Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Watumiaji wa Mtando wa Snapcat Wataka Kubadilishiwa Mfumo

$
0
0
Watumiaji wa Mtando wa Snapcat Wataka Kubadilishiwa Mfumo
Moja kati ya habari za kimataifa leo February 15, 2018 ni kwamba siku chache baada ya mtandao wa Snapchat kubadili mfumo wake, watu Milioni 1 kutoka nchini mbalimbali Duniani wamesaini ombi la kuomba wamiliki wa mtandao huo kurudisha mfumo wa zamani wa kutumia mtandao huo.

Inaelezwa kuwa design hiyo mpya ya Snapchat ilifanyika kwa lengo la kutenganisha mwingiliano wa moja kwa moja baina ya marafiki na maudhui kutoka kwa watu maarufu na wenye ushawishi kwa namna tofauti.

Mwanzilishi wa Snapchat Evan Spiegel aliandika katika blog yake kuwa aliamini kuwa mwingiliano huo ulipelekea ongezeko la habari za uongo na ndio sababu za kuamua kubadilisha na kutenganisha maudhui hayo.

Watumiaji wa Snapchat wameeleza kuwa mfumo mpya huo wa mtandao huu ni mgumu kutumia ukilinganisha na uliopita na kwamba, vipengele vingi vilivyoongezwa kwenye mtandao huo havina maana na vinapoteza maana nzima ya kutumia mtandao huo tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwenye mfumo huu mpya wa Snapchat, taarifa za marafiki wa mtumiaji zinaonekana na kupatikana upande wa kushoto wa ukurasa huo wa Snapchat huku taarifa za watu maarufu zinapatikana katika upande wa kulia tu.

Luteni Jenerali Ndomba Amuasa Mnadhimu Mkuuwa JWTZ "Usilete Ukabila"

$
0
0
Luteni Jenerali Ndomba Amuasa Mnadhimu Mkuuwa JWTZ  "Usilete Ukabila"
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba amefunguka na kumuasa Meja Jenerali, Yakubu Hassan Mohamed ambaye ameapishwa leo Februari 15, 2018 kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania


Luteni Jenerali Samuel Ndomba amemtaka kiongozi huyo wa jeshi kutofanya kazi kwa kuangalia ukabila au kuwa na upendeleo wowote kwa ndugu, marafiki au imani ya dini yake na kumtaka kuwa kiongozi mwenye kutenda haki.

"Baada ya kuteuliwa tu jana inawezekana marafiki wamesema Mungu atupe nini na sisi tutafaidi hapana wewe si Mnadhimu Mkuu wa marafiki ila ujue wewe ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Wewe ni Muislam kuteuliwa kwako inawezekana Waislam wamesema na sisi tumepata hiyo siyo sahihi kwani wewe si Mnadhimu Mkuu wa Waislam bali wewe ni Mnadhimu Mkuu wa watu wa dini zote, inawezekana Kabila lako watu wa Irangi huko wanasema na sisi Wairangi siku nyingi tulikuwa hatujapata sasa tumepata watatuona na Mahakama Kuu inahamia huko huko sasa angalia hicho wewe si Mnadhimu Mkuu wa wa Irangi bali wewe ni Mnadhimu Mkuu wa Makabila yote hao wote ni wako" alisisitiza Ndomba

Aidha Ndomba aliendelea kumshauri Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na kumweleza kuwa asikubali familia yake ikavaa koti lake lakini pia akamtaka asijikite kwenye kazi moja kwa moja na kuisahau familia yake na kudai hilo litakuwa ni tatizo.

Fid Q Afunguka Kuhusu Mahusiano Yake ya Kimapenzi

$
0
0
Fid Q Afunguka Kuhusu Mahusiano Yake ya Kimapenzi
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q ameeleza ni kwanini sasa hivi ameamua kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi tofauti na hapo awali.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Fresh’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kwa sasa amempata mtu ambaye wanaendana sawa kimtazamo hasa katika maongezi yao.

“Sikuwa na hiyo picha kwamba nakuja kuwa wa kwake, sema nilikuwa navutiwa na maongezi yake, yaani naongea na mtu ambaye anajua vitu vingi ambayo na mimi navijua,” amesema Fid Q.

“Unajua kuna vitu fulani unakuwa unaongea na watu, kuna watu wanakuwa wanakuona kama chizi na kuna mtu mwingine ikitokea unaongea naye na anakuelewa, labda vitu vya kisaikolojia na anakuelewa unaona inanoga, kwa hiyo hicho ndio kitu kilivutia zaidi,” ameongeza.

Rapper huyo ameongeza kuwa baada ya mazungumzo ya hapa na pale na mrembo huyo amegundua kuwa wapishana siku moja katika kuzaliwa (birthday), Fid Q amezaliwa, August 13 na mpenzie August 14.

Tausi Awapa Makavu Wanaomsema Vibaya Kuhusu Mavazi Yake

$
0
0
Tausi Awapa Makavu Wanaomsema Vibaya Kuhusu Mavazi Yake
Msanii wa filamu nchini Tanzania na Rais wa watoto, Tausi Mdegela amefunguka na 'kuwachamba' watu wanaomsema vibaya kuhusiana na mavazi yake anayovaa na kudai kama inawakera basi wakanunue nguo wampelekee na sio kumpangia cha kuvaa.


Tausi ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri baada ya baadhi mashabiki zake wakimshambulia kuhusu nguo zake katika mitandao ya kijamii.

"Mimi ni Tausi na nitabaki kuwa Tausi tuu, nivae joho, pensi hata taiti ni mimi tu. Kwa hiyo mtu hawezi kunipangia maamuzi kuhusu mavazi eti usivae hichi vaa kile. Niletee dera halafu chukua zile pensi choma 'simple' tu", amesema Tausi.

Pamoja na hayo, Tausi ameendelea kwa kusema "kwa sababu mimi nimenunua hiyo pensi yangu ni hela ambayo niliyokuwa nayo hiyo siku nikaona nisiondoke mikono mitupu nikanunua hiyo pensi. Wewe ambaye inakukwaza niletee nguo ambayo unahisi nitapendeza tofauti na ninavyovaa".

Kwa upande mwingine, Tausi amedai kama mpenzi wake akimsifia kuwa amependeza kutokana na mavazi aliyoyavaa hawezi kumpa nafasi mtu mwingine kumsikiliza juu ya alichokivaa.

Sadifa Afutiwa Kesi Mahakamani Aachiwa Huru

$
0
0
Sadifa Afutiwa Kesi Mahakamani Aachiwa Huru
Mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Dodoma imemwachia mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha maombi ya kuifuta kesi iliyokuwa ikimkabili.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 15, 2018 na hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Fovo baada kuridhia ombi la wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Biswalo Biswalo kuiomba mahakama kuifuta kesi hiyo.

Desemba 9, 2017, Sadifa alikamatwa na Takukuru akiwa nyumbani kwake Mailimbili mjini hapa akituhumiwa kugawa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja huo.

Mbunge huyo wa Donge na mjumbe wa kamati kuu ya CCM aliyemaliza muda wake, baada ya kukamatwa alilala mahabusu kwa siku tatu baada ya kukosa dhamana.

Katika shtaka la kwanza, Sadifa alidaiwa aliwahonga wanachama ili wamchague Rashid Mohamed Rashid ambaye alikuwa akiwania umakamu mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo.

Shtaka la pili, alidaiwa kuwaahidi kuwalipia gharama za usafiri wanachama wa umoja huo kwa kuwasafirisha kutoka Dodoma hadi Kagera kama zawadi ili wamchague Rashid.

Recho Kizunguzungu Akana Kutoka Kimapenzi na TID "TID Hawezi Kuwa Mtu Wangu"

$
0
0
Recho Akana Kutoka Kimapenzi na TID "TID Hawezi Kuwa Mtu Wangu"
Msanii wa muziki Bongo, Rachel amesema hajawahi kutoka kimapenzi na TID kama inavyokuwa ikiripotiwa.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Same Boy’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na wala hajawahi kubeba ujauzito wa TID.

“Niseme tu TID sio bwana yangu, sio mtu wangu, TID hawezi kuwa mtu wangu, TID mkubwa ujue, ana type zake, mimi nina type zangu za wanaume ambao natakiwa ni date nao, TID siyo type ya wanaume ambao naweza ku-date nao, kirafiki kuongea sawa,” amesema.

“Naomba nieleweke, sijawahi kutoka kimapenzi na TID, sijawahi kubeba mimba ya TID hata mara moja,” amesisitiza Rachel.

Alichokisema Edo Kumwembe Baada ya Zuma Kujiuzulu na Zari Kumwacha Daimond

$
0
0
Alichokisema Edo Kumwembe Baada ya Zuma Kujiuzulu na Zari Kumwacha Daimond
Moja kati ya stori zilizochukua headlines usiku wa jana February 14 2018 ni pamoja na maamuzi ya Zari The Boss Lady kutangaza kuachana na mpenzi wake Diamond Platnumz kwa madai ya skendo za usaliti wa kimapenzi.

Kingine kilichochukua headlines ni maamuzi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kutangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo ya Urais kwa tuhuma mbalimbali ambazo zimetolewa na chama chake.



Mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe ambaye anapenda kuandika vitu vya utani katika account yake ya instagram baada ya matukio hayo akaandika hivi “Rais wangu Zuma kajiuzulu, shemeji yangu Zari kajiuzulu, kocha wangu Wenger HATAKI 😀😀😀😀😀😀”

Waziri Majaliwa Awataka Watendaji Kuwafuata Wananchi na Si Kukaa Ofisini

$
0
0
Waziri Majaliwa Awataka Watendaji Kuwafuata Wananchi na Si Kukaa Ofisini
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa wilaya na watendaji wa halmashauri kutoka maofisini kuwafuata wananchi maeneo yao ili kusikiliza kero zao.

Amesema hayo leo Februari 15, 2018 katika Ikulu ndogo jijini Mwanza baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali na dini.

"Watendaji hamna sababu ya kukaa ofisini wakati wananchi wanahangaika na kero, nendeni kwa wananchi kwa kuwa wao hawana uwezo lakini nyie mnawezeshwa kila kitu,” amesema Majaliwa.

Pia, Majaliwa ameagiza watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanakuwa na Ilani ya CCM, kuisoma na kuielewa hata kama mtendaji atakuwa sio kada wa chama.

Pia, ameagiza kufanya operesheni kuhakikisha mipaka ya Ziwa Victoria inalindwa kwa kuwahoji watu wote ambao watakuwa na mashaka nao,  si kufanya operesheni ya  uvuvi haramu pekee.

Majaliwa amesema lengo la ziara yake ni kukagua huduma muhimu za afya, maji, elimu na miundombinu  kwa kuwa Serikali inahitaji kuona wananchi wanapata mabadiliko makubwa katika maendeleo.

Amesema kwenye ziara yake atatembelea mashamba ya pamba kujionea maendeleo na kuzungumza na wakulima, lengo la Serikali ni kufufua zao hilo na jitihada zimeanza.


Madiwani Watatu wa Chadema Wamejiuzulu Nafasi Zao na Kujiunga CCM.

$
0
0
 Madiwani Watatu wa Chadema Wamejiuzulu Nafasi Zao na Kujiunga CCM.
Habari kutoka mkoani Arusha leo February 15, 2018 ni kwamba madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika wilaya ya Ngorongoro wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM.

Wamedai kuwa uamuzi wao huo wa kukihama chama cha CHADEMA ni wa kumuunga mkono Raisi John Magufuli katika utendaji wake wa kazi.

Madiwani hao ni Daniel Olkery wa kata ya Ngorongoro, Lazaro Saitoti kata ya Ngoile pamoja na Sokoine Moir ambaye ni diwani wa kata ya Alaitole.

Shilole Arudi Kwao Igunga..... Atoa Msaada Katika Shule Aliyowahi Kusoma

$
0
0
Shilole Arudi Kwao Igunga..... Atoa Msaada Katika Shule Aliyowahi Kusoma
Moja kati ya jambo la msingi ambalo wasanii na watu maarufu wamekuwa wakilifanya ni kurudisha fadhila kwa jamii ambapo wengi wao wamekuwa wakitoa misaada katika shule au vituo vya watoto wanaoishi maisha magumu, Shilole ameingia kwenye list ya mastaa walioamua kurudisha fadhila kwa jamii..

Shilole ametoa msaada wa Pen, Penseli pamoja na vifutio kwa wanafunzi wa shule ya Igunga aliyosoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba ambapo baada ya kutoa zawadi hizo alipost kwenye ukurasa wake wa instagram na kuandika.

…>>>“Mapema jana nilikuwa shule ya msingi Igunga ambayo nilisoma hapo kuanzia la kwanza mpaka la saba! Kukumbuka ulipotoka ni jambo jema sana na kuchangia kidogo niliwapa zawad ya pen! Pensel! na vifutio asante Flaviana Matata foundation kwa kunisaport kwa hili 🙏🙏” – Shilole


Kesi ya Masogange Yafika Mwisho Sasa Kusubiria Hukumu

$
0
0
Kesi ya Masogange Yafika Mwisho Sasa Kusubiria Hukumu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 21, 2018 itatoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga na mshtakiwa mwenyewe kujitetea.

Akiongozwa na Mawakili Nehemiah Nkoko na Ruben Simwanza kutoa utetezi wake leo Masogange ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote.

Masogange  anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi wake amedai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.

Akijitetea Masogange alidai kuwa mbali ya ‘Uvideo Queen’ pia alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo.

Alidai kuwa Februari 14,2017 polisi walienda nyumbani kwake, yeye hakuwepo, alikuwepo dada yake, yeye alikuwa amempeleka mjomba wake kununua vitu Ocadeco.

"Polisi waliniulizia, dada yangu aliwauliza nyie ni kina nani, wakamueleza kuwa wao ni ndugu zetu, dada yangu aliwaambia sisi hatua ndugu kama nyie", alieleza Masogange.

Alieleza kuwa polisi hao walimuweka chini ya ulinzi dada yake na kumtaka ampigie simu na ajifanye anaumwa ili arudi nyumbani.

Masogange alieleza kuwa dada yake alimpigia simu na kumueleza anaumwa sana, naye akamjulisha kuwa ataenda muda sio mrefu, lakini alikwenda saa 12 jioni.

Alidai kuwa ilipofika nyumbani kwake getini kabla hajashuka kwenye gari alimuona mlinzi amekaa na watu wanne, aliwasalimia na kuingia ndani.

Aliendelea kudai kuwa ilipofika ndani alimkuta dada yake, askari wa kike na askari wawili wa kiume, walimueleza wanasubiri yeye na wakajitambulisha kuwa wao ni polisi.

Masogange alidai kuwa aliwauliza wanashida gani na wakamueleza kuwa wamekwenda kufanya upekuzi, wakapekuwa wakamueleza kuwa hawatapata kitu chochote.

Alidai baada ya upekuzi huo, alichukuliwa na kupelekwa kituo kuu cha polisi na kwamba walipofika mapokezi akaandikisha jina na wakampeleka rumande ambapo alikaa siku tisa.

Aliongeza kuwa baada ya kukamatwa Februari 14, 2017 na Februari 15, 2017 akiwa polisi alipelekwa katika ofisi iliyokuwa na watu 15 ambapo kwa nyakati tofauti alikuwa akimuuliza maswali.

Baada ya mahojiano, Masogange alidai kuwa alipelekwa Mwananyamala ambapo alioneshwa picha mbili za wanaume wawili, akaulizwa kama anawafahamu na kuwaeleza kuwa hawafahamu.

Alidai baada ya hapo alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo afande Judy alishuka katika gari walilokuwa nalo, akamuita mama wa makamo, akamuomba kikontena kidogo cha plastiki cha kuhifadhia mkojo na Masogange akaambiwa angozane na mama hiyo.

Aliendelea kudai aliongozana naye, wakaingia chooni ambapo huyi mama wa makamo alimkabidhi kikontena hicho cha kuwekea mkojo, akaingia chooni mwenyewe akatoa mkojo na kumkabidhi hiyo mama wa makamo .

Masogange alidai kuwa baada ya hapo afande Judy walimueleza hiyo mama wa makamo kuwa watawasiliana, na akarejeshwa polisi.

Masogange aliendelea kutoa utetezi wake alidai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.

Alibainisha kuwa mtu anayetumia dawa za kulevya hawezi kuhimili kukaa siku bila ya kutumia dawa za kulevya utetemeka na kuwa kama amechanganyikiwa, lakini yeye alikaa na hali yake ikiwamo nzuri.

" Mheshimiwa mimi sijawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja nipo tayari hata mahakama yako ijiridhishe kwa kunipima." Alieleza Masogange.

Wakili wa Serikali, Kakula alimuuliza Masogange kuwa ni sahihi alikamatwa Februari 14,2017.

Masogange ni kweli

Kakula ni sahihi Februari 15,2018 ulipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali

Masogange: kweli

Kakula uliongozwa na askari wa kike akiwa na chupa

Masogange hapana

Kakula ni sahihi huo mkojo ni wewe mwenyewe uliutoa na kumkabidhi yule mama wa makamo

Masogange: ndiyo

Masogange katika kesi hiyo anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Pia, anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Polepole Awataka Polisi Kuwazuia Chadema Kulinda Kura

$
0
0
Polepole Awataka Polisi Kuwazuia Chadema Kulinda Kura
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakilindi kura kwani hilo si jukumu lao.


Polepole amesema hayo leo Februari 15, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mdogo wa Ubunge na nafasi za udiwani ambao unatarajia kufanyika Februari 17 2018 na kudai kuwa mpaka sasa wamepata taarifa kuwa CHADEMA wanachukua watu kutoka mikoani kuja kulinda kura kitu ambacho hakikubaliki.

"Zipo nyumba kadhaa hapa Dar es Salaam ambazo zimehifadhi watu wasio wakazi wametoka mikoa mbalimbali kuja hapa kwa kigezo cha kulinda kura, sisi hatufanyi siasa za matukio wala kutafuta kiki baada ya kujua hili tumewajulisha jeshi la polisi juu ya nyumba hizo na watu hao, kitakachofuata ni kushugulika na watu hao ambao hawapendi utaratibu mzuri na desturi yetu nzuri ya uchaguzi"

"Kura hazilindwi na watu wanaoletwa kwa makundi bali kura kwa mujibu wa Katiba, Sheria ya uchaguzi na kanuni mbalimbali za uchaguzi zimewekewa utaratibu wa kisheria kuhakikisha mwenye yake na anaipata hiyo, upo utaratibu wa mawakala kila chama kina wakala huyo ndiye atakayeshiriki kuhesabu, kujua hii kura yangu au si yangu sasa unapoanza kuandaa watu wasiojulikana na kuwaleta Dar es Salaam ni kuleta taharuki na mpango huo msingi wake ni kutisha wakina mama, vijana na wazee wasijitokeze kwenda kupiga kura, tumesema jeshi la polisi tafadhali tena tafadhali sana watu wasiohusika na usimamizi wa zoezi la uchaguzi ni sheria hawapaswi kuwepo wanatakiwa kuwepo kwenye maeneo yao wakafanye kazi zao za kujiletea kipato, uchaguzi haulindwi na mabaunsa, kura hailindwi bali dola ina vyombo vyake ambavyo sisi wote vyama vya siasa tumekubaliana" alisisitiza Polepole

Waliojiunganishia Bomba la Mafuta Waiomba Mahakama Iwapatie Dhamana

$
0
0
Waliojiunganishia Bomba la Mafuta Waiomba Mahakama Iwapatie Dhamana
Mfanyakazi Mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (TAZAMA) Samwel Nyakirang’ani (63) na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa kujiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iwapatie dhamana.

Maombi hayo wameyawasilishwa kupitia Wakili wao, Kusalika Augustine mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo alidai wateja wake wanahitaji kupata dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

Kutokana na maombi hayo, upande wa mashtaka uliomba kesi hiyo iahirishwe ili wajibu hoja hizo, ambapo Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi February 22, 2018.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Nyangi Mataro ambaye ni Mwalimu wa Shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Wengine ni mfanyabaishara, Farijia Ahmed, Malaki Mathia, Kristomsi Angelus, Pamfili Nkoronko na Hunry Fredrick.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali Bomba la Mafuta ya  Dizeli, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.

Hivi Hapa Vikosi vya Simba na Mwadui Vitakavyoumana Leo

$
0
0
Hivi Hapa Vikosi vya Simba na Mwadui Vitakavyoumana Leo
Ikiwa umebaki muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa Mwadui FC dhidi ya Simba katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, vikosi vya wachezaji wa timu zote mbili wamewekwa hadharani.

Kwa upande wa Mwadui wachezaji wao watakaoanza katika mchezo huo ni
Anold Massawe,
Revocatus,
David Luhende,
Joram Mgeveke,
Iddy Mfaume,
Awesu Awesu,
Jean-Marie Girukwishaka,
Paul Nonga,
Evarigestus Mjwahuki,
Miraji Athuman.

Wachezaji wa akiba ni
Denis Dionis,
Morice Malaki,
Yassin Salum,
Anthony Matogolo,
Athuman Rajabu,
Gerard Mathias,
Jackson Salvatory.

Wakati huo huo kikosi cha wachezaji wa Simba ni
Aishi Manula,
Shomari Kapombe,
Mohamed Hussein,
Juuko Murshid,
Yusuph Mlipili,
Erasto Nyoni,
Shiza Kichuya,
Said Ndemla,
Emmanuel Okwi,
John Bocco,
James Kotei.

Wachezaji wa akiba ni
Emmanuel Mseja,
Ally Shomary,
Laudit Mavugo,
Nicholas Gyan,
Mwinyi Kazimoto,
Mzamiru Yassin,
Paul Bukaba.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, Ajiuzulu Wadhifa Wake

$
0
0
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, Ajiuzulu Wadhifa Wake
WAZIRI Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, amejiuzulu wadhifa huo baada kuandika barua kwa chama chake cha Ethiopia People’s Democratic Front akiomba kung’atuka, licha ya chama hicho kutobainisha iwapo kimekubali uamuzi wake au la.


Desalegn amesema kuwa amejiuzulu ili kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo. Wananchi, wakereketwa wa Ethiopia People’s Revolutionary Democratic Front na serikali inataka kupata ufanisi wa mabadiliko yaliyowekwa wakati  wa mgogoro wa kisiasa nchini humo. Wengi wamepoteza maisha, wengine makazi huku mali zao zikiharibiwa.

“Ili kupata suluhu na ufanisi wa mabadiliko yaliyowekwa, na suluhu tuliyoweka,  nimewasilisha barua ya kujizulu majukumu yangu katika serikali na katika chama kwa hiari yangu,” alisema katika runinga ya taifa ya EBCTV.

Viongozi wa Chadema Wavamia Ofisi za Tume ya Uchaguzi Kudai Viapo vya Mawakala Wao

$
0
0
Viongozi wa Chadema Wavamia Ofisi za Tume ya Uchaguzi Kudai Viapo vya Mawakala Wao
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wamekwenda makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kudai viapo vya mawakala wa chama hicho katika uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni.

Baada ya kufika katika ofisi hizo leo Februari 15, 2018 saa 6:30 mchana, Mbowe na viongozi hao wamekwenda moja kwa moja katika ofisi za Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima.

Awali Mbowe amewaeleza waandishi wa habari waliopo katika ofisi hizo kuwa licha ya kumpigia simu ya mkononi Kailima hampati, baadaye kubainisha kuwa ameelezwa na mkurugenzi huyo kuhorodhesha madai yao na kumpa taarifa.

“Tumekubaliana naye katika hilo na nimewaita wabunge tumeingia kwenye chumba maalum hapa NEC ili kuoroshesha madai yetu,” amesema.

Amesema baada ya kuorodhesha watawasiliana na Kailima na kwamba amewaahidi kuyatafutia ufumbuzi malalamiko yao leo.

Februari 10, 2018 Chadema na CUF vilidai kuwepo kwa njama jimbo la Kinondoni baada ya mawakala wao kulazimishwa kula kiapo bila kukabidhiwa viapo vyao.

Madai hayo yalitolewa na mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kinondoni, Waziri Muhuzi na mkurugenzi wa habari, uenezi na uhusiano wa umma wa CUF, Abdul Kambaya, kubainisha kuwa endapo viapo havitatolewa katika muda muafaka mawakala wao wanaweza kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kusimamia kura za ubunge na udiwani.

Hoja tano za Chadema dhidi ya Nec

Mbowe amesema malalamiko ya Chadema kwa NEC ni; Mosi, mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni kukataa kuwaapisha mawakala wa ziada, kwamba vituo vipo 613 na amewaapisha mawakala 613.

Pili, ni Kailima kukataa wabunge na madiwani wa Chadema kuwa mawakala; tatu, Kailima kuja na sharti jipya kutaka mawakala wote wawe na vitambulisho; nne, kutotolewa kwa hati za viapo kwa mawakala hadi sasa; tano,  kituo cha majumuisho ya kura hakifahamiki.

Mwenyekiti ANC Cyril Ramaphosa Amepishwa Kuwa Rais wa Afrika Kusini

$
0
0
Mwenyekiti ANC Cyril Ramaphosa Amepishwa Kuwa Rais wa Afrika Kusini
Mwenyekiti wa chama tawala cha ANC Cyril Ramaphosa amepishwa kuwa rais wa Afrika Kusini baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu.

Rais huyo mpya alikuwa mtu wa pekee aliyeteuliwa siku ya Alhamisi huku uteuzi huo ukiungwa mkono kwa shangwe bungeni.

Bwana Zuma alikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa chama chake cha ANC kilichomtaka ajiuzulu la sivyo akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani dhidi yake bungeni.

Katika taarifa ya runinga, alisema kuwa anajiuzulu mara moja lakini hakubaliani na uamuzi wa chama.

Bwana Zuma anakabiliwa na madai kadhaa ya ufisadi lakini amekana kufanya makosa yoyote.

Akiwa naibu wa rais Ramaphosa anakuwa kaimu wa rais mara moja baada ya Zuma kujiuzulu.

Taarifa ya serikali inasema kuwa bunge litamchagua rais mpya wa Afrika Kusini Alhamisi jioni.

Bwana Zuma ,mwanachama wa jeshi la ANC wakati wa ubaguzi wa rangi, alipitia nyadhfa kadhaa za chama hicho hadi kuwa rais.

Cyril Ramaphosa na Jacob Zuma
Image caption
Cyril Ramaphosa na Jacob Zuma
Aliliongoza taifa hilo kwa muda mrefu baada ya ubaguzi wa rangi.

Lakini anaachilia madaraka akikabiliwa na kashfa kadhaa huku uchumi wa Afrika kusini ukiwa katika hali mbaya.

Siku ya Jumatano, maafisa wa polisi walivamia nyumba ya Johanesburg ya familia ya Gupta iliokuwa na ushawishi mkubwa serikalini.

Familia hiyo imeshutumiwa kwa kutumia urafiki wao wa karibu na rais Zuma kujilimbikizia ushawishi mkubwa wa kisiasa .

Hatahivyo familia hiyo imekana hayo.

Nini kinafanyika sasa?
Kwa mujibu wa katiba , iwapo kutatokea pengo katika wadhifa wa rais, aliyeko chini ya wadhifa huo anakaimu urais:

Kama naibu rais, na pia mwenyekiti wa chama tawala ANC. Bwana Ramaphosa ndiye anayepokea wadhifa huo.

Licha ya taarifa za awali kwamba angependa kuchukuwa muda uliosalia kujitayarisha kwa uchaguzi wa mwakani, akiwa ndiye kaimu rais hivi sasa, anatarajiwa kuapishwa rasmi kama rais na bunge.

Nini hatma ya ANC?
Chama cha ANC kimeshinda kila uchaguzi Afrika kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mnamo 1994.

Kwa raia wengi wa Afrika kusini ndiyo chama kilichowaletea uhuru dhidi ya uovu na utawala uliogubikwa na ubaguzi wa rangi, na hili sio jambo linaloweza kusahaulika kwa urahisi.

Lakini umaarufu wake umekuwa ukififia , na kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa kweli kwamba huenda chama hicho kikapoteza uongozi - hususan iwapo upinzani utaunga muungano.

ANC kilipata pigo la aibu katika uchaguzi wa serikali za kieneo mnamo 2016.

Licha ya kwamba kilipata kura zaidi dhidi ya vyama vingine, kilipoteza miji mikubwa ukiwemo mji mkuu kibiashara wa Johannesburg na Pretoria.

Wakati hapana shaka kwamba maisha ya raia wengi nchini yameimarika, wengi wanahisi yaliobadilika hayajatosha chini ya utawala wa chama hicho cha ANC.

Wajumbe wa ANC huchaguliwa kutoka matawi mbali mbali kote nchini
Afrika kusini bado ni mojawapo wa mataifa yasio na usawa duniani na zaidi ya nusu ya idadi ya watu wanaoishi nchini humo wanaishi katika umaskini.

Tuhuma za rushwa katika serikali ya ANC zimeongeza chumvi kwa hisia iliopo kwamba kundi fulani la matajiri walio na uhusiano na wanasiasa wanafaidi huku raia wa kawaida wakiteseka.

Pia kuna hisia miongoni mwa Waafrika weusi nchini kwamba ngazi ya uongozi iliyoundwa chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi bado ikaliko.

Ugavi mpya wa ardhi iliyonyakuliwa kutoka kwa mtu mweusi wakati wa utawala wa kibepari unachukua muda mrefu mno kutekelezwa.


Chama cha ANC kimeahidi kushinikiza ugavi huo wa ardhi - kiasi cha kuahidi kuibadili katiba kuruhusu kuichukuwa ardhi iliyokuwa imenyakulia, bila ya wamiliki wa sasa kulipwa fidia.

Na kimeidhinisha sera ya "mageuzi makali ya kiuchmi" - inayonuia kurudisha uongozi wa kiuchumi mikononi mwa iadi kubwa ya watu weusi nchini.

Lakini iwapo kinataka kuendelea kushikilia sifa na imani ya uwekezaji, tchama hicho pia kinahitaji kuwashawishi wafanya biashara kwamba Afrika kusini haitofuata mkonodo iliyoufuta Zimbabwe.

Kusawazisha maslahi ya wapiga kura dhid ya wafanyabiashara na huenda uchumi ukaishia kuwa changamoto kubwa kwa chama cha ANC huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa mwakani 2019.

Makonda Apata Tena Msaada wa Majengo Matano ya Walimu

$
0
0
Makonda Apata Tena Msaada wa Majengo Matano ya Walimu
Ubalozi wa China nchini Tanzania umemzawadia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda majengo matano ya kisasa kwaajili ya ofisi za walimu baada ya kupeleka ombi la kuhitaji msaada wa kuboresha mazingira ya walimu.


Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke amesema kwa miezi mitatu aliyoishi hapa nchini tangu alipoteuliwa kuwa balozi ameshuhudia maendeleo makubwa na serikali ya mkoa hivyo wameona wasikae kimya kwenye jambo linalolenga kuleta ukombozi wa uchumi kupitia elimu.

Majengo hayo ambayo  yatajengwa kwenye wilaya tano za mkoa wa Dar es salaam ambapo leo Mh. Makonda ameweka jiwe la msingi pamoja na kukabidhi Ramani ya jengo kuashiria kuanza kwa ujenzi huo kwenye shule ya sekondari Makumbusho.



Akiushukuru Ubalozi huo, Makonda amesemaujenzi wa majengo hayo kwa kiasi kikubwa unaenda kupunguza mateso ya walimu kufanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kufanya kazi kwenye madarasa.

Amesema dhamira yake ni kuboresha mazingira ya walimu ni kuwawezesha kutoa elimu bora itakayowezesha Taifa kuwa na wataalamu wa kutosha.

Majengo hayo yanatarajiwa kuwa na na Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi, Ofisi ya walimu wote, ukumbi wa mikutano, chumba cha kuhifadhi mitihani, vifaa vya michezo, chumba cha muhasibu, chumba cha kubadili nguo, mapokezi, vyoo, bafu ikiwa na samani za kutosha.

Yanga Yafunguka Kuhusu Mlinda Mlango Wao

$
0
0
Yanga Yakanusha Kuhusu Kusajiliwa kwa Mlinda Mlango Wao
Timu ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Meneja wake Hafidh Saleh amefunguka na kudai si kweli jina la mlinda mlango namba moja wa timu hiyo, Youthe Rostand halijasajiliwa CAF kama baadhi ya watu wanavyodai.


Saleh ametoa kauli hiyo leo kupitia moja ya mtandao wa kijamii wa wanajangawani baada ya kuenea uvumbi wa muda mrefu kuwa mlinda mlango huyo hatoweza kucheza mashindano ya kimataifa kutokana na kutosajiliwa katikan Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

"Huo ni uzushi tu usiokuwa na maana, jina la golikipa Youthe Rostand limetumwa CAF na leseni yake ya kucheza mashindano ya kimataifa tunayo. Hivyo siyo kweli kwamba jina lake halikutumwa kama wanavyodai. Kuhusu kucheza au kutocheza mchezo inategemea na benchi la ufundi jinsi walivyopanga kulingana na mchezo husika", amesema Saleh.

Kwa upande mwingine, kikosi cha Yanga kipo katika mapumziko mafupi siku ya leo na kesho (Ijumaa) kikosi hicho kinatarajiwa kuendelea na mazoezi ikiwa ni matayarisho ya kuelekea katika mpambano wao wa marudio dhidi ya St Louis ya Shelisheli.

Mwamuzi Jonesia Rukyaa Ameteuliwa Kuchezesha Michuano ya Algarve Nchini Ureno

$
0
0
Mwamuzi Jonesia Rukyaa Ameteuliwa Kuchezesha Michuano ya Algarve Nchini Ureno
Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limesema kuwa mwamuzi wa kike nchini mwenye beji ya Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA), Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuchezesha mchezo wa michuano ya Algarve kwa mwaka huu nchini Ureno zitakazo anaza Februari 28.

“Mwamuzi wa kike kutoka Tanzania mwenye beji ya FIFA Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuchezesha mechi za Algarve Cup 2018 nchini Ureno zitakazoanza Feb 28 hadi Machi 07, 2018.”

Michuano hiyo yaAlgarve ni michuano inayoshirikisha timu za wanawake ambayo itaanza kutimua vumbi mwezi huu wa Februari na kumalizika Machi 7 mwaka huu.

Jumla ya timu 12 zimealikwa katika michuano hii ambapo zitagawanyika katika makundi matatu wakati mataifa ya takayoshiriki ni.



Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images