Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104666 articles
Browse latest View live

Diamond Aweka Wazi Mahusiano Yake na Baba Yake Mzazi

$
0
0
Diamond Aweka Wazi Mahusiano Yake na Baba Yake Mzazi
Baada ya tetesi za muda mrefu kuzagaa kuwa Msanii wa Muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz kuwa hana mahusiano mazuri na baba yake mzazi, Hatimaye Diamond ameweka wazi ukweli wote kwa kukanusha taarifa hizo.

Diamond amesema kuna watu wenye hira ndio wanaokuza mambo lakini yeye huwa anawasiliana naye na huwa anamsaidia pale anapokuwa na kitu.

Ingawaje Diamond amekiri wazi kwamba hana mazoea naye kama ilivyo kwa mama yake mzazi lakini hakuna bifu kama baadhi ya watu wanavyokuza mambo.

Kwa upande mwingine, Diamond amewakanya baadhi ya watu ambao wanampeleka baba yake hadi kwenye geti lake na kumpiga picha ili kuupotosha umma kuwa amemfungia geti baba yake, waache hiyo tabia kwa sababu inaathiri hadi familia nyingine.

Mzee Majuto Atoa ya Moyoni " Niombeeni Tezi Dume si Mchezo"

$
0
0
Mzee Majuto Atoa ya Moyoni " Niombeeni Tezi Dume si Mchezo"
MKONGWE wa filamu za Kibongo aliye kipenzi cha wengi, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ambaye kwa sasa ni mgonjwa ametoa ya moyoni kuwa bado anaumwa hivyo kuwaomba wasanii wenzake na Watanzania kumuombea.

Akizungumza na Star Mix, Mzee Majuto alisema Februari 11, mwaka huu anatarajia kurudi tena katika Hospitali ya Tumaini, Dar alikokuwa amelazwa awali na kuruhusiwa baada ya daktari wake kufiwa ambapo ndiyo ataenda kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa tezi dume unaomsumbua.

“Niliruhusiwa Jumamosi iliyopita lakini bado naumwa, tezi dume si mchezo, ninachoweza kuwaambia wasanii wenzangu na Watanzania kwa jumla, waniombee tu,” alisema Mzee Majuto.

Zari Aonyesha Jeuri ya Pesa Atumia Zaidi ya Milioni 6 Kwaajili ya Viatu vya Watoto Wake

$
0
0
Zari Aonyesha Jeuri ya Pesa Atumia Zaidi ya Milioni 6 Kwaajili ya Viatu vya Watoto Wake
Zari the boss lady siku kadhaa zilizopita alikuwa Dubai kwaajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya rafiki yake  Zowda Mkandila  akiwa katika matembezi Dubai, Zari aliamua kutumia zaidi ya Milioni 6 kwa ajili ya kuwanunulia watoto wake viatu aina ya Balenciaga.

Kiatu aina ya Balenciaga alichonunua Zari kwaajili ya watoto wake kinauzwa Dola 692 za Kimarekani ambapo ni zaidi ya shilingi Milioni  1.5 za Kitanzania kwa pair moja ya kiatu.

Kupitia Snapchat account ya Zari aliandika “Ni kwa ajili yangu na watoto wangu tutavivaa wote vikiwa vyeusi” hiyo ni baada ya Zari kununua viatu hivyo ndio akaamua kuvipost Snapchat.

Mke wa Tambwe Hiza Aeleza Mazingira ya Dk. za Mwisho za Uhai Wake

$
0
0
Mke wa Tambwe Hiza Aeleza Mazingira ya Dk. za Mwisho za Uhai Wake
WAKATI familia ikikaa na kujipanga jana kwa ajili ya mazishi ya kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tambwe Hiza, mkewe Mariam Masoud, ameelezea mazingira ya dakika za mwisho za uhai wake.


Akizungumza na Nipashe jana, mjane huyo alisema  mume wake hakubahatika hata kufika hospitali kupata matibabu ya kuokoa maisha yake baada ya kubanwa na pumu alfajiri ya jana.

Mariam alisema mumewe alibanwa na ugonjwa huo saa 11:00 alfajiri na ndipo alipowasha gari ili akimbie hospitali kuwahi matibabu.

Alisema, lakini alipotoka tu kwenye uzio wa nyumba yake, alishindwa kuendesha gari na kulisimamisha katikati ya barabara.

Alisema baada ya kuziba barabara, gari la wanafunzi lililokuwa nyuma yake lilimpigia honi muda mrefu kujaribu kumtaka apishe njia, lakini wakati huo alishaishiwa nguvu na hakuwa na uwezo wa kuliendesha.

“Mume wangu huwa anasumbuliwa na pumu pamoja na shinikizo la damu, kwa pamoja kwa muda mrefu sana, na imekuwa ikimbana mara kwa mara na kuna kipindi huwa inazidi, lakini akitumia dawa huwa anapona,” alisema Mariam na kueleza zaidi:

“Na hata humu ndani dawa zake anazotumia huwa zipo wakati wote ikiwamo zile za kupuliza na inapozidi sana huwa anakimbilia hospitali.

“Lakini leo (jana) alfajiri ilimbana tena, kwa hiyo akawa amechukua gari lake na kuendesha mwenyewe ili aende hapo hospitali ya Kizuiani, lakini alifanikiwa kutoka tu hapo nje ya uzio, akashindwa kuendelea na kwa sababu ni barabarani akawa ameziba (njia).

“Dereva wa gari la wanafunzi alipofika na kuona barabara imezibwa akampigia honi na alivyoona hasogei akaenda kumwangalia.

“Alivyomsogelea na kuzungumza naye alimwomba dereva huyo wa wanafunzi amwendeshe hadi hospitali,  lakini kabla ya kufika mbali akawa amekufa humo humo kwenye gari.”

Mariam alisema juzi mume wake alikuwa na nguvu na alikuwa akiendelea vizuri na shughuli zake, ikiwamo kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni.

Kwa upande wake, kaka wa marehemu, Charles Hiza, alisema ni kweli mdogo wake alifariki kwenye gari kabla ya kufika hospitali.

“Hospitali siyo mbali, lakini alifia njiani wakati anapelekwa na huyo dereva wa gari la wanafunzi na alimsaidia baada ya kuona ameshindwa kuendesha gari na akiwa ameziba barabara,” alisema Charles.“Hospitali waliamua tu kupokea maiti na kuthibitisha kuwa amefariki.”

Alisema mwili wa marehemu Tambwe umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke wakati wakisubiri taratibu za mazishi kukamilika.

MIAKA 30Mtoto wa marehemu, Turo Hiza alisema baba yake alikuwa akisumbuliwa na pumu kwa karibu miaka 30 na tatizo hilo limekuwa likimtokea mara kwa mara.

“Kutembea na dawa imekuwa ni kawaida yake... vidonge, sindano (na) hata ya ‘kuspray’ (kupuliza), lakini kwa jana alizidiwa sana kwa sababu pia hakukuwa na mtu wa kumsaidia kuendesha gari,” alisema Turo.

“Kifo cha baba ni pigo kwetu sisi watoto wake, lakini pia ni pigo kwa familia nzima kwa sababu yeye ndiye alikuwa anategemewa sana na kama mnavyojua baba yetu, kama ambavyo alikuwa mcheshi huko kwenye mambo ya kisiasa, ndivyo hivyo alivyokuwa katika familia yake,” alisema mtoto huyo.

“Alikuwa ni rafiki yetu wa karibu, mshauri mkubwa na aliyetegemewa na kila mtu.”

Akizungumza wakati akihojiwa na kituo cha Redio cha East Africa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu ambaye ni mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, alisema pamoja na kwamba kifo cha Tambwe ni pigo kubwa kwa familia na chama, kwake ni zaidi.

“Kifo cha Tambwe kwangu ni pigo kubwa zaidi, nimemfahamu siku nyingi na ni rafiki yangu mkubwa sana, amekuwa miongoni mwa timu ya kampeni zangu, tumekuwa tukizunguka naye kila siku, kila mahali na amekuwa akiteka hisia za wananchi katika kampeni  kutokana na lugha yake ya ushawishi,” alisema.

“Tambwe hakutakiwa kuniacha katika kipindi hiki, kwa kweli kifo chake kimenishtua sana. Jana (juzi) tulifanya wote kampeni na tulipomaliza kama kawaida, wanachama walitusindikiza mpaka ofisi za Chadema Kanda ya Pwani kwa ajili ya kwenda kufanya tathmini na tulikaa pale hadi majira ya saa tano usiku ndipo tukatawanyika.”

Katibu wa Chadema mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo, alisema juzi baada ya kampeni za kumnadi Mwalimu, Tambwe alimuuliza maswali mengi ambayo hakuwahi kumuuliza ikiwamo kutaka kupafahamu nyumbani kwake.

“Siku zote tulikuwa naye, lakini juzi aliniuliza maswali ambayo hajawahi kuniuliza,” alisema Kileo.

Hii Hapa Hali ya Mfumuko wa Bei kwa Mwezi Januari

$
0
0
Hii Hapa Hali ya Mfumuko wa Bei kwa Mwezi Januari
Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Januari, 2018 umeendelea kubaki palepale asilimia 4.0 kama ilivyokuwa mwezi Disemba, 2017.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018 imekuwa sawa na kasi ilivyokuwakwa mwaka ulioishia mwezi desemba, 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema kuendelea kubaki palepale kwa Mfumuko wa Bei wa mwezi Januari, 2018 kumechangiwa na bei za baadhi ya bidhaa za vyakula kutobadilika.

“Baadhi ya bei za vyakula zilizochangia mfumuko wa bei kubaki asilimia 4.0 kati ya mwezi Januari 2017 na Januari 2018 ni pamoja na mahindi kwa asilimia 8.0, maharage kwa asilimia 4.3, samaki kwa asilimia 9.0 na ndizi za kupika asilimia 9.0”, alisema Bw. Kwesigabo.

Aidha Kwesigabo aliongeza kuwa baadhi ya bei za bidhaa zisizo za chakula zilizochangia mfumuko wa bei kwa mwezi Januari, 2018 kubaki palepale ni pamoja na sare za shule kwa asilimia 2.3, huduma za afya katika hospitali binafsi asilimia 10.0, mkaa asilimia 9.4, vitabu vya shule asilimia 2.7 pamoja na gharama za malazi kwa asilimia 3.2.

Vilevile Kwesigabo alisema kuwa kwa upande wa mfumuko wa bei usiohusisha vyakula na nishati kwa mwezi Januari, 2018 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 1.4 kutoka asilimia 1.3 kama ilivyokuwa mwezi Desemba 2017.

Kwesigabo aliongeza kuwa mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018 umepungua hadi asilimia 3.0 toka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2017 na kwa upande wa Kenya kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018 umeongezeka hadi asilimia 4.83 toka asilimia 4.50 kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba 2017.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo Ijumaa

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..
na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Wema Sepetu Alizwa Mamilioni ya Pesa

$
0
0
Wema Sepetu Alizwa Mamilioni ya Pesa
Wiki moja baada ya akaunti ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu kudukuliwa na wajanja wa mjini, mrembo huyo anadaiwa kupigwa mamilioni.

Habari zilizolifikia dawati la Gazeti la IJUMAA zilieleza kuwa, tangu mrembo huyo adukuliwe akaunti yake  yenye wafuasi zaidi ya milioni tatu, wajanja hao wamekuwa wakiitumia ndivyo sivyo kwa kuposti matangazo mbalimbali ya kibiashara ambapo wanachukua pesa bila ya Wema kujua.



Inaelezwa kuwa, Wema alikuwa akitumia akaunti hiyo kupitia namba ya simu ya mtandao maarufu wa mawasiliano nchini ambapo wadukuzi walifanikiwa kumiliki namba hiyo ambayo hutumia moja kwa moja kuwasiliana na wafanyabiashara mbalimbali wa mtandao kwa mgongo wa Wema na kuvuna pesa.


Wema Sepetu akiwa kwenye pozi.

Wajanja hao, kwa siku moja tu hutumia akaunti hiyo kuvuna zaidi ya laki saba ambapo kwa wastani wa tangazo moja huchukua kiasi cha shilingi elfu hamsini hadi laki moja.



WATAALAMU WANASEMAJE?

Juma Abdul ambaye ni mtaalam wa masuala ya mtandao aliliambia Ijumaa kuwa, kwa hesabu ya haraka, tangazo moja hudumu kwa saa moja hadi tatu kutegemeana na maelewano ya mteja.

“Kwanza wale wateja wanaotuma matangazo, wengi hufanya makubaliano kupitia Direct Messages (DM) ambapo huamini wanawasiliana na mhusika mwenyewe (Wema) na hutumia namba yake ya simu kumtumia pesa bila kujua kuwa ni wadukuzi.


…Akifanya yake.

“Katika makubaliano hayo, huenda yanakuwa kwa saa au hata siku nzima kutegemeana na kiasi walichoafikiana na kwa hesabu ya haraka ni laki saba hadi nane kwa siku. Kwa hiyo kwa wiki nzima tangu wameanza kutumia akaunti yake wamefanikiwa kujipatia kuposti zaidi ya matangazo hamsini ambayo kimahesabu ni zaidi ya milioni 20,” alisema Juma.



WEMA ASAKWA

Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Wema kujua nini hatma ya akaunti hiyo ambayo inampotezea zaidi ya mamilioni tangu imedukuliwa ambapo simu yake iliita bila majibu.

Hata hivyo, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ulioonesha wazi kumfikia lakini hakujibu.


MENEJA WAKE HUYU HAPA!

IJUMAA  lilifanikiwa kumpata Meneja wa Wema, Neema Ndepanya na baada ya kuelezwa taarifa hizo alifafanua kuwa, jambo hilo lipo mikononi mwao na kwamba kuna vijana wawili wanaofanya kazi kwa ukaribu na Wema, Bestizo na mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda ambao wanafuatilia kwa ukaribu.

“Ni kweli kabisa mpaka sasa Bestizo na Kadinda wanafuatilia kwenye mtandao wa simu (anautaja) kujua kwa nini wameshindwa kuthibiti suala hilo hadi sasa ambapo matapeli wanatumia njia kuwaibia watu kupitia akaunti hiyo,” alisema Neema.


Sugu Awatumia Ujumbe kwa Watanzania " Msiogope Pazeni Sauti"

$
0
0
 Sugu Awatumia Ujumbe kwa Watanzania " Msiogope Pazeni Sauti"
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ametuma ujumbe kwa watanzania na kuwasihi wasiogope bali waendelee kupaza sauti.


Mbunge huyo ametoa ujumbe wake huo kupitia Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule  (Prof Jay) ambaye yupo mkoani Mbeya kwa ajili ya kusikiliza kesi ya mbunge huyo ambaye anatuhumiwa kwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye mkutano wa hadhara.

Katika kesi hiyo inayoendelea leo asubuhi mkoani Mbeya anategemewa RCO na RPC wa Mbeya kusimama kutoa ushahidi wao leo.

Sugu pamoja  Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanadaiwa kufanya uchochezi kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Desemba 30, mwaka jana akiwa katika viwanja vya mikutano vya shule ya msingi Mwenge iliyopo jijini Mbeya.

Viongozi wote hao wawili walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Januari 16 na kupelekwa mahabusu siku hiyo hiyo , baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.

Sugu kwa sasa anawakilishwa mahakamani na Wakili Peter Kibatala baada ya Mawakili wake wa awali kujivua.

Video: Viatu Vyamuumbua Diamondi Atembea Peku Baada ya Kumkatikia Hadharani

$
0
0
Video: Viatu Vyamuumbua Diamondi Atembea Peku Baada ya Kumkatikia Hadharani
Nassib Abduli (Diamond) wakati akielekea Mahakama ya watoto  gafla kiatu alichokuwa amevaa aina ya Sendozi kilikatika ikamlazimu kukaa kwenye benchi wanalokaa askari Magereza .


Serikali Yawachukulia Hatua Jeshi la Polisi

$
0
0
Serikali Yawachukulia Hatua  Jeshi la Polisi
Serikali ya Tanzania kupitia Jeshi la Polisi nchini limewachukulia hatua mbalimbali za kinidhamu takribani askari 105 ikiwa pamoja na kuwafukuza kazi


Hayo yamebainishwa na  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Hamad Masauni katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA) Sofia Mwakagenda alilotaka kufahamu kuwa kuna sheria yeyote ya nchi inayomruhusu Askari Polisi kumkamata mtuhumiwa, kumpiga na kumtesa kabla ya kumfikisha katika kituo cha polisi.

"Kwa mujibu wa mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kifungu cha 11 kinaelekeza namna ya ukamataji, kwamba kifungu hicho hakimruhusu askari kumpiga na kumtesa raia wakati wowote anapokuwa kizuizini. Kanuni za utendaji wa Jeshi la Polisi (PGO) askari yoyote anapobainika kufanya vitendo vya kupiga au kutesa raia huchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi au kufikishwa mahakamani", amesema Masauni.

Pamoja na hayo, Masauni ameendelea kwa kusema "katika kipindi cha Januari hadi Disemba 2017 jumla ya askari polisi 105 waliotenda makosa mbalimbali wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa pamoja na kufukuzwa kazi".

Kwa upande mwingine, Masauni amesema muda mwingine aina ya ukamataji muharifu huwa inategemeana na muonekano wake ukoje.

Huduma za Serikali ya Marekani Zakwama kwa Mara Nyengine

$
0
0
Huduma za Serikali ya Marekani Zakwama kwa Mara Nyengine
Huduma za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaofaa.

Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa kufadhili bajeti hiyo kukamilika.

Lakini seneta wa Republican Rand Paul alimaliza matumaini ya kupigwa kwa kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya matumizi.

Mnamo mwezi Januari , kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku tatu.

Hatahivyo wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani ili kupata ,mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini.

Mabunge yote ya seneti na lile la uwakilishi ni sharti yaidhinishe matumizi hayo ya miaka miwili.


Maboksi ya pizza yalipelekwa katika bunge hilo huku watu wakitarajia kwamba utakuwa usiku mrefu kwa viongozi hao
Mkwamo huo ulitarajiwa ikiwa imesalia saa moja kabla ya muda kukamilika wakati bunge la seneti lilipopiga kura ya mapumziko.

Lakini licha ya kuchleweshwa ,bunge hilo linatarajiwa kupigia kura matumizi hayo.

Bunge la uwakilishi halitapiga kura yoyote hadi pale bunge la seneti litakapoidhinisha matumizi hayo.

Haijulikani ni vipi bunge la Congress litaendelea na vile huduma za umma zitakavyoathirika.

Hatua hiyo itasababisha kupanda kwa matumizi hadi $300bn (£215bn) - Kitu ambacho seneta Paul anasisitiza hawezi kuunga mkono.


Huku ufadhili wa bajeti ya idara ya ulinzi ukionekana kuwafurahisha maafisa wa maswala ya usalama, wahafidhana wanapinga athari za deni la taifa hilo.

Seneta Paul aliyekasirika aliwakemea wenzake wa chama cha Republican akidai ufisadi unaoendelea.

''Niligombea wadhfa huu kwa sababu nilikuwa mkosoaji mkubwa wa deni la Trilioni za madola katika utawala wa rais Obama''.

Hatimaye Serikali ya Kenya Yavifungulia Vituo vya Runinga Vya Citizen Tv na Inooro TV

$
0
0
Hatimaye Serikali ya Kenya Wavifungulia  Vituo vya Runinga Vya Citizen Tv na Inooro TV
Kutoka +254 Kenya ni headlines juu ya headlines Leo February 9, 2018 nikupe stori kuhusu Vituo vya runinga vya Citizen TV na Inooro Tv vimefunguliwa tena nchini Kenya baada ya kufungiwa kwa zaidi ya wiki moja.

 Vituo hivi viwili ndivyo vilivyokuwa vimesalia kurejeshwa hewani, baada ya KTN News na NTV kufunguliwa wiki hii.
Serikali ilizima mitambo ya TV hizo wiki iliyopita, baada ya kudai kuwa vilikuwa vimepanga kuonesha moja kwa moja kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa upinzani NASA, kama Rais wa Kenya.

Mahakama Yamuhukumu Miezi 16 Jela Sanchez

$
0
0
Mahakama Yamuhukumu Miezi 16 Jela Sanchez
February 9, 2018 nakusogezea stori kutoka kwa Staa mpya wa klabu  ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.

Hukumu hiyo imetolewa February 8, 2018 , Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.

Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela, lakini badala yake amelipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.

Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa kufanya kosa kama hilo.

Hizi Hapa Sababu Zinazofanya Wanawake Kupata Ukimwi Zaidi ya Wanaume

$
0
0
Hizi Hapa Sababu Zinazofanya Wanawake Kupata Ukimwi Zaidi ya Wanaume
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile leo Februari 9, 2018 ameweka wazi sababu nne ambazo zinapelekea wanawake wengi zaidi kuonekana wanapata maambukizi ya UKIMWI ukilinganisha na wanaume.


Ndugulile amesema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe (CUF), Khalifa Mohamed Issa ambaye alitaka kufahamu sababu za kitaalam zilizopelekea idadi kubwa ya wanawake kuwa ndio waathirika wa virusi vya UKIMWI kuliko wanaume. Akijibu swali hilo Ndugulile alikiri kuwepo kwa sababu nne.

"Sababu za kitaalam zinazosababisha wanawake wengi kuathirika zaidi na maambukizi ya VVU na UKIMWI yapo kama manne moja ni sababu ya kimaumbile na kibaolojia, mwanamke yupo katika hatari zaidi ya kupata VVU ukilinganisha na wanaume kwa kuwa maumbile ya mwanamke ni rahisi kupata michubuko wakati wa tendo la ndoa na hivyo kurahisisha virusi vya UKIMWI kupenya aidha maumbile ya mwanamke hupokea mbegu za kiume kutoka kwa wanaume wakati wa tendo la ndoa iwapo mwanamke atafanya mapenzi na mwanaume mwenye VVU mwanamke huyo anaweza kuambukizwa maambukizi ya UKIMWI"

Naibu Waziri wa Afya aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa

"Sababu ya pili kwamba kuna tabia na mazingira hatarishi ambayo husababisha hatari zaidi kwa wanawake kuambukizwa VVU ikiwa ni pamoja na kufanya biashara ya ngono na kuanza mapenzi katika umri mdogo, lakini sababu ya tatu ni mfume dume uliokuwepo katika jamii yetu unawapa fursa wanaume ya kuamua kufanya ngono na wanawake wengi, kutotumia kondom, kuoa wasichana wenye umri mdogo na hata kufanya ukatili wa kijinsia. Mfumo huu unasababisha wanawake kuambukizwa VVU na hata kushindwa kueleza ukweli kwa wenza wao kuhofia kuachika, kutengwa au kufukuzwa katika familia"

"Sababu ya mwisho ni kwamba wanawake wengi hujitokeza kupima kuliko wanaume hivyo nitoe rai kwa wanaume kujitokeza kupima tusitumie wenza wetu kama kipimo cha maambukizi yetu sisi" alisisitiza Ndugulile

Inakisiwa kuwa kwa Tanzania idadi ya watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI imefikia milioni moja laki tano huku idadi ya wanawake ikiwa kubwa zaidi kulinganisha na wanaume.

Ray C Amkingia Kifua Diamond "Naumiaga Sana Nikiona Huyu Mtoto Anasemwa"

$
0
0
Ray C Amkingia Kifua Diamond "Naumiaga Sana Nikiona Huyu Mtoto Anasemwa"
February 9, 2018 story ambayo imeshika headlines kwenye mitandao ya kijamii ni ya msanii mkongwe katika game ya Bongo Fleva Ray C baada ya kupost picha ya Diamond Platnumz na kuandika ujumbe kwa mashabiki wa muziki wanaomponda Diamond Platnumz

Kupitia ukurasa wa instagram wa Ray C ameandika caption inayosema



“Mi naumiaga sana nikiona huyu mtoto anasemwa semwa kila siku! Amefanya mapinduzi makubwa sana huyu mtoto! kama una macho unaona! Muziki wa Tanzania umefika mbali sana sababu ya watu kama hawa! Nigeria wanafika mbali sana kwa sababu wanasapotiana lakini Bongo sijui kwanini tunapenda” – Ray C

Kuzodoana! Kushushana! Kuchukiana! Dah!! Yani huyu alieanzisha hizi social media Mungu amlaani!! #MunguakulindeDogo#DontgiveU#Mtakujakumuuamtotowawatu”

Maneno haya yanatafsiriwa kuwa yanawalenga wale wote ambao hawaoni mafanikio aliyoyaleta Diamond Platnumz katika muziki wa Bongo Fleva na kuufanya ujulikane kimataifa zaidi na wamekuwa wakimuangalia Diamond katika upande ambao anakosea tu.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Lema Awasha Moto Bungeni Spika Kulipiwa Matibabu

$
0
0
Lema Awasha Moto Bungeni Spika Kulipiwa Matibabu
Mbunge  Godbless Lema amefunguka na kutoa malalamiko yake bungeni kuhusu kitendo cha Bunge kugharamia matibabu ya Spika wa Bunge Job Ndugai nchini India huku Mbunge Tundu Lissu mpaka sasa kutogharamiwa matibabu na bunge.

Lema amewasha moto huo wakati wakijadili taarifa ya Utawala bora, Katiba na Sheria na kusema kitendo ambacho Bunge linakifanya si haki na si sawa kwani ni undumilakuwili kuwapa watu wengine haki huku wengine wakinyimwa haki hiyo ya msingi.

"Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa Spika Job Ndugai nafahamu yupo India kwa ajili ya 'checkup' na matibabu na vilevile Mhe. Lissu ambaye na yeye yupo Ubelgiji kwa ajili ya matibabu. Mhe Spika anatumia fedha za bunge na Serikali kwa ajili ya matibabu na ni mbunge wa bunge la Jamhuri ya Tanzania na Mhe. Lissu tumeendelea kumkusanyia pesa mitaani kwa vikopo na yeye vilevile ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii 'double standard' inayoendelea katika taifa hili kwamba Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anaweza kutibiwa na Serikali na Bunge na Mbunge anayetokana na upinzani aliyepigwa risasi Dodoma hawezi kutibiwa na bunge wa Serikali Mhe. Mwenyekiti Bob Marley ana wimbo unasema 'only time will tel'"
"Chief yupo oposition kapigwa risasi, kifungu namba 24 section one ya Sheria ya uendeshaji bunge kinaeleza ni nani anapaswa kuwa na jukumu la pale inapotokea mbunge amepata matatizo na kama sitaweza kujadili maslahi ya wabunge siyo Lissu peke yake ya wabunge wote akiwa ameumia au hajaumia Mhe. nipo tayari nisiwe mbunge, kama sisi ni wabunge hatuwezi kujadili maslahi ya wabunge? Huyu anasimama anaongea mzaa hapa tunaogea kuna mtu amepotea anaitwa Ben Sanane na kuna watu wanapotea na haya mambo yanahusu utawala bora, Katiba na Sheria na haya mambo ni ya msingi kuliko madaraja, lami haya mambo tukiyajaili kwa mioyo tunajenga msingi imara kwa sababu kuna watu wamepotea kuna mtu ameumia yupo hospitali na tunapojadili hatuwashtumu tunataka mrudi kwenye mstari, mjue tunajadili damu za watu"

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amkosoa Rais Kuhusu Katiba Mpya

$
0
0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amkosoa Rais Kuhusu Katiba Mpya
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amekosoa jaribio la Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kutaka kubadilisha Katiba ya nchi hiyo hatua ambayo itamruhusu kukaa madarakani kwa muongo mwingine au zaidi.


Katibu Mkuu Guterres amesema, upinzani na mashirika ya kiraia ni lazima yashirikishwe kwenye maamuzi yoyote ya kubadili Katiba ili kuzuia uwezekano wa nchi hiyo kutumbukia kwenye mzozo zaidi.

Ameongeza kuwa, anatambua Burundi kama nchi inayo mamlaka ya kujiamulia mambo yake kama taifa huru lakini akaonya kuwa jambo la kubadili Katiba linahitaji maridhiano ya pande zote.

Wakati huo huo muungano wa wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni nje ya nchi CNARED unaendelea kulaani jaribio lolote la kubadili Katiba, ukibaini kwamba hali hiyo utaitumbukiza Burundi katika machafuko, zaidi ya yale yaliyotokea tangu mwaka 1993 hadi 2004.

Wamiliki wa Hoteli Wapewa Mtihani Mzito

$
0
0
Wamiliki wa Hoteli Wapewa Mtihani Mzito

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wamiliki na waendeshaji wa hoteli za daraja la kati kumwandikia mapendekezo yatakayomwezesha kutoa uamuzi sahihi wa namna wanavyoweza kuchangia mapato ya nchi.
Akizungumza jijini hapa leo Februari 9, Dk Kigwangalla  amesema uchunguzi wao umebaini kuwa hoteli zenye hadi ya kati na nyumba za kulala wageni maarufu 'Guest House' zimekua zikipokea watalii wengi kutokana na ubora wake unaochangiwa na unafuu wa bei.
Amesema tafsiri ya watalii haimaanishi Wazungu pekee bali ni wageni wowote wanaotumia nyumba za kulala wageni kutoka nje ya eneo hilo wakiwemo wanaofika kwa ajili ya mikutano na shughuli za biashara.
''Mnaweza kuniambia hoteli zetu zina hadhi ya chini kwa sababu bei ya chumba ni kati ya Sh40,000 hadi 70,000 lakini tunafahamu hizi hoteli Wazungu wameshazijua na wanalala kwenye hoteli zenu na mnaweza kuanza kuwatoza kwa dola,"amesema Kigwangalla.
Amesema lengo la Serikali ni kuwawezesha kukusanya mapato yanayosaidia kuipa uwezo wa kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali zikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara, usambazaji wa huduma ya maji, elimu na afya.

Mmoja wa wamiliki wa hoteli hizo, Amani Charles amesema wanakusudia mapendekezo watakayowasilisha kwa Dk Kigwangalla baada ya kukubaliana yatawawezesha kufanya biashara kwa njia nzuri badala ya kunyonywa kimapato kutokana na kutokuwepo usawa wa malipo.

Amesema mkanganyiko wa malipo unatokana na wao kutakiwa kulipa kwa dola ya Marekani 1.5 kwa kitanda ambayo ni karibu Sh2,000 wakati wateja wao wanalipa kwa fedha za Kitanzania huku uamuzi wa kulipa kwa kiwango maalumu kwa mwaka au kwa asilimia kulingana na wateja wanaolala.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema utaratibu ambao umeshawekwa na Mamlaka ya mapato(TRA) mkoa wa Arusha utaendelea kwa sababu Serikali imeshaweka malengo ya makusanyo na wale ambao ukadiriaji wa mapato yao umefanyika hivi karibuni utapatiwa majibu na Waziri wa Maliasili na Utalii.
Viewing all 104666 articles
Browse latest View live




Latest Images