Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Sadifa: Sikuwa na Kosa Ila Namuachia Mungu

0
0
Sadifa: Sikuwa na Kosa Ila Namuachia Mungu
Wakati mahakama ikimuachia baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kueleza kuwa haina nia ya kuendelea na kesi, aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Juma Hamis amesema anajua hakuwa na kosa ila anamuachia Mungu.

Sadifa alitoa kauli hiyo jana baada ya kuachiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma baada ya mashtaka kuwasilisha maombi ya kuifuta kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana.

Wakili wa Takukuru, Biswaro Biswaro aliwasilisha maombi ya kuifuta kesi hiyo kwa hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo, Joseph Fovo.

Biswaro alisema kesi hiyo jana ilitakiwa kutajwa lakini wamewasilisha maombi ya kuifuta chini ya kifungu cha 68(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Fovo alisema mahakama inakubaliana na maombi hayo na inaondoa kesi hiyo.

Alisema mshtakiwa atakuwa huru kwa sasa na kuwa uamuzi huo hautazuia kukamatwa tena kwa kosa hilo kama upande wa Jamhuri utaona kuna sababu ya kufanya hivyo.

Akizungumza nje ya Mahakama, Sadifa ambaye alikuwa anatetewa na wakili Godfrey Wasonga, alisema: “Uamuzi ya Mahakama kwangu naona ni sahihi na mimi naona sina hatia kwa sababu sina kosa lolote, kubwa zaidi ninaloweza kusema ni kumuachia Mungu.”

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge (CCM, alisema binafsi amesoma sheria kwa kiasi kikubwa alijua hakuwa na kosa na kuhoji: “Mtu akija nyumbani kwako kwa utamaduni wa Kitanzania akinywa soda ni kosa?”

Desemba 11 mwaka jana Sadifa alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa na makosa mawili ya utoaji wa rushwa.

Mbunge huyo alidaiwa kutenda makosa hayo Desemba 9 mwaka huu katika makazi yake kata ya Mnada mjini Dodoma akiwa kama Mwenyekiti wa Taifa UVCCM na mwajiri wa umoja huo   

Wakili Ataka Kortini Kuelezwa Maendeleo Kesi Mke wa Bilionea Msuya

0
0
Wakili Ataka Kortini Kuelezwa Maendeleo Kesi Mke wa Bilionea Msuya
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, ameutaka upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), kuieleza mahakama hatua waliyofikia kuhusiana na upelelezi wa shauri hilo.

Mbali na Mriti, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, Revocatus Muyela (40) ambao wote wanakabiliwa na shtaka mmoja la mauaji ya dada yake bilionea Msuya, Aneth Msuya.

Kibatala alidai hayo jana mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa Serikali, Patrick Mwita kudai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi unaendelea.

Awali, wakili Mwita alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kufuatilia jalada kama limeshatoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Kutokana na maelezo ya pande zote, hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 21, huku akiutaka upande wa mashtaka watakapokuja kueleza hatua waliyofikia katika kesi hiyo.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji, wanadaiwa kumuua Aneth.

Hata hivyo, Februari 23, 2017 washtakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa shtaka moja la mauaji upya.

Katika kesi hiyo namba 5/2017, wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam

Polepole: Wapinzani Kuweni na Uvumilivu Kushindwa ndo Kawaida Yenu

0
0
Polepole: Wapinzani Kuweni na Uvumilivu Kushindwa ndo Kawaida Yenu

Ikiwa imebakia siku moja kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa marudio, Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amevitaka vyama vya upinzani viwe na uvumilivu kwa kuwa kushindwa ni kawaida yao katika chaguzi.

Polepole ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mdogo wa marudio wa Ubunge na nafasi za udiwani ambao unatarajia kufanyika (kesho) Februari 17. 2018 na kudai sababu kubwa za upinzani kushindwa ni kutokana na wao kuwa wabinafsi.

"Napenda ifahamike kwa herufi kubwa, ni kawaida ya CCM kushinda na tunashinda kwa sababu tumefanya kazi nzuri ya kushughulika na shida za watu na watu wameona, wanatupenda, wanatuheshimu, wanatuthamini na wakati wote wanatupa kura nyingi za kishindo", amesema Polepole.

Pamoja na hayo, Polepole ameendelea kwa kusema "nitoe rai kwa vyama vya upinzani kuwa na uvumilivu kwa sababu ni kawaida yao kushindwa, kutokana na wao hawashughuliki na shida za watu, wamekuwa wabinafsi wanajitizama wao wenyewe, wamekuwa wapinga maendeleo kwa kila jambo jema linalofanywa. Rai yangu unaposhindwa kuwa na uvumilivu".

Kwa upande mwingine, Polepole amesema vyama vya upinzani ni kawaida yao mara zote kupinga ustawi wa watanzania pamoja na kuwa wapingaji wa maendeleo jambo ambalo ndio linawafanya kutoaminika kwa jamii kuwapa kura za ushindi.

Nigeria Yapiga Hatua Yazindua Ndege Isiyo na Rubani

0
0
Nigeria Yapiga Hatua Yazindua Ndege Isiyo na Rubani
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza kutengenezwa nchini humo.

Kifaa hicho kilichotengenezwa na Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na wapiganaji pamoja na majambazi.

Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi nyingine.

Nigeria imekuwa ikikabiliwa na kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo

Baada ya Kuapishwa Kuwa Balozi wa Sweden Dk.Slaa Amwahidi Kutomwangusha Rais Magufuli

0
0
Baada ya Kuapishwa Kuwa Balozi wa Sweden Dk.Slaa Amwahidi  Kutomwangusha Rais Magufuli
IKIWA ni dakika chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuwaapisha Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden na Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Slaa amefunguka kuwa hatomuangusha Rais na badala yake atajituma kwa nguvu zake zote kulitumikia taifa kwa manufaa ya nchi.

“Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu, pia nikushukuru Rais Magufuli kwa kunichagua kulitumikia Taifa, wewe unafahamu vigezo ulivyotumia kuniteua.

“Ninakuahidi nitafanya kazi yangu kwa moyo wangu wote, akili yangu yote na kwa nguvu zangu zote ili kujenga uchumi wa kati wa nchi yetu, Mwenyezi Mungu akinisaidia pia nikishirikiana na timu ya wote. Mimi katika siasa zangu sijawahi kutoa ahadi, lakini leo naweza kusema tu kwamba sitokuangusha,” alisema Dkt. Slaa.

Masogange Asimulia Mahakama Tukio Zima Namna Alivyokamatwa na Polisi

0
0
Masogange Asimulia Mahakama Tukio Zima Namna Alivyokamatwa na Polisi
Msanii Agnes Gerald maarufu Masogange anayekabiliwa na kutumia kutumia dawa za kulevya amesimulia tukio zima namna alivyokamatwa, huku Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikipanga Februari 21 kutoa hukumu.

Akiongozwa na mawakili Nehemiah Nkoko na Ruben Simwanza kutoa utetezi wake jana, Masogange aliiomba mahakama hiyo imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote.

Masogange anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi wake alidai kuwa hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja. Aliiambia mahakama kuwa mbali ya usanii, alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo. Alieleza kuwa Februari 14, 2017 polisi walikwenda nyumbani kwake bila yeye kuwapo kwa sababu alikuwa amempeleka mjomba wake duka la Ocadeco kununua vitu, hivyo walimkuta dada yake.

Aliongeza kuwa polisi hao walimweka dada yake chini ya ulinzi na kumtaka ampigie simu na kujifanye anaumwa ili arudi nyumbani, hivyo alitii amri na baada ya kumjulisha hivyo alimuahidi kuwa atarejea nyumbani punde lakini alirudi saa 12:00 jioni.

Aliendelea kuwa alipofika nyumbani kwake getini kabla hajashuka kwenye gari, alimuona mlinzi amekaa na watu wanne, aliwasalimia na kuingia ndani lakini ilipoingia ndani alimkuta dada yake, askari wa kike na wengine wawili wa kiume, walijitambulisha kwake na kumweleza kuwa wanamsubiri.

Masogange alidai aliwauliza shida yao na walimjibu kuwa wamekwenda kufanya upekuzi, lakini hawajapata kitu chochote.

Baada ya upekuzi huo, walimpeleka Kituo Kikuu cha Polisi na walipofika mapokezi akaandikisha jina na wakampeleka rumande ambako alikaa siku tisa.

Aliongeza kuwa baada ya kukamatwa Februari 14,2017, siku iliyofuatia akiwa polisi alipelekwa ofisi iliyokuwa na watu 15 ambako kwa nyakati tofauti alikuwa wakimuuliza maswali.

Baada ya kufunga ushahidi wake, hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri alisema atatoa hukumu Februari 21.   

Waziri Kigwangalla Ajibu Hoja ya Mange Kimambi

0
0
Waziri Kigwangalla Ajibu Hoja ya Mange Kimambi
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kujibu hoja ambayo Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, Mange aliibua kwenye mtandao wake Instagram kudai Waziri huyo ameshiriki kuwaingiza chaka Watanzania ili watapeliwe pesa


Waziri Kigwangalla akijibu hoja hiyo amesema kwamba yeye alialikwa kama mgeni wa heshima na kuwa alikuwa hawatambui watu hao binafsi na wala biashara yao alikuwa haitambui na alipoitwa kuzindua tawi lao hapa nchini alishindwa kuwakatalia ila hana maslahi binafsi katika kampuni hiyo. 

"Nimeona nitoe ufafanuzi kwenye hili jambo. Maana kila mjadala juu ya hii kampuni ya ..... unapoibuka, jina langu linakuja, na mara nyingine picha yangu inawekwa. Ukweli ni kwamba, nilialikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wake kama mgeni wa heshima; mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa wakati huo, Dr. Adelhelm Meru. Niliamini kwa heshima ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ambao ndiyo wenye dhamana ya usajili wa biashara zote nchini, ni lazima ni watu halali na bado ninaamini kama kuna shida mamlaka husika zitachunguza na kuchukua hatua stahiki na kama hakuna shida basi ni vema mamlaka husika zikatoa mwongozo utakaowaondoa hofu wananchi wenzetu wenye ‘interest’ ya kushiriki kwenye biashara hii"

"Baada ya kufika eneo la tukio, kiitifaki ikaonekana nami lazima nishiriki zoezi, nikashindwa kukataa. Nadhani inafahamika kwamba nimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kwa vitendo jitihada nyingi mbalimbali za wajasiriamali vijana ambao wameamua kutoka #NjeYaBox. Hata hawa nilishindwa kuwakatalia. Ukweli ni kuwa, siwajui wao binafsi ‘at personal’ level na wala biashara yao, umiliki wake na muundo wake siujui zaidi ya kuelewa kwa juu juu kuwa ni ‘network marketing’. Ifahamike hapa kuwa sina maslahi yoyote yale kwenye biashara hii na wala sikushiriki uzinduzi wake kwa malengo ya kutoa ushawishi ili watu wajiunge, na natoa rai kwamba wanaotaka kujiunga ama kuacha kujiunga wasitumie picha za ushiriki wangu siku ya uzinduzi, kwa namna yoyote ile, kujenga uhalali wa aina yoyote ile, bali watumie vipimo vyao vingine kufanya uamuzi na siyo picha zangu" alisema Kigwangalla

Mbali na hilo Waziri Kigwangalla aliwaonya watu mbalimbali na Taasisi ambazo zimekuwa zikitumia picha yake hiyo kwa lengo la kuhamasisha watu kushiriki katika biashara hiyo na kusema hatahusika na matokeo yoyote yale na kuwa akibaini kuna mtu au Taasisi inafanya hivyo atachukua hatua za kisheria.

"Sintohusika na matokeo yoyote yale, chanya ama hasi, ya ushiriki wa mtu yeyote yule ama taasisi yoyote ile, kwenye shughuli za kampuni hii. Naomba pia izingatiwe kwamba, jina langu ama picha yangu haijaruhusiwa kutumika kama bango la matangazo ya biashara ya mtu au taasisi yoyote ile, na hivyo kufanya hivyo ni kosa kisheria na ikibainika nitachukua hatua kali za kisheria" alisisitiza

Rosa Ree Afunguka Kuhusu Nyimbo Zake za You Tube Zilivyofutwa na The Industry

0
0
Rosa Ree Afunguka Kuhusu Nyimbo Zake za You Tube Zilivyofutwa na The Industry
Rapper Rosa Ree amefunguka ishu ya ngoma zake za awali kutopatikana katika official channel YouTube kama ilivyokuwa awali.

Kipindi msanii huyo yupo chini ya label ya The Industry ngoma zake kama One Time, Up In The Air zilipatikana katika channel ya YouTube ya label hiyo lakini tangu aondoke The Industry channel hiyo imefutwa.

Rosa Ree ameimbia Bongo5 ni kitu ambacho anakifahamu toka mwanzo ila hajaamua kukipa nafasi kwa sasa katika muziki wake bali ameamua kujikita katika kutengeneza kazi nyingine mpya na zenye ubora.

“Sijakaa kuwaza hicho kitu kwa sababu kipaji ni kitu ambacho kipo, ni creativity na nina uwezo mkubwa, hizo zilishapita nimefungua channel yangu mpya nina focus for the future.” amesema Rosa Ree.

Pia ameongeza kuwa The Industry wana haki zote kufanya hivyo kwani nyimbo hizo wao ndio wanazimiliki kisheria. Rosa Ree kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Marathon’.

The Industry ni label ambayo ipo chini ya kundi la Navy Kenzo, Label hii ilianza rasmi May, 2016 ikiwa na wasanii watatu, Wildad, Selina na Rosa Ree ila wote hawapo hapo kwa sasa.

Habari Njema kwa Wanaopenda Muonekano Mzuri, Dawa za Asili Zisizo na Kemikali

0
0

WEKA MUONEKANO WAKO VIZUR SASA, NIWAUZA WA PRODUCT ZA ASILI NA MAFUTA YASIO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI KWA MATUMIZI NA MATOKEO NI KWAARAKA KUANZIA WEEK (2) HADI (4)🍌🍍🥑

1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _100,000/
2) KUREFUSH NYWELE KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA 100,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO KUWA NA UMBO ZURI (HIPS & BATKS)KUNADAWA AINA TATU (@)KUPAK 100,000/(B) KUNYWA (C)VIDONGE_130,000/
4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, KIUNONI KUPAK _100,000/
5)TOA KITAMBI KABISA(@) KUPAK 10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING MAJAN 130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE
@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _90,000/
8) PIA UNA KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_90,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_80,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_80,000/
13) KUWA MWEUPE WAKUPENDEZA(@) VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU VINYWELEO MWILINI _100,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME (@)JELI AINAZOTE 100,000/(B)VIDONGE MAX MAN NA AINA NYINGI_ 100,000/
16) ENGEZA MAUMBIL YA KIUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_130,000/
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUFIKA KILELE_100,000/
18) RUDISH(BIKRA) 100,000/
19)ONDOA MAFUTA USONI _90,000/
20) ONDOA MIKUNJO USON_80,000/(21) ENGEZA MGUU_100,000/ 21) TUDISH NYELE KWENYE KIPARA 150,000/ 22) DAW YA NGIRI YAKUVIMBA NA KULEGEA 100,000/🍍🍉🥑

TUNAPATIKAN DAR E SALAAM:PIA NJE YA NCHI TUNATUMA MIZIGO,NA KWA MIKOAN KOTE UTAPATA *KESSY* NI WAAMINIFU WA KUTUM MIZIGO NA KUFIKA KWA WAKATI PIGA CM (+255) 0719955528
0756259180
0785371237
@ *Pendeza_kessy_product*
Delivery POPOTE ULIPO,

Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela kwa Kulawiti Mtoto wa Miaka Mitatu

0
0
Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela kwa Kulawiti Mtoto wa Miaka Mitatu
Mahakama ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imemhukumu kifungo cha maisha jela, Frank Mlyuka (24) baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti  mtoto wa kike wa miaka mitatu.

Mbali na hukumu hiyo, Mlyuka ametakiwa kulipa Sh5milioni kama fidia kwa wazazi wa mtoto huyo.

Akisoma hukumu hiyo juzi Februari 14, 2018 Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Hussein Marengu amesema Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha kuwa Mlyuka alitenda makosa hayo na mwenyewe kukiri mbele ya Mahakama.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Nashoni Simon amesema mshtakiwa alitenda makosa hayo Februari 9, 2018 katika Kijiji cha Kihesa Mgagao wilayani Kilolo.

Kwa mujibu wa mwendesha mashataka huyo, siku hiyo mshtakiwa alipita nyumbani kwa mama mkubwa wa mtoto huyo, Jestina Lubiba na kumkuta mtoto huyo akicheza na wenzake.

Amesema mshtakiwa alimwita mtoto huyo ndani na kumwingiza jikoni ambapo alimbaka na kumlawiti, kumsababishia maumivu makali na kwamba baada ya tukio hilo aliondoka.

Amesema mtoto huyo baada ya kufanyiwa kitendo hicho alitoa taarifa kwa mama yake mkubwa, ambapo msako ulianza na mshtakiwa huyo kukamatwa huku mtoto huyo akipelekwa zahanati ya Pomerini, baadaye kuhamishiwa

Hospitali ya Rufaa Iringa alikolazwa kwa siku moja.

Hakimu Marengu ameeleza kuwa miongoni mwa vielelezo vinavyothibitisha kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo ya kubaka na kulawiti ni hati ya maelezo ya mshtakiwa mbele ya walinzi wa amani na taarifa ya daktari.

Alipotakiwa kujitetea, Myuka anayeishi na wazazi wake amesema ametenda kosa hilo akiwa amelewa na hana cha kujitetea.

Wakati huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah amekiri kuongezeka matukio ya ubakaji wilayani humo na kubainisha kuwa wastani wa watoto wanne hubakwa kila mwezi.

Rayvan Aweka Wazi Mkwanja Wa WCB Wanaolipwa na Diamond

0
0
Rayvan Aweka Wazi Mkwanja Wa WCB Wanaolipwa na Diamond
MSANII anayefanya poa kutoka Crew ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Rayvan ametumia muda wake kukaa chini na Global Entertainment na kuelezea utaratibu mzima unaotumiwa na bosi wao Diamond Platnumz kuwalipa mishahara na posho kadhaa zinazotokana na shoo ambazo wamekuwa wakizifanya.
Akizungumza na Global Entertainment, alisema kuwa Crew hiyo imekuwa ikilipwa vizuri mishahara huku ikiwataka wasanii wake kuingiza kiasi flani cha fedha wanazopata katika shoo zao kwenye mfuko wa kampuni tofauti na bosi wao Diamond ambaye hakatwi hata senti ya shoo.

“Kutokana na maisha mazuri ya WCB, ndiyo maana utaona siku hizi anaweza kuibuka msanii wake yoyote na kutoa ushuhuda juu ya kiasi cha fedha ya maisha anayoipata jambo ambalo baadhi yao wanaona kama majigambo lakini uhalisia unabaki kuwa kweli maisha ndani ya WCB siyo mambaya.

“Suala la Harmonize kusikika akisema ana fedha huo ulikuwa kama ushuhuda wake kwani kila mtu ananjia yake ya kushuhudia jambo ambalo anatendewa au alilokuwa akitendewa katika maisha yake ya nyuma au anayoendelea kuyaishi kwa sasa,” alisema Rayvan.

Waomba Sheria ya Kupimwa Ukimwi kwa Lazima Itungwe

0
0
Waomba Sheria ya Kupimwa Ukimwi kwa Lazima Itungwe
Baraza la watu watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Katika halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe wameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kutunga Sheria itakayopelekea watu kupima Ukimwi kwa lazima.


Hayo yamesemwa na watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Konga ya Mbozi wakati walipotembelewa na Kamati ya Bunge ya Ukimwi ambayo ipo ziarani mkoani humo.

Wamesema  kuwa hatua hiyo itasaidia kwenye Mapambano ya Maambukizi na kuenea kwa ugonjwa huo ili kutimiza azma ya serikali ya 0.0.0 kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 hakuna Maambukizi Mapya ya Ukimwi.

Mmoja wa Waathirika hao Stephan Jonas alisema njia ya Mbadada ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni kuweka sheria ya kulazimisha kila kaya kupima ugonjwa huo.

"hili  suala inatakiwa liwe la lazima kwa sababu watu hawapimi, wanashindwa kujitambua hivyo wanaendelea kueneza kwa wengine sheria ikiwepo kila mtu apime kwa lazima itasaidia sana," alisema 

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge, Dr Jasmini Bunga alikubalina na Ombi hilo na kueleza kuwa litasaidia mkakati wa serikali wa kukabiliana na Maambukizi mapya ya Ukimwi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la JSI linashughulika na Mifumo ya maisha na Ustawi wa  Jamii Dr. Tulia Tuhuma alisema shirika lake litaendelea kufuatilia maendeleo ya Konga (Vikundi vya watu wanaoishi na Virusi vya ukimwi) pamoja na kusaidia utoaji wa huduma ya Ukimwi.

Wivu Wamtesa Linah Aamua Kumficha Mumewe Ili Asichukuliwe

0
0
Wivu Wamtesa Linah Aamua Kumficha Mumewe Ili Asichukuliwe
Mwanamuziki diva wa Bongo Fleva, Linah Sanga ' Ndege Mnana' ameweka wazi hofu yake juu ya kuibiwa baba wa mtoto wake na wadada wa mjini (nyakunyaku) ndiyo sababu ya kupunguza kasi ya kumuweka mtandaoni kama jinsi ilivyokuwa awali.


Linah ameweka wazi hofu yake hiyo mbele ya kamer za eNEWZ wakati akifafanua tetesi za kupigwa kibuti na mfanyabishara huyo (Shabani Mchovu)  ambaye wamefanikiwa kupata mtoto wa kike mwaka 2017.

Linah amesema kwamba yeye na Mchovu tayari wana takribani miaka miwili kwenye mahusiano na watu wengi wanafahamu kuwa ni wapenzi hivyo kumuanika mitandaoni ni kuzidi kuwatamanisha nyaku nyaku kumnyakua mpenzi wake ili kutaka kujua anakitu gani ambacho yeye anakipata kwa mpenzi wake huyo.



Aidha mwanamuziki huyo ambaye amerudi na ngoma mpya 'Same Boy' aliyomshirikisha Rachel Kizunguzungu amesema kwamba  "mchumba wangu ni mtu ambaye anaheshima katika ofisi yake, hivyo siiwezi kumuingiza kwenye drama za kitoto au kumweka wazi haswa kwenye mitandao  kwa kuwa nahofia kumshushia heshima yake lakini pia. Hayo ni mambo ya kitoto sana kuanika mapicha picha ukiwa na mpenzi wako".

Aidha ameweka sawa tetesi za kuchwa na kusema kwamba mapenzi na mpenzi wake hayajapungua wala hayajaisha na tangu wafanikiwe kupata

Mashine za Kielectroniki Pasua Kichwa Wafanyabiashala Walalamikia Wino Wake

0
0
Mashine za Kielectroniki Pasua Kichwa Wafanyabiashala Walalamikia Wino Wake
Baadhi ya wafanyabiashara jijini hapa wamedai wino unaotumika kutolea risiti kwenye mashine za kieletroniki za EFD haudumu muda mrefu, jambo linalowafanya kushindwa kutunza vizuri kumbukumbu za mauzo.

Kutokana na tatizo hilo, wanalazimika kuingia gharama nyingine ya kupiga kopi risiti za mauzo ili kuweka kumbukumbu zinazoweza kudumu kwa muda mrefu tofauti na zinazotoka moja kwa moja kwenye mashine hizo.

Mfanyabiashara kutoka Soko la Uyole, Regnet Sangwa alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapaswa kufanya uchunguzi ili kuja na suluhisho la wino unaotumika udumu kwa muda mrefu kwenye risiti hizo kabla ya kuzisambaza kwa wafanyabiashara.

“Maandishi ya risiti hizi yanafutika ndani ya muda mfupi sana, jambo linalofanya wengi wetu tushindwe kuweka kumbukumbu sahihi au tofauti na hapo inanilazimu niingie gharama nyingine kwenda kupiga kopi,” alisema Sangwa.

“Tunalazimika kufanya hivi kwa sababu muda mwingine wenzetu wa TRA wanakuja na kudai kumbukumbu za mauzo, sasa kama hukupiga kopi na zile original zinakuwa zimefutika maandishi ndio inakuwa shida, tunaambiwa tunakwepa kulipa kodi.”

Mfanyabiashara huyo alisema Serikali ilipaswa kufanya uchunguzi wa awali wa mashine hizo kabla ya kuwapelekea wafanyabishara na kwamba, zina upungufu mwingi ikiwamo kutokuwa na sehemu ya kuandika jina la mnunuzi, bali zinaandika jina la mmiliki wa biashara jambo ambalo linawapa wakati mgumu.

Mfanyabiashara mwingine, Riziki Sanga wa Uyole alisema mashine hizo zina masharti mengi katika matumizi na ni rahisi kuharibika.

Alisema mawakala wanaosambaza mashine hizo wamekuwa hawatoi elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara ya namna ya kuzitumia kwa ufanisi na kujikuta wanaziharibu mara kwa mara.

Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Charles Bajungu alisema tatizo la wino katika mashine hizo wanaliona kuwa ni changamoto kutokana na kutodumu kwa muda mrefu. Hata hivyo alisema wanalishughulikia.

“Kuna baadhi ya changamoto kwenye mashine hizo ikiwamo ya risiti kutokuwa na jina la mnunuzi pamoja na wino unaotumika kutodumu kwa muda ambao tulitarajia, lakini tunaendelea kuzifanyia marekebisho, muda si mrefu tatizo hilo litakuwa limepata ufumbuzi,” alisema.

Bajungu alisema baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa huo wana utamaduni wa kukwepa kulipa kodi kwa kisingizio kuwa elimu haitolewi ipasavyo.

Alisema wanafanya makosa kwa kwa kuwa elimu ya mlipakodi pamoja na matumizi ya mashine za EFD imekuwa ikitolewa mara kwa mara.

Alisema mawakala wanaohusika na usambazaji wa mashine hizo muda wote wako mitaani na wamekuwa wakitoa elimu juu ya matumizi yake kabla, hivyo si kweli kwamba hawawajibiki kutoa elimu ya matumizi sahihi.   

Rais Magufuli Awaapisha Dk.Slaa, Mboweto

0
0
Rais Magufuli Awaapisha Dk.Slaa, Mboweto
Leo Februari 16, 2018 Rais John Magufuli amewaapisha mabalozi wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nigeria na Sweden.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi inaeleza kuwa walioapishwa ni Muhidin Ally Mboweto ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Dk Willbrod Peter Slaa ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.

Uteuzi wa Mabalozi hao kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa umeanza jana Februaru 15, 2018.



Sare na Mwadui Yamtoa Povu Haji Manara

0
0
Sare na Mwadui Yamtoa Povu Haji Manara
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya klabu ya Simba Haji Manara amesema Simba sio timu ya kwanza kutoa sare au kufungwa na Mwadui hivyo mashabiki wasiongee sana.


Kupitia moja ya kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii Manara ameandika ujumbe ambao unaonekana kuwa povu kwa mashabiki wa wapinzani wao huku akiweka wazi kuwa sare ya jana dhidi ya Mwadui FC kamwe haijaitoa Simba kwenye njia.

''Simba haitatoka mstarini na washabiki wetu tulieni na wajibu wenu ni kuiombea timu na kuisuport'', ameandika Manara ikiwa ni chini ya siku moja tangu timu hiyo itoe sare ya 2-2 dhidi ya Mwadui ugenini Shinyanga.



Aidha Manara ameongeza ''Mwadui imezifunga Singida United na kabla yetu sisi waliwafunga Mtibwa 3-1 kule Shinyanga, wametoka sare na Yanga na Azam tena wakiwa kwao Dar, hizo ndio 'big five' kwenye ligi kwa sasa, sisi kutoka nao sare kwao 'why' iwe nongwa tena ugenini'', ?.

Baada ya sare ya jana Simba imefikisha alama 42 ikiwa kileleni kwa alama 5 zaidi ya Yanga ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 37 huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 34.

Masikini! Madeni Yasababisha Mtangazaji Maarufu wa TV Kuuza Figo Yake

0
0
Masikini! Madeni Yasababisha Mtangazaji Maarufu wa TV Kuuza Figo Yake
Ukiwa hauna pesa unaweza ukajiona wewe ndiye mtu mwenye matatizo pengine kuliko watu maarufu unaowaona kila siku kwenye runinga au kuwasikiliza redioni, lakini ukweli ni kwamba maisha hayapo hivyo kila mtu anachangamoto zake. Hii imedhihirishwa na mtangazaji nguli wa kituo cha Citizen TV, Swaleh Mdoe ambaye ametangaza kuuza figo yake moja ili aweze kulipa madeni yanayomkabili.

Swaleh Mdoe ambaye amejipatia umaarufu nchini Kenya kupitia kipindi cha ‘Tafakari na Babu’ cha Citizen TV kinachoruka kwa lugha ya kiswahili amesema anauza figo yake kwa shilingi milioni 1 za Kenya ambayo sawa na milioni 23 za kitanzania.

Msomaji huyo nguli wa taarifa ya habari ya Citizen TV leo Ijumaa Februari 16, 2018 akifanya mahojiano na kituo cha Radio cha Ghetto FM cha Jijini Nairobi nchini Kenya, amesema kuwa kwa sasa yupo katika mtikisiko wa kiuchumi kwani anadaiwa fedha nyingi ndiyo maana amechukua maamuzi hayo.

“Nimejitafakari kwa kina mimi na daktari wangu hadi kuchukua maamuzi ya kutangaza kuuza figo yangu moja, Kuna mambo hayapo sawa kiuchumi kwa upande wangu nataka niyamalize mwenyewe hivyo natangaza kuuza figo yangu kwa yeyote anayehitaji asisite kunitafuta kupitia 0722-733130. Nataka nifanye hili haraka na nitatoa matangazo mengine kwenye magazeti,“amesema Swaleh Mdoe.

Hata hivyo, amesema ingawaje ni mtu maarufu nchini Kenya hataki kutangaza michango watu wamchangie kwani anaona atawabunguzi watu ambao hawahusiki na madeni hayo.

“Sitaki kuwabughuzi watu wengine kwa sababu ya umaarufu wangu, nadhani figo moja inatosha kulipa madeni yangu yote na mwili wangu utakuwa na afya kama nilivyo sasa,“amesema Mdoe na kuwataka Wakenya wenye matatizo ya uhitaji wa figo wamtafute.

Maneno ya Zari Leo Baada ya Masaa Machache Kutangaza Kumuacha Diamond

0
0
Maneno ya Zari Leo Baada ya Masaa Machache Kutangaza Kumuacha Diamond
Baada ya kupita takribani kwa masaa 35 tangu Zari The Bosslady kutangaza kuachana na Diamond, mrembo huyo ameibuka na ujumbe mpya ambao unaonekana kama ametupa jiwe gizani.

Kupitia mtandao wa Instagram leo (Ijumaa), mrembo huyo amepost picha mbili zenye ujumbe tofauti. Katiaka picha ya kwanza hiyo hapo juu ambayo ameiweka kwenye mtandao huo, Zari ameandika, “Consistency is key #Mompreuer.”

Wakati huo huo kwenye picha nyingine malkia huyo ameandika, “Me when people ask what I do…. whatever it takes👌.”

Martini Kadinda Afunguka Kuhusu Ukaribu Wake na Wema Swpetu

0
0
Martini Kadinda Afunguka Kuhusu Ukaribu Wake na Wema Swpetu
Aliyekuwa meneja wa Wema Sepetu Martin Kadinda amefunguka ni kwanini kipindi hiki haonekani karibu sana na mrembo huyo kama ilivyokuwa awali.

Mbunifu huyo wa mavazi amesema si kwamba hayupo karibu na Wema ila kazi wanazofanya kwa sasa hazihitaji kusikika katika vyombo vya habari.

“Kuna wakati unafika inabidi ufanye vitu vingine sio kwamba sipo karibu naye lakini tume-focus kwenye vitu vingine zaidi ambavyo we think sio media inahitajika kuvijua sana but kidogo ambacho wanakipata ndio wanatakiwa kukipata,” amesema.

Marthin ameongeza kuwa Wema alikuwa anachukulia kawaida mambo yake ambayo hata yasingetakiwa kusikika katika vyombo vya habari lakini wamemueleza hilo halifai kwani vitu vingi havifanikiwa vikiwa kwenye media kila siku.

Ridhiwan Kikwete Awaasa Wakazi wa Kinondoni Kuhusu Mtulia

0
0
Ridhiwan Kikwete Awaasa Wakazi wa Kinondoni Kuhusu Mtulia
Mbunge wa Chalinze kupitia tiketi ya CCM, Ridhiwan Kikwete ni moja ya viongozi waliohudhuria kwenye kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni kumnadi Mgombea wa chama hicho, Maulid Mtulia na kuwaasa wananchi wa jimbo hilo kumchagua Maulid Mtulia.


Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa na Waziri wa Tamisemi ,Suleiman Jaffo

Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kinondoni wanapaswa kumchagua Mtulia kama kiongozi wao kwani yeye atakuwa daraja kati ya wananchi na Maendeleo.

“Kinondoni tunachagua (Maulid Mtulia) Daraja litakayeunganisha wananchi na Maendeleo, #hapakazitu,”ameandika Mhe. Ridhiwan Kikwete kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Marudio ya Uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Februari 17, 2018.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images