Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live

BREAKING: Tangazo la Majina ya Watumishi wa Umma wanaostahili kulipwa madai ya malimbikizo ya Mishahara baada ya Uhakiki

$
0
0
Tangazo la Majina ya Watumishi wa Umma wanaostahili kulipwa madai ya malimbikizo ya Mishahara baada ya Uhakiki

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..
na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Iyobo Hawezi Kuzishangaa Picha Zangu za Utupu- Aunt Ezekiel

$
0
0
Iyobo Hawezi Kuzishangaa Picha Zangu za Utupu- Aunt Ezekiel
STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amesema kuwa Moses Iyobo ambaye ni mzazi mwenziye hashtushwi hata kidogo na picha anazopiga akiwa amevaa mashuka na za nusu utupu kwa sababu anajua ni kwa ajili ya kibiashara tu.

Akizungumza na Mikito Nusunusu Aunt, alisema kuwa mara nyingi hata picha ambazo anapiga na Iyobo anakuwa pembeni kwa maana ni za matangazo ya sabuni yake hivyo hawezi kuvaa nguo ya kawaida anapokuwa bafuni zaidi ya taulo kuonyesha uhalisia.

“Iyobo hawezi hata siku moja akazishangaa picha hizo kwani ni za matangazo nazoziweka mtandaoni, maana anajua kabisa ni za kazi na si za kitu kingine chochote kile kwa maana hata yeye anakuwepo na anatoa mawazo mbalimbali katika picha hizo zipigwaje,” alisema Aunt.

Tambwe Hizza Kuzikwa Leo Makaburi ya Chang'ombe

$
0
0
Tambwe Hizza Kuzikwa Leo Makaburi ya Chang'ombe
MWILI wa Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Richard Tamilway maarufu kwa jina la ‘Tambwe’ aliyefariki dunia jana asubuhi nyumbani kwake Mbagala Kizuiani, unatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi katika Makaburi ya Temeke Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Global Publishers, kaka wa marehemu aitwaye Charles Tamilway amesema kuwa taratibu za kuuhifadhi mwili wa kaka yake katika nyumba yake ya milele zinaendelea kufanyika na kama ratiba isipobadilika, mwili huo utahifadhiwa kesho Jumamosi kama ilivyopangwa.

Naye mjane wa marehemu, Mariamu Masoud, alisema  mume wake hakubahatika hata kufika hospitali kupata matibabu ya kuokoa maisha yake baada ya kuugua ghafla, hivyo anamuomba mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mumewe mahali pema peponi.

Hizza anafahamika sana kwa siasa zake akiwa Chama cha Wananchi (CUF), baadaye akahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa chama hicho na mwaka 2015 aliamua kuondoka CCM na kuhamia CHADEMA.

Team Zari Wamtolea Uvivu Esma Wamwita Mnafki “Akiwa na Mnafiki Akili Zangu Ndio Zilivyoamka Leo”

$
0
0
Team Zari Wamtolea Uvivu Esma “Akiwa na Mnafiki Akili Zangu Ndio Zilivyoamka Leo”
Stori ambayo inatrend kwenye mitandao ya kijamii na hii ni kutoka kwenye fan page ya Zari the boss lady inayotumia jina la Zarithe_ kupost picha ya Zari pamoja na Esma Platnumz.

Kupitia fan page ya Zarithe_ ambayo ni account ya instagram inayoendeshwa na shabiki ilipost picha ya Zari akiwa na wifi yake Esma na kuandika ” #tbt @zarithebosslady akiwa na mnafki 😂😂😂 akili zangu ndo zilivyoamka Leo”


Baada ya fan page hiyo kupost picha na kuandika caption Esma ambaye ni dada yake na Diamond Platnumz alioneshwa kukasirishwa na kujibu kwa ku-comment baada ya kupostiwa na kuitwa mnafiki.

“huwa naskia burudani sana mnaponiweka katika pages zenu tena mnafki mbwa kabisa tena mbwa koko”

Story zinazoenea chini kwa chini zinaeleza kuwa Zari na familia ya Diamond akiwemo Esma hawapo sawa toka Esma aonekane akiwa karibu na Wema Sepetu ambaye ni mpenzi wa zamani wa Diamond, hiyo pia ndio inadaiwa kuwa ni sababu ya Zari kutokumpost Esma wakati wa birthday yake na kumtakia kheri ya kumbukumbu ya kuzaliwa.

Spika Ndugai Kuamua Hatma Zitto Kabwe

$
0
0
 Spika Ndugai Kuamua Hatma Zitto Kabwe
KUADHIBIWA ama kutoadhibiwa na Bunge kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kuko chini ya Spika Job Ndugai baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kukamilisha uchunguzi wa shauri lake.


Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo anakabiliwa na tuhuma za kudharau mamlaka ya Spika kutokana na kauli yake kwamba, "Bunge limewekwa mfukoni na serikali."

Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana taarifa ya shughuli za Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kipindi cha kuanzia Januari 2017 hadi Januari 2018, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Almas Maige, alisema tayari wameshakamilisha uchunguzi wa shauri hilo.

Pia alisema kamati yake imeshamshauri Spika hatua za kuchukua kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.

Maige ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), alisema kuwa katika mkutano wa nane wa Bunge, baada ya Spika kupokea na kuikabidhi serikali taarifa za kamati mbili alizoziunda Julai tano kwa ajili ya kufanya uchunguzi katika sekta ya madini, Zitto aliandika kwenye mtandao wa Twitter maneno ya dharau dhidi ya Spika.

Spika aliunda kamati mbili za kuchunguza na kuishauri serikali kuhusu mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya madini ya Tanzanite na almasi.

"Kamati ilifanya uchunguzi wa shauri hili na kukamilisha kisha kumshauri Spika kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge," Maige alisema.

Spika Ndugai hakuongoza kikao hata kimoja katika mkutano wa wiki mbili uliomalizika jana.

John Bocco: Mimi, Okwi Mwendo Hule Hule Wapinzani Watakoma

$
0
0
John Bocco: Mimi, Okwi Mwendo Hule Hule Wapinzani Watakoma
MSHAMBULIAJI na nahodha wa Simba, John Bocco ameshindwa kuzuia hisia zake na kutamka kuwa kama akiendelea kupangwa na Mganda, Emmanuel Okwi kwenye mechi, basi wapinzani watakoma.

Hayo, aliyasema mara baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara kumalizika dhidi ya Azam FC kwa timu yao kupata ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Okwi akiunganisha krosi safi ya Mghana, Asante Kwasi.

Bao hilo liliisaidia timu hiyo kuendelea kukaa kileleni ikiongoza kwa idadi ya pointi 41 juu ya Yanga wenye pointi
34 na Azam 33.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Bocco alisema anapenda kucheza na mchezaji wa aina ya Okwi ndani ya uwanja kutokana na aina yake ya uchezaji huku akitimiza majukumu yake ya kufunga na kutengeneza mabao. Bocco alisema anajivunia kucheza na mshambuliaji wa aina hiyo huku akiwa na matarajio makubwa ya kuendelea kuifungia Simba katika mechi zijazo za ligi kuu na michuano ya kimataifa.

“Najivunia sana kucheza na mchezaji wa aina hii ya Okwi, niseme ni kati ya wachezaji wenye viwango vizuri ambao mimi ninatamani kuendelea kucheza nao pamoja.

“Uwepo wake uwanjani unanifanya nicheze kwa kujituma nikiamini nitapata
matokeo mazuri kama ilivyokuwa tulivyocheza na Azam katika mechi hii iliyopita. “Mechi ilikuwa ngumu kama mlivyoona, lakini alifunga bao kwa wakati sahihi katika mechi muhimu ambayo Simba ilizihitaji pointi hizo muhimu katika kuelekea kuuchukua ubingwa huu wa ligi,” alisema Bocco.

Aidha, mshambuliaji huyo hakuishia hapo, aliendelea kummwagia sifa mshambuliaji huyo kwa kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram kuweka picha yake na kutamka: “Huwa namuitaga Emma, respect broo, binafsi najivunia kucheza na mchezaji wa kiwango chako, asante bro kwa kutupatia pointi tatu muhimu kwenye mechi muhimu kwa wakati sahihi.

Ajibu Kuongeza Nguvu Leo Mechi Dhidi ya Shelisheli

$
0
0
Ajibu Kuongeza Nguvu Leo Mechi Dhidi ya Shelisheli
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ibrahim Ajibu na chipukizi anayekua kwa kasi, Yohana Nkomola wamerejesha matumaini kwenye timu hiyo na leo Jumamosi huenda wakawepo kwenye orodha ya kikosi kitakachoivaa St Louis ya Shelisheli. Yanga itawakaribisha wapinzani wao hao katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ajibu anarejea uwanjani akitokea kupona majeraha ya goti aliyoyapata kwenye Ligi Kuu Bara wakati timu hiyo ilipovaana na Azam FC na Nkomola yeye alipata maumivu ya misuli katika mchezo wa Ruvu Shooting.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu, alisema wachezaji hao wameanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzao juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Bavu alisema kurejea kwa wachezaji hao kumeimarisha kikosi chao kutokana na kupunguza idadi ya wachezaji majeruhi waliokuwa wanaiandama timu hiyo.

“Niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga kuwa, wachezaji wetu muhimu waliokuwa majeruhi Ajibu na Nkomola wamepona na jana (juzi Jumatano) walianza mazoezi ya pamoja na wenzao.

“Kwa maana hiyo hivi sasa wapo fiti kucheza mechi ya kimataifa kama kocha akihitaji kuwatumia, lakini mimi kama kocha niseme wapo fiti kwa ajili ya kuipambania timu yao ya Yanga. “Kipa wetu Rostand (Youthe) aliyepata majeraha ya enka kwenye mechi iliyopita na Lipuli FC naye anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti kabla ya kuanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzake,” alisema Bavu.

Makamu Rais wa Marekani Agoma Kula Chakula cha Jioni na Dada wa Rais wa Korea Kaskazini

$
0
0
Makamu Rais wa Marekani Agoma Kula Chakula cha Jioni na Dada wa Rais wa Korea Kaskazini
Makamu rais wa Marekani, Mike Pence amegoma kuwepo katika chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.

Taarifa kutoka chombo cha habari cha Yo hap kimesema kuwa Pence alionana kidogo na bwana Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso.

Wakati huo huo, rais wa Korea ya Kusini Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un katika sherehe za ufumbuzi wa mashindano ya michezo ya Olympiki ya msimu wa baridi.

Rais wa Korea ya Kusini Moon Jae-in ameshikana mikono na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini
Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Pence alimleta Fred Warmbier kama mgeni Korea Kusini, baba wa kijana mdogo wa Marekani aliyekufa baada ya kutolewa gerezani huko Korea Kaskazini.

Bwana Pence na Kim Yong-nam walikuwa wenyeji wa rais wa Korea Kusini kabla ya sherehe haijaanza huko Pyeongchang.

Lakini Makamu rais wa Marekani alikaa kwenye tafrija hiyo kwa dakika tano tu na kuondoka.

Katika shughuli hiyo, Bwana Moon alisema anatarajia mashindano hayo ya michezo ya Olimpiki msimu wa baridi yataweza kukumbukwa kama siku nzuri ya kuanza kuwa na amani.


Hata hivyo ziara yake inaonekana kuwa ishara kwamba Kim Jong un yuko tayari kuimarisha uhusiano na Korea Kusini ,nchi ambazo zilikuwa katika mvutano kwa kipindi kirefu.

Je Unasumbuliwa na Tatizo la Nguvu za Kiume?

$
0
0
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume limekuwa kwa lika zote Tiba sahihi ya matatizo haya
Chanzo chake na visababisho vyake

DALILI: mwili kuchoka maumivu ya mgongo na kiuno kutopata choo vizuli kinakuwa kigumu kama cha mbuzi
RADI: hutibu matatizo kwa mda mfupi na inakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika (30) kwa tendo(1) utaludia Mara (4) bila kuchoka pia uongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa maradufu

BOMBA; dawa ya kupunguza matiti makubwa unene na kitambi
ITUJA; dawa inatibu michilizi mwilini inaongeza makalio hips miguu saizi uipendayo

HUDUMA HIZI NA ZINGINE UTAZIPATA POPOTE TANZANIA MUONE DR LAJABU AU PIGA SIM 0711494261 au 0783823120 

Nape Nnauye Awapa Makavu Usalama wa Taifa

$
0
0
Nape Nnauye Awapa Makavu Usalama wa Taifa
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini haifanyi kazi zake ipasavyo inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania.

Nnape ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma na kuishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali, kukumbuka jukumu lao la la kuhakikisha wanalinda uchumi nchi katika kipindi hichi, ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia huko na sio pengine.

Kutoka na hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika amemjibu Nape na wabunge wengine kwamba kazi ya Idara ya Usalama wa Taifa sio kutafuta watu waliopotea au kuumizwa kama wanavyodai na laiti wangelifahamu wanachokifanya wangekaa kimya.

"Kazi ya usalama wa Taifa nchi yeyote ni kutafuta habari na kuishauri serikali. Kwa kifupi tu mimi nasema hoja mlizozitoa kuhusu idara kwamba haishauri serikali mambo ya uchumi na mambo mengine hamna ushahidi", amesema Kapteni Mkuchika.

Pamoja na hayo, Kapteni Mkuchika ameendelea kwa kusema "sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, kazi zilizopitishwa kwa mujibu wa Bunge kuna shughuli nne za idara kwamba ni kukusanya na kutafuta habari pamoja na kuzifanyia tathmini na wanapoyafanya hayo hawayafanyi katika mkutano wa hadhra, kushirikiana na vyombo vya idara nyingine vinashughulikana na usalama wa nchi, kuwashauri Mawaziri ili waishauri serikali na mambo yote ya kuujumu uchumi na vingine wanayafanya kimya kimya".

Kwa upande mwingine, shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Taifa zimehairishwa jana jioni (Ijumaa) mpaka Aprili 03 mwaka 2018.


Samatta Aumia Tena Kwenye Mchezo Dhidi ya Zulte-Waregem

$
0
0
Samatta Aumia Tena Kwenye Mchezo Dhidi ya  Zulte-Waregem
Nyota wa Tanzania Mbwana Ally Samatta anayekipiga kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ameumia tena kwenye mchezo wa jana wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Zulte-Waregem kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo.

Samatta aliumia na kutolewa dakika ya 36 huku nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji Dieumerci N'Dongala ambapo timu hizo zilikuwa sare ya 1-1, matokeo ambayo yalidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Genk ilifanya vizuri na  kupata mabao mawili yaliyofungwa na kiungo Thomas Buffel dakika ya 59 na kiungo Alejandro Pozuelo dakika ya 90, hivyo kufanya Genk iliyokuwa nyumbani kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-1.

Katika mchezo huo wa jana usiku nahodha huyo wa Taifa Stars alikuwa anacheza mechi yake ya tano tangu apone maumivu ya mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia iliyochanika Novemba, mwaka jana.



Dogo Janja Amwagia Sifa Irene Uwoya "Mke Wangu ni Mganga wa Jiko Vyakula Anavyopika Hatari Sana"

$
0
0
Dogo Janja Amwagia Sifa Irene Uwoya "Mke Wangu ni Mganga wa Jiko Vyakula Anavyopika Hatari Sana"
Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amefunguka kinachomvutia kutoka kwa mke wake Irene Uwoya msimu huu wa wapendanao (valentine).

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Ngarenaro’ ameiambia ITV kwa sasa anavutika zaidi na mapishi ya mkewe.

“Vyakula anavyonikipia mke wangu hatari sana, fundi jikoni, mganga wa jiko. Ni wanamke mwenye vision, ni mtu ambaye tunaelewana, tunasikilizana, ni marafiki,” amesema Dogo Janja.

Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa November mwaka jana, 2017 hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili ya ndoa hiyo kutokana na namna walivyoliweka suala hilo

Waziri Majaliwa: Hali ya Usalama wa Chakula Nchini Imeimarika

$
0
0
Waziri Majaliwa:  Hali ya Usalama wa Chakula Nchini Imeimarika
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hali ya usalama wa chakula nchini imeimarika kutokana na uzalishaji mzuri wa mazao ya chakula.

Waziri Majaliwa ameyasema hayo wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 10 wa Bunge la 11 mjini Dodoma Bunge na kutaja mazao hayo kuwa ni pamoja na mahindi yaliyovunwa katika mikoa ya Ruvuma, Njombe, Iringa, Katavi, Kigoma, Mbeya, Songwe na Rukwa.

"Matarajio yetu kuwa hali ya mavuno msimu huu itakuwa nzuri kwa sababu mwenendo wa unyeshaji wa mvua za vuli ulikuwa wa kuridhisha katika maeneo mengi nchini. Serikali inaendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa hali ya utengamano na usalama wa chakula unaendelea kuwa imara kwa wananchi wote na kwa wakati wote", amesema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amesema serikali inawezesha wafanyabiashara wa mazao ya chakula kuendelea kusafirisha na kuuza mazao ya chakula nje na ndani ya nchi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema upatikanaji na usambazaji wa pembejeo kwa wakulima umeimarika, ambapo takwimu zinaonesha kwamba hadi kufikia Februari Mosi, 2018 upatikanaji wa mbolea nchini kwa ajili ya mahindi na tumbaku ulifikia tani 250,376 sawa na asilimia 51.6 ya wastani wa mahitaji ya tani 485,000 kwa mwaka.

Mimba ya Gigy Money Ipo Hatarini Kuharibika Kutokana na Kipigo cha Mpenzi Wake

$
0
0
Mimba ya Gigy Mone Ipo Hatarini Kuharibika Kutokana na Kipigo cha Mpenzi Wake
BAADA ya staa wa muziki wa Bongo Fleva na muuza sura katika video mbalimbali za wasanii wa muziki ambaye kwa sasa ni mjamzito, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kukiri hivi karibuni kwamba anapigwa na mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Moj, imeelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kichanga chake kufia tumboni.

Awali, Gigy Money aliandika waraka mzito kupitia page yake ya Instagram akielezea mateso anayoyapitia kwenye mapenzi kwa sasa huku akisema anachukia mwanaume anayepiga wanawake wajawazito.

“Kiukweli leo nina stress sana na ndiyo maana nimeona bora niseme kwani ninachokiamini mimi siyo peke yangu ninayeyapitia haya kuna muda unaweza ukakufuru Mungu kwa maneno ambayo kesho na keshokutwa huwezi kuyarudisha kinywani, katika makosa ambayo najua nimeyafanya ni kupenda lakini kupenda siyo dhambi, nimepitia mengi sana kwenye mapenzi kiasi cha kufikia kupungua kimwili.

“Hakuna kitu kibaya na kigumu kama kumuaminisha mtu unampenda, unaweka nguvu na jitihada zako katika mapenzi kuna muda unawaza sijui niachie ngazi kwani unayempenda yawezekana anampenda mtu mwingine na anayekupenda humpendi hata kidogo… nimepitia vingi sana kwa watu walio karibu nami wanaweza wakawa wanajua baadhi ya mateso na utumwa wa mapenzi niliowahi kupitia na bado najiuliza kwa nini wanaume ni wagumu kuonesha hisia zao za ukweli? Inashangaza mwanaume anaweza kuishi na wewe pika pakua lakini anayempenda yuko mbali na upeo wa macho yake.

“Wanaume wa Bongo wajeuri, unabeba mimba dharau atakufanyia mwanamke wake wa nje atakuonesha, kiukweli inauma ndiyo lakini naamini ni hatua za maisha na ukuaji, naamini nimedondoka hatua moja lakini naweza kuinuka hatua 8, Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na single mother’s siyo, wote baba wa watoto wamefariki wengi wetu huwaga tunawakimbiza watoto wetu mbali na maisha na mateso tuliyowahi kuyapitia kwa baba zao, hakuna mtu anayeweza kunielewa ila mkiona mtu anaandika hivi ujue yanazidi…,” ilisomeka sehemu ya waraka huo.



Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Gigy ili kueleza zaidi kuhusu mateso aliyokiri kwamba anayapitia kwenye waraka huo lakini simu yake iliita bila kupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu chochote.

Kutokana na Gigy kueleza mateso hayo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta daktari anayejulikana kwa jina la Marise Richard wa Marise Dispensary na kueleza kuwa, kama staa huyo anapigwa na kupewa stresi nyingi, kuna hatari kubwa ya kichanga kilicho tumboni mwake kufa.

“Kumpiga mwanamke mjamzito ni hatari sana kwani mimba inaweza kuharibika na kama kiumbe kimeshakuwa cha miezi kadhaa kinaweza kufa tumboni, hivyo vipigo kwa wanawake wajawazito ni hatari,” alisema Dokta Marise.



MSIKILIZE MPENZI WAKE

Ili kuujua ukweli wa waraka huo wa Gigy, gazeti hili lilimtafuta Moj na kumuuliza kuhusiana na madai hayo ya kumpiga Gigy ambapo alisema hayana ukweli.

“Unajua mwanamke siku zote akiwa mjamzito anakuwa na hasira sana na ndiyo inayotokea kwa Gigy, wakati mwingine anakuwa na hasira kupitiliza ndiyo anaandika mambo ya ajabu kama hayo, simpigi na hakuna kitu kama hicho kabisa,” alisema Moj.
Chanzo: Global Publishers

Yanga Yajipanga Kuimaliza Shelisheli Taifa Leo

$
0
0
Yanga Yajipanga Kuimaliza Shelisheli Leo
KAZI imeanza! Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amesema hawatacheza soka la kujilinda katika mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St. Louis na badala yake watashambulia kuanzia dakika ya kwanza ili kumaliza mechi hiyo mapema.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri Matokeo ya Sportpesa, jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa raundi ya awali utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lwandamina aliiambia Nipashe jana kuwa wanataka kuutumia vyema uwanja wa nyumbani hivyo watacheza kwa tahadhari lakini ‘hawatapaki basi’ dhidi ya klabu hiyo kutoka Shelisheli.

“Tumewaona wapinzani wetu kupitia baadhi ya mikanda yao ya video, si timu mbaya, lakini lazima tuonyeshe kuwa tupo nyumbani, tutacheza soka la kushambulia lakini wakati huo  huo tutakuwa makini kwenye kujilinda,” alisema Lwandamina.

Aliongeza kuwa anafahamu wapinzani wao watacheza soka la kujilinda kwa lengo la kuwabana ili wawe katika nafasi nzuri kwenye mchezo wa marudio utakaofanyika baada ya wiki mbili huko Shelisheli.

“Tutacheza kwa kasi zaidi dakika 15 za kwanza ili tupate bao la kuongoza, hii itatusaidia kushusha presha ya mchezo,” alisema.

Ajibu, Chirwa kuongozaKuelekea kwenye huo, Lwandamina, amepanga kuwatumia kwa pamoja washambuliaji, Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa.

Ajibu ambaye amekosa baadhi ya michezo ya ligi kuu kutokana na kuwa majeruhi lakini sasa amepona na leo ataongoza safu ya ushambuliaji pamoja na Chirwa ambaye kwa sasa yupo kwenye kiwango cha juu.

Aidha, golikipa namba moja, Youthe Rostand, naye anatarajiwa kuanza katika mchezo huo baada ya kupona na kufanya mazoezi ya pamoja na nyota wenzake.

Wajanja Wamliza Mbasha Wamuibia Kila Kitu Nyumbani Kwake

$
0
0
Wajanja Wamliza Mbasha Wamuibia Kila Kitu Nyumbani Kwake
ALIYEKUWA mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiwa safarini Arusha amekombwa kila kitu na majambazi nyumbani kwake Tabata Kimanga mchana kweupe.

Mtu wa karibu na Mbasha aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, Mbasha alichanganyikiwa baada ya kurudi na kukuta amekombwa kila kitu cha ndani na majambazi.

Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la Mikito Nusunusu, lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kuibiwa kila kitu na kusema kuwa mpaka sasa amesharipoti polisi na uchunguzi bado unaendelea.

“Yaani sina la kusema walioniliza wamefanya kazi kwani wamechukua kila kitu cha ndani na kwa kweli wamenirudisha nyuma sana hata sielewi naanzia wapi,” alisema Mbasha.

Wakielezea tukio hilo majirani wa eneo hilo walisema kuwa mitaa hiyo mida ya mchana huwa ni tulivu sana kwani watu wengi huwa wanakwenda makazini ndio maana hata majambazi hao wakafanikiwa kuiba kila kitu bila kushtukiwa.

“Si unajua nyumba zetu ni za mageti makubwa mtu kujua moja kwa moja kuwa kwa f’lan kaingia mtu huwa si rahisi lakini tukio hilo limetokea kweli,” alisema jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ali

Temba Afunguka Kuhusu Kumfumania Mkewe na Mwanaume Mwingine

$
0
0
Temba Afunguka Kuhusu Kumfumania Mkewe na Mwanaume Mwingine
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka kundi la TMK Wanaume na kiongozi wa Mkubwa na Wanaye Mhe. Temba anadaiwa kumfumania mkewe akiwa na mwanaume na ndiyo chanzo cha kuachana na mkewe huyo Bibi Cheka ameweka wazi.


Akiongea kwenye kipindi cha eNewz Bibi Cheka amesema kuwa Mhe. Temba alimfumania mkewe akiwa na mwanaume mwingine ndani ya nyumba yake na kumfukuza kisha mwanamke huyo kuolewa na mwanaume mwingine, Bibi Cheka amemwaga mchele huo baada ya kusikia Temba akijitapa kuwa uongozi wao ulimmjengea nyumba kubwa na kudai kuwa bibi huyo hana shukrani.

Kwa upande wa Temba alifunguka na kusema kuwa hizo taarifa hazina ukweli wowote kwani yeye na familia yake wapo vizuri wala hakuna jambo kama hilo analodai Bibi Cheka

"Hapana mimi nipo na familia yangu watoto zangu wapo nyumbani na mama yao yupo likizo saizi hivyo nimetoka hapo ameniandali chai vizuri saizi ndiyo natoka kwenda kuonana na jamaa zangu tunakikao kidogo , sasa sijui yeye anaushahidi gani kusema nimeachana na mke wangu na hata kama kweli labda nimeachana naye haihusiani na mambo haya tuzungumze mambo ya muziki, sijawahi kumfumania mke wangu na sijui kwanini bibi amezungumza hayo huenda labda amekasirika"

Mtulia: Polisi Msiwafanye Waendesha Bodaboda Kama Gari Lenu la Mshahara

$
0
0
Mtulia: Polisi Msiwafanye Waendesha Bodaboda Kama Gari Lenu la Mshahara
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia amelitaka Jeshi la Polisi hasa wa usalama barabarani waache kuwafanya waendesha bodaboda kama gari lao la mshahara kwa kuwabambikia kesi zisizokuwa za kweli pindi wanapo wakamata.

Mgombea huyo ametoa kauli hiyo akiwa kwenye muendelezo wa kuomba ridhaa huku zikiwa zimebakia takribani siku saba ili wananchi wa Jimbo la Kinondoni pamoja na Siha kushiriki zoezi la kupiga kura katika uchaguzi huo mdogo wa marudio na waweze kupata wawakilishi wao ambao kwa mara ya kwanza wataingia bungeni mjini Dodoma Aprili 03 endapo zoezi hilo litakamilika kwa amani na usalama.

"Tuna kwenda kuhakikisha tunaleta mfumo mzuri wa kuvitambua vituo vyote vya bodaboda pamoja na kuvisajili ndani ya Jimbo la Kinondoni lakini tunawambia polisi hawa vijana wamejiajiri wasibuguziwe, sio watuhumiwa wala majambazi", amesema Mtulia.

Pamoja na hayo, Mtulia ameendelea kwa kusema "naenda kupiga marufuku bodaboda kuwa gari la mshahara kwa polisi, wakamateni wanapokuwa na makosa ya kisheria na wala msibawabikize kesi".

Kwa upande mwingine, Mtulia amedai endapo atarudishwa na wananchi hao katika Jimbo la Kinondoni basi atahakikisha matatizo yote waliyokuwa nayo yatatatuliwa bila ya wasi wasi wa aina yeyote.

Nafasi za Ajira zilizotangazwa Leo Jumamosi

Viewing all 104771 articles
Browse latest View live




Latest Images