawachukulia hatua kali,"amesema Mnyeti.

Mnyeti amesema anayo majina na taarifa za baadhi ya watumishi wanaofanya kazi kizembe na kuzorotesha  shughuli za Serikali.

"Pamoja na ofisa tarafa huyo,  pia nakukabidhi majina mengine ya watumishi ambao wanatekeleza maagizo ya viongozi wa vyama vingine vya kisasa badala ya kutekeleza maagizo ya viongozi wa Serikali inayoongozwa na CCM," amesema Mnyeti.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga amesema watumishi wa halmashauri hiyo wamejipanga kuhakikisha wanawatumikia wananchi ipasavyo.

Waliomuibia kwa Kutumia Silaha Baby Madaha Wahukumiwa Miaka 30 Jela

$
0
0
Waliomuibia kwa Kutumia Silaha Baby Madaha Wahukumiwa Miaka 30 Jela
February 6, 2019 nikusogezee kilichojiri katika Mahakama za Tanzania ikiwa ni pamoja na hukumu ya kesi ya waliomuibia kwa kutumia silaha Msanii wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ambapo Mahakama ya Wilaya Kinondoni imewahukumu miaka 30 jela.

Katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa watatu ambao ni Benard Joseph na Yaram Leonard lakini Mahakama iliamua kumfutia kesi mshtakiwa wa tatu Asma Mwaipopo, ambaye aliugua matatizo ya uzazi na kufariki dunia wakati kesi ilipokuwa ikiendelea.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Joyce Mushi, ambapo amesema Mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na mashahidi nane kutoka upande wa mashtaka na kwa sababu ulikuwa na vielelezo vya kutosha.

“Kwa mazingira hayo mahakama hii inawatia hatiani kwa kosa la hilo kutokana na ushahidi wa kina uliowasilishwa hapa na mashahidi hao kutoka upande wa mlalamikaji kwani nimeuthibitisha pasi na shaka,” amesema Hakimu Mushi.

Kutokana na hatua hiyo, amesema kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 jela, ambapo hilo litakuwa ni onyo na fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za wizi wa kutumia silaha.

Washtakiwa hao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo December 15, 2016 na kwa mujibu wa hati ya mashtaka walitenda kosa hilo November 7, 2016 maeneo ya Mbezi Makonde Dar es Salaam Wilaya ya Kinondoni.

Katika wizi huo inadaiwa waliiba Simu moja aina ya Samsung, Hati ya kusafiria yenye namba 791848, Wallet, USD Dola 1000, Begi dogo, Chaja ya simu na vinginevyo aidha kabla na baada ya kuchukua mali hizo walimtisha Msanii huyo ili kujipatia mali hizo.

Marekani, Urusi Zafikia Lengo la Kudhibiti Silaha za nyuklia

$
0
0
Marekani na Urusi zimetoa taarifa kwa nyakati tofauti zikisema zimefikia lengo muhimu la kudhibiti silaha za nyuklia, baada ya kuongezeka wasiwasi kuhusu wajibu wao katika upunguzaji wa silaha hizo.

Mataifa mawili hayo yanayoongoza kuwa na silaha nyingi za nyuklia yamethibitisha kuwa yanaendelea kutekeleza Mkataba Mpya wa START (Strategic Arms Reduction Treaty) ambao ulianza kufanya kazi mwaka 2011.

Makubaliano hayo ya pande mbili yanazitaka kila nchi kuwa na vichwa vya nyuklia chini ya 1,550, na unazilazimisha kupunguza makombora na ndege za kivita. Jumatatu ilikuwa siku ya mwisho ya kuthibitisha utekelezaji wa mkataba huo.

Wakati Marekani imesema imepunguza vichwa vyake vya nyuklia vilivyosambazwa maeneo mbalimbali duniani hadi 1,393, Urusi imeeleza kuwa imepunguza idadi ya silaha hizo hadi 1,444.

Hata hivyo Urusi imekuwa ikiimarisha silaha zake za nyuklia zitumikazo kwenye masafa mafupi ambazo hazipo kwenye mkataba huo.

Rais wa Marekani Donald Trump wiki iliyopita aliutangaza mkakati wa nyuklia wa utawala wake akisema unataka kuimarishwa kwa uwezo wa kujilinda ili kukabiliana na Urusi na nchi nyingine zinazojiimarisha kijeshi.

Watalaam wa kupunguza silaha wanaonya kuwa dunia huenda inarejea kwenye zama za Vita Baridi wakati ambapo hali ya wasiwasi ilikuwa juu kati ya Marekani na Urusi.

Sijaja Kuapishwa Kuwa Balozi Nimekuja, CCBRT Ndicho Kilichonileta- Dr. Slaa

$
0
0
Sijaja Kuapishwa Kuwa Balozi Nimekuja CCBRT Ndicho Kilichonileta- Dr. Slaa
Kama unadhani Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa amekuja nchini kwa ajili ya kuapishwa utakuwa umekosea sana. Yupo nchini kushughulikia usajili wa Hospitali ya CCBRT.

Katibu mkuu huyo wa zamani wa Chadema, ametoa kauli hiyo leo Februari 6, 2018 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Clouds.

“Familia yangu nimeiacha Canada, wengine wanajua, sikuja kwa sababu ya ubalozi. Mimi ni mwenyekiti wa CCBRT ndicho kimenileta na wengine mnafahamu katika nchi yetu mengi yanafanyika,” amesema.

Novemba 23 mwaka jana, Rais John Magufuli alimteua Dk Slaa kuwa balozi, lakini mpaka sasa hajaapishwa na kupangiwa kituo cha kazi.

Soma: Dk Slaa ateuliwa kuwa balozi

Dk Slaa ambaye kwa sasa anaishi Canada alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kupitishwa kuwa mgombea urais kupitia muungano wa Ukawa.

Alisema chama chake hakikutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kuwapokea baadhi ya makada wa CCM akiwamo Lowassa.

Januari 29, 2018, Dk Slaa alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu Dar es Salaam na kumshukuru kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Katika kipindi hicho, Dk Slaa ameulizwa kama amekuja kula kiapo na kupangiwa kituo cha kazi, lakini amepinga jambo hilo na kubainisha kuwa amekuja kushughulikia usajili wa hospitali hiyo kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa bodi.

Amesema kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria, CCBRT inatakiwa kujiandikisha upya vinginevyo itafutwa.

Kuhusu taarifa kuwa ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za nyumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, amesema: “Hizo ni propanganda nisingependa kuzizungumza lakini Supermarket inayozungumzwa si kama mnavyofikiri ni kubwa.

“Kitu kikubwa tunatofautiana katika mtazamo, fikra  tunavyofanya vitu vyetu. Canada haina mwenyewe kuna raia wa kutoka kila nchi. Sisi hapa tunasema hapa kazi tu lakini kule ni maisha. Unakuta waziri anatoka ofisini kwake anakwenda kufanya kazi nyingine, baadaye anatoka na kwenda kufanya nyingine. Kufanya kazi tatu ni kawaida.”

Ametolea mfano ufanyaji kazi wa Canada na Tanzania amesema baadhi ya Watanzania huingia ofisini na kusoma magazeti, au kutumia simu kufanya biashara zao.

“Canada utaingia ofisini na simu au ipad lakini utaiacha getini na matokeo yake nchi ile ni matajiri. Watu ni matajiri kila mtu ana utambuliso wa maisha mazuri ni kwa sababu wanafanya kazi na huduma zote ziko vizuri,” amesema.

Kuhusu kufunga ndoa amesema: “Siasa za Tanzania zilichangia mimi kutokufunga ndoa kwa kipindi chote lakini Februari 2016 kule Canada nilifunga ndoa (na Josephine Mushumbusi), ile si ndoa kwani tulishakaa, kanisa ilichokuja kufanya ni kuhalalisha tu.”

Maneno ya Sheikh Wetu Kwa huyu Mange Siyo ya Sawa..Haikupashwa Kutumia Vitisho vya Namna Hiyo

$
0
0
Assalam aleykum waungwana,

Mimi ni Muislamu mwenye akili timamu na ninaitakidi Sheikh  ni Muislamu mwenzangu.

Huwenda baadhi ya watu watahisi kama mimi sio Muislamu ila nimetumia mwanya huu kukashifu hii dini lakini hapana jamani mimi ni Muislamu japo sio maarufu hata mtaani kwangu, lakini hilo halinizuii kusema au kujadili.

Maneno ya sheikh  kwa huyu dada Mange Kimambi kama ambavyo wengi wetu tumesikia sioya sawa kabisa hasa kitendo cha yeye kusema huu ndo mwaka wa mwisho kabisa hatotukana tena sasa mwaka wa mwisho kivipi?

Haoni kama kajiingiza kwenye dhana mbaya na watu wahisi kama atafanya watu wamhisi vibaya au wahisi kama Uislamu kweli ni uchawi wa kutupiana majini na mashetani?

Kitendo chake cha kukata kwa kusema huu ndo mwaka wa mwisho na kama keshajua kitakachomtokea huyo binti kwa huu mwaka na huko tunasema ni kujua ghaibu(mambo yaliyofichikana ya baadae au sasa)na hilo jambo liko kwake Allah na sio kwa kiumbe yeyote yule.

Nafasi yake kama kiongozi wa dini alitakiwa atumie nafasi hiyo kumfahamisha Mange kwa maneno mazuri kabisa huwenda angefahamu huyo Mange kwa sababu yeye shekhe hakuwekwa kuhukumu bali kawekwa kuwaelimisha watu na sio vinginevyo na hatakiwi kushindwa walakukata tamaa juu ya mtu fulani.

Huyo Mange ni mara ya ngapi hii kuwatukana sheikh Alhadi? Si ndio ya kwanza tu? Vipi sheikhe Swabru (subira)iko wapi?

Kusema hivi simtakasi na wala hakutomtakasa Mange Kimambi laa bali tunafahamu kwamba anachofanya sio sawa lakini sisi tumeona shekhe wetu anasikika na kasimama kwa niaba ya waislamu sasa huwenda watu wakaona kama uislamu umeruhusu au ndivyo uislamu ulivyo mtu akikuvunjia adabu basi utoe kitisho au ukamshitakie kwa Allah kwa lengo la kumzimisha na sio kwa lengo la kubadili uovu wake uwe mwema.

Hata mtume wetu enzi hizo alikuja muarabu wa mashambani(bedui)akakojoa msikitini watu wakahamaki wakataka kumpiga lakini bwana mtume akawakataza na akamuita yule bedui akaanza kumpa maneno malaini kana kwamba kapatia kile kitendo kumbe ni kosa kubwa sana.

Ikiwa huyu kanajisi nyumba ya ibada mbele ya mtume wa Mungu lakini kapewa maneno malaini na hakupewa vitisho, vipi aje mtu amtukane mtu tena kwa sababu za kidunia tu ukaanze vitisho na mashtaka?

Shekhe anatakiwa amuombee kwa Mungu dada huyo aache tabia hiyo na azungumze kwa mema kabisa kwenye mitandao hiyo ja kijamii.

Wengine watanilaumu watasema mara ooh kama nasaha si ukampe kwa siri mbona unatoa hadharani.

Nasema hivi"""nasaha za siri ni kwa yale makosa ya siri mfano mtu kazini kwa kujificha au kaiba basi hapo unatakikana ukamnasihai kwa siri kwa sababu lile jambo halikuenea kwa watu lakini akifanya jambo hadharani kabisa na watu wakalichukulia ni sawa basi hapo lazima utoe nasaha au umkosoe hadharani ili kuwaokoa hawa watu walioamini jambo hilo.

Hivyo kauli hiyo yenye kitisho haikuwa sawa kabisa kabisa.

By Lelelu/JF

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba, Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0

Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?


Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Madhara ya Kula Chips, Mayai na Kinywaji Cha Soda Haya Hapa

$
0
0
LEO tutazungumzia vyakula hatari kwa afya zetu. Vyakula tunavyotakiwa kuvila, hatuvili na pengine upatikanaji wake ni wa shida, hivyo tunalazimika kula vilivyopo licha ya kuwa vina madhara kwa afya zetu.

Hali hii imeongeza idadi ya wagonjwa na magonjwa sugu. Chakula kikuu cha mijini ni chips, kuku, mayai, soda, juisi za makopo au paketi, nyama choma na pombe. Pia kuna mkate mweupe, maandazi na chapati. Vyakula hivi huliwa kila siku, lakini ukivichambua utagundua vina madhara makubwa kiafya kama tutakavyoona hapa chini.

CHIPS

Chips ambayo kwa kawaida hutengenezwa kutokana na viazi mviringo na kukaangwa kwenye mafuta, ni chakula kinachotakiwa kuliwa kwa kiasi kidogo sana na kwa nadra sana, kwa sababu kiko kwenye kundi la vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo huliwa kwa uchache.

KUKU

Kwa kawaida, kuku wengi wanaotumika kwenye biashara ni kuku wa kisasa. Nyama ya kuku hawa haina virutubisho sawa na kuku wa kienyeji. Hii inatokana na ukweli kwamba kuku hao hulishwa madawa mbalimbali ya kuwakinga na magonjwa na hulishwa vyakula vilivyochanganywa madawa ili wakue haraka. Kwa mazingira hayo, nyama itokanayo na kuku wa aina hii haiwezi kuwa bora.

Kiasili kuku huishi mazingira huru kwa kula vyakula ambavyo hujenga na kuukinga mwili wake dhidi ya magonjwa mbalimbali, kuku wa aina hii ndiye anayefaa kuliwa na kuleta faida ya nyama ya kuku inayokusudiwa.

MAYAI

Halikadhalika, mayai yanayopatikana kwa wingi mijini ni yale yatokanayo na kuku wa kufuga wa kisasa. Kiasili, mayai ya kuku wa kufuga, hayawezi kuwa sawa na mayai yatokanayo na kuku wa kienyeji.

Huhitaji kuwa mwanasayansi kuona tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na kuku wa kufuga, kwani mayai hayo yakipikwa huwa tofauti kwa ladha na hata rangi. Ni ukweli ulio wazi kuwa kuku wa kufugwa hulishwa vyakula vya kutengeneza ambavyo ndani yake huwekwa kemikali na madawa mbalimbali, wakati kuku wa kienyeji hula vyakula asili kwa kujitafutia wenyewe na mazingira wanayoishi ndiyo yanayowafanya wawe tofauti na bora. Hivyo ni dhahiri kwamba mayai tunayokula ya kuku wa kisasa yana madhara zaidi kuliko faida mwilini.



SODA

Moja ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa na watu wengi ni soda. Wengi hudhani ni kinywaji ambacho hakina madhara kabisa kwa mtumiaji. Familia nyingi zimeamini kuwa soda ni kinywaji bora na hata watoto wetu wamerithishwa imani hii. Lakini kwa upande wa pili wa kinywaji hiki, siyo kinywaji salama kama ambavyo imekuwa ikielezwa. Siwezi kusema moja kwa moja kuwa mtu huruhusiwi kabisa kunywa soda lakini watu walitakiwa kuelimishwa na kuelezwa madhara ya kupenda kunywa soda na athari anazoweza kuzipata mtu kiafya. Naamini tahadhari inayotolewa kwa wanywa pombe na wavuta sigara ingefanywa pia kwa wanywa soda.

Utafiti unaonesha kuwa soda, huwekwa sukari nyingi kiasi kisichopungua vijiko sita katika chupa moja. Kiwango hicho cha sukari ni kingi zaidi ya mara tano ya kile kinachoruhusiwa kwa mtu kutumia kwa siku. Madhara ya sukari mwilini ni mengi, yakiwemo ya kudhoofisha kinga ya mwili na viungo kwenye sehemu za maungio na pia huongeza uzito wa mwili. Ukitaka kujua soda ina madhara kiafya, fanya utafiti binafsi na utagundua haya ninayoyaandika.

Kunywa soda zisizopungua tatu kwa muda mfupi, kisha lala usiku kama kawaida halafu wakati wa kuamka asubuhi, usikilize mwili wako. Utaamka ukiwa na maumivu mwili mzima, utajihisi uchovu, hasa sehemu za maungio, mfano wa mtu aliyefanya mazoezi mazito au kazi nzito siku iliyopita. Hiyo ni

kutokana na kuingiza kiwango kingi cha sukari mwilini.

JUISI

Wengi hudhani juisi ni kinywaji baridi kisicho na kilevi wala madhara kwa mnywaji. Lakini utakuwa sahihi ukizungumzia juisi zilizotengenezwa kwa matunda halisi bila kuongezewa vitu vingine. Siku hizi juisi nyingi zinazouzwa kila sehemu ni zile zilizoongezwa sukari nyingi.

Juisi nyingi hutengenezwa kwa kuchanganya maji, sukari na rangi zilizotengenezwa kwa kemikali mbalimbali zikiwemo zenye ladha ya matunda (siyo matunda halisi). Juisi za aina hii ndiyo nyingi na zinapatikana kila kona ya nchi hii, waathirika zaidi wakiwa watoto wetu ambao hupenda kunywa kwa kufuata utamu wa sukari nyingi zilizowekwa na ladha za matunda.

Utafiti umeonesha kemikali zinazowekwa kwenye vinywaji hivi vya kwenye makopo au plastiki, hudhoofisha kinga ya mwili na huwa chanzo cha magonjwa ya saratani na mengine hatarishi. Nakusihi kuacha kunywa kabisa juisi hizo na usimpe mwanao. Badala yake tengeneza juisi wenyewe kwa kutumia matunda halisi ili kupata faida katika miili yetu.

Mrembo Tunda Ana Umbo Dogo Lakini ni Kivuruge Hatari...

$
0
0
SIKU za nyuma kidogo, utakubaliana na mimi kwamba mastaa kama vile Wema Sepetu, Irene Uwoya, Kajala Masanja, Jack Wolper na wengineo ndiyo waliokuwa wakitawala kwenye vyombo vya habari kwa kila siku kuibuka na vijimambo.

 Kwa jina lingine tunaweza kusema, madada hawa walikuwa ‘scandal makers’ lakini sasa hivi wote kimyaaa, kabinti kadogo kenye umri usiozidi miaka 24 ambako kameonekana kwenye video za wanamuziki kadhaa Bongo ndiko kanakotamba kwa sasa.


MAISHA YAKE

Maisha yake yamekuwa yakiibua viulizo vingi sana kwani mara kwa mara amekuwa akionekana kwenye viwanja mbalimbali vya starehe bila watu kujua shughuli inayomuingizia kipato.

Maswali ni kwamba, anapata wapi hizo fedha za kujiachia kila siku? Mbona haonekani kufanya kazi ambayo imemtambulisha ya kuuza sura kwenye video ‘video queen’, kazi ambayo kimsingi hailipi kihivyo Bongo?

 Watu wanahoji, hata kama anapewa na wazazi wake, haiingii mzazi aendelee kumruhusu mwanaye aponde raha kila siku bila kufanya jambo lolote la maana.

Kwa idadi ya kazi zake za video queen, kipato cha kazi yake hiyo ambayo inafahamika wengi wao hulipwa kidogo au kutolipwa kabisa, kamwe haiingii akilini kwamba ndizo zinazomuwezesha kufanya kufuru ya starehe kila uchwao.

Ukitembelea ukurasa wake wa Instagram, utaona jinsi ambavyo kila siku mrembo huyo yuko bize kwenye mahoteli makubwa akila na kunywa huku chanzo cha starehe hizo kikitajwa kuwa huenda ni vigogo wanamuwezesha.

 Ukitazama pia aina ya picha anazopiga na kuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, zina viashiria fulani ambavyo si vizuri na watu kuhoji kwamba huenda akawa anafanya hivyo kutafuta soko la wanaume.

 MSURURU WA WANAUME

Japo haiwezi kupatikana idadi kamili ya wanaume ambao ametajwa kuanguka nao dhambini lakini mrembo huyu anatajwa kama miongoni mwa warembo ambao wana msururu mrefu wa wanaume mastaa na wasio mastaa.

Kama hiyo haitoshi, Tunda pia anatajwa ‘kujiweka’ kwa watu wakubwa waliomzidi umri kama ilivyojidhihirisha hivi karibuni baada ya kuvuja kipande cha video kikimuonesha akifanya mambo ya kimalovee na mtoto wa marehemu Kingunge Ngombale Mwiru, Kinje.



Kwa mastaa wanaofahamika, Tunda alishawahi pia kudumu muda mfupi penzini na bwa’mdogo anayefanya muziki wa Hip Hop, Young D. Baadaye alimwagana naye, pia ameingia kwenye himaya ya staa wa Bongo Fleva, Diamond.

Usisahau ni Tunda huyuhuyu, iliwahi kuvuja video yake akiwa na mchekeshashi Stan Bakora wakifanya mambo ya chumbani.



NI KIVURUGE KWELI KWELI

Amemwagana na bwa’mdogo Young D ambaye kwa macho inaonekana kabisa ni saizi yake. Amehamishia majeshi kwa Diamond ambaye kidogo amemzidi yeye umri.

Diamond ana watoto wawili, amezaa na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Amesababisha mpasuko mkubwa katika penzi hilo lakini pia, Tunda huyohuyo ametibua ndoa ya Kinje.



MATUKIO MABAYA

Tunda amekuwa akitajwa kuwa na mwenendo mbaya kutokana na maisha yake kutoeleweka nini hasa chanzo cha mapato yake. Aliwahi pia kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujihusisha na madawa ya kulevya.



KAZI ZAKE

Ukiachana na ngoma za hivi karibuni, Tunda ni video queen ambaye ameonekana kwenye Wimbo wa Barnaba na Amini unaokwenda kwa jina la Why Me, wimbo wa Matonya aliomshirikisha Christian Bella wa Agwelina, wa TID unaoitwa Raha, wa Christian Bella, Dully Sykes na Tanzanite unaoitwa Ndombolo ya Solo na Wimbo wa Timbulo unaoitwa Sina Makosa ambazo ni za muda kidogo.



AJIFUNZE

Mambo anayoyafanya hayalingani na umri wake, ni vyema Tunda akajitambua. Akajua kwamba kuna maisha baada ya hizi starehe anazozifanya, kuna magonjwa na kuna matatizo makubwa yanayoweza kumpata kama tu ataendelea kuishi maisha ya anasa.

Namshauri atubu, atafute shughuli halali ya kufanya, akiendelea na mwenendo huu, mwisho wake utakuwa mbaya

Je Unasumbuliwa na Tatizo la Nguvu za Kiume?

$
0
0

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume limekuwa kwa lika zote Tiba sahihi ya matatizo haya
Chanzo chake na visababisho vyake

DALILI: mwili kuchoka maumivu ya mgongo na kiuno kutopata choo vizuli kinakuwa kigumu kama cha mbuzi
RADI: hutibu matatizo kwa mda mfupi na inakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika (30) kwa tendo(1) utaludia Mara (4) bila kuchoka pia uongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa maradufu

BOMBA; dawa ya kupunguza matiti makubwa unene na kitambi
ITUJA; dawa inatibu michilizi mwilini inaongeza makalio hips miguu saizi uipendayo

HUDUMA HIZI NA ZINGINE UTAZIPATA POPOTE TANZANIA MUONE DR LAJABU AU PIGA SIM 0711494261 au 0783823120

Waziri Ummy Eeleza yaliyomkuta Aliyekuwa Mkurugenzi Benki ya Wanawake

$
0
0

Dodoma. Watumishi 20 akiwamo aliyekuwa mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Magreth Chacha wamefikishwa katika vyombo vya uchunguzi kwa lengo la kuangalia uwezekano wa kuwashtaki kutokana na kuitia hasara benki hiyo.

Kauli hiyo imetolea leo Februari 6, 2018 bungeni mjini Dodoma na waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na kwamba watumishi hao wanachunguzwa na Takukuru na Polisi.

Amesema mkurugenzi huyo amekabidhiwa katika vyombo hivyo tangu Julai mwaka jana.

“Tuliamua kumpeleka Magreth na watumishi wengine jumla wapo 20. Vyombo vyetu vinawachunguza maana kumekuwa na tatizo kubwa katika benki hiyo ikiwamo kukopesha Saccos, lakini uchunguzi unaonyesha hakuna hata mtu mmoja aliyekopa,”amesema Ummy.

Waziri huyo alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu (CCM), Faida Mohammed Bakari aliyehoji hatua zilizochukuliwa kwa watu waliohujumu benki hiyo aliyodai imeshindwa kutimiza wajibu wake.

Katika swali lake la msingi, Faida alitaka kujua ni lini TWB itaanzisha tawi lake Zanzibar kwa ajili ya kuwapatia huduma za mikopo yenye riba nafuu na kuwainua kiuchumi wanawake wa Zanzibar.

Akijibu swali hilo la msingi, naibu waziri wa Afya, Dk Faustine Ndungulile amesema benki hiyo iliyoanzishwa mwaka 2009, lengo lake lilikuwa kuwakwamua wanawake na umaskini kwa masharti nafuu.

Dk Ndugulile amesema mpango wa benki hiyo ni kuhakikisha huduma zake zinawafikia wanawake  mikoa yote ya Tanzania,  ikiwamo Zanzibar kulingana na upatikanaji wa mtaji.

Mwananchi

Mbunge Ahoji Uhalali wa BAKWATA kuwa Msemaji wa Waislamu

$
0
0

Na Esther Mbusi, Dodoma

Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), amehoji uhalali wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuwa wasemaji wa waisalamu nchini.

Akiomba mwongozo wa Spika bungeni leo Jumatatu Februari 5, Bobali alisema Waislamu wana madhehebu mengi lakini taasisi pekee ndiyo inayosikilizwa na serikali ni Bakwata.

“Madhehebu mengine hayatambuliwi na hata ushiriki wa viongozi wakubwa wa kitaifa hushiriki Bakwata, hivi Bakwata ndiyo taasisi pekee iliyopewa mamlaka na serikali ya kuwasemea waislamu wa nchi hii,” alihoji Bobali.

Hata hivyo, akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alisema mwongozo huo umekosa sifa kwa mujibu wa kanuni ambapo zinamtaka muomba mwongozo kuzingatia jambo lililotokea bungeni na suala la Bakwata halijazungumzwa bungeni.

Chanzo: Mtanzania

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Uongozi wa Ruvu Shooting Wamuomba Radhi Okwi

$
0
0
Uongozi wa Ruvu Shooting Wamuomba Radhi Okwi
Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting kupitia kwa msemaji wake Masau Bwire umemuomba radhi mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi kufuatia kufanyiwa tukio lisilo la kiungwana na mchezaji wao Mau Bofu.

Masau Bwire amesema wao kama uongozi wa Ruvu Shooting, pamoja na mchezaji mwenyewe wamekiri kufanya kosa hilo na wanamuomba radhi Okwi mwenyewe, uongozi wa Simba pamoja na wapenda soka wote.

Bofu alimpiga kiwiko Okwi katika dakika ya 43 ya mchezo kati ya timu hizo siku ya Jumapili wikiendi iliyopita, kwenye Uwanja wa Uhuru, ambapo mwamuzi alimtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja licha ya kuwa tayari alikuwa na kadi ya njano.

Kitendo hicho kilisababisha Okwi asiendelee na mchezo hivyo kulazimika kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Laudit Mavugo. Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Okwi anaongoza orodha ya wafungaji msimu huu akiwa na mabao 12 hadi sasa, wakati klabu yake ya Simba ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 38.

Rosa Ree Amkana Young Dee "Sina Mahusiano ya Kimapenzi na Young Dee"

$
0
0
Rosa Ree Amkana Young Dee "Sina Mahusiano ya Kimapenzi na Young Dee"
Msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree amefunguka ukweli wa taarifa zilizodai alikuwa akitoka kimapenzi na Young Dee.

Rosa Ree amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani yeye na Young Dee walikuwa pamoja kwa ajili ya kazi tu.

“Mimi na Young Dee tulienda kufanya tour pamoja, tulienda kufanya kazi. Katika industry yetu, society yetu ni kama ukimuona mtu ana come together na mtu mwingine unachukulia wanatoka pamoja, hapana haiko hivyo,” Rosa Ree ameiambia Bongo5.

“Labda inaweza ikawa hivyo kwa watu wengine haikuwa hivyo iliishia kwenye kazi, mimi na Young Dee hatuna mahusiano wa kimapenzi,” amesema.

Rosa Ree kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Marathon’ aliyomshirikisha Bill Nass mara baada ya kutamba na ngoma ‘Dow’.

Aliyeingiza Fedha Kinyume cha Sheria Alipa Faini ya Milioni 100

$
0
0
Aliyeingiza Fedha Kinyume cha Sheria Alipa Faini ya Milioni 100
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu raia wa Uganda, Winfred Businge kulipa faini ya Sh100 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Businge (33), amelipa faini hivyo kukwepa kifungo.

Hukumu imetolewa leo Jumanne Februari 6,2018 na hakimu mkazi mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa kukiri kosa.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani akidaiwa kuingiza nchini dola 1 milioni za Marekani (Sh2.2 bilioni) bila kutoa taarifa kwa mamlaka ya forodha.

Businge anadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 11,2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Soma: Raia wa Uganda kizimbani kwa kuingiza Dola milioni moja nchini

Kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na wakili wa Serikali mwandamizi, Awamu Mbagwa na mshtakiwa aliwakilishwa na wakili Hudson Ndusyepo.

Mshtakiwa aliposomewa shtaka kwa mara ya kwanza alikana na alikuwa nje kwa dhamana.

Kwa mara ya kwanza, Rais John Magufuli Desemba 13,2017 alizungumza kuhusu fedha hizo alipokuwa akifungua tawi la Benki ya CRDB mjini Dodoma.

Nassari Afikishwa Mahakamani kwa Shtaka la Shambulio

$
0
0
Nassari Afikishwa Mahakamani kwa Shtaka la Shambulio
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kujibu shtaka la shambulio.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Fortunatus Muhalila mbele ya hakimu Jasmine Abdul amedai Desemba 14,2014

Nassari alimshambulia Neeman Ngudu.

Anadaiwa kutenda kosa hilo eneo la Makiba kwa kumpiga mateke Ngudu na kumsababishia maumivu akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Muhalila amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na ameiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kutajwa shtaka hilo.

Nassari anayetetewa na wakili Sheki Mfinanga alikana kutenda kosa hilo.

Hakimu Abdul aliahirisha kesi hadi Machi 6,2018 itakapotajwa.

Nassari alidhaminiwa na diwani Gabriel Mwanda wa Kata ya Ambuseri aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.

Mazungumzo ya Upatanisho wa Amani Kuhusu Sudan Kusini Yagonga Mwamba

$
0
0
Mazungumzo ya Upatanisho wa  Amani Kuhusu Sudan Kusini Yagonga Mwamba
Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa Sudan kuisni nchini Ethiopia yamegonga mwamba kwa baada ya wajumbe kususia kikao hicho, Radio Tamazuj inaripoti.

Hii ikiwa ni jitihada ya hivi karibuni kusitisha mapigano ya kiraia yaliodumu zaidi ya miaka minne mpaka kufikia sasa.

Kituo hicho cha utangazaji kinasema ujumbe wa serikali ulitaka zaidi ya wajumbe watatu wahudhurie kikao hicho. Pande hizo mbili zinatarajia kufufua makubaliano ya amani ya mwaka 2015.

Duru tofauti mjini Addis Ababa zimeiambia Radio Tamazuj kwamba ujumbe wa serikali uliamua kususia kikao cha leo mchana kwasababu walitaka zaidi ya wajumbe watatu kuhudhuria.

Raia wa Sudan kusini avuka mto akiwa amebeba bundukiHaki miliki ya pichaREUTERS
"Serikali inataka wajumbe zaidi ya watatuu wahuhudhurie lakini IGAD inaruhusu watau pekee," mmoja wao alisema.

Kikao cha pili leo mchana kinafafanua kuhusu ajenda ya awamu ya pili ya mpango wa kufufua makubaliano ya amani ya mwaka 2015.

Sudan Kusini yaonywa kukumbwa na maafa
Sudan Kusini yaua raia wake
Mazungumzo hayo yanajiri katika wakati ambapo kunajumuiya ya imatiafa inazidi kushindwa kuuvumili utawala wa kisiasa na kijeshi wa taifa hilo changa barani Afrika.

Wajumbe wa Sudan Kusini walipewa ujumbe mkavu muda mfupi kabla ya kutarajiwa kaunza kikao hicho. Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, aliwaambia kwamba wanahusika kwa jinamizi wanalolishuhudia hivi sasa raia wa Sudan kusini.


Makubaliano ya mwisho ya kusitisha mapigano yalitiwa saini mkesha wa Krismasi na ulidumu kwa saa kadhaa.

Katika miaka minne iliyopita, maelfu ya watu wameuawa katika mapigano na kiasi ya thuluthi moja ya raia nchini wameachwa bila ya makaazi.

Marekani iliunga pakubwa mkono uhuru wa Sudan kusini mnamo 2011.

Lakini wiki iliyopita Marekani iliidhinisha vikwazo vya silaha na hivi karibuni mkuu wa muungano wa Afrika ameitisha kuidhinisha vikwazo dhidi ya wanaorefusha mzozo huo.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images