Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni

$
0
0
Dar es Salaam. Matokeo ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni yaliyobandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yanaonyesha mgombea wa CCM, Maulid Mtulia anazidi kuongoza katika baadhi ya vituo.

Katika matokeo hayo, Mtulia anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu huku wa CUF, Salum Rajab Juma akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo;

Kituo cha Mbuyuni 3 Kata ya Tandale
Mtulia amepata kura  53
Juma 3 na Mwalimu 18


Kituo cha Mashuka 2 Kata ya Tandale, 

Mwalimu amepata kura 16
Juma 7
Mtulia 53.


Kituo cha Mashuka 1 Kata ya Tandale 

Mtulia amepata kura 59
Mwalimu 14 
Juma 3.


Kituo cha Ofisi ya Mpakani -7 Kata ya Ndugumbi

Mtulia amepata kura 33
Mwalimu 20, Juma 6 
Mgombea wa Tadea 1


Kituo cha Mpakani -3 Kata ya Ndugumbi

Mtulia amepata kura 49
Mwalimu 14, Juma 16 
Mgombea wa Tadea 1


Kituo cha Serikali ya Mtaa Bwawani 4 Kata ya Kijitomyama 

Mtulia amepata kura 237
Mwalimu 21
Juma 1.


Kituo cha Bwawani 01 Kata ya Kijitonyama, 

Mwalimu amepata kura 23
Mtulia 100.


Kituo cha Bwawani 2 Kata ya Kijitonyama

Mtulia amepata kura 37
Mwalimu 24 
Juma 1


Kituo cha Weo 1 Kata ya Makumbusho

Mtulia amepata kura 35
Mwalimu 20
Juma 3


Kata ya Sokoni Makumbusho A-1 Kata ya Kijitonyama

Mtulia amepata kura 30
Mwalimu 12
Ashiri Saidi 1.


Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani B Kata ya Makumbusho,

Mwalimu amepata kura 13,
Mtulia kura 39 
Mgombea wa UMD 1.


Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani C 1 Kata ya Makumbusho

Mtulia amepata kura 41
Mwalimu 15
Juma 9


Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala C 2 Kata ya Makumbusho

Mtulia amepata kura 42
Mwalimu kura 21
Juma 15


Kituo cha Kijitonyama 2  Kata ya Kijitonyama

Mwalimu amepata kura 20
Mtulia 29 na Juma 1


Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama B2 Kata ya Kijitonyama

Mtulia amepata kura 78
Mwalimu kura 24
Ally Abdallah wa Tadea 1


Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama A-2 Kata ya Kijitonyama

Mwalimu amepata kura 24
Mtulia 68
Ally Abdallah wa Tadea 1


Kituo cha Shule ya Msingi Kisiwani D 2 Kata ya Makumbusho

Mtulia amepata kura 37
Mwalimu 21
Mgombea wa NRA 1


Kituo cha Shule ya Msingi Minazini C 1 Kata ya Makumbusho

Mtulia amepata kura 46
Mwalimu 20
Juma 12


Kituo cha Ofisi ya Serikali ya Mtaa Kijitonyama 2 Kata ya Kijitonyama

Mtulia amepata kura 25
Mwalimu kura 36


Kituo cha Ofisi ya Weo-3 Kata ya Kijitonyama

Mtulia amepata 22
Mwalimu 20


Kituo cha Mwenge Zahanati Kata ya Kijitonyama

Mtulia amepata 19
Mwalimu 12.


Kata ya Mwenge Zahanati 2 Kata ya Kijitonyama

Mtulia amepata kura 56
Mwalimu 13


Matokeo zaidi yataendelea kukujia hapahapa

Mtangazaji wa Citizen Tv, Swaleh Mdoe atangaza kuuza figo ili alipe madeni

$
0
0
Ukiwa hauna pesa unaweza ukajiona wewe ndiye mtu mwenye matatizo pengine kuliko watu maarufu unaowaona kila siku kwenye runinga au kuwasikiliza redioni, lakini ukweli ni kwamba maisha hayapo hivyo kila mtu anachangamoto zake. Hii imedhihirishwa na mtangazaji nguli wa kituo cha Citizen TV, Swaleh Mdoe ambaye ametangaza kuuza figo yake moja ili aweze kulipa madeni yanayomkabili.

Swaleh Mdoe ambaye amejipatia umaarufu nchini Kenya kupitia kipindi cha ‘Tafakari na Babu’ cha Citizen TV kinachoruka kwa lugha ya kiswahili amesema anauza figo yake kwa shilingi milioni 1 za Kenya ambayo sawa na milioni 23 za kitanzania.

Msomaji huyo nguli wa taarifa ya habari ya Citizen TV leo Ijumaa Februari 16, 2018 akifanya mahojiano na kituo cha Radio cha Ghetto FM cha Jijini Nairobi nchini Kenya, amesema kuwa kwa sasa yupo katika mtikisiko wa kiuchumi kwani anadaiwa fedha nyingi ndiyo maana amechukua maamuzi hayo.

“Nimejitafakari kwa kina mimi na daktari wangu hadi kuchukua maamuzi ya kutangaza kuuza figo yangu moja, Kuna mambo hayapo sawa kiuchumi kwa upande wangu nataka niyamalize mwenyewe hivyo natangaza kuuza figo yangu kwa yeyote anayehitaji asisite kunitafuta kupitia 0722-733130. Nataka nifanye hili haraka na nitatoa matangazo mengine kwenye magazeti,“amesema Swaleh Mdoe.

Hata hivyo, amesema ingawaje ni mtu maarufu nchini Kenya hataki kutangaza michango watu wamchangie kwani anaona atawabunguzi watu ambao hawahusiki na madeni hayo.

“Sitaki kuwabughuzi watu wengine kwa sababu ya umaarufu wangu, nadhani figo moja inatosha kulipa madeni yangu yote na mwili wangu utakuwa na afya kama nilivyo sasa,“amesema Mdoe na kuwataka Wakenya wenye matatizo ya uhitaji wa figo wamtafute.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA.

Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Hii Ndiyo Michepuko Iliyosababisha Diamond Kutoswa na Zari

$
0
0

Habari za Diamond na Zari kuachana bado zinatawala kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakiwa wameshtushwa kusikia kuwa couple iliyokuwa inapendwa na mashabiki zao imevinjika.

Huku sababu ya Zari kumwaga Diamond ikiwa ni wazi kabisa kuwa ni michepuko ambapo Zari ameweka wazi sababu juu iliyomfanya mpaka akafikia uamuzi wa kumuacha Baba watoto wake ni yeye kuzidisha kuchepuka.

Kwenye mahusiano yao yote kumekuwa na tetesi za Diamond kuwa na mahusiano na wanawake wengine, ingawa mara nyingi amekuwa akikataa na kudai ni uzushi lakini pia na Zari amekuwa akimsamehe na wawili hao huishia kurudiana.

Jambo hili lilimpelekea Zari kushindwa kuvumilia na kucharaza waraka katika mtandao wa instagram akieleza kuwa amechoshwa na tabia hiyo ya Diamond na anaachana nae ili kulinda heshima yake.

 UNDERSTAND THAT THIS IS VERY DIFFICULT FOR ME TO DO. THERE HAVE BEEN MULTIPLE RUMORS SOME WITH EVIDENCE FLOATING AROUND IN ALL SORTS OF MEDIA IN REGARDS TO DIAMOND’S CONSTANT CHEATING AND SADLY I HAVE DECIDED TO END MY RELATIONSHIP WITH DIAMOND, AS MY RESPECT, INTEGRITY, DIGNITY & WELL BEING CANNOT BE COMPROMISED. WE ARE SEPARATING AS PARTNERS BUT NOT AS PARENTS. THIS DOESN’T REDUCE ME AS A SELF-MADE INDIVIDUAL, AND AS A CARING MOTHER, AND THE BOSS LADY YOU HAVE ALL COME TO KNOW. I WILL CONTINUE TO BUILD AS A MOGUL, I WILL INSPIRE THE WORLD OF WOMEN TO BECOME BOSS LADIES TOO. I WILL TEACH MY FOUR SONS TO ALWAYS RESPECT WOMEN, AND TEACH MY DAUGHTER WHAT SELF-RESPECT MEANS. UNLIKE MANY, I’VE BEEN IN THE ENTERTAINMENT INDUSTRY FOR 12 YEARS, AND THROUGH ALL MY CHALLENGES I CAME OUT A VICTOR BECAUSE I AM A WINNER, AND SO ARE ALL OF YOU ZARI SUPPORTERS. HAPPY VALENTINE’S

A POST SHARED BY ZARI (@ZARITHEBOSSLADY) ON FEB 14, 2018 AT 10:17AM PST


Baadhi ya michepuko ambayo inasemekana kuchangia kuvunja uhusiano wa Diamond na Zari ni hawa hapa:

Hamisa Mobetto



Hamisa anatajwa kuharibu uhusiano wa Diamond na Zari tangu mwaka jana alipojitokeza na kukiri kuzaa naye, na kuanzia hapo mahusiano ya Diamond na Zari yakaanza kuyumba ingawa alimsamehe lakini bado kulikuwa kuna mpasuko tayari.

Irene/ Officiallyn



Irene na Diamond wametajwa kuwa na mahusiano kwa muda mrefu sana tangu alipotokea kwenye video ya kwetu ya Rayvanny kama video queen kumekuwa na tetesi kuwa walikuwa wote South Africa at the same time akiwa na Zari na familia.

Shady



Huyu ni mwanamitindo kutoka nchini Rwanda tetesi za Diamond kutoka na Shady zilianza kusikika alitoa za kusafiri na kuelekea nchini Rwanda lakini zilipamba moto alipoenda Rwanda mwezi uliopita baada ya picha wakiwa pamoja kusambaa mtandaoni.

Mia



Mwezi uliopita kuna video ilisambaa mtandaoni ambayo ilimuonyesha Mia akiwa Madale ambapo baadae ilikuja kuonekana kuwa alienda pale na dancer wa Diamond ambaye alikuwa na mahusiano naye jambo ambalo Mia alikuja kulikana na kusema alienda pale na Diamond ambaye aliishia kulala naye.

Tunda



Uhusiano wa Tunda na Diamond ulikamata sana headlines ambapo inasemekana amekuwa mchepuko wake wa siku nyingi sana video iliyowaonyesha wakiwa pamoja ilisambaa mwezi uliopita.

Wema Sepetu



Wema na Diamond walitengeneza headlines wiki chache zilizopita baada ya kuonekana wakikumbatiana na kubusiana hadharani kwenye party huku kukiwa kuna tetesi kuwa wamerudiana.

Aliyemrekodi Trafiki Akipokea Rushwa Atafutwa na Polisi

$
0
0

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linamsaka dereva aliyempa rushwa ya shilingi 5,000 askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye amefukuzwa kazi, kwa ajili ya kukamilisha upelelezi.

Katikati ya wiki, video fupi iliyokuwa ikionyesha askari huyo akipewa rushwa na dereva wa gari ndogo ilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusababisha Polisi kumchukulia hatua trafiki huyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, aliwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam “video ile” iliwashutua na walichukua hatua mara moja za kumfukuza kazi na sasa ni raia wa kawaida

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi Jumanne Murilo, alisema askari huyo alifukuzwa tangu Jumanne.

Kamanda Murilo alisema askari huyo hadi anafukuzwa kazi ndani ya Jeshi la Polisi alikuwa amefanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na nusu.

“Tukio hili lilifanyika eneo la Mwenge na baada ya kulibaini tulianza uchunguzi wetu ambao juzi (Jumanne) ulikamilika na kubaini tukio hilo lilikuwa la kweli (kwamba) amepokea rushwa. Hivyo tumemuondoa kazini,” alisema juzi Kamanda Murilo.

Kamanda Murilo ambaye hakumtaja jina askari huyo aliwakumbusha trafiki kuzingatia maadili ya kazi na taratibu za kijeshi zilizowekwa. Akirejea taarifa hizo, Mambosasa alisema upelelezi wa shauri hilo unaendelea hata hivyo.

“Kwa sasa upelelezi unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ambaye kwa sasa si askari tena,” alisema Kamanda Mambosasa.

“Lakini kama ambavyo sheria za rushwa zinavyoelekeza ni lazima tumpate na aliyehusika kutoa rushwa ili kupata ushahidi wa kesi hiyo,” alisema Mambosasa.

Alieleza zaidi kuwa ingawa wanamsaka mtuhumiwa huyo namba mbili, pia wanamshukuru kwa ushirikianao uliowezesha kupatikana kwa askari huyo na hatua kuchukuliwa dhidi yake.

“Badala ya raia kulalamika na kusema Jeshi la Polisi halifanyi kazi ni vyema mkatoa taarifa kama alivyotoa huyu aliyerekodi video, aliyewezesha kumnasa aliyekuwa askari wetu na tukambaini kweli na kosa la kuomba rushwa ya Sh. 5,000 wakati serikali inapambana na matukio kama hayo,” alisema.

Katika tukio hilo, dereva aliyeombwa rushwa alimrekodi askari huyo kupitia simu ya mkononi wakati akimpatia rushwa hiyo iliyowekwa chini ya leseni.

Vitendo vya kuwarekodi video trafiki wanaopokea rushwa vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara, ambapo Oktoba mwaka jana, Sajini Hamad Kassim wa Kituo cha Mkokotoni visiwani Zanzibar, alionekana akipokea rushwa ya Sh. 10,000.

Rushwa hiyo aliiomba kutoka kwa raia wa kigeni baada ya kumkamata akiwa hajafunga mkanda wakati akiendesha gari.

Aidha, mwaka 2015 aliyekuwa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo Anthon Temu, mwenye namba F785 alifukuzwa kazi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kupitia ushahidi wa video.

Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji ambaye alisema lilitokea barabara kuu ya Chalinze-Segera.

Alisema kupitia mitandao ya kijamii, askari huyo alionekana akipokea rushwa kutoka kwa dereva wa gari alilokuwa amelisimamisha kwa ajili ya kukagua makosa yanayoweza kuhatarisha usalama barabarani.

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

JE UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:

Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

Mwimbaji Chemical Afunguka Kuhusu Picha Inayosambaa Akipigana Mabusu na Producer wake

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Chemical amefunguka kuhusu picha zake na producer Max Maizer.

Chemical amesema picha hizo zilipigwa wakati waki-shoot video ya ngoma ‘Asali’ lakini zikuja kuwa gumzo kutokana watu hawajamzoea kumuona katika hali hiyo ila ni vitu ambavyo vipo katika maisha yake ya kawaida.

“Inawezekana walikuwa hawaamini lakini watu kama sisi ni romantic, we are very romantic basi hawajuagi watu,” Chemical ameiambia EATV na kuoengeza, “Nasisi hatutaki waonyesha kwa sababu wanaweza wakaganda, wakang’ang’ania.”.

Chemical na Max Maizer

Producer Max Maizer amehusika kutengeza ngoma kadhaa za Chemical ikiwemo mpya ya sasa ‘Asali’ ambayo amemshirikisha Beka Flavour.

Pogba aondolewa kwenye kikosi cha Man United

$
0
0
Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Man United ya England Paul Pogba ameondolewa kwenye kikosi cha Man United ambacho kilikuwa kinatarajiwa kucheza game ya FA dhidi ya Huddersfield.

Imeripotiwa kuwa Pogba ameondolewa kwenye kikosi kinachotarajia kucheza game ya FA dhidi ya Huddersfield leo saa 20:30 kwa saa za Afrika Mashariki, baada ya kuugua ghafla lakini ugonjwa wake haujatajwa.Kwa mujibu wa mtandao wa standard.co.uk umeripoti kuwa  ugonjwa wa Pogba haujatajwa anasumbuliwa na tatizo gani lakini nafasi yake amepewa Ethan Hamilton mchezaji wa Man United wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23

Hata hivyo kabla ya kuripotiwa kwa taarifa za kuondolewa kwa Pogba kikosini, kuna stori kuwa Pogba hana furaha na nafasi anayochezeshwa na Jose Mourinho katika kikosi cha Man United na imeripotiwa kuwa hawapo katika mahusiano mazuri kwa sasa.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe Akamatwa Kwa Tuhuma za Kumpa PHD Mke wa Mugabe

$
0
0

ZIMBABWE: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Levi Nyagura Akamatwa kwa tuhuma za kumtunuku Shahada za Uzamivu(PhD) Mke wa aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Robert Mugabe

Bi Grace Mugabe alitunukiwa Shahada hiyo baada ya kusoma kwa miezi michache kinyume cha utaratibu huku kukiwa na harufu ya rushwa

Wakufunzi kutoka Idara ya Sosholojia chuoni hapo wamesema kuwa hawajaona nyaraka zozote za kuthibitisha kuwa Bi. Grace Mugabe alistahili kutunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu na kuomba mamlaka husika zimfutie Bi. Grace Shahada hiyo

Polisi sita washikiliwa kwa uchunguzi kifo cha mwanafunzi NIT

$
0
0

olisi inawashikilia askari wake sita na silaha zao kwa ajili ya uchunguzi kuhusu tukio la kuuawa kwa risasi mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akweline.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hayo leo Februari 18,2018 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ulinzi wakati wa kampeni, upigaji kura, na utangazaji matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni uliofanyika jana Februari 17,2018.

Amesema polisi iliunda timu ya upelelezi kuchunguza chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo kilichotokea Februari 16,2018 wakati polisi wakiwatawanya wanachama wa Chadema waliokuwa wanakwenda ofisi za mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kushinikiza mawakala wao kupatiwa barua za viapo vyao.


Kamanda Mambosasa amesema polisi pia inawachunguza watuhumiwa 40 ili kubaini iwapo miongoni mwao walikuwepo waliokuwa na silaha za moto.

Amesema pia wanaendelea kuwatafuta wafuasi na viongozi wa Chadema walioshiriki kushawishi wafuasi wao kushiriki kwenye maandamano.  

Wakati huohuo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika taarifa aliyoitoa jana Februari 17,2018 alisema chama hicho kinalitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu aliyehusika na tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo.

Polepole alisema polisi imhoji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wenzake walioshiriki maandamano aliyosema hayakuwa halali yaliyosababisha uhai wa Mtanzania kupotea.

Shyrose Bhanji kuhusu mwanafunzi aliyepigwa risasi ‘Serikali ya CCM haiwezi kukwepa lawama

$
0
0

Kukiwa bado na taharuki miongoni mwa Watanzania kuhusu Mwanafunzi wa chuo cha NIT aliyepigwa risasi kwenye maandamano, Hatimaye aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji ametoa ya moyoni na kuweka wazi msimamo wake juu ya tukio hilo na kusema kuwa chama chake cha CCM na serikali haviwezi kukwepa lawama.

Bhanji amesema  kuwa tukio hilo linamfanya ashindwe kula wala kulala kwani ameuawa kikatili na hakua na hatia yoyote ile.

“Serikali ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo. Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu; nimeshindwa kula na nashindwa kupata usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu wangu naomba unisaidie,“ameandika Bhanji kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanafunzi huyo aliyetambulika kwa jina la Aqulina Akwilini alipigwa risasi na jeshi la polisi Februari 16, 2018 katika eneo la Mkwajuni -Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati jeshi la polisi likiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni.

Mtandao wa Wanafunzi Wamtaka Waziri Mwigulu Nchemba ajiuzulu

$
0
0

Leo February 18, 2018 Mwenyekiti wa mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kujiuzulu kutokana kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT. Pia kama atashindwa basi Rais amtengue.

“Tunamuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, ajiuzulu kwa sababu ameshindwa kusimamia nafasi yake na kuangalia mienendo ya Jeshi la Polisi ambapo kila siku matukio yanatokea,” -Nondo

“Haya matukio yamekuwa yakishamiri sana ambapo yalianzia kwa wanasiasa, ambapo tulikuwa tukiyasikia haya matukio hadi kwa wanafunzi na watu wasiokuwa na hatia,” -Nondo

Jeshi la Polisi DSM linawasaka Viongozi wa CHADEMA

$
0
0

Leo February 18, 2018 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia Askari Polisi sita kutokana na kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT Akwilina Maftahmwenye miaka 22.

Mambosasa amesema February 16, 2018 CHADEMA walifanya mkutano wa kufunga kampeni katika viwanja vya Buibui Mwananyamala ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe alipanda jukwaani na kukatisha mkutano na kuhamasisha wafuasi wa chama hicho kuandamana.

SACP Mambosasa amesema kuwa Jeshi limeunda timu ya Upelelezi ili kuchunguza chanzo cha kifo cha binti huyo.

“Katika uchunguzi huo tunawashikilia askari 6 kufuatia tukio hilo pia silaha zao zinachunguzwa ikiwa ni pamoja ni pamoja na kuzipeleka kwa wataalamu wa milipuko,”-Kamanda Mambosasa

Pia Kamanda Mambosasa amesema Jeshi hilo linawachunguza watuhumiwa 40 ili kubaini kama miongoni mwao walikuwa na silaha za moto na linaendelea kuwatafuta wafuasi na Viongozi wa CHADEMA walioshiriki kushawishi wafuasi wao kushiriki katika maandamano.

Rais Magufulu Alaani Tukioa la Mwanafunzi Kupigwa Risasa...Atoa Maagizo Haya..

$
0
0

IKULU, DAR: Rais Magufuli amesikitishwa na kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Aqulina Akwilini aliyepigwa risasi ktk Maandamano ya CHADEMA

Rais kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameviagiza Vyombo vya Dola kuchunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua waliohusika kusababisha kifo hicho

Rais pia ametoa pole kwa Familia, Ndugu, Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) na wote walioguswa na msiba huu

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora


Wahamiaji haramu wabuni njia mpya kuingia barani Ulaya

$
0
0

Wahamiaji haramu wagundua njia mpya ya kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kwa kupitia nchini Bosnia Herzegovina.

Hapo awali  wahamiaji walikuwa wakipitia nchini Ugiriki, Makedonia, Serbia, Hungary au Kroasia kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi.

Njia hiyo ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakimbizi ilifungwa Machi mwaka 2016.

Kwa sasa wahamiaji haramu na wakimbizi wanajaribu kutumia Kroasia kupitia Bosnia Herzegovina kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kutafuta hifadhi.

Katika kipindi hiki cha baridi, maimamu katika hutoa hifadhi za muda kwa wahamiaji wanaoathirika na baridi katika safari zao.

Wahamiaji 35 wamepewa hifadhi  na maimamu mjini Sarayevo wajikinge na baridi.

Wengi miongoni mwa wahamiaji hao ni raia kutoka Pakistan, Afghanistan, Syria, Libya na Morocco.

Jeshi la Polisi Bosnia  limefahamisha kuwa watu zaidi ya 750 wameingia nchini humo kinyume cha sheria  Januari  mwaka 2018 wakitaraji kuendelea na safari yao Ulaya Magharibi.

Mama kuwa makini House Girl Yaweza Kuwa Mke Mwenzio

$
0
0


Ivi ni vibaya House girl kuolewa na baba mwenye nyumba?

Ndugu msomaji  , karibu kwenye makala hii maalumu, nimeamua kuandika habari hii ili kujaribu kupunguza mifarakano kwenye familia zetu especially familia zenye wafanyakazi wa ndani wanaojulikana kama house girl.

Katika mada hii nimekuwa nikikutana na maswali mengi sana ambayo mda mwingine yalikuwa yakituchanganya hata sisi wenyewe katika kuwajibu wahusika, maswali haya malanyingi yalikuwa yakiulizwa na akina mama.

Na kwa upande wa akina baba maswali yao sio mengi ukilinganisha na akina mama, sasa napenda nianze kwa kusema mambo yafuatayo ili wote twende sawa.

WAJIBU WA MWANAUME KATIKA FAMILIA:
Mwanaume anawajibu wa kutimiza mahitaji yote ya msingi katika familia yake, moja ya majukumu hayo ni pamoja na kutoa pesa za matunzo ya familia yake kadri ipasavyo, kuonyesha upendo wa dhati kwa mama pamoja na watoto wake, na mambo mengineyo nk.

WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA FAMILIA:
Mwanamke ndiye mtendaji mkuu wa familia kwa upande wa nyumbani ukiachilia mbali ya kwamba baba ndiye kichwa cha familia, mwanamke anamajukumu mengi kwa upande wa nyumbani moja ya majukumu yake ni pamoja na kupika chakula cha familia, kufua nguo za mumewe pamoja na nguo za watoto, kuakikisha nyumba pamoja na eneo linaloizunguka nyumba ni safi, kuonyesha upendo wa dhati kwa mumewe pamoja na watoto wake, nk.

Ndugu msomaji wa makala hii, nadhani mpaka hapo tayari umeisha anza kupata mwanga kuhusu jibu la swali la makala yetu, sasa twende kuona wajibu wa mfanya kazi wa ndani kama house girl.

House girl wajibu wake ni kuakikisha anafanya usafi wa kuizunguka eneo la  nyumba kwa nje na kufanya usafi huo kwa upande wa ndani kwa baadhi tu ya maeneo ya nyumba hiyo pamoja na kuwaogesha watoto, kufua nguo za watoto, na kufanya kazi ndogo ndogo za nyumbani.

House girl hatakiwi kufanya usafi chumbani kwa mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kufua au kupiga pasi nguo za mume wa mama mwenye nyumba, house girl hatakiwi kumuandalia chakula au chai mume wa mama mwenye nyumba, nk.

Sasa ukiona house girl anafanya kazi zote nilizosema kuwa hatakiwi kuzifanya pindi awapo nyumbani kwako, ukiwa kama mama mwenye akili timamu jua kabisa tayari umeamua kumuletea mumeo mke mdogo na pia usipige kelele wala kulaumu maana jitihada zote za kumuandaa mke mwenzio umezifanya wewe mwenyewe.

Ushauri wangu kwenu akina mama na akina dada nikwamba, hatukatai kuwa wafanyakazi wa ndani hawafai, ila jitaidi mfanyakazi wako awe na mipaka ya kazi, mwanaume anaamua kumuoa house girl kwa sababu yeye amechukua majukumu yote ya mama mwenye nyumba, sasa wewe mama usianze kumtupia maneno mtoto wa watu pamoja na mumeo maana yote hayo umeyataka wewe mwenyewe.

Watu 66 wamefariki baada ya Ndege ya abiria kuanguka

$
0
0

Watu 66 wamefariki baada ya Ndege ya abiria kuanguka kusini mwa nchi hiyo

Hii inakuwa ni ndege ya pili kuanguka katika nchi hiyo katika kipindi cha siku siku 10

Ndege nyingi za abiria nchini humo zimechakaa kutokana na nchi hiyo kuwekewa vikwazo kwa takribani muongo mmoja sasa

Makao makuu ya CUF Zanzibar yazingirwa na Polisi

$
0
0

Polisi Zanzibar wamezingira makao makuu ya ofisi ya CUF kwa maelezo kuwa wamepata taarifa kwamba kuna mpango wa uvamizi.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba polisi wana ajenda mbili; kuishikilia kimabavu ofisi hiyo au kuweka vitu vya hatari na kisha kuwakamata viongozi wa chama hicho.

Akizungumza na MCL Digital, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali amethibitisha polisi kulizunguka jengo hilo.

“Ni kweli tumeliweka chini ya ulinzi, kwanza ni kwa sababu  kuna viashiria vya watu kufanya uhalifu katika ofisi ya CUF ya Mtendeni tumeweka ulinzi kwanza,” amesema.

“Hatua ya pili tunataka kuingia ndani ili kuthibitisha maneno yanayosemwa ili kama ni kweli tujue tunakabiliana vipi.”

Katika maelezo yake Mtatiro amesema, “Polisi wakiwa na magari kadhaa, wameivamia makao makuu ya CUF  Mtendeni, Zanzibar saa 12:10 jioni hii. Inaonekana na inahisiwa wana ajenda mbili.”

“Moja ni kuikalia makao makuu hiyo kimabavu ili kesho Jumatatu waikabidhi kwa bwana yule ili kutekeleza mkakati maalum, au wana lengo la kuingia kimabavu na kuweka vitu hatari na kisha kuwakamata viongozi wa CUF na kudai walitunza vitu hatari ofisini hapo. Tunafuatilia jambo hili kwa ukaribu.”

Waziri Nchemba afunguka kuhusu Akwilina

$
0
0

Dr Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kutoka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Maftah.

Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Geita wilaya ya Chato wakati wa uzinduzi wa Gereza la wilaya ya Chato.

Waziri Dr. Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuchukua hatua kwa askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.

“Kama Waziri mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha ya binti wetu ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza kujirudia tena kwa kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia hasahasa katika masuala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na ninalaani kwa nguvu zote.” -Waziri Mwigulu

Dr. Mwigulu amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza kusababisha madhara kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna hii watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wahusika wafikishwe katika vyombo vya usalama.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images