Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

ACT-Wazalendo Wapongeza Ujumbe wa Maaskofu Katoliki

0
0
ACT-Wazalendo Wapongeza Ujumbe wa Maaskofu Katoliki
Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema ujumbe wa Kwaresma mwaka 2018 uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuhusu masuala  ya kisiasa, kichumi na kijamii unaonyesha jinsi demokrasia inavyominywa nchini.

TEC imetoa ujumbe huo Februari, 2018 ulioandikwa na maaskofu wote 35 wa baraza hilo, wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa kukumbuka siku 40 za Kristo kufunga na kwenda jangwani.

Akizungumza na wanahabari  leo Februari 12, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu amesema, “Tunawapongeza  sana viongozi wetu wa dini kwa kujitokeza waziwazi kuonyesha ugandamizaji wa haki unaoendelea nchini.”

“TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike.”

Katika ujumbe huo,  TEC wamezungumzia hali ya kisiasa na kusema uamuzi wa Serikali kuzuia, maandamano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha Katiba ya nchi.

Shaibu ameitaka Srikali kuondoa zuio batili la vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara ya kuzungumza na wananchi.

Mbali na hilo, Shaibu ameiomba Serikali itoe taarifa ya uchunguzi kupotea kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory  Gwanda aliyefikisha siku 84 tangu kupotea kwake sanjari na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Simon  Kanguye.

Simba, Yanga Acheni Kulalamika- Mwakyembe

0
0
Simba, Yanga Acheni Kulalamika- Mwakyembe
Baada ya kumalizika kwa mchezo wa kombe la shirikisho Afrika ambao Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi ya Gendarmerie Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na matokeo yaliyopatikana huku akiwataka Yanga SC kuacha kulalamika na badala yake waweke akili yao zaidi katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya St Louis.

“Ni bahatika kuiyona mechi ya leo, ilikuwa nzuri sana unaiyona Simba SC kama timu ambayo kweli ilikuwa kambini na ina mwalimu na uwelewano wa hali ya juu.”

“Mechi ulikuwa nzuri sana nimefurahia na kama kiwango cha mchezo wa mpira Tanzania kitakuwa hiki kama alivyosema mzee wetu Ali Hassan Mwinyi sisi siyo tena kichwa cha mwendawazimu ila cha muungwana ambacho kila mtu lazima akisogelee kwa uwangalifu mkubwa sana.”

Waziri Mwakyembe alipo ulizwa kuhusu malalamiko ya Yanga SC kukosa nafasi ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi yao ya kimataifa dhidi ya St Louis amesema

“Niwashauri Yanga SC kwamba akili yao yote ikazanie mechi ya marudiano inayo kuja waache mambo ya kulalamika hakuna dawa hakuna muarubaini ya kushinda ni mazoezi na timu kuweza kuelewana nimeona gonga safi za leo za Simba SC kwa kweli nimeona goli zaidi ya saba ila kwa bahati mbaya sana yamekwenda manne.”

“Kuhusu Yanga SC kulalamika sisi hatujapata malalamiko rasmi ila nimeyaskia bungeni watu wakisema lakini cha msingi ni kwamba wote mnajua uwanja wetu wa taifa umetoka kwenye ukarabati mkubwa sana tumekabidhiwa ukiwa na garantii wa kuweza kuutumia kwa zaidi ya miaka 10 bila kuweka nyasi mpya lakini una masharti yake.”

“Huwezi ukawa na mechi kubwa tatu kwa wiki katika uwanja huu ukifanya hivyo hatuwezi kuwa nao kwa zaidi ya miaka mitatu ijayo.”

“Kilichotokea wiki hii tulikuwa na mchezo wa Azam FC na Simba SC wiki hii moja, huku tukijua tuna mechi mbili za kimataifa na katika mchezo huo timu ngeni inapewa kipau mbele katika uwanja ule ule ambao niwa wenyeji kwa upande wa timu hizi Yanga SC na Simba tulichukulia wana ujua.”

Waziri Mwakyembe amezitaka klabu hizi kongwe Yanga SC na Simba SC ambazo zina umri wa zaidi ya miaka 80 kuwa na viwanja vyao.

Serikali Kuimarisha Mifumo ya Utoaji Huduma za Dawa

0
0
Serikali Kuimarisha Mifumo ya Utoaji Huduma za Dawa
SERIKALI imesisitiza kwamba itaendelea kuimarisha mifumo yake ya utoaji huduma za dawa kutokana na ukweli kwamba ya dawa zinatumika kwa wanyama na binadamu na kuleta usugu wa ugonjwa
husika kwa mgonjwa na gharama kubwa kwa taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dr Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa siku nne wa Jukwaa la kudhibiti usambazaji na uzalishaji wa bidhaa za madawa Afrika ambapo nchi 18 zipo nchini kujadili namna bora ya kudhibiti madawa yasiyo na viwango katika soko ili kuimarisha na ustawisha afya za wananchi wake.

“Tanzania ni moja ya nchini iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa dawa feki kwa Afrika nzima na mamlaka ya dawa na vipodozi nchini ina maabara za kisasa na watalaamu wa kutosha wa kuweza kufanya ukaguzi wenye ubora na viwango vya kimataifa,” amesema Ndungulile.

Ameongeza kwamba Tanzania imeweza kujitosheleza kwa dawa za kutosha na zenye viwango vya kimataifa na changamoto kubwa ilikuwa  kudhibiti dawa zinazoingia kwa njia ya panya ambapo tayari mamlaka husika wameshafungua ofisi za kanda ambazo zimefanya kazi kubwa kupunguza mianya ya dawa zinazoingia kwa njia ya panya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi Agnes Kijo amefafanua kwamba wataalamu kutoka nchi za Cameron, Ivori Coasti, Mali, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Mauritius, Senegal, Ethiopia, Sudan, Guinea, Sierra Leone, Uganda, Malawi, Zambia, Zimbabwe na Afrika kusini watakutana kwa siku nne ili kuja na mpango kabambe wa kudhibiti dawa bandia.

“katika mkutano huu jambo kuu litakuwa na kwa namna ngani tunaweza kudhibiti dawa bandia kwenye masoko na kuhakikisha kwamba wazalishaji pia wanatoa dawa zenye ubora unaokubalika katika soko,”
amesema  Kijo.

Kijo ameongeza kwamba TFDA kwa sasa ina maabara 24 nchi nzima zenye vifaa vya kisasa vya kufanya ukaguzi
nchini nzima na ofisi saba za kikanda ambazo zina wataalamu wa kutosha kuweza  kuhudumia sehemu za mikoani.

Herry Muziki Amtosa Diva "Kurudiana na Naye Siwezi"

0
0
Herry Muziki Amtosa Diva "Kurudiana na Naye Siwezi"
Msanii Heri amesema hawezi kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Diva baada ya kuzinguana hivi karibuni.

Muimbaji huyo amesema baada ya kuachana na Diva ndio itakuwa mwisho wa yeye kuingia katika mahusiano na mtu maarufu.

“Sikuwa nime-date na mtu maarufu before, wakwanza ni yeye, kwa hiyo baada yaku-date naye imekuwa ni experience kwangu, after that nisingependa ku-date na mtu maarufu.” Heri Muziki ameiambia Bongo5.

nafikiri hata yeye mwenyewe hawezi kurudiana na mimi, kwa hiyo tunaweza kumake peace hata kama hatutakuwa marafiki kila mtu anaendelea na maisha yake,” ameongeza.

Wawili hao mara baada ya kupishana na kuamua kuachana kulipelekea Diva kutoa sauti ya Heri Muziki katika wimbo ‘Waambie’ ambao Heri alifanya kwa kushirikiana na Mr. Paul pamoja na Mwana FA na Diva kuweka sauti pale alipoondoa sauti ya Heri Muziki ingawa wimbo huo ulishatoka awali.

Msukuma: Lema, Mbowe na Msigwa Wamekuwa Watetezi wa Wezi wa Madini

0
0
Msukuma: Lema, Mbowe na Msigwa Wamekuwa Watetezi wa Wezi wa Madini
Mbunge wa Geita Vijijini kwa tiketi ya (CCM) Joseph Kasheku aka Musukuma amefunguka na kusema kuwa yeye licha ya kuishia darasa la saba lakini uwezo wake wa akili ni mkubwa kuliko Mhe. Freeman Mbowe.


Musukuma amesema hayo Februari 11, 2018 aliposhiriki katika kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Kinondoni ambapo alitumia jukwaa hilo kujibu kauli za watu kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka asijifananishe na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe ndipo hapo aliposema kuwa akili zake ni zaidi ya kiongozi huyo wa CHADEMA.

"Huko kwenye mitandao wanasema mimi siwezi kujilinganisha na Mbowe nataka niwaambie na mnisikilize mimi nina akili kuliko huyo Mbowe, kwanza mimi ni darasa la saba kama niliweza kuwazungusha wao wenyewe wakakologa nikachomoka bado mimi nitakuwa mjinga" Alihoji

Msukuma aliendelea kusema kuwa wabunge wa upinzania akiwepo Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Peter Msigwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wamekuwa watetezi wa wezi wa madini bungeni. 

"Tukikamata mwizi au tukitumbua jipu linatetewa bungeni na upinzani wale wale waliowaaminisha Watanzania kwamba nchi hii imeibiwa kwa muda mrefu, Msigwa na Lema wamepiga kelele miaka yote toka mimi nikiliangalia bunge wakisema tunaibiwa madini lakini Rais wetu aliposhika madini wakakaa kikao na kuanza kuwatetea bungeni" alisema Msigwa

Mahakamani: Ofisa wa TRA Amekana Kumiliki Magari 19

0
0
Mahakamani: Ofisa wa TRA Amekana Kumiliki Magari 19
Ofisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amekana kumiliki magari 19 yenye thamani ya Shilingi Milioni 197,601,207 yasiyolingana na kipato chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mushi amekana umiliki huo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati akisomewa maelezo ya awali (Ph) na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter.

Katika usomewaji wa maelezo hayo, Mushi alikubali majukumu yake ambayo ni kufanya upembuzi na uhakiki wa makadirio ya kodi na bidhaa zinazoingia nchini na kusafirishwa nje ya nchi ambapo alipoajiriwa mwaka 2011 mshahara wake ulikuwa Shilingi Laki nane na mwaka 2016 ulifikia shilingi Milioni 1,190,700.

Wakili Vitalis amedai kwa kipindi chote July 2011 hadi March 2016 mshtakiwa alijipatia kipato cha jumla ya shilingi Milioni 56.7 kama mshahara na marupurupu, ambapo Mushi alikataa.

Mushi alikataa kumiliki magari 19 ambayo anadaiwa aliyaingiza nchini kutokea Japan yakiwa na thamani ya shilingi  Milioni 197,601, 207.

Magari hayo ni, Toyota Ra4, Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki Carry, Toyota ipsum, toyota wish, Toyota mark ll, Toyota regiusage, Toyota estima, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota crown, Toyota hiace, Toyota estima, Toyota passo, Suzuki carry, yote yakiwa na thamani ya Shilingi Milioni 197,601,207

Wakili Vitalis amedai kuwa mshtakiwa anamiliki ardhi au viwanja alivyovinunua kwa nyakati tofauti akiwa mtumishi wa TRA plot namba 2263 block b kimbiji kigamboni chenye thamani ya Milioni 8,400,000 huku shamba la Mabwepande heka moja lenye thamani ya Shilingi Milioni 7.

Pia mshtakiwa huyo alikataa kuwa July 2011 na March 2016 alifanya miamala ya jumla ya shilingi Milioni  310,993,647.33. Pia alikataa kati ya March 2, 2012 na Match 30, 2016 kwenye namba ya simu alifanya miamala wa shilingi 1,632,915, 485.

Katika maelezo hayo, mshtakiwa alikubali kwamba anamiliki shule mbili za awali ambazo ni active tot’s zone maeneo ya Kinyerezi na Mikocheni Dar es Salaam zilizosajiliwa mwaka 2014 na 2016 lakini amekataa kuwa shule hizo zina thamani Milioni 65,063,751.11

Wakili Peter amedai kuwa fedha hizo na mali anazomiliki mshtakiwa hazilingani na kipato chake halali na hivyo hawezi kuelezea utajiri aliokuwa nao.

Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi March 12,2018 kwaajili ya kusikilizwa.

Serikali ya China Yaridhia Kutoa Bilioni 138 Kwaajili ya Ujenzi wa Chuo Kikuu

0
0
Serikali ya China Yaridhia Kutoa Bilioni 138 Kwaajili ya Ujenzi wa Chuo Kikuu
February 12, 2018 Good News niliyoipokea toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ni kuhusu serikali ya China imeridhia kutoa msaada wa Dola za Marekani Milioni 62 sawa na Shilingi Bilioni 138.3 za Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Usafirishaji hapa nchini.

Balozi wa China hapa nchini Wang Ke amesema hayo leo February 12, 2018 muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kumkabidhi barua yenye ujumbe wa Rais wa China Xi Jinping, Ikulu Dar es Salaam.

Wang Ke ameeleza kuwa msaada huo ni sehemu ya misaada na miradi mbalimbali ambayo China inaitekeleza hapa nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na Tanzania.

President Magufuli amemuomba Wang Ke kumfikishia shukrani zake kwa Rais wa China kwa ujumbe na msaada huo ambao amesema utasaidia kuimarisha huduma za usafirishaji hapa nchini.

Kutokujiamini ni Janga Kubwa la Wanaume wa Kibongo Mbele ya Wanawake

0
0
Bila hata kwenda mbali angalia Hizi Statement kadhaa za Wanaume Wasiojiamini:

1. Usimtambulishe Mkeo Utagongewa

2. Usioe mwanamke mzuri

3. Mwanamke mzuri hatulii kwenye ndoa

4. Usioe mwanamke aliekuzidi kipato

5. Usioe mchaga/muhaya

6. Usioe mwanamke aliekuzidi elimu

7. Kama wewe mfupi usitafute mwanamke mrefu

HIVI KWA NINI HAMJIAMINI?

Ukiangalia kwa wenzetu hii kitu ni tofauti sana ila hapa yaani ukidate mtu ambae hajiamini ni janga statement kama hizi hazimkauki mdomoni:

1. Sikuamini kabisa
2. I cant handle this relationship(Dude you cant handle her personality she is too smart)
3. You gat attitude(Noop ana vision ya hali ya juu wewe sio saizi yake.

NA WANAKAGUA SIMU HAO KAMA WAPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI

Kujiamini ni credit kubwa sana kwa mwanaume wa kisasa
Hata ukiwa na ela kama hujiamini utaumwa ulcers.

~By  Masai dada

Zitto Kabwe Amtembelea Samatta Nyumbani Kwake Ubelgiji

0
0
Zitto Kabwe Amtembelea Samatta Nyumbani Kwake Ubelgiji
Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa jana jioni alikwenda Genk nchini Ubelgiji nyumbani kwa nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta.

Zitto amesema kuwa amefurahi kumsalimia na kumjulia hali Samatta huku akieleza kuwa amefurahi kumkuta akiwa mzima wa afya.

Nimepita Kumsabahi Nahodha Samatta – Zitto

Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji.

Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi.

Namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Genk
Ubelgiji
Februari 13, 2018

Rais Magufuli Amteua Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL

0
0
Rais Magufuli Amteua Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) na Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Uteuzi wa Dkt. Omari Rashid Nundu na Bw. Waziri Waziri Kindamba umeanza tarehe 01 Februari, 2018.

Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Omari Rashid Nundu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania (Tanzania Telecommunication Company Limited – TTCL) na Bw. Waziri Waziri Kindamba alikuwa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.

Pamoja na kufanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwahamisha wafanyakazi wote na maafisa wa umma (Employees and Public Officers) wa iliyokuwa TTCL kwenda TTCL Corporation.

Pia Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa kutoivunja bodi ya iliyokuwa TTCL, wajumbe wake wote kuendelea na nafasi zao na kujaza nafasi za wajumbe zilizobaki ikiwa ni pamoja na nafasi moja ya mjumbe kutoka Zanzibar.

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ilibadilishwa rasmi tarehe 28 Novemba, 2017 na kuwa Shirika la Simu Tanzania (TTCL Corporation) baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutia saini sheria namba 12 ya mwaka 2017 ya Shirika la Simu Tanzania (TTCL Corporation) na tarehe 01 Februari, 2018 TTCL Corporation ilianza kufanya kazi rasmi.

Karani Adai Nyoka Alikula Mamilioni ya Pesa

0
0
Karani Adai Nyoka Alikula Mamilioni ya Pesa
Karani mmoja nchini Nigeria amefukuzwa kazi baada ya kuwaambia wakaguzi wa hesabu kuwa nyoka alikula naira milioni 36.

Pesa hizo ni sawa na dola 100,000 za kimarekani.

Karani Philomena Chieshe alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya bodi ya mtihani ya Nigeria inayokusanya pesa za mtihani.

Bodi hiyo ya mtihania iliiambia BBC kuwa ilitupilia mbali madai yake na imeanisha kumchukulia hatua za kinidhamu.,

Kisa hicho kimezua shutuma na dhihaka kwenye mitandao ya kijamio nchini Nigeria.

Nayo tume ya kupambana na rushwa nchini Nigeria iliandika ujumbe huu katika Twitter ambayo nembo yake ni mwewe.


Ngoma, Yanga Mambo Safi Wamalizana

0
0
SIKU chache baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kutamka hatua yao ya kufikiria kuvunja mkataba na mshambuliaji wake, Donald Ngoma, kufuatia majeraha sugu, suala hilo sasa halipo, imeelezwa.

Ngoma, ambaye anaendelea kuuguza majeraha yake ya goti, anategemewa kuanza mazoezi wiki hii baada ya kudaiwa kupona.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, kwa sasa inaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini ikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mmoja wa viongozi wa timu hiyo aliliambia Nipashe jana kuwa, Ngoma anajiandaa kurejea uwanjani hivi karibuni, hivyo suala la kukatishwa mkataba wake limesitishwa.

"Hayo yalikuwa mapendekezo, kwamba kama hatorejea uwanjani kwa muda mrefu ni vyema mkataba wake ukakatishwa, lakini Ngoma ameanza kupona na hivi karibuni ataanza mazoezi mepesi kabla ya kuungana na wenzake," alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Kwa upande wake, Meneja wa klabu hiyo, Hafidh Saleh, alimwambia mwandishi wetu kuwa taarifa alizonazo juu ya mshambuliaji huyo ni kuwa anaendelea kupona na hivi karibuni atarejea uwanjani.

"Hayo masuala ya mkataba ni ya uongozi zaidi, mimi binafsi sifahamu, ninachojua Ngoma anaendelea kupona na mwenyewe amesema anakaribia kurejea uwanjani," alisema Saleh.

Alisema amewasiliana na mchezaji huyo na kumhakikishia kuwa taratibu ameanza kupona na anatarajia kuanza mazoezi hivi karibuni.

Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alikaririwa akisema kuwa wanafikiria kuuvunja mkataba na nyota huyo kwa kuwa amekuwa na majeraha ya muda mrefu.

Katika hatua nyingine, Yanga imepanga kuelekea Shelisheli mapema zaidi kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya St Louis ya nchini humo.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumamosi iliyopita, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0.

Ili kusonga mbele, wawakilishi hao wa Tanzania Bara wanahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote katika mechi hiyo ya marudiano.

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

0
0

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba, Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

0
0

Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?


Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521 

Daimond, Hamisa Mobetto Warudi Tena Mahakamani Kuweka Kumbukumbu za Kumtunza Mtoto Wao

0
0
Daimond, Hamisa Mobetto Warudi Tena Mahakamani
February 13, 2018 stori inayoshika headlines ni ya Kimahakama ambapo Nyota wa muziki wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao.

Diamond na Mobetto wamefika Mahakamani hapo, ikiwa ni wiki moja baada ya kufika na kusuluhishwa.

Namnukuu Hamisa akizungumza nje ya Mahakama Mobetto “Maamuzi nimeridhika nayo na tumekubaliana kuhusu matunzo ya mtoto, Pande zote mbili tulikaa na kukubaliana, nashukuru kila mtu tumekubaliana na tumeridhika, hivyo yamekwisha.”

Naye Diamond Platnumza amesema mara ya mwisho ilikuwa ni usuluhishi haikuwa Kesi na Leo tumeweka rekodi sawa ili kutunza kumbukumbu na kuweka vitu sawa ili yasije kuzushwa mengine ya uongo na kweli.

“Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani. Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.” Diamond Platnumz

Simba, Yanga Kumaliza Vipolo Vyao Kabla ya Kusafiri kwa Mechi za Kimataifa

0
0
Simba, Yanga Kumaliza Vipolo Vyao Kabla ya Kusafiri kwa Mechi za Kimataifa
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC iliyopo kileleni mwa msimamo na mabingwa watetezi Yanga SC iliyopo nafasi ya pili zinatarajiwa kucheza mechi zao za viporo za VPL kabla ya kusafiri kwa mechi za kimataifa.


Yanga ambayo haikucheza mchezo wake wa raundi ya 18 kutokana na wikiendi ililiyopita kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St. Lousi ya Shelisheli, itaikaribisha Majimaji FC kwenye uwanja wa Uhuru.

Simba wao hawakucheza mchezo wao wa raundi ya 18 kutokana na kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo walicheza na Gendarmerie ya Djibouti. Alhamisi watakuwa mjini Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

Tayari Yanga wameshaweka wazi kuwa watasafiri siku ya Jumapili Februari 18 kuelekea Shelisheli kwaajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Februari 21. Simba bado hawajatangaza lini wataondoka nchini.

Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 41 huku wapinzani wao wa Alhamisi Mwadui wakiwa katika nafasi ya 12 na alama 18. Yanga ina alama 34 katika nafasi ya tatu huku Majimaji wakiwa nafasi ya 14 na alama 14.

Waziri Aagiza Kuwafuta Kazi Watumshi 65

0
0
Waziri Aagiza Kuwafuta Kazi Watumshi 65
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemwagiza katibu Mkuu Wizara ya uvuvi Dk. Yohana Budeba pamoja na wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya katika mikoa ya kanda ya ziwa,Kuwafuta kazi mara moja watumishi 65 na viongozi wa kamati za usimamizi wa raslimali za uvuvi (BMU) 26 baada ya kubainika wanashiriki kufadhili uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria.


Akihitimisha operesheni maalum ya kitaifa ya kupambana na kudhibiti uvuvi na biasahara haramu ya mazao ya uvuvi katika ukanda wa Ziwa Victoria iliyodumu kwa siku 40, katika ukumbi wa chuo Kikuu cha benki jijini Mwanza, Mpina amesema operesheni hiyo itaendelea hadi disemba mwaka huu ili kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa huku akidai hatasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kukwamisha juhudi za serikali.

Waziri Mpina pia ameonesha kuchukizwa na kitendo cha askari wa wanyamapori wa hifadhi ya kisiwa cha Lubodo mkoani geita kuwazuia watendaji wa kikosi cha operesheni hiyo wakati wa msako dhidi ya uvuvi haramu.

Operesheni hiyo ilianza Januari mosi mwaka huu, ambapo jumla ya wadau 1,200 waliopo kwenye sekta ya uvuvi nchini walikutwa na makosa mbalimbali na kutozwa faini ya shilingi Bilioni 4.7, huku tani 73 za samaki wasiokidhi kiwango wakigawiwa kwa wananchi,na tani 173 za mazao ya uvuvi zilitaifishwa,huku mali na zana mbalimbali za uvuvi zenye thamani kubwa ya fedha zikiteketezwa kwa moto.

Halima Mdee: Tunataka Haki Itendeke Kwenye Ujaguzi wa Jumamosi

0
0
Halima Mdee: Tunataka Haki Itendeke Kwenye Ujaguzi wa Jumamosi
Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee amefunguka na kudai katika uchaguzi huu wa marudio unaotarajiwa kufanyika Jumamosi (Februari 17) anataka haki itendeke kwa wagombea ili amani na utulivu wa nchi uendelee kuwepo.

Mdee ametoa kauli hiyo akiwa anamuombea ridhaa mgombea wao wa jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu ili aweze kuwa muwakilishi wa wananchi hao na kusema safarii hawatakubali kuona dhuluma ikiendelea kutendeka za kuiba kura za mgombea fulani na kwenda kwengine kama walivyozoelea kuwafanyia.

"Huu uchaguzi tunataka watawala wajue kwamba kila mbinu wanayoifanya tunaijua lakini hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Tunataka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Taifa (NEC), Polisi pamoja na wasimamizi wa uchaguzi ambao watakaotumwa na CCM wajue iwe jua, mvua, matope au mchanga, tunahitaji mwenye haki yake apewe", amesema Mdee.

Pamoja na hayo, Mdee ameendelea kwa kusema "Maulid Mtulia akishinda apewe Mtulia, Salum Mwalimu akishinda apewe Salum Mwalimu. Wananchi tumechoka kufikilia kuja hapa, wananchi tumechoka kufanywa mazuzu wakati tunajielewa.Tunataka mfumo wa demokrasia uwaachiliwe ili amani na utulivu wa nchi yetu ipate kubaki kwa sababu ikivunjwa haitabaki na hakuna mtu atakayepona".

Kwa upande mwingine, Halima Mdee amesema katika nchi zilizoendelea kidemokrasia huwa hakuna vyama vinavyotawala milele wala kuwadanganya wananchi.

Jacob Zuma Agoma Kujiuzulu Urais

0
0
Jacob Zuma Agoma Kujiuzulu Urais
Rais Jacob Zuma amekataa kujiuzulu mara moja kama mkuu wa nchi, wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha African National Congress (ANC) iliyoamua kumuita.

Uamuzi wa chombo hicho cha juu cha uamuzi cha chama kiliamua kumuita kikitumia kifungu kilichomo katika Katiba ya ANC kinachoipa halmashauri hiyo mamlaka ya kumuita mtumishi wa Serikali.

Chama kilikuwa kinatarajiwa kumuandikia Zuma barua Jumanne asubuhi kumfahamisha kuhusu uamuzi huo.

Halmashauri Kuu ilifanyika mkutano wa saa 13 mfululizo huko Irene nje kidogo ya Pretoria. Kikao hicho kilichoitishwa kwa haraka kilianza saa 8:00 Jumatatu mchana na kumalizika saa 9:00 usiku kuamkia Jumanne.

Saa 5:00 usiku NEC iliamuru kumuelekeza Rais wa ANC, Cyril Ramaphosa na Katibu mkuu, Ace Magashule kwenda nyumbani kwa Zuma kwenye makazi yake Mahlamba Ndlofu mjini Pretoria kumpa hati ya kujiuzulu au kukubali kufukuzwa na chama.

Kikao kati ya wajumbe wawili hao na Zuma kilidumu chini ya saa moja ambapo mkuu huyo wa nchi alikataa kutii.

Ramaphosa na Magashule walirudi kwenye kikao cha NEC na kutoa mrejesho saa 6:00 usiku. Ukumbi ulikuwa umefungwa wakati ambapo wale wawili waliondoka kwenda kukutana na Zuma.

Vyanzo kutoka ndani ya NEC vililiambia shirika la News24 kwamba wakati wa kikao cha watatu hao Zuma aliwauliza wajumbe waliotumwa: "Kitu gani kibaya nimefanya".

"Zuma aliwajibu Ramaphosa na Magashule kuwa atawajibu hadharani chama kitakapokuwa kimeamua kumwita," kilisema chanzo.

ANC inatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari juu ya matokeo ya mkutano wa NEC saa 6:00 Jumanne mchana. Zuma inasemekana anataka kuendelea kubaki kwenye majengo ya Serikali yaitwayo Umoja kwa miezi mitatu ili aweze kushiriki matukio mawili. Hata hivyo, NEC ilikataa masharti yake.

Vyanzo vilisisitiza kuwa Zuma alitaka kubaki kama mkuu wa Serikali hadi wakati wa mkutano wa kilele wa nchi nne za Brics utakapofanyika na alitaka kuhudhuria mkutano mwingine wa Umoja wa Afrika.

Mkutano wa Brics umepangwa kufanyika Julai mjini Sandton ikiwa na maana Zuma atakuwa madarakani kwa miezi mitano zaidi. Zuma aliiongoza Afrika Kusini kuingia kwenye umoja wa kiuchumi wa Brazil, Russia, India na China maarufu kama Brics.

Tamisemi Yatolea Ufafanuzi Tamko la RC Makonda

0
0
Tamisemi Yatolea Ufafanuzi Tamko la RC Makonda
Tamko la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusimamisha shughuli za mabaraza ya ardhi ya kata limetolewa ufafanuzi, Tamisemi imesema.

Jumamosi iliyopita Makonda akipokea ripoti kutoka kwa wanasheria waliosikiliza kero za wananchi kwa uratibu wa ofisi yake, alitamka kusitisha shughuli za mabaraza hayo.

Hata hivyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mussa Iyombe alizungumza na Mwananchi jana kuhusu tamko la Makonda alisema mkuu huyo wa mkoa ameshatoa ufafanuzi kwa maandishi.

Alisema Makonda alikana kuwa hajasimamisha mabaraza hayo kufanya kazi.

“Tulimtaka atuandikie barua ya kutueleza na tayari ameshafanya hivyo, tumemalizana naye kwa maandishi, hakusimamisha mabaraza hayo kufanya kazi,” alisema Iyombe.

Alisema, “Mtapata taarifa mkimuuliza mwenyewe, kwa upande wetu tumemalizana naye.”

Alipotakiwa kusema kama mkuu huyo wa mkoa alitakiwa kuandika barua baada ya kuvunja kipengele kipi cha sheria kutokana na tamko lake Iyombe alisema:

“Sitaki kusema alivunja kipengele ni wewe wasema, ninachosema kama kiongozi lazima unachokisema wananchi wakielewe, kulikuwa na maswali watu wanahoji kuhusu suala hilo ndiyo maana tukamtaka atufafanulie na amefanya hivyo kwa maandishi. ”

Makonda alipotafutwa kuzungumzia suala hilo jana, simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokewa.

Wakati Iyombe akisema hayo, Ofisa Mtendaji Kata ya Kigogo, Ole Rosai akizungumzia tamko la Makonda jana alisema, “Mimi nilisikia tu katika vyombo vya habari kwa hiyo nasubiri mwongozo kutoka kwa mkurugenzi kujua utekelezaji wake.”

Kauli ya Rosai iliungwa mkono na Ofisa Mtendaji Kata ya Ubungo, Isack Waziri aliyesema bado hawaelewi utekelezaji wake.

“Ni kweli lazima tupate maelekezo rasmi ya kimaandishi lakini kama bosi wako amesema unafanyaje? Tumewasiliana na mwanasheria wa manispaa (ya Ubungo) katueleza analifuatilia,” alisema Waziri.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Nassib Mmbaga alisema, “Hili jambo si limetokea juzi, ili litekelezwe linahitaji kuandikiwa barua lakini kwa sasa na sisi tunasubiri maelekezo kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa kuwa linatekelezwa hivi na hivi. Kwa hiyo tunasubiri.”

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando hakupatikana kuzungumzia tamko hilo.

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alisema, “Serikali haifanyi kazi kwa kauli za WhatsApp au redio. Maelekezo tunapata kutoka kwa katibu mkuu Tamisemi.”

Jacob ambaye pia ni Diwani wa Ubungo alisema, “Hata Rais anapotoa maelekezo huwa baadaye yanaambatana na barua.”

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula alipoulizwa na Mwananchi kuhusu kusimamishwa kwa mabaraza hayo alisema, “Hayo wasiliana na Waziri wa Tamisemi, hayako katika wizara yangu. Tamisemi ndiyo yanawahusu.”

Rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Felix Kibodya akizungumza na Mwananchi juzi alisema mabaraza hayo yalianzishwa mwaka 1985 ili kushughulikia migogoro ya ardhi na halmashauri zilipewa jukumu la kuyasimamia.

Alisema mabaraza hayo yaliongezewa nguvu zaidi kwenye Sheria ya ardhi ya Kijiji ya mwaka 1999 na Sheria ya Utatuzi wa Migogoro ya mwaka 2002.

Kibodya alisema haiwezekani mabaraza hayo kusimamishwa kufanya shughuli zake kwa kuwa mambo ya kisheria hayawezi kuondolewa kwa matamko ya jukwaani.
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images