Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Kiongozi wa Chadema Auawa Kikatili Mbowe Asimulia Alivyotekwa

$
0
0
Kiongozi wa Chadema Auawa Kikatili Mbowe Asimulia Alivyotekwa
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kiongozi wa chama hicho katika Kata ya Hananasif, Daniel John amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 13, 2018, Mbowe alisema John alitoweka siku moja iliyopita. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hana taarifa hizo lakini anawasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.

Amesema baada ya mawasiliano atatoa ufafanuzi leo  Februari 14,2018. Mbowe alisema John ambaye ni katibu kata alitoweka akiwa na Reginald Mallya ambaye alijikuta yupo ufukweni mwa bahari.
Mbowe alisema walitoa taarifa polisi kuhusu kutoweka kwa John na kwamba, walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walielezwa kuna mwili ulipelekwa na polisi. Alisema mwili huo ulitambuliwa na mkewe John na una michubuko inayoashiria alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa umebonyea kuashiria alipigwa na kitu kizito.
Kuhusu Mallya alisema alipigwa panga kichwani na alivunjwa mkono. Mbowe ametaka polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo. Mallya aliyekuwapo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari alisema walikuwa wakitembea na John ndipo waliposimamishwa na kuingizwa ndani ya gari.
Alisema alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipozinduka alijikuta ufukweni alikojikokota hadi barabarani ambako alipata msaada wa bajaji na alikwenda Hospitali ya Mwananyamala alikotakiwa kuwa na taarifa ya polisi ambayo aliipata Kituo cha Polisi Oysterbay.

Faiza Afunguka Siri ya Wanaume Aliozaa Nao

$
0
0
 Faiza Afunguka Siri ya Wanaume Aliozaa Nao
MWIGIZAJI wa Bongo Movies ambaye ni miongoni mwa mastaa wenye wafuasi wengi kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Faiza Ally ameanika siri za wanaume aliozaa nao kwamba, wakati wa ujauzito wa watoto wao walikuwa wakimlea kama malaika kwa sababu walihitaji watoto na walikuwa tayari kuwa na familia.

Faiza aliiambia Risasi Vibes kuwa, akianza na ujauzito wake wa kwanza wa mwanaye Sasha aliyezaa na mwanamuziki ambaye pia ni mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, alikuwa akimlea vizuri kuliko kawaida na hata aliyezaa naye mtoto wa pili anayejulikana kwa jina la Peter, raia wa Marekani naye alikuwa akimpa malezi bora ndiyo maana alifanikiwa kuzaa watoto wazuri.

“Kutokana na malezi mazuri ambayo nimekuwa nikiyapata wakati wa ujauzito, kiukweli ninahamasika kuendelea kuzaa kwa sababu huwa ninalelewa kama malkia, jambo ambalo linanishangaza kusikia wanaume wengine wanawapiga wanawake wao wawapo wajawazito,” alisema Faiza.

Serikali Yataja Maeneo Yanayotumika Kupitisha Dawa za Kulevya

$
0
0
Serikali Yataja Maeneo Yanayotumika Kupitisha Dawa za Kulevya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imebaini maeneo ya bahari kuu, bandari, vituo vya mabasi na viwanja vya ndege ndio yanatumika zaidi kupitisha dawa za kulevya.

Amesema wafanyabiashara, wasambazaji na watumiaji wa dawa hizo wameendelea kukamatwa lengo likiwa ni kuhakikisha biashara hiyo inamalizika nchini.

Taarifa iliyotolewa leo Februari 13, 2018 na ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa kiongozi huyo ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi gari kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Amesema mbali na kukamata meli, pia Serikali imewakamata wasambazaji pamoja na kundi kubwa la wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara hiyo sambamba na watumiaji.

Waziri Mkuu amesema lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na kizazi chenye uwezo wa kuzalisha mali.

Amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya, ambapo hivi karibuni imekamata meli nyingi, moja ikiwa inatokea pwani ya Msumbiji na ilikamatiwa maeneo ya Mtwara ikiwa na dawa nyingi za kulevya.

“Ni wakati wa Serikali kuendelea kuiwezesha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na leo hii tunawakabidhi gari hili jipya kabisa ili iweze kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo,” amesema

Pia, amewataka Watanzania waachane na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kazi ya kusambaza, kuzalisha na kutumia na watakaokamatwa wakijihusisha nazo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa sasa Serikali inajenga maabara ambayo itatumiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa wanazozikamata.

Ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa mara wanapowabaini wafanyabiashara, watumiaji na wasambazaji wa dawa hizo.

Pia wahakikishe wanawalinda vijana ili wasijihusishe na dawa za kulevya.

Kwa upande wake, Sianga ameishukuru Serikali kwa kuipatia mamlaka hiyo gari ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waachane na biashara hiyo huku akiwasihi kupambana kuhakikisha dawa za kulevya haziingii nchini.

Amesema mbali na kudhibiti biashara hiyo, pia wanatoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya vikiwemo vitendo viovu vinavyofanywa na watumiaji ili wachukie na waache kutumia dawa hizo.

Kikwete: Busara Itumike Kupunguza Changamoto za Wakimbizi

$
0
0
Kikwete: Busara Itumike Kupunguza Changamoto za Wakimbizi
Rais Mstaafu Kikwete amesema umefika wakati busara kutumika kupunguza changamoto za wakimbizi miongoni mwa nchi za Afrika ikiwa siku chache zimepita tangu Tanzania itangaze msimamo wa kutoendelea kuwapa nafasi ya ajira, ukazi wa kudumu, umiliki ardhi


Akizungumza kwenye mkutano wa jopo la viongozi mbalimbali duniani lililoundwa kuangalia mfumo wa kuhudumia wakimbizi na jinsi ya kumaliza migogoro iliyopo katika nchi mbalimbali, jijini Dare s Salaam, Dk. Kikwete amesema, jopo hilo pamoja na mambo mengine limekutana kupokea taarifa ya changamoto na kujua jinsi gani nchi zenye uwezo mdogo zinaweza kusaidiwa na Jumuiya ya Kimataifa.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dk. Augustine Mahiga, amesisitiza msimamo wa Tanzania wa kutoendelea  kuwapa nafasi ya ajira, umiliki wa ardhi na ukazi wa kudumu wakimbizi kwa kutumia mkopo wa Benki ya Duniani bila kuzingatia mikataba ya Kimataifa iliyopo na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa ingilie kati suala hilo.

Aidha amesema, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kujiridhisha na kuona ukiukwaji wa mikataba ya kimataifa ya kusaidia wakimbizi inakiukwa pamoja na msaada wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi, UNHCR bado halikidhi mahitaji yaliyopo na kukanusha si kweli kwamba Tanzania haitaki kusaidia wakimbizi.

Polisi Wataka Benjamin Netanyahu Ashtakiwe

$
0
0
Polisi Wataka Benjamin Netanyahu Ashtakiwe
Polisi nchini Israel imesema Waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu anapaswa kushtakiwa na mashtaka ya rushwa yanayomkabili.

Taarifa iliyotolewa na polisi imesema, wana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani Bwana Netanyahu kwa rushwa, ufisadi na kuvunjwa uaminifu katika kesi mbili tofauti.

Waziri mkuu wa Israel anatuhumiwa kwa kutaka gazeti la nchi hiyo la Yediot Aharonot kuchapisha taarifa yake kwa upendeleo, ikiwa kama takrima kulisaidia kuweza kudhibiti magazeti yanayoshindana nayo.

Polisi wanasema mhariri wa gazeti hilo Arnon Mozes naye pia anapaswa kushtakiwa.

Madai mengine ni kwamba Waziri huyo mkuu aliyeongoza nchi hiyon toka mwaka 2009 alipokea zawadi ya kiasi cha dola 283,000 kutoka kwa msanii wa Hollwood Mogul Arnon Milchan na washabiki wengine, ili kuweza kumsaidia kupata Visa ya marekani.

Polisi wanasema Milchan ambaye ni Mtayarishaji wa Filamu naye pia atashtakiwa kwa tuhuza za rushwa.

Akizungumza kupitia Televisheni ya Israel, Benjamin Netanyahu amesema madau hayo hayana msingi wowote na ataendelea kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo.

Hata hivyo upinzani nchini Israel, wamemtaka Netanyahu ajiuzulu kutokana na tuhuma hizo dhidi yake.

Vyombo vya habari nchini Israel vimesema tayari Bweana Netanyahu amehojiwa mara saba.

Uamuzi wa Mwanasheria mkuuu wa serrikali wa juu ya kumshtaki inaweza kuchukua miezi kadhaa.

Uchaguzi wa bunge nchini humo umepangwa kufanyika November mwakani.

Diva Kubeba Mimba Mwaka Huu Baba Kijacho ni Heri Musiki?

$
0
0
Diva Kubeba Mimba Mwaka Huu  Baba Kijacho ni Heri Musiki?
Baada ya headlines za mtangazaji wa Clouds FM Diva The Bawse kudaiwa kuachana na mpenzi wake Heri Muziki kufuatia tofauti zao zilizotokea wakiwa kwenye interview Leo Tena, leo  kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika ujumbe uliowashitua wengi na kuzua maswali.

Kupitia katika twitter account yake Diva ameandika “Tangaza mwaka huu lazima niwe na ujauzito By ANY MEANS… Anzeni countdown” Kauli hiyo ya Diva imezidi kuleta maswali kwani yeye ni mjamzito? Kama sio atazaaa na nani?
Tunasikia Diva na Heri Muziki wameachana ? Lakini wajuzi wa mambo wanadai kuwa kwa kauli hiyo basi Diva atakuwa mjamzito tayari maana kama anatamani kupata mtoto ndani ya mwaka huu, kwa sasa imebakia miezi 9 mwaka uishe so kama sio mjamzito  ni wazi hawezi kupata mtoto ndani ya mwaka huu hapo itakuwa mwakani.

Ukraine Yawaokoa Wanandoa Wanaotafuta Vizazi vya kukopesha

$
0
0
Ukraine Yawaokoa Wanandoa Wanaotafuta Vizazi vya kukopesha
Ukraine, ni miongoni mwa mataifa masikini barani Ulaya , na limeanza kuwa kivutio kikubwa kwa wanandoa wanaotaka kubebewa mimba .Fedha zinazopewa wanawake wanaoshiriki katika mpango huo zinawavutia wanawake wengi , lakini pia kuna changamoto zake.

Ana* alikuwa na miaka 18 wakati alipogundua kuhusu biashara ya kubeba mimba kupitia kwa runinga.

Alikuwa amemaliza shule ya upili na alikuwa na mpango wa kufanya kazi katika hoteli katika mji wa magharibi wa Ukrain ambapo watalii huzuru. Kazi hiyo hulipa $200 kwa mwezi , lakini kwa kumbebea mtu mwengine mimba aligundua anaweza kujipatia $20,000 (£14,000).

Familia ya Ana sio masikini kwa viwango vya kawaida. Mamake ni mhasibu na amekuwa akimsaidia kila mara.

Lakini anasema alivutiwa na biashara ya kubeba mimba , kwa kuwa alitaka kupata fedha ili kuweza kununua vitu vya ghali ,kurekebisha nyumba , gari na mambo mengine.

Ijapokuwa mamia ya wanawake hushiriki katika biashara hiyo ,mpango huo hauzungumziwi hadharani nchini Ukraine.

Wanandoa wa kigeni wamekuwa wakitembelea taifa hilo kwa wingi tangu 2015, wakati vituo vya kubeba mimba barani Asia vilipoanza kufunga viwanda vyao moja baada ya chengine , huku kukiwa na ripoti za unyanyasaji.

Huku wakizuiwa nchini India, Nepal na Thailand , waliamua kuelekea Ukraine ikiwa ni miongoni mwa maeneo machache ambayo yanaendelea na biashara hiyo pamoja na gharama kama ile ya Marekani.

''Tuna wanadoa wengi wasio na watoto wanaokuja katika taifa hili'', alisema Ana ambaye hakutaka kutambulishwa. Wakati alipokuwa na umri wa miaka 21 na baada ya miaka kadhaa ya kufanya kazi hotelini , Ana hatimaye alikubali kubeba mimba .

Chini ya sheria ya Ukraine ,mama atakayebeba mimba lazima awe na mtoto wake mwenyewe kabla ya kushiriki katika biashara ya kubeba mimba ya mtu mwengine.

Iwapo una mtoto wako mwenyewe hautakuwa na mapenzi mengi na mtoto uliombeba , kulingana na wale wanaowaajiri wanawake hao.

Ana anatumai atajinunulia jumba moja la ghorofa nyumbani kwao , Kamyanets-Podilskyi
Ni safari ndefu.
Ana alianza kuutazama mtandao ambao wanawake wanaobeba mimba za biashara , maajenti, kliniki na wafanyibiashara wa biashara hiyo huweka matangazo yao.

Na muda mfupi baadaye alielekea katika mji mkuu wa Kiev yapata kilomita 450 ili kukaguliwa kiafya.

Aliandikisha kandarasi na wanadoa kutoka Slovenia waliokuwa na tatizo la kupata mtoto.

Ana alikuwa na bahati, kiinitete kiliwekwa katika kizazi chake na kuanza mpango wote wa kubeba mimba kwa minajili ya biashara. Lakini ni wakati huo ambapo changamoto zilianza , anasema.

Anasema kuwa huduma za kiafya wanazopewa ni za kiwango cha chini, wanawake wengine waliobeba mimba walikuwa na matatizo ya kiafya ambayo hayakuangaziwa ama hata kutibiwa kwa wakati na hivyobasi kuzua matatizo mengine, anasema.

Aliweka malalamishi yake katika mtandao wa kijamii ili kuwaonya wanawake wengine lakini alikemewa na kliniki hiyo na sasa bado anaogopa kuwataja hadharani.

Mtoto aliyejifungua alizaliwa akiwa na afya njema lakini mpango wote ulikuwa wa kuogofya.

Bado, amekubali kwa mare nyengine kubeba mimba nyengine wakati huu akiwabebea wanadoa wa Japan. wanafuatilia maswala yote kupitia wakili mmoja mjini Kiev na kuna uwezekano mkubwa kwamba hatokutana nao ana kwa ana.

Ana wakati huu amekuwa na makini katika kuchagua kliniki ,lakini iwapo mpango wote utafanikiwa , kufikia miaka 24 atakuwa amejifungua watoto watatu , mmoja akiwa wake na wengine wawili wa mtu mwengine.

Mama na watoto wake wawili wakitembea karibu na eneo la kumbukumbu la vita vya pili vya dunia katika eneo lililojaa theluji la Kamyanets-Podilskyi

Mama na watoto wake wawili wakitembea karibu na eneo la kumbukumbu la vita vya pili vya dunia katika eneo lililojaa theluji la Kamyanets-Podilskyi

Mahitaji ya kubeba mimba kwa lengo la kupata malipo nchini Ukraine yamepanda kwa asilimia 1000 katika kipindi cha miaka 2 iliopita pekee , anasema Sam Everringham wa shirika la familia kupitia ubebaji mimba wa biashara , shirika la hisani nchini Sidney ambalo huwashauri wanaotarajiwa kuwa wazazi.

Taifa hilo anaongezea, limejipata kwa bahati mbaya miongoni mwa mataifa ambayo yanaruhusu utalii wa kubeba mimba za biashara.

Licha ya kwamba sheria hiyo ni halali nchini Ukraine inawatambua wazazi wanaotarajiwa kuwa wazazi kutoka wakati mimba inaposhika na haitoi kiwango cha mwisho cha fedha ambazo anayebeba mimba hiyo atalipwa -hatua inayowapatia fursa wanaobeba kunadi bei.

Lakini haimaanishi kwamba ni swala la moja kwa moja. Ikitegemea unakotoka , mkakati wa kumtoa mtoto huyo nje ya taoifa hilo inaweza kuwa ndoto kali huku wanandoa kutoka mataifa kadhaa ikiwemo Uingereza wakilazimika kusalia nchini humo kwa miezi kadhaa.

Huku kliniki nyingi nchini Ukraine zikionekana kufanya kazi kwa uwazi na kuwahudumia wanawake hao vizuri washirika wengi katika sekta hiyo pamoja na wanawake wanaobeba mimba hizo huzungumzia kuhusu wale walio na sifa mbaya.

Kuna ripoti kadhaa ambazo hazijathibitishwa kuhusu viinitete vinavyobadilishwa na ukaguzi wa kiafya wa viwango vya chini

"Kuna mifano ambapo maajenti wa UKraine wamekataa kulipa gharama za kubeba mimba iwapo mbebaji atakiuka miko mikali , iwapo ataavya mimba'', kulingana na bi Everingham.

Kuna mifano mibaya ambapo maajenti hubadilika na kuwa wanyama iwapo mpango wa kubeba mimba haukuwafurahisha wazazi.

Wanawake wanaobeba mimba za biashara wakisafiri kutoka Kiev kutoka nyumbani kwao kwa ukaguzi wa kila mara
Image caption
Wanawake wanaobeba mimba za biashara wakisafiri kutoka Kiev kutoka nyumbani kwao kwa ukaguzi wa kila mara
Olga Bogomolets, daktari na mbunge ambaye anaongoza kamati ya bunge nchini Ukraine kuhusu afya anasema kuwa anaamini wanawake wadogo wanavutiwa na kubeba mimba za biashara kutokana na kuanguka kwa hali ya maisha katika taifa hilo.

Uchumi wa taifa hilo uliathiriwa na mfumuko mbaya 2014 na 2015 kutokana na mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine kati ya jeshi na wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi.

Sekta hiyo kulingana na bi Bogomolets haijadhibitiwa vilivyo hivyobasi swala hilo linawaweka wabebabaji mimba na wazazi wanaolipa katika hatari

Tetiana anaishi na mamake lakini ameficha mimba alionayo akisema kuwa angependa kuelekea Kiev kutafuta kazi.Jana ambaye alijifungua mizezi miwli iliopita , anamshauri Tetiana anafaa kuchukulia biashara ya kubeba mimba kama kazi ya kawaida .

Anakumbuka mtoto aliyejifungua akichukuliwa mara tu alipojifungua huku akiwa amechoka katika kitanda chake.Anakiri kwamba hisia za kujifungua humjaa na alifikiria kuhusu mtoto huyo alipoelekea nyumbani.

Utakuwa mtu mbaya sana kutohisi hilo., anasema.lakini unapoona furaha na tabasamu kutoka kwa wazazi wenyewe, unagundua kwamba kila kitu kiko sawa na mtoto yuko katika hali nzuri.

Akiwa nyumbani na mwanawe magharibi mwa Ukraine, Ana pia anafikiria jukumu lake la kubeba mimba.Karibuni ataanza safari ya saa saba ya treni ili kuelekea kuelekea Kiev ili kuwekwa kiinitete katika kizazi chake.

Ijapokuwa ni hatua ngumu, ana matumaini ya kile atakachopata. Anataka kutumia fedha hizo kujinunulia jumba moja la ghorofa. Na pia anafurahia kile atakachowafanyia wazazi waliomlipa kuwabebea mimba.

''Wakati wanapobubujikwa na machopzi ya furaha na kukushukuru, unahisi kitu ulichowafanyia'', anasema. Walinimbia kwamba mimi ni mtu muhimu sana katika maisha yao''.

Vitambulisho Maalumu Kutumika Kuingia Katika Machimbo ya Mererani

$
0
0
Vitambulisho Maalumu Kutumika Kuingia Katika Machimbo ya Mererani
Serikali imetangaza utaratibu mpya wa kuingia katika machimbo ya Tanzanite yaliyopo Mererani ambapo kuanzia Februari 15 ni lazima mtu awe na kitambulisho maalumu.

Akizungumza na wachimbaji wa madini hayo jana Februari 13 mjini hapa, Kamishna na Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma alisema vitambulisho vitakavyotakiwa ni vile vinavyotolewa na Wizara ya Madini.

Juma alisema hadi sasa ni vitambulisho 6,000 ambavyo tayari vimetolewa na katika machimbo hayo kuna wachimbaji zaidi ya 15,000.

“Baada ya ujenzi wa ukuta kukamilika sisi kama wizara tutaanza Februari 15 kudhibiti kuingia migodini,” alisema.

Alisema wamiliki wa migodi yote, wachimbaji na madalali wa madini pamoja na watu wengine ambao watataka kuingia kwenye eneo lililozungushwa ukuta lazima wawe na vitambulisho.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula alisema agizo hilo la Serikali halina utani, hivyo ni lazima wanaotaka kuingia migodini wafuate sheria.

Alisema lengo ya mpango huo ni kuhakikisha madini hayatoroshwi na pia Serikali inapata stahiki zake kabla ya madini kutoka nje ya uzio.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (Marema), Sadiki Mnenei alisema wanaunga mkono mpango wa vitambulisho, lakini wanaomba muda zaidi wa kuzuia wasio na vitambulisho hadi Machi mosi.

“Ili kutoathiri kazi zetu tunaomba utaratibu mpya kuanza mwezi ujao kwani gharama za kitambulisho ni kubwa kwa kuwa kila mchimbaji anatakiwa kutoa Sh3,500 na mmiliki wa mgodi Sh5,000,” alisema.

Alisema kwa wastani mgodi mmoja una zaidi ya wafanyakazi 100, hivyo wote kuwapa vitambulisho wakati mmoja ni vigumu.

Simba Wamuacha Asante Kwasi

$
0
0
Simba Wamuacha  Asante Kwasi
KIKOSI cha Simba kimewasili salama jijini Mwanza asubuhi kwa ndege tayari kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao Mwadui FC huku wakimuacha beki wao kiraka Mghana, Asante Kwasi.

Simba inatarajiwa kuvaana na Mwadui kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.



Katika mechi hiyo, Simba wataingia uwanjani wakiwa na morali ya hali juu baada ya kuanza vizuri michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwafunga Gendarmerie ya Djibouti mabao 4-0.



Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma alisema wanashukuru kikosi chao kimefi ka salama kikiwa na morali ya hali ya juu katika kuhakikisha wanarejea jijini Dar es Salaam na pointi tatu.



Djuma alisema, msafara huo umeondoka na wachezaji wote isipokuwa Kwasi anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye mechi zilizopita za ligi kuu.



“Tumewasili salama mkoani Mwanza kwa ndege na kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa keshokutwa (kesho) dhidi ya Mwadui na jambo la kushukuru kwetu kama benchi la ufundi kuwa wachezaji wetu wako fi ti kwa ajili ya mechi hiyo.



“Kwasi tumemuacha Dar es Salaam kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye michezo iliyopita ya ligi kuu.



“Hivyo, kama benchi la ufundi tukiongozwa na bosi wetu Lechantre (Pierre) tayari tumeanza kumuandaa Tshabalala (Mohamed              Hussein) kwa kumpa mbinu za uchezaji kama unavyojua Kwasi alikuwa ashauzoea mfumo mpya wa kocha unaohitaji kukaba na kushambulia ndani ya wakati mmoja,” alisema Djuma.

Mama Diamond Ajitoa Katika Ugomvi wa Zari na Mobetto "Mimi Simo"

$
0
0
Mama Diamond Awatosa Zari na Mobetto
Mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim amejitoa kwenye gogoro linaloendelea kati ya ‘wakweze’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na Hamisa Mobeto.

Kabla ya kauli ya mama Diamond juu ya warembo hao mapema wiki hii, wikiendi iliyopita kuliibuka ubuyu kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kuwa, ugomvi kati ya Zari na Mobeto ulikuwa umeibuka upya baada ya kupoa kwa siku kadhaa.

Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ulibaini kwamba, ugomvi baina ya wawili hao ulirejea upya baada ya Mobeto kukutana na Diamond kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii na kukubaliana juu ya malezi ya mtoto wao, Abdulatif Nasibu ‘Prince Dully’.

Ilisemekana kwamba, kuna maneno aliyoweka Zari kwenye Mtandao wa Snapchat yakiashiria kutokuwepo kwa maelewano kati yake na Diamond kufuatia tukio hilo lililoonekana kumweka jamaa huyo karibu na Mobeto.


Kama hiyo haitoshi, kuna ubuyu kuwa, ugomvi huo uliingia hadi kwenye familia ya Diamond ukimhusisha mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ na mdogo wake aitwaye, Esma Khan ‘Esma Platnumz’.

Kufuatia hali hiyo, gazeti hili lilimtafuta mama Diamond na kumuuliza juu ya sakata hilo na kwamba je, ni kweli alikuwa na ugomvi na Zari ambapo aliamua kutoa ya moyoni akisema kuwa, mambo yanayowahusu watu hao hataki ahusishwe nayo.



“Naomba mambo yanayowahusu hao (Zari, Mobeto na Diamond) waulizwe wenyewe mimi simo,” alisema mama Diamond.

Kwa upande wake Esma aliliambia gazeti hili kuwa, kwa sasa hajishughulishi na mambo ya nyumbani kwao badala yake anadili na maisha ya familia yake na mumewe, Petit Man.

“Kwa sasa siwezi kudili na mambo ya nyumbani kwetu, nadili na maisha yangu na familia yangu,” alisema Esma.



Kwa upande wake, Mobeto, simu yake ya mkononi haikuwa hewani kila ilipopigwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi haukupokelewa.

Kumekuwa na habari nyingi juu ya kuwepo kwa kutoelewana kati ya Zari na familia ya Diamond huku Mobeto na na Wema Sepetu wakihusishwa.

Rais Magufuli Aungana na Wakristo Wengine Kushiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu

$
0
0
Rais Magufuli Aungana na Wakristo Wengine Kushiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu inaoashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma.

Magufuli akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika ibada iliyoongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar, leo Februari 14, 2018.



Viongozi Watano wa Kiislamu Watoweka Katika Mazingira ya Kutatanisha

$
0
0
Viongozi Watano wa Kiislamu Watoweka Katika Mazingira ya Kutatanisha
Viongozi watano wa Dini ya Kiislamu wanadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (Jumaza) imeviomba vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa suala hilo.

Viongozi hao ni mlezi wa taasisi za Kiislamu, Amir Haji Khamis Haji mkazi wa Mpendae, Hamad Ali Haji mkazi wa Fuoni, Suleiman Juma Suleiman (Makadara), Salum Said Chande (Kinuni) na Abbas Said Chasuma wa Kizimbani.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali alisema jana kwamba hawajui walipo.

Awali, naibu katibu mtendaji wa Jumaza, Khamis Yussuf Khamis alisema kupotea kwa watu hao hakuleti taswira nzuri na kuvitaka vyombo kuliona hilo na kulifanyia kazi haraka.

Alisema kuwa vyombo hivyo ndivyo vyenye jukumu la kuhakikisha amani na haki za raia wote visiwani Zanzibar zinapatikana kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

Alisema Jumaza itaendelea kufuata taratibu za kisheria katika kuhakikisha waumini hao wa dini ya Kiislamu wanatafutwa hadi kupatikana ili kuzipa faraja familia na jamaa hao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Ali alisema Jeshi la Polisi linasikitishwa na tukio hilo na kuahidi kushirikiana na familia za waliopotelewa kuwasaka walipo.

Watu Watatu Wakamatwa na Nyara za Serikali Zenye Thamani ya Milioni 33

$
0
0
Watu Watatu Wakamatwa na Nyara za Serikali Zenye Thamani ya Milioni 33
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, oparesheni na doria zenye tija ambapo February 5, 2018 katika maeneo ya Mwanjelwa Polisi wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na nyara za Serikali ambazo ni vipande vinne vya meno ya Tembo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Mohammed Mpinga amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Kenedy Lupembe Simsokwe ambaye Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha SAUT – Tawi la Mbeya, Mathew Elikana Mwanjala ambaye ni Mpiga picha na Shaban Mkwiche.

Mpinga amesema baada ya kukamatwa na kupekuliwa, watuhumiwa walikutwa na nyara hizo ambazo ni Vipande vinne vya Meno ya Tembo ambavyo vina uzito wa Kilogram 5 na thamani yake ni Tshs 33,000,000/=. 

Kamanda Mpinga amesema taratibu za kisheria zinafanyika ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani na imeitaka jamii kuacha tabia ya kuwa na tamaa ya kujipatia utajiri wa haraka kwa kutumia njia za mkato zisizo halali, badala yake wafanye kazi halali ili kupata kipato halali.

Wolper Awatolea Uvivu Wanaume Wadangaji Awapa Somo Hili

$
0
0
Wolper Awatolea Uvivu Wanaume Wadangaji Awapa Somo Hili
February 14,2018 nazidi kukusogezea karibu stories zilizochukua headlines kupitia mitandao ya kijamii ambapo kwenye upande wa instagram muigizaji Jacquline Wolper amewaponda wanaume wanaotegemea wanawake kupata kipato au fedha.

Kupitia instagram account ya Jacquline Wolper amepost video ya mchekeshaji Wakuvanga au Mama Atupele na kuandika caption “Naomba mjifunze kitu wanaume wadangaji, mnadangwa au unadanga mwisho wa siku unageuka houseboy kwa unayoenda kupambana nayo..sio kila unachoona kipo kama unavyoona! Haya katarina njoo hapa😂😂”

Kutokana na caption hiyo ya Jacquline Wolper wengi wameitafsiri kuwa ni somo kwa wanaume wanaotegemea kila kitu kutoka kwa wanawake na kila wanachokiona sio kama kilivyo.

Chuzi: Sina Mpango wa Kuoa Maishani Mwangu

$
0
0
Chuzi: Sina Mpango wa Kuoa Maishani Mwangu
WAKATI akiwa na watoto wanne aliozaa na mama tofauti, mwigizaji mkongwe wa Bongo Movies, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuzi’ ameibuka na kueleza kwamba kamwe hana mpango wa kuoa.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Chuzi alisema kuwa, uamuzi wake ni kwamba hataoa hadi mwisho wa maisha yake na anachokifanya kwa sasa ni kuwalea watoto hao wanne alionao hivyo wanaosubiri aoe au waliotarajia awaoe, waandike maumivu.

“Sina mpango wa kuoa maishani mwangu, watoto wanne nilionao ambao ni Abdrahim, Abdmalick, Salma na Ahmed wananitosha. Kwa sasa natafuta fedha kwa kasi ili niwalee vizuri maana ndiyo kazi iliyobakia,” alisema Chuzi.

Mwana Aipongeza Serikali "Nguo za Heshima Ndio Kila Kitu"

$
0
0
Mwana Amuunga Mkono Waziri Shonza "Nguo za Heshima Ndio Kila Kitu"
MWANA-DASHOSTI wa Bongo Movies, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ amefunguka kuwa kitendo cha Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kupiga marufuku mastaa wa kike kujiachia nusu utupu, ndiyo kila kitu katika kurudisha hadhi iliyopotea ya sinema za Kibongo.

Mwana alisema kuwa, baadhi ya mastaa, hasa wa filamu wanaojiachia nusu utupu ndiyo waliochangia kushuka kwa sanaa hivyo waziri amefanya jambo la maana kupiga marufuku na kuwachukulia hatua wale ambao wanaendelea kusambaza picha hizo za kihasara kwenye mitandao ya kijamii.

“Sijawahi kukaa nusu utupu na sidhani kama itatokea, ninaipongeza sana serikali kwa kupiga marufuku picha za nusu utupu zilizokuwa zikitupiwa mitandaoni na baadhi ya wasanii kwani zinaharibu maadili ya Kitanzania, ninaamini sasa hadhi ya filamu itarudi maana jamii ilitudharau kutokana na mambo kama hayo,” alisema Mwana.

Familia Yenye Utata ya Gupta Mwenye Mahusiano ya Karibu na Rais Jacob Zuma Yavamiwa na Polisi

$
0
0
 Familia Yenye Utata ya Gupta Mwenye  Mahusiano ya Karibu na Rais Jacob Zuma Yavamiwa na Polisi
Askari Polisi mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini wameizingira nyumba ya familia ya kitajiri ya ‘Gupta’ ambayo ipo na mahusiano ya karibu na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Picha inayohusiana
Rais Jacob Zuma akiwa na baadhi ya wanafamilia ya kifahari ya GUPTA.

Kwa mujibu wa mtandao wa Reuters umedai kuwa polisi wamezingira barabara zote zinazoingia kwenye eneo la nyumba za familia hiyo huku wakiwa na silaha nzito za kijeshi.

Msemaji wa jeshi la polisi mjini  Johannesburg, Hangwani Mulaudzi amethibitisha taarifa hiza lakini amekataa kutolea maelezo kwa nini nyumba hiyo ya kifahari imezingirwa na polisi.

Tangu mwaka 20015 familia ya Gupta imekuwa ikishutumiwa na viongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini kuwa inahifadhi mali za wizi zinazoibwa serikalini na Rais Zuma.

Ulinzi huo umekuja katika kipindi hiki ambacho Chama cha ANC kwa sauti moja kimetoa tamko la kumshinikiza Rais Jacob Zuma kujiuzulu nafasi yake ya urais.

Jana chama hicho kilimpa masaa 48 Rais Jacob Zuma kujiuzulu urais huku mwenyewe akitaka apewe muda wa miezi mitatu hadi sita kuchukua uamuzi huo.

Habari Njema kwa Wanaopenda Muonekano Mzuri kwa Kututoa Dawa za Asili Zisizo na Kemikali

$
0
0

WEKA MUONEKANO WAKO VIZUR SASA, NIWAUZA WA PRODUCT ZA ASILI NA MAFUTA YASIO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI KWA MATUMIZI NA MATOKEO NI KWAARAKA KUANZIA WEEK (2) HADI (4)🍌🍍🥑

1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _100,000/
2) KUREFUSH NYWELE KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA 100,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO KUWA NA UMBO ZURI (HIPS & BATKS)KUNADAWA AINA TATU (@)KUPAK 100,000/(B) KUNYWA (C)VIDONGE_130,000/
4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, KIUNONI KUPAK _100,000/
5)TOA KITAMBI KABISA(@) KUPAK 10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING MAJAN 130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE
@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _90,000/
8) PIA UNA KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_90,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_80,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_80,000/
13) KUWA MWEUPE WAKUPENDEZA(@) VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU VINYWELEO MWILINI _100,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME (@)JELI AINAZOTE 100,000/(B)VIDONGE MAX MAN NA AINA NYINGI_ 100,000/
16) ENGEZA MAUMBIL YA KIUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_130,000/
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUFIKA KILELE_100,000/
18) RUDISH(BIKRA) 100,000/
19)ONDOA MAFUTA USONI _90,000/
20) ONDOA MIKUNJO USON_80,000/(21) ENGEZA MGUU_100,000/ 21) TUDISH NYELE KWENYE KIPARA 150,000/ 22) DAW YA NGIRI YAKUVIMBA NA KULEGEA 100,000/🍍🍉🥑

TUNAPATIKAN DAR E SALAAM:PIA NJE YA NCHI TUNATUMA MIZIGO,NA KWA MIKOAN KOTE UTAPATA *KESSY* NI WAAMINIFU WA KUTUM MIZIGO NA KUFIKA KWA WAKATI PIGA CM (+255) 0719955528
0756259180
0785371237
@ *Pendeza_kessy_product*
Delivery POPOTE ULIPO,

Wazanzibar elfu 40 Wafungua Kesi Mahakamani Wakihoji Uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

$
0
0

Wazanzibar elfu 40 wafungua kesi Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki(EACJ) wakihoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
-
Kesi hiyo imefunguliwa katika Masijala ya Mahakama hiyo iliyoko Dar na Rashid Adiy kwa niaba ya wenzake 39,999
-
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ), Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makonda Aliwakia Gazeti " Kuna Gazeti Linaangaika Sana Kunichonganisha Siwezi Kulifumbia Macho"

$
0
0
Makonda Aliwakia Gazeti " Kuna Gazeti Linaangaika Sana Kunichonganisha Siwezi Kulifumbia Macho"
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuna gazeti moja nchini limekuwa likiandika habari za kumchonganisha yeye na viongozi wengine au taasisi nyingine za serikali,  jambo ambalo amesema halikubaliki wala hawezi kulifumbia macho.

 Makonda ameyasema hayo leo, Feb. 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa Jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Amana, iliyopo Ilala jijini Dar ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

 Kauli hiyo ya Makonda imekuja kutokana na maamuzi yake ya kuvunja mabaraza yote ya ardhi ya mkoa wa Dar, na kutaka kazi hizo zifanywe na makatibu tarafa hadi pale ambapo utaratibu mwingine utawekwa, jambo ambalo baadhi ya vyombo vya habari na wanaharakati walidai kuwa anaingilia kazi ya mahakama.

 “Kuna gazeti moja linahangaika sana kuandika vitu vibaya kuhusu Mkoa wa Dar, wanajifanya wanajua sana sheria, wanachonganisha, na leo nimeona wameandika tena, wasitupotezee muda.

“Aliyeanza kugombanisha duniani ni shetani, lakini ilifika wakati akashindwa, hili gazeti raha yao wanataka wasikie mahakama imemkataa Mkuu wa Mkoa, hawaoni mateso ya wanachi wala kuyaripoti.

“Sasa aelewe tu kwamba hawatafanikiwa, nimeangalia nikabaini kuna ardhi moja bosi wao aliichukuaga, ipo tu limebaki poli katika eneo moja katika Wilaya ya Ubungo, tutaangalia taratibu angalau tuwapatie watu lijengwe soko la kisasa pale,” alisema Makonda bila kutaja ni gazeti gani.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images