Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Rais wa Liberia George Weah Amfuta Kazi Waziri wa Sheria

$
0
0
Rais wa Liberia George Weah Amfuta Kazi Waziri wa Sheria
February 9, 2108 Rais mpya wa Liberia Charles Gibson, baada ya malalamiko ambayo yamesababisha kupokonywa leseni ya Uwakili baada ya kumtapeli mteja wake.

Kabla ya uteuzi wake, Gibson alikuwa amepatikana na hatia hiyo na Mahakama ya Juu baada ya kumtapeli mteja wake Dola za Marekani 25,000 na kuagizwa kuzirejesha.
Rais Weah amemteua Musa Dean aliyekuwa Wakili katika Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi hiyo. Mwanasoka huyo wa zamani wa Liberia alichaguliwa kuwa rais mteule ikiwa ni katika jaribio lake la pili.

Dogo Janja, Irene Uwoya Mapenzi ni Moto ....... Amwita Dogo Janja Baba Krish

$
0
0
miezi kadhaa imepita tokea muigizaji Staa Irene Uwoya afunge ndoa na msanii Dogo Janja na kwa upande wao wameonekana kuridhika na ndoa yao ingawa maneno yalikuwa mengi kutoka kwa mashabiki.

Mapenzi kati yao yanaonekana kushamiri na kudumu hii ni baada ya Dogo Janja kukabidhiwa majukumu kama baba wa familia baada ya kuitwa Baba Krish katika comment kupitia instagram akaunti ya Irene Uwoya na jina hili kuonekana kama ndio hutumika kati yao.

Niki wa Pili Awafunda Wanandoa "Vyombo Hata Vikiwa Vichafu Namna Gani Huwezi Kwenda Vioshea Lalalani"

$
0
0
Niki wa Pili Awafunda Wanandoa "Vyombo Hata Vikiwa Vichafu Namna Nani Huwezi Kwenda Vioshea Lalalani"
Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amefunguka na kuitaka jamii hasa watu waliopo kwenye ndoa kuacha tabia ya kusuluhisha matatizo yao kupita majirani na badala amewashauri wafanyie chumbani.


Nikki ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo rundo la kesi za ndoa zinaanikwa kwenye mitandao ya kijamii huku wengine mtaani kwa lengo la kupata msaada juu ya tatizo hilo huku wengine wakitumia kama fimbo kuwadhalilisha wenza wao.

"Vyombo hata vikiwa vichafu namna gani huwezi kwenda vioshea jalalani, utavioshea kwenye karo tena karo safi. Basi ndoa hata kama imechafuka kiasi gani, jaribu kuisafishia chumbani sio kwa majirani au kitaani",amesema Nikki.

Nikki wa Pili ametoa ushauri huo kwa jamii ikiwa zimebakia takribani siku tano kuadhimisha siku maalumu ya wapenda nao kama wengine wanavyopenda kuita 'Valentine Day' ambapo siku hiyo inapambwa na upendo na faraja japo kuwa jamii inaimizwa kuwa na upendo kwa wenza wao siku zote.

Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini Apandishwa Kizimbani

$
0
0
Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini Apandishwa Kizimbani
Aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini, Ally Bondo Samaje amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka.

Samaje amefikishwa katika mahakamani hiyo  jijini Dar es Salaam leo Februari 9, 2018.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambna na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa  kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, April 9, 2013  na Juni 21, 2013 Makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.

Amesema akiwa Kaimu Kamishna wa Madini, alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kuishauri Bodi ya Madini katika utoaji wa leseni ya madini ya Graphite na Marble kwa Kampuni ya Tanzaniteone Mining Limited na State Mining Corporation.

Katika shtaka la pili, April 16, 2013 makao Makuu ya Wizara ya Nishati iliyopo wilaya ya Ilala, akiwa Kaimu Kamishna wa Madini na Katibu wa Bodi ya Ushauri wa Madini kutoka wizarani, alitumia vibaya madaraka yake kwa kutoa maelekezo kwa msaidizi wake John Nayopa kuandaa leseni za madini ya Graphite and Marble, bila kufuata sheria ya madini.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili na mmojawapo kusaini bondi ya Sh 50milioni.

Pia mshtakiwa hatakiwi kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Mahakama.

Instagram, Twiter Zampa Utajiri Neymar

$
0
0
Instagram, Twiter Zampa Utajiri Neymar
Kweli mwenye nacho uongezewa. Mshambuliaji ghali zaidi Neymar anaingiza karibu nusu milioni kwa kila ujumbe wake anaotuma kwenye mitandao yake ya kijamii.
Kwa mujibu wa utafiti mpya unaonyesha vyanzo vya mapato ya Neymar umeonyesha jinsi nyota huyo wa Paris Saint-Germain ni mtambo wa kutegeneza fedha.
Pamoja na kupokea euro 37 milioni kwa mwaka katika mshahara wake, nyota huyo wa Brazil kwa sasa anaingiza katika zaidi ya euro 459,000 kwa kila tangazo analotuma katika akaunti zake za Twitter, Instagram kwa mujibu wa utafiti wa Blinkfire.
"Kama ukichukua mambo yake yote aliyotuma katika akaunti zake za mitandao ya kijamii kwa Januari na Neymar, inakadiliwa kufikia jumla ya thamani ya euro 34 milioni," aliandika mkurungezi wa Blinkfire, Christian Olivares. "Kiasi hiko ndicho anachopaswa kuingiza kutokana na matangazo anayoweka hapo."
#bornmercurialpic.twitter.com/8c3aHEkLG7
? Neymar Jr (@neymarjr) 6 de febrero de 2018
Akaunti hizo zimeendelea kupata watu wengi wanaozifuatilia kila siku kwa sasa katika Instagram inawatu wanaoifuata 88.8 milioni, Facebook watu 60 milioni wakati katika Twitter anawatu 37.6 milioni.

Waziri Mwigulu Ata Agiza kwa Jeshi la Polisi Kuziachia Pikipiki Zinazoshikilia

$
0
0
Waziri Mwigulu Aagiza Kuachiwa Pikipiki Zinazoshikiliwa na Jeshi la Polisi
February 9, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dr. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa muda mrefu na zina makosa madogo na kwamba wasikae nazo kwa muda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Dr. Mwigulu amesema zile yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, dawa ya kulevya wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka Mahakamani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazirudishe kwa wamiliki na kuwapa elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi, waelekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono kwa kutatua yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” – Dr Mwigulu

Amesema kuwa ipo haja sasa vijana kufundishwa zaidi kuhusu sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila anapopita katika vituo vya polisi hukuta pikipiki nyingi na makosa yao ni madogomadogo.

Yanga Kibaluani Kesho Kuumana na Shelisheli St Louis

$
0
0
Yanga Kibaruani Kesho Kuumana na Shelisheli St Louis
Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kushuka Dimbani Kesho Jumamosi kuumana na Mabingwa wa Shelisheli St Louis, lakini kikosi hicho kitawakosa nyota wake wanne wa kikosi cha kwanza.

Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa ya Daktari wa timu hiyo Edward Bavu imeonesha kuwa wachezaji Donald Ngoma, Abdalah Shaibu, Yahana Nkomola na Amiss Tambwe hawatakuwa sehemu ya mchezo huo.

Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema, mchezo wa kesho ni muhimu kwa timu yake na kwani utaisaidia Yanga kufikia malengo yake katika michuano ya kimataifa.

Kwa upande wake kocha mkuu wa St Louis ya Shelisheli Michel Renald amesema wamekuja kucheza na yanga na wanaiheshimu na mchezo wa kesho watahakikisha wanautumia vyema kupata matokeoyatakayowawezesha kusonga mbele katika ligi ya Mabingwa.

Yanga inatarajiwa kutupa karata yake ya kwanza katika michuano ya ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa kuumana na mambingwa wa Shelisheli St Louis katika mchezo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Uhuru Jijini Dar es salaam.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba, Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?


Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Sakata la Yanga Kuzuiliwa Kufanya Mazoezi Katika Uwanja wa Taifa Latinga Bungeni

$
0
0
Sakata la Yanga Kuzuiliwa Kufanya Mazoezi Katika Uwanja wa Taifa Latinga Bungeni
Sakata la Klabu ya Yanga kuzuiliwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa lililotokea siku ya jana (Alhamisi) limezua sura mpya na kufanya Waziri mwenye dhamana Dkt. Harrison Mwakyembe kulitolea ufafanuzi Bungeni.


Dkt. Mwakyembe ametoa ufafanuzi huo leo (Ijumaa) katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge kilichomalizika kwa kuhairishwa shughuli zake mpaka Aprili 03, mwaka 2018 mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali ambapo aliitaka serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iingilie kati suala la timu za Tanzania zikienda kucheza kimataifa huwa zinawekewa zengwe lakini wao wakija kucheza huku wanapewa kipaumbele baadhi ya vitu.

"Haturuhisiwi hicho kiwanja kukitumikisha kubeba michezo zaidi ya mitatu kwa wiki moja na endapo utafanya hivyo unaingiza uswahili na hata kikiharibika huwezi kwenda kudai kwa mtu aliyekupa 'guranty' kwamba kitaka zaidi ya  miaka 10", amesema Dkt. Mwakyembe.

Pamoja na hayo, Dkt. Mwakyembe ameendelea kwa kusema "kwa hiyo wiki hii tuna mechi mbili muhimu kesho (Jumamosi) wanacheza Yanga dhidi ya St. Louis na kesho kutwa wanaingia Simba SC (Jumapili) kucheza na timu kutoka Djibout. Kanuni za kimataifa zinataka timu ngeni hiyo ya kimataifa lazima ifanye mazoezi katika kiwanja ambacho kitachezwa mechi hiyo lakini hata FIFA wanatambua hicho kiwanja ni cha timu za hapa nchini. Kwa hiyo Yanga na Simba wanaufahamu vizuri uwanja huo ndio maana wakapewa kipaumbele wageni ili waweze nao kuujua".

Aidha, Dkt. Mwakyembe amesema anahisi kuna uswahili umeshaanza kuingia katika uwanja wa Taifa na kutaka baadhi ya watu kushughulikiwa.

"Uswahili umeshaanza kuingia katika uwanja wetu wa Taifa, na mimi nashukuru kwa haya maneno niliyoyapata nadhani kuna vijana wangu pale wanahitaji wadhibitiwe kwa kweli. Kwa hiyo nataka nifafanue kwamba ni haki ya wageni wapewe nafasi ya kufanya mazoezi na sisi tukafanyie katika viwanja vingine", amesisitiza Dkt. Mwakeymbe.

Kwa upande mwingine, Dkt. Mwakyembe amesema ili uwanja huo uweze kutunzika katika mazingira mazuri bila ya kuharibiwa jambo lolote ndani ya  miaka 10 ni lazima yawepo masharti ya utumiaji.

CUF: Lipumba Ajaingia Mitini Kumnadi Mgombea Ubunge Siha

$
0
0
CUF: Lipumba Ajaingia Mitini Kumnadi Mgombea Ubunge Siha
Chama cha Wananchi (CUF), kimesema mwenyekiti wao wa Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, hajaingia mitini katika kumnadi mgombea wao ubunge Jimbo la Siha, Tumsifuel Mwanri.

Ujio wa Profesa Lipumba umeahirishwa zaidi ya mara tatu, na ndiye mara zote alikuwa akitajwa kuwa angezindua kampeni za chama hicho Jimbo la Siha.

Awali mgombea huyo, amekaririwa akisema chama hicho kingezindua kampeni Januari 27 katika kijiji cha Miti mirefu na mgeni rasmi angekuwa Profesa Lipumba, lakini hata hivyo hakutokea siku hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutotokea, chama hicho kikatoa taarifa kuwa Profesa Lipumba angezindua kampeni za chama hicho Februari 8 katika mji wa Sanyajuu ingawa nako hakutokea.

Pamoja na kutotokea, mgombea wake wa ubunge ameendelea na kampeni zake akinadiwa na Naibu Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CUF Taifa, Masoud Omar hali inayozua minong’ono.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 9, Omar amesema, Profesa Lipumba hajaingia mitini kwenye kampeni za Jimbo la Siha na kwamba kilichotokea ni ratiba zake kuingiliana na za Siha.

Omar amesema kuna baadhi ya watu katika Jimbo hilo wanaeneza uvumi  kuwa Profesa Lipumba amemtelekeza mgombea wao jambo alilosema si kweli bali wanaendelea kufanya mawasiliano naye na atafika jimboni humo.

Amefafanua kuwa awali alitakiwa kuzindua kampeni za chama hicho Kata ya Miti Mirefu lakini ratiba ziliingiliana na kutakiwa kwenda Pemba na juzi alikuwa na mkutano na viongozi wa CUF Kinondoni.

“Tunafanya mawasiliano naye atakuja kwenye kampeni wala msitie hofu ili kuhakikisha jimbo tunalichukua na watu wapuuze maneno kwamba Profesa Lipumba ameingia mitini,” amesema.

Akiwa katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Lawate, mgombea ubunge wa CUF, Mwanri, amesema endapo watamchagua kuwa mbunge wao atahakikisha anaiboresha miundombinu ya soko la Lawate.

Tenga Apata Shavu Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa (TFF)

$
0
0
Tenga Apata Shavu  Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa (TFF)
Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF), Leodgar Tenga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa(TFF).

Waziri wa Habari Utamaduni wa Michezo, Harison Mwakyembe amethibitisha hilo kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Ijumaa mchana.

Mwakyembe pia amewateua wajumbe sita wa BMT ambao ni Profesa Mkumbwa Mtambo, Beatrice Singano, Kanali Mstaafu Juma Ikangaa,Joseph Ndumbaro,Rehema Madenge na Salmini Kaniki.

Awali, BMT ilikuwa chini ya Dioniz Malinzi ambae uteuzi wake ulisitishwa na Wizara baada ya kutoridhika na utendaji wake.

Haji Manyara Ampa Makavu Kivuyo wa ITV

$
0
0
Haji Manyara Ampa Makavu Kivuyo wa ITV
Yupo mwanahabari mmoja jana aliandika makala isemayo ufungeni  Uwanja wa Taifa,kwenye andishi lake liliojaa makosa makubwa ya kalamu na tanahui za kiuandishi,mwandishi huyo licha ya upotofu mkubwa aliuofanya juu ya matumizi ya Uwanja wa Taifa pia alinilisha maneno ya uongo juu ya kauli yangu kuhusu mchezo wa kesho baina ya Yanga na timu toka Shelisheli.

Najua kwa kumjibu kwangu itampa umaarufu ambao siku hizi unaitwa kiki,lakini kumuacha itakuwa anadhani mm au wanasimba wanamuogopa kwa kuwa anafanya kazi ya utangazaji kwenye moja ya vituo vya Televisheni vinavyoheshimika nchini.

Kwa hili la Yanga kutoruhusiwa kuutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na kulaumu wamiliki wa uwanja ambao ni Serikali ni wajibu wangu kama mdau wa Soka kumhabarisha huyu jamaa anaependa kutumia lahaja za kikwaya kwaya na kingonjera ktk utangazaji kwamba,hakuna mahali kokote na nchi yoyote Afrika kwa klabu ya Tanzania au Timu ya Taifa ilipozuiwa kutumia uwanja utakaotumika siku ya mchezo ikiwa ugenini.


Hiyo ni kanuni ya FIFA na CAF na haina mjadala wa matumizi yake,kwake yeye anadhani kwa Washelisheli kuruhusiwa kuutumia Uwanja wa Taifa leo ni kuwapendelea,laa hasha!ni kanuni ndizo zinazotaka timu ngeni kutumia uwanja utakaotumika kwa ajili ya mchezo siku moja kabla ya mechi yenyewe.

Pia kwenye makala yake ameelezea kusikitishwa kwake na Yanga kutoruhusiwa kuutumia Uwanja wa Taifa kwa mazoezi wakati huu ikijiandaa kwa ajili ya mchezo huo,huku akiishutumu wamiliki kuwa wanataka kuugeuza uwanja huo kwa mambo ya kisiasa..hakuishia hapo mpiga zumari huyo akawalaumu na walioukarabati uwanja utaalamu wao ni wa kutiliwa mashaka kwa kupanga matumizi ya Uwanja huo wa kisasa kabisa.

Na akahoji mbona vwanja vkubwa Afrika na Ulaya vinatumika kila siku akimaanisha hata kwa mazoezi?  Laa haulaaaa!!! Jamaa hajui kisha anajiona anajua..nimpe elimu ndogo tu ya ufahamu kwake na kwa wingine,, hakuna vilabu vinavyotumia hvyo alivyoviita vwanja vikubwa kwa mazoezi..mazoezi kwenye hvyo vwanja hutumiwa na timu ngeni siku moja kabla ya mchezo,narudia ni timu ngeni tena siku ya kuamkia mchezo.

Klabu zote hutumia vwanja vyake vya mazoezi kwa maandalizi yake ya mechi na sio kukaa kulaumu Serikali na waliovikarabati kampuni ya Spotipesa huku hujui nn unaandika.

Kujitia uzalendo pori kwa kulaumu jambo la kikanuni ni kujitia hamnazo kusudi, kwangu mm uzalendo ungekuwa kutuhimiza Simba na Yanga tuwe na vwanja vyetu wenyewe kwa ajili ya mazoezi,Simba tuanze haraka mradi wa Bunju na kwa Yanga shime iendelee ya kujaza vifusi pale Jangwani.

Mtangazaji huyu ambae hutumia sanaa ya majukwaani ktk kazi yake pia alinilaumu mm na kunilisha maneno eti nimewataka washabiki wetu wakaishangilie Yanga kwenye mchezo wake wa kesho na akadai nafanya propaganda ili kuwahadaa wanayanga.

Kwanza mm sikusema washabiki wetu wakaishangilie Yanga.. nilichosema na kutoa rai yangu tuachane na utamaduni wa kuzomeana inapokuja ishu ya kuwakilisha nchi,kwangu mm huo c utamaduni wa kishabiki kokote ulimwenguni,hauwezi kuukuta nchi yoyote hata zile zenye ushabiki uliokubuhu wa mpira,iwe Spain,Misri,Uturuki na hata Tunisia.

Mcheza sanaa huyu alienda mbali zaid kwa kudai eti nimesema hvyo kwa kuwa najua Yanga watashinda kesho,hvyo ninawahadaa,uhh lalaaa! Sijui ni aina gani ya mwandishi anayejipambanua hadharani mahaba yake hadharani kwa klabu moja,Na kwa kufanya hvyo sijui atapataje legitimacy ya kupata stori  toka kwetu!!!

Kauli hyo ilipaswa itolewe na uongozi wa Yanga lakini pia wao hawawezi sababu mm nimeongea na washabiki wetu ambao mm ni msemaji wao.

Inaonekana jamaa ana chuki zake na Simba na ndio maana mara nyingi amekuwa akitushambulia bila sababu, makala yake ya mwisho huku akitumia tafsida ya waimba Taarabu,alimtahadharisha kocha wetu mpya kwa mafumbo yanayotumiwa majumbani kwa kebehi kubwa sana..

Nilikaa kimya sababu hang'ati, yaani hana sumu, lakini kwa hili nimeamua kumjibu sababu uongo ukiachwa sana huaminika na mm nimejiapiza nikiwa msemaji wa klabu hii kubwa kabisa nchini,sitaacha klabu yangu ishutumiwe kwa mambo ya uongo na ya kuzua toka kwa yoyote yule,wajibu wangu mwingine klabuni ni kuitetea na kulinda Image na brand ya Simba.

Sina maana kuwa kila tufanyalo ni sahihi,au nnazuia kukosolewa,Hapana....maana yangu tukosolewa tunapostahili tena kwa heshma,hii ni klabu ya Watu sio klabu ya kijiweni....

Ijumaa kareem...

Yanga Wamuweka Ngoma Kiporo

$
0
0
Yanga Wamuweka Ngoma Kiporo
Suala la mchezaji Donald Ngoma limebaki kiporo tena baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kushindwa kufikia maamuzi pamoja na siku za hivi karibuni kuahidi kulishughulikia.

Akiongea leo Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema taarifa ya awali kutoka ofisi ya katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Mkwasa, kuwa suala la Ngoma linafanyiwa vikao jambo hilo limeshindwa kukamilika.

''Ukaribu wa michezo na majukumu mengi hapa katikati umefanya kushindikana kufikiwa kwa kile kilichokuwa kimepangwa au kulichotakiwa kujadiliwa kuhusiana na mchezaji huyo'', amesema.

Aidha Ten pia ameongeza kuwa majeraha kwa wachezaji hayazuiliki na pia wapo wachezaji waliokaa nje kwa muda mrefu na wakarejea wakasaidia timu zao hivyo Donald yupo ni mchezaji wa Yanga mpaka hapo taarifa nyingine itakapotolewa.

Kwa upande wake daktari wa timu hiyo Yanga Dr. Bavu amesema Ngoma ni miongoni mwa wachezaji wanne ambao bado ni majeruhi. Hivi karibuni Yanga walitoa taarifa kuwa wanasuburi ripoti ya dakatari juu ya afya ya Ngoma ili waweze kutoa uamzi.

Nataka Shetta Aniite ‘Baby ’Sipendi Aniite Mama Qayllah, – Mke wa Shetta

$
0
0
Nataka Shetta Aniite ‘Baby ’Sipendi Aniite Mama Qayllah,  – Mke wa Shetta
Mke wa msanii wa muziki Shetta, ‘Mama Qayllah’ amefunguka kwa kudai kwamba hapendi kuitwa ‘Mama Qayllah’ na mume wake huyo.


Mrembo huyo ambaye haonekani kwenye matukio mengi ya starehe, amedai anapenda mume wake amuite Baby na sio jina lingine.

“Kusema kweli kitu ambacho sipendi kutoka kwa mume wangu ni kuitwa ‘Mama Qayllah’, mimi nataka aniite Baby,” Mama Qayllah alikiambia kipindi cha Leo Tena Cha Clouds TV.

Wawili hao wameweza kukaa kwenye maisha ya ndoa kwa miaka 7.

Kwanini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.


NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.


MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA.


MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.


NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,


Je unamali yako unauza hupati wateja?

Wasiliana nami 0716-263605

Shahidi Akana Kuona Mkojo wa Wema Sepetu

$
0
0
Kesi ya msanii  Wema Sepetu ya kukutwa na msokoto wa bangi imesikilizwa jana February 8, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Inspekta wa Polisi, Wille aliieleza Mahakama kuwa hakuwepo wakati Wema akichukuliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa serikali.

Shahidi huyo aliyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati alipoulizwa maswali na Wakili wa Wema, Alberto Msando.

Katika ushahidi wake, Inspekta Wille, alidai hakuwahi kupeleka sampuli za mkojo  za washtakiwa wenzake Wema ambao ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Shahidi  huyo alidai kuwa aliijaza fomu ya kupeleka sampuli ya mkojo wa Wema saa nne asubuhi akiwa ofisini kwake na kuandika maneno  mkojo uko ndani ya chupa ya plastiki.

==>Mahojiano kati ya wakili Msando na shahidi yalikuwa hivi:

Wakili: Katika hii fomu shahidi umejaza kuwa mkojo ulikuwa ndani ya chupa ya plastiki. Nataka kujua je uliuona huo mkojo kama ni wa Wema?

Shahidi:  Nilijaza fomu kutokana na uzoefu wangu wa miaka 15.

Wakili: Ulijaza fomu ya kisheria ya kupima sampuli kabla ya mshtakiwa kufika kwa Mkemia Mkuu wa Serikali?

Shahidi: Ndio uzoefu wangu.

Wakili: Mkojo uliokabidhi uliupata wapi?

Shahidi:Kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakili: Je ulikuwapo wakati mshtakiwa anachukuliwa sampuli ya mkojo?

Shahidi : Sikuwapo.

Wakili: Inawezekana ukasema hujui kilichokuwa ndani ya chupa ya plastiki kwa vile haukuwapo?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Wakati Mkemia Mkuu unamkabidhi mkojo  chupa ya plastiki ilikuwa imewekwa lakiri?

Shahidi: Ndiyo

Wakili: Je, ulikaa muda gani katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali?

Shahidi: Niliondoka baada ya kukabidhi fomu, ilikuwa kama saa 5:00 asubuhi.

Wakili: Ulihusika kwenda kukagua nyumbani kwa mshtakiwa wa kwanza?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Je, ulipekua chumba anacholala mshtakiwa wa kwanza?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Je, vitu mlivyokuta katika upekuzi wenu vilikutwa sehemu gani?

Shahidi: Katika upekuzi msokoto wa bangi na rizza ya kusokotea bangi ilikutwa jikoni juu ya kabati la vyombo na walikuta msokoto wa bangi uliotumika ukiwa ndani ya kiberiti dirishani katika chumba wanacholala wafanyakazi wake.

Wakili: Je, kwenye hicho chumba mlichokuta msokoto ni wa mshtakiwa wa pili au wa tatu?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Je, huo msokoto ni wa mshtakiwa wa kwanza?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Je mshtakiwa wa pili na watatu alipimwa sampuli ya mkojo?

Shahidi: Hapana.

 Mahakama iliipokea hati ya ukamataji mali iliyojazwa katika upekuzi uliofanyika nyumbani kwa Wema Sepetu  kama kielelezo.

Kesi imeahirishwa hadi Februari 26 na 27, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka.

Habari Njema kwa watumishi wote wanaoidai Serikali....Madeni Yote Yanalipwa Mwezi Huu

$
0
0
Serikali imetangaza neema kwa watumishi wake wote wanaoidai malimbikizo ya madeni kwa kueleza kuwa itaanza kuyalipa madeni hayo ndani ya mwezi huu wa Februri 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Fedha na Mipango ameeleza kuwa mwisho wa mwezi Februari 2018, serikali itawalipa kwa mkupuo mmoja watumishi wake wote malimbikizo ya madeni na madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi.

“Madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi Bilioni 16.25 kwa walimu 15,919, na Tsh. Bilioni 27.15 kwa watumishi 11,470 wasiokuwa walimu. Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya TZS Bilioni 43.39 yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja,” amesema Waziri Mpango.

Ameongeza kuwa kwa malipo ya madai haya ambayo kwa baadhi ya watumishi yana muda wa zaidi ya miaka kumi, majina ya wadai yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho Jumamosi februari 10, 2018.

“Malipo ya madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka 10, majina ya walipwaji yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018,” amesema Waziri Mpango.

Waziri Mpango amesema madai haya yanajumuisha malimbikizo ya mishahara, nyongeza ya mishahara pamoja na tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu nafasi.

“Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara… Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi Bilioni 43.39 ikiwa ni 34% ya madai yote, yalihakikiwa na kuonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho” amesema.

Aidha amesema kutokana na zoezi la uhakiki lililofanyika, serikali imeweza kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na 66% ya madai yote zilizokuwa zilipwe kimakosa kutokana na uwepo wa watumishi wengi wenye vyeti feki.

“Zoezi la uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika, limeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na 66% ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo… Kama tungekurupuka tu tukalipa, tungekuwa tumetumia vibaya fedha za watanzania shilingi bilioni 84.22,” amesema Waziri.

Vile vile amesema kuwa serikali itaendelea kulipa madeni yote ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuepukana na malimbikizo ambayo kwa namna moja au nyingine, yanaweza kuisababishia serikali hasara.

“Serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza, ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili,” amesema.

Sugu na Masonga Waachiwa kwa Dhamana....Hukumu Yao ni February 26

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga katika kesi inayowakabili ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Sugu na Masonga wamekaa mahabusu kwa muda wa siku 24 baada ya kunyimwa dhamana na mahakama hiyo kutokana na hoja za upande wa  Jamhuri.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wawili baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia mahakama hiyo kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.

Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kwamba Februari 19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo.

Hakimu Mteite amekubaliana  na hoja hiyo ya mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.

"Washtakiwa wote wanaachiwa kwa dhamana, na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa hati ya dhamana ya maneno ya Sh5 milioni kwa kila mmoja.

Msigwa apelekwa Kamati ya Maadili

$
0
0
Dk Tulia Ackson Mwansasu amempeleka Mbunge wa Iringa  Mch Peter Msigwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili akatoe ushahidi wake wa namna ufisadi ulivyofanyika kwenye mradi wa mfumo wa uhamiaji mtandao (E-Immigration)

Tulia Ackson amesema hayo baada ya Msigwa kudai kuwa ana taarifa za kutosha juu ya ufisadi uliofanyika katika mradi uliozinduliwa na Rais Magufuli hivi karibuni na kudai kuwa Kambi ya Upinzani bungeni wanazo nyaraka za kutosha ambazo hazina mashaka kuhusu namna ufisadi ulivyofanyika katika mradi huo chini ya Serikali ambayo inajipambanua kupambana na ufisadi. Kufuatia kauli hiyo ndipo hapo Naibu Spika aliagiza Mbunge huyo kwenda kutoa taarifa hizo kwa Kamati ya maadili.

"Mhe. Msigwa taarifa ulizonazo kuhusu ufisadi uliofanyika kwenye hili zoezi zipelekwe kwenye hii kamati, Kamati itakuja kulishauri bunge tufanye nini na huo ufisadi unaoendelea hayo maeneo kwa hiyo naiagiza kamati imuite Mhe. Peter Msigwa na yeye namuagiza Mhe. Msigwa apeleke huko hizo nyaraka ili bunge liweze kushauriwa na kuchukua hatua mahususi" alisema Tulia Ackson.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli  Januari 31, 2018  alizindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli Asiikitishwa na Hatua Zilizochukuliwa na Umoja wa Mataifa -UN

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa waliopo hapa nchini kuwa katika mwaka 2018 Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kuboresha miundombinu ya barabara, reli na usafiri wa anga, kuongeza uzalishaji wa umeme na kukabiliana na vikwazo vya biashara.

Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 09 Februari, 2018 katika hafla ya mwaka mpya aliyowaandalia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kutokana na dhamira hiyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Mabalozi hao kuwahamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchi zao, kuja hapa nchini kuwekeza na kufanya biashara mbalimbali na kwamba Serikali itatoa ushirikiano wowote utakaohitajika.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema mwaka 2017 ulikuwa wenye mafanikio makubwa kwa Serikali kitaifa na kimataifa, ambapo iliendelea kutekeleza mpango wa maendeleo wa miaka 5 (2016/17-2020/2012) unaolenga kuiwezesha nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na ametaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi kulikowezesha kuongezeka kwa mapato kwa asilimia 7.87, ikiwemo rekodi ya juu kuwahi kufikiwa hapa nchini ya ukusanyaji wa Shilingi Trilioni 1.66 mwezi Desemba 2017.

Mafanikio mengine ni ukuaji mzuri wa uchumi wa asilimia 6.8 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017, kudhibiti mfumuko wa bei uliokuwa chini ya asilimia 5.5, kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuboresha huduma za kijamii zinazowagusa zaidi wananchi kama vile afya, elimu na maji.

Kuhusu azma ya kujenga viwanda, Mhe. Rais Magufuli amesema utekelezaji wa azma hii unakwenda vizuri ambapo katika kipindi cha miaka miwili viwanda 3,500 vimejengwa na vingine vingi vinaendelea kujengwa.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema kama ilivyofanya katika mwaka 2017 Tanzania itaendelea kutekeleza majukumu mbalimbali ya kikanda na kimataifa ikiwemo kushiriki katika juhudi za kutafuta amani, kushiriki harakati za usuluhishi wa migogoro ikiwemo ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jamhuri ya Afrika ya Kati, Lebanon, Sudan na Sudani kusini.

Hata hivyo ameelezea kusikitishwa kwake na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuanza kutekeleza sera ya kupunguza gharama kwenye misheni za kulinda amani kwani kwa kufanya hivyo itadhohofisha jitihada za kutafuta amani kwenye maeneo yenye migogoro na kuhatarisha maisha ya walinda amani pamoja na raia wasio na hatia wanaoishi kwenye maeneo yenye migogoro.

Pia, Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na nia njema ya mpango wa majaribio wa kutafuta suluhu la kudumu ya tatizo la wakimbizi (Comprehensive Refugee Response Framework – CRRF) Tanzania imeamua kujitoa kutokana na changamoto za kiusalama na ukosefu wa fedha za kugharamia mpango huo.

Mhe. Rais Magufuli amezungumzia taarifa za kukamatwa kwa meli zenye kupeperusha bendera ya Tanzania zikiwa zimehusika katika uhalifu na kuwahakikishia Mabalozi hao kuwa meli hizo sio za Tanzania bali zilijipatia usajili wa Tanzania, na kwamba kufuatia hali hiyo Tanzania imechukua hatua ya kusitisha usajili wa meli zote 470 zenye usajili wa Tanzania na kusitisha zoezi la usajili mpya wa meli wakati uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika.

Kwa upande wake Naibu Kiongozi wa Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa hapa nchini ambaye ni Balozi wa Saharawi Mhe. Brahim Salehe El-Mami Buseif amempongeza Mhe. Rais Magufuli na Serikali yake kwa juhudi kubwa zilizofanyika kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na kuongeza ukusanyaji wa mapato na ameahidi kuwa Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kufanikisha miradi mbalimbali.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Februari, 2018
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images